Subhaanallah
Imekusanywa na kutafsiriwa na
Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Tunapotufu, tunaizunguka Al Kaaba kuanzia jiwe jeusi
tukiliwacha upande wetu wa kushoto, na maana
yake ni kuwa;
tunaizunguka kwa njia hiyo mara
saba kinyume na mishale (mikono)
ya saa (anti clockwise).
Wataalamu wa sayansi
wanasema kuwa kila chembe ya
atomi (atom), ambazo
ni viduchu vya kila kitu,
ndani yake mna electrons, protons na
neutrons. Electron iliyomo ndani
ya atom, nayo pia inazunguka kinyume na
inavyozunguka mishale ya saa (anti clockwise). Mzunguko ule ule tunaozunguka
sisi tunapotufu Al Kaaba.
Sayari, kama vile Ardhi
(Earth), Mercury, Venus, Jupiter n.k. zinajizunguka zenyewe mzunguko ule ule
kama tunavyoizunguka Al Kaaba kinyume na
inavyozunguka mishale ya saa. Wakati
huo huo sayari
hizo zinalizunguka jua kwa mzunguko huo huo
wa kinyume na inavyozunguka mishale ya saa.
Jua lenyewe nalo linajizunguka
mzunguko huo huo kama
tunavyoizunguka sisi Al Kaaba, na haya
yanatokea katika sayari zote ulimwenguni.
Kila kitu kinatii amri
ya Mwenyezi Mungu na
kuzunguka kama kilivyoamrishwa.
Dr.
Mohammed Ali Albar, Mshauri
wa Matibabu
ya Kiislamu katika King Fahad Medical
Research Center na Mwalimu
katika Chuo kikuu cha Mfalme Abdul Aziz - Jeddah, na ambaye ameandika vitabu vingi vikiwemo;
Aids, Drugs, Waislamu katika Urusi nk. na ambaye pia ni
mjumbe mtendaji katika Halmashuri kuu ya Miujiza
ya Sayansi katika Qurani, anasema:
"Mwenyezi Mungu
Anasema:
إِنَّا خَلَقْنَا الاِنسَانَ
مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ
"Kwa
hakika tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika
(ya mwanamume na mwanamke)."
Suratud Dahar- 2
"Wadudu wa mbegu ya uhai (sperms) ambayo ni maji
ya uzazi ya mwanamume, mnajua
kiasi gani ukubwa wake?" Aliendelea Mwanachuoni huyo , "Nyinyi mnatumia Meter katika vipimo vyenu, au Centimeter
(moja katika mia), na Millimeter (moja katika elfu),
lakini vidudu hivi vya uzazi
kwa sababu ya udogo wake vinapimwa
kwa 'Micron', yaani
(moja katika milioni) na ukubwa
wa kila mdudu
katika hao ni Micron 5 hadi 6.
Wadudu hawa juu ya udogo wao,
mara wanapoingia ndani ya tumbo
la uzazi wanakwenda mbio kuelekea katika
yai la mwanamke (Ovam) kwa
kasi inayoshinda kasi ya bingwa
wa kukimbia ulimwenguni mara mbili, iwapo itakisiwa
kwa ukubwa wake mdudu huyo.
Yai hilo la mwanamke,
'Ovam', ni kubwa kuliko wadudu
hao wa uzazi, Yai
ni zuri, lenye kupendeza sana, na ukubwa
wake ni kiasi cha Micron
120. Juu yake pana mfano wa
taji ambalo wataalamu wa uzazi
wanaliita 'Taji linalongaa', linalotoka katika mfuko unaohifadhi
na kuyapevusha mayai hayo huku
likivutwa kuelekea penye Ovam kupitia ndani ya
mirija ya Falopi (Fallopian tubes).
Mirija hiyo inalivuta
yai hilo
kwa nguvu za nywele nywele
zilizojaa ndani ya tube hizo, huku likiingia humo pole pole, tena kwa maringo
huku liking'aa ili kuwavutia wadudu
hao walikimbilie.
Idadi ya wadudu wanaopatikana katika mchupo mmoja wa maji ya
uzazi (sperms) wanakadiriwa
kufikia milioni mia tatu hadi
milioni mia tano, na wote
hao wanalikimbilia yai hilo, na
karibu wote wanakufa njiani kabla ya kulifikia,
isipokuwa kiasi cha mia tano tu
wanaobaki, na mwisho wao wanafika
nje tu ya
yai hilo.
Mara baada ya
wadudu hao ambao idadi yao inakaribia mia tano wanapolifikia
yai hilo, panatokea jambo la ajabu sana, jambo
ambalo halijagunduliwa isipokuwa katika mwisho wa mwaka
elfu moja mia tisa na
sabini katika karne hii.
Yai hilo 'Ovum'
linaanza kuzunguka mzunguko ule ule
kama tunavyoizunguka Al Kaaba kinyume na
inavyozunguka mishale ya saa, na
wadudu waliobaki nao wanaanza kuzunguka
mzunguko ule ule, tena mara
saba, kisha mdudu mmoja tu
ndiye anayeingia ndani ya yai
hilo na wote
waliobaki wanakufa wakiwa nje ya
yai."
Dr.
Mohammed Ali Albaar anaendelea
kusema:
"Ipo filamu
juu ya tukio
hilo, niliiona
na kumsikia mtangazaji wa kizungu,
akipiga ukelele akisema:
"Sielewi kwa nini wadudu hawa wanalizunguka
yai hili kabla ya kufa?"
Angalia namna gani ulivyomtukuza Mola wako kabla
ya kuingia ndani ya yai
lako ewe mwanadamu kabla hata hujazaliwa. Unalizunguka yai
ukiwa tumboni mwa mama yako kama tunavyoizunguka Al Kaaba, tena mara
saba. Kisha Mola wako anachagua
mmoja tu kati ya wadudu
hao, ambaye ni wewe uliyesalimika miongoni mwa mamilioni waliokuwemo
humo ukaweza kuingia ndani ya
yai hilo, kisha yai likafungika
na wadudu wa uzazi wote
waliobakia wakafa.
Kisha baadaye wanakuja
wadudu wa
uzazi wengine wengi, kwa mamilioni,
lakini wote hao wanaishia mlangoni
tu, wanakufa, haruhusiwi kuingia ndani ya yai
zaidi ya mmoja tu aliyekwishatangulia
kuingia".
سُبْحَانَ الَّذِي خَلَقَ
الازْوَاجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنبِتُ الارْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ
وَمِمَّا لَا
يَعْلَمُونَ
"Ametukuka Mwenyezi Mungu ِAliyeumba dume na jike katika(vitu)
vyote; katika vile ioteshavyo ardhi, na katika nafsi
zao (wanadamu) na katika vile wasivyovijua".
Ya Sin -
36
Na katika Suratul Israa (Bani Israil)
aya ya 44 Mwenyezi Mungu anasema:
تسبح له السماوات
السبع والأرض ومن فيهن وإن من شيء إلا يسبح بحمده ولكن لا تفقهون تسبيحهم إنه كان
حليما غفورا
"Zinamtukuza zote
mbingu saba
na ardhi na vilivyomo ndani
yake. Na hakuna chochote ila
kinamsabihi (Mwenyezi Mungu) kwa sifa
Zake njema. Lakini nyinyi hamfahamu kusabihi (kutukuza) kwake. Hakika Yeye Mwenyezi Mungu ni Mpole
(na) Mwingi wa kusamehe."
Na Akasema:
وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ
بِحَمْدِهِ وَالْمَلاَئِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ
بِهَا مَن يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللّهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ
"Na radi inamsabihi Mwenyezi Mungu kwa kumshukuru na (pia) Malaika
(humsabihi) kwa kumuogopa .
Na (Mwenyezi Mungu) hupeleka mapigo ya radi na kumpiga nayo amtakaye.
Na hao (makafiri)
wanabishana juu ya MwenyeziMungu (kuwa yuko kweli
au hayuko) na
hali (ya kuwa yuko na)
Yeye ni Mkali
wa kuadhibu".
Ar Raad -13
Imesimuliwa na Abi Huraira (Radhiya llahu anhu) kuwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wasallam) amesema:
"Maneno mawili
mepesi ulimini na mazito
katika mizani na yanapendwa sana
na AlRahmani (Mwenyezi Mungu) (nayo ni):
سبحان الله وبحمده سبحان
الله العظيم
"Sub haana Llah Wabihamdihi
Sub haana Llahul Adhiym".
Bukhari na Muslim.