![]()
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuletea mwezi
huu mtukufu wenye Rehma na
Maghfira na kutuepusha na Moto,
na pia tunamshukuru
kwa kutupa fursa hii mara
moja kila mwaka ya kujirekebisha,
kutubu na kurudi kwake Subhanahu
wa Taala.
Kule kuwaona Waislamu kwa furaha na
hamu kubwa wakikimbilia kuuona mwezi ukiandama ili siku ya
pili yake waanze kufunga, ni dalili ya
kuupenda kwao mwezi huu mtukufu.
Na kule kuwaona wakijaa misikitini kwa ajili ya
kusali Sala zao za fardhi
pamoja na Sala ya Taraweh
ni dalili ya kuupenda na
kuufurahikia kwao mwezi huu mtukufu.
Kule kuwaona Waislamu wakishikamana na misahafu na kuisoma
kwa wingi, ni dalili ya
kuyapenda maneno ya Mola wao
Mtukufu Subhanahu wa Taala na
kuupenda kwao wahyi alioteremshiwa Mtume wao Muhammad (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) ndani ya mwezi
huu mtukufu.
Kule kuwaona Waislamu ndani ya mwezi
huu mtukufu wakihudhuria kwa wingi katika madarsa,
ni dalili kuwa nyoyo zao
zimeuelekea
Na Mwenyezi Mungu ameufadhilisha mwezi huu mtukufu
kupita miezi yote, na Yeye
Subhanahu wa Taala ndiye Mwenye
kufadhilisha anachokitaka juu ya kingine.
Ni mwezi wa Rehma,
Hata thawabu zake mwezi
huu zinakhitalifiana na miezi mingine.
Ibada zote Mwenyezi Mungu
anawalipa waja wake moja kwa kumi,
isipokuwa saumu na subira, hivi
Mwenyezi Mungu analipa kupita kiasi.
Katika kufanya amali njema
kwa mfano, Mwenyezi Mungu humlipa mja wake mfano wa amali
hiyo Moja Kwa Kumi.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Afanyae
kitendo kizuri, atalipwa mfano wake mara kumi, na
afanyae kitendo kibaya (kimoja) hatalipwa ila sawa
nacho tu, nao hawatadhulumiwa".
Katika kuwasaidia ndugu wa nasaba na
katika kusaidia katika kila jambo
la kheri, Mwenyezi Mungu humlipa mja
wake mfano wa amali hiyo Moja
Kwa Mia Saba, Na Humzidishia
Amtakaye.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Mfano
wa wale wanaotoa
Al Baqarah-
261
Lakini katika SAUMU na SUBIRA, Mwenyezi Mungu humlipa mja wake Pasipo Hisabu
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na bila
shaka wafanyao SUBIRA watapewa ujira wao Pasipo hisabu".
Al Zumar - 10
Na katika hadith al Qudusiy Mwenyezi Mungu anasema;
"Amali
zote za mwanadamu
ni zake, isipokuwa Saumu, hiyo ni Yangu,
na Mimi ndiye nitakayemjazi. Anaacha chakula chake na
kinywaji chake na matamanio yake
kwa ajili Yangu…"
Na katika riwaya nyingine;
"Amali
zote ninalipa moja kwa kumi,
na nyengine zinafikia moja kwa mara mia
saba, isipokuwa saumu, (Funga), hii Mimi Mwenyewe ninamlipa."
Maulamaa wameleta tafisiri nyingi katika kauli
ya Mwenyezi Mungu aliposema;
"Isipokuwa saumu hiyo ni
yangu."
Wakasema kuwa; juu ya
kuwa amali zote ni kwa
ajili Yake Subhanahu wa Taala,
lakini saumu haina riyaa ndani
yake
Kwa mfano katika ibada
ya Sala, mtu anaweza kujionyesha
mbele ya watu kuwa anasali
wakati moyoni mwake hana khushuu
mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini saumu inakhitalifiana
na ibada nyingine kwa sababu
ni kitendo cha moyo, na mtu
anapokuwa peke yake anaweza kula
na kunywa bila kuonekana.
Aliyefunga anapata ujira mara
mbili, ujira kwa ajili ya
kufunga na mwengine kwa ajili
ya kusubiri, maana aliyefunga anatakiwa awe na subira kubwa ya
kujizuwia na matamanio ya nafsi,
na pia kustahamili
maudhi ya watu nk.
Kwa ajili hiyo Mwenyezi
Mungu anamlipa pasipo hisabu, na wakati huo
huo anakuwa amefunga na kwa
ajili hiyo jaza yake analipwa
na Mola wake Subhanahu wa Taala.
Mola wetu tutakabalie amali zenu njema
na uzijaalie ziwe halisi kwa
ajili yako – Aamin.