·
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mwezi wa Ramadhani ndio huo unatutoka, na
hazikubaki isipokuwa siku chache sana. Aliyeutumia ipasavyo amefuzu, ama yule
aliyepunguza ndani yake akacheza basi siku hizi chache zilizobaki azimalize kwa
wema, kwani ubora wa amali ni mwisho wake. Kwa hivyo ongezeni juhudi katika siku
chache hizi zilizobaki kwa kufanya amali njema ili Mola wenu akusifieni mbele ya
Malaika wake.
·
Ewe mwezi wa Ramadhani! Pole pole, kwani machozi ya wanaokupenda yanazidi
kumiminika, na kwa kufarikiana nawe nyoyo zao zinaumia na kuungulika.
Huenda katika
kusali nyakati za usiku ndani ya siku zilizobaki huku ukiagwa, kukasaidia katika
kuuzima moto wa shauku wa yale waliyopunguza ndani yako.
Huenda nyakati
hizo za kutubu na kuacha maasi kukaziba pengo la yale yaliyopungua katika funga
yako.
Huenda
aliyechelewa na kuukosa msafara wa waliokubaliwa akawahi na kuwa pamoja nao.
Huenda
mateka wa madhambi yake akawahi kujikomboa na kuwa huru.
Huenda
anayestahiki kuingizwa Motoni akafanikiwa kuepushwa nao kwa toba ya kweli na kwa
kushukuru.
Huenda
Rehma za Mwenyezi Mungu zikamkumba mtu asi akaongoka na kujinusuru.
Wasalla
llahu alaa sayiduna Muhammad wa Alaa aalihi wa Sahbihi wa sallam