UDHU NA
FAIDA ZAKE
Mara nyingi
Katika kusisitiza jambo
Mtume {S.A.W} anasema:
"Jee sikwambiini juu ya jambo kuwa
jambo hili Mwenyezi Mungu hufuta dhambi na hunyanyua
daraja zake?"
Wakasema Masahaba:
"Ndio ewe Mtume wa
MwenyeziMungu tuambie".
Akasema Mtume {S.A.W}:
"Kutimilisha udhu
pamoja na shida zake".
Kwa mujibu wa
hadithi hii inaonyesha kuwa udhu uliokamilika una cheo chake maalum mbele ya
Mwenyezi Mungu na ule uliokosa ukamilifu huwa na kasoro na kutokua na baraka au
kutokamilika mbele ya Mwenyezi Mungu. Na wakati mwengine kukosekana kwa
taratibu nzuri hupelekea makosa na kasoro, mfano kutokuwa na nia na azma ya
kutia udhu au kutopiga Bismillahi wakati wa kuanza kutia udhu, vile vile utaratibu
wa kiislamu ni kwamba kila jambo jema kama hili la udhu hufanywa kwa kutumia
mkono wa kulia. Basi udhu
Inafaa tuelewe kwamba udhu unakuwa ni
lazima kwa mwenye hadathi anaetaka kufanya ibada ya sala iwe sala hio ni
faradhi au sunna na vile vile katika sala ya maiti na pia katika sijda ya
kisomo, na hasa hasa udhu unalazimika wakati wa kugusa msahafu na japo ni iwe
ni aya iliyoandikwa katika karatasi.
Inasuniwa na
kupendezeshwa udhu kwa muosha maiti au mchukuaji, kwani Mtume {S.A.W} anasema:
"Atakae mkosha
maiti basi aoge na atakaemchukua basi atawadhe".
Jambo muhimu katika udhu ni kuondoa kabisa vizuizi ambavyo vitazuia ngozi ya kiungo
cha udhu kupata maji, mfano mafuta ya mgando na rangi za kuchani wanazotumia
wanawake kujipambia hazifai kabisa. Na kwa wale wenye
kuvaa pete vidoleni mwao wanatakiwa wahakikishe zinapata maji sehemu zote
zilizozunguka pete hiyo au kuziba na hii na kwa zile pete zenye kubana. Kwa
piko na vipodozi vyengine ambavyo vinazuia maji kufika
ngozini havifai kwani vitaharibu taratibu za udhu. Ama hina na
mafuta mengine mepesi ambayo hayazuii kufika maji kwenye ngozi hayo
yanaruhusika kwa masharti yake.
Inafaa tuzingatie kwamba kama hakuna
dharura mtu anatakiwa atie udhu yeye mwenyewe bila ya msaada wa mtu mwengine na
vile vile kabla ya kutia udhu anatakia asuwaki[apige mswaki] ili kuondoa karaha
ya uchafu mdomoni mwake na hii ni kwa yule ambae hakufunga [funga ya ramadhani
au ya sunna].
Muislamu kuwa na
udhu wakati wote ni jambo muhimu
Kufanya israfu katika jambo la kutia udhu
ni jambo la haramu na karaha, na sirafu inakuwa kwa
kuzidisha kiwango kinachotakiwa
Jambao la msingi kwa
muislamu ni kuelewa kwamba udhu ni kitu muhimu
"Kujitoharisha ni
nusu ya uislamu".
Kwa kutakiwa tuwe na
udhu wakati wote hasa hasa tunaposoma Qur’aani na darasa za hadithi na vitabu
vya elimu ya kisheria. Na mtu anapoghadhibika kwani udhu
unazima chuki za mtu.