
IDADI YA WAISLAMU
YAONGEZEKA UENGEREZA
23/02/2004
Gazeti
la Sunday Times la London limeandika leo
kuwa zaidi ya Waingereza weupe
elfu 14 wameingia katika dini ya
Kiislamu baada ya kuona kuwa
mwenendo na tabia za kizungu
zinawapotosha.
Gazeti
hilo
linalotolewa kila wiki limeendelea kueleza kuwa; kutokana
na utafiti wenye kuaminika imeonekana kuwa Waingereza wengi wenye kumiliki ardhi na watu
mashuhuri na maarufu wameingia katika dini ya
Kiislamu jambo linalowafurahisha sana
Waislamu wa Uingereza kwa sababu
ya himaya watakayoweza kuipata kutokana na mwenendo
huo.
Gazeti
hilo
likimnukuu mwandishi wa utafiti huu
Yahya Bert aliyekuwa akijulikana hapo mwanzo kwa jina
la Jonathan Bert ambaye ni mwana wa Lord Bert aliyekuwa mkurugenzi wa Idhaa ya
BBC kuwa amesema:
"Wapo
zaidi ya Waingereza weupe 14200 walioingia katika dini ya Kiislamu
wakiwemo watu mashuhuri na
kwamba katika siku chache zijazo
wengi zaidi wanategemea kuingia katika dini hii.
Gazeti
hilo
limeendelea kusema kuwa wengi kati
ya walioingia katika dini ya
Kiislamu wamevutiwa na makala ya
Charles Logan Eton aliyekuwa mwana
diplomasi maarufu aliyeandika kitabu kiitwacho 'Uislamu na Ubinadamu'.
Sunday Times likimnukuu Eton limeandika
kuwa; baada ya kuandika kitabu
chake hicho, Eton
alipata barua nyingi kutoka kwa watu mbali mbali waliofurahishwa
na kitabu hicho.
Gazeti
hilo
limeandika pia kuwa wapo Waingereza
wengi walioingia katika dini ya
Kiislamu baada ya kufanya urafiki
na Waislamu na wengine baada
ya kusoma makala mbali mbali
juu ya Uislamu
mfano wa Ema Clark mjukuu wa waziri mkuu
wa zamani wa Uingereza Herbert.
Gazeti
hilo
limeeleza pia kuwa mchezaji cricket maarufu wa Pakistan Imran Khan na aliyekuwa
muimbaji maarufu wa Uingereza Cat Stevens (Yusuf Islam) wamefanya juhudi kubwa katika
kuwafanya Waingereza wengi kuingia katika
dini ya Kiislamu.
Gazeti
lingine la Kiingereza limeandika kuwa idadi ya wanawake
walioingia katika dini ya Kiislamu
kwa njia
ya ndoa inakaribia
elfu 77
Wikala ya habari ya Kiislamu
23/02/2004