VUNJA
JUNGU
Assalaamu Alaykum Warahmatullah!
Ni baada ya siku chache tu kwa msaada wake
Allah Karim utakuwa unapumua na kuishi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwezi ambao huwapa waislamu fursa ya kuitekeleza mojawapo ya nguzo
tano za Uislamu, swaumu ya Ramadhani. Katika kuuheshimu, kuutukuza na kuuenzi mwezi huu mtukufu, Mtumishi wa uma {WEBSITE
UISLAMU}, itakutumikia kwa kukuletea mfululizo wa makala maalumu zihusianazo na
mwezi wako huu. Lengo kuu la makala hizi likiwa ni
kukumbusha wewe msomaji wetu:-
Utukufu wa mwezi wa Ramadhani ili uuthamini,
kwani asiyekujua hakuthamini.
Swaumu ya Ramadhani na yote yanayofungamana
nayo, ili uweze kufunga
Haya ndiyo malengo mama ya makala hizi ambazo tunatumai kwa msaada na taufiq yake Allah yatakunufaisha na kujibu
maswali yako mengi. Ambayo kwa namna moja au nyingine
yamekuwa yanakutatiza kuhusiana na swaumu hii ya Ramadhani.
Naam, Ramadhani hiyo mlangoni mwako inabisha hodi. Wewe kama muislamu
umejiandaje kuupokea mwezi wako huu mtukufu? Je, wewe ni
mmoja wa wale wanaoupokea mwezi wa Ramadhani kwa kile kinachojulikana
Hebu na tujiulize kwa pamoja, tulivunjao
Ikiwa vunja jungu linaashiria jambo, basi jambo
Ewe ndugu mpenzi wee! Elewa na ufahamu fika
kwamba Ramadhani ipokelewayo na kukaribishwa na vunja jungu haitakuwa na athari
yo yote kwako wewe ambaye ndiwe mlengwa wa Ramadhani na wala sio Mola wako.
Kwako Ramadhani haitakuwa ila mithili ya kujenga
nyumba angani bila ya kuwa na msingi imara uliokita ardhini. Ewe ndugu mpenzi
mvunja jungu, utaendelea kulivunja
Aya inakuongoza kutambua kwamba unapovunja jungu, hufanyi hivyo ila ni kwa hilaki na maangamivu ya nafsi yako wewe mwenyewe
leo hapa duniani na kesho kule akhera. Ambapo utapewa daftari la amali zako
uikute na vunja jungu yako, hapo ndipo utasema: “…OLE
WETU! NAMNA GANI MADAFTARI HAYA! HAYALIACHI DOGO WALA KUBWA ILA YAMELIDHIBITI
(yameliandika)! NA WATAKUTA YOTE YALE WALIYOYAFANYA
YAMEHUDHURIA HAPO; NA MOLA WAKO HAMDHULUMU YO YOTE”. [
Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-anasema:
“Jibril alinijia na akaniambia: Ewe Muhammad! Ishi utakavyoishi, hakika wewe ni mwenye kufa. Na penda ukipendacho hakika utatengana
nacho, na tenda ulitakalo hakika utalipwa kwalo…” Al-Baihaqiy
Elewa ewe ndugu mpenzi ukiwa mwana kuelewa, elewa kwamba kwa mujibu wa hadithi hii:-
Vunja jungu yako ina mwisho wake ambao ni kufa
kunakoashiria mwanzo wa safari ngumu ya kuhudhurishwa mbele ya Mola wako. Hii
ndiyo siku anayoitaja Mola wako kwa kauli yake tukufu:
“NA IOGOPENI SIKU AMBAYO MTARUDISHWA KWA ALLAH, KISHA VIUMBE WOTE WATALIPWA KWA
UKAMILIFU YOTE WALIYOYACHUMA; NAO HAWATADHULUMIWA”. [2:281]
Lewa
Ewe mvunja jungu wee! Hebu waidhika na sehemu hii ya kauli ya swahaba
wa Mtume;Sayyidna Abdullah Ibn Abbas-Allah amuwiye
radhi:
“Ewe mtenda dhambi wee! Usijiaminishe na matokeo ya
dhambi yako na tambua kwamba kiifuatiacho dhambi hiyo ni kikubwa kuliko dhambi
yenyewe.
Kwani kule kutokuwaonea kwako haya malaika walioko kuliani na kushotoni kwako wakati unapofanya dhambi, hakupungui kuwa
ni dhambi.
Na kicheko chako wakati unatenda dhambi na
ilhali hujui Allah atakufanya nini, ni kikubwa zaidi kuliko hiyo dhambi
uitendayo.
Na kuichelea kwako dhambi unapofanikiwa kuitenda, ni
kukubwa zaidi kuliko hiyo dhambi yenyewe.
Na kuihuzunikia kwako dhambi kwa kushindwa
kuitenda, ni kukubwa zaidi kuliko dhambi husika.
Haya mpenzi mvunja jungu, ikiwa mpaka hapa bado hujawaaidhika na ukaacha kulivunja
Mtu mmoja alimwambia Sufyaan Thauriy-Allah amuwiye
radhi-nipe nasaha ambazo nikizifanyia kazi sitathubutu kumuasi Allah. Sufyaan akamwambia: Yakumbuke mambo matano:
Je, inastahiki kwako kumuasi Allah na ilhali
yeye ndiye anayekuruzuku?
Je, unadhani kuwa wewe unamuasi Allah na
ilhali yeye anakuona?
Je, unaweza kumuasi Allah nje ya ufalme/milki yake?
Je, unaweza kuyaakhirisha mauti yakikujia?
Je, siku ya kiyama utakuwa una uwezo wa
kujiondoshea adhabu?
Yule mtu akajibu: Siwezi lo lote katika hayo. Sufyaan akamwambia: Basi
vipi unathubutu kumuasi yule anayekuruzuku, anakuona, nawe uko katika milki
yake, akakuandikia mauti na wala huwezi kuizuia adhabu
yake isikufike? Akasema mtu yule: Wallah sitamuasi muda wa
uhai wangu.
Hebu nawe mvunja jungu, jiulize maswali matano hayo
halafu ndio uamue ama kulivunja jungu au kutokulivunja. Kumbuka ewe ndugu muislamu kwamba:-
Kuvunja jungu ni kumuasi Allah na Mtume wake:
“NA ANAYEMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, NA KUIRUKA MIPAKA YAKE (Allah) ATAMUINGIZA
MOTONI. HUMO ATAKAA MILELE NA ATAPATA ADHABU ZIFEDHEHESHAZO”. [
Kuvunja jungu ni kuudhihaki mwezi mtukufu wa
Ramadhani. Na kuudhihaki mwezi huu hakumaanishi kingine zaidi
ya kuidhihaki Qur-ani Tukufu. Nako huku kuidhihaki Qur-ani, hakika si
vinginevyo ila ni kumdhihaki aliyeshushiwa Qur-ani
Mtume. Na hakuna anayethubutu kupinga kwamba kumdhihaki Bwana Mtume ni kumdhihaki Allah akiyemtuma. Na huko kumdhihaki Allah ni ukafiri tu na si vinginevyo: “AMA WALE WALIOKUFURU,
NITAWAADHIBU ADHABU KALI KATIKA DUNIA NA AKHERA, WALA HAWATAPATA WASAIDIZI WA
KUWASAIDIA”. [
Vunja jungu ni khadaa na ghururi za dunia.
Uovu basi si huko kukhadaika, bali ni kushikilia
kukhadaika baada ya kutanabahishwa.
Mwisho Mtumishi wa uma {WEBSITE UISLAMU}
anakutakieni kila la kheri, fanaka na baraka tele za Allah katika mwezi huu wa
Ramadhani. Allah Karim tunamuomba aijaalie Ramadhani hii kuwa ni yenye kuleta mabadiliko na mapinduzi ya kiimani katika
nyoyo za waislamu po pote pale walipo ulimwenguni.
Wasalaamu Alaykum Warahmatullah.
Shahrun Mubaaraku.