Lifuatalo ni
shairi lililotungwa na Ustadh Saleh
Barkey
MALIPO
YAKIDHIHIRI
Malipo yakidhihiri - Hayamjali hodari
Huwafika majabari - Wenye nguvu wajeuri
Hubana wasofikiri - Waharibifu washari
Pia wasio dhamiri - Madhalimu mashuhuri
Malipo yakidhihiri - Hayataki ushauri
Huvunja wenye viburi - Wapendao ufakhari
Huwasibu matajiri - Wa inadi
na ghururi
Pia wasengenyi siri - Hata laghai
waghuri
Malipo yakidhihiri - Hutesa yakaathiri
Hukumba yakaadhiri - Mafatani watiriri
Huliza walovinjari - Kwa vitimbi vya
dhahiri
Pia wapenda khabari - Waso na niya tahuri
Mlipaji ni
Qadiri - Alotuumba Qahari
Jirudi mja uqiri - Mabaya hayana kheri
Tubu usifanye ari - Tubu kwa Mola Ghafuri
Malipo ayaghairi - Ulipwe mema mazuri
Saleh Muhammed Barkey