Muhammad Faraj
Hiki ni kisa cha kusisimuwa juu ya Masahaba watatu
(Radhiya Llahu anhum), waliofanya makosa, na walipomuendea Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) kumuomba msamaha, aliwataka wasubiri
mpaka Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala atakapoteremsha hukmu juu yao, wakati
wenzao waliofanya kosa lile lile walipomuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) hakuwataka wasubiri, bali aliwakubalia udhuru wao,
akawaombea maghfira, kisha akamauchia Mwenyezi Mungu juu ya ukweli wa udhuru
wao.
Hili ni fundisho kubwa kwetu Waislamu la kujifunza
subira katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, pamoja na kujifunza namna gani
Masahaba (Radhiya Llahu anhum) walikuwa watiifu kwa kiongozi wao na kipenzi
chao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam).
Masahaba watatu hawa (Radhiya Llahu anhum) walisubiri
mpaka ardhi yote wakaiona dhiki, juu ya ukubwa wake, na mpaka wakatambua kuwa
hapana pa kukimbilia isipokuwa kwake Subhanahu wa Taala.
Hiki ni kisa cha vita vya Tabuk, ambapo kwa mara ya
mwanzo jeshi la Waislamu lilijitayarisha kupambana na jeshi kubwa la Warumi
katika mwaka wa 9 Hijri wakati wa joto kali sana, katika vita vilivyojulikana
kama ni Vita vya Dhiki.
Watu wapatao themanini katika watu wa Madina
hawakufuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
kwenda Tabuk kushiriki katika vita hivyo, watu ambao wengi kati
Walikuwepo pia wasioshiriki kwa sababu ya maradhi au
udhaifu wa siha zao au kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kumiliki wanyama wa
kuwapanda kuwapeleka vitani. Na wengine hawakushiriki kwa sababu ya uvivu tu.
Kaab bin Maalik (Radhiya Llahu anhu), mmoja katika
Masahaba waliojulikana kwa ucha Mungu ambaye pia alikuwa mmoja katika washairi
maarufu
Kaab alishiriki pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) katika vita vyote dhidi ya washirikina
isipokuwa vita vya Badar, na hii ilikuwa kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alipotoka na kundi dogo la Waislamu wapatao
mia tatu na kidogo katika vita hivyo vya Badar hakuwa na nia ya kupigana vita
vikubwa, bali alikuwa na nia ya kuuteka msafara mdogo wa Abu Sufiyan uliokuwa
ukitokea nchi ya Sham.
Katika vita vya Uhud, Kaab (Radhiya Llahu anhu)
alibadilishana nguo na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam). Yeye alivaa nguo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam) zenye rangi ya manjano na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wa Sallam) alivaa nguo za Kaab (Radhiya Llahu anhu).
Katika vita hivyo Kaab (Radhiya Llahu anhu) alipata
majeraha kumi na moja.
Hebu tumuache Kaab mwenyewe (Radhiya Llahu anhu)
atuhadithie kisa chake cha kutokushiriki katika vita hivyo vya Tabuk.
Anasema Kaab (Radhiya Llahu anhu):
Sikupata kuwa katika hali nzuri kwa hali
na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) alikuwa katika hali ya kujitayarisha, na Waislamu pia wakawa
katika hali hiyo, na watu walikuwa wengi
Nikasema:
'Kesho mimi nitajitayarisha nijiunge nao.'
Nikawa nakwenda nikirudi bila ya kufanya
chochote, huku nikijisemesha nafsini mwangu:
'Wakati wowote ninapotaka nitaweza
kujitayarisha nijiunge nao'.
Nikaendelea na hali hiyo mpaka mambo
yalipoanza kupamba moto, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam) alipoamua kuondoka asubuhi ya siku ya pili yake pamoja na Waislamu, na
mimi bado sikuwa nimejitayarisha kwa chochote.
Nikasema:
'Nitajitayarisha siku ifuatayo baada ya
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) kuondoka, au hata
baada ya siku mbili kisha nitakutana nao njiani kabla ya wao kuwasili Tabuk.'
Nikatoka asubuhi ya siku ya pili ili
nianze kujitayarisha na kununua mahitajio yangu ya vitani, hatimae nikarudi
nyumbani bila kufanya chochote.
Nikawa katika hali hiyo mpaka zikatufikia
habari kuwa Waislamu wamekwishawasili Tabuk na kwamba vita vishaanza, ndipo
iliponipitikia niondoke ili niwawahi.Yareti ningefanya hivyo.
Lakini sikujaaliwa.
Nikawa kila ninapotoka nje ya nyumba yangu
na kuonana na watu, ninahuzunika
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) hakuuuliza juu yangu mpaka walipowasili Tabuk, akasema huku
akiwa amekaa pamoja na watu:
"Amefanya nini Kaab?"
Mmoja katika watu wa Bani Salama akasema:
"Limemzuwia tandiko
Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu)
akasema:
"Maneno mabaya yaliyoje uliyosema;
Wallahi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi tunavyomjua ni mtu anayependa kheri
tu".
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) akanyamza.
Kaab (Radhiya Llahu anhu) anaendelea kuelezea:
"Niliposikia kuwa misafara inaanza
kurudi nikaanza kujisemesha huku nikifikiri uongo upi niuseme hata Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) (anisadiki na) asighadhibike
nami? Nikawaendea jamaa zangu wale wenye hekima kutaka ushauri wao.
Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) alipowasili Madina, mimi nilikuwa nishafikia uamuzi
kuwa sina budi kumuambia ukweli, na kwamba nikisema uongo sitoweza kuokoka nao.
Nikaamua kuwa lazima niseme kweli tu.
Asubuhi iliyofuata Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) aliwasili, na ilikuwa kawaida yake anapowasili
kwanza huenda msikitini kusali rakaa mbili, kisha hukaa hapo muda kidogo kwa
ajili ya kusikiliza matatizo ya watu.
Wale waliobaki Madina wasiende vitani
wakaanza kumuendea huku wakimtolea (kila aina ya) udhuru, na walikuwa kiasi cha
watu themanini na kidogo hivi.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) aliwakubalia wote udhuru wao na kuwaombea maghufira na
kumuachia Mola wao ukweli wa udhuru walioutoa. Nilipomsogelea mimi na
kumsalimia alitabasamu huku akionyesha dalili ya kughadhibika nami, kisha
akaniambia:
"Njoo."
Nikamuendea mpaka nikakaa mbele yake.
Akaniuliza:
"Nini kilichokufanya ubaki nyuma, si
ulikuwa ushajitolea kupigana?"
Nikamuambia:
"Ndiyo, Wallahi ningeulizwa suali hili
na mwengine asiyekuwa wewe katika watu wa dunia ningeweza kusalimika kwa kutoa
udhuru wowote ule. Lakini nilijishauri
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) akaniambia:
"Ama huyu amesema kweli. Inuka na
ungoje mpaka Mwenyezi Mungu atakapotoa uamuzi wake juu yako."
Nikainuka na kuondoka hapo, na watu wa
kabila la Bani Salamah wakainuka kunifuata, wakaniambia:
"Wallahi sisi tunavyokujuwa ni kuwa
hujapata kufanya kosa kabla ya hili, kwa nini umeshindwa kutoa udhuru (wowote)
Wakawa wanaendelea kunilaumu mpaka
nikafikiria nirudi tena kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam) na kutoa udhuru wowote na kujidanganya nafsi yangu.
Kisha nikawaambia:
"Yuko mwengine aliyekuwa
Wakasema:
"Wawili, wamesema kama ulivyosema na
wakaambiwa
Nikauliza:
"Nani hao?"
Wakaniambia;
"Mirara bin Rabial Umariy na Hilal bin
Umayyah Al Waqii-y."
Hawa ni watu wawili wacha Mungu waliopigana
vita vya Badar na walijulikana kuwa ni wenye mfano mwema.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) akaamrisha sote watatu tusisemeshwe na mtu.
Tukawa tunawaepuka watu na wao wanatuepuka.
Haukupita muda watu wakaanza kutubadilikia hata nikaichukia ardhi ikawa
'Mdomo wake ulitikisika kuijibu salamu au haukutikisika?'
Mara nyingi huswali karibu yake, na baada
ya swala, humtizama kwa kuibiaibia huku nikijishughulisha na dua baada ya
Swala, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alikuwa mara
nyingine akiniangalia, lakini ninapomuangalia mimi, yeye huugeuza uso wake.
Dhiki ya kupigwa pande ilipozidi nikaamua
siku moja kwenda nyumbani kwa Abi Qatadah ambaye ni mtoto wa ami yangu, na
nilikuwa nikimpenda
Nikamuambia:
"
Akanyamaza asinijibu kitu. Nikamuuliza tena
suala
'Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio
wanaojua.'
Machozi yakanitoka. Nikaondoka na kuruka
ukuta nikatoka nje.
Siku moja nilipokuwa nikitembea sokoni
nikamsikia mmoja katika watu wa Sham aliyekuja kufanya biashara ya vyakula
akisema:
'Nani atakayenipeleka kwa Kaab bin Maalik?'
Watu wakamuelekeza kwangu. Akanijia na
kunipa barua iliyotoka kwa mfalme Ghassan iliyoandikwa yafuatayo:
'Nimepata habari kuwa sahibu yako amekupiga
pande, na Mola wako amekufanya usiwe na raha, kwa hivyo njoo kwetu
tutakuliwaza.'
Nikasema moyoni mwangu:
'Huu pia ni mtihani mwengine.’
Nikaitumbukiza barua ile ndani ya tanuri la moto na
kuiunguza, na ilipofika siku ya arubaini katika zile siku hamsini, mjumbe
kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alinijia na
kuniambia:
"Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) anakuamrisha usimkaribie mkeo."
Nikamuuliza:
'Nimtaliki au nifanyeje?'
Akaniambia:
'Bali uwe mbali naye
na usimkaribie.'
Na wenzangu wale
wawili wakapewa amri kama niliyopewa mimi.
Nikamuambia mke wangu:
'Nenda kwa wazee wako
na ubaki kwao mpaka Mwenyezi Mungu atakapotoa amri yake.'
Mke wa Hilaal bin
Umayyah alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
na kumuambia:
'Ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu, kwa hakika mume wangu Hilal ni mtu mzima
asiyeweza kujitumikia
mwenyewe na hana mfanya kazi wa kumsaidia, utachukizwa iwapo nitabaki kwake na
kumhudumia?'
Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) akamuambia:
'Hapana
(sitochukizwa), lakini asikukaribie'.
Akasema:
'Wallahi yeye hana
haja ya kufanya jambo lolote. Tokea yalipotokea yaliyotokea, mpaka leo hana
isipokuwa kulia tu.'
Baadhi ya watu wangu
wakaniambia:
'Na wewe ungelimuomba
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) amruhusu mkeo
akutumikie kama alivyomruhusu mke wa Hilaal bin Umayyah.'
Nikawaambia:
'Wallahi mimi
sitomuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam). Sijui
atanijibu nini nitakapomuomba, kwa sababu mimi ni kijana bado.'
Nikaendelea katika
hali hiyo kwa muda wa siku kumi nyingine, mpaka zikakamilika siku hamsini tokea
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alipowataka watu
wasitusemeshe.
Baada ya kuswali swala
ya alfajiri ya siku ya hamsini, nikapanda juu ya dari la mojawapo ya nyumba
zetu na kukaa. Na wakati nilipokuwa katika hali ile aliyoisema Mwenyezi Mungu
kuwa:
'Hata ardhi ikawa dhiki
kwao, pamoja na wasaa wake'
Nikasikia sauti kali
ikitokea juu ya jabali ikisema:
'Ewe Kaab pokea habari njema.'
Pale pale nilipo nikaporomoka na kusujudu,
nikajua kuwa faraja imekwishawasili.
Baada ya swala ya alfajiri Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) aliwatangazia watu juu ya
kusamehewa kwetu na Mwenyezi Mungu, na watu wakatoka na kuanza kutupa habari
njema hizo. Wengine wakaja kwangu na wengine wakaenda kwa sahibu zangu.
Walikuja wakiwa wamepanda wanyama wao na
wengine kwa miguu kwa ajili ya kutupongeza. Na aliponijia yule niliyeisikia
sauti yake akinipa habari njema pale mwanzo, nilimvisha guo langu
'Tunakupongeza kwa toba iliyokuja kutoka kwa
Allah.'
'Nilipoingia msikitini, Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alikuwa amekaa akiwa amezungukwa na
watu, na Twalha bin Ubaydullah alikuwa wa mwanzo kunijia mbio na kunipa mkono
na kunipongeza. Hakusimama na kunipongeza katika Muhajirin mahali pale
isipokuwa Twalha, sitomsahau kwa tendo
Nilipomsalimia Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) huku uso wake ukiwa unang'ara kwa furaha, na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) anapofurahi, uso wake
huwa unang'ara mfano wa kipande cha mwezi, akaniambia:
'Pokea habari njema za kufikiwa na siku
bora kupita siku zote tokea ulipozaliwa.'
Nikamuuliza:
'Msamaha huu umetoka kwako ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu, au kutoka kwa Mwenyezi Mungu?'
Akanijibu:
'
Nikiwa bado nimekaa mbele yake nikamuambia:
'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya
kutubiwa kwangu huku, nataka kutoa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) akaniambia:
'Zuwia
Nikamuabia:
'Mimi nitazuwia sehemu yangu ya Khaibar'.
Nikawa kila siku naiambia nafsi yangu:
'Mweyezi Mungu ameniokoa kwa ajili ya
kusema kweli. Kwa ajili hiyo katika maisha yangu sitotamka isipokuwa kweli tu.
Kwani Wallahi simjui Muislamu yeyote aliyepata mtihani mkubwa kutoka kwa Allah
kwa ajili ya kusema kweli tokea siku niliyozungumza na Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam) mpaka leo hii, kuliko mtihani nilioupata mimi.
Na mimi namuomba Mwenyezi Mungu anihifadhi katika siku zangu zilizobaki."
(Mwisho wa maneno ya Kaab bin Maalik (Radhiya Llahu
anhu).
Kisa hiki ni sababu ya kuteremshwa kwa aya zifuatazo
zilizomo katika Suratul Tawbah:
"Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya
Nabii na Wahajiri na Ansari
walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada
ya kukaribia nyoyo za baadhi
Na pia wale watatu walio achwa nyuma
hata dunia wakaiona dhiki juu ya
ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na
wakayakinika kuwa hapana pa
kumkimbia Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake
Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika
Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu”.
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na
kuweni pamoja na wakweli.
Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio
jirani zao kubakia nyuma
wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi
zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa
ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha
makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni
kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema.
Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa,
wala hawalivuki bonde, ila
huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora
ya waliyo kuwa wakiya- tenda.”
At Tawbah -117- 121
Na haya ndiyo wanayostahiki Wahajir (Watu wa Makka) na
Ma Ansar (Watu wa Madina), pamoja na makabila yanayokaa nje ya Madina, kwa
sababu wao ndio walioubeba Uislamu juu ya vichwa vyao na wakapambana na kila
aina ya dhiki, tabu mateso.
Watu hawa walikuwa wakati wote wakisubiri ishara tu
kutoka kwa kiongozi wao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam) akiwataka kwenda kupigana Jihadi, na bila ya kurudi nyuma walikuwa
wakiuitikia mwito wake.
Walistahiki maghfira na ujira mwema kutoka kwa Mola
wao kutokana na kila bonde walilopitia na kila usiku waliokesha na kila njaa
waliyostahamili huku wakiwaghadhibisha makafiri kwa kushikamana kwao na kwa
ushujaa wao. Walistahiki maghfira kutokana na kila jeraha walilopata katika
kupigana Jihadi, na kutokana na kila kidogo au kikubwa walichotoa kwa ajili ya
Mola wao.
Ama kuhusu wale wanafiki waliobaki nyuma bila udhuru
wowote kisha wakaenda kutoa udhuru wa
uongo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) Mwenyezi
Mungu alisema juu
"Watakutoleeni udhuru mtapo
warudia. Sema: Msitoe udhuru; hatukuaminini.
Mwenyezi Mungu amekwisha tueleza khabari
zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha
mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa
mkiyatenda.
Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu mtakapo rudi
kwao ili muwaachilie mbali.
Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najsi,
na makaazi
kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyachuma.
Wanakuapieni ili muwe
radhi nao. Basi hata mkiwa radhi nao nyiye,
Mwenyezi Mungu hawi
radhi na watu wapotofu."
At Tawbah -
.94-96