MANENO YA HEKIMA: UKARIMU
Na Hassan Hemed Abdallah.
Amesema Allah (S.W):
Mfano wa
wale wanaotoa
Wale wanaotoa
Na wanakuuliza
watoe nini? Sema Vilivyokuzidieni.
(Albaqarah 2:219)
Wanakuuliza watoe nini? Sema
Enyi mlioamini!
toeni katika
vile tulivyokupeni kabla haijafika siku amabayo hapatakuwa kujikomboa wala urafiki (wa kusaidiana)
wala uombezi. Na waliokufuru ndio
waliojidhulumu (kweli kweli). (Al baqarah
2:254)
Enyi mlioamini!
toeni katika
vile vizuri mlivyochuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa
vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe
msingevipokea isipokua kwa kutoviangalia (basi Mungu atapokea
kibaya?) basi jueni kwamba Mwenyezi
Mungu ni mkwasi na asifiwaye.
(Al baqarah 2:267)
Wale watowao
Ambao huamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na
Mwenyezi Mungu na Mtume wake na
husimamisha sala na hutoa katika
yale tuliyowapa. (Al baqarah 2:3)
Maamkiano
Na miongoni mwenu atakayemtii Mwenyezi Mungu na
Mtume wake na kutenda mema. Tutampa malipo
yake mara mbili na kuwaandalia
riziki yenye hishima. (Al
Ahzab 33:31)
Muamini Mwenyezi Mungu na
Mtume wake, na toeni katika yale
aliyokupeni. Basi wale walioamini miongoni mwenu na wakatoa,
wana malipo makubwa. (Al-Hadyad 57:7)
Na huwalisha chakula
masikini na
mayatima na wafungwa, na hali
ya kuwa wenyewe
wanakipenda (chakula hicho) (Ad-dahr 76:8)
Soma na Mola wako ni
karimu
Amesema Mtume
Muhammad (S.A.W): Ogopeni moto japo
kwa kutoa sadaka upande wa
tende.
Hakuna hata
siku moja ambayo waja watapambazukiwa
ila malaika wawili huteremka. Basi husema mmoja
wao: Ewe Mola! mpe mwenye
kutoa badala yake, na husema
mwengine: Ewe Mola! mpe mwenye
kufutika asiyetoa hilaki (ya
Toa ewe mwanadamu! utapewa, sadaka
haipunguzi kitu katika
Mtu mmoja alimuuliza
Mtume (S.A.W): Ni upi uislam uliokua bora? akasema Mtume (S.A.W), "kulisha chakula, na kutoa
salamu kwa unaemjua na usiemjua."
Mkarimu yuko karibu na
Allah, yuko karibu na pepo, yuko
karibu na watu.
Mwenye kumuamini
Allah na siku
ya mwisho basi amkirimu mgeni
wake.
Amesema Imam Ally bin Abi Talib:
Miongoni
mwa amali bora zaidi kwa
mkarimu ni kughafilika na anayo yajua.
Amesema Abul-Fathi Al-bustiy:
Atakaekuwa mkarimu kwa ajili
ya
Imesemwa:
Hakua mkarimu anaetoa baada ya
kuombwa, lakini mkarimu ni
yule anaetoa bila ya kuomba.
Ninaona
watu marafiki wa ukarimu, wala
sijaona bakhili katika ulimwengu kwa rafiki.
Amesema Bibi Fatma (R.A)
Aliye karibu mno miongoni
mwenu na
Allah ni aliye karimu mno kwenu.
Amesema Imam Hassan
bin Ally bin Abi Talib:
Atakae kuwa
mkarimu atapata utukufu, na atakae
kuwa bakhili atadharauliwa na kwa hakika aliye
mkarimu mno kwa watu ni
yule anaetoa na kumpa asiyetarajia
kitu kwake na hakika mkombozi
mkubwa kwa watu ni yule
anayekomboa kutokana na kudra.
Amesema Jabran Khalily:
Hakuwa mkarimu kwa kunipa
mimi wakati haja yangu ni
kubwa kuliko yako, bali mkarimu
ni kunipa mimi hali yakuwa
haja yako ni kubwa zaidi
kuliko yangu.
Amesema Goethe
Nipe
na usitaje na kuzungumza ulichonipa.
Amesema:
Mchirizi
wa maji wenye
kumwangilia ni bora kuliko mto
usiomwagilia.
Atakaetoa kwa ajili ya
Aliyemkarimu mno miongoni mwa
watu ni
yule anaetoa kutokana na kichache
alichonacho na akauhifadhi uso wa muombaji na
kudhalilika.
Maneno ya hekima ya Waarabu:
Jiepushe na
uvamizi wa mkarimu anapohisi njaa, mnyonge anaposhiba.
Methali za Waaabu:
Mkarimu anapotoa ahadi hutekeleza.
Ukarimu hutokana na
kuwepo.
Methali za Waswahili:
Mwaka ni majira,
leo mvua kesho jua.
Kutoa ni moyo na wala sio
utajiri