·
Muhammad Baawazir
BismiLLaah
WalhamduliLLaah Waswalaatu Wassalaamu ‘alaa RasuuliLLaah, wa ba'ad
Ni
mwezi ambao Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم alikuwa
akifunga
"
كان رسول الله
صلى الله عليه
وآله وسلم
يصوم حتى نقول
لا يفطر،
ويفطر حتى
نقول لا يصوم،
وما رأيت رسول
الله استكمل
صيام شهر إلا
رمضان وما
رأيته أكثر
صياماً منه في
شعبان"
رواه
البخاري ومسلم
“Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم alikuwa akifunga hadi tukadhani kuwa hatofungua kamwe, na
alikuwa akiacha kufunga hadi tukadhani hatofunga tena.
Sijamuona Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم akifunga mwezi mzima kama
alivyokuwa akifunga Ramadhaan, na sijamuona akifunga mara nyingi
Swawm
Na Fadhila Za Mwezi Wa Sha'abaan
Juu ya
kwamba Mtume الله
عليه وآله
وسلم صلى alikuwa
akifunga mara
nyingi zaidi katika mwezi wa Sha’abaan kuliko miezi mingine ukiondosha
Ramadhaan,
Imepokewa
kuwa Ibn ‘Abbaas عنهما رضي الله amesema:
‘‘Mtume wa Allaah صلى الله
عليه وآله
وسلم hakuwahi
kufunga mwezi wowote kikamilifu isipokuwa Ramadhaan. [Al-Bukhaariy]
Kukithirisha
kwake Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم ibada katika mwezi huu wa
Sha'abaan, ni kutokana na maelezo yake mwenyewe alipoulizwa na Usaamah bin Zayd
رضي
الله عنه sababu ya kufunga
((ذاك
شهر تغفل
الناس فيه
عنه، بين رجب ورمضان،
وهو شهر ترفع
فيه الأعمال
إلى رب العالمين،
وأحب أن يرفع
عملي وأنا
صائم))
“[Sha'abaan]
ni mwezi ambao watu hawautilii
Hadiyth
hii na Hadiyth nyengine za Mjumbe wa Allaah صلى
الله عليه
وآله وسلم zinahimiza
kufanya amali njema pale watu wanapoghafilika na kumkumbuka Allaah na ‘Ibaadah,
Mjumbe wa Allaah صلى
الله عليه
وآله وسلم amesema:
“Ibaadah wakati wa matatizo (fitnah) ni
Faida na ubora wa kumuabudu Allaah سبحانه
وتعالى wakati watu wameghafilika na
kumkumbuka Allaah سبحانه
وتعالى zimekuja kwa sababu ‘Ibaadah
katika nyakati
Kufunga
katika mwezi wa Sha'abaan ni mazoezi kabla ya
Ramadhaan. Hata hivyo, kufunga mwezi mzima wa
Sha'abaan ni Makruhu (hakupendezi) na ni kinyume na Sunnah za Mjumbe wa Allaah صلى
الله عليه
وآله وسلم.
Ibn
'Abbaas رضي
الله عنهما amesema:
“Msiutangulie
Ramadhaan kwa (kufunga) siku moja au mbili, ila kwa
wale tu wenye mazoea ya kufunga kila mara, na kwa hali hiyo hao wanaweza
kufunga (siku hizo)” Al-Bukhaariy
Pia
imekatazwa kufunga katika mwisho wa Sha'abaan kwa nia ya kutozikosa siku za
mwanzo wa Ramadhaan, isipokuwa kwa wale wenye tabia na mpangilio wa kufunga na
ikawa siku za mwisho za Sha'abaan zimetokezea sambamba na siku ambazo mtu yule
kawaida huwa anafunga, kama vile za Jumatatu na Alkhamiys au imemkuta akiwa
anaendelea kulipa Swawm ya deni.
Imeripotiwa
katika Swahiyh Al-Bukhaariy kutoka kwa Abu Hurayrah رضي
الله عنه kuwa Mtume صلى الله
عليه وآله
وسلم amesema: “Kufunga katika mwisho wa Sha'abban
kumekatazwa ili kuweka tofauti kati ya Swawm za Sunnah na Swawm za faradhi.”
Vile
vile ni kinga ya kuwakinga watu na kuanguka katika mtego wa Shetani, ambaye
amewashawishi watu wa Kitabu kuongeza Swawm zaidi ya zile Allaahسبحانه
وتعالى Alizowafaradhishia. Kwa sababu hiyo hiyo, imekatazwa pia kufunga siku ya ‘Yawmu
Shakk”. Siku ya shaka ni ile siku ambayo
watu hawana uhakika juu ya kuanza kwa Ramadhaan, kwa sababu ya hali ya mawingu
kufunga na mwezi kutoonekana au sababu nyinginezo.
Na
Imaam Ibn Rajab رحمه
الله amesema:
''Funga katika Sha'abaan ni bora kuliko
funga katika masiku matakatifu (ambayo ni Dhul Qa'adah, Dhul Hijjah,
Muharram na Rajab zilizotajwa katika Suratut Tawbah Aayah ya 36), na Swawm
zilizo bora ni zile (zitambulikazo) ambazo ziko karibu na Ramadhaan, kabla
au baada. Hadhi na daraja ya Swawm hizi ni
Nisfu
Sha'abaan: Kuna Ukweli Wowote?
Pamoja na ubora huo na daraja hiyo ya mwezi wa Sha'abaan,
Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم hakuihusisha siku maalum katika mwezi wa Sha'abaan
kufunga. Alikuwa akifunga kwa wingi iwezekanavyo lakini hakutueleza na wala
hakuichagua siku ya tarehe 15 ya Sha'abaan kufunga kutokana na sifa zake
alizozitaja hapo nyuma, ila tu ametaja Fadhila za usiku huu kutokana na hadiyth
hii ambayo hata hivyo haikutaja kuwa kuna ibada maalum inapaswa ifanyike siku
hii au usiku wake.
عن
أبي موسى
الأشعري رضي
الله عنه عن
رسول الله صلى
الله عليه
وسلم قال: ((إن
الله ليطلع في
ليلة النصف
من شعبان
فيغفر لجميع
خلقه إلا
لمشرك أو
مشاحن))
رواه
ابن ماجة
وحسنه الألباني
في السلسلة
الصحيحة
Imetoka kwa
Abu Muusa Al-Ash'ariy رضي
الله عنه kwamba
Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم kasema:
“Allaah سبحانه
وتعالى Hutokea Katika usiku wa 15 wa Sha'abaan, na Huwasamehe
wote isipokuwa Washirikina na wale wenye uadui kwa wengine.” Ibn
Maajah na imesemwa kuwa ni Hadiyth Hasan na Shaykh
Al-Albaaniy.
Jambo
la kushangaza ni kwamba wengi katika Waislam kwa uchache wa elimu na pia kwa
kufuata mafundisho yasiyo sahihi ambayo amesingiziwa nayo Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم, wameitenga siku hiyo ya Nisfu Sha'abaan kufunga na kusimama
kisimamo cha usiku na kusoma nyiradi mbalimbali ambazo wamezitunga na pia
kusherehekea kwa namna mbalimbali. Sehemu nyingi ulimwenguni hufanya sherehe na Swawm pamoja na kuswali
Kuna
waliyoipa jina la Shab-E-Baraat au Laylatul Bara-at (usiku wa
kuachiwa huru [na moto], au wa kusamehewa) kama huko bara
“Mwenyeezi
Mungu Anawaachia huru waja wake walio motoni kulingana na
idadi ya nywele zilizo katika ngozi za mbuzi/kondoo wa Banu Kalb.”
Vilevile
kuna imani potofu kabisa katika siku hii, ambapo kuna baadhi ya watu wanaamini
kuwa kushuka kwa Malaika na Ruuh usiku huo
Katika
Surah hiyo ya Al-Qadr ambayo watu hao wameifasiri na
kuielewa kinyume, Allaah سبحانه
وتعالى Anasema:
}}تَنَزَّلُ
الْمَلَائِكَةُ
وَالرُّوحُ
فِيهَا
بِإِذْنِ
رَبِّهِم
مِّن كُلِّ
أَمْرٍ{{
{{Huteremka
(katika usiku huo wa Qadr) Malaika pamoja na Ruuh kwa
idhini ya Mola wao kwa kila jambo}} Al-Qadr: 4.
Pia
wengine wameuhusisha huo usiku wa katikati ya mwezi wa
Sha'abaan na maneno 'Laylati-m-Mubaarakatin' (Usiku uliobarikiwa) yaliyo
katika Aayah ya 3 katika Suratud-Dukhaan isemayo:
}}إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ
فِي لَيْلَةٍ
مُّبَارَكَةٍ
إِنَّا
كُنَّا
مُنذِرِينَ{{
{{Kwa
yakini tumeteremsha (Qur-aan) katika usiku uliobarikiwa, bila shaka sisi ni waonyaji}} Ad-Dukhaan: 4
Wakifasiri
huo usiku uliobarikiwa kuwa ni wa 15 Sha'abaan. Lakini
hiyo ni tafsiri potofu kabisa kwani inajulikana wazi
bila shaka kuwa 'Laylatim Mubaarakatin' iliyokusudiwa hapo kwenye Surah
hiyo ni usiku uliopo katika mwezi wa Ramadhaan. Na
}}شَهْرُ
رَمَضَانَ
الَّذِيَ
أُنزِلَ
فِيهِ
الْقُرْآنُ
هُدًى
لِّلنَّاسِ
وَبَيِّنَاتٍ
مِّنَ
الْهُدَى
وَالْفُرْقَانِ{{
{{Ni
mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa (ndani ya mwezi
huo) Qur-aan ili uwe uongozi kwa kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na
upambanuzi (wa baina ya haki na batili)...}} Al Baqarah: 185
Basi
hayo wayasemayo baadhi ya watu kuwa usiku huo ni usiku wa kuamkia mwezi 15
Sha'abaan ambao pia wanauita 'Qismatur Rizq' (Mgao wa riziki) si maneno
ya kweli, bali ni uzushi na upotofu uliozoeleka na ambao umeenezwa katika Dini
hii tukufu na kuichafua na kuivuruga hadi imekuwa sasa ni vigumu sana
kupambanua la batili na la haki katika Dini hii iliyokamilika na isiyo na haja
ya nyongeza za waongezao.
Pia
du’aa zisomwazo ndani ya usiku huo zina kila aina ya uzushi upinganao na Qur-aan,
Wanachuoni
mabingwa wa fani ya Hadiyth wamebaini kuwa hakuna hata
Hadiyth moja iliyo sahihi katika Hadiyth zilizozagaa ambazo zinazungumzia
fadhila na utukufu wa mwezi wa Sha'abaan au haswa tarehe 15 ya Sha'abaan
isipokuwa hiyo iliyotajwa juu ya kwamba Allaah سبحانه
وتعالى Hutokea usiku huo na kuwasamehe waja wake isipokuwa
waliomshirikisha na wenye uadui. Na
zaidi ni kuwa zote ima dhaifu au mawdhu'u (za uongo/
kutungwa). Wanachuoni mbali mbali kama Maimaam Ash-Shawkaaniy, Ibnul Jawziy,
Ibnu Hibbaan, Al Qurtubiy رحمهم
الله حميعا wamelaumu
mno na kuzikana Hadiyth au mapokezi hayo yasiyo sahihi kuhusiana na Sha'abaan
au siku hiyo ya Nisfu Sha'abaan. (Rejea vitabu vyao
Katika
baadhi ya Hadiyth za kutungwa ni
“Katika
siku hii (ya 15 Sha'abaan) Mwenyeezi Mungu Huwaachia huru watu kutoka katika
Moto wa Jahannam idadi inayolingana na nywele zilizomo
katika kondoo wa kabila la Banu Kalb.” Na Hadiyth hii Imaam
At-Tirmidhiy anasema ni mbovu na dhaifu.
Na
nyingine inasema:
“Yeyote
atakayeswali rakaa kumi na nne za Swalah katika usiku
wa tarehe 15 ya Sha'abaan atapata ujira ulio sawa na kufunga Swawm na Hija ya
miaka ishirini.”
na pia isemayo:
“Kuwa
ubora wa siku hii ni kwa sababu jaala ya mwanaadam ndiyo
huwa katika siku hii, pia mipango ya mazazi na vifo hupangwa.”
Na
riwaya dhaifu nyinginezo ni
Hadiyth
zote hizo hapo juu kwa matamshi hayo, hazina
uthibitisho wowote wa usahihi wake kisheria. Kwa hiyo hakuna Hadiyth hata moja
sahihi yenye kuthibitisha kuitenga au kuihusisha siku ya tarehe 15 ya Sha'abaan
kufanya ‘Ibaadah maalum
Pia
tunapata mafundisho kuwa kutenga siku maalum kwa ibada
maalum ni jambo linalokwenda kinyume na sheria, isipokuwa lile lililotajwa
au kufundishwa na Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم
Mwenyewe
Mtume صلى
الله عليه
وآله وسلم anasema: “Msitenge Usiku (wa
kuamkia) Ijumaa kuutenga na usiku mwengine (wowote) kwa kuswali, na msitenge
siku ya Ijumaa miongoni mwa masiku kwa kufunga, ila yule aliyezoea
kufunga na funga yake ikaangukia siku hii [Ijumaa].” Muslim
Na hili
latuthibitishia wazi kuwa ‘Ibaadah na matendo yote
mazuri hayafanywi katika siku fulani au usiku maalum tu na kuachwa nyingine,
maana kufanya hivyo hakutatimiza wajibu wa Mja wa kumuabudu Mola wake. Mja
hupaswa kumuabudu Mola wake siku zote za umri wa
maisha yake yote hadi atakapoiaga dunia, kwani ‘Ibaadah ni kusudio la msingi la
kuumbwa kwake. Anasema Allaah سبحانه
وتعالى:
}}وَاعْبُدْ
رَبَّكَ
حَتَّى
يَأْتِيَكَ
الْيَقِينُ{{
{{Na
umuabudu Mola wako hadi ikufikie hiyo yakini (Nayo ni
mauti)}} Al-Hijr: 99.
Na
ndivyo ilivyokuwa ada ya Mtume صلى الله
عليه وآله
وسلم kumuabudu Mwenyeezi Mungu muda wote wa
mwaka mzima, masiku yote, usiku na mchana alitumia katika
kumtumikia Allaah وتعالى سبحانه.
Ukumbusho
Katika Sha'abaan
Iwapo bado unahitajika kulipa Swawm za faradhi za Ramadhaan
iliyopita, fanya haraka kulipa kabla ya Ramadhaan nyingine haijafika. Hairuhusiwi kuchelewesha Swawm zilizokosekana mpaka kufikia
Ramadhaan inayofuata, isipokuwa katika hali ya ulazima (mfano udhuru
unaokubalika ambao umeendelea baina ya Ramadhaan mbili).
Mama wa Waumini 'Aaishah عنها رضي
الله amesema,
“Ilikuwa
nnazo siku za kulipa za Ramadhaan na sikuweza kuzilipa
isipokuwa (katika mwezi wa) Sha'abaan.” Al-Bukhaariy
Yeyote
aliyekuwa na uwezo wa kulipa Swawm zilizompita/
zilizomfutu kabla ya Ramadhaan (ya pili) na asifanye hivyo, basi atalazimika
kuzilipa baada ya Ramadhaan (ya pili), na zaidi analazimika kutubia na kumlisha
maskini mmoja kwa kila siku iliyompita/ iliyomfutu. [Huu ni msimamo wa Maimam Maalik, Ash-Shafi’iy na Ahmad]
na unaoonekana kuwa sahihi zaidi.
Wa Allaahu A’alam