MTUKUFU
RAMADHANI
SWALEH SUHEIL ABEID
1
Kwa jina lako Rahimu
naanza kusimuliya
Mola wetu Mkarimu
Ya Rabi nijaaliya
Nikadiri kukhitimu haya nalokusudiya
Niusifu mwezi mwema mtukufu Ramadhani
2
Rabi
peleka salamu
zende kwa
wetu Nabiya
Mtume wetu Adhimu Muhamadi Hashimiya
Na
Swahaba Akiramu
na Isilamu
jamiya
Niusifu mwezi mwema mtukufu Ramadhani
3
Ya Rabi tupe mwafaka
tufunge bila udhiya
Saumu yenye baraka
kwako twaitaradhiya
Tuifunge huno mwaka
na mwakani kwa afiya
Tuufunge mwezi mwema mtukufu
Ramadhani
4
Karibu wetu mgeni
kwa hamu
twakungojeya
Ulotukuka yakini
nuru ulivyo eneya
Mtukufu Ramadhani
karibu twakupokeya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
5
Mtakatifu adhimu
sote twakukongoweya
Mwezi uliye muhimu
Mola met’utunukiya
Twafurahi Isilamu
kila pembe ya duniya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
6
Mtukufu mwezi mwema
wa sisi
kunyenyekeya
Mwenye kuyatenda mema bila
ya kufanya ri’ya
Tamswamehe Karima
madhambi kumfutiya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
7
Mwezi wa nyingi faida
metukuzwa na Jaliya
Mwezi mwema wa Ibada
na imani kutungiya
Huondoka zote shida
nafusi zikatuliya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
8
Mwezi huno wa maana
ameusifu Nabiya
Ni bora wajulikana
kwa kheri
nyingi kungiya
Mwezi wa neema
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
9
Mwezi mwema wa swiyamu
wa mema kujichumiya
Milango ya Jahanamu
Rahimu huifungiya
Na
ya Janatu Naimu
wazi hutufunguliya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
10
Ni
mwezi wa
Quraani
mwanzo kuteremkiya
Alipokuja pangoni
Jibirili kwa
Nabiya
Ilikiuwa Ramadhani
wah’ayi alipokeya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
11
Mashetani makafiri
wawi wa
kuharibiya
Hawawezi kuathiri
wasiwasi kututiya
Huwafungia Qahari
mbali wakatokomeya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
12
Imo
Lelatil Qad’ri
usiku huo kungiya
Bora
Miezi inayo jiri
ya taqwimu Hijiriya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
13
Na
hushuka Malaika
mbinguni wakatokeya
Kwa amri ya Rabuka
duniyani kufikiya
Amani hunawirika
hadi swabahi kungiya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
14
Usiku mwema kipita
wakati huo kungiya
Na
ukija kukukuta
Ibadani umengiya
Hakika utaipata
Rehema yake Jaliya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
15
Haya basi Isilamu
mgeni ashaingiya
Natutimize saumu
tuifungeni kwa
niya
Swala zote tuzikimu
za suna na faridhiya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
16
Mashekhe na masharifu wahimizeni jamiya
Hima tufungeni safu
Tarawehe kuqimiya
Tumlekee Raufu kwa kuomba
na kuliya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
17
Darasani tuhimize
wenzetu kuhudhuriya
Kwa wakati tufulize
misikitini kungiya
Mawaidha tusikize atatujazi Jaliya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu
Ramadhani
18
Haya shime muombeni
Mola kumnyenyekeya
Quraani isomeni
kila siku juz’u moya
Mukiweza ongezeni
muzidi kukaririya
Kongo mwezi wetu mwema mtukufu Ramadhani
19
Na akhiri nimefika
beti nalokusudiya
Chache naloziandika
tosha kumi na tisiya
Namshukuru Rabuka
shairi limetimiya
La
kuswifu mwezi mwema mtukufu
Ramadhani
20
Amina Rabi Dayani Dua yetu kubaliya
Ya Ilahi tuauni
tuepushe na
udhiya
Tuifunge Ramadhani kwa furaha
na afiya
Twaomba yake neema
mtukufu Ramadhani