1) Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi,
Waja tuko hamkani,
la kheri hatumaizi
Tumejaa nuksani, usiondoke barizi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
2) Waja tuko hamkani, bakia wetu mpenzi
Tumedhofu
nafusini, keleshi tunu tuenzi
Tutazama madhambini, ukiuka mwana enzi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
3) Tutazama madhambini,
utatushinda uhunzi
Auni Rabbi Muini, tusijegeuka panzi
Misumeno muilini, kuchonga kwetu vibanzi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
4) Auni Rabbi Muini, sasa kwetu
ndio kazi
Vishawishi
vya shetani, bayani vyawekwa wazi
Vioja vya runingani, sumile havimaizi
Muwaddau
Ramadhani, mgeni wetu azizi.
5) Vioja vya runingani, mrama lenda jahazi
Alotufunza mgeni, dawamu maendelezi
Etualika ugeni, Rabbana Mola Mlezi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
6) Alotufunza mgeni,
utamu wa
tunda lozi
Tutakuwa punguwani, kukacha hayo malezi
Wendapo hadi mwakani, tuwe
hai maombezi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
7) Wendapo hadi
mwakani, kuja tena l'azizi
Sote minalfaizini, nabubujika machozi
Hujaja wauka kwani, mgeni
wetu mwombezi?
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
8) Sote minalfaizini,
idi fitri muizzi
Si kuvaa nguo ngeni,
na wala
bora mchuzi
Ni kumkwepa
shetani, nasaha nazibarizi
Muwaddau Ramadhani, mgeni wetu azizi.
9) Ni kumkwepa shetani,
Allah katupa malezi
Tisia si asharani, witiri
beti ni
hizi
Natudumu ibadani, hili ni
langu ombezi
Muwaddau Ramadhani, nabubujika machozi.
Nakutakieni nyote sikukuu njema.
Ndugu yenu,
Ahmed.Rashid