MJUWE SAHABA THUMAMA BIN UTHAAL
AL-HANAFIY.
na Suleyman Mohd Said.
Katika mwaka wa sita tokea kuhamia Madina, Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)
aliamua kueneza
ulinganio wa kiislam kwa watu wasiokuwa waarabu wa Makka na akandika barua nane kwenda kwa wafalme wa
kiarabu na wafalme wasio waarabu na
alikuwa miongoni mwa aliowaandikia barua ni Thumaamah bin Uthaal Al-Hanafiy
huyo alikuwa kiongozi wa kiarabu na bwana miongoni mwa mabwana wa kabila la
Hanafiy na mfalme Al- Yamaamah ambaye amri yake haipingwi. Na alipata barua ya Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW) hali ya kuwa mwenye kudharau, kisha akajitakasa yeye na
makosa yake na akaziba masikio yake kusikiliza ulinganio wa haki na wa kheri akapandwa na
shetani na shetani akampoteza kutaka kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) na
akapata fursa ya kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) lakini akashindwa na
Mwenyezi Mung u akamuokoa Mtume wake kutokana na shari hiyo.
Lakini Thumaamah alishindwa kumuuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) na
badala yake kuwaua masahaba wengi katika uuwaji mbaya na wenye kutisha na haikupita muda mkubwa akaamua kwenda
kufanya ibada ya umra na alipofika njiani karibu na Madina akatekwa na waislam
na wakamchukua Madina pamoja na watu wake na wakafungwa katika nguzo za msikiti
wa Madina ili kumsuburi Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) atoe hukmu juu ya mateka
hao, na pale alipoingia Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)msikitini akamuona
Thumaamah amefungwa katika nguzo na akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) kuwaambia
masahaba zake “jee munamjua nani muliyemteka?” Wakajibu “hatujui ewe mjumbe wa Allah” na akasema Mtume huyo ni Thumaamah bin Uthaal
Al-Hanafiy mfanyieni wema wala musimtese
kisha akarejea Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) kwa watu wake akawaambia
kusanyeni mlicho nacho miongoni mwa vyakula na mpelekeeni Thumaamah, kisha
akaamrisha ngamia wake akamwe maziwa asubuhi na jioni ili apelekewe na
yakatekelezwa yote hayo kabla Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) hajaonana naye na
akazungumza naye, baada ya hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) akonana naye kwa
ajili ya kumlingania katika uislam na akamuuliza “una nini ewe Thumaamah?”
Akasema “mimi ni mzima kabisa ewe Muhammad……pindi
ukiniuwa basi unauwa binaadamu …….. na pindi
utanineemesha basi unamneemesha mwenye kushukuru…….. na
ukiwa unataka
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) akaondoka akamuacha siku mbili, kisha
akaonana naye tena mara ya pili akamwambia “una nini ewe Thumaamah?”, Akajibu “sina
chochote isipikuwa
Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW) akamuacha na akamjia siku nyengine na
akamuuliza suala lile lile la mwanzo nae akajibu jibu
Bwana Thumama baada ya
kufunguliwa akaondoka hadi akafikia karibu na mwisho wakutoka katika mji wa
Madina karibu na sehemu inayoitwa Bakii, akakuta maji akakoga kisha akarudi
Madina mpaka akafika katika msikiti wa Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW) na akasilimu mbele ya masahaba kisha akaelekea kwa
Mtume na akamuambia “Ewe mjumbe wa Allah hakika nilikuwa nikikuchukia kabla ya
kusilimu kwangu kuliko watu wote duniani, lakini baada ya kusilimu hakuna mtu
ninayempenda katika ulimwengu huu zaidi yako
ewe! Mtume nimewauwa waisilamu wengi kabla kusilimu kwangu kwa hivyo
nini nifanye ili niweze kusamehewa madhambi yangu?”. Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)akamjibu “ hakika Uislam unafuta yale madhambi yote
yaliyotangulia.” Kisha akasema sahaba huyu kumuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)kuwa
“h akika nitawauwa makafiri kuliko nilivyowauwa waislam na nitajifungamanisha
na upanga wangu huu pamoja na watu wangu katika kukuokoa wewe pamoja na dini ya
kiislam”, kisha akamuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)amruhusu aende Makka
akatimize ibada ya Umrah ambayo aliikusudia kuifanya lakini kwa namna
walivyoizowea Makafiri na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)akamruhusu na akamwambia
nenda lakini iwe kwa namna alivyoataka Allah na Mtume wake na hapo ikabidi
afundishwe namna ya kufanya Umra ndipo akaelekea Makka.
Thumama alipofika Makka akazisoma Talbiya (ni takbira zinazosomwa kwa
mwenye kufanya ibada hii na Hijja baada ya kuhirimia na inasuniwa kuzileta kwa
sauti ) huku anaingia katika mji wa Makka nae ni muislam wa kwanza kudhihirisha
talbiya katika mji wa Makka. Makafiri waliposikia talbiya zile wakataharuki na
kuchanganyikiwa na huku wakijiandaa kwa mapambano kwa kuchukuwa panga zao
wakidhani kuwa washaingiliwa na waislam huku wakiifuata sehemu itokapo sauti na
walipomjuwa kuwa ni bwana Thumama ndie anaeleta talbiya zile wakanywea kwa
kumuona mtu mkubwa kama huyu kuweza kusilimu.
Mmoja kati ya vijana wa Kikureshi alitaka
kumrushia mshale ili amuuwe lakini vigogo wa Kikureshi wakamkanya na
kumtahadharisha kuwa si mtu wa kufanyiwa uadui, bwana Thumama aliendelea kuleta
talbiya zake huku anawapitia Makafiri kwa ufakhari na akawaambia, “Enyi
makafiri ikiwa mtanidhuru basi nitakukatieni kukuleteeni chakula na mtakufa kwa
njaa”. Hapo tena Makureshi wakamuuliza “una nini ewe Thumama?
Umeiwacha dini yako na kuwatukana mababu zako?”
Akawajibu “hakika mimi sijawatukana mababu zangu bali nimeifuata dini iliyo
bora kuliko dini zote” kisha akawaambia
“ Naapa kwa jina la Mola Mtukufu hakika nitakaporudi Yamama haitokufikieni hata
chembe moja ya chakula mpaka muifuate dini ya Muhammad”.
Baada ya hapo akafanya Umra yake kisha akaondoka kurudi kwao na
alipofika tu kwa watu wake akawazuia kutuma chakula kwa watu wa Makka na
kutokana na hali hiyo watu wa Makka wakafikwa na hali mbaya ya uhaba wachakula
hadi kuhatarisha maisha yao na vitu vikapanda bei jambo ambalo likawapelekea
wamuandikie Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)na kumuomba awaombee kwa bwana Thumama
alete chakula Makka wakaandika barua kuelekea Madina yakiwemo maneno haya: “
Ewe Muhammad hakika ahadi yetu kwako kuwatembelea jamaa na hakika umekata
mawasiliano kwetu na kuwaua watoto wetu na baba zetu kwa upanga na sasa
unawauwa watoto wetu kwa njaa na hakika Thumama bin Uthaal ametukatia sisi
chakula na ametudhuru, hivyo ukiona barua hii muandikie au muambie atuletee yale aliyoyazuia ambayo tunatahitaji
basi fanya hivyo”.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)alipoipata barua hii hapo hapo akamuandikia
barua bwana Thumama ili awapelekee chakula ndipo bwana Thumama akawaruhusu watu
wake kupeleka chakula na shida
ikaondoka haya yote yalikuwa ni kutokana
na imani yake juu ya dini hii na matendo yake ameyafungamanisha na matakwa ya
Bwana Mtume SAW.
Kutokana na haya yaliyotokezea nayo ya kusilimu Bwana huyu kwa khiyari
yake baada ya kuachwa huru na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) pamoja na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW) kuwafungulia mlango wa kupelekewa chakula Makafiri wa
Makka tunafahamu namna ya uislam ulivyokuwa
ukilinganiwa wala haikuwa upanga ndio
sababu ya kusilimu watu kama inavyodaiwa na maadui wa dini hii, bali
ilikuwa ni tabia njema za Mtume wetu Muhammad SAW na ulinganiaji wa khiyari
ndio uliosababisha watu wengi kuukubali Uislam kwa imani thabiti na hata sahaba
huyu alipoulizwa kwa nini ukasilimu baada ya kuachiwa huru tu? “Akasema kuwa
hakika mani iliniingia tokea nilipofungwa lakini lau
ningesilimu ingesemwa kuwa nimesilimu ili niwachwe huru ndipo nilipokuwa huru
nikasilimu kwa khiyari yangu”. Kwa kweli aliyoyaona bwana huyu wakati
alipofungwa kiasi asilimu kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW)kama
tulivyoona aliamrisha afanyiwe wema na kupelekewa chakula kila wakati wa kula
hakikuwa chakula cha kutupwa kama wanavyofanyiwa wafungwa wengi duniani , bali kilikuwa ni chakula cha minal ali haya
ni kufahamisha kuwa uislam si dini ya uadui na mateso bali ni dini ya upendo na
rehema.
Thumama alikuwa ni miongoni kwa waliosimama kidete kuinusuru dini hii ya
kiislam baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) kuondoka ulimwenguni, kwani walijitokeza
baadhi ya waislam kurudi katika dini zao za zamani kwa kudhani kuwa dini hii ni
dini ya Muhammad akifa na dini imekufa na wamesahau kuwa dini hii ni ya
mwenyewe Allah aliyetuumba na hakuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) isipokuwa ni
mjumbe tu kwa watu wote .
Tena alipotaka Musaylamatil Kadhab kuwatowa watu wa kabila la Hanafi
katika Uislam kwa kuwshawishi na kudai kuwa Utume umebaki kwake akasimama
sahaba huyu bwana Thumama na kuwalingania watu wake wa kabila la Hanafi na
kuwatahadharisha kuiwacha dini yao ya kiislam na akawaambia “hakika Muhammad ni
Mtume wa mwisho hakuna Mtume baada yake kisha akawasomea aya hizi za suratul
Ghafir zenye maana yafuatayo:
“Ha mim, Uteremsho wa kitabu umetoka kwa Allah
mwenye nguvu mwenye kujuwa, Anaesamehe dhambi na kupokea toba mkali wa kuadhibu
mwenye ukarimu hakuna Mungu illa yeye na marejeo ni kwake.”
Baada ya hapo watu hao wakamuunga mkono na wakawa ni miongoni mwa
waislam wanaolingania watu wasije wakatoka katika dini hii na wakaungana na
Khalifa Abubakar bin Siddiq katika kuwapiga vita wale waliyortadi
.
Mola ampe bwana Thumama bin Uthaal kheri na amkirimu
pepo yake ambayo ameahidi kwa wenye kumtii. “AMIN”.