Suali;

Aslam aleykum kuna swali linanitaza ninaomba ufafanuzi.

Mimi ninaishi marekani ya kaskazini. Ninapokwenda msikitini baada kumaliza kutia udhu kutokana na baridi kali ya marekani inanibidi tujifute maji ya udhu.

Je kidini inakubalika kuufuta udhu naomba jibu

 

Majibu;

Anasema Imam Annawawiy kuwa ipo khitilafu baina ya maulamaa katika Masaala ya kupangusa maji baada ya kutia udhu. Wapo wanaosema kuwa ni Makruh na wapo wanaosema kuwa Inajuzu na hapana ubaya wowote., lakini hapana anayesema kuwa kupangusa  kunavunja udhu juu ya kuwa maulamaa wengi wanaona kuwa hapana ubaya wowote katika kupangusa.

Wanaosema kuwa ni Makruh, dalili yao ni ile hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) siku ile alipoletewa kitambaa na Bibi Maymuna (RA) kwa ajili ya kujipangusia nacho maji baada ya kutawadha,  na Mtume (SAW) akakirudisha kitambaa kile bila kujipangusia nacho

Wanasema kuwa kwa vile Mtume (SAW) hakujipangusa, hii ni dalili kuwa kuacha kujipangusa ni bora kuliko kujipangusa, wakati huo huo ingekuwa haijuzu kujipangusa basi Mtume (SAW) lazima angewajulisha juu ya hilo.

Na hii ndiyo hoja waliyonayo wengi miongoni mwa maulamaa kuwa hapana ubaya kujipangusa maji baada ya kutawadha, hasa panapo udhuru kama vile baridi nk..

Wallahu taala aalam

Wassalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh