Madhambi yanapozidi moyo hupigwa
mhuri;
MOYO
Impokelewa kuwa siku moja Omar bin Khattab (RA)
alimuuliza Ali bin Abu Talib (RA);
"Ewe Abal Hassan (baba yake Hassan), huenda ikawa
umeona na kusikia yale ambayo mimi sikuona wala kusikia,
Ali (RA) akamwambia;
"Uliza"
Omar (RA) akasema;
"Mtu anampenda mwenzake juu ya kuwa hajaona kheri
yoyote kutoka kwake, na mwengine anamchukia mwenzake (bure bure tu) juu ya kuwa
hajaona ubaya wowote kutoka kwake."
Ali (RA) akasema;
"Ndiyo, nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)
akisema; "Hakika nyoyo ni askari waliotayarishwa. Zinakutana (nyoyo) angani,
kisha zile zinazochunukiana zinapendana, na zile zinazokhitalifiana zinachukiana."
Omar (RA) akasema;
"Moja hiyo. Ama suali la pili; Mtu huwa anahadithia
jambo kisha ghafla anasahau, kisha mara baada ya kusahau anakumbuka tena."
Ali (RA) akasema;
"Ndiyo, nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) akisema;
'Kila moyo hupitiwa na kiwingu
Sahih Al Jamea.
Ndugu yangu Muislamu, usiuendekeze moyo wako ukapenda na
kuchukia kwa matamanio ya nafsi, ukaipenda dunia na kuichukia akhera, au ukaipenda
batil na kuichukia haki bure bure tu, eti kwa sababu moyo wako haujampenda yule
aliyekujulisha haki hiyo. Ukiendelea kuiendekeza nafsi yako basi hutoweza
kuiona haki wala kuifuata. Ukitaka kufanikiwa, nenda kinyume na nafsi yako na
umtii Mola wako, kwani nafsi siku zote inaamrisha maovu, na kumbuka kuwa jihadi
ya nafsi ni kubwa kupita jihadi ya mwili.
Anasema Abdul Qader al Jaylani (Mwenyezi Mungu
amrehemu);
"Ukishindwa kuimiliki nafsi yako usitegemee kupata
mafanikio kutoka kwa Mola wako, kwani Mwenyezi Mungu yuko pamoja na mwenye
kumtii na mwenye kujipendekeza Kwake. Utakuwaje karibu na Mfalme wakati nafsi
yako si
Wewe ndiye mwenye kustahiki zaidi kuionea huruma nafsi
yako. Sasa ikiwa wewe mwenyewe huionei huruma unategemea nani atakuhurumia?
Jitahidi katika kuipunguzia matumaini, na daima ikumbushe juu ya kifo na katika
kumchunga Mwenyezi Mungu. Iambie;
'Faida uliyoichuma ni yako na hasara uliyoichuma ni juu
yako'.
Hapana atakayekupa katika thawabu zake, huna budi
kuzifanyia kazi wewe mwenyewe, (na kumbuka kuwa siku hiyo hatofuzu isipokuwa
atakayekuja kwa Mola wake na Moyo Safi.)"
Janatu naimu fil
Jinani
Jini na Insi wanaitamani
Jumla ya watu Hawaioni
Ila kwa amali Kutaqadama
Thamani ya Pepo Ukiitaka
Thiqi moyo wako kutozunguka
Thubutisha taa Yake
Rabuka
(Shairi nimenukuu kutoka katika tafsiri ya Sheikh
Abdullah Saleh Al Farsy – Mwenyezi Mungu amrehemu)
Kuyadharau madhambi ni moja katika sababu kubwa ya
kudhoofika kwa moyo, nayo hurimbikika juu ya mtu mpaka yakamuangamiza.
Imepokelewa kutoka kwa watu wema kuwa;
"Mcha Mungu anapotenda dhambi ndogo huiona
Katika hadithi iliyosimulia na Al Bayhaqiy anasema Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW);
"Hakika nyoyo zinaingia kutu
Wakamuuliza; "Vipi unasafika ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu?"
Akasema;
"Kusoma
Na katika hadithi nyingine Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)
amesema;
"Hakika Muislamu anapotenda dhambi linaingia ndani
ya moyo wake doa jeusi, na anapotubu na kuomba maghfira doa
"Sivyo hivyo!
Na mwenye kufanya maasi makubwa au mwenye kuyadharau
madogo si
Katika qurani tukufu Mwenyezi Mungu amemlani kila mwenye
kueneza ufisadi juu ya ardhi na mwenye kuwakata ndugu wa nasaba, na kila mwenye
kumuudhi Mwenyezi Mungu na mwenye kumuudhi Mtume wake (SAW), na akamlani kila
mwenye kuuficha ukweli na kuuficha uongofu ulioteremshwa kutoka kwa Mwenyezi
Mungu, na akawalani wanaowasingizia uongo wanawake wema, na akamlani kila
mwenye kuufanya mwenendo wa kikafiri kuwa bora kuliko mwenendo wa Kiislamu nk.
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) pia amewalani wengi
katika wafanyao maasi; Amemlani mchongaji nyusi na mwenye kuchongwa, amemlani
mwenye kuunganisha nywele zake na nywele za bandia, amemlani mwenye kuunguza
ngozi yake kwa kufanya 'tatoo', amemlani anayekula riba na mwenye kulisha riba
pamoja na mashahidi wake, amemlani mwizi, amemlani mwenye kula rushwa na mwenye
kutoa, amemlani mlevi na mtiaji pombe na mkamuaji na mchujaji na muuzaji na
mnunuaji na mwenye kula thamani yake na mbebaji na anayepelekewa.
Amemlani mpigaji ramli na amewalani makhanithi wanaume
na wanawake wanaoingiliana wenyewe kwa wenyewe, na amemlani mwenye kuchinja mnyama
kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na amemlani mwenye kueneza
ufisadi na ujambazi na amemlani mwenye kumficha jambazi, na amemlani kila
mwenye kuchonga masanamu, na amemlani mwenye kutenda kitendo cha qaumu Lut, na
amemlani mwenye kumtukana baba yake na mama yake, na amemlani mwenye
kumuingilia mnyama, na amemlani mwenye kumfisidi mwanamke akamfanya amchukie
mumewe, na amemlani mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma, na akatujulisha kuwa
mwanamke anayekataa kulala na mumewe kuwa analaaniwa na Malaika mpaka asubuhi inapoingia,
na amemlani mwenye kujinasibisha na ubini usiokuwa wa baba yake, na akatujulisha
kuwa atakayemuelekezea ndugu yake Muislamu silaha au upande wa ukali wa kisu au
wa upanga au chuma analaaniwa na Malaika, na amemlani kila mwenye kumtukana
Sahaba wake.
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amemlani pia mwanamume
mwenye kuvaa nguo za kike na mwanamke mwenye kuvaa nguo za kiume, na akawalani
wengi wengine.
Inatosha laana ya Mwenyezi Mungu na ya Mtume wake (SAW)
kumfanya mtu ayakimbie maasi, lakini juu ya laani hiyo mwenye kufanya maasi
hayo anapata pia madhambi pamoja na ghadhabu za Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala na moyo wake unasibiwa na maradhi ambapo hatoweza tena kuiona raha mpaka
atakapotubu na kurudi kwa Mola wake.
Usitizame udogo wa maasi bali mtizame Nani unayemuasi -
Subhanahu wa Taala na umtukuze ili kila anapoangalia ndani ya moyo wako asione
isipokuwa Moyo Safi.
Anasema Abdul Qader al Jaylani (Mwenyezi Mungu
amrehemu);
"Mmoja wenu akiwa mgonjwa akafahamishwa na mganga
dawa ya kumponyesha, hatoona raha mpaka aipate dawa hiyo. Kwa hivyo mchungeni
Mola wenu Azza wa Jallah mnapokuwa peke yenu na mnapokuwa mbele za watu. Uwe
kama Yupo mbele yako unamuona, kwani hata
Mwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu moyoni mwake huyo ndiye
mwenye kumkumbuka kweli, ama asiyemkumbuka moyoni mwake, huyo hamkumbuki kweli.
Ulimi ni mwana wa moyo na unaufuta. Jishughulishe na kusikiliza mawaidha, kwa
sababu moyo ulio mbali na mawaidha unapofoka. Kutubu kweli ni kumtukuza
Mwenyezi Mungu katika amri zote. Na kwa ajili hii wamesema baadhi
Enyi washirikina, enyi mnaoabudu masanamu
yaliyokuzungukeni, na wenye kuabudu vyeo vyenu na mishahara yenu na wakubwa
wenu na wafalme wenu. Hamumuoni Mwenyezi Mungu? Kila mwenye kuona kuwa yupo
asiyekuwa Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wa kumnufaisha au kumdhuru, huyo yupo
mbali na Mwenyezi Mungu na huyo hamuabudu Mwenyezi Mungu. Huyo anamuabudu yule
anayemdhania kuwa anaweza kumnufaisha, leo mtu huyo yumo ndani ya ghadhabu za
Mwenyezi Mungu na kesho atakuwa ndani ya moto wa Jahannam. Hatosalimika na moto
huo isipokuwa mcha Mungu, mwenye kumpwekesha, aliyetubu akaja na Moyo
(Mwisho wa maneno ya Al Jaylani)
Anasema
Muadh Al Razi;
"Nashangazwa
ninapomuon Muislamu anapoomba dua akasema; 'Mola wangu usinijaalie nikawa kichekesho mbele ya adui zako', kisha
wakati huo huo anamuasi na kujifanya
kuwa kichekesho mbele
Amesema Dha
Nnun;
"Mwenye
kufanya khiana kwa siri, Mwenyezi Mungu atamfedhehesha mbele za watu."
Bila shaka athari
ya madhambi ni kubwa
Mwenyezi
Mungu anasema;
"Atawaletea
mpaka siku ya Kiama watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya."
Al Aaraf –
167
Na maasi
nayo yana athari mbaya ndani ya nyoyo na ndani ya mwili, na mojawapo ya athari
zake ni kuikosa elimu. Kwa sababu elimu ni nuru, na maasi yanaizima nuru hiyo
Kutoka kwa
Abu Huraira (RA) amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Kwa
yakini Moyo unachakaa katika kifua cha mmoja wenu
Imam Ahmed
na Attirmidhy
Imepokelewa
kuwa mara ya mwanzo Imam Shafi alipokwenda kutafuta elimu kwa Imam Malik
(Mwenyezi Mungu awarehemu), na wakati huo alikuwa kijana mdogo, na alipomuona
namna alivyoweza kukihifadhi kitabu cha Muwata'a katika siku chache tu, na
alipoiona nuru ya ucha Mungu usoni pake, Imam Malik alimwambia Imam Shafi;
"Mimi
naona kuwa Mwenyezi Mungu ameingiza moyoni mwako nuru, kwa hivyo usiizime kwa
kiza cha maasi."
Imam Shafi
alitunga shairi maarufu

Na maana
yake ni;
'NilimshitakiaWaqii
(mwalimu wake), kupungua uwezo wangu wa kuhifadhi, naye akaninasihi niache
maasi, akanambia kwamba elimu ni nuru, na nuru ya Mwenyezi Mungu hatunukiwi mtu
asi'.
Haya
yanasemekana yalimkuta Imam Shafi alipokuwa sokoni akaona kwa bahati mbaya tu kisigino
cha mwanamke. Vipi basi hali zetu sisi wakati huu kutokana na tunayoyaona kila
siku masokoni na mabarabarani na kwengineko.
Tunamuomba
Mwenyezi Mungu atuepushe na ghadhabu zake na atufanye tuchukizwe kuangalia na
hata kuyasogelea maasi, na atutahirishe nyoyo zetu ziwe mbali na unafiki na
aingize nyoyoni mwetu nuru yake na azijaalie nyoyo zetu ziwe Nyoyo Safi - Amin.
Ukitaka kuujuwa unadhifu wa dhahabu basi ipambanishwe na
moto. Ikibadilika rangi utajuwa kuwa hiyo si
Mwenyezi Mungu anasema;
"Je, Watu wanadhani wataachwa (wasitiwe katika
misukosuko) kwa kuwa wanasema ;"Tumeamini", basi ndio wasijaribiwe?
Hapana; bila shaka tuliwatia katika tabu wale waliokuwa
kabla
Al Ankabuut – 3
Hapa Mwenyezi Mungu anauliza kwa maana ya kukanusha kuwa
walioamini kikweli wasidhani kuwa wataachwa vivi hivi tu, bali atawaingiza
katika mitihani kama alivyowaingiza waliotangulia kabla yao, wakathibiti mbele
ya mitihani hiyo, juu ya kuwa Mwenyezi Mungu anamjuwa nani mwenye kuamini kweli
na nani asiyeamini, kwani Mwenyezi Mungu anajuwa kila kinachotokea na
kitakachotokea na kile kisichotokea, na kile ambacho hakijatokea lau kama
kingetokea vipi kingekuwa.
Mwenyezi Mungu alimuingiza katika mtihani kipenzi chake
(Khalil wake) Ibrahim (AS) akamtaka amchinje mwanawe, na kipenzi chake huyo
akatii pale alipooteshwa kumchinja mwanawe
wa pekee Ismail (AS) na mwanawe akakubali kutii amri alopewa baba yake ndani ya
ndoto yake hiyo (na ndoto za Mitume ni wahyi), na alipomlaza mwanawe kifudifudi
ili asiuone uso wake akamuonea huruma, na baada ya Ismail kutoa shahada na
Ibrahim kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu huku akijitayarisha kumchinja mwanawe,
Mwenyezi Mungu akamfunulia Nabii Ibrahim (AS) kuwa asimchinje mwanawe na badala
yake akamkomboa kwa kondoo.
Kisa
hicho kimeelezwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema;
“Basi
wote wawili walipojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu), na akamlaza kifudifudi
(amchinje).
Pale
pale tulimwita; “Ewe Ibrahim; Umekwishasadikisha ndoto. (Usimchinje mwanao).”
Kwa yakini hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema.
Bila
shaka (jambo) hili ni jaribio lililo dhahiri, (mtihani ulio dhahiri).
Basi
tukamkomboa kwa mnyama wa kuchinjwa mtukufu.”
As
Saaffaat – 103-107
Na imepokelewa katika hadithi kuwa wenye kuingizwa
katika mitihani mikubwa zaidi ni Mitume kisha watu wema, kisha wanaowafuatilia
na wanaowafuatilia, kila mtu kiasi cha imani yake.
Na imepokelewa pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)
alikuwa akipenda kuomba dua ifuatayo;
"Ya muthabbita l qulub thabbit qalbiy alaa
diynika."
(Ewe Mwenye kuzithibitisha nyoyo, uthibitishe moyo wangu
katika dini yako.)
Wakamuuliza;
"Unaogopa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"
Akasema;
"Kipi kitakachonipa dhamana wakati nyoyo zipo baina
ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu anazigeuza apendavyo."
Attirmidhiy na Al Hakim
Na Mwenyezi Mungu anasema;
"Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume
wake anapokuiteni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri (wa duniani na Akhera) Na
jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na jueni ya kuwa
kwake Yeye mtakusanywa."
Al Anfal – 24
Katika kuifasiri aya hii anasema Sayed Qutub katika
tafsiri yake iitwayo 'Fiy Dhilal al Quraan';
"Muitikieni Mola wenu kwa kumtii kwa hiari zenu juu
ya kuwa akitaka anao uwezo wa kukulazimisheni kumtii."
Sayid Qutub akaendelea kusema;
"Mwenyezi Mungu anasema; 'Na jueni ya kuwa Mwenyezi
Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake'. Na hii ni picha tukufu adhimu ya uwezo
wa kuzitiisha nyoyo, kwani Mwenyezi Mungu anaingia kati ya mtu na moyo wake na
kuutenga moyo wake mbali na nafsi yake. Anaweza kuuzuwia na kuufanya atakavyo
na kuugeuza atakavyo wakati mwenye moyo huo hana uwezo wowote, juu ya kuwa moyo
huo ni wake na umo ndani ya kifua chake.
Fundisho hili linamtaka mtu awe macho wakati wote, na
awe na tahadhari wakati wote asije akateleza, na pia awe wakati wote akimchunga
Mola wake usije moyo wake ukageuzwa, ukaghafilika na kupotoka.
Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) mwenyewe alikuwa
mwingi wa kutamka maneno haya; "Allahumma Ya muqallibal qulub thabbit
qalbiy alaa diynika." Na yeye ndiye yeye, kipenzi cha Mola wake (SAW),
itakuwaje basi sisi watu wa kawaida tusiokuwa mitume wala si katika waliokingwa?
Na maneno haya wanaambiwa walioamini. Mwenyezi Mungu
anasema;
"Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume
wake anapokuiteni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri."
Na maana yake ni kuwa; 'Mwenyezi Mungu anao uwezo wa
kukulazimisheni mkamtii – angetaka – lakini anakukirimuni kwa kukuiteni katika
uongofu kwa hiari zenu ili mupate ujira mwema kutoka Kwake.
Kisha akasema; "Na jueni ya kuwa kwake Yeye
mtakusanywa."
(Mwisho wa maneno ya Sayed Qutub)
Kwa hivyo ndugu zangu Waislam; Nyoyo zenu zimo mikononi
Mwake, kisha baada ya hapo mtakusanywa kwake, kwa hivyo hamna pa kukimbilia
isipokuwa kwake, hapa duniani na huko Akhera. Na juu ya uwezo Wake wote huo,
bado anakuiteni kwake kwa hiari zenu na kwa
uhuru wenu bila kukulazimisheni, na hataki chochote kutoka kwenu
isipokuwa kitu kimoja tu. Nacho ni kuja kwake kwa Moyo Safi."
Ucha Mungu wa kweli ni ucha Mungu wa Moyo na si ucha
Mungu wa viungo, kwa sababu Mwenyezi
Mungu haangalii nyuso zenu wala hatizami miili yenu, bali anaangalia ndani ya
nyoyo zenu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Namna hii; anayezihishimu alama za (dini ya)
Mwenyezi Mungu, basi
Al Hajj – 32
Na akasema juu ya wanyama wanaochinjwa katika Hija;
"Nyama zao (wanyama hao wanaochinjwa) hazimfikii
Mwenyezi Mungu wala damu zao. Lakini inamfikia ta-a yenu (ucha Mungu wenu)."
Al Hajj – 37
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Ucha Mungu upo hapa." Akaashiria kifuani
pake.
Muslim
Kwa ajili hii lengo kubwa la Ibilisi ni kuushambulia na kuuharibu
moyo wa Muislamu, na akeshafanikiwa hayo anakuwa keshalifikia lengo lake.
Na katika hadithi Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anasema;
"Katika mwili mna kipande cha nyama, kikitengenea,
mwili wote unatengenea, na kikiharibika, mwili wote unaharibika. Kitu hicho ni
Moyo".
Bukhari na Muslim na wengine
Mwenyezi Mungu ametufundisha namna ya kujikinga Kwake
kutokana na shari ya Ibilisi mwenye kuingiza wasiwasi ndani ya nyoyo, Akasema;
"Sema najikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu.
Mfalme wa watu.
Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma.
Atiaye wasiwasi nyoyoni mwa watu.
(Ambaye ni) Katika majini na watu."
Suratun Naas
Na katika hadithi yenye udhaifu kidogo ndani yake,
imepokelewa kuwa Ibilisi hushika hatamu za moyo wa mwandamu, na (mwanadamu) anapomkumbuka
(akamdhukuru) Mwenyezi Mungu, hapo (ibilisi) hurudi nyuma.
Na hadithi hii inapata nguvu kutokana na kauli ya
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala isemayo;
"Wale wanaomuogopa (Mwenyezi Mungu) zinapowagusa
pepesi za Shetani (wakasahu) mara hukumbuka (wakamdhukuru Mwenyezi Mungu),
tahamaki wamekwishaona njia."
Al Aaraf – 201
Kwa ajili ya yote hayo, watu wema waliotangulia walikuwa
wakijishughulisha
Imepokelewa kuwa mmoja katika wacha Mungu wa wakati
wake, na jina lake ni Maymun bin Maharan aliyekuwa mwandishi na mshauri wa Omar
bin Abdul Aziz (RA) alipohisi kuwa imani yake inaanza kupungua na hapati tena
ule utulivu alokuwa akiupata katika Sala zake wala haioni tena ile raha alokuwa
akiiona anaposoma qurani, akaamua kufuatana na mwanawe kuifunga safari ndefu ya
kwenda kwa Al Hassan al Basry akamshitakie hali yake, na Al Hassan ni katika
maulamaa wakubwa wa At Tabiina (waliokuja baada ya Masahaba wa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW)), na wakati huo Maymun alikuwa na umri mkubwa sana.
Hebu tumsikilize mwanawe Amr akituhadithia juu ya safari
'Safari ilikuwa ndefu
Tuliendelea hivyo mpaka tulipowasili
Baada ya kusalimiana, baba yangu akamwambia;
"Ewe Al Hassan! Hakika moyo wangu umekuwa dhaifu
(imani yangu imepungua), Nifunge au nifanye nini?"
Al Hassan akaisoma kauli ya Mwenyezi Mungu;
![]()
"Unaonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka. Kisha
iwafikie (adhabu) waliyokuwa wakiahidiwa? Yatawafaa nini yale
waliyostareheshwa."
Ash Shuara – 205-207
Baada ya kuisikia aya hiyo baba yangu akaanguka na
kuzimia, na miguu ya Al Hassan ikaanza kutetemeka mfano wa mbuzi anayetaka
kuchinjwa.
Nikamuuliza baba
yangu tulipokuwa tukiondoka;
"Baba! huyu ndiye Al Hassan? Nilidhani atakuwa
kupita hivi"
Akanambia;
"Mwanangu! Amezisoma aya, lau
Maharan akaifunga safari ya kurudi kwao akiwa mwenye
furaha baada ya kusomewa aya zilizoutakasa na kuuzindua moyo wake.
Na hivi ndivyo ilivyo kwa kila mwenye moyo ulio na uhai
wenye kufahamu. Wale ambao nyoyo zao zishachanganyika na qurani, utawaona zikiwaathiri
mara wanaposomewa aya, wanakuwa
"Kwa yakini katika jambo hili mna ukumbusho kwa
mwenye moyo au kwa ategaye siko, naye mwenyewe awe hadhiri."
Qaf
Kumbuka kwamba kwa moyo wako unasafiri kuelekea kwa Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taala, na si kwa viungo vya mwili wako.
Anasema Ibnu l Qayim katika 'Al Fawaid';
"Na kumbuka kwamba mwaka ni mfano wa mti, na miezi
ni matawi na siku ni mfano wa mashada yake, na saa ni mfano wa majani na pumzi
ni mfano wa matunda yake. Basi mwenye kuzivuta pumzi zake katika ta-a ya
Mwenyezi Mungu, huyo matunda ya mti wake yanakuwa mema, ama yule mwenye
kuzivuta katika maasi, matunda yake ni maovu, na kuvuna kwake matunda ya mti
huo ni siku ya Kiama, na siku hiyo itabainika wapi mtu alikuwa akivutia pumzi
zake.
Wakati mwengine Mwenyezi Mungu humtia adabu mtu asi kwa
kumpa
Mwenyezi Mungu anasema;
"Je! Wanafikiri yakuwa yale tunayowapa (nayo ni)
Al Muminun – 55 – 56
Kuwa na umri mrefu huwa kuzuri kwa watu wema kwa sababu
huongezeka wema wao na huongezeka pia thawabu zao, lakini kwa watu waovu hiyo
ni adhabu itokayo kwa Mola wao.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Wala wasidhani wale wanaokufuru kwamba huu muda
tunaowapa (wakaishi kwa satarehe) ni bora kwao. Hakika tunawapa muda na wanazidi
madhambi. Na itakuwa kwao adhabu ya kuwadhalilisha."
Aali Imran - 178
Ajabu ya wanadamu ni kuwa nyoyo zinakufa huku adhabu
zinateremka juu
Anasema Ibni l Qayim katika kitabu chake ' Sayd al
khatir';
"Adhabu kubwa kupita zote ni kule mtu asihisi kuwa
anatiwa adabu, na kubwa zaidi ni kuwa utamuona akifurahi anapokuwa katika adabu
hiyo akidhani kuwa ananeemeshwa, hasa anapotiwa ndani ya mtihani kwa kupewa
(Mwisho wa maneno ya Ibnul Qayim).
Mwanadamu anaponeemeshwa akajaaliwa kuwa na
Kwa nadharia hii anauona mtihani alokuwa ndani yake kuwa
ni neema na anayaona majaribio waliopewa wenzake kuwa ni mtihani utokao kwa
Mwenyezi Mungu.
Fikra zote mbili hizo ni makosa, kwani Mwenyezi Mungu humneemesha
mja wake apate kumshukuru na kuitumia neema hiyo katika mambo ya kheri, na humpunguzia
mwengine katika riziki yake au katika dunia yake ili apate kusubiri na kupata
jaza itokayo kwa Mola wake, na wote hao wamo ndani ya mtihani. Usidhani kuwa
anachotowa Mwenyezi Mungu katika mambo ya kidunia kuwa yana uzito wowote katika
mezani Yake Subhanahau wa Taala, kwani Mwenyezi Mungu humpa mtu mwema na humpa muovu
pia kwa ajili ya kuwapa mitihani, lakini moyo usiokuwa na imani hauwezi
kuidiriki hekima hii.
"Lakini mwanaadamu, Mola wake Anapomfanyia mtihani
Akamtukuza na kumneemesha, basi husema; "Mola wangu amenitukuza. Na
Anapomfanyia mtihani akampunguzia riziki yake, husema; Mola Wangu
Amenidhalilisha . Sivyo hivyo!
Al Fajr – 15 – 20
Kuhusu kauli ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu; '
"Nyumba ya Kiislamu yenye kheri kupita zote ni ile
anayoishi ndani yake yatima mwenye kutizamwa kwa wema. Na nyumba ya Kiislamu
yenye shari kupita zote ni ile anayoishi ndani yake yatima mwenye kudhalilishwa."
Na akasema;
"Mimi na mwenye kumlea yatima tuko
Kheri haipatikani isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi
Mungu. Na mtu mwema haridhiki na jambo lisilo na kheri ndani yake, na shari
haipati isipokuwa mtu mwenye nafsi ovu mwenye kuikimbilia shari hiyo kutokana
na udhaifu wa kuona kwake na udhaifu wa imani, Na mwenye kuikimbilia shari
akaicha kheri ni mtu mwenye kuchaguwa kilichokuwa duni akaacha kilichokuwa
bora, kwani kilicho duni hawezi kuridhika nacho mwenye Moyo Safi.
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anasema;
"Siku ambayo hayatafaa
Ash Shuaraa – 88 – 89
Maulamaa wanasema kuwa 'Moyo Safi' (Qalbin Saliym) ni
Moyo usiokuwa na uchafu wala dhambi. Na baadhi
Maulamaa wanasema;
"Imani huongezeka na kupungua".
Inaongezeka kwa kufanya mema na inapungua kwa kufanya
maasi.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na wanaposomewa Aya zake huwazidishia imani."
Al Anfal – 2
Na akasema;
"Ama wale walioamini inwazidishia imani nao
wanafurahi."
At Tawaba – 124
Muislamu lazima azifahamu sababu zinazopunguza imani na
zinazoizidisha ili aweze kuutakasa moyo wake uweze kukabiliana na mitihani.
Siku moja mfalme wa Luqman mwenye hekima "Luqman al
Hakiym" alichinja mbuzi wawili kisha akamtaka Luqman amtolee kutoka katika
kila mbuzi hao vipande viwili vibaya kupita vyote na viwili vizuri kupita vyote.
Luqman akachagua moyo na ulimi kutoka katika kila mbuzi.
(yaani alikata kutoka katika mbuzi wa kwanza moyo na ulimi, na katika mbuzi wa
pili pia akakata moyo na ulimi).
Mfalme akamuuliza;
"Nilikwambia uchague kutoka KILA mbuzi sehemu
mbili, lakini wewe umechagua kutoka katika mbuzi wote viwili hivi tu (Moyo na
ulimi)?"
Luqman akasema;
"Hakuna vibaya kuliko hivi vinapoharibika, na
hakuna vizuri kuliko hivi vinapotengenea".
Baadhi ya watu hujipangia minasaba maalum kwa ajili ya
kuanzisha upya maisha
'Nitakapotimia umri fulani nitabadilisha mwenendo
wangu."
Na mwengine huchaguwa unapoingia mwaka mpya kwa mfano akasema;
"Kuanzia mwaka huu nitaubadilisha mwenendo
wangu."
Na wengine hujiwekea minasaba mbali mbali kwa ajili hiyo.
Hili ni jambo jema, lakini muhimu zaidi ni kuibadilisha nafsi yako kwanza, kubadilisha
ndani yako, kuubadilisha moyo wako. Maana moyo ukeshakinai unakuwa ushapiga
hatua kubwa mbele katika kujibadilisha kutoka katika hali na kuingia katika
hali nyingine.
Mtu baadhi ya siku hupekuwa pekuwa ndani ya meza yake akatowa
vijikaratasi asivyohitajia na kuvichanachana, akatowa pini pini asizozihitajia
na kuzitupa, akapanga upya kila
kinachohitaji kupangwa. Ikiwa meza ina umuhimu wa kushughulikia na kupangwa
namna hii, basi nafsi ya mtu inastahiki zaidi kupewa umuhimu huo.
Mwenyezi Mungu anatuhimiza kuzisafisha na kuzitakasa
nafsi zetu kila siku.
Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Inapoingia nusu ya mwisho ya usiku au theluthi ya
mwisho, Mwenyezi Mungu hushuka mpaka katika mbingu za dunia akasema; 'Yupo
mwenye kuomba nikampa? Yupo mwenye kuomba dua nikamkubalia? Yupo mwenye kuomba
maghfira nikamghufiria?', mpaka alfajiri inapoingia.
Muslim
Na katika riwaya nyingine;
'Mtu anakuwa karibu zaidi na Mola wake wakati wa usiku
mzito."
Huu ni ule wakati usiku unapoanza kutoweka na alfajiri
inapoanza kujisogeza, ni ule wakati watu wote wamelala wakakoromeana isipokuwa watu
maalum, watu mahsusi tu wanaoziinua mbavu zao kutoka vitandani ili kumuabudu
Mola wao kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo.
Ianze kazi hiyo ndugu yangu Muislamu, kwani imani inapunguwa
na nafsi inadhoofika kwa wingi wa kupambana na matamanio ya dunia pamoja na
mitihani mbali mbali, na utakapoiacha nafsi bila kuiwaidhi na kuipambanisha na
nuru ya Mwenyezi Mungu, basi itaachana na kupotea. Ni wewe peke yako unayeweza
kuiokoa.
Rudi haraka kwa Mola wako usije ukaingia katika wale
Mwenyezi Mungu anaosema juu
"Wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata
matamanio
Al Kahf – 28
Na katika hadithi l Qudusiy, Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala anasema;
"Ewe mwanadamu! Utakaponiomba na kurudi kwangu
nitakusamehe yote uliyonayo wala sijali.
Ewe mwanadamu! Lau kama madhambi yako yatafika mbinguni,
kisha ukaomba kwangu maghfira, nitakusamehe wala sijali.
Ewe mwanadamu! Lau kama utanijia ukiwa na madhambi
yaliyoijaza ardhi, kisha ukakutana nami ukiwa hujanishirikisha na lolote, na Mimi
nitakujia na maghfira yaliyoijaza ardhi."
Attirmidhiy
Na kumbuka siku zote kuwa Mwenyezi Mungu amekuumba kwa
ajili ya kukukirimu na si kwa ajili ya kukudhalilisha, ndiyo maana akawaamrisha
Malaika wakusujudie.
Kuwa mbali na Mwenyezi Mungu hakukuongezei isipokuwa
machungu, upungufu wa raha ndani ya moyo, hata uhodari wa mtu na uerevu wake
unageuka kuwa masaibu pale unapokosa baraka za Mwenyezi Mungu.
'Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola wangu. Umeniumba na mimi
ni mja wako, na mimi nitatimiza ahadi yako na waadi wako kiasi niwezavyo.
Najikinga kwako kutokana na kila shari uloumba. Nakiri juu ya neema zote
ulizonineemesha nazo. Na ninakiri juu ya dhambi zangu. Kwa hivyo nisamehe,
kwani hapana mwenye kusamehe madhambi isipokuwa wewe'.
Katika makosa makubwa wanayofanya wanadamu ni kuishi
ndani ya ndoto wanazojipangia za kesho
Na mtu anapojipangia kesho yake, akaanza kuingia katika
bahari ya ndoto isiyo na mwisho na kujiingiza katika wahka na wasi wasi na
mawazo yasiyo na upeo, huku akiendelea kujitia dhiki na mashaka nafsini mwake,
huyo anaingia katika makosa makubwa
Kwa nini basi mtu haishi ndani ya siku yake hii akamuachia
Mwenyezi Mungu kesho yake?
Si vibaya mtu kujipangia kesho yake, lakini vibaya ni
kule kuzama ndani ya fikra na mawazo yasiyokuwa na mwisho; 'Itakuwaje kama
nikiachishwa kazi? Nitafanya nini meli ikizama na
Hizi ni fikra ambazo haijuzu mtu kujishughulisha nazo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Atakayeamka akiwa yupo katika amani, mwenye afya
njema, anacho chakula cha kumtosha kwa siku moja, huyo ni sawa na aliyemiliki
dunia na kila kilichokuwemo ndani yake."
Attirmidhiy
Mtu kama huyu anatakia nini tena kujitia dhiki
akafikiria kuachishwa kazi au kupoteza
Imepokelewa kuwa Nabi Ibrahim (AS) anapoamka asubuhi alikuwa
akisema;
"Mola wangu hiki ni kiumbe kipya (hii ni siku
mpya), kwa hivyo nifungulie siku hii kwa ta-a yako na unikhitimishie kwa
maghfira yako na radhi zako, na uniruzuku mema utakayonikubalia na unitakasie
wema huo na unizidishie, na nitakapofanya ovu unisamehe, kwani Wewe ni mwingi
wa kusamehe, Mpole, Mwenye kurehemu, Mkarimu."
Imepokelewa kuwa Abi Hazim alikuwa akisema;
Tofauti baina yangu na wafalme ni siku moja tu.
Jana yetu, ishapita, hawaionei raha tena wao wala mimi.
Kesho yetu, haijafika, kwa hivyo mimi na wao ni sawa
katika kuisubiri.
Tofauti yetu ni siku ya leo. Itakuwaje leo?
Unapoambiwa uishi ndani ya siku yako, haina maana kuwa
uipuuze kesho yako, au uache kuifanyia hesabu, kwani mtu kujipangia kesho yake ni
dalili ya ukamilifu wa akili. Lakini ipo tofauti baina ya kujipangia na kuifikiria,
na baina ya kuwaza na kuingiza wahka moyoni kwa ajili ya kesho isiyo na uhakika,
na ipo tofauti baina ya kuitayarisha na kuzama ndani yake, baina ya kuamka na
kuitumia leo yako, na baina ya kulala na kuiota kesho hiyo.
Sufyan Al Thauri ambaye ni katika maulamaa wakubwa wa
Attabiina, alikuwa mtu mwenye
"Tumeamka na ufalme upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu
asiye na mshirika, na Kwake tutafufuliwa."
Attirmidhiy
Na alikuwa unapoingia usiku akirudia kusema maneno hayo
hayo kisha akiomba kwa kusema;
"Allahumma inniy asbahatu minka fiy niamatin wa
afiyatin wa sitrin. Faatmim niamatika alayya wa aafiyatuka wasitruka fi ddunya
wal akhirah."
Abu Daud
Na maana yake;
"Mola wangu kwa
uwezo wako niko katika neema na afya na sitara. Kwa hivyo nikamilishie
neema Yako juu yangu na afya Yako na sitara Yako duniani na akhera."
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Juwa halipandi isipokuwa Mwenyezi Mungu huwatuma
Malaika wake wakasema; "Enyi watu! Rudini kwa Mola wenu. Hakika kidogo
chenye kutosheleza ni bora kuliko kingi chenye kubabaisha."
Na halichi juwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atawatuma
Malaika waseme;
"Mola wetu mlipe mema kila mwenye kutoa (katika
Attarghiyb wal Tarhiyb
Anasema Sheikh Al Ghazali katika 'Jaddid Hayatak';
"Hapana baya kuliko mtu kuiba katika maisha yake.
Unajuwa vipi mtu anaiba katika maisha yake?
"Anapokuwa mtoto mdogo husema; Nitakapokuwa kijana
nitafanya hivi na vile.
Na anapokuwa kijana husema; Nitakapokuwa mtu mzima
nitafanya hivi na vile.
Na anapokuwa mtu mzima husema; Nikeshaowa nitafanya hivi
na vile.
Akishaowa atasema; Nitafanya nitakapokuwa na nafasi
nzuri.
Akeshazeeka akayatizama maisha yake tokea hukoo
alikotoka anaona kuwa ameyapoteza buree. Tatizo letu ni kuwa hatusomi kuwa
thamani ya maisha ni ile siku yako. Hatuyajuwi hayo mpaka wakati unapopita na
kumalizika".
Huenda mtu akawa anaishi katika amani na afya njema bila
kuhisi wala kuithamini neema hiyo tukufu aliyotunukiwa na Mola wake Subhanahu
wa Taala, na wakati huo huo fikra na mawazo yake yote yapo katika mali na
utajiri bila kuelewa kuwa kuidharau neema hii ya afya ni dhambi na ni kwenda
kinyume na ukweli.
Waarabu wanasema;
"Afya njema ni taji ipo juu ya vichwa vya wenye
siha, hawaioni taji hiyo isipokuwa wagonjwa."
Yaani mgonjwa anamuona mwenye afya yake
Imepokelewa kuwa mtu mmoja alimuuliza Abdullah bin Amru
bin Aas (RA);
"Mimi si mmoja katika masikini wa watu wa
Makka?"
Abdullah (RA) akamuuliza;
"Unaye mke?"
Akajibu;
"Ninaye."
Akamuuliza tena;
"Unayo nyumba ya kulala?"
Akasema;
"Ninayo."
Akamwambia;
"Basi wewe ni miongoni mwa matajiri."
Akasema;
"Ninaye na mtumishi pia."
Abdullah (RA) akamwambia;
"Babi wewe ni katika wafalme."
Sisi ni matajiri, Alhamdulillah! lakini hatuijuwi
thamani ya neema tuliyo ndani yake. Mmoja wetu anapoumwa na jino tu au kichwa
au homa, dunia yote anaiona chungu.
Imesimuliwa kuwa mfalme mmoja aliyekuwa tajiri
Imesimuliwa pia kuwa mtu mmoja alipotea jangwani
akashikwa na kiu na baada ya kutembea siku nyingi akaona kwa mbali guduria, akafurahi
akidhani kuwa ndani yake mna maji, lakini mara baada ya kulifikia guduria
Impokelewa kuwa siku moja mfalme aliyekuwa katika safari
zake za kuwinda alipotea njia akaishiwa na maji. Akamtuma mtumishi wake amtafutie
maji, na baada ya kuhangaika
"Uliza lakini fanya haraka maana nina kiu
Mtumishi akasema; "Iwapo duniani hapana maji
mengine isipokuwa haya tu, utakuwa tayari kuyanunua kwa thamani gani?"
Mfalme akasema; "Nusu ya ufamle wangu."
Mtumishi akampa mfalme maji, na baada ya kunywa
akamuuliza tena;
"
Mfalme akasema; "Nusu ya pili ya ufalme
wangu."
Mtumishi akasema; "Ufalme thamani yake sawa na
kikombe cha maji."
Hiyal qanaatu tahfadhuha takun malikan - Walaw la alaa
raahatul badani
Undhur liman malaka dduniya biakmaliha – Hal raaha minha
bighayri l qutni wal kafani?
Tafsiri; Ni kukinai tu, ukiweza ushakuwa mfalme - hata
Mtizame aliyemiliki dunia na kila kizuri ndani yake
- Aliondoka na nini hapa duniani
isipokuwa pamba na sanda?
Siku zote usiitizame nafsi yako, wala usiwatizame walio
juu yako, bali watizame walio chini yako.
Ikiwa unayo kazi, wapo wasio na kazi. Ikiwa afya yako ni
njema, wapo wagonjwa kwa mamilioni. Ikiwa unaumwa wapo wasioweza kutembea.
Ikiwa upo kitandani wapo wasioweza kuvuta pumzi mpaka wasaidiwe kwa vifaa vya
hospitali, nk.
Anasema Sh. Muhammad Al Ghazali katika 'Jaddid Hayatak';
Madaktari wanasema kuwa mmoja katika kila watu ishirini
wanaoishi Marekani watakuwa wagonjwa katika hospitali za maradhi ya akili, na
katika ukweli unaotia uchungu ni kuwa kati ya kila vijana sita waliokwenda
kujiandikisha jeshi wakati wa vita vya ulimwengu vya mwisho walikataliwa kwa
ajili ya kuwa na maradhi ya mwili au upungufu wa akili.
Alipokuwa akiwahutubia madaktari katika hospitali ya
Mayo huko Marekani, Dr. Haroldsin alisema;
"Tumedurusu hali za wafanya biashara vijana mpaka
wenye kufikia umri wa miaka arubaini, ikatubainikia kuwa si chini ya watu
wawili katika kila watatu wanapata mojawapo ya maradhi aina tatu yenye asili ya
dhiki ya nafsi. Na maradhi hayo ni; kukumtika kwa moyo 'palpitation', donda la
tumbo 'gastric ulcer' au hypertension, na haya ni baada ya kufikia umri wa
miaka arubaini na mitano."
Je, hii ndiyo thamani ya mafanikio? Ivo anahesabiwa kuwa
amefanikiwa yule aliyenunua mafaniko kwa maradhi ya donda la tumbo na mapigo ya
haraka ya moyo wake? Na maradhi yatamfaidia nini hata
Anasema Dr. W. S. Alvares;
"Imebainika kuwa maradhi manne katika kila maradhi
matano hayatokani na mwili, bali yanatokana na hofu na dhiki ya nafsi, chuki au
wasi wasi usiokuwa na msingi."
(Mwisho wa maneno ya Sh. Al Ghazali)
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anasema;
"Atakayezielekeza juhudi zake zote katika jambo
moja tu, basi Mwenyezi Mungu atamuondolea dhiki za dunia. Na atakayezielekeza
juhudi zake katika mambo mengi tofauti na wala asimjali Mwenyezi Mungu popote
alipo, basi ataangamia."
Al Hakim.
Anasema Sheikh Al Ghazali katika 'Jadid Hayatak'
akimnukuu Dil Carington kuwa anasema;
"Nimeishi
Naam! Hapana aliyenigongea mlango kunitahadharisha kuwa
mtu mmoja katika kila watu elfu kumi wanaoishi Marekani wana hatari ya kupata
maradhi ya ugonjwa wa akili wa 'nervous breakdown' unaoletwa na mashaka au kazi
nyingi au dhiki ya nafsi, kwani inajulikana kuwa kila dollar inapoteremka thamani
yake katika masoko ya pesa 'stock market' basi sukari inapanda na kuongezeka
katika mikojo na katika damu ndani ya miili ya wanaokula hasara katika masoko
hayo."
Dawa gani iliyo bora ya kutibia maradhi haya kuliko
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) aliposema;
"Mwenye kujishughulisha na akhera, Mwenyezi Mungu
humuingizia kukinai moyoni mwake, na dunia itamjia mbio. Na mwenye kujishughulisha
na dunia, Mwenyezi Mungu humuingizia ufakiri, na hatopata katika dunia
isipokuwa kile kile kichache alichokwisha andikiwa?"
Attirmidhiy
Na katika riwaya nyingine;
"Mwenye kuipa umuhimu akhera yake, Mwenyezi Mungu
atampa yote mawili (akhera na dunia) na atampa kinaa ndani ya moyo wake. Na mja
anapojisogeza kwa moyo wake mbele ya Mola wake, basi Mwenyezi Mungu atazijaalia
nyoyo za Waislamu zimpende na kumuombea rehma, na Mwenyezi Mungu atamharakishia
kila la kheri."
Al Baihaqy
Mafundisho haya yanatujulisha juu ya uhaba wa thamani ya
dunia hii ambayo ingelikuwa mbele ya Mwenyezi Mungu ina uzito hata wa kisasi
cha ubawa wa mbu, basi Mwenyezi Mungu asingemnywisha kafiri hata fundo la maji.
Hata hivyo hii isichukuliwe kuwa tunatakiwa tuiache
dunia moja kwa moja na kujishughulisha na akhera peke yake
Lakini juhudi hii isitufanye tukazisahau nyoyo zetu
tukajishughulisha na mali, kwani mali tutakayoichuma ni kwa ajili ya matumizi
na si kwa ajili ya kurimbika, ni kwa ajili ya kunyanyua hali zetu na kujikinga
na balaa, na si kwa ajili ya kuwa nayo tu, kisha tukaacha muongozo mwema
tulowekewa na Mtume wetu Muhammad (SAW) aliposema;
"Amestarehe aliyechuma
Attarghiyb wal Tarhiyb
Anasema Dil Carington;
"Utafiti umethibitisha kuwa dhiki ya nafsi ni
muuwaji nambari moja katika nchi ya Marekani. Katika vita vya mwisho vya
ulimwengu wameuliwa katika vijana wetu waliokwenda vitani kiasi cha laki tatu
unusu, wakati watu wapatao milioni mbili walikufa kwa maradhi ya dhiki ya nafsi
katika wakati huo huo. Na hii ndiyo sababu iliyomfanya Dr. Alex Karel aseme
kuwa; 'Matajiri na wafanya biashara wasiojuwa namna ya kujiepusha na dhiki ya
nafsi wanakufa wakiwa na umri mdogo..'
Wanaokufa kwa maradhi haya miongoni mwa Wamarekani wenye
asili za Kiafrika na wenye asili za Kichina ni wachache
Jadid Hayatak
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
"Enyi watu! Hakika ya utajiri si utajiri wa
Abu Yaala
Imepokelewa kutoka kwa Ibni Omar (RA) kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW) alikuwa mara nyingi anapoondoka katika kikao akiomba dua ifuatayo;

Na maana yake ni;
"Mola wetu! Tujaalie tuwe na uoga utakaotuwezesha kujikinga
na kukuasi, na tuwe watiifu ili tuweze kuingia katika Pepo yako, na (utugawie)
katika yakini itakayotusahilishia katika kupambana na masaibu ya dunia.
Mola wetu tudumishie kusikia kwetu na kuona kwetu na
nguvu zetu tunapokuwa hai, na utubakishie mpaka kufa kwetu, na ujaalie visasi
vyetu viwe kwa wenye kutudhulumu, na utunusuru juu ya adui zetu, na usijaalie
masaibu yetu yakawa katika dini yetu, na usiijalie dunia ikawa ni kubwa lenye
kutushughulisha, wala (dunia) isiwe lengo la elimu yetu, na wala
usitusalitishie asiyeturehemu."
Attirmidhiy
Dua za namna hii na zipo nyingi