|
Jamani mbona vishindo? Jamani msiwe kando Muone
ya duniani Zilizali kwa vishindo Vimbunga na matufani Vinagonga kama nyundo Havisiti abadani Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Tsunami ilibashiri Kimbunga
cha baharini Indonesha Kashimiri Bara
Hindi na Japani Ikafika taathiri Hadi
kwetu visiwani Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Katirina kikafwata Kikaja
kikinguruma Mvua bila kusita Na
upepo wa naqama Miti ilikatakata na
majumba yakazama Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Kikaja kimbunga Rita Dharuba
ya ufukweni Kilipiga na kusita Ikawa
ni afueni Kwa haraka kikapita Mitaa
ya pwani pwani Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Kukazuka zilizali Bara hindi Afghani Kilishitadi ukali Nchini
Pakistani Roho pia amuali Hasara
iso kifani Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Sasa bara Afrika Ukame
umeenea Njaa isiyosemeka Miti haitaki mea Mazao yaatilika Na roho zinapotea Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Baharini na barani Ufisadi
wadhihiri Bila hofu ya Manani Maasi
yanakithiri Hatujali hatuoni Tunavamia
kikiri Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Wapi tunaelekea Mbeleni
hatutizami Ina ghururi dunia Tunaona
hatusomi Hatutaki kusikia Tunazidi
hatukomi Ufisadi wadhihiri Baharini
na barani Muhammad Faraj -------------------------------- Huyu anataharuki Huyu anataharuki na
yule anakimbia Wazama hawaibuki kwa
anasa za dunia Ana tabu makhluqi dunia
kun'gan'gania Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Anadhani haondoki milele
atabakia Hajali hashughuliki ya
kesho kufikiria Atapoitwa na Haki hana
pa kukimbilia Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Hapana kitachobaki wala
kitachosalia Ila Wajihi wa Haki uso
wa Mola Jalia Huwezi sema sitaki wala
hata kukimbia Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Kila kitu tahiliki Qurani
yatuambia Sasa kwa nini hutaki mbegu
njema kufukia Upate njema riziki na
rehema za Jalia Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Allahu wetu khaliqi mengi
katutunikia Sisahau yako haki sehemuyo
ya dunia Na hayo uyadiriki Mola
alivyousia Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Kwa wema uwe shabiki watu
kuwatunukia Hata asostahiki wewe
uwe maridhia Ufisadi ni halaki iepuke
yake njia Kila kitu tahiliki ila
uso wa Jalia Mola wetu warehemu walokwisha
tangulia Nanyi mlobaki humu msidhani
tabakia Angebaki muadhamu habibi
wetu Nabia Hapana atayebaki ila
uso wa Jalia Muhammad Faraj |
Msalieni Nabiya (r)
|
Watoto wangu vipenzi Rabi Khaliqul Ibadi Mikono
nainyanyua Mitupu isijerudi Ipokee
yangu dua Nakuomba Ya Wadudi Kwa
moyo uliotuwa Ya Ilahi Ya manani Waepushe
na balia Watoto wangu vipenzi Uwajaze
na imani Waongeze tarkizi Waifuzu
mitihani Uwe kwao ni Mlinzi Ya
Rabi Ya Rahamani Ya Ilahi Ya Manani Waepushe
na balia Waepushe na shetani na
kila unochukia Waongoze kwa amani ya
akhera na dunia Wafwate watamakani Sirati
Ilo sawiya Ya Ilahi Ya Manani Waepushe
na balia Wahifadhi Qur’ani na
masomo Wasali misikitini ni
sunnah yake Nabiya Wasiache abadani Kukutii
ya Jaliya Ya ilahi ya Manani waepushe
na balia Waepushe na haramu wao
na wenzao pia Wana wa kiislamu kila
pembe ya dunia Wafunuwe wafahamu wawe
Kwako maridhia Ya ilahi ya Manani waepushe
na balia Muhammad Faraj -------------------------------- Toba ya Rabb Mikono ninainuwa Ilahi
Rabbinnasi Huku nikiomba duwa Ewe
Maliki Mkwasi Pekeyo Mwenye uluwa Kwa
mwengine haipasi Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Niruzuku ghufurani Niepushe
na maasi Nakuomba ya Manani Dhamiri
inanighasi Naungua kifuani Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Kheri ukinishushia Nasahau
kwa wepesi Mitihani yanijia Mimi
nazidisha kasi Wewe wanichukulia Miye
nazidi kuasi Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Ujalie ucha Mungu Uwe
kwangu ni libasi Adui wako na wangu Wasiwasi
lkhannasi Mfunge mtie pingu Asiipate
nafasi Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Twa'a iwe ni sibugha Nipambe
kwa ikhlasi Nikutii kwa faragha pia
mbele ya unasi Uniepushe na zagha Unitowe
wasiwasi Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Rabbi siku ya Miadi Ninywe
ndani ya gilasi Aninywishe Muhamadi Kiu
kwangu kiwe basi Unirehemu Wadudi Unipe
Firidausi Rabbi tutakabalie Ewe
Samiu Alimu Muhammad
Faraj Tafsiri: ya baadhi ya maneno: 1- Sibugha = 'Pambo' Mwenyezi Mungu anasema:
"Sibughatullah = Pambo la Mwenyezi Mungu." Al Baqarah -138 2- Zagha = 'Kupotoka' Mwenyezi Mungu
anasema: "Falamma zaaghu azaagha Llahu qulubahum = Walipo potoka,
Mwenyezi Mungu aliziachia nyoyo zao zipotoke." Saff -5 |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||