HUKMU ZA KUWEKA SUTRA MBELE YA ANAYESALI
Neno 'Sutra'
maana yake ni hifadhi, kinga, himaya, sitara, ulinzi nk. Na maana yake ni
kuweka kitu mbele yako unapokuwa unasali ili kitu hicho kiwe
Hukmu yake;
Ni
vizuri kwa anayesali kujiwekea 'Sutra' (sitara) mbele yake kwa ajili ya kuzuwia
mtu asipite mbele yake na ili asiwe akianglia huku na kule wakati wa kusali.
Imepokelewa
kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:
"Mmoja
wenu anaposali ajiwekee Sutra na awe karibu nayo."
Abu Daud
na Ibni Majah.
Imepokelewa
pia kuwa Masahaba (RA) walikuwa wakijiwekea mikuki mbele
Maulamaa
wanasema kuwa ni vizuri kujiwekea Sutra ikiwa unahofia mtu asipite mbele yako,
ama ukiwa huhofii basi si lazima, na hii inatokana na hadithi iliyosimuliwa na
Imam Ahmad na Abu Daud na Al Baihaqiy kuwa Ibni Abbas (RA) alisali mahali penye
uwazi na hakuweka mbele yake kitu chochote.
Vipi inapatikana Sutra?
Imepokelewa
kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:
"Anaposali
mmoja wenu basi ajiwekee Sutra mbele yake hata
Ahmad na
Al Hakim
Na
katika hadithi nyingine:
"Ikiwa
hajapata mkuki basi hata fimbo."
Na
akasema:
"Anaposali
mmoja wenu ajiwekee kitu mbele yake, na asipopata kitu basi hata fimbo, na
Ahmad na
Abu Daud na wengine
Imepokelewa
pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amewahi kusali akiielekea
nguzo (
Sutra ya Imam ni Sutra ya maamuma
Sutra ya
Imamu ni Sutra ya maamuma wote walio nyuma yake.
Kutoka
kwa Amru bin Shuaib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake amesema:
"Tulikuwa
safarini pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) katika njia iliyonyanyuka
karibu na Makkah, na ulipowadia wakati wa Sala akatusalisha akiwa ameuelekea
ukuta na kuufanya kuwa kibla na sisi tukiwa nyuma yake. Kondoo akataka kupita
mbele yake, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) akawa anamzuwia asipite mpaka
akamlazimisha apite nyuma yake."
Imam
Ahmad na Abu Daud.
Na
kutoka kwa Ibni Abbas (RA) amesema:
"Nilikuwa
nimepanda punda na wakati huo nilikuwa nishabaleghe na Mtume (SAW) alikuwa
akisalisha watu Mina, nikapita mbele ya baadhi ya safu za watu wanaosali nyuma
yake, nikampumzisha punda na kuingia
ndani ya safu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) hakunikataza."
Imepokelewa
na maimam wote
Na hizi
ni dalili kuwa haijuzu kupita mbele ya imamu, lakini inajuzu kupita mbele ya
safu za maamuma kwa sababu Sutra ya imamu ni Sutra ya maamuma.
Haramu kupita mbele ya anayesali
Anasema
Abu Juhaym kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:
"Lau
kama angejuwa malipo yake (dhambi zake) mwenye kupita mbele ya anayesali, basi
angehiari kungoja arubaini kuliko kupita mbele yake."
Hakutaja
kama hizo 40 ni siku au miezi au miaka.
Imepokelewa
na maimamu wote.
Wakiisherehesha
hadithi hii, maulamaa waanasema:
"Hii
kama anasali akiwa ameweka mbele yake Sutra. Ikiwa hajaweka Sutra basi si
haramu kupita mbele yake. Na ikiwa amejiwekea Sutra, basi anayo haki ya
kumsukuma na kumzuwia yeyote asipite mbele yake awe ni mwanadamu au
mnyama."
Imepokelewa
kuwa siku moja Abu Said al Khodari (RA) alikuwa akisali na mtu mmoja alijaribu
kupita mbele yake, na Abu Said (RA) akamzuwia na alipojaribu kupita kwa nguvu
akamsukuma.
Alipoulizwa
kwa nini alifanya hivyo akasema:
"Nilimsikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) akisema:
"Mmoja
wenu akisali na mbele yake amejiwekea Sutra kujisitiri na watu, basi mtu yeyote
akitaka kupita baina yake na baina ya Sutra hiyo amzuwie na akikataa apigane
naye kwani huyo ni shetani."
Bukhari
na Muslim