|
|
Uadilifu wa Masahaba na
Utatanishi wa hadithi ya Hodhi
|
|
Yamekusanywa na kutafsiriwa na
Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Yaliyomo
Zipo baadhi ya hadithi zenye
utatanishi au zenye kubeba maana zaidi ya moja, ambazo wakristo katika tovuti
zao huzitumia kwa kuzifasiri hadithi hizo kwa maslahi yao, au kwa maana
wanayoitaka wao, kinyume na maana yake ya kweli, kwa ajili ya kuupiga vita
Uislamu.
Kinachoskitisha zaidi ni kuwa wapo
baadhi ya Waislamu ambao kwa kutaka maslahi yao, bila kujali athari
wanayoiacha, utawakuta wakipoteza wakati wao mkubwa wakifanya utafiti na
kunukuu hadithi za aina hizo huku wakitaja baadhi ya makosa ya kibinadamu yaliyowahi
kutendwa na baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum), kisha wanayakuza makosa
hayo na kuyafanya kuwa ni dalili ya ubaya wa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Yareti kama wakati wao
wangeliupoteza katika kufanya utafiti juu ya maadui wa Mwenyezi Mungu kama vile
Abu Jahal au mnafiki Abdullahi bin Saluul au Firauni au Haaman au Abu Lu'ulua
al Majusiy, aliyemuuwa Khalifa wa pili wa Waislamu Umar bin Khattab (Radhiya
Llahu anhu). Bali kinyume na hivyo, utawaona wanaunyamazia uadui wao watu hao,
juu ya kuwa ukafiri wao umethibiti ndani ya Qurani tukufu na ndani ya
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na
badala yake wanaziunguza juhudi zao katika kujaribu kuwapaka matope Masahaba wa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Kwa kufanya hivyo wanawapa makafiri
silaha kali pamoja na ushahidi wanaoutaka katika kuupiga vita Uislamu na
kuwapiga vita waliotuletea dini hii, kwa sababu kwa kuwatuhumu Masahaba bila ya
uhakika wala ushahidi ulio wazi, ni kuutuhumu Uislamu waliotuletea Masahaba hao
(Radhiya Llahu anhum) baada ya kuupokea kutoka kwa sahibu yao Mtume wa Mwenyezi
Mungu, Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Miongoni mwa hadithi wanayoitumia
katika ubabaishaji wao huo ni ile hadithi maarufu ya Hodhi, na namna Malaika
watakavyowarudisha watu watakaotaka kunywa ndani ya hodhi hilo la Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), wakidai kuwa hadithi hiyo
inawakusudia Masahaba hawa (Radhiya Llahu anhum) sahibu zake Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na marafiki zake na wenzake alioanza nao
tokea siku ile ya mwanzo ya kuwalingania watu katika dini hii tukufu.
Imepokelewa katika hadithi hiyo kuwa Siku
ya Kiama, wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
atakapokuwa anawanywisha watu maji kutoka katika hodhi lake, watakuja Malaika
na kuwaondoa makundi kati yao, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) atakaposema:
"Hawa ni katika
Masahaba wangu."
Malaika watajibu:
"Je Unajuwa
waliyoyazuwa baada yako?”
Na katika riwaya nyingine, Malaika
watasema:
"Walirtaddi hawa
wakarudi nyuma."
Anasema Ibni Abdul Barr: "Maana
hasa
ya hadithi hizi ni kuwa kila mwenye
kuzusha mambo katika dini, atakuwa miongoni mwa watakaofukuzwa penye hodhi ya
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)."
Tukiendelea na kuichambuwa Shubha
hii inayowakanganya baadhi ya watu wakadhani kuwa watakao ondolewa penye hodhi ni
hawa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
waliosimama naye tokea siku za mwanzo kisha wakaendelea kusimama naye katika
shida zake zote na vita vyote dhidi ya makafiri; vita vya Badar, vita vya Bani
Qaynuqaa, vita vya Uhud, vita Khandaq, Fathi Makka, Hunayn na vita mbali mbali.
Hawa ambao baada ya kufariki kwa sahibu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) waliendelea kuisimamia dini hii kidete na kuipigania
kwa hali zao na mali zao mpaka ikaenea ulimwengu mzima.
Daraja ya Masahaba na heshima yao
katika dini ni jambo lisilokubali kujadiliwa na Muislamu yeyote mkweli mwenye
kupenda haki, kwa sababu hawa ndio ambao Mwenyezi Mungu aliwahusisha kwa
kuwafanya kuwa sahibu zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
sallam), wakamsadiki na kumfuata na kumnusuru na wakaifuata nuru aliyokuja
nayo, na wakafanya kila juhudi kwa kujitolea roho zao na mali zao kwa ajili ya
kuipigania dini hii tukufu mpaka ilipokamilika.
Hawa ndio wale waliosifiwa na Mwenyezi
Mungu walipoambiwa kuwa wao ni umma bora kupita zote zilizoletwa kwa ajili ya
watu. Na Mwenyezi Mungu Akaridhika nao.
Masahaba ni waaminifu wa umma huu
walioibeba sheria na kuieneza ulimwenguni kote mpaka ikatufikia sisi hivi sasa.
Hii Qur'ani tuliyo nayo na haya mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) yametufikia kupitia kwao (Radhiya Llahu anhum).
Kwa hivyo kitendo cha kuwatilia shaka
Masahaba hawa watukufu katika uadilifu wao ni katika kuipiga vita dini na
kuwafanya watu wasiamini masdari za dini tulizopokea kutoka kwa Masahaba hao
watukufu (Radhiya Llahu anhum). Kwa sababu Qurani tukufu na Mafundisho ya Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), yote tumeyapata kupitia
kwao.
Ndiyo maana maulamaa wa Kiislamu
wanatutaka tuwe na msimamo imara dhidi ya kila mwenye kuwatuhumu Masahaba wa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Inasikitisha kuona kuwa wapo miongoni
mwa Waislamu wenye kuwatuhumu baadhi ya Masahaba, na wanafanya hivyo makusudi
kwa ajili ya kukifikia kile wanachokitaka tu, na wakazitumia hizi hadithi za
hodhi katika kujaribu kuwapaka matope Masahaba hawa watukufu (Radhiya Llahu
anhum).
Katika kujaribu kuharibu sifa za
Masahaba (Radhiya Llahu anhum), wakazitumia hadithi mfano wa hii inayosema:
"Wakati mimi
nimesimama, litakuja kundi, nitakapowajuwa, atatoka mtu kutoka kwangu na
kusema: 'Twendeni', Nitasema: 'Wapi?' Atasema: 'Motoni wallahi.' Nitasema:
'Wana makosa gani?' Atasema: 'Hawa wamertaddi na kurudi nyuma baada
yako.."
Bukhari na wengine
Maulamaa wanasema:
Wa kwanza kutoa hukmu Yake kuwa
Masahaba (Radhiya Llahu anhum), ni watu waadilifu ni Mwenyezi Mungu Subhanahu
wa Taala na Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kama ilivyoandikwa
ndani ya Qurani tukufu na kama ilivyokuja kwa njia Mutawaatirah katika
Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na miongoni
mwa hukmu hizo ni kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:
ãøõÍóãøóÏñ ÑøóÓõæáõ Çááøóåö æóÇáøóÐöíäó ãóÚóåõ ÃóÔöÏøóÇÁ Úóáóì
ÇáúßõÝøóÇÑö ÑõÍóãóÇÁ Èóíúäóåõãú ÊóÑóÇåõãú ÑõßøóÚðÇ ÓõÌøóÏðÇ íóÈúÊóÛõæäó ÝóÖúáÇ
ãøöäó Çááøóåö æóÑöÖúæóÇäðÇ ÓöíãóÇåõãú Ýöí æõÌõæåöåöã ãøöäú ÃóËóÑö ÇáÓøõÌõæÏö
Ðóáößó ãóËóáõåõãú Ýöí ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóãóËóáõåõãú Ýöí ÇáúÅöäÌöíáö ßóÒóÑúÚò
ÃóÎúÑóÌó ÔóØúÃóåõ ÝóÂÒóÑóåõ ÝóÇÓúÊóÛúáóÙó ÝóÇÓúÊóæóì Úóáóì ÓõæÞöåö íõÚúÌöÈõ
ÇáÒøõÑøóÇÚó áöíóÛöíÙó Èöåöãõ ÇáúßõÝøóÇÑó æóÚóÏó Çááøóåõ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ
æóÚóãöáõæÇ ÇáÕøóÇáöÍóÇÊö ãöäúåõã ãøóÛúÝöÑóÉð æóÃóÌúÑðÇ ÚóÙöíãðÇ
Muhammad
ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri,
na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila
na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya
kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama
mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa
juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao
makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao
msamaha na ujira mkubwa.
Al
Fat'h – 29
Na Akasema:
æóÇáÓøóÇÈöÞõæäó ÇáÃóæøóáõæäó ãöäó ÇáúãõåóÇÌöÑöíäó æóÇáÃóäÕóÇÑö
æóÇáøóÐöíäó ÇÊøóÈóÚõæåõã ÈöÅöÍúÓóÇäò
ÑøóÖöíó Çááøåõ Úóäúåõãú æóÑóÖõæÇú Úóäúåõ æóÃóÚóÏøó áóåõãú ÌóäøóÇÊò ÊóÌúÑöí
ÊóÍúÊóåóÇ ÇáÃóäúåóÇÑõ ÎóÇáöÏöíäó ÝöíåóÇ ÃóÈóÏÇð Ðóáößó ÇáúÝóæúÒõ
ÇáúÚóÙöíãõ
“Na wale
walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa
wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia
Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu
kukubwa.”
At
Tawba 100
Na Akasema:
áóÜßöäö ÇáÑøóÓõæáõ æóÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ãóÚóåõ ÌóÇåóÏõæÇú
ÈöÃóãúæóÇáöåöãú æóÃóäÝõÓöåöãú æóÃõæúáóÜÆößó áóåõãõ ÇáúÎóíúÑóÇÊõ æóÃõæúáóÜÆößó
åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
Lakini
Mtume na wale walio amini pamoja naye walipigania Jihadi kwa mali zao na nafsi
zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa.
At
Tawba – 88
áóÞóÏú ÑóÖöíó Çááøóåõ Úóäö ÇáúãõÄúãöäöíäó ÅöÐú íõÈóÇíöÚõæäóßó
ÊóÍúÊó ÇáÔøóÌóÑóÉö ÝóÚóáöãó ãóÇ Ýöí ÞõáõæÈöåöãú ÝóÃóäÒóáó ÇáÓøóßöíäóÉó
Úóáóíúåöãú æóÃóËóÇÈóåõãú ÝóÊúÍðÇ ÞóÑöíÈðÇ
Na Akasema:
Kwa
hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti,
na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa
kwa Ushindi wa karibu.
Al
Fat'h – 18
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
"Kheri ya watu ni wa karne
yangu kisha wanaowafuata kisha wanaowafuata."
Bukhari na Muslim
Na kauli yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
aliposema:
"Msiwatukane Sahaba wangu.
Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hata mmoja wenu
atajitolea katika njia ya MwenyeziMungu kugawa dhahabu ukubwa wake mfano wa
jabali Uhud, basi hatofikia gao lao wala hata nusu ya gao lao".
Bukhari na Muslim
Na akasema:
"Allah Allah! (nakuusieni) juu
ya Sahaba wangu. Msiwageuze kuwa malengo yenu baada ya kuondoka kwangu. Kwani
mwenye kuwapenda basi kwa kunipenda mimi (ndiyo) amewapenda, na mwenye
kuwachukia basi kwa kunichukia mimi (ndiyo) amewachukia. Na mwenye kuwaudhi
ameniudhi (na) mimi, na mwenye kuniudhi mimi amemuudhi Allah, na mwenye
kumuudhi Allah, anakaribia Kumnyakuwa."
Attirmidhy
Zipo hadithi nyingi za namna hii zenye kuwasifia na
kueleza juu ya fadhila zao mbali mbali na mitihani waliyopambana nayo, na
kututaka wafuasi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
kuwaheshimu na kuwakirimu na kutowaudhi wala kuwageuza kuwa ni malengo yetu
tunayoyatumia kila tunapotaka kuipitisha batil yetu. Na nasaha zote hizi
zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Amesema Imam Ibni Najjar:
"Aliyesifiwa namna hii na
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, itakuwaje tena asiwe muadilifu. Ikiwa mbele
ya mahakama wanatosha mashahidi wawili tu kuthibitisha uadilifu wa mtu, itakuwaje
basi ikiwa ushahidi unatoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi Subhanahu wa
Taala."
Shar'hi ya Kawkab Al Muniyr (2/475)
Anasema Al Khatwiyb Al Baghdaadiy
"Usafi wa Masahaba (Radhiya
Llahu anhum) na uadilifu wao hauna lazma ya kusifiwa na wanadamu baada ya
kusifiwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Aliyeangalia ndani ya nafsi zao
akatujulisha juu ya ukweli wao.
Na hata kama Mwenyezi Mungu
asingetujulisha juu ya sifa zao na kuridhika Kwake nao, basi kule kupigana kwao
Jihaad kwa mali zao na nafsi zao, wamewaua baba zao na watoto wao waliopigana
upande wa makafiri, haya yanatokana na yakini waliyokuwa nayo ndani ya nyoyo
zao juu ya nusra ya Mwenyezi Mungu iliyowajia."
Al Kifayah fiy Ilm Annhihaayah – 48-49
Kwa
hivyo kuzichukulia zile hadithi za hodhi kuwa waliokusudiwa ni hawa Masahaba wa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) waliomsadiki na
kumuamini, wakamsaidia na kumnusuru, kunakuwa ni kuzikataa aya zote na riwaya
zote zilizo sahihi zenye kutubainishia fadhila zao na heshima yao mbele ya
Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Kuwatuhumu
Masahaba (Radhiya Llahu anhum) ni mfano wa kuukataa ushahidi wa Mwenyezi Mungu
Subhanahu wa Taala, kwa sababu itakuwaje Mwenyezi Mungu atujulishe juu ya watu
Alioridhika nao na kutujulisha juu ya fadhila zao na kwamba atawaingiza katika
Pepo Yake, kisha asijuwe kuwa watu hao siku moja watakuja kurtaddi na
kubadilisha na kuzuwa nk.
Na
huko pia ni kuzikanusha kauli za Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) aliyetujulisha juu ya kuridhika na Sahibu zake na kuwabashiria Pepo
aliposema:
"Abubakar (yumo) Peponi, na Umar (yumo) Peponi na
Uthmaan (yumo) Peponi na Aliy (yumo) Peponi na Twalha (yumo) Peponi na Az
Zubeir (yumo) Peponi na Abdul Rahman bin Auf (yumo) Peponi na Saad (yumo)
Peponi na Saeed (yumo) Peponi na Abu Ubaydah (yumo) Peponi"
Muslim na Attirmidhiy na Imam Ahmad na wengine
Na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alifariki dunia akiwa
ameridhika nao.
Na
akasema (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
"Haingii Motoni aliyeshiriki katika vita vya
Badar."
Imam Ahmed na Attabarani na wengine
Hivyo
kweli inawezekana maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) yapingane yenyewe kwa yenyewe? Leo amuambie kuwa wewe utaingia Peponi,
na kesho amkute katika watakaorudishwa mbele ya hodhi?
Huku
ni kukanusha wazi wazi maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wa sallam). Tutakwenda wapi na ile riwaya ya Attabarani kutoka kwa Abu Dar'daa
(Radhiya Llahu anhu) kuwa alimuwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa sallam):
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Allah
anijaalie nisiwe katika hao"
Akasema: "Wewe si katika hao."
Inawezekana
kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) asijuwe hali ya
Masahaba wengine akaweza kujuwa hali ya Abu Dar'daa alipomjulisha kuwa hatokuwa
miongoni mwa watakao ondolewa penye hodhi?
Waliowahi
kuonana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hawakuwa
watu wa aina moja. Wapo miongoni mwao waliokuwa wanafiki waliokuwa
wakijidhihirisha kinyume na walivyo, juu ya kuwa walikuwa wakishiriki vitani.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
ÅöÐóÇ ÌóÇÁóßó ÇáúÜãõäóÇÝöÞõæäó ÞóÇáõæÇ äóÔúåóÏõ Åöäøóßó
áóÑóÓõæáõ Çááåö æóÇááåõ íóÚúáóãõ Åöäøóßó áóÑóÓõæáõåõ æóÇááåõ íóÔúåóÏõ Åöäøó
ÇáúÜãõäóÇÝöÞöíäó áóßóÇÐöÈõæäó {ÇáãõäóÇÝöÞæä: 1}.
Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa
wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa
Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni
waongo.
Al Muafiqun - 1
Na
wanapokuwa vitani huwa wakisema:
íóÞõæáõæäó áóÆöä ÑøóÌóÚúäóÇ Åöáóì ÇáúãóÏöíäóÉö áóíõÎúÑöÌóäøó ÇáÇóÚóÒøõ
ãöäúåóÇ ÇáÇÐóáøó æóáöáøóåö ÇáúÚöÒøóÉõ æóáöÑóÓõæáöåö æóáöáúãõÄúãöäöíäó æóáóßöäøó
ÇáúãõäóÇÝöÞöíäó áÇ íóÚúáóãõæäó {ÇáãõäóÇÝöÞæä: 8}.
Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila
ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu -
Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.
Al Munafiqun - 8
Walikuwepo
pia waliokuwa wakitia shaka, na pia walikuwepo wenye imani dhaifu miongoni mwa
mabedui ambao wengi wao walirtaddi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) kufariki dunia.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
æóãöãøóäú Íóæúáóßõãú ãöäó ÇáÇÚúÑóÇÈö
ãõäóÇÝöÞõæäó æóãöäú Ãóåúáö ÇáúÜãóÏöíäóÉö ãóÑóÏõæÇ Úóáóì ÇáäøöÝóÇÞö áÇ
ÊóÚúáóãõåõãú äóÍúäõ äóÚúáóãõåõãú ÓóäõÚóÐøöÈõåõãú ãóÑøóÊóíúäö Ëõãøó íõÑóÏøõæäó
Åöáóì ÚóÐóÇÈò ÚóÙöíãò- ÇáÊæÈÉ
Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na
katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui.
Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu
kubwa.
At Tawbah – 102
Hadithi
zimeeleza wazi wazi wasfu na sababu za watu watako ondolewa penye hodhi, na
wasfu huo haukubaliani na wasfu wa Mashaba (Radhiya Llahu anhum) waliolelewa na
kufundishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na
mpaka alipofariki dunia alikuwa radhi nao.
Na
hii ni dalili kuwa Masahaba (Radhiya Llahu anhum) hawana uhusiano wowote na
hadithi hizi, kwani hapana Sahaba hata mmoja aliyertaddi wala aliyezusha.
Umar
na Uthmaan (Radhiya Llahu anhum) wanaowatuhumiwa kuwa walizusha, wao
walichofanya ni kuhuisha Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa sallam), na wala hawajazusha jambo jipya katika dini. na hao tulisema
kwamba tumeamrishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
kufuata mwenendo wao.
Anasema
Imam Al Khutaaby:
"Hapana hata Sahaba mmoja aliyertaddi, bali waliortaddi ni makabila
ya kibedui wasiowahi kuipigania dini, na kwa ajili hiyo haipasi kuwatuhumu
Masahaba wale maarufu."
Fathu l Baari 00/385
Anasema
Imam Al Baghdadiy:
"Wamekubaliana maulamaa wote wa Kisunni 'Ij'maa' kuwa
waliortaddi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kufariki
dunia walikuwa ni watu wa kabila la Bani Kindah na Hanifa na Fizaarah na Bani
Asad na Bani Bakar bin Wail. Hawa hawakuwa miongoni mwa watu wa Madina wala
watu wa Makka kabla ya kutekwa mji wa Makka. Na kisheria wanaoitwa Muhajirin ni
wale tu waliohajir kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
kabla ya Fat'hi Makka."
Al Farqu baynal Firaq
Wamekhitalifiana
maulamaa juu ya nani atakaye ondolewa penye hodhi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) baada ya wote kukubaliana kuwa waliokusudiwa si Masahaba hawa
tunaowajuwa sisi.
Amesema
Imam An Nawawiy (Mwenyezi Mungu Amrehemu) katika sharhi yake ya Muslim 3/136
-137 katika kuisherehesha hadithi hii ambayo ndani yake imo kauli ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliposema: "Unajuwa namna waliyozusha baada yako?" 'Waliokusudiwa ni wanafiki waliortaddi na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) atakapowaita ataambiwa: "Hawa siwo uliahidiwa, kwani hawa
walibadilisha."
Na
rai nyingine inasema kuwa watu hao ni wale waliokuwa Waislamu wakati wa Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam), kisha wakartaddi baada ya kufariki kwake. Na
atakapowaita, ataambiwa kuwa walirtaddi baada yake.
Rai
ya tatu ni kuwa; hawa ni watu waliotenda maasi makubwa na Bida'h
wakafariki kabla ya kutubu, juu ya kuwa walikuwa Waislamu.
Kauli
kama hizi pia alizitaja Al Qurtuby katika Al Muf'him 1/503
Ikajulikana
kuwa Masahaba (Radhiya Llahu anhum) hawamo katika wasfu huu. Na kama mtu
atarudi kusoma wasfu wa nani Sahaba uliotajwa na maulamaa mbali mbali atauona
uhakika wa hayo.
Maulamaa
wanasema kuwa Sahaba ni: "Mtu aliyemuona Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akiwa Muislamu na akafariki
dunia akiwa katika hali hiyo."
Wasfu
huu unawatowa wanafik na waliortaddi, kwani wao si Masahaba aslan. Watakuwaje
Masahaba wakati Masahaba ni maadui wa waliortaddi na maadui wa wanafik. Waliwapiga
vita mpaka Mwenyezi Mungu Alipowapa ushindi juu yao. Na haya yalitokea baada ya
kufariki dunia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam),
wakati waliportaddi makabila mengi ya kiarabu.
Na
pia kuhusu kitendo cha Bida'h, ambayo ni sababu mojawapo ya kuondoshwa hodhini.
Masahaba (Radhiya Llahu anhum) walikuwa msitari wa mbele kupiga vita kila aina
ya Bida'h, bali matendo ya Bida'h hayajaenea isipokuwa baada ya kumalizika zama
zao Masahaba hawa (Radhiya Llahu anhum), na dalili ya maneno haya ni kauli ya
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliposema:
"Nyota ndizo zinazolinda mbingu, zitakapo ondoka, mbingu zitajiwa
na kile kilicho ahidiwa, na mimi ni mlinzi wa Sahibu zangu, nitakapo ondoka
watakuja Sahibu zangu. Na Sahibu zangu ni walinzi wa umma wangu, watakapoondoka,
umati wangu utajiwa na kile walicho ahidiwa."
Muslim, Imam Ahmad, Attirmidhiy na wengine.
Anasema
Imam An Nawawiy:
(Na Sahibu zangu ni walinzi wa umma wangu, watakapoondoka, umati wangu
watajiwa na kile walicho ahidiwa.) "Maana yake ni kuwa baada ya kuondoka Masahaba
watakuja wazushi na fitan …."
Misimamo
imara kama hii ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum), ambao baada ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kufariki dunia, walipopambana
na maadui, na wakati huo huo walipambana na waliortaddi, na wakati huo huo walifungua nchi nyingi na nyoyo nyingi, yote
haya ni dalili kuwa wao ndio hasa wanaostahiki kunywa maji ndani ya hodhi.
Inawezekana
pia kuwa watako ondolewa penye hodhi ni watu wenye wasfu ule wa kurtaddi, kwa
sababu katika hadithi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
"Nitaambiwa kuwa hawa walirtaddi baada yako."
Ikiwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema kuwa sababu ya
kuondoshwa penye hodhi ni kwa kurtaddi na kufanya matendo ya Bida'h, kwa hivyo
bila shaka yoyote watakao ondoshwa hapo ni wale waliortaddi na waliozusha, na
hapana hata mmoja kati ya Masahaba hawa aliyenukuliwa kuwa alirtaddi.
Anasema
Imam Ibni Abdul Bir:
"Yeyote atakayezusha (atakayeingiza Bida'h yake) katika dini,
atakuwa miongoni mwa watakao ondoshwa penye hodhi."
Amesema
Al Qurtuby katika At Tadhkirah 1/348:
"Maulamaa wetu wote wamesema kuwa; kila aliyertaddi katika dini au
aliyezusha Bida'h yake, kile asichokitolea amri Yake Mwenyezi Mungu, huyo
atakuwa miongoni mwa watakaofukuzwa penye hodhi."
Kule
kusema kuwa alikuwa akiwajuwa, si lazima kumaanishe kuwa aliwahi kuwaona, bali
aliwajuwa kwa alama maalum kama ilivyokuja katika Sahih Muslim kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alisema:
"Watarudishwa katika umati wangu ninaowajuwa kama mtu anavyowajuwa
ngamia wake." Wakamuuliza: "Utatujuwa?" Akasema: "Ndiyo,
mtakuwa na alama hawana alama hizo wengine isipokuwa nyinyi. Mtarudishwa kutoka
kwangu mkiwa weupe hamna madowa kwa athari ya udhu, na wengine miongoni mwenu
watazuiliwa hawatoweza kunifikia. Nitasema: "Ewe Mola wangu! Hawa ni
sahibu zangu." Atanijibu Malaika: "Unajuwa waliyozuwa baada
yako?"
Kwa
hivyo pale Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliposema: "miongoni mwenu", alikusudia 'miongoni
mwa umati wake', na maana yake ni kuwa;
watafufuliwa umati wake wote kwa alama za udhu, na maana yake ni kuwa
watafufuliwa pamoja na Waislamu wenzao, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) atawajuwa kutokana na athari yao ya udhu.
Nne:
Riwaya hizi zimepokelewa kutoka vitabu sahih kutoka kwa hao Masahaba (Radhiya
Llahu anhum), akiwemo Umar na Abu Hurayrah na Aisha na Ummu Salamah na
Hudhayfah na Abu Saeed Al Khodhary na Ibni Masaud na Anas na Sahal bin Saad na
Ibni Abbas na Mu'awiyah na wengine (Radhiya Llahu anhum).
Sasa
ikiwa hawa ndio waliokusudiwa kuwa ndio watakaofukuzwa penye hodhi, inaingia
akili kweli waje kutuhadithia na kutuhakikishia kuwa maneno haya wameyasikia
kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), juu ya
kuwa ndani ya hadithi hizi wanatuhumiwa kuwa watakuja kurtaddi na kubadilisha
na kuingiza Bida'h?
Tano:
Wangelikuwa waliokusudiwa katika hadithi hizi ni Masahaba ambao Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwahutubia na
kuwahadithia juu ya matukio haya, asingelikuwa na haja ya kusema: "Watarudishwa makundi ya watu kutoka kwangu."
Au "Watu miongoni mwa Sahibu zangu
watarudishwa penye hodhi." Au akasema: "Kisha
atachukuliwa mmojawapo miongoni mwa sahibu zangu." Badala yake
angeliwaambia moja kwa moja bila kuwaficha, akawaambia kwa mfano: "Mtaondolewa penye hodhi, na kupelekwa mbali
nami." Au "Fulani na fulani
mtaondolewa penye hodhi." Na maneno yenye mfano huo, hii ikiwa ni
dalili nyingine kuwa Masahaba sio hawa waliokusudiwa katika riwaya hizi.
Sita:
Lafdhi zilizokuja katika riwaya hizi kama vile 'Rahat' ÑåØ na maana yake ni kikundi cha watu wasiotimia kumi nk. Ni dalili kuwa
watakao ondolewa ni wachache sana.
Saba:
Wengine wakatowa hata majina ya baadhi ya Masahaba watakaotolewa penye hodhi.
Na sisi tunawauliza; Wametowa wapi kauli za kuwahusisha baadhi ya Masahaba kuwa
wao ndio watakao ondolewa penye hodhi, na kwamba wao ndio waliortaddi na
kuzusha mambo katika dini, kisha wakawapangia wengine kuwa hao hawataondolewa?
Wakati hadithi hazikutaja kwa majina yupi ataondolewa na yupi atakayebaki.
Ushahidi walioutumia dhidi ya wenzao unaweza pia kutumiwa dhidi ya wanaowataka
wao, juu ya kuwa sisi hatusema hivyo, hasa kwa vile hapana nassi inayoeleza kwa
uwazi kuwa Fulani ataondolewa na Fulani atabaki. Hadithi sahihi zimetuthibitishia kusifiwa kwa
Masahaba wote kwa ujumla, na kututhibitishia pia kuwa wao ni watu wa Peponi.
Kwa
hivyo tunasema; Hao Masahaba mnaowadhania kuwa watarudishwa penye hodhi, zipo
dalili nyingi sana kutoka kwenye Qur'ani na Sunnah zenye kuwasifia na
kuwatakasa kwamba wao ndio walioamini hasa na kututhibitishia kwa dalili
isiyokuwa na shaka kuwa wao ni watu wa Peponi.
Kutokana
na haya, haki inadhihiri, na utatanishi unatoweka kwa sababu ya ushahidi
usikuwa na uzito wowote.
Tunamuomba
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Atupe mwisho mwema na atufufue chini ya
bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) pamoja na
Masahaba wake watukufu (Radhiya Llahu anhum).
Kwa kumaliza tunasema:
Kwanza; waliokusudiwa kuwa
ni Masahaba katika hadithi hizi ni wanafiki waliokuwa wakijifanya Waislamu
mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).
Mwenyezi Mungu amesema:
æóãöãøóäú Íóæúáóßõãú ãöäó ÇáÇÚúÑóÇÈö
ãõäóÇÝöÞõæäó æóãöäú Ãóåúáö ÇáúÜãóÏöíäóÉö ãóÑóÏõæÇ Úóáóì ÇáäøöÝóÇÞö áÇ
ÊóÚúáóãõåõãú äóÍúäõ äóÚúáóãõåõãú ÓóäõÚóÐøöÈõåõãú ãóÑøóÊóíúäö Ëõãøó íõÑóÏøõæäó
Åöáóì ÚóÐóÇÈò ÚóÙöíãò- ÇáÊæÈÉ
Na katika
mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo
walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara
mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.
At Tawbah – 102
Pili; waliokusudiwa ni wale waliortaddi baada ya kufariki
dunia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Inajulikana
kuwa wengi miongoni mwa makabila ya kiarabu yalirtaddi baada ya kufariki dunia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na hawa ndio kwa
ajili yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) atasema:
"Sahibu zangu hawa." Na ataambiwa: "Hujuwi wewe
waliyozusha baada yako. Waliendelea hawa kurtaddi tokea ulipofariki
dunia."
Tatu;
inaweza kumaanisha pia kuwa kila aliyemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) hata kama hakuwa Sahaba kwa maana ya neno hilo, na
dalili ni yule mkuu wa wanafiki Abullah bin Ubay bin Salul aliposema:
íóÞõæáõæäó áóÆöä
ÑøóÌóÚúäóÇ Åöáóì ÇáúãóÏöíäóÉö áóíõÎúÑöÌóäøó ÇáÇóÚóÒøõ ãöäúåóÇ ÇáÇÐóáøó
æóáöáøóåö ÇáúÚöÒøóÉõ æóáöÑóÓõæáöåö æóáöáúãõÄúãöäöíäó æóáóßöäøó ÇáúãõäóÇÝöÞöíäó áÇ
íóÚúáóãõæäó {ÇáãõäóÇÝöÞæä: 8}.
Wanasema:
Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge.
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini.
Lakini wanaafiki hawajui.
Al Munafiqun - 8