kutoka

Al Hidaaya

Yaliyomo

VILOSA. 1

Kunafa  (Vitamu vya nchi za Sham) 2

PUDINI YA NAZI 4

KEKI YA JIBINI (Cheese Cake)

KEKI YA KAROTI

KEKI YA  SEMOLINA NA JOZI  (WALNUT) 7

BASBUSA - (Shaam) 8

PURI 9

VIBIBI 10

MKATE WA KIFARANSA (french toast) 11

VIKEKI VIDOGO  VYA CHENGA ZA SHAYIRI  - (OATMEAL MUFFINS) 12

PAI YA KUKU (CHICKEN PIE) 13

KEKI YA NANASI 15

KEKI ZA VIKOMBE ZA NAZI - (COCONUT MUFFINS) 16

MKATE WA NYAMA. 17

MAANDAZI YA KUPAMBIA. 18

KEKI ZA VIKOMBE. 19

MKATE WA MAYAI 20

KEKI YA TENDE. 21

MKATE WA UFUTA. 22

KHALYAT AN-NAHL   (MZINGA WA NYUKI) 23

KEKI YA MAZIWA. 24

Maandazi 25

KEKI YA MARMAR (MARBLE CAKE) 27

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 27

KEKI YA NDIZI NA NAZI 28

BISKUTI ZA UFUTA NA JAM

BISKUTI ZA MAYAI

BISKUTI ZA KASTADI

BISKUTI ZA TENDE

BISKUTI ZA CORNFLAKES. 34

MITAI 35

VIBISKUTI VYA KUYAYUKA MDOMONI 36

DONATI 37

BISKUTI ZA JAM... 38

VISHETI: 39

VILEJA VYA KARANGA. 40

BISKUTI ZA NJUGU/MATUNDA MAKAVU - (ROCK CAKES) 41

VIBISKUTI VYA MATUNDA MAKAVU NA CORNFLAKES.. 42

VIBISKUTI VYA SIAGI 43

BISKUTI ZA TANGAWIZI 44

WALI WA KICHINA WA KAMBA NA KUKU.. 45

BIRIANI YA TUNA. 46

KABABU  ZA ROJO.. 47

Mkate wa sinia. 47

SUPU YA MAHINDI, KAROTI NA VIAZI 49

Zanzibar Grilled Fish (Samaki wa Kupaka) 50

Bar Shish Kebabs (Mishkaki) 51

Grilled Zanzibar Queen Prawns. 52

Garlic Prawns (Kamba wa Vitunguu Thomu) 53

Mango Chutney (Kachumbari ya Embe. 54

KISAMVU.. 55

MKATE WA UFUTA (SESAME BREAD) 56

VILOSA.. 57

KEKI YA NDIZI 58

VITUMBUA.. 59

KEKI YA ZABIBU.. 60

Makange ya kuku.. 61

Mishkaki kwa ndizi mzuzu.. 62

NDIZI ZA MKONO WA TEMBO.. 63

NYAMA YA KABICHI NA NJEGERE.. 64

WALI KWA NYAMA YA MAHARAGE YA MAGANDA.. 65

DESSETI YA NDIZI 66

Doughnuts. 67

CHAPATI ZA MAJI 68

FUTARI YA MAHARAGE NA VIAZI VITAMU.. 69

BIRIYANI YA NYAMA YA MBUZI 70

BIRIYANI 72

KASHATA ZA KARANGA. 74

WALI ULIOFUNGWA KWA KABEJI 75

MATOKE.. 76

KIBURU.. 77

BEANS CAKE.. 78

SAMAKI WA KUPAKA.. 79

MLENDA WA BAMIA NA KARANGA.. 80

MAJANI YA MABOGA. 81

KATLESI ZA SAMAKI 82

WALI NA NJEGERE.. 83

VIAZI VYA GARAI 85

KABABU ZA KUKU.. 86

MBATATA ZA UROJO/ZANZIBAR MIX.. 87

MAKBUS (WALI WA KIARABU) 88

FISH FINGER.. 89

GITHERI NA VITUNGUU VYA KUKAANGA.. 90

KACHORI 91

 

 Rudi juu

VILOSA

 

VIPIMO

 

Mchele                                             1/2 Kikombe

Semolin                                            1 Vikombe

Tui  la nazi                                        3/4  Kikombe

Maziwa                                             1/2 Kikombe

Mayai                                                3

Hamira                                             1 kijiko cha chai kijae

Rose essence                                  kidogo

Zaafarani                                          kidogo

Sukari                                               1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUTENGENEZA

  1. Roweka mchele tokea usiku
  2. Uchuje mchele maji yote
  3. Weka kwenye mashine ya kusagia (Blender)
  4. Tia mayai, maziwa, sukari, hamira, rose essence, zaafarani. Kisha usagesana mpaka chenga za mchele zote zisagike.
  5. Tia semolina na tui la nazi, kasha endelea kusaga katika blender, kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
  6. Mimina katika bakuli kubwa, funika iwache iuumuke.
  7. Ikishaumuka choma kama unavyochoma vitumbua.
  8. Shira ikipowa, tumbukiza Vilosa kwa kiasi kiasi, changanya na uvitoe uviweke upande katika sahani ya kupakulia.
  9. Endelea kufanya mpaka vyote vimalizike.

 

SHIRA  

**Tengeneza mapema ipowe. Na isiwe nzito

Sukari                        2 Vikombe

Maji                            1 kikombe

Zaafarani                    kidogo

Rose                           essence


 Rudi juu

 

Kunafa  (Vitamu vya nchi za Sham)

 

 

Muda wa kutengeneza                                                     dakika 20

Muda wa kupika                                                               dakika 25

 

VIPIMO

Kataif Pastry  (Tambi za Kataif)                           ½ Kg   =  Pakti moja 

Cheese ya Mazorella                                           ¼ Kg 

Cheese ya Ricotta                                               ¼ Kg

(Ukipenda tumia Cheese ya Ricota pekee hivyo itakuwa ½ Kg )

Maziwa                                                                ½  glass

Siagi au samli  (iliyoyayushwa)                           ½ kikombe

 

SHIRA

Maji                                                                     1 ½  Kikombe

Sukari                                                                 2  Vikombe

Zaafarani  (iroweke na maji kidogo)                                                          

 

NAMNA YA KUTENGENEZA

  1. Kata karatasi ya Wax paper size ya bakuli uweke katika bakuli la Pyrex (la kupikia ndani ya oven) Bakuli lisiwe lenye shimo sana (sio deep) {sio lazima kuweka karatasi ya Wax ukipenda tu}
  2. Kwaruza (Grate) cheese ya Mazorella na ya Ricotta ichanganye pamoja kisha weka katika bakuli.     
  3. Tia maziwa yamoto kidogo katika cheese na changanya vizuri.  Kisha ingandamize vizuri ikae sawa katika bakuli.
  4. Katakata Tambi za Kataif ndogo ndogo kwa mkono na kuzichambua kama urefu wa 3 cm na kuziweka zote katika bakuli.

 

  1. Pasha moto siagi au samli katika Microwave. Nyunyiza katika Kataif uliyoichambua katika bakuli itaipa rangi ya dhahabu.

 

  1. Sasa weka Tambi za Kataif juu ya cheese uliyokwishaweka katika bakuli ya Pyrex na ieneze vizuri kote huku unaigandamiza katika cheese ili igande humo.   

 

  1. Pika ndani ya oven kwa dakika  20- 25   katika moto wa 300- 350  Deg au  mpaka uanze kuona imebadilika rangu kama ya dhahabu kidogo.
  2. Itoe katika oven iweke nje ipowe.
  3. Sasa pika shira   kwa kuchemsha maji na sukari na ipike mpaka shira iwe nzito kidogo sio sana.  Weka Zaafarani uliyoiroweka na maji kidogo. Unaweza kuongeza rangi ya machungwa ukipenda kuipa rangi zaidi. 

 

  1. Mwagia shira juu ya Kunafa. Ikate kate vipande vya mraba (square) kwenye bakuli.       

 

Na sasa iko tayari kuila. 

 

KIDOKEZO  (TIPS)

Inapendeza kuila vugu vugu.


 

 Rudi juu

PUDINI YA NAZI

 

        3 vikombe vya maziwa

        1 kikombe cha unga wa mahindi

        ½ kikombe cha sukari ya hudhurungi (brown sugar)

        1/3 kikombe cha zabibu

        ½ kijiko cha chai cha vanila

        ½ kijiko cha chai cha iliki iliyosagwa

        2 vijiko vya kulia vya siagi

        ½ kikombe cha nazi iliyokunwa yenye sukari. (Sweetened shredded coconut)

 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.

  1. Pasha moto maziwa kwenye sufuria kisha mimina unga wa mahindi ndani yake na ukoroge.
  2. Ongezea sukari, vanilla, iliki, na siagi. Koroga mpaka ichemke kisha upunguze moto huku unakoroga mara kwa mara mpaka mchanganyiko uwe mzito na maziwa yote yawe yamekwisha. Epua na uwache ipoe kidogo.
  3. Chukua chombo cha kumiminia ambacho kina urembo (kama kwenye picha). Kipake siagi alafu unyunyize kikombe ¼ cha ile nazi iliyokunwa.
  4. Mimina ile pudini ndani ya hicho chombo na uweke ndani ya friji siku moja ili ipate kushikana.
  5. Ukiwa tayari kupakuwa, toa pudini kwa makini uweke kwenye sahani nzuri. Nyunyizia ile nazi iliyobaki kupambia

 Rudi juu

 

KEKI YA JIBINI (Cheese Cake) - (Na Ummu Sumayyah)

 

 VIPIMO

Malai ya Jibini (Cream Cheese)               2x 450g
Sukari                                                         1/2 Kikombe
Mayai                                                       2
Unga wa ngano                                       1 Kijiko cha chai
Mtindi (yogurt)                                         1/2 Kikombe cha chai
Ukoko wa tayari  (ready crust)                2
Mananasi ya kopo                                  1
Kastadi ya unga                                     1 Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.    Washa oveni 350°F.

2.    Kwenye bakuli la mashine, changanya malai ya jibini, sukari, mtindi na unga upige hadi ichanganyike vizuri.

3.    Kisha tia mayai na upige kidogo.

4.    Ikisha changanyika vizuri mimina juu ya ule ukoko (crust) na utandaze kila kipembe.

5.    Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 15, kisha weka moto wa 300°F na uchome kwa muda wa saa moja.

6.    Ikishaiva iache ipoe na huku uitayarishie sosi yake.

7.    Katika kisufuria, tia ile juisi ya mananasi utakayoitoa kwenye kopo, pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga hadi iwe nzito.

8.    Mimina juu ya Keki Ya Jibini na upange mananasi. Ukipenda weka cheri au jelly katikati ya duara ya mananasi.

9.    Iweke kwenye friji ipate baridi na itakuwa tayari kwa kuliwa.

 

KIDOKEZO: Unaweza ukagawanya vipimo mara mbili ukatoa keki moja.


 Rudi juu

 

KEKI YA KAROTI - (Na Ummu Sumayyah)

 

VIPIMO
Unga                                           1 Kikombe cha chai
Baking soda                                1 Kijiko cha chai
Iliki ya unga                                1/2 Kijiko cha chai
Chumvi                                       1/4 Kijiko cha chai
Mayai                                          2
Mafuta                                               1/4  Kikombe cha chai
Sukari                                         1/2  Kikombe cha chai
Sukari ya hudhurungi

(brown sugar)                             1/3 Kikombe cha chai

 Mtindi (yogurt)                           1/3 Kikombe cha chai
Karoti iliyokaruzwa                    1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.    Washa oveni moto wa 350°F.

2.    Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.

3.    Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.

4.    Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.

5.    Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.

6.    Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.

7.    Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.

8.    Tengeneza sukari laini (icing sugar) 1/2 kikombe na vijiko 2 vya maji na unyunyizie juu; na ikisha kauka itakuwa tayari kuliwa.

 

 Rudi juu

 

 

KEKI YA  SEMOLINA NA JOZI  (WALNUT)

VIPIMO

 

Mayai                                                  5

Sukari                                                 2 Vikombe vya chai

Mafuta                                                2 Vikombe vya chai

Maziwa                                               2 Vikombe vya chai

Semolina                                            2 vikombe vya chai

Baking powder                                   3 Vijiko vya chai

Jozi zilizosagwa (Walnuts)                4 Vikombe vya chai

Ganda la ndimu iliyokaruzwa            1

Unga                                                 ½ kuzidi kidogo kikombe cha chai  

 

SHIRA 

Sukari                                               4 Vikombe vya chai 

Mai                                                   4 Vikombe vya chai

Ndimu                                              3 Slesi

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

  1. Washa oveni moto wa 300F.
  2. Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri vipimo vyote pamoja isipokuwa kikombe kimoja cha jozi (walnuts), ya kunyunyizia juu kupambia.
  3. Mimina mchanganyiko kwenye chombo cha kuvumbika.
  4. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 45 au zaidi hadi iwive.
  5. Ipike shira kwa kuiacha ichemke dakika 1.
  6. Kisha mimina juu ya keki iliyokwishaiva, na unyunyizie ile jozi iliyobaki
  7. Iache ipoe kabisa kabla ya kuandaa.

 KIDOKEZO: Inapendeza kuliwa ikiwa baridi


 Rudi juu

 

BASBUSA - (Shaam)

 

VIPIMO                                           

 Unga wa Semolina                                 2 Vikombe

Siagi (butter) au samli                             3/4 kikombe

Sukari                                                     3/4 kikombe

Mtindi (Yoghurt au buttermilk)                1 1/4 kikombe

Vanila                                                     1-2 kijiko cha chai

Baking powder                                       1 kijiko cha chai

Baking soda                                           1 1/2 kijiko cha chai

 

Lozi zilizomenywa maganda kwa ajili ya kupambia. 

 

SHIRA

Sukari                                        1 kikombe

Maji                                            1 kikombe

Ndimu ya maji                           1 kijiko cha chai

Pika shira mapema. Chemsha kwa muda wa dakika 20-25 itakapopoa iwe nzito kidogo sio nyepesi sana.

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Washa oveni moto wa 350ºF
  2. Yayusha siagi au samli na iache ipowe.
  3. Changanya sukari na mtindi katika bakuli kubwa.
  4. Changanya semolina, vanila, baking powder, baking soda katika bakuli jengine.
  5. Tia mchanganyiko wa semolina katika bakuli lenye mchanganyiko wa sukari na mtindi na changanya vizuri.
  6. Paka siagi katika sinia ya oveni (baking tray) ya saizi 11" x 7 " au 13" x 9" na tandaza mchanganyiko.
  7. Weka alama ya kukata vipande vipande vya mraba (square) na katika kila kipande weka lozi moja juu yake kupambia.
  8. Iache kwa muda wa dakika 15-20 kabla ya kuipika.
  9. Pika (bake) kwa muda wa dakika 30 au zaidi kidogo hadi iwive na igeuke rangi.
  10. Epua katika oveni na mwagia shira wakati bado imoto na shira iwe iliyopoa baridi.

 

KIDOKEZO:

Ikiwa basbusa ni imoto basi shira iwe baridi, na ikiwa basbusa ni ibaridi basi shira iwe imoto.


 Rudi juu

 

PURI

 

 

VIPIMO

Unga                                                        3 Vikombe

Mafuta ya zaituni au ya kawaida             ¼ kikombe

Chumvi                                                    kiasi

Maji ya dafu dafu                                     ½ kikombe takriban

Mafuta ya kukaangia katika karai       

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

  1. Changanya vitu vyote katika bakuli, kisha ukande unga uwe kama wa chapati. Ikibidi uongoze maji au unga ongeza kwani inategemea na mafuta utakayotumia.
  2. Fanya madonge madogo madogo, kisha yafunike kwa kwa mfuko wa plastiki au kitamba yasipate upepo kwa muda wa dakika 15-20
  3. Pasha moto mafuta huku unasukuma madonge yawe kiasi tu.
  4. Kaanga madonge ukitia moja moja au mawili mawili inategemea na ukubwa wa karai. Kaanga hadi yafure na kubadilika rangi.
  5. Epua na yatie katika chujio yatoke mafuta yakiwa tayari kuliwa.

 

KIDOKEZO:

 

Puri nzuri kuliwa na kuku wa kuchoma na sosi zake kama sosi ya ukwaju.


 Rudi juu

 

VIBIBI

 

VIPIMO

Mchele                                                       2 Vikombe

Tui la nazi                                                  1 1/2 Kikombe

Mafuta                                                       1 kijiko cha supu

Hamira                                                       2 Vijiko vya chai

Unga wa ngano                                        1 kijiko cha supu

Hiliki                                                           kiasi upendavyo

Sukari                                                        ¾ au 1 Kikombe

  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

  1. Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
  2. Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari, ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
  3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike, kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
  4. Ukishafura, mimina sukari na changanya vizuri; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
  5. Weka chuma kipate moto.
  6. Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
  7. Utazame ikishaiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
  8. Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.

 

KIDOKEZO: 

Unaweza kutumia chuma kisichoganda (non stick); nacho hakitaraji kutiwa mafuta.


 Rudi juu

 

MKATE WA KIFARANSA (french toast)

 

VIPIMO
 
 
Mayai                                             6
 Maziwa                                          11/2 Vikombe vya chai
 Vanilla/iliki                                      Kidogo
 Mdalasini ya unga                          1/4 -1/2 Kijiko cha chai
 Kungu manga(nutmeg)                  Kidogo
 Ganda la ndimu iliyokaruzwa        1 kijiko cha supu
 (lemon zest)
 Maji ya machungwa                      1/4 Kikombe cha chai
 sukari                                            1 Kijiko cha supu
 Mkate wa slesi                              6

 
 
 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
   
1} 
Changanya pamoja vipimo vyote isipokuwa mkate kwenye bakuli; weka kando.
 2} Panga mikate katika chombo kikubwa (trei), kisha mimina ule mchanganyiko wa           mayai juu yake na iache irowanike dakika 5 hivi.
3} Weka chuma kipate moto, kisha tia siagi au/na mafuta na upange mikate kadha kama itakavyotosha kwenye chuma cha kuchomea.
4} Iwche hadi iive na kuwa rangi ya dhahabu, kisha geuza upande wa pili na endelea hivyo hivyo mpaka umalize mikate yote.
5} Panga katika sahani na itakuwa tayari kuliwa na shira ya matunda kama maple syrup.

 


 

 Rudi juu

VIKEKI VIDOGO  VYA CHENGA ZA SHAYIRI  - (OATMEAL MUFFINS)

 

 

 VIPIMO

 

Unga                                           2 Vikombe

Chenga za shayiri (oatmeal)       1Kikombe

Baking Powder                            1 Kijiko Cha Supu

Baking Soda                                1/2 Kijiko Cha Chai

Chumvi                                        1/2 Kijiko Cha Chai

Sukari Ya Buni  (Brown Sugar)   1 Kikombe

Mdalasini                                     1 Kijiko Cha Chai

Kungu manga (nutmeg)              1/2 Kijiko Cha Chai

Mayai                                           2

Mafuta                                         1/2 Kikombe

Mtindi (yogurt)                             11/2 Vikombe

Vanilla                                         1 Kijiko Cha Chai

Karoti Ziliokunwa (grated)           1 Kikombe(Karoti 3)

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.         Chunga pamoja unga, oatmeal, baking powder, baking soda, chumvi, sukari ya buni, mdalasini na kungu manga.

2.         Changanya mayai, mafuta, mtindi na vanilla kwenye bakuli. Tia karoti kisha ule mchanganyiko wa unga.

3.         Chota mchanganyiko kwa kijiko tia ndani ya treya maalum ya kupikia muffins/cupcakes.

4.         Pika (bake) katika oveni lenye moto wa 350F kwa dakika 30.

 Rudi juu

 

 

PAI YA KUKU (CHICKEN PIE)

 

VIPIMO

Unga wa kitobosha (puff pastry)                   397-400 gm

Nyama ya kuku bila ya mifupa                      ratili (LB)

Kabichi iliyokatwa nyembamba

nyembamba                                                  2 Vikombe vya chai              

Thomu/Tangawizi iliyosagwa                        1 kijiko cha chakula

Chumvi                                                          kiasi

Pili pili manga                                                1 kijiko cha chakula

Jirah (bizari ya pilau)                                     1 kijiko cha chai

Mdalasini                                                       1 kijiko cha chai

Dania (corriander powder)                            1 kijiko cha chai

Ndimu au limau                                             2 Vijiko vya chakula

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Kama unga wa kitobosha (puff-pastry) uko katika barafu toa mapema kidogo.

2.      Washa jiko la oveni moto wa kiasi cha kiwango 375-400  Deg.

3.      Kata nyama ya kuku vipande vipande kisha itie kwenye sufuria na tia ndani yake, thomu/tangawazi, chumvi, pilipili manga, jirah, mdalasini, dania na ndimu. 

4.      Mpike kuku kwa moto mdogo mdogo hadi awive. Akihitaji maji, tia kidogo tu kiasi cha kumpika awive asibakie na maji. 

5.      Epua na chambua kuku. (Unaweze kutumia sehemu ya kuku ya mifupa, hivyo itabidi uchambue na kutoa mifupa pembeni).

6.      Sukuma unga wa kitobosha (puff-pastry). (Ukipenda kata madonge mawili zitokee pai mbili).

7.      Kuku atakuwa ameshapoa, mchanganye na kabichi vizuri ongeza vikolezo ukipenda kama chumvi, pilipili manga na ndimu.

8.      Weka mchanganyiko wa kuku na kabichi katikakati katika unga uliosukuma na kata kama miba ya samaki (kama ilivyo katika picha)

9.      Suka kufunika vizuri kuku, huku unabana msuko ili ugandane. 

10.   Ziweke pai katika trei ya oveni iliyopakwa siagi kidogo.

11.   Pika katika oven ambalo litakuwa tayari limeshashika moto unaohitajika. Pika hadi zigeuke rangi na ziwive.

12.   Epua, ziweke katika sahani ya kupakulia zikiwa tayari.


 

 Rudi juu

KEKI YA NANASI

  

VIPIMO 
 

Unga                                                        2 vikombe vya chai 

Sukari                                                      1 ½ kikombe cha chai 

Mafuta                                                     1 ½ kikombe cha chai 

Baking powder                                        2 vijiko vya chai 

Siagi                                                        ¼ kikombe cha chai 

Mayai                                                      6 

Sukari ya hudhurungi (brown)                1 ¾  kikombe cha chai 

Manasi ya kopo yaliyokatwa duara        1 kopo 
  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
 

1.      Unayeyusha sukari ya hudhurungi pamoja na siagi. Ikishayeyuka vizuri unamimina kwenye sufuria au trei ya kuchomea keki.

2.      Panga vipande vya nanasi kwenye hiyo sufuria/trei. Weka pembeni. Ukipenda katikati ya duara ndogo ya nanasi weka cheri moja.

3.      Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la mashine, piga mayai, sukari, vanilla mpaka iwe kama malai (crème) na nzito.

4.      Mimina unga pamoja na baking powder, piga kidogo, mwisho mimina mafuta.

5.      Mimina huo mchanganyiko kwenye sufuria/trei uliyopanga vipande vya nanasi, tayari kuchoma.

6.      Weka moto 180 C choma kwa muda wa dakika 30 – 35.

7.      Ikishaiva, acha ipowe kwa muda wa dakika 7, mimina chini juu kwenya sahani, tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO: Ukipenda tengeneza kastadi umimine juu yake iwe kama 'Kitindamlo' (dessert)


 

KEKI ZA VIKOMBE ZA NAZI - (COCONUT MUFFINS)

 

 

VIPIMO

 

Unga                                        ½ kikombe

Sukari                                      ¼ kikombe

Siagi (margarine)                    1 kikombe

Mayai                                       3

Baking powder                         ½ kijicko cha chai

Maziwa mazito                         kopo 1 (285ml)

Nazi (machicha)                      200 gms

Vanilla                                     ½ kijiko cha chai teaspoon

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Tia kwenye bakuli siagi na sukari piga kwa mashine mpaka iwe laini kama malai (Cream)

2.      Tia mayai piga vizuri.

3.      Tia unga na baking powder.

4.      Tia nazi.

5.      Tia maziwa na vanilla, piga kidogo.

6.      Tumia treya za vishimo vya duara (muffin tray), weka karatasi zake, kisha tia mchanganyiko wa keki kiasi usijaze katika vishimo.

7.      Choma (bake) katika moto wa 325 C

8.      Choma kwa muda wa dakika 10 – 15 mpaka iwe rangi ya udongo kidogo (brown).

9.      Epua na tayari kwa kuliwa

 


 Rudi juu

 


MKATE WA NYAMA

  

VIPIMO

Nyama ya kusaga                                   ½ LB

Kitunguu maji kilichokatwa kidogo          1

kidogo (chopped)

Thomu na tangawizi iliyosagawa            1 Kijiko cha chai                   

Pilipili manga ya unga                             1 kijiko cha chai

Unga wa ngano                                       2-3 vikombe

Hamira                                                    1 au 1½ kijiko cha chakula 

Chumvi                                                   ½ kijiko cha chai

Mayai                                                      5

Siagi                                                        225g

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Tia katika nyama thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, (ukipenda bizari zako nyingine), vitunguu, kisha iache kama muda wa saa moja ili vikolee hivyo vitu kwenye nyama.

2.      Ikaushe nyama mpaka iwive kama nyama ya sambusa.

3.      Vunja mayai manne na la tano liache pembeni. Yatie kwenye bakuli upige kama kiasi cha dakika mbili.

4.      Tia unga kwenye mayai na changanya vizuri kisha tia hamira na chumvi halafu changanya kwa sekunde chache tu.

5.      Halafu tia siagi kwenye bakuli la unga na uchanganye vizuri mpaka uchanganyike vizuri yaani lifanyike donge halafu uzunguushie karatasi ya plastiki (plastic wrap) au mfuko wa plastiki, na uweke kwenye friji kwa usiku mzima ulale yaani ni vizuri ulale siku nzima ili ladha yake itokeze.

6.      Siku ya pili toa unga kutoka kwenye friji na uweke kwa muda wa saa moja ili ukande kwa kutumia siagi na lile yai moja lililobakia mpaka uwe laini.

7.      Sukuma kwa kifimbo kama unataka kufanya chapati, yaani utandaze kwa kifimbo halafu ukishakua bapa (flat) chukua nyama yako itandaze juu ya ule mkate yaani nyunyiza kwenye ule unga ulioutandaza.

8.      Kunja unga (roll) na nyama yake ukisha unauzunguusha duara ili kuutia kwenye treya yako ya kubake unauacha uumuke.

9.      Ukishakuumuka unapaka siagi au yai juu yake ukisha unaupika katika jiko (oven) kama unavyopika mikate mengine kwa moto wa 350 Deg. Na kwa muda wa kama dakika 20 au zaidi hadi uwive.

 

Kidokezo

Ni vizuri kuliwa kwa chai au juice


 Rudi juu

 

MAANDAZI YA KUPAMBIA.

 

VIPIMO 

Unga                 3 Magi

Sukari               1 Kikombe

Mayai                2

Hamira              2 Vijiko vya chakula

Hiliki                  1 Kijiko cha chai

Nazi                  1 Ya kopo

Samli                2 Vijiko vya chakula (jaza)

Ufuta                 3 Vijiko vya chakula 
 
 
JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 
  

1.      Unatia hamira kwenye kibakuli na maji kama robo kikombe hivi ikisha unaichanganya mpaka ichanganyike na unaiweka pembeni.  

2.      Unautia unga kwenye bakuli au sinia ikisha unatia na sukari na hiliki, unapasha moto samli na unaitia ikisha unauchanganya unga na samli mpaka uchanganyike uzuri.  

3.      Unapiga mayai kwenye bakuli unayatia, unauchanganya tena halafu unatia na ile hamira ulokwisha ivuruga, huku unaendelea kuuchanganya. 

4.      Hapo sasa ndio unachukuwa ile nazi ya kopo unaitia kidogo kidogo huku unaukanda mpaka ulainike. Unga wa maandazi haya unakuwa mlaini zaidi kuliko maandazi ya mafuta.  Kama nazi haitatosha unaweza kuongeza maziwa au hata maji kidogo mpaka ulainike vizuri unga.   

5.      Ukishamaliza kuukanda utie kwenye bakuli na uwache kwa dakika 10, halafu uchanganye tena bila kuutia kitu chochote. 

6.      Halafu chukuwa treya ipakae mafuta au samli, kisha chukuwa unga usokote kama unavouona hapo juu, au kama unataka kuufanya staili nyingine pia unaweza, unausokota mpaka unamaliza unga wote.

7.      Ukimaliza nyunyiza ufuta juu ya maandazi ulokwisha yasokota, halafu tia treya ya maandazi ndani ya jiko (oven) lakini usiwashe moto, subiri mpaka maandazi yaumuke vizuri.  

8.      Maandazi yakisha kuumuka vizuri sana, washa moto (bake) kwenye jiko na uweke namba 350 kwa muda wa dakika 15, na baada ya hapo punguza moto weka 300 mpaka ukishakuyaona yamewiva. 

9.      Yakiwiva yatoe kwenye jiko na uyapake mafuta juu kidogo ili yalainike na uyawache yapoe, na yakishapoa yatakuwa tayari kuliwa. 

 


 Rudi juu

 

KEKI ZA VIKOMBE

  

 VIPIMO

Unga wa ngano              vikombe 2-3

Mayai                             6

Maziwa                          kikombe 1

Sukari                            kikombe 1

Siagi                              kikombe 1

Baking powder              vijiko vya chai 2-3 (kijiko 1 kwa kikombe cha unga1)

Vanilla                           kijiko cha chai 1

Rose essence               kijiko cha chai robo (kiasi unavyotaka harufu ijitokeze)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Saga siagi, sukari, mayai na essence ya vanilla na rose

2.      Ikishasagika tia unga na maziwa koroga tena.

3.      Mwisho tia baking powder na koroga mpaka ichanganyike.

4.      Washa oven lako moto wa 350’F kwa dakika 2-3.

5.