Nguo fupi (swali)
|
Hili latuhuzunisha |
nguo fupi mitaani |
|
Tena zina kerehesha |
nizionapo mwilini |
|
Nguo zisisitirisha |
aibu siyo kifani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwanini mwakaa kimya? |
|
|
|
|
Nguo zinahuzunisha |
mwajitia matatani |
|
Waume kutamanisha |
zinachangia kuzini |
|
Jamii zatukanisha |
zawatia utumwani |
|
Wetu vigogo nchini |
Kwanini mwakaa kimya |
|
|
|
|
Nguo hadhi zawashusha |
sawa |
|
Unyama kudhihirisha |
nyuso haya hazioni |
|
Mavazi haya yachosha |
kila muda twalaani |
|
Wetu vigogo nchini |
Kwanini mwakaa kimya? |
|
|
|
|
Na ukweli
waonyesha |
wasivyo kuwa makini |
|
Uchi wajitembezesha |
afadhali punguani |
|
Kwanini mwajidumisha |
na kujishusha thamani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwa nini mwakaa
kimya? |
|
|
|
|
Kwa nini mwajiuzisha |
kusiko taadhimani |
|
Nyie mwajishughulisha |
kujitoa heshimani |
|
Vichupi mwajivalisha |
kuzagaa hadharani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwanini mwakaa kimya? |
|
|
|
|
Ubakaji kuzidisha |
jamii matatizoni |
|
Na lisilo
pendezesha |
kwanini kulithamini |
|
Kwenu nyie mwajikosha |
msiwekwe hatiani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwanini mwakaa kimya |
|
|
|
|
Sio kuwa na watisha |
tu ninauthamini |
|
Ndo mana nawajulisha |
miili isitirini |
|
Heshima mtapandishwa |
vaa vimini chumbani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwa nini mwakaa kimya |
|
|
|
|
Nyie zawafurahisha |
nguo fupi mapajani |
|
Kwao nyie mwajikosha |
msiwekwe lawamani |
|
Twaomba kuwasitisha |
mwaogopa kitugani |
|
Wetu vigogo nchini |
kwanini mwakaa kimya? |
|
|
|
|
Twashauri kupitisha |
sheria zilo makini |
|
Sio kuwachelewesha |
kwani wanawapa nini |
|
Hapa ninahitimisha |
nguo fupi kumuni |
|
Wetu vigogo nchini |
kwanini mwakaa kimya? |
All Hajj Udii
(Sauti Ya Nasaha) (Yarabi
Stara)