Kutoa zaka

Utangulizi 2

Maana ya Zaka. 4

Kufaradhishwa Zaka. 5

Umuhimu wake (katika Qur’ani) 5

Umuhimu wake (katika Sunnah) 6

Wasiotoa Zaka (katika Qur’ani) 8

Wasiotoa Zaka (katika Sunnah) 9

Hukmu ya asiyetowa Zaka. 10

Wanaowajibika kutowa. 11

Mtoto na mpungufu wa akili 12

Mwenye deni 12

Aliyefariki 13

Nia. 13

Kutowa panapowajibika. 14

Kuitanguliza. 14

Kuomba dua. 14

Mali inayotolewa Zaka. 15

Dhahabu na  Fedha. 15

Wakati wa Mtume. 16

Nisabu yake. 16

Fedha. 17

Zaka ya Deni (Mwenye kudai) 17

Zaka ya Mapambo. 18

Zaka ya Biashara. 19

Namna ya kutoa Zaka ya Biashara. 20

Kumbuka. 20

Wenye kupokea mishahara. 21

Zaka ya Mazao. 21

Niswabu ya Mazao. 21

Toeni katika vizuri 22

Zaka ya mifugo

Zaka ya ngamia. 23

Zaka ya ng’ombe. 24

Zaka ya mbuzi 24

Wanyama wengine. 24

Zaka ya madini ya kale. 24

Zakatul Fitri 24

Hikma yake. 25

Mwenye kuitowa. 26

Kiasi chake. 26

Wakati wa kuitowa. 26

Kuitanguliza. 26

Sadaka. 27

Aina za Sadaka. 29

Wenye kustahiki zaidi 30

Kuiharibu sadaka. 31

Katika mali ya haramu. 31

Kuwasaidia wanyama. 32

Sadakatuh jaariyah. 32

Kushukuru. 32

Wanaostahiki Zaka. 33

Mafakiri masikini 34

Wenye kuzitumikia. 34

Wenye kutiwa nguvu. 35

Katika kugomboa. 36

Kumsaidia mwenye deni 37

Katika kutengeneza. 37

Katika kupewa wasafiri 37

Walioharimishwa kupewa. 37

Watu wema. 39

 

 

Kuinunua Zaka. 39

Kuisafirisha Zaka. 40

Kuidhihirisha Zaka. 41

 

Muhammad Faraj Salem Al Saiy

http://mawaidha.info/

Utangulizi

Kutoa Zaka ni nguzo ya tatu ya Islam. Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Nguzo za Islam ni tano. Shahada kuwa hapana Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Kusimamisha Swala, na Kutoa Zaka, na Kufunga mwezi wa Ramadhan na Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo wa kufika huko".

 

Kufaridhishwa kwa Zaka ni jambo muhimu na tukufu sana kwa Waislam kwa sababu ya wingi wa faida yake na kwa ajili ya haja kubwa ya kuwepo kwa jambo hilo, kutokana na masikini na mafakiri wanaohitajia sana msaada wa ndugu zao wenye uwezo, kwani katika Kutoa Zaka uhusiano mzuri unajengeka baina ya Waislam matajiri na Waislam masikini, na hii ni kwa sababu siku zote moyo wa mtu huelekea na kumpenda yule anayemfanyia wema na ihsani. Zaka inasaidia pia katika kuzisafisha na kuzitakasa nyoyo.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ÎõÐú ãöäú ÃóãúæóÇáöåöãú ÕóÏóÞóÉð ÊõØóåøöÑõåõãú æóÊõÒóßøöíåöã ÈöåóÇ

"Chukuwa Sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao)".

At Tawba - 103

 

Katika kutoa Zaka au Sadaka kunaizoesha nafsi katika kuwapendelea kheri watu wenye haja na katika kuwaonea huruma na pia kunaipatia nafsi baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Mwenyezi Mungu öAnasema:

æóãóÇ ÃóäÝóÞúÊõã ãøöä ÔóíúÁò Ýóåõæó íõÎúáöÝõåõ æóåõæó ÎóíúÑõ ÇáÑøóÇÒöÞöíäó

"Na chochote mtakachotoa, basi Yeye Atakilipa; naye ni Mbora wa wanaoruzuku".

Saba-a - 39

 

Na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenyezi Mungu anasema: 'Ewe mwanadamu, toa na sisi tutakupa"

 

Anasema Ibni Uthaimiyn:

"Kutoa Zaka ni jambo liliofaradhishwa katika Uislam, na ni nguzo muhimu sana baada ya Shahada mbili na Swala, na dalili ya kuwajibika kwake imo ndani ya Qurani na pia katika mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), pamoja na ijmai ya Waislam, na yeyote anayeikanusha nguzo hii anakuwa Kafir aliyertadi katika Uislam, na hukumu yake ni kutubishwa, na akitubu anasamehewa. Ama akikataa kutubu na akaendelea kuikanusha basi hukmu yake ni kuuliwa.

Ama anayeifanyia ubakhili au akapunguza katika Zaka yake, huyo anakuwa miongoni mwa madhalimu wanaostahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÇáøóÐöíäó íóßúäöÒõæäó ÇáÐøóåóÈó æóÇáúÝöÖøóÉó æóáÇó íõäÝöÞõæäóåóÇ Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóÈóÔøöÑúåõã ÈöÚóÐóÇÈò Ãóáöíãò. íóæúãó íõÍúãóì ÚóáóíúåóÇ Ýöí äóÇÑö Ìóåóäøóãó ÝóÊõßúæóì ÈöåóÇ ÌöÈóÇåõåõãú æóÌõäæÈõåõãú æóÙõåõæÑõåõãú åóÜÐóÇ ãóÇ ßóäóÒúÊõãú áÃóäÝõÓößõãú ÝóÐõæÞõæÇú ãóÇ ßõäÊõãú ÊóßúäöÒõæäó

"Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inyoumiza inayowangoja.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambia); "Haya ndiyo (yale mali) mliyojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya."

At Tawba - 34 - 35

 

"Miongini mwa faida za kutoa Zaka anazozipata mtu katika dini yake" anaendelea kusema Sh. Ibin Uthaimiyn, "Ni kuitimiza nguzo katika nguzo za Kiislam, jambo litakalomletea mtu furaha katika dunia yake na katika akhera yake, na pia inazidi kumkaribisha mja kwa Mola wake na kumuongezea Imani, kama ilivyo katika mambo yote ya kumtii Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala."

Rudi juu

Maana ya Zaka

Zaka ni ile haki Aliyoifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa Muislam katika mali yake anayotakiwa kuwapa wanaostahiki. Neno Zaka, katika lugha (katika kamusi ya lugha ya kiarabu) maana yake ni 'Kujitakasa', kwa sababu anayetoa Zaka anataraji kuitakasa mali yake, nafsi yake na kupata baraka kutoka kwa Mola wake.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ÎõÐú ãöäú ÃóãúæóÇáöåöãú ÕóÏóÞóÉð ÊõØóåøöÑõåõãú æóÊõÒóßøöíåöã ÈöåóÇ

"Chukuwa Sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao)".

At Tawba - 103

 

Zaka ni nguzo ya tatu ya Uislam iliyofaradhishwa katika Qurani tukufu na katika mafundisho ya Mtume mtukufu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na kwa sababu ya umuhimu wake, Mwenyezi Mungu ameitaja mara themanini na mbili katika Qurani kwa kuifuatanisha pamoja na Swala.

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

"Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipomteua Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) kuwa gavana wa nchi ya Yemen na kadhi wao alimwambia:

"Unakwenda katika nchi ya watu wa Ahlul Kitab, kwa hivyo (kwanza) walinganie katika shahada ya Laa ilaaha illa Llah na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakitii juu ya hilo, wafundishe kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia Swala tano mchana na usiku, wakitii juu ya hilo, wafundishe kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia Sadaka (Zaka) za mali zao, zichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kurejeshewa masikini wao, na kama wakitii juu ya hilo, usije ukachukuwa mali zao zenye thamani, na uiogope dua ya aliyedhulumiwa, kwani hapana kizuizi baina yake (dua hiyo) na baina ya Mwenyezi Mungu".

Imesimuliwa na Maimamu wote wa hadithi

 

Imesimuliwa pia na Attabarani kutoka kwa Aliy (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenyezi Mungu amewafaradhishia matajiri wa Kiislam katika mali zao kiasi cha kuwatosha masikini wao. Na (masikini) wasingepata tabu ya njaa na mavazi isipokuwa kutokana na ubakhili wa matajiri wao. Jueni kuwa Mwenyezi Mungu atawahesabia hesabu nzito sana na atawapa adhabu iumizayo".

Rudi juu

Kufaradhishwa Zaka

Zaka imefaradhishwa wakati Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipokuwa Makka katika siku za mwanzo za Uislam, lakini hapakuwekwa Nisaab, (kiwango cha mali ambacho mtu akiwa nacho kwa muda wa mwaka analazimika kuitolea Zaka), wala kiasi cha kulipa, isipokuwa waliachiwa Waislam wenyewe kukisia kiasi cha kutoa.

Katika mwaka wa Pili baada ya Hijra, ilifaradhishwa kiasi chake katika kila aina ya mali na kubainishwa vizuri.

Rudi juu

Umuhimu wake (katika Qur’ani)

Katika Qurani tukufu na katika Mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), yamo mafunzo mengi yanayopendekeza Kutoa Zaka na yanayowakemea wale wasioitoa.

Katika Qurani Mwenyezi Mungu Anasema:

ÎõÐú ãöäú ÃóãúæóÇáöåöãú ÕóÏóÞóÉð ÊõØóåøöÑõåõãú æóÊõÒóßøöíåöã ÈöåóÇ

"(Ewe Mtume) Chukuwa Sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao)".

At Tawba - 103

 

Na maana yake ni "Chukuwa ewe Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) Sadaka maalum kutoka katika mali za Waislam na uwape wanaostahiki ili wenye mali 'wasafike' kutokana na uchafu wa ubakhili na tamaa, na kutokana na ubaya wa kuwanyima masikini haki zao na pia 'uwatakase' nafsi zao kwa sadaka hizo na wapate baraka za Mola wao ili waweze kupata furaha za hapa duniani na za huko akhera.

 

Na Akasema:

Åöäøó ÇáúãõÊøóÞöíäó Ýöí ÌóäøóÇÊò æóÚõíõæäò. ÂÎöÐöíäó ãóÇ ÂÊóÇåõãú ÑóÈøõåõãú Åöäøóåõãú ßóÇäõæÇ ÞóÈúáó Ðóáößó ãõÍúÓöäöíäó. ßóÇäõæÇ ÞóáöíáðÇ ãøöäó Çááøóíúáö ãóÇ íóåúÌóÚõæäó. æóÈöÇáúÃóÓúÍóÇÑö åõãú íóÓúÊóÛúÝöÑõæäó. æóÝöí ÃóãúæóÇáöåöãú ÍóÞøñ áøöáÓøóÇÆöáö æóÇáúãóÍúÑõæãö

"Hakika wachamungu watakuwa katika Mabustani na chemchem.

Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi.

Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.

Walikuwa wakilala kidogo tu nyakati za usiku.

Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.

Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba".

Adhariyaat 15-19

 

Katika aya hiÆi Mwenyezi anatuelezea juu ya wale atakaowaingiza katika bustani Zake na chemchem, kwa sababu walipokuwa huko duniani walikuwa wenye kulala muda mfupi sana nyakati za usiku, na sehemu kubwa ya usiku, walikuwa wakiswali, na nyakati za kabla ya kuingia alfajiri walikuwa wakiomba maghfira huku wakijikurubisha kwake Subhanahu wa Taala.

 

Walikuwa pia watu wenye kutoa katika mali zao kuwapa fakiri na maskini, wenye kuomba na wasiyo omba huku wakiwaonea huruma.

Na Mwenyezi Mungu Akasema pia:

æóÇáúãõÄúãöäõæäó æóÇáúãõÄúãöäóÇÊõ ÈóÚúÖõåõãú ÃóæúáöíóÇÁ ÈóÚúÖò íóÃúãõÑõæäó ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóíóäúåóæúäó Úóäö ÇáúãõäßóÑö æóíõÞöíãõæäó ÇáÕøóáÇóÉó æóíõÄúÊõæäó ÇáÒøóßóÇÉó æóíõØöíÚõæäó Çááøåó æóÑóÓõæáóåõ ÃõæúáóÜÆößó ÓóíóÑúÍóãõåõãõ Çááøåõ Åöäøó Çááøåó ÚóÒöíÒñ Íóßöíãñ

"Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima".

At Tawba – 71

Rudi juu

Umuhimu wake (katika Sunnah)

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mambo matatu naapa juu yake na nakuhadithieni hadithi muihifadhi (vizuri).

Mali haipungui kwa kutoka sadaka, na mtu anapodhulumiwa akasubiri, basi Mwenyezi Mungu humuongezea utukufu, na mtu anapojifungulia mlango wa kuombaomba, basi Mwenyezi Mungu humfungulia mlango wa ufakiri".

Attirmidhy kutoka kwa Abi Kabsha al Anmaary (Radhiya Llahu anhum)

 

Na kutoka kwa Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa; Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Hakika Mwenyezi Mungu anazikubali Sadaka na anazipokea kwa mkono wake wa kuume na anailea kama mmoja wenu anavyomlea nyumbu wake mpaka tonge (anayoitoa sadaka) inafikia ukubwa wa jabali Uhud".

Ahmed - Attirmidhiy na ameisahihisha

 

Hadithi hii inatujulisha kuwa mtu anapotoa Zaka au Sadaka, basi Zaka hiyo inaingia mikononi mwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala kwanza, kabla haijaingia mikononi mwa masikini anayepewa, ikitufahamisha jinsi gani Mwenyezi Mungu anavyoitukuza ibada hii ya Kutoa Zaka na jinsi anavyompenda mja wake mwenye kutoa Zaka au Sadaka hata akaipokea kwa mikono yake Mwenyewe Subhanahu wa Taala kwanza, akaizidisha jaza yake na kuifanya iwe na ukubwa wa Jabali Uhud.

 

Anasema Waki’i:

"Hadithi hii pia inasadikisha kauli yake Subhanahu wa Taala katika Qurani pale Aliposema:

íóÚúáóãõæÇú Ãóäøó Çááøåó åõæó íóÞúÈóáõ ÇáÊøóæúÈóÉó Úóäú ÚöÈóÇÏöåö æóíóÃúÎõÐõ ÇáÕøóÏóÞóÇÊö

"Je! Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba za waja Wake na kuzipokea Sadaka?"

At Tawba - 104

 

Na öAliposema:

íóãúÍóÞõ Çááøåõ ÇáúÑøöÈóÇ æóíõÑúÈöí ÇáÕøóÏóÞóÇÊö

"Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba, na huyatia baraka (mali inayotolewa) Sadaka".

Al Baqarah - 276

 

Imepokelewa kuwa Anas (Radhiya Llahu anhu) amesema:

"Mtu mmoja kutoka katika kabila la Bani Tamim alimwendea Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kumwambia:

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nina mali nyingi na nina jamaa wengi na wageni huja kwangu kwa wingi. Kwa hivyo nijulishe nini nifanye na vipi nitowe?"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

"Utoe Zaka kutoka katika mali yako, kwa sababu hiyo ni tohara itakayokutahirisha, na uwaendee watu wako (ndugu zako wa nasaba), na uijue haki ya masikini na ya jirani na ya muombaji".

Ahmed

 

Na Kutoka kwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mambo matatu naapa juu yake, Mwenyezi Mungu hawezi kumfanya aliye na sehemu yake katika Uislam akawa sawa na yule asiye na sehemu. Na sehemu za Uislam ni tatu. Swala, Funga na Zaka. Na Mwenyezi Mungu anapokuwa pamoja na mja wake hapa duniani, basi huko akhera hamuachi akawa na mwengine asiyekuwa Yeye. Na mtu anayewapenda watu hapa duniani, basi siku ya Kiama Mwenyezi Mungu Atamjaalie awe pamoja nao…."

Ahmed

 

Na kutoka kwa Jabir (Radhiya Llahu anhu) amesema:

"Mtu mmoja alimuuliza Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam);

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; Unasemaje juu ya mtu anayetoa Zaka ya mali yake?"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Atakayetoa Zaka ya mali yake, keshaiondoa shari yake".

Rudi juu

Wasiotoa Zaka (katika Qur’ani)

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÇáøóÐöíäó íóßúäöÒõæäó ÇáÐøóåóÈó æóÇáúÝöÖøóÉó æóáÇó íõäÝöÞõæäóåóÇ Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóÈóÔøöÑúåõã ÈöÚóÐóÇÈò Ãóáöíãò. íóæúãó íõÍúãóì ÚóáóíúåóÇ Ýöí äóÇÑö Ìóåóäøóãó ÝóÊõßúæóì ÈöåóÇ ÌöÈóÇåõåõãú æóÌõäæÈõåõãú æóÙõåõæÑõåõãú åóÜÐóÇ ãóÇ ßóäóÒúÊõãú áÃóäÝõÓößõãú ÝóÐõæÞõæÇú ãóÇ ßõäÊõãú ÊóßúäöÒõæäó

"Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inyoumiza inayowangoja.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambia); "Haya ndiyo (yale mali) mliyojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya."

At Tawba - 34 - 35

 

Na akasema:

æóáÇó íóÍúÓóÈóäøó ÇáøóÐöíäó íóÈúÎóáõæäó ÈöãóÇ ÂÊóÇåõãõ Çááøåõ ãöä ÝóÖúáöåö åõæó ÎóíúÑðÇ áøóåõãú Èóáú åõæó ÔóÑøñ áøóåõãú ÓóíõØóæøóÞõæäó ãóÇ ÈóÎöáõæÇú Èöåö íóæúãó ÇáúÞöíóÇãóÉö æóáöáøåö ãöíÑóÇËõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö æóÇááøåõ ÈöãóÇ ÊóÚúãóáõæäó ÎóÈöíÑñ

"Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao (kufanya ubakhili huko). La, ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni) za yale waliyoyafanyia ubakhili - siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ana khabari za yote mnayoyafanya."

Aali Imran - 180

 

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu amesema 'Sayutawwaquwna' na maana yake ni (Watafungwa kongwa) badala ya 'Sawfa yutawwaquna'. (Watakuja kufungwa kongwa).

Ameacha kutumia neno Sawfa’ akaiunganisha moja kwa moja kwa kusema: 'Sayutawwaquwna' kwa ajili ya kutujulisha ukaribu wa mtu kukumbana na adhabu hizo. Kwa sababu mtu akeshakufa tu kiama chake kishasimama, na kuanzia hapo mpaka siku ya Kiama ataanza kukumbana na baadhi ya adhabu kutokana na yale maovu aliyoyatenda.

Wangapi wametoka majumbani mwao kwa miguu yao wenyewe, wakarudishwa wakiwa wamebebwa. Wangapi walifunga wenyewe vifungo vya suruali zao, wakaja kufunguliwa na waoshaji maiti.

Mwanadamu anapotafakari juu ya wale wanaobebwa juu ya majeneza kila siku na kupelekwa makaburini wakiacha mali zao nyingi nyuma yao, mali zitakazokuja kufaidiwa na warithi, ataona namna gani yeye alivyohangaika kuichuma mali hiyo na nani atakayekuja kufaidika nayo, na nani atakayehesabiwa juu ya mali hiyo.

Ikiwa mali imepatikana kwa njia zisizokuwa za halali au ikiwa mali hiyo haikutolewa ndani yake haki ya Mwenyezi Mungu, basi mali hizo watasatarehe nayo warithi, na yule aliyechuma ndiye atakayeulizwa na Mwenyezi Mungu na kuhesabiwa.

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Akamaliza aya hii kwa kusema:

æóáöáøåö ãöíÑóÇËõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö æóÇááøåõ ÈöãóÇ ÊóÚúãóáõæäó ÎóÈöíÑñ

"Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ana khabari za yote mnayoyafanya."

 

Na maana yake ni kuwa hata kama utawaachia mali hiyo watu wako, wao pia watakuja kufa na watakaokuja baadaye nao watakufa, na mwisho kabisa hapana atakayebaki isipokuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, siku atakayozirithi mbingu na ardhi na kila kilicho juu yake.

Rudi juu

Wasiotoa Zaka (katika Sunnah)

Imepokelewa kutoka kwa Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Atakayepewa mali kisha asitoe Zaka yake, basi mali hiyo Siku ya Kiama itageuzwa kuwa joka dume lenye upara, mwenye madoa mawili machoni pake (kutokana na wingi wa sumu aliyonayo), atajizungusha katika mwili wa mtu huyo, kisha atamkaba shingoni pake huku akimwambia:

"Mimi ndiyo hazina yako uliyokuwa ukiikusanya, mimi ndiyo mali yako", kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akaisoma aya hii:

æóáÇó íóÍúÓóÈóäøó ÇáøóÐöíäó íóÈúÎóáõæäó ÈöãóÇ ÂÊóÇåõãõ Çááøåõ ãöä ÝóÖúáöåö åõæó ÎóíúÑðÇ áøóåõãú

"Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao (kufanya ubakhili huko)".

Bukhari na Muslim

Na kutoka kwa Abdillahi bin Umar bin Khattab - Radhiyallahu anhuma amesema kuwa; "Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Enyi watu wa Madina, mambo matano mkija mkapewa mtihani juu yake na kuteremshiwa - Najikinga kwa Mwenyezi Mungu yasije yakakukuteni - Hautoenea uzinzi katika kaumu mpaka wakafikia kujitangazia, (isipokuwa) yatakuja kuenea kwao maradhi (aina mpya) ambayo hayajakuwepo kwa waliowatangulia, na hawatopunjwa watu katika vipimo na katika mezani isipokuwa wataletewa umasikini na shida ya kupatikana vitu, na dhulma ya ufalme. Na watakapoacha (watu) kutoka Zaka ya mali zao, watanyimwa mvua, na lau kama si kwa ajili ya wanyama, basi isingenyesha mvua. Na watakapovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu na ahadi ya Mtume wake, watasalitishiwa adui asiyekuwa mwenzao achukuwe baadhi ya vilivyo mikononi mwao. Na ikiwa viongozi wao hawatahukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi vitafanywa vita vyao viwe baina yao"

Ibni Majah - Al Bazaar na Al Bayhaqi

Rudi juu

Hukmu ya asiyetowa Zaka

Kutoa Zaka ni fardhi, na ni katika mambo waliyokubaliana maulamaa wote kuwa yeyote anayeikanusha fardhi hii anakuwa kesha toka katika dini akiwa ni kafiri aliyertadi, isipokuwa kama mtu huyo ni Muislam mpya, na kwa ajili hiyo husameheka kutokana na kutoelewa kwake.

Ama yule anayeacha kutoa Zaka lakini wakati huo huo hakanushi kuwajibika kwake, huyo anapata dhambi ya kuacha kuitoa, lakini kuacha huko hakumtoi katika dini, isipokuwa ikiwa anaishi katika nchi inayohukumiwa na sheria ya Kiislam, basi anayehukumu atatakiwa aichukuwe Zaka hiyo kwa nguvu.

 

Ipo hitilafu baina ya maulamaa iwapo anayeacha kutoa Zaka atozwe gharama kwa kuacha kwake huko kwa ajili ya kumtia adabu, na gharama yenyewe ni kuchukuliwa nusu ya mali yake, na hii inatokana na hadithi iliyotolewa na Imam Ahmad na Annasaiy na Abu Daud na Al Haakim na Al Bayhaqiy kutoka kwa Bahza bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kuwa amesema:

"Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

"…Atakayekataa (kutoa Zaka) tutaichukuwa (kwa nguvu, na pia tutachukua) pamoja na nusu ya mali yake haki katika haki ya Mola wetu Mtukufu na watu wa Aali Muhammad si halali kwao kuchukuwa chochote katika hiyo (Zaka)".

Amesema Imam Ahmed kuwa isnadi ya hadithi hii ni sahihi na amesema Al Hakim kuwa hii ni hadithi sahihi.

 

Hata hivyo wapo baadhi ya maulamaa walioidhoofisha hadithi hii na wengine wakasema kuwa hukmu hii ilifutwa baadaye, wakiegemea baadhi ya hadithi zinazoelezea juu ya baadhi ya watu waliochelewa kulipa Zaka na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hakuwachukulia nusu ya mali zao.

Ama ikiwa watu watakataa kutoa Zaka wakiwa wanaelewa kuwa ni jambo la wajibu, na ikiwa zipo nguvu za kuweza kupambana nao, basi watapigwa vita mpaka wakubali kuitoa. Na hii inatokana na hadithi iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim kuwa Abdillahi bin Umar (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka watowe shahad ya; Laa ilaaha illa Llah Muhammadan Rasulu Llah, na wasimamishe Swala na watowe Zaka. Wakishafanya hivyo, damu yao na mali zao zitakingika kwangu isipokuwa katika kulipa haki za Kiislam, na hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu".

 

Imeelezwa na Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) kuwa; Alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na Abubakar akawa (Khalifa), baadhi ya waarabu walikataa kutoa Zaka, na Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alitayarisha jeshi akupambana nao.

Umar akasema (kumuuliza Abubakar):

"Vipi unataka kupigana vita na watu (Waislam), wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alisema:

"Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka watowe shahada ya; Laa ilaaha illa Llah na atakayetamka hayo itakingika kwangu mali yake na nafsi yake isipokuwa katika haki yake (anayodaiwa au kisasi kwa makosa aliyofanya), na hesabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu?”

Abubakar (Radhiya Llahu anhu) akasema:

"Wallahi nitampiga vita yeyote atakayetenganisha baina ya Swala na Zaka, kwa sababu Zaka ni katika 'haki yake' (shahada hiyo). Wallahi lau kama wataacha kunipa mbuzi mdogo (na katika riwaya nyingine 'Kamba') iliyokuwa ikilipwa wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), ningewapiga vita kwa kukataa kwao kuitoa".

Umar (Radhiya Llahu anhu) akasema:

"Wallahi nilipoona kuwa Mwenyezi Mungu amemfungulia Abubakar kifua chake aamue kuwapiga vita, nikajuwa kuwa yuko katika haki".

Muslim - Abu Daud - na Attirmidhy na maimamu wengine wa hadithi.

Rudi juu

Wanaowajibika kutowa

·        Muislam anayemiliki Niswaab, nacho ni 'Kiwango maalum cha mali kilichowekwa na sheria katika aina yoyote ile ya mali inayowajibika kuitolea Zaka.

·        Niswaab hiyo lazima iwe ishatolewa ndani yake mahitajio ya dharura ya lazima kama vile chakula, mavazi, makazi, vyombo vya nyumbani, chombo cha usafiri na vyombo vyake vya kufanyia kazi, madeni nk.

·        Lazima kiwango hicho kiwe kimemilikiwa kwa muda wa mwaka mzima (mwaka wa Kiislam) bila kupungua katika wakati wowote ule ndani ya mwaka huo, na kama kitapungua katika wakati wowote ule kabla ya kutimia mwaka, basi hesabu nyingine mpya itaanzwa kuanzia pale kinapokamilika tena Kiwango hicho.

Amesema Imam An Nawawiy:

"Madhehebu yetu na madhehebu ya Maimam Malik na Ahmad na ya maulamaa walio wengi ni kuwa; Mali inayotolewa Zaka kwa ajili yake, kama vile dhahabu, fedha na wanyama wa kufugwa, lazima kiwango chake kibaki kwa muda wa mwaka mzima bila kupungua. Na wakati wowote ule kitakapopungua, basi mwaka wake unakatika, na wakati wowote ule kitakapotimia tena, unaanza kuhesabiwa mwaka mwingine".

 

Abu Hanifa anasema:

"Kinachotakiwa ni kuwepo kwa Kiwango (Niswaab) mwanzo wa mwaka na mwisho wake, na haidhuru iwapo kitapungua katikati ya mwaka, hata kama mtu alikuwa nazo Dirham mia mbili kisha zikapotea zote katikati ya mwaka na akabakiwa na dhirham moja tu, au kama alikuwa na kondoo arubaini wakapungua na akabaki mmoja tu, kisha mwisho wa mwaka akaweza kumiliki (Dirham) mia mbili kamili au (kondoo) arubaini kamili, basi itawajibika Zaka kwa vyote".

 

Masharti haya hayahusiani na Zaka za mazao na matunda, kwa sababu vitu hivyo Zaka yake inatolewa siku ya mavuno.

Mwenyezi Mungu anasema:

ÃóËúãóÑó æóÂÊõæÇú ÍóÞøóåõ íóæúãó ÍóÕóÇÏöåö

"Na toeni haki yake siku ya kuvuna kwake".

Al An-am – 141

Rudi juu

Mtoto na mpungufu wa akili

Inamuwajibikia aliyekabidhiwa mali ya yatima au ya mtu mwenye upungufu wa akili kuitolea Zaka mali hiyo ikifikia kiwango chake.

Kutoka kwa Abdillahi bin Amru (Radhiya Llahu anhu), anasema kuwa; Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenye kumlea yatima mwenye mali, basi aifanyie biashara mali hiyo na asiiache mpaka ikamalizika kwa kuliwa na Sadaka (Zaka)".

 

Anasema Sh. Sayed Sabeq katika Fiqhis Sunnah kuwa; Isnadi yake ina udhaifu ndani yake. Akaendelea kusema:

“Anasema Al Hafidh kuwa hadithi hii ina ushahidi kuwa ni 'Mursal' iliyorushwa moja kwa moja mpaka kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) bila ya kutaja isnadi. Ama Imam Shafi ameikubali (hadithi hii) kwa sababu zipo hadithi nyingi zinazoelezea juu ya kuwajibika kwa Zaka katika mali yoyote ile.  Anasema Imam Attirmidhiy kuwa wanavyuoni wamekhitalifiana juu ya kuwajibika kuitolea Zaka mali ya yatima,” amemaliza kusema Sh. Sayed Sabeq.

Rudi juu

Mwenye deni

Mwenyezi kumiliki kiwango kinachomwajibisha kutoka Zaka, na wakati huo huo anadaiwa, kwanza anatoa kiasi cha deni analodaiwa, kisha anailipia Zaka mali iliyobaki ikiwa bado inafikia kiwango cha kutolewa Zaka. Ama ikiwa mali iliyobaki haifikii kiwango, basi hatoi Zaka, kwa sababu wakati huo anahesabiwa kuwa ni mtu fakiri, na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anasema:

"Hatoi Sadaka (Zaka) isipokuwa mtu tajiri".

Ahmad

 

Na amesema:

"Ichukuliwa (mali ya Zaka) kutoka kwa matajiri wao na kurudishiwa mafakiri wao".

Rudi juu

Aliyefariki

Anasema Sayyid Sabeq katika Fiqhis Sunnah kuwa, katika madhehebu ya Imam Shafi na Ahmad na Abu Thour, ni kuwa mtu akifarki na akaacha deni la Zaka, basi inawajibika katika mali yake kwanza kutolewa deni la Zaka hata kabla ya kutimizwa wasia aloacha na kabla ya kupewa warithi.

Mwenyezi Mungu anasema:

ãöä ÈóÚúÏö æóÕöíøóÉò íõæÕöí ÈöåóÇ Ãóæú Ïóíúäò

"Baada ya kutoa aliyoyausia au kulipa deni".

An Nisaa - 11

 

Na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Deni la Mwenyezi Mungu linastahiki zaidi kulipwa".

Na Zaka ni deni la Mwenyezi Mungu.

 

Kutoka kwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

“Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Mama yangu amefariki na anadaiwa saumu ya mwezi mzima, je nimlipie?"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamuuliza:

"Mama yako angelikuwa na deni ungemlipia?"

Akasema:

"Naam, ningemlipia".

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

"Basi deni la Mwenyezi Mungu linastahiki zaidi kulipwa".

Bukhari na Muslim

Nia

Zaka ni ibada, na kwa ajili hiyo Kutia Nia ni jambo muhimu kama ilivyo katika ibada yoyote ile. Na nia ni kitu cha moyoni na hakina uhusiano na ulimi, na kusudi lake ni kuwa mtu anapotoa Zaka akusudie kuitoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Hakika ya amali yoyote ni kutokana na nia, na mtu hulipwa kutokan na nia yake".

Rudi juu

Kutowa panapowajibika

Inawajibika kuitoa Zaka pale wakati wake unapowadia, na haijuzu kuichelewesha isipokuwa kwa dharura inayokubalika.

Kutoka kwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) amesema kuwa; Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Haichanganyiki mali pamoja na Zaka isipokuwa itaiangamiza", na katika riwaya nyingine;

"Inakuwa ishakuwajibikia katika mali yako kuitolea Zaka, kisha usiitoe, kwa hivyo (mali ya) haramu (isiyotolewa Zaka) inaiangamiza (mali ya) halali".

Shafi na Bukhari katika 'Attariykh'

Kuitanguliza

Inajuzu kuitanguliza na kuitoa kabla ya kufikia wakati wake hata kabla ya miaka miwili.

Anasema Al Shoukani katika kitabu chake 'Naylu l Awtaar';

"Maulamaa wengi kama vile Azzuhriy na Al Hassan al Basriy na Maimam Shafi na Ahmad na Abu Hanifa wamejuzisha kuitanguliza Zaka kabla ya kufikia wakati wake".

 

Ama Imam Malik na Sufyan al Thouriy na baadhi nyingine ya maulamaa wameona kuwa haijuzu kuitanguliza kabla ya wakati wake, wao wameziegemea zile hadithi zinazowajibisha kutoa Zaka baada ya kukamilika mwaka.

 

Anasema Ibni Rushd:

"Hitilafu iliyopo baina ya maulamaa ni kuwa - Zaka ni Ibada au haki iliyowajibishwa kupewa masikini. Wanaosema kuwa Zaka ni Ibada, wao wameifananisha na Swala na wakasema kuwa haiwezekani kutolewa kabla ya kufikia wakati wake.

Ama wale wenye kuona kuwa ni haki iliyowajibika, wamejuzisha kuitoa kabla ya kufikia wakati wake ikiwa mtu mwenyewe amejitolea kufanya hivyo".

 

Ama Imam Shafi ameegema madai yake katika hadithi inayosema kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kuchukuwa katika mali ya Al Abbas (Radhiya Llahu anhu) na kuitolea Zaka kabla ya kufikia wakati wake.

Rudi juu

Kuomba dua

Inapendeza kumuombea dua mtoaji Zaka, pale anapoitoa.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ÎõÐú ãöäú ÃóãúæóÇáöåöãú ÕóÏóÞóÉð ÊõØóåøöÑõåõãú æóÊõÒóßøöíåöã ÈöåóÇ æóÕóáøö Úóáóíúåöãú Åöäøó ÕóáÇóÊóßó Óóßóäñ áøóåõãú

"Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu. "

At Tawba - 103

 

Kutoka kwa Abudullahi bin Abi Aufiy amesema:

“Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa pale anapoletewa mali ya Zaka akisema: "Allahumma salliy alayhim". Na baba yangu siku moja alimpelekea mali ya Zaka akasema: "Allahumma salliy alaa aali Abi Aufiy".

Ahmad na wengineo.

 

Imepokelewa kutoka kwa Wail bin Hajar kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimuombea mtu mmoja aliyeleta ngamia wa Zaka akasema:

"Allahumma barik fiyhi wa fiy Ibilihi". (Mwenyezi Mungu mbariki yeye na ngamia wake)

Anasema Imam Shafi:

"Ni Sunnah kwa Imam anapopokea mali ya Zaka kumuombea dua mtoaji kwa kumwambia: "Aajaraka Llahu fiyma aatayta, wa baarik laka fiyma abqayta".

(Mwenyezi Mungu akupe ujira mwema katika ulichotoa na akubarikie katika kilichobaki).

Rudi juu

Mali inayotolewa Zaka

1.   Dhahabu na Fedha

2.   Mazao na Matunda

3.   Mali ya Biashara

4.   Wanayama wa kufugwa

5.   Dhahabu na Fesha

Dhahabu na  Fedha

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÇáøóÐöíäó íóßúäöÒõæäó ÇáÐøóåóÈó æóÇáúÝöÖøóÉó æóáÇó íõäÝöÞõæäóåóÇ Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóÈóÔøöÑúåõã ÈöÚóÐóÇÈò Ãóáöíãò. íóæúãó íõÍúãóì ÚóáóíúåóÇ Ýöí äóÇÑö Ìóåóäøóãó ÝóÊõßúæóì ÈöåóÇ ÌöÈóÇåõåõãú æóÌõäæÈõåõãú æóÙõåõæÑõåõãú åóÜÐóÇ ãóÇ ßóäóÒúÊõãú áÃóäÝõÓößõãú ÝóÐõæÞõæÇú ãóÇ ßõäÊõãú ÊóßúäöÒõæäó

"Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza inayowangoja.

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambia); "Haya ndiyo (yale mali) mliyolimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya."

At Tawba - 34 - 35

 

Kwa hivyo mwenye kumiliki viwili hivyo (Dhahabu au Fedha) ikiwa ni katika mfumo wa pesa au mikufu au vipande (vinoo), ikitimia nisabu yake na kukamilisha mwaka na akawa hana deni, wala shida yoyote, anawajibika kuitolea Zaka yake.

Rudi juu

Wakati wa Mtume

Wakati wa Mtume Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam), watu wa Bara Arabu walikuwa wakifanya biashara zao kwa njia ya kubadilishana bidhaa, na hawakuwa wakitumia pesa isipokuwa wachache sana walioweza kumiliki pesa za dhahabu na za fedha zilizokuwa zikitumika katika nchi za jirani.

Pesa zilizotengenezwa kwa dhahabu zilikuwa zikiitwa Dinari, na zilikuwa zikiletwa kutoka nchi za Warumi kama vile Byzantine na nyenginezo, na walikuwa pia wakitumia pesa zilizotengenezwa kwa fedha zilizokuwa zikiitwa Dirham na hizi zilikuwa zikitoka nchi ya Wafursi - Iran.

Kwa vile pesa hizo zilikuwa zikiwafikia zikiwa na uzito mbali mbali, na kiasi mbali mbali, nyengine ndogo ndogo na nyengine kubwa kubwa, na hazikuwa na kiasi maalum wala uzito maalum, kwa hivyo watu wa Makka hawakuwa wakizitumia kama zinavyotumiwa pesa za kawaida, bali walikuwa wakizipima na kuzipa thamani maalum waliyokubalina.

Miongoni mwa vipimo walivyokuwa wakitumia ilikuwa ratili, ambayo wakati huo ilikuwa na uzito wa wakia kumi na mbili na walikuwa pia wakitumia vipimo vya Mithqaal.

Kutokana na kipimo cha Mithqaal, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Haitolewi Zaka ikiwa dhahabu haikutimia Mithqaal ishirini ".

 

Karatasi za benki (Bank notes) zinazopigwa chapa na serikali tofauti ulimwenguni, hupigwa chapa kulingana na Dhahabu na Fedha inayomiliki serikali hizo, ama sivyo serikali yoyote masikini au yenye madeni ingelipiga chapa idadi ya noti yenye thamani kubwa kuliko dhahabu waliyo nayo na kuweza kulipa madeni yao na kujitajirisha.

Rudi juu

Nisabu yake

Dhahabu hailipiwi kitu mpaka ifikie Nisabu yake na imilikiwe (nisabu hiyo) kwa muda wa mwaka (Mwaka wa Kiislam).

Nisabu ya dhahabu ni mithqaal 20 au gramu 92 au Tola71/2 au wakia 3. (Baadhi ya maulamaa wanasema kuwa Nisabu yake ni gramu 85 au Tola 5 au wakia 2), na hii inatokana na ugumu wa kuweza kukisia bei ya vipimo vilivyokuwa vikitumika wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na vinavyotumika wakati wetu huu. Hapana hitilafu juu ya kiwango cha Mithqaal 20 isipokuwa hitilafu ipo katika kuifasiri Mithqaal katika vipimo vya kisasa.

 

Inapofikia kiwango hicho, na kubaki muda wa mwaka, unaichukua na kuipeleka kuipima kwa sonara au kwa wajuzi, na baada ya kuijua thamani yake unailipia 2.5% (mbili unusu katika mia) ya thamani ya dhahabu yote.

Nisabu ya dhahabu ndiyo Nisabu ya pesa za kawaida.

Kwa mfano katika nchi ya UAE, bei ya gramu tisini na mbili ya dhahabu ni Dh. 2575/-

Kwa hivyo hicho ndicho kiwango cha kuanzia kulipia Zaka. Na dhahabu yako inapofikia kiwango hicho unailipia Dh. 64 /- ambayo ni mbili unusu katika mia ya thamani hiyo. Dhabu inapozidi, na Zaka yake inaongezeka.

Unailipia thamani ya dhahabu tu bila kuhesabu ujira wa mfuo au kazi ya mkono au thamani ya nakhshi zake. (Gharama za ufulishaji hazimo).

Rudi juu

Fedha

Nisabu ya fedha ni mithqaal 140 au Tola 36 au wakia 141/2.

Ikifikia kiwango hicho na ikamilikiwa muda wa mwaka, inalipiwa moja katika arubaini au mbili unusu katika mia ya thamani yake.

Zaka ya Deni (Mwenye kudai)

Maulamaa wameigawa deni katika hali mbili.

1-  Ikiwa anayedaiwa ni mtu tajiri au mtu muaminifu, deni hilo litachukuliwa mfano wa pesa zilizowekwa dhamana katika benki ambapo wakati wowote mtu anaweza kuzipata au ana uhakika wa kulipwa deni lake.

Katika hali hii zipo rai tatu.

a)   Ya kwanza ni kuwa mwenye kudai anatakiwa ailipie mali hiyo Zaka yake, juu ya kuwa halazimiki kuilipia mpaka pale atakapozipata na wakati huo atailipia pamoja na Zaka ya siku zote za nyuma.

b)   Ya pili ni kuwa analazimika kuilipia Zaka yake kila unapotimia mwaka, kwa sababu pesa hizo zitahesabiwa mfano wa pesa zilizowekwa benki, na hii ni kwa sababu aliyekopeshwa ni mtu tajiri au muaminifu kiasi cha kuwa ana uhakika wa kulipwa au wa kuzipata pesa zake hizo wakati wowote ule anapozitaka.

c)    Rai ya tatu ni kuwa hazilipii mpaka pale atakapolipwa deni hilo, na hapo atazilipia Zaka ya mwaka ule mmoja tu.

Anasema Sheikh Mohammad bin Uthaymiyn:

"Rai ya mwanzo, nayo ni kuilipia Zaka ya miaka yote pale atakapozipata pesa zake ni bora zaidi na inakubalika zaidi".

 

2-  Ikiwa anayedaiwa ni mtu masikini au mtu asiyekuwa muaminifu, haimuwajibikii mwenye kudai kuzitolea Zaka pesa hizo mpaka pake atakapozipata na kubaki nazo muda wa mwaka mzima kisha atazilipia Zaka ya mwaka huo tu, ambao mali yake hiyo ilibaki kwake kama kawaida ya utoaji wa Zaka.

Anasema Sheikh Bin Uthaimiyn:

"Haijuzu kumdai au kumlazimisha mtu masikini au kumshitaki na hatimaye kumuingiza jela na kumtenganisha na watu wake ikiwa mtu huyo hana kweli uwezo wa kulipa deni, na ikiwa mtu huyo hafanyi ujanja wa kuchelewesha makusudi, na badala yake tunatakiwa tumsitahamilie mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapomfariji.

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÇÊøóÞõæÇú íóæúãðÇ ÊõÑúÌóÚõæäó Ýöíåö Åöáóì Çááøåö Ëõãøó ÊõæóÝøóì ßõáøõ äóÝúÓò ãøóÇ ßóÓóÈóÊú æóåõãú áÇó íõÙúáóãõæäó

"Na kama (mkopi) ana dhiki, basi (mdai) angoje mpaka afarijike, na kama nyinyi (mnaodai mkizisamehe deni zenu) mkazifanya sadaka, basi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua haya (basi fanyeni).

Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha viumbe wote watalipwa kwa ukamiliyote waliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa".

Al Baqarah - 280 - 281

Mtu akisema:

"Pesa zangu kwanini nisizidai?", Anaendelea kusema Sh. Bin Uthaimiyn,

"Tunamwamia:

Ni kweli pesa zako, lakini wewe mwenyewe ndiye uliyemkopesha pesa hizo. Pale alipokujia kutaka kukukopa ungelimtafutia udhuru wowote ule, kisha ukampa kiasi chochote cha mali ikiwa kama ni msaada tu kutoka kwako, basi yansingekukuta haya. Lakini umkopeshe na hali unajuwa kuwa mtu huyu ni masikini, kisha akishindwa kukulipa ukamshitaki, umtie jela na kumtenganisha na mke na watoto wake, jambo hilo ni haramu kabisa na haijuzu kwa Muislam kulitenda".

(Mwisho wa maneno ya Sheikh Ibni Uthaimiyn).

Rudi juu

Zaka ya Mapambo

Maulamaa wamekhitalifiana katika kuzitolea Zaka dhahabu na fedha za mapambo.

Wapo waliosema kuwa dhahabu au fedha ya kujipamba inapofikia Nisabu yake lazima itolewe Zaka yake, na hawa wameegemeza hadithi ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema kumwambia mwanamke mmoja aliyemvisha mwanawe mkufu wa dhahabu akamwambia:

"Unailipia Zaka yake?"

Akasema:

"La, hatuilipii"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

"Huogopi Mwenyezi Mungu akakuvalisheni mikufu ya Moto? Zilipie Zaka yake".

Imam Ahmad

 

Na pia hadithi iliyosimuliwa na Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) aliposema:

"Aliingia chumbani kwangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akaniona nimevaa pete za fedha. Akaniuliza:

"Nini hiki Ewe Aisha?"

Nikamwambia:

"Nimezitengeneza ili nijipambe kwa ajili yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu".

Akasema:

"Unazilipia Zaka yake?"

Nikasema:

"Hapana."

Akasema:

"Hiyo inatosha kwa (kukupatia adhabu ya) Moto".

Abu Daud - Addaraqutni na Al Baihaqi

 

Ama wale wanaosema kuwa Dhahabu ya mapambo hailipiwi Zaka, wao wameegemeza hoja zao katika hadithi iliyosimuliwa na Al Baihaqiy inayosema:

"Jabir bin Abdillah (Radhiya Llahu anhu) aliulizwa juu ya mapambo:

"Yanatolewa Zaka?

Akasema:

"La, hayatolewi"

Akaulizwa:

"Hata kama thamani yake itafikia Dinari elfu moja?'

Akasema:

"Zaidi" (hata kama zaidi ya thamani hiyo)

Na pia hadithi iliyomo katika Muwataa, kitabu cha Imam Malik inayosema:

"Bibi Aisha alikuwa akiwalea wana wa kaka yake mayatima na walikuwa na mapambo na hakuwa akiyatolea Zaka.”

 

Atakayezichunguza hadithi hizi na zile, ataona kuwa zile zinazolazimisha kuitolea Zaka dhahabu au fedha ya mapambo ndizo zenye nguvu zaidi na zenye uhakika zaidi kuliko zisizolazimisha - Wallahu Taala Aalam.

Rudi juu

Zaka ya Biashara

Hukmu yake

Wapo baadhi ya maulamaa ambao ni wachache sana wanaosema kuwa hapana dalili ya kuwa mali ya biashara inatolewa Zaka, lakini dalili zilizomo ndani ya Qurani na Sunnah zinaleta maana kinyume na rai zao.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ÎõÐú ãöäú ÃóãúæóÇáöåöãú ÕóÏóÞóÉð ÊõØóåøöÑõåõãú æóÊõÒóßøöíåöã ÈöåóÇ æóÕóáøö Úóáóíúåöãú Åöäøó ÕóáÇóÊóßó Óóßóäñ áøóåõãú

"Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu."

At Tawba - 103

Aya hii inaleta maana ya ujumla kuwa Zaka inatakiwa itolewe kutoka katika mali zao (Matajiri), mali ya aina yoyote ile ikiwemo mali ya biashara, bila kufafanua aina ya mali hiyo.

Na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Ichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kurudishiwa mafakiri wao".

Kwa hivyo dalili hizi zinatujulisha kuwa mali yoyote ile, ikiwemo mali ya biashara, lazima itolewe Zaka, na kwamba Zaka hiyo ichukuliwe kutoka kwa matajiri, na bila shaka wafanya biashara ni matajiri, na kwamba irudishwe kwa masikini. Muhimu mali hiyo iwe imekifikia kile kiwango cha kutolewa Zaka (Niswabu) na imekamilisha muda wa mwaka.

Rudi juu

Namna ya kutoa Zaka ya Biashara

Mwenye kumiliki mali ya biashara iliyofikia Niswabu, akishakamilisha mwaka anatakiwa ahesabu mali yake yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya biashara. Kama ni mfaya biashara wa nyumba, basi azihesabu nyumba zake (zile tu alizozitayarisha kwa ajili ya biashara), au ardhi au vyombo vya nyumbani, magari au nguo au biashara ya aina yoyote ile. Atavihesabu vitu alivyokuwa navyo kwa ajili ya biashara pamoja na kuzihesabu pesa zote alizonazo kwa ajili ya biashara kisha atazitolea Zaka yake, nayo ni mbili unusu katika mia au moja katika arubaini.

Atafanya hesabu hiyo bila kujali kama wakati wowote ule ndani ya mwaka ule pesa hizo zilipungua au kuongezeka.

Rudi juu

Kumbuka

Ikumbukwe kuwa vitakavyohesabiwa ni vitu vilivyotayarishwa kwa ajili ya biashara tu.

Kwa mfano mtu anamiliki magari hata yakifikia idadi ya magari kumi au zaidi, au atataka kuuza gari lake mwenyewe kwa ajili ya kulibadilisha tu na kununua gari jengine au ardhi au nyumba au chochote kile, ikiwa anataka kuuza kwa ajili ya kutaka kununua kingine badala yake au kwa ajili ya mahitajio mengine yasiyokuwa ya kibiashara, basi mali hiyo haitolei Zaka ya biashara, na hii ni kwa sababu nia ya kuviuza vitu hivyo si kwa ajili ya biashara.

Kumbuka pia kuwa Zaka inatolewa kutokana na asili ya chochote kilichoongezeka kutokana mali hiyo wakati wowote ule katika mwaka. Ama kile kilichoongezeka kutokana na asili nyingine, basi mwaka wake unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ile iliyoongezeka mali hiyo.

Kwa mfano;

Mfanya biashara alikuwa akiendela kupata faida katika biashara yake na kufikia kiasi cha Shilingi laki kumi, kisha katika mwezi wa mwisho au hata katika siku ya mwisho kabla ya kutimia mwaka, akapata faida kiasi cha Shilingi laki saba, pesa zote hizo ZITAHESABIWA pamoja na Zaka ya biashara ya mwaka huo, kwa sababu asili yake (faida iliyopatikana) inatokana na biashara hiyo anayoitolea Zaka.

Mfano mwingine:

Mfanya biashara alikuwa akiendelea kupata faida katika biashara yake na kufikia kiasi cha shilingi laki kumi, kisha katika mwezi wa kumi na mbili au katika siku ya mwisho au siku yoyote ile ya mwaka huo kabla ya kuingia muda wa kulipa Zaka ya mwaka ule, mtu huyo akarithi pesa kutoka kwa jamaa yake aliyefariki kiasi cha Shilingi milioni moja.

Pesa hizo alizorithi HAZITOHESABIWA katika Zaka ya mwaka huo, bali ataanza kuzihesabia mwaka wake mpya kuanzia siku ile alizozipata pesa hizo. Kwa sababu asili ya pesa hizo hazitokani na biashara ile anayoitolea Zaka, bali inatokana na asili nyingine, ambayo ni urithi.

Rudi juu

Wenye kupokea mishahara

Kwa kawaida mwenye kupokea mshahara pesa zake huongezeka na kupungua katika miezi mbali mbali. Kwa vile itakuwa vigumu kwake kuweka hesabu ya kila mwezi pale zinapokamilisha Niswabu au kuongozeka pale zinapopungua, wanavyuoni wakasema kuwa mtu huyo ataanza kuuhesabu mwaka wake kuanzia siku ile aliyoweza kutimiza Nisabu, na kuanzia mwezi huo, atakuwa akiitolea Zaka mali yake kila anapotimiza mwaka.

Zaka ya Mazao

Mwenyezi Mungu amewajibisha kuyatolea Zaka mazao Aliposema:

æóåõæó ÇáøóÐöí ÃóäÔóÃó ÌóäøóÇÊò ãøóÚúÑõæÔóÇÊò æóÛóíúÑó ãóÚúÑõæÔóÇÊò æóÇáäøóÎúáó æóÇáÒøóÑúÚó ãõÎúÊóáöÝðÇ Ãõßõáõåõ æóÇáÒøóíúÊõæäó æóÇáÑøõãøóÇäó ãõÊóÔóÇÈöåðÇ æóÛóíúÑó ãõÊóÔóÇÈöåò ßõáõæÇú ãöä ËóãóÑöåö ÅöÐóÇ ÃóËúãóÑó æóÂÊõæÇú ÍóÞøóåõ íóæúãó ÍóÕóÇÏöåö

"Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye alyeiumba miti inayoegemezwa na isiyoegemezwa, na mitende na mimea yenye matunda mbali mbaIi, na (akaumba) mizaituni na mikomamanga inayofananana na isiyofanana. Kuleni matunda yake inapotoa matunda na toeni haki yake siku ya kuvuna kwake".

Al An-am - 141

 

Katika kuifasiri aya hii amesema Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu):

'Haki yake, ni Zaka yake iliyofaradhishwa".

 

Wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), Zaka ya mazao ilikuwa ikitolewa katika Mahindi, Ngano, Mtama, Tende na Zabibu na wengine wakaongeza 'Mchele' na wengine wakasema kuwa Zaka ya mazao inatolewa katika chakula chochote kile kinachoweza kubaki muda mrefu kama vile mwaka au zaidi bila kuharibika.

Matunda, hayakuwa yakitolewa Zaka isipokuwa Tende na Zabibu. Matunda mengine hayakuwa yakitolewa Zaka isipokuwa kama matunda hayo ni kwa ajili ya biashara, basi hapo itatolewa Zaka ya biashara na si Zaka ya Mazao.

Zaka ya Mazao inatolewa siku ya kuvuna na kabla ya kuuzwa wala kuliwa na si lazima itimie mwaka.

Rudi juu

Niswabu ya Mazao

Mazao hayatolewi Zaka mpaka yatimie Wiski tano yakiwa safi bila magamba. Kama hayajasafishwa, basi lazima yatimie wiski kumi.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Chini ya Wiski tano haitolewi Zaka".

Imam Ahmad na Al Bayhaqiy

 

Wiski 5 ni sawa na pishi 300, kwa sababu wiski moja ni sawa na pishi sitini kwa pishi iliyokuwa ikitumika wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na pishi sitini mara tano ni sawa na pishi mia tatu.

Kwa vipimo vya kisasa, anasema Ustadh Said Abdullah Seif Al Hatimiy katika kitabu chake 'Kutoa Zaka':

"Niswaab ya mazao ni Wisqi 5. Moja ni kilo 60 yaani kilo 300. Kilo moja ni ratili 13/4 (ratili mbili kasorobo) (300 mara 13/4 = ratili 525).

Kilo karibu ni sawa na pishi ya mbao (vibaba vinne)."

Mwisho wa maneno ya Ustadh Said Al Hatimiy.

 

Kwa hivyo mazao yakifikia pishi 300 au ratili 525 yanakuwa yamefikia Niswaab yake (kiwango chake) na yatatolewa Zaka yake ambayo ni moja juu ya kumi (one tenth), hii ikiwa mazao hayo yanapata maji yake bila kuyahangaikia, yaani kama vile kunyeshewa na mvua au maji ya mito au chemchem nk.

Ama ikiwa mkulima anayatilia maji yeye mwenyewe kwa kuyahangaikia maji hayo, basi Zaka yake itapungua na itakuwa ni nusu ya moja juu ya kumi.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Kilichonyeshewa na mvua au maji yanayopita (waadi) au yaliyotwama (Zaka yake ni) moja katika kumi na kilichomiminiwa maji nusu ya moja katika kumi".

Bukhari na wengineo.

 

Mwenyezi Mungu ameamrisha kuitoa Zaka ya mazao; "Siku ya kuvuna kwake", na maana yake ni; kabla hakijaliwa wala kugawiwa chochote kile ndani yake, na ikiwa mtu amekwishafanya hivyo kwa kusahau, basi itambidi akisie kile alichotoa au alichouza na akitolee Zaka yake.

Ama kile alichokula mkulima kabla ya kuvuna, hakimo katika hesabu.

Alipoulizwa Imam Ahmad juu ya wanachokula wenye ardhi kabla ya mavuno alisema:

"Hapana neno ikiwa atakula katika mazao yake kiasi anachohitajia".

Anasema Sh. Sayed Sabiq:

"Kauli hii pia imetamkwa na Imam Shafi na Allayth na Ibni Hazm'.

Ama Imam Malik na Imam Abu Hanifa wanasema:

"Anachokula mtu katika mazao yake kabla ya mavuno atahesabiwa katika Niswaab"

Mwisho wa maneno ya Sayed Sabiq.

Rudi juu

Toeni katika vizuri

Baadhi ya wenye kumiliki mitende walikuwa wakitoa Zaka yao ya mazao katika tende au zabibu au mazao yasiyokuwa mazuri. Walikuwa wakichagua mazao yasiyokuwa mazuri na kuyatolea Zaka, na yale mazuri walikuwa wakichukua wenyewe.

Mwenyezi Mungu Akasema:

íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÃóäÝöÞõæÇú ãöä ØóíøöÈóÇÊö ãóÇ ßóÓóÈúÊõãú æóãöãøóÇ ÃóÎúÑóÌúäóÇ áóßõã ãøöäó ÇáÃóÑúÖö æóáÇó ÊóíóãøóãõæÇú ÇáúÎóÈöíËó ãöäúåõ ÊõäÝöÞõæäó æóáóÓúÊõã ÈöÂÎöÐöíåö ÅöáÇøó Ãóä ÊõÛúãöÖõæÇú Ýöíåö æóÇÚúáóãõæÇú Ãóäøó Çááøåó Ûóäöíøñ ÍóãöíÏñ

"Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kutoviangalia (Basi Mungu atapokea vibaya?). Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi na asifiwaye".

Al Baqarah - 267

 

Anasema Imam As Shoukani:

"Hii ni dalili kuwa, haijuzu mtu kuwapa watu Zaka katika yale mazao mabovu na yasiyokuwa mazuri."

Zaka ya wanyama wa kufugwa

Wanyama wanaofugwa wanalazimika kutolewa Zaka kwa masharti yafuatayo:

1.   Lazima watimie Niswabu

2.   Wakamilishe mwaka

3.   Wawe wanyama wa kufugwa.

Wanyama wasiokuwa wa kufugwa kama vile wa kupandwa au wanaotumiwa kwa kubeba mizigo au kwa kilimo n.k. Hawa hawatolewi Zaka.

Wanyama wanaotolewa Zaka ni Ngamia, Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo.

Rudi juu

Zaka ya ngamia

Ngamia hawatolewi Zaka mpaka watimie watano. Wakitimia watano wa kufugwa hadi tisa na kutimiza mwaka chini ya milki ya mtu, basi atawatolea mbuzi mmoja.

Wakitimia ngamia 10 mpaka 14 atawatolea mbuzi wawili.

Na hivyo hivyo kila wakizidi ngamia watano ataongeza mbuzi mmoja.

Wakitimia ngamia 25 mpaka 35 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha mwaka na kuingia mwaka wa pili au mtoto wa ngamia dume aliyekamilisha mwaka wa 2 na anaingia wa 3.

Kuanzia ngamia 36 mpaka 45 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 2 na keshaingia wa 3.

Kuanzia ngamia 46 mpaka 60 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 3 na kuingia wa 4.

Kuanzia ngamia 61 mpaka 75 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 4 na kuingia mwaka wa 5.

Kuanzia ngamia 76 mpaka 90 atatoa watoto wa ngamia wawili jike waliokamilisha miaka miwili na kuingia wa tatu.

Kuanzia ngamia 91 mpaka 120 atatoa watoto wa ngamia wa kike wawili waliotimia miaka 3 na kuingia mwaka wa 4.

Wakizidi kuliko hapo, basi katika kila ngamia 40 atatoa mtoto wa ngamia wa kike aliyekamilisha miaka 2 na kuingia wa 3. Na katika kila ngamia 50 waliozidi kuliko hapo atatoa mtoto wa ngami wa kike aliyekamilisha miaka 3 na kuingia wa nne.

Anasema Sayed Sabeq katika Fiqhis Sunnah:

"Hawatolewi Zaka ngamia dume ikiwa wapo wa kike, lakini anatolewa mtoto wa ngamia wa kiume aliyetimia miaka miwili na kuingia wa tatu ikiwa hajapatikana wa kike aliyekamilisha mwaka na kuingia wa pili.

Rudi juu

Zaka ya ng’ombe

Ng'ombe hawatolewi Zaka mpaka watimie 30 wa kufugwa. Wanapotimia 30 mpaka 39 wa kufugwa na kukamilisha mwaka, atatolewa ndama aliyekamilisha mwaka mmoja.

Wakitimia ng'ombe 40 mpaka 59 atatolewa ndama asiyepungua umri wa miaka miwili.

Wakitimia ng'ombe 60 mpaka 79 atatolewa ndama wawili wa mwaka mmoja.

Kutoka hapo, kila wakizidi ng'ombe 30, ataongeza kutoa ndama wa mwaka mmoja.

Na kila wakizidi ng'ombe 40 atawatolea ndama wa miaka miwili.

Zaka ya mbuzi

Mbuzi hawatolewi Zaka mpaka watimie 40, na wakitimia arubaini mpaka 120 wa kufugwa na kukamilisha mwaka kwa mwenye kuwamiliki, atawatolea mtoto wa mbuzi wa mwaka mmoja.

Hatowatolea tena mpaka wafikie idadi yao mbuzi 121.

Wakiongezeka na kutimia 121 mpaka 200, atawatolea mtoto wa miaka miwili.

Kuanzia mbuzi 201 mpaka 300 atawatolea kondoo watatu.

Wakizidi kuliko mbuzi 300, basi atawatolea kondoo mmoja katika kila mbuzi mia waliozidi.

Inaruhusiwa pia kutoa mbuzi badala ya kondoo.

Rudi juu

Wanyama wengine

Wanyama wengine wasiokuwa hawa kama vile farasi, nyumbu, punda na wengineo, hawatolewi Zaka isipokuwa kama ni kwa ajili ya biashara.

Zaka ya madini ya kale

Madini inayotolewa ardhini kama vile petroli, gesi, shaba, chuma n.k, hivi vyote havitolewi Zaka, isipokuwa dhahabu na fedha tu na tushaelezea hapo mwanzo namna ya kutoa Zaka yake. Ama vilivyobaki vinatolewa Zaka ya biashara baada ya kuchimbuliwa au kutolewa na kuuzwa.

Zakatul Fitri

Imefaridhishwa katika mwezi wa Shaabani mwaka wa 2 baada ya Hijra (baada ya kuhamia Madina). Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alifaridhisha Zakatul Fitr ili iitakase saumu kutokana na dhambi ndogo ndogo zilizopatikana ndani ya mazungumzo na matendo. Na wakati huo huo Zaka hiyo iwe msaada kwa mafakiri na wasiojiweza katika kuisherehekea Sikukuu.

Imepokelewa kutoka kwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

"Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alifaridhisha Zaka ya Fitri kwa ajili ya kumtakasa aliyefunga kutokana na dhambi ndogo ndogo za mazungumzo na matendo, na ili wafaidike masikini . Atakayeitoa kabla ya Swala (ya Idi) inakubaliwa kama Zaka ya Fitri na atakayeitoa baada ya Swala inakubaliwa kama Sadaka ya kawaida."

Abu Daud – Ibni Majah na Addaraqutni

 

Alikuwa (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akitoa Zaka ya Fitri siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhan kabla ya Swala ya Idi kuswaliwa.

Abu Daud na Ibni Majah na Al Hakim

 

Kila aliyefunga Mwezi wa Ramadhani mwenye kumiliki chakula cha kumtosha kwa muda wa siku moja, inamwajibikia kutoa Zakatul Fitri, nayo ni pishi ya tende au pishi ya ngano au pishi ya shaiyri. Anatakiwa atowe kwa ajili yake na kwa ajili ya kila anayemtegemea kama vile wanawe, wakeze nk. na kuwapa masikini ili nao wapate kufurahi katika Siku ya Sikukuu.

Kwa vipimo vya kisasa, pishi moja ya mbao iliyokuwa ikitumika wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni kiasi cha kilo 2.

Zaka hii ni wajibu kwa kila Muislam mdogo na mkubwa, mwanamume au mwanamke.

Ibni Umar (Radhiya Llahu anhu) amesema:

"Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amefaridhisha kwa kila mtu kutoa Zakatul Fitri katika mwezi wa Ramadhani, pishi ya tende (au) pishi ya shaiyri, ikiwa yeye ni mtumwa au mtu aliye huru, mwanamume au mwanamke, mdogo au mkubwa miongoni mwa Waislam".

Bukhari na Muslim

Rudi juu

Hikma yake

Zakatul Fitri ilifaridhishwa katika mwezi wa Shaabani mwaka wa pili baada ya Hijra kwa ajili ya kumtwahirisha aliyefunga kutokana na makosa yoyote yale aliyotenda katika mwezi wa Ramadhani pale alipokuwa amefunga, kama vile mazungumzo ya upuuzi au madhambi, na wakati huo huo Zaka hiyo itawafaa masikini na wahitaji ili nao wapate kufurahi pamoja na Waislam wenzao siku ya Sikukuu.

Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) amesema:

"Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amefaridhisha Zakatul Fitri kwa ajili ya kumtahirisha aliyefunga kutokana na maneno ya upuuzi au madhambi madogo madogo na ili masikini nao wapate chakula. Atakayeitoa (Zaka hiyo) kabla ya Swala (ya Idi) inakubaliwa Zaka yake, ama atakayeitoa baada ya Swala (ya Idi), itahesabiwa kama ni Sadaka ya kawaida tu".

Abu Daud na Ibni Majah na Addaraqutniy

Mwenye kuitowa

Anayeitoa Zaka hiyo ni mtu aliyefunga. Anajitolea yeye mwenyewe, mkewe na watoto wake wanaomtegemea na anawatolea pia wote wale wanaomtegemea wakiwemo watumishi wake.

Kiasi chake

Iliyowajibishwa katika Zakatul Fitri ni pishi ya ngano au ya shaiyri au ya tende au zabibu au mchele au mahindi na vinginevyo vilivyo na mfano huo katika vyakula.

Imam Abu Hanifa peke yake amejuzisha kutoa pesa zenye thamani hiyo badala ya kutoa nafaka panapo udhuru

Rudi juu

Wakati wa kuitowa

Maulamaa wengi wamekubalina kuwa Zakatul Fitri itolewe katika Ramadhani ya mwisho, lakini wamekhitalifiana juu ya wakati maalum unaowajibika kuitoa.

Wapo waliosema kuwa wakati unaowajibika kuitoa ni pale jua la Ramadhani ya mwisho linapozama, na wengine wakasema kuwa wakati wake ni kuanzia baada ya kuingia alfajiri ya siku ya Sikukuu.

Kutokana na hitilafu hii tunapata faida ya kuwajibika kumtolea Zaka hiyo mtoto aliyezaliwa kabla ya kuingia alfajiri ya siku ya Sikukuu na baada ya jua kuzama, je mtoto huyo anatolewa Zaka?

Kwa wale wenye kufuata rai kuwa wakati wa kuitoa Zaka hiyo ni pale jua la siku ya Ramadhani ya mwisho kuzama, mtoto huyo hatolewi Zaka kwa sababu amezaliwa baada ya kumalizika wakati wa kuwajibika, na kwa wenye kufuata rai ya pili, kwa sababu amezaliwa kabla ya wakati unaomwajibika.

Kuitanguliza

Maulamaa wengi wanakubali kuwa Zakatul Fitri inaweza kutangulizwa na kutolewa kabla ya wakati wake kwa siku moja au mbili.

Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibni Umar (Radhiya Llahu anhu) inasema:

"Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ametuamrisha kuitoa Zakatul Fitri kabla ya watu kutoka msikitini (katika Sala ya Idi)".

 

Anasema Nafe-a (Radhiya Llahu anhu):

"Ibni Umar (Radhiya Llahu anhu) alikuwa akiitoa kwa siku moja au siku mbili kabla ya Siku ya Sikukuu".

 

Ama zaidi ya hapo, maulamaa wamekhitalifiana.

Imam Abu Hanifa amesema:

"Inaweza kutolewa wakati wowote ule katika mwezi wa Ramadhani".

Imam Shafi amesema:

"Inajuzu kuitoa (hata) katika siku za mwanzo za mwezi wa Ramadhani".

Imam Malik amesema:

"Inajuzu kutanguliza kwa siku moja au mbili kabla ya Sikukuu".

Lakini maulamaa wote wamekubaliana kuwa haijuzu kuiahirisha na kuitowa baada ya Idi.

Rudi juu

Sadaka

Muislam anaipa mali yake mtazamo wa aina nyingine kabisa tofauti na asiyekuwa Muislam, kwani dini ya Kiislam inampa kila mtu haki ya kutafuta mali na kufanya biashara ya halali na kuwa tajiri anayeweza kumiliki mali nyingi. Isipokuwa baada ya kuimiliki mali hiyo, analazimika kuwapa maskini Zaka, ambayo ni haki yao maalum waliyopangiwa na Mola wao Subhanahu wa Taala.

Wakati huo huo Muislam anatakiwa ajipatie thawabu nyingi zaidi na ajiepushe na shari nyingi pamoja na kuwasaidia ndugu na jamaa zake, na masikini waislamu wenzake wenye kuhitaji, kwa kutowa kiasi kingine katika mali zao kwa hiari yao wenyewe na kwa kiasi anachokitaka mwenyewe, na hii inaitwa 'Sadaka'.

Kinyume na njia inayotumika katika nchi za kikoministi za kuwanyang'anya matajiri mali zao kwa nguvu na kuwapa masikini, kitendo cha dhulma na cha ufisadi, kwa sababu binadamu kwa kawaida wanakhitalifiana katika ujuzi na katika jitihada zao, na kwa ajili hiyo lazima wahitalifiane katika ujira na mapato yao, kwani katika kuwafanya watu wote wawe sawa katika mapato, utakuwa unamweka katika daraja moja mvivu na mwenye kujitahidi, hodari na asiyekuwa hodari, mtaalamu na asiyekuwa mtaalamu.

Hii ikiwa mali hiyo wanayonyang'anywa matajiri wanapewa kweli masikini na wale wanaostahiki, na ikiwa watu wote watakuwa sawa kweli, lakini uhakika wa mambo umethithibitisha kuwa yanayotendeka ni kinyume kabisa na maneno yao, kwani wao huwanyang'anya mali matajiri na kuwapa viongozi wa vyama vyao pamoja na vibaraka wao.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ãøóÇ ÃóÝóÇÁ Çááøóåõ Úóáóì ÑóÓõæáöåö ãöäú Ãóåúáö ÇáúÞõÑóì Ýóáöáøóåö æóáöáÑøóÓõæáö æóáöÐöí ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúíóÊóÇãóì æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÇÈúäö ÇáÓøóÈöíáö ßóíú áóÇ íóßõæäó ÏõæáóÉð Èóíúäó ÇáúÃóÛúäöíóÇÁ ãöäßõãú

"Mali aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili isiwe kinyang'anyiro baina ya matajiri wenu tu."

Al Hashar - 7

 

Mwenyezi Mungu katika aya hii anatujulisha kuwa jamaa na mayatima na masikini na wasafiri walioharibikiwa wana haki zao katika mali zetu, na anawakataza matajiri wasiifanye mali ikawa kinyang'anyiro baina yao tu na kusahau haki za wengine.

Muislam pia anatakiwa aitumie mali yake katika kuijenga akhera yake na kujitayarishia Pepo yake.

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÇÈúÊóÛö ÝöíãóÇ ÂÊóÇßó Çááøóåõ ÇáÏøóÇÑó ÇáÇÎöÑóÉó æóáóÇ ÊóäÓó äóÕöíÈóßó ãöäó ÇáÏøõäúíóÇ æóÃóÍúÓöä ßóãóÇ ÃóÍúÓóäó Çááøóåõ Åöáóíúßó æóáóÇ ÊóÈúÛö ÇáúÝóÓóÇÏó Ýöí ÇáÇóÑúÖö Åöäøó Çááøóåó áóÇ íõÍöÈøõ ÇáúãõÝúÓöÏöíäó

"Na utafute kwa yale aliyokupa Mwenyezi Mungu - makazi mazuri ya akhera, wala usisahau sehemu yako ya dunia, na ufanye wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia, wala usitafute kufanya ufisadi katika nchi, bila shaka Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi".

Al Qasas - 77

 

Haya ndiyo mafundisho ya Kiislam yaliyo kinyume kabisa na mafundisho ya mafisadi wanaojishughulisha na kukusanya mali tu na kurimbika, na wakati huo huo yanatufundisha kuwa Musilam hatakiwi abaki msikitini tu akifanya ibada bila kujishughulisha na elimu pamoja na kufanya biashara, na kuwaachia makafiri peke yao katika uwanja wa elimu na biashara na viwanda, na kwa ajili hiyo wanapata nguvu ya kututawala kiuchumi na kielimu, bali Muislam anatakiwa asiisahau pia sehemu yake ya dunia.

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóáÇ ÊóäÓó äóÕöíÈóßó ãöäó ÇáÏøõäúíóÇ æóÃóÍúÓöä ßóãóÇ ÃóÍúÓóäó Çááøóåõ Åöáóíúßó

"Wala usisahau sehemu yako ya dunia, na ufanye wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia".

Al Qasas - 77

 

Dini ya Kiislam inatutaka tuwe msitari wa mbele katika kutoa, na Mwenyezi Mungu amewaahidi kheri nyingi wale wanaotoa katika njia Yake.

Mwenyezi Mungu öAnasema:

ãøóËóáõ ÇáøóÐöíäó íõäÝöÞõæäó ÃóãúæóÇáóåõãú Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ßóãóËóáö ÍóÈøóÉò ÃóäÈóÊóÊú ÓóÈúÚó ÓóäóÇÈöáó Ýöí ßõáøö ÓõäÈõáóÉò ãøöÆóÉõ ÍóÈøóÉò æóÇááøåõ íõÖóÇÚöÝõ áöãóä íóÔóÇÁ æóÇááøåõ æóÇÓöÚñ Úóáöíãñ

"Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyotoa mashuke saba; ikawa katika kila shuke pana punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, (zaidi kuliko hivi), na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa mkubwa (na) Mwenye Kujua".

Al Baqarah - 261

 

Na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Hakika ya sadaka inazima ghadhabu ya Mola Mlezi na inamuondolea maiti adhabu"

Attirmidhiy

Na akasema:

"Haipiti asubuhi wanayoiamkia watu, ila Malaika wawili wanateremka. Mmoja wao anasema: "Mwenyezi Mungu muongezee mtoaji badala ya kile anachokitoa".Na mwengine anasema: "Mwenyezi Mungu mharibie mali yake (usiite baraka) aliyeacha kutoa ".

Muslim

Rudi juu

Aina za Sadaka

Sadaka haina maana ya kutoa pesa tu au kumsaidia mtu, bali Sadaka ziko aina nyingi sana.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Kila Muislam anatakiwa atoe Sadaka".

Wakasema:

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, asiyekuwa na mali (je)?"

Akasema:

"Afanye kazi kwa mikono yake, ajisaidie nafsi yake kisha atoe Sadaka".

Wakasema:

"Ikiwa hajapata?"

Akasema:

"Amsaidie mwenye shida".

Wakasema:

"Asipompata?"

Akasema:

"Afanye mema na aache shari, kwani akifanya hivyo anaandikiwa (thawabu ya) Sadaka".

Bukhari na wengineo

 

Na katika riwaya nyingnem amesema:

"Kila siku jua linapochomoza nafsi inaandikiwa juu ya kila inachotenda (katika thawabu ya) Sadaka. Katika hayo ni kuwapatanisha wawili wanaogombana (anaandikiwa mtu thawabu ya kutoa) Sadaka. Akimsaidia mtu kumnyanyua ili aweze kumpanda mnyama wake, anaandikiwa Sadaka, akimnyanyulia mzigo wake, Sadaka, kuondoa udhia barabarani, Sadaka, neno jema, Sadaka, na kila hatua anayokwenda msikitini Sadaka".

Ahmad na wengineo

 

Na akasema:

"Kati yenu kama yupo mwenye kuuogopa moto, basi atoe Sadaka walau kwa nusu ya tende, na asiyepata, basi kwa neno jema”.

Ahmad na Muslim

 

Na akasema:

"Siku ya Kiama Mwenyezi Mungu Atasema:

"Ewe mwanadamu, niliumwa (kwa nini) hukunitembelea?"

Atasema (mwanadamu):

"Ewe Mola Mlezi, vipi nitakutembelea na wewe ni Mola wa Ulimwengu?"

Atasema:

"Hukujuwa kuwa mja wangu fulani alikuwa akiumwa na hukumtembelea? Ama ungelimtembelea, ungelinikuta kwake. Ewe mwanadamu nimekuomba chakula na wewe hukunilisha?"

Atasema:

"Ewe Mola wangu, vipi nitakulisha na wewe ni Mola wa ulimwengu wote?"

Atasema:

"Hukujuwa kuwa fulani alikuomba chakula na hukumpa. Huelewe kuwa ungelimpa chakula, ungelikikuta kwangu?

Ewe mwanadamu, nilikuomba maji hukunipa".

Atasema:

"Ewe Mola wangu, vipi nitakunywesha nawe ni Mola wa Ulimwengu wote?'

Atasema:

"Mtu fulani alikuomba maji, na wewe hukumpa. Ama ungelimpa ungeyakuta hayo kwangu".

Muslim

 

Na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema pia:

"Mtu hapandi kitu au halimi kitu kisha mwanadamu akala katika mazao hayo au mnyama au chochote ila ataandikiwa kwa ajili yake Sadaka".

Ahmad na Attirmidhiy

 

Na akasema:

"Kila wema ni Sadaka, na katika wema ni kumkabili mwenzio kwa uso wa bashasha…(uso mkunjufu)."

Ahmad na Attirmidhiy

Rudi juu

Wenye kustahiki zaidi

Watu wako, mkeo na watoto wako pamoja na ndugu zako wa nasaba ndio wanaoistahiki zaidi sadaka yako.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mmoja wenu akiwa fakiri, basi ajitosheleze nafsi yake, kinachozidi awape watoto wake, kinachozidi, awape ndugu zake wa nasaba, na kikizidi basi atoe huku na kule".

Ahmad na Muslim

 

Hukumu ya Sadaka inahitilafiana na ya Zaka, kwani mali ya Zaka haijuzu kupewa asiyekuwa Muislam, lakini Sadaka anaweza kupewa asiyekuwa Muislam.

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóíõØúÚöãõæäó ÇáØøóÚóÇãó Úóáóì ÍõÈøöåö ãöÓúßöíäðÇ æóíóÊöíãðÇ æóÃóÓöíÑðÇ

"Na huwalisha chakula maskini na mayatima na wafungwa na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda".

Ad Dahar - 8

 

Neno lililotumika kwa 'wafungwa', katika aya hii ni 'Asiyran', na maana yake ni mateka wa kivita ambaye bila shaka ni kafiri aliyetekwa baada ya kupigana vita dhidi ya Waislam, lakini juu ya hivyo Mwenyezi Mungu anawasifia Waislam wanaowalisha chakula wafungwa hao.

Rudi juu

Kuiharibu sadaka

Haijuzu kumsimbulia au kumdharau anayepokea Sadaka kwa sababu kilichomfanya akubali kuipokea sadaka hiyo ni umasikini wake, na mtu kumtakabaria masikini ni dhambi kubwa sana, na anapofanya hivyo thawabu zake zinapotea bure.

Mwenyezi Mungu Anasema:

íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú áÇó ÊõÈúØöáõæÇú ÕóÏóÞóÇÊößõã ÈöÇáúãóäøö æóÇáÃÐóì ßóÇáøóÐöí íõäÝöÞõ ãóÇáóåõ ÑöÆóÇÁ ÇáäøóÇÓö æóáÇó íõÄúãöäõ ÈöÇááøåö æóÇáúíóæúãö ÇáÂÎöÑö

"Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho".

Al Baqarah – 264

Rudi juu

 

 

Kutowa katika mali ya haramu

Mwenyezi Mungu haikubali sadaka ikiwa inatokana na mali ya haramu. Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Enyi watu! Mwenyezi Mungu ni mzuri na hakubali isipokuwa kizuri tu".

 

Imesimuliwa kuwa siku moja mtu mmoja aliiba tufaa kisha akaliuza, na pesa alizopata akawagawia masikini.

Habari zilipomfikia kadhi wa mji huo, akamwita na kumuuliza:

"Kwa nini umeiba kisha ukazigawa sadaka pesa za mali ya wizi?"

Yule mtu akajibu:

"Kwa sababu Mwenyezi Mungu Anasema:

ãóä ÌóÇÁ ÈöÇáúÍóÓóäóÉö Ýóáóåõ ÚóÔúÑõ ÃóãúËóÇáöåóÇ æóãóä ÌóÇÁ ÈöÇáÓøóíøöÆóÉö ÝóáÇó íõÌúÒóì ÅöáÇøó ãöËúáóåóÇ

"Afanyae kitendo kizuri atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyae kitendo kibaya hatalipwa ila sawa nacho tu".

Al An am - 160

Kwa hivyo, akaendekelea kusema mtu Yule aliyeiba tufaa: ‘Kutokana na aya hii, mimi nilipoiba tufaa nilifanya kitendo kibaya nikalipwa dhambi moja tu sawa na tufaa moja nililoiba, lakini nilipowagawia masikini nilifanya kitendo chema nikalipwa mara kumi, na thawabu 10 nilizozipata kwa kuligawa tufaa lile,ukitoa ile dhambi moja ya kuiba, nitabakiwa na thawabu tisa"

Kadhi akamwambia:

"Lakini umesahau jambo moja ewe ndugu Muislam, (Mwenyezi Mungu ni mwema, na hakubali isipokuwa chema tu).”

Rudi juu

Kuwasaidia wanyama

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alisema kuwaambia Masahaba (Radhiya Llahu anhum):

"Mtu mmoja aliyekuwa akitembea, alishikwa na kiu, akaona kisima mbele yake, akateremka na kunywa maji ndani yake kisha akatoka. Alipokuwa akitoka alimuona mbwa akihema kwa kiu. Yule mtu akasema; "Bila shaka mbwa huyu ameshikwa na kiu kama nilivyoshikwa mimi. Akateremka (tena) kisimani, akajaza maji kiatu chake, kisha akamshika kichwa chake mbwa yule na kumnywesha.

Akashukuriwa na Mwenyezi Mungu na kughufuriwa".

Masahaba (Radhiya Llahu anhu) wakasema:

"Hata katika wanyama tunapata thawabu?"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Katika kila chenye uhai mna thawabu".

Bukhari

Sadakatuh jaariyah

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mwanadamu anapokufa, amali zake zote zinakatika isipokuwa tatu. Sadakatun jaariah (Sadaka inayoendela), au elimu yenye kunufaisha watu, au mtoto mwema anayemuombea".

Ahmad na Muslim

Rudi juu

 

Kushukuru

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Atakayekufanyieni wema mlipeni, na ikiwa hamna cha kumlipa, basi muombeeni dua mpaka muhisi kuwa mumemlipa".

Abu Daud na Annasai

 

Imesimuliwa na Imam Ahmad kutoka kwa Al Ash-ath bin Qays kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Hamshukuru Mwenyezi Mungu yule aisyewashukuru watu."

Ahmad

 

Na akasema:

"Alieyetendewa jema, akasema kumwambia aliyemtendea: “Jazaaka Llahu khayran', (MwenyeziMungu akujaze kheri), huyo amekwisha shukuru kama inavyotakikana".

Rudi juu

Wanaostahiki Zaka

Sadaka ya kawaida, anapewa mtu yeyote hata akiwa si Muislam, ama Zakatul Fitri wanapewa watu wa aina mbili tu, nao ni masikini na mafakiri Waislam.

Zakatul Maal (Zaka ya mali), hii wanapewa aina 8 tu ya Waislamu waliowataja na Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu Aliposema:

ÅöäøóãóÇ ÇáÕøóÏóÞóÇÊõ áöáúÝõÞóÑóÇÁ æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÇáúÚóÇãöáöíäó ÚóáóíúåóÇ æóÇáúãõÄóáøóÝóÉö ÞõáõæÈõåõãú æóÝöí ÇáÑøöÞóÇÈö æóÇáúÛóÇÑöãöíäó æóÝöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóÇÈúäö ÇáÓøóÈöíáö ÝóÑöíÖóÉð ãøöäó Çááøåö æóÇááøåõ Úóáöíãñ Íóßöíãñ

"Sadaka hupewa (watu hawa):-

·        Mafakiri na

·        Masikini na

·        Wanaozitumikia na

·        Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislam) na

·        Katika kuwapa uungwana watumwa na

·        Katika kuwasaidia Wenye deni na

·        Katika (kutengeneza) Mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na

·        Katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa).

Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".

At Tawaba - 60.

 

Ayakayeichunguza aya hii ataona kuwa Mwenyezi Mungu ametumia neno 'Lil' katika kuwataja watu aina nne wa mwanzo wanaostahiki kupewa Zaka. Na hii inaitwa Laam ya tamliyk, na maana yake ni kuwa lazima kuwamilikisha watu wa aina nne wa mwanzo (yaani kuwapa mikononi mwao) Zaka yao.

Mwenyezi Mungu öAnasema:

ÅöäøóãóÇ ÇáÕøóÏóÞóÇÊõ áöáúÝõÞóÑóÇÁ æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÇáúÚóÇãöáöíäó ÚóáóíúåóÇ æóÇáúãõÄóáøóÝóÉö ÞõáõæÈõåõãú

Ama katika aina nne waliobaki, Mwenyezi Mungu ametumia neno 'Fiy'. Na kwa kutumia neno hilo Mwenyezi Mungu hatulazimishi, kuwamilikisha kwa kuwapa Zaka yao mikononi mwao.

Mwenyezi Mungu anasema:

æóÝöí ÇáÑøöÞóÇÈö æóÇáúÛóÇÑöãöíäó æóÝöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóÇÈúäö ÇáÓøóÈöíáö

Kwa hivyo katika aina nne za mwisho, kwa mfano kama unataka kumsaidia mwenye deni, hulazimiki kumpa pesa hizo mkononi mwake, bali unaweza kwenda kumlipia deni hilo moja kwa moja bila ya kumkabidhi mdaiwa huyo pesa hizo mkononi mwake. Hata hivyo, ukitaka unaweza pia kumkabidhi mweyewe mkononi mwake.

Ukitaka kuzitumia pesa za Zaka katika njia ya Mwenyezi Mungu, unaweza kununua kwa mfano silaha na kuwakabidhi wapiganaji 'Mujahidiin' au unaweza kuzitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu bila ya kumkabidhi mtu pesa hizo mkononi mwake, wakati huo huo unaweza ukitaka kuwakabidhi wanaohusika au wajuzi ili ipate kutumika kwa usahihi zaidi.

 Rudi juu

Mafakiri masikini

Juu ya kuwa watu wamehitalifiana juu ya nani masikini na nani fakiri, lakini kwa ujumla hawa ni watu ambao wanachokipata hakiwatoshi katika matumizi yao ya kila siku.

Mtu anaweza kuwa masikini hata kama anapata mshahara mkubwa lakini wakati huo huo ana watoto wengi au wazee na ndugu wanaomtegemea anaowajibika kuwatizama, au ana madeni kiasi ambapo juu ya kuwa anapata mshahara mkubwa, pesa hizo hazimtoshi kuwalisha watu wake hao.

Kwa ajili hiyo juu ya tofauti iliyopo baina ya masikini na fakiri katika sharhi yake, lakini katika kuhitajia kwao msaada, wote wawili wapo katika hali moja.

Zipo hadithi zinazotujulisha kuwa wapo baadhi ya masikini wenye kustahi kuombaomba juu ya shida kubwa walokuwa nazo. Waislam wanatakiwa wawachunguze watu wa aina hii na kuwasaidia na wasiwaache mpaka hali zao zikawa mbaya.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anasema:

"Masikini si yule anayeomba akapewa tende moja au mbili akaondoka, au tonge moja au mbili, lakini masikini wa kweli ni yule anayejizuwia. Someni mkitaka (kauli ya Mwenyezi Mung isemayo):

ÇáÊøóÚóÝøõÝö ÊóÚúÑöÝõåõã ÈöÓöíãóÇåõãú áÇó íóÓúÃóáõæäó ÇáäøóÇÓó ÅöáúÍóÇÝðÇ

"Utawafahamu kwa alama zao hawawaombi watu wakafanya ung'ang'anizi".

 

Anayepewa Zaka ni Masikini au Fakiri Muislam tu, ama Masikini au Fakiri asiyekuwa Muislam hapewi katika mali ya Zaka, na kama Fakiri asiyekuwa Muislam atahitajia msaada, basi atapewa katika mali ya Sadaka na si ya Zaka.

Rudi juu

Wenye kuzitumikia

Wanaozitumikia Zaka ni wale waliopewa jukumu la kuipokea, kuikusanya kutoka kwa matajiri na wenye kazi ya kuihifadhi, waandishi, na wenye kuigawa, wakiwemo wachungaji wa wanyama wa Zaka.

Ili waweze kupewa katika Mali ya Zaka, watu hao lazima wawe Waislam, na wasiwe katika wale walioharamishwa kupokea Zaka katika watu wa Ahlul Bayt ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika Banu Abdul Muttalib ambao tutawataja baadaye.

Katika wanaoitumikia Zaka, hata akiwa mtu tajiri basi anastahiki kupewa katika mali hiyo, na ikiwa mtu wa aina hiyo amepewa na wakubwa wanaohusika na akawa hana haja nayo mali hiyo, basi aichukuwe na kuwagawia anaowataka au kumnunulia zawadi anayemtaka.

Imepokelewa kuwa Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alipokuwa akifanya kazi ya kukusanya mali ya Zaka, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimpa katika mali hiyo.

Umar (Radhiya Llahu anhu) akasema:

"Mimi najitolea tu na sina haja ya kulipwa, mpe mwenye kuzihitajia zaidi kuliko mimi".

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

"Alichokupa Mwenyezi Mungu katika mali hii bila ya wewe mwenyewe kuiomba, uichukuwe na uitumie au itolee Sadaka."

Bukhari na Annasai

Rudi juu

Wenye kutiwa nguvu

Hawa ni watu wanaopewa katika mali ya Zaka kwa ajili ya kulainishwa nyoyo zao na kutiwa nguvu kutokana na udhaifu wa nyoyo hizo, na wengine hupewa kwa ajili ya kuwaepusha Waislam na shari zao, au kuwavutia katika kuupenda Uislam na kuupa nguvu.

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwapa wakubwa wa makabila ya kiarabu na hasa makabila ya kibedui kwa ajili ya kuwapendekeza katika Uislam.

Imepokelewa kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimpa mtu mmoja aitwae Safwan bin Umayyah ngamia wengi sana katika ngamia wa ngawira waliopatikana katika vita vya Hunain, na Safwan huyu alikuwa mkubwa wa kabila lake.

Safwan alikuwa wakati huo bado hajasilimu, na alipopewa mali hiyo, akarudi kwa watu wake na kuwaambia:

"Enyi watu wangu, ingieni katika dini ya Kiislam, kwani Muhammad anatoa utoaji wa mtu asiyeogopa ufakiri".

(Mwenye kuchunguza, ataona kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwatendea makabila ya Kibedui tofauti na anavyowatendea watu wa mijini. Alikuwa akiwachukulia kwa akili zao. Na hii ni kwa sababu Mabedui ni watu wagumu sana kufahamu. Hata katika kuuliza masuali, Mabedui walikuwa wakimuuliza Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) masuali na kujibiwa, wakati masuali hayo hayo wangeuliza Masahaba wanaokaa mjini (Radhiya Llahu anhum), basi Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) angekasirika nayo masuali hayo).

 

Wakati wa ukhalifa wake Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alikuwa akiendelea kuwapa watu wa aina hii, lakini Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) siku moja alikataa kutoa, akawaambia:

"Hii Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akikupeni kwa ajili ya kuzizowesha nyoyo zenu na kuzilainisha, lakini sasa Mwenyezi Mungu amekwishautukuza Uislam na hatuna haja nanyi tena, mkitaka ingieni katika Uislam, na kama hamtaki basi baina yetu na baina yenu ni panga. Mwenyezi Mungu amesema:

æóÞõáö ÇáúÍóÞøõ ãöä ÑøóÈøößõãú Ýóãóä ÔóÇÁ ÝóáúíõÄúãöä æóãóä ÔóÇÁ ÝóáúíóßúÝõÑú

"Na sema; 'Huu ni ukweli ulotoka kwa Mola wenu, basi anayetaka na aamini na anayetaka na akufuru.”

Al Kahf - 29

 

Anasema Sayed Sabeq katika Fiqhis Sunnah:

"Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alikubaliana na Umar (Radhiya Llahu anhu) katika uamuzi wake huo, na hapana hata Sahaba mmoja (Radhiya Llahu anhum) aliyepinga. Na hii ni katika Ijtihadi zake Umar (Radhiya Llahu anhu), na hata makhalifa waliokuja baada yake, Uthmaan na Aliy (Radhiya llahu anhum) hawakuwapa tena watu wa aina hii katika mali ya Zaka.

Hata hivyo," anaendela kusema Sh. Sabeq, "hii haimaanishi kuwa watu wa aina hii wasipewe, na Imam yeyote yule atakayetawala na akaona kuwa ipo haja ya kuwapa watu wa aina hii, basi atawapa kwa sababu dalili ipo katika Qurani na Sunnah.”

Rudi juu

Katika kugomboa

Uislam umeijaalia ibada hii ya kuwagomboa mateka na watumwa kuwa ni kitendo kinachompatia mtu thawabu nyingi sana na kumuingiza katika Pepo za Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Kutoka kwa Al Barra-a (Radhiya Llahu anhu) amesema:

"Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kumwambia:

"Nijulishe juu ya amali (njema) itakayonikurubisha na Pepo na kunibaidisha na Moto".

Akasema:

"Waachie huru watu na wagomboe watumwa".

Akauliza (tena):

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, si yote hayo yanabeba maana moja tu?"

Akasema:

"La, (sivyo), 'kuwaachia huru' ni kujihusisha peke yako katika kuwaacha huru, na 'kuwagomboa' ni kusaidia katika kulipa thamani ya kuwagomboa".

Ahmed na Addaraqutniy.

 

Wakati ule ilikuwa mtumwa anaweza kuandikiana na kukubaliana kuwa atakapoweza kulipa malipo fulani katika muda fulani, ataachwa huru. Kwa hivyo Waislam walitakiwa wawasaidie watu wa aina hiyo kwa kuwalipia kiasi hicho ili waweze kujigomboa.

Rudi juu

Kumsaidia mwenye deni

Hawa ni wale wenye madeni makubwa wakashindwa kuyalipa kutokana na kula hasara katika biashara zao nk. Sharti madeni hayo yawe katika mambo ya halali au yatokane na maasi aliyotubu nayo mtu huyo.

 

Imepokelewa kutoka kwa Maimam Ahmad na Abu Daud na Ibni Majah na Attirmidhiy, kutoka kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alisema:

"Mas-ala (ya kuwasaidia wenye madeni), hayawi halali isipokuwa katika mambo matatu; aliye fakiri sana, au mwenye deni zito sana, au mwenye kudaiwa damu (ya diya - fidiya).”

(Huyu ni mtu aliyejikuta amebebeshwa deni la diya kutokana na ndugu yake au jamaa yake aliyeuwa kwa bahati mbaya. Ikiwa hajalipa diya hiyo, basi ndugu yake huyo au jamaa yake atauliwa kwa ajili ya kulipa kisasi)

Rudi juu

Katika kutengeneza

(Fiy sabiyli Llah), ni njia yoyote ile inayomfikisha mtu katika kumpatia radhi za Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, juu ya kuwa maulamaa wengi wanasema kuwa haya ni mambo yanayohusiana na vita vya Jihadi tu pamoja na watu wanaopigana vita hivyo.

Hawa wana sehemu yao katika mali ya Zaka wanayopewa hata kama askari mpiganaji Jihadi ni tajiri anayejiweza.

Anasema Sayed Sabeq, katika Fiqhis Sunnah:

"Maulamaa wengine wamesema kuwa inajuzu kuzitumia pesa hizo katika kutengeneza njia inayowapeleka watu Makka kwa ajili ya Hija na katika kuwanunulia maji ya kunywa na chakula ikiwa hapana mali nyingine inayoweza kutumiwa katika kazi hiyo. Inajuzu pia kuzitumia katika kuwasomesha na kuwatayarisha walinganiaji wa dini kwa ajili ya kuwapeleka katika nchi zisizokuwa za Kiislam kwa ajili ya kufanya da-awa nk."

 

Vitu vinavyonunuliwa kutokana na pesa za Zaka kwa ajili ya vita, kama vile farasi, panga, nk. lazima virudishwe katika nyumba ya hazina ya Waislam (Baytul maal) baada ya kumalizika kwa vita.

Katika kupewa wasafiri

Msafiri aliyeishiwa na pesa akawa hana njia nyingine ya kupata pesa za matumizi, huyu anapewa katika mali ya Zaka, sharti safari yake hiyo iwe katika mambo ya twa-a na si katika kumuasi Mola wake, hata akiwa msafiri huyo huko kwao alikotoka ni mtu tajiri mwenye mali nyingi.

Rudi juu

Walioharimishwa kupewa

1.   Kafiri

Katika hadithi iliyotangulia, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Zichukuliwe kutoka kwa matajiri Wao na kurejeshewa masikini Wao"

Na maana yake ni kuwa:-

Zichukuliwe kutoka kwa matajiri wa Kiislam na kupewa masikini wa Kiislam.

 

2.   Bani Hashim

Nao ni watoto wa Aliy na Aqiyl na Jaafar na Al Abbas na Al Harith (Radhiyallahu anhum).

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Sadaka haijuzu kupewa kwa watu wa Muhammad".

Muslim

 

Maulamaa wamekhatalifiana juu ya ukoo wa Bani Al Muttalib, iwapo nao pia hawapewi katika mali ya Zaka au wanapewa.

Imam Shafi amesema kuwa hawa nao wasipewe katika mali ya Zaka, na hii inatokana na hadithi iliyotolewa na Imam Shafi na Imam Ahmad na Imam Bukhari kutoka kwa Jubair bin Mut-am aliposema:

"Siku ya Khaibar (baada ya kumalizika vita hivyo), Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliikusanya upande mmoja sehemu ya ngawira ya watu wa ukoo wake katika Bani Hashim na ya Bani Al Muttalib na akawaacha (watu wa kabila lake) katika Bani Nofel na Bani Abdu Shams. Tukamwendea mimi na Uthman bin Affan na kumuuliza:

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hawa ni Bani Hashim na sisi hatukanushi fadhila zao kutokana daraja yako mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini vipi hawa ndugu zetu katika Bani Al Muttalib, umewaingiza wao ukatuacha sisi wakati nasaba yao na yetu juu yako ni sawa sawa?"

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Sisi na Bani Muttalib hatujafarikiana katika ujahilia wala katika Uislam, bali sisi na wao ni kitu kimoja". Akaviingiza vidole vyake vya mkono wa kulia ndani ya vidole vya mkono wa kushoto na kuvichanganya."

 

Kutokana na ushahidi huu, baadhi ya maulamaa wakasema;

'Bani Muttalib nao pia wanaingia katika kuharamishiwa kupewa katika Mali ya Zaka".

 

3.   Baba na watoto

Haijuzu mtu kumpa katika mali ya Zaka baba yake, mama yake, watoto wake na babu zake, na hii ni kwa sababu mtoaji Zaka anawajibika kuwatizama watu hao na kuwapa katika mali yake, na kwa ajili hiyo, watu hao wanalazimika kuwa matajiri kutokana na utajiri wake.

 

4.   Mke

Haijuzu mtu kumpa mkewe katika mali ya Zaka, na jambo hili linakubaliwa na maulamaa wote na hii ni kwa sababu mtu anawajibika kumtizama na kumpa mkewe katika mali yake kama anavyowajibika kuwapa wazee wake wawili akiwa anao uwezo huo.

Anasema Ibnil Mundhir:

"Isipokuwa kama mke ana deni, basi hupewa Zaka katika ile sehemu ya kuwasaidia wenye madeni kwa ajili ya kulipa deni hilo".

Ama ikiwa mke ni tajiri mwenye uwezo wa kutoa Zaka, basi yeye anarushusiwa kumpa mumewe katika mali ya Zaka kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema:

"Amesema kweli Ibni Masaud, mumeo na mwanao wanastahiki zaidi kuwapa Sadaka".

Bukhari

 

5.   Haijuzu kuitumia mali ya Zaka kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kama vile kujenga misikiti, kununua misahafu, kununua vifaa vya kusaidia kuosha maiti nk. Na hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu kwa hekima yake keshazitaja na kuzisherehesha njia za kutoka Zaka katika aya iliyotangulia ya Surat At Tawba -60, na akaikamilisha aya hiyo kwa kusema;

 

"Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".

Rudi juu

Watu wema

Zaka anapewa Muislam anayeistahiki akiwa Muislam huyo ni mtu mwema au mtu asi, isipokuwa mtu asi hapewi kaika mali ya Zaka ikiwa itajulikana kwa uhakika kuwa atakuja kuitumia mali hiyo katika kuuendeleza uasi wake.

Ikijulikana kwa uhakika kuwa ataitumia mali hiyo katika kumuasi Mwenyezi Mungu, basi mtu huyo atanyimwa, ama ikiwa hayajulikani hayo, au ikijulikana kuwa ataitumia mali hiyo katika shida zake, basi hapo atapewa.

Hata hivyo ni bora kwa mtoaji Zaka aihusishe mali hiyo kwa kuwapa watu wema au maulamaa wanaostahiki wanaoifayia kazi elimu yao, kwani Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Walisheni chakula chenu wachaMungu na mnaowajuwa katika walioamini (kweli)".

Ahmad

 

Anasema Ibni Taymiya:

"Asiyeswali hapewi katika mali ya Zaka mpaka pale atakapotubu akawa anaswali."

 

Anasema Sayed Sabeq:

"Katika kundi hilo wanaingia pia wale wanaomuasi Mwenyezi Mungu bila kujali wala kuona haya, na kuendelea kuzama katika maasi huku nyoyo zao zikiwa zishafisidika na dhamiri zao zimekwisha haribika".

 

Hawa hawapewi katika mali ya Zaka isipokuwa kama Zaka hiyo itawasaidia katika kuwaongoza mwongozo ulio sahihi au itawasaidia katika kutoka hali yao hiyo.

Rudi juu

Kuinunua Zaka

Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amekataza mtu kuinunua Zaka yake.

Kutoka kwa Abdillahi bin Umar (Radhiya Llahu anhu), amesema:

"Umar (Radhiya Llahu anhu) alimtoa farasi wake Sadaka fiy sabiyli Llah, kisha akamkuta farasi huyo anauzwa na akataka kumnunua. Akamuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) juu ya jambo hilo, akamwambia:

"Usimnunue na wala usirudie (kutaka kuimiliki tena) Sadaka yako"

Bukhari, Muslim na wengineo

 

Baadhi ya maulamaa wakasema kuwa kukataza huko ni kwa ajili ya kujiepusha tu, na si kwa ajili ya kuharamisha, wakiegemea hadithi nyingine inayoruhusu mtu kuipokea sadaka yake kama zawadi itokayo kwa masikini aliyempa.

Rudi juu

Kuisafirisha Zaka

Mulamaa wengi wamekubali kuwa mali ya Zaka (Zakatul Maal - si Zakatul Fitr) inaweza kusafirishwa na kutolewa katika nchi nyingine kwa wanaoistahiki zaidi ikiwa watu wa mji anaoishi mtoaji hawaihitajii zaidi mali hiyo. Ama ikiwa katika nchi hiyo wapo wanaoihitajia, basi zipo hadithi zinazotujulisha kuwa Zaka ya kila nchi wanapewa masikini wake.

Katika madhehebu ya Imam Abu Hanifa, wao wanasema:

"Ni Makruh kuisafirisha mali ya Zaka isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kumsaidia ndugu wa nasaba mwenye kuihitajia, na hii inatokana na umuhimu wa kuunganisha undugu huo, au pia kwa ajili ya watu wenye shida sana katika watu wa nchi yake, au kwa ajili ya kuiondoa kutoka nchi ya kikafiri na kuipeleka katika nchi ya kiislam."

 

Madhehebu ya Imam Shafi yanasema:

"Haijuzu kuisafirisha mali ya Zaka na inawajibika kutolewa katika nchi iliyochumwa mali hiyo isipokuwa pakikosekana wenye kuihitajia Zaka hiyo katika nchi hiyo".

 

Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) alipewa ugavana wa nchi ya Yemen na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na alipotawala Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alimuacha Muadh aendelea kuwa gavana wa nchi hiyo. Lakini Muadh (Radhiya Llahu anhu) alipompelekea Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) theluthi ya mali ya Zaka, Umar (Radhiya Llahu anhu) alikataa kuzipokea akamwambia:

"Sikukupeleka uwe mchotaji (wa mali) wala mpokeaji wa kodi, bali nimekupeleka kwa ajili ya kuchukua mali (ya Zaka) kutoka kwa matajiri wao na kuzirudisha kwa masikini wao".

Muadh (Radhiya Llahu anhu) akasema:

"Nisingekuletea ila kwa sababu sikumpata (masikini) anayezistahiki kuzichukua".

Rudi juu

Kuidhihirisha Zaka

Inazuju kwa mtoaji kuidhihirisha au kuitoa kwa siri Zaka yake, yote sawa ikiwa anachokitowa ni Sadaka ya kawaida au Zaka ya mali, ingawaje kuitoa kwa siri ni bora zaidi.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Åöä ÊõÈúÏõæÇú ÇáÕøóÏóÞóÇÊö ÝóäöÚöãøóÇ åöíó æóÅöä ÊõÎúÝõæåóÇ æóÊõÄúÊõæåóÇ ÇáúÝõÞóÑóÇÁ Ýóåõæó ÎóíúÑñ áøõßõãú

"Kama mkitoa sadaka kwa dhahiri ni vizuri, na kama mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri, basi huo ni ubora zaidi kwenu".

Al Baqarah - 271