KHALID NA HAYDAR
Kumlilia Al
Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)
Ziara ya
kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu)
Kwa nini Abu
Hurairah (Radhiya Llahu anhu)?
Kimeandikwa na Abdullah Abdul Rahman Al Raashid
Kimefasiriwa na Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Hakika shukrani zote anazistahiki
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, tunamuomba
atusaidie katika shida zetu, atusamehe madhambi yetu, atukinge na shari za
nafsi zetu na shari za amali zetu ovu.
Swala na
salamu zimfikie yule aliyeletwa akiwa ni rehma kwa walimwengu wote,
aliyeufikisha ujumbe, akaiwasilisha amana, akawanasihi umma, na akapigana
jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki. Mola wetu mtukufu
tunakuomba umswalie na umsalimie Mtume wako huyu
pamoja na Aali zake na Sahaba zake wakarimu.
Yule atakaye Mwenyezi Mungu
kumuongoza basi hapana wa kumpoteza, na anayeachiwa
basi hana wa kumuonoza. Ninakiri kuwa hapana apasaye kuabudiwa isipokuwa
Mwenyezi Mungu Asiye na mshirika, na ninakiri kwamba
Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni Mtume wake wa mwisho na mjumbe wake
wa mwisho.
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala Anasema:
æóãóÇ ÂÊóÇßõãõ ÇáÑøóÓõæáõ ÝóÎõÐõæåõ æóãóÇ äóåóÇßõãú Úóäúåõ
ÝóÇäÊóåõæÇ æóÇÊøóÞõæÇ Çááøóåó Åöäøó Çááøóåó ÔóÏöíÏõ ÇáúÚöÞóÇÈö
“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho
kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi
Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.”
Al Hashr – 7
Na Akasema:
áóÞóÏú
ßóÇäó áóßõãú Ýöí ÑóÓõæáö Çááøóåö ÃõÓúæóÉñ ÍóÓóäóÉñ áøöãóä ßóÇäó íóÑúÌõæ Çááøóåó
æóÇáúíóæúãó ÇáúÂÎöÑó æóÐóßóÑó Çááøóåó ßóËöíÑðÇ
“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema
(mfano mwema wa kuufuata) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu
kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi
Mungu sana.”
Al Ahzab – 21
Na Akasema:
åõæó
ÇáøóÐöí ÃóÑúÓóáó ÑóÓõæáóåõ ÈöÇáúåõÏóì æóÏöíäö ÇáúÍóÞøö áöíõÙúåöÑóåõ Úóáóì
ÇáÏøöíäö ßõáøöåö æóßóÝóì ÈöÇááøóåö ÔóåöíÏðÇ
“Yeye ndiye aliyemtuma
Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze
juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.”
Al Fath – 28
Na ökasema:
ÝóÐóáößõãõ
Çááøåõ ÑóÈøõßõãõ ÇáúÍóÞøõ ÝóãóÇÐóÇ ÈóÚúÏó ÇáúÍóÞøö ÅöáÇøó ÇáÖøóáÇóáõ ÝóÃóäøóì
ÊõÕúÑóÝõæäó
“Basi
huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya
haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa?”
Yunus
- 32
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika ya ukweli unaongoza katika wema, na wema unaongoza Peponi. Na mtu huwa anapenda kusema kweli na anahakikisha kuwa kila asemalo ni la kweli, mpaka
anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msemakweli.
Na hakika ya uongo unaongoza katika uovu, na uovu unaongoza Motoni. Na mtu huwa
anapenda kusema uongo na anahakikisha kuwa kila asemalo anatia uongo ndani yake,
mpaka anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni (mtu) muongo”.
Bukhari na Muslim
Kutokana na aya na
hadithi zilizotangulia, tunafahamu kuwa Muislamu wa kweli ni yule ambaye mara
anapotambua kuwa itikadi aliyo nayo inakwenda kinyume na mafundisho ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) basi huiacha mara moja bila
kubishana na bila kutafuta visingizio, na hakubali kufuata ila yale tu
aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
aliyetumwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala kwa uongofu na Dini ya Haki.
Na Muislamu wa
kweli anayeitaka Pepo ya Mola wake hakubali kufuata yale aliyoyakuta ndani ya
vitabu visivyo na ushahidi wowote wa kielimu ndani yake, vitabu vilivyojaa
hadithi za uongo, visivyokuwa na wapokezi wanaojulikana (narrators).
Ukweli siku zote uko wazi na hauhitajii kupambwa kwa falsafa, lakini uongo, ndio wenye
kujificha na unahitajia kupambwa sana ili uweze kubabaisha.
Elimu ya kweli ni ile
yenye kauli za; “Mwenyezi Mungu Amesema,”au
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema”.
(ÞÇá Çááå æÞÇá ÇáÑÓæá)
Muislamu ni
mtu mwenye hekima, na hawezi kukubali kila anachotupiwa masikoni mwake bila
kupima na kutumia akili, kwani anajua vizuri kuwa dini hii ni dini ya haki, na
kwamba Siku ya Kiama atakuja kuulizwa juu ya kila alichotenda.
Mwenye akili timamu ataona kuwa
ndani ya vitabu vya Shia mna maelfu kwa maelfu ya
hadithi Maudhui walizosingiziwa watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa wamesema, lakini ukweli ni kuwa
hadithi hizo zimepachikwa tu na watu wasiopenda kuuona Umoja wa Kiislamu
ukisonga mbele.
Anayetaka kujadiliana kwa nia ya kuupata ukweli, basi lazima aondoe inadi na siku
zote sikio lake liwe wazi, na mara anapouna ukweli basi aufuate, na asiwe kama
wale waliosema:
Èóáú ÞóÇáõæÇ ÅöäøóÇ æóÌóÏúäóÇ
ÂÈóÇÁäóÇ Úóáóì ÃõãøóÉò æóÅöäøóÇ Úóáóì ÂËóÇÑöåöã ãøõåúÊóÏõæäó
“Hakika
sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo
zao.”
Al Zukhruff – 22
Bali awe katika wale wanaosema:
Þõáú
åóÜÐöåö ÓóÈöíáöí ÃóÏúÚõæ Åöáóì Çááøåö Úóáóì ÈóÕöíÑóÉò ÃóäóÇú æóãóäö ÇÊøóÈóÚóäöí
æóÓõÈúÍóÇäó Çááøåö æóãóÇ ÃóäóÇú ãöäó ÇáúãõÔúÑößöíäó
“Sema: Hii ndiyo Njia
yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua -
mimi na wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika
washirikina.”
Yusuf – 108
Na asiutie kufuli moyo wake hata
ikamsibu kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
Ãóãú Úóáóì ÞõáõæÈò ÃóÞúÝóÇáõåóÇ
“Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?”
Muhammad – 24
Kwa hivyo anayetaka kujadili
kikweli kwa nia ya kuutafuta ukweli na si kufanya inadi tu, basi huyo anaingia
katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo;
æóÅä íóßõä áåõãõ ÇáúÍóÞøõ íóÃÊõæÇ Åöáóíúå ãõÐúÚöäöíäó
“Na ikiwa haki
ni yao, wanamjia kwa kut'ii.”
An Nur – 49
Ukweli unapatikana katika
kufuata hadithi zilizosihi isnadi zake, ama hadithi zisizosihi isnadi hata ziwe
zimeandikwa na mtu mtukufu wa aina gani, hizo haziwezi kuwa na nuru ya kuongoza
kuelekea Peponi, kwani hapana kiumbe mwenye kauli tukufu kuliko Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Kwa hivyo hadithi iliyosihi
isnadi lazima ifuatwe, ama kauli zisizo na isnadi wala msingi, na zile zisizo
na uhakika, lazima ziachwe mara ukweli unapodhihirika.
Tutaandika makala haya kwa
njia ya majadiliano matulivu baina ya Khalid na Haydar.
Khalid: Assalaam
alykum wa Rahmatullahi wa barakatuh. karibu ewe
Haydar: Wa alaykumu
ssalaam ewe ndugu Khalid
Khalid: Unaonekana
kama kwamba una tatizo?
Haydar: Ndiyo, na
yareti jambo lenyewe lingekuwa jepesi, lakini inaelekea ni gumu sana na
sitoweza kulitatua.
Khalid: Ni jambo gani tena hilo ewe Haydar?
Haydar: Hii khitilafu
iliyopo baina ya Mashia na Masunni kwa kweli inautia dhiki moyo wangu.
Khalid: Kweli
ndugu yangu, unaonaje tukajadiliana juu ya jambo hili muhimu kwa utulivu ili
tuweze kuzifahamu vizuri fikra na itikadi za Mashia na Masunni huenda tukaweza
kuzikaribisha fikra zetu.
Haydar: Maneno yako ni ya kweli. Jambo hili ni muhimu sana, bora tujadiliane juu ya maudhui haya lakini
kwa utulivu kama ulivyosema, huenda tukafanikiwa kuzifanya pande mbili hizi
ziwe karibu zaidi.
Khalid: Vizuri, unaonaje basi tukajadiliana
juu ya zile kadhia muhimu za Madhehebu mawili haya ili
huenda tukaweza kupanua fikra zetu juu ya itikadi za Masunni na Mashia kwa nia
ya kutaka kuzifanya ziwe karibu zaidi.
Haydar: Sawa, jambo hili ni muhimu sana, kwa hivyo
tuanze kujadiliana.
Khalid: Nakuomba usikasirike tu, kwani itabidi
kuzungumza juu ya kadhia zote kwa uwazi bila kuficha. Kwa hivyo ikiwa umekubali basi nakuomba uanze wewe kuzungumza.
Haydar: Kwa vile kusudi letu ni kuitafuta haki, mimi
sitokasirika. Kwa hivyo tuanze tokea pale Ushia ulipoanza, na ni jambo
linalojulikana na kila Muislamu kuwa Umeanza tokea siku ile Muhammad (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alipoanza kuwalingania watu katika Uislamu, isipokuwa
baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kufariki dunia
Masahaba hawakuupa umuhimu Uimamu wala ule Usia alouacha Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Khalid: Umuhimu
wa Uimamu umeanza kabla ya hapo unaposema wewe, na zamani kuliko unavyodhania,
kwani Maulamaa wa Kishia wameandika ndani ya vitabu vyao kuwa Uimamu ulikuwa
ukijulikana na Mitume yote, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha ‘Usul al Kafi’
(437/1) kutoka kwa Abu Hassan kuwa amesema;
“Uimamu umeandikwa
ndani ya vitabu vya Mitume yote. Hakuletwa Mtume yeyote isipokuwa ameeleza juu
ya Utume wa Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na juu ya Usia wa (Uimamu
wa)Aliy alayhi ssalaam”.
Na baadhi ya
maulamaa wamesema kama unavyosema wewe, na kauli yako hii inajulikana sana
miongoni mwa watu wa kawaida.
Anasema Al
Noubakhty katika kitabu chake kiitwacho ‘Firaq al Shia’ ukurasa wa 17 kuwa
Ushia umeanza pale Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipoanza
kuwalingania watu katika Uislamu, na kwamba walikuwa wakiitwa ‘Shiat Ali’
(wafuasi wa Ali), wakiwemo Miqdad bin Al Aswad na Salman al Farsy na Abu Dhar
na Ammar bin Yasir na walikuwa wakijulikana sana kwa kumpenda kwao Ali, na
walikuwa daima wakizungumza juu ya Uimamu wake,.
Na Ibni Nadim
katika kitabu chake kiitwacho ‘Al Faharasat’ ukurasa wa 249 ameeleza kuwa
Mashia walianza kuonekana baada ya vita vya ngamia ‘Maarakat al Jamal’, na
kwambaAliy alikuwa akiwaita kuwa ni Mawalii waliotakasika.
Haydar: Kutokana na haya
tunaelewa kuwa Ushia hauna uhusiano wowote na yule mtu anayejulikana kwa jina
la Ibni Sawdaa Abdullahi bin Saba-a na kwamba yote yanayosemwa juu yake mtu
huyo ni khurafaat – uongo uliozushwa tu na kwamba mtu huyo hakuishi duniani
aslan.
Khalid: Mwanadamu
ni adui wa asichokijua, na haki inajulikana kwa kuifuatilia na kwa kuitafuta
kwa nia halisi, kwani mtu huyu ametajwa ndani ya vitabu maarufu vinavyoaminika
vya Madhehebu ya Kishia vikiwemo vitabu vya ‘Firaq al Shia kilichoandikwa na Al
Noubakhty, na kitabu cha ‘Rijaal al Koshy’, na pia katika sharhi ya Nahjul
Balagha na vinginevyo.
Hader: Unataka nifahamu kutokana na maneno
yako kuwa Ushia haukuanza pale Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alipouchukuwa kwa
nguvu Ukhalifa kutoka kwa Amiri wa Waislam Aliy (Radhiya Llahu anhu).
Khalid: Kadhia
hii si kama inavyoelezwa na watu wanaofuata matamanio ya nafsi zao, kwani
Ukhalifa wa Abubakar Al Siddique (Radhiya Llahu anhu) umepatikana baada ya watu
wenye maarifa na hikma kumchagua, na baada ya Masahaba wote kukubaliana kwanza
mahali panapoitwa Saqifa, kisha watu wote waliobaki wakafungamana naye
msikitini, na hivi ndivyo ilivyokuwa katika Ukhalifa wa Umar na Uthmaan (Radhiya
Llahu anhu), na alipouliwa Uthmaan (Radhiya Llahu anhu) watu wote wakazielekeza
nyuso zao kwaAliy (Radhiya Llahu anhu) na kumtaka awe Khalifa wao, naAliy (Radhiya
Llahu anhu) akawaambia;
“Msinichaguwe mimi
(bora) mchaguweni mwingine, kwani tumekabiliwa na jambo lenye sura nyingi na
rangi nyingi na nyoyo hazisimami wala akili haithibiti. Msiponichaguwa mimi,
nitakuwa sawa na yeyote kati yenu, na huenda nikamtii zaidi yule mtakayemchagua
kuongoza amri yenu kuliko mtakavyonitii mimi. Bora mimi niwe waziri kuliko kuwa
Amiri (Khalifa).” Na melezo haya yameandikwa ndani ya kitabu chenu kitukufu
Nahjul Balaghah – 136
Na haya yanakubaliana
pia na alivyoelezea Al Mufiyd katika kitabu kiitwacho ‘Al Irshad’, ikiwa ni
dalili kuwa hapana ushahidi unaoonesha kuwaAliy (Radhiya Llahu anhu) ndiye
aliyechaguliwa kuongoza baada ya kufariki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam).
Haydar: Unataka kuniambia
kuwa juu ya umuhimu wa kadhia ya Uimamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) hakuacha usia wowote juu ya nani atakayetawala baada ya
kufariki kwake?
Khalid: Kuwa
na Imam atakayewaongoza Waislamu ni jambo muhimu sana kwa umma, lakini
tusilifanye jambo hili likawa ndiyo nguzo muhimu sana katika dini na kwamba
katika kuiamini nguzo hii tu kutamuingiza mtu Peponi na kwamba daraja yake ni
sawa na daraja ya Utume kama alivyoandika Hadi al Taharani katika kitabu
kiitwacho ‘Wadai al Nubuwah’ ukurasa wa 114 aliposema;
“Uimamu ni bora
kuliko utume kwani daraja yake ni ya tatu aliyomtakasa nayo Ibrahim baada ya
utume na Ukhalil”.
Haydar: Huenda hii ikawa
ni rai ya aalim huyu peke yake na maulamaa wengine wa Kishia hawakubaliani na
rai yake.
Khalid: Riwaya zifuatazo zitalijibu suali
lako;
Amesema Al Khashif
al Ghitwa-a katika kitabu chake kiitwacho Aslu Shia ukurasa wa 58;
“Cheo cha Imam ni cha
Mwenyezi Mungu kilicho sawa na Utume”.
Ama Khomeni katika kitabu chake kiitwacho ‘Al
Hukumat al Islamiah ukurasa wa 52 ameandika;
“Hakika Uimamu ni
daraja kubwa na tukufu, na Ufalme wenye kutiiwa na kila kitu kilichomo
ulimwenguni vikiwemo ‘atoms’. Na ni jambo la lazima katika madhehebu yetu
kuamini kuwa daraja la Maimamu wetu haifikiwi hata na Malaika walio karibu (na
Mwenyezi Mungu) wala Mtume aliyetumwa”.
Haydar: Maulamaa wetu wameupa umuhimu Uimamu
kutokana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alivyoupa
umuhimu.
Khalid: Kama
kweli jambo hilo lina umuhimu huo, kwanini basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akalipuuza na asimchague atakayeushika baada yake? Bali
jambo hili halikutajwa kabisa ndani ya Qurani ambayo Mwenyezi Mungu ameihifadhi
kutokana na kubadilishwa na kugeuzwa. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) hakuwahi kulitaja kwa ufasaha hata pale alipokuwa
akiisalimisha roho yake kwa Mola wake, wala hata wakati ule alipowakusanya
Waislamu wote katika Hija yake ya kuaga alipowahutubia akasema;
“Huenda
sitokuoneni tena baada ya mwaka wenu huu”.
Ile ilikuwa ni
fursa isiyoweza kulipika wala kurudi tena iliyoweza kuwakusanya Waislamu kutoka
pembe zote za Bara ya Arabuni ya kuwaeleza juu ya Usia wa Imamu atakayetawala
baada yake.
Kwa hivyo jambo
hili halikuwa na umuhimu ule mnaoupa nyinyi hata muifanye kuwa ni nguzo
mojawapo muhimu sana ya dini.na kwamba asiyeiamini anakuwa kafiri.
Ama Khomeini yeye
anayo tafsiri nyingine kinyume na wanavyosema maulaaa hao juu ya sababu
iliyomfanya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) asizungumie jambo hili
la uimamu.
Haydar: Tafsiri gani nyingine tena?
Khalid: Anasema
Khomeni katika kitabu chake kiitwacho ‘Kashf al Asraar’ (kuzifichua siri) kuwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliificha siri hii ya
Uimamu katika siku za mwanzo za daawa yake alipokuwa Makka, akihofia kuwaambia
watu jambo kubwa kama hili mpaka Mwenyezi Mungu alipomlazimisha kufanya hivyo pale
alipomwambia;
‘Ewe Mtume!
Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hukufanya, basi
hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi
Mungu hawaongozi watu wanaokufuru.”
Al Maidah – 67
Kisha akamuamrisha tena katika kauli yake Subhanahu
wa Taala;
“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni kuzirudisha
amana kwa wenywe (wanozistahiki)”
An Nisaa - 58
Anasema Imam Khomeni katika kitabu chake kiitwcho
‘Al Hukumah al Islamiyah’ ukurasa wa 81 kuwa;
“Mwenyezi Mungu hapa anamuamrisha Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) airudishe amana, yaani aurudishe (Uimamu) Uongozi kwa
wenyewe (wanaostahiki), yaani amrudushie Amiri l Muuminin alayhi ssalaam (Ali
bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu)) na yeye amrudishie atakayemfuata nk..”
Na maneno haya maana yake ni
kuwaAliy (Radhiya Llahu anhu) ndiye mwenye haki na kwamba Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) anatakiwa amrudishieAliy amana yake hiyo, na kama mnavyoona
kuwa tafsiri hii ni ya kupotosha na haina dalili yoyote ndani yake. Hii
ukijumuisha pia kulifasiri kwake neno ‘Amana’ kuwa maana yake ‘Uimamu’ Imam
Khomeni hapa anabadilisha na kuyapotosha maneno ya
Mwenyezi Mungu, na anaonesha ujinga wake wa kutojuwa sababu za kuteremshwa kwa
aya hizi.
Haydar: Lakini Khalifa wa mwanzo alikwenda
kinyume na kawaida ya ushauriano (Shura), kwani hakushauriana na Waislamu
wenzake pale alipomchagua Khalifa atakayetawala baada yake na hili ni jambo la
fardhi.
Khalid: Hakuna
mtu aliyefaridhisha jambo hili, na kwa yeyote atakayefuatilia mwenendo wa Al
Siddique (Radhiya Llahu anhu) atajua kwa uhakika kuwa alikuwa mtu mwenye
kuchunga maslahi ya Umma huu na akiutakia kila la kheri. Kwa hivyo jambo hili
halikuwa sudfa wala kosa, kwa sababu Waislamu walimtaka Abubakar (Radhiya Llahu
anhu) atoe ushauri wake juu ya nani anayemdhania kuwa atafaa kutawala baada
yake, ndipo alipomtaja Umar (Radhiya Llahu anhu) na kwa mwenye kufuata mwenendo
wa Umar (Radhiya Llahu anhu) pamoja na Masahaba wakati wa ukhalifa wake ataiona
hekima kubwa aliyokuwa nayo Abubakar pale alipomtaja Umar awe Khalifa baada
yake, lakini mtu afanye nini ikiwa chuki na bughudha dhidi ya Makhalifa hawa
wawili zishajazwa ndani ya nyoyo za baadhi ya watu?
Haydar: Zile kauli zinazosema kuwa Imamu ni
mtu aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na kwamba uimamu umekamatana na utume,
unataka kuniambia kuwa kauli hizo hazina dalili zilizo thabiti?
Khalid: Suali
hili ingefaa uwaulize wale walioifanya kadhia hii ya Uimamu kuwa ni nguzo ya
dini, kisha wakaibunia milango yake na mambo mengi, kisha wakauleta uzushi wa
mrithi wa Faqih na mabalozi wake, kisha vikatungwa vitabu visivyo na idadi
kuhusu jambo hili, yote haya kwa ajili ya kuilazimisha itikadi hii. Kutokana na
yote haya ni vizuri kama ungewataka hao waliouleta uzushi huu wakupe dalili
kutoka katika Qurani au kutoka katika mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam)( juu ya itikadi hii.
Haydar: Utanisamehe kidogo, maana sijauelewa
vizuri bado msimamo wako kuhusu Uimamu. Yaani unataka kuniambia kuwa hapana
‘nassi’ yoyote katika Qurani wala katika mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) juu ya Uimamu waAliy na maimamu waliokuja baada yake?
Khalid: Tukichukulia
kimjadala tu kwamba Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimtaja Aliy (Radhiya
Llahu anhu) kwa jina kuwa ndiye atakayekuwa Khalifa baada yake, na kwamba Al
Siddique aliuchukuwa kwa nguvu ukhalifa huo, huoni wewe mwenyewe kuwa wakati wa
ukhalifa wa Abubakar na Umar dola ya Kiislamu ilipata mafanikio mengi sana,
utulivu ulipatikana ndani yake, na hitilafu iliondoka baina ya Waislamu
wakaweza kuziteka nchi nyingi sana za kikafiri? Haya yote yalipatikana wakati
wa ukhalifa wa Abubakar na Umar na sehemu kubwa ya Ukhalifa wa Uthmaan
(Radhiyallahu anhum ajmaiyn).
Hebu niambie ewe
ndugu Haydar wangelikuwa kweli watu hawa wamekwenda kinyume na nguzo muhimu
sana ya dini kupita nguzo zote kama mnavyosema, vipi basi Mwenyezi Mungu
angewapa mafanikio kama haya katika kuzifungua nchi mbali mbali wao pamoja na
watoto wao. Isitoshe, wakati wote huo hapakuwa hata mtu mmoja aliyekuwa
akizungumza juu ya Uimamu au juu ya kunyanganywaAliy (Radhiya Llahu anhu)
ukhalifa wake.
Haydar: Huenda ikawa Amiril Muuminin alayhi
ssalaam hakulalamika kwa sababu ya kuona kwake mbali, alikuwa hataki kuleta
mfarakano baina ya Waislamu.
Khalid: Tuchukulie kuwa mambo yalikuwa kama
unavyosema, lakini baada ya kuuliwa Aliy (Radhiya Llahu anhu) na ukhalifa
ulpoangukia kwa Al Hassan (Radhiya Llahu anhu) tulimuona akimkabidhi ukhalifa
huo Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu), tena kwa hiari yake. Sasa je, inajuzu kwa
mtu asiyetenda makosa (Maasum) kuiangusha nguzo hii muhimu sana ya Uimamu
ambayo ni tukufu kupita zote kama mnavyosema, na kumpa mtu duni yake kwa
daraja. Tena ampe kwa hiari yake bila kulazimishwa baada ya kupita miezi sita
tu tokea alipouliwa baba yake? Isitoshe, tunasoma katika vitabu vya historia
kuwa Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu) alitawala kwa muda wa kiasi cha miaka
ishirini huku Waislamu wakipata ushindi baada ya ushindi dhidi ya majeshi ya
makafiri kupitia miaka yote iliyopita, na kwa ajili hiyo dini ya Mwenyezi Mungu
ikazidi kusambaa na kuenea kila pembe ya ulimwengu, na hili si jambo la
kushangaza kwa sababu Mu'awiyah na Masahaba wenzake (Radhiya llahu anhum)
walioifanya kazi hiyo wanatoka katika madrasa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam).
Haydar: Tujadiliane ewe ndugu mpenzi kikweli na
bila kuficha chochote juu ya kadhiya muhimu na isiyostahamilika katika jamii
yoyote ya Kiislamu. Naomba kifua chako kiwe laini kusikiliza.
Khalid: Hatukuamua kuzungumza isipokuwa kwa
sababu ya kunasihiana na kuijuwa haki ilipo, na pia kwa ajili ya kujiepusha na
ukireketwa.
Haydar: Hivi ndivyo ninavyokujuwa. Kwa hivyo
nataka unielezee juu ya sababu ya kupenda kuwakufurisha wenzenu na
kuwavurumishia tuhuma za ukafiri ndugu zenu wanaoswali kama nyinyi, juu ya kuwa
msingi wa mafundisho ya dini yetu ni kumdhania Muislamu mwenzio mema, na
kumtafutia udhuru kwa yale aliyojitahidi katika kujikaribisha kwa Mwenyezi
Mungu.
Khaled: Unajuwa ewe ndugu Haydar kuwa hapana
dhulma kuliko kumshrikisha Mwenyezi Mungu? Na
hapana jema kuliko 'Tawhiyd' (kumpwekesha Mwenyezi Mungu)? Na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipokuwa Makka alikuwa
akiwalingania watu katika kadhia moja tu, nayo ni:
ÇÚúÈõÏõæÇ Çááøóåó ãóÇ áóßõã ãøöäú Åáóåò ÛóíúÑõåõ ÃóÝóáÇ ÊÊøóÞõæäó } (ÇáÃÚÑÇÝ : 65)
Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi
hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?
Wakati wote huo hakuwa akiwafundisha
namna ya kutawadha wala kutoa Zaka wa Kuhiji
nk. Kwa hivyo wito wake (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) hapo mwanzo ulikuwa kuithibitisha itikadi ya Tawhiyd vifuani mwa
Masahaba, na kila kitu kikaja baada yake.
Haydar: Haya yanajulikana na hayana shaka
yoyote ndani yake, lakini kwa nini mnawachukiza watu kwa kuwakufurisha mbele ya
Waislamu wenzao?
Khalid: Kutokana na niliyosoma ndani ya
vitabu, nimeona kuwa maulamaa wengi wa Kishia ndiyo watumiaji wakubwa wa neno
Kafir wakiwakufurisha Waislamu wenzao pamoja na maulamaa wao, mfano Hussayn
Annajafiy katika kitabu chake Jawhar al Kalaam 6/62 aliposema: "Na kila mwenye kuwapinga wenye haki (Shia) basi huyo ni kafir na
hapana hitilafu yoyote juu ya haya."
Haydar: Tuziache kauli kama hizi na tuiangalie
sira ya Al Mustafaa (Swallah Llahu alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya jambo hili.
Khalid: Mwenye kufuatilia sira ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na namna alivyowalea Masahaba
wake (Radhiya Llahu anhum), ataona kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) alikuwa akiwatanabahisha na kuwatahadharisha kwa haraka sana kila
anapoona jambo lolote linalofanana na shirki kwa ajili ya kuilinda Tawhiyd na kujiepusha na ushirikina.
Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala Anasema:
Åöäøó
Çááøóåó áÇ íóÛúÝöÑõ Ãóä íõÔúÑóßó Èöåö æóíóÛúÝöÑõ ãóÇ Ïõæäó Ðóáößó áöãóä íóÔóÇÁõ
} (ÇáäÓÇÁ : 48)
"Hakika
Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa."
Kwa hivyo dhambi yoyote ni nyepesi, kinyume na shirki.
Haydar: Tukubaliane kwanza juu ya kusudi la
neno Shirk kabla ya kulizungumzia.
Khalid: Neno Shirk kama inavyojulikana katika
lugha ya kiarabu linatokana na kushiriki, yaani kwa maana ya kumjaalia
mwanadamu kama ni mwenzi wa Allah akafanywa mwanadamu huyo kuwa anao uwezo ama
wote au baadhi ya uwezo Alionao Mwenyezi
Mungu. Sheria imetaja mifano mingi mfano wa watu wa Makka walivyokuwa
wakiyajaalia masanamu kuwa yanao uwezo wa aina hiyo. Walikuwa wakiyaomba kama
wanavyomuomba Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo shirki ni kumjaalia mwingine kwa
kitendo au kutamka maneno au kuwa na itikadi kuwa anao uwezo alionao Allah, au
kumfananisha mwingine na Allah. Kwa hivyo mtu akiapa kwa mwingine asiyekuwa
Allah anakuwa keshafanya kitendo cha shirki kwa kauli yake hiyo, na akichinja
kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allah anakuwa kesha fanya kitendo cha shirki.
Na ikiwa ataamini kuwa aliyeapa kwa jina lake au aliyechinja kwa ajili yake
kuwa anao uwezo wa kunufanisha au kudhuru kinyume na Allah, basi mtu huyo
anakuwa kesha toka katika mila ya Kiislamu na kuingia katika mila ya Kufru.
Akiwa mtu huyo ni
jaahil asiyejuwa anachofanya, basi
inapasa kumtahadharisha na kumfundisha kuwa jambo hilo halijuzu kutendwa na
kwamba ni haramu, hata kama alikusudia kutabaruk tu, kwa sababu Dua na Tawafu
na Kiapo na Kuchinja na Swala na Hija na mengine ya mfano huo katika mambo ya
ibada hayajuzu kuelekezewa mwengine isipokuwa Allah peke Yake, na haya ndiyo
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyokuwa
akiwafundisha na kuwakataza watu wa Makka kwa muda wote ule.
Haydar: Unayosema ni katika mambo
yanayojulikana na maulamaa wote wa Kishia. Kipi kipya katika haya uliyoyasema?
Khaled: Niliyoyasema ni mepya katika masikio
ya maulamaa wa Kishia, bali wapo miongoni mwao waliohusisha ushirikina na dini
wakaupa ushirikina huo jina jipya, kama alivyosema Yusuf Al Baharani katika
kitabu chake Al Hadaaiq An Naadhirah (18/153): "Pana tofauti gani baina ya kumkufuru Mwenyezi
Mungu na kuwakufuru maimamu alayhimussalaam baada ya kuthibiti kuwa Uimamu ni
msingi wa dini?"
Haydar: Hizi ni miongoni mwa kauli chache
zisizokubalika kutoka kwa maulamaa wa dini na haikubaliki kuwa ni hoja dhidi
yetu, kwa sababu hatujapata kumuona yeyote kati ya maulaa wetu asiyeamrisha juu
ya Tawhiyd na kukataza kumshirikisha Mwenyezi Mungu, bali jambo hili
hawalifanyii mchezo.
Khaled: Al
Khomeini kwa mfano; aliuliza suali katika kitabu chake Kashf al asraar
ukurasa wa 65, kisha akalijibu mwenyewe kwa ajili ya kutubainishia itikadi yake
katika jambo hili aliposema: "Hakika
jawabu ya suali hili linafahamika zaidi kutokana na maana ya shirki, na
mlikwisha juwa kuwa shirki ni kumshirikisha Allah na mwengine au kumuabudu
mwingine kama anavyoabudiwa Allah, au kumuomba mwingine kama kwamba yeye ndiye Allah
au mshirka wake, au anao uwezo wa kuathiri. Bali yote hayo hayahesabiwi kuwa ni
shirki au kufru ikiwa mwenye kuomba anaamini kuwa Allah anao uwezo wa kujibu
ombi kupitia kwa waliopoteza maisha yao kwa ajili ya dini Yake, na walipoteza
roho zao kwa ajili Yake Allahu Taala." Unajuwa ndugu yangu Haydar maneno haya yamefungua
mlango upi?
Haydar: Maneno ya Imam Mwenyezi Mungu
amtukuze, yanafahamika vizuri kwangu. Kwani wewe unataka kusema nini?
Khaled: Nataka kukufahamisha kuwa Khomeini
ametamka jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
hajapata kulisema, wala wale waliokuja baada yake hawajapata kulisema katika
kutujulisha maana ya Shirki, na maneno haya ya Khomeini yamefungua milango
ifuatayo:
1.
Kwamba Muislamu anaweza kuomba shifaa kwa kutumia uchawi
au kuvaa hirizi kwa kujikinga na maradhi. (Soma kitabu cha Bihaar al Anwaar
(94/193)
2.
Kuomba
istikhara kwa njia ya lozi au jiwe litakaloweza kumsaidia mwanadamu. Soma kitabu cha Attahdhiyb
(1/306) na Furu'a al Kafi (1/131)
3.
Itikadi kuwa Maimamu wana haki ya
kufanya watakavyo juu ya ardhi na kwamba wao ndio
miungu juu ya ardhi. Soma Bihaar al Anwaar Uk.
95
4.
Itikadi kuwa Maimamu wanao uwezo wa kuamua katika mambo ya kidunia na mambo ya hali ya hewa.
Soma kitabu cha Al Ikhtiswaas cha Al Mufiyd Uk.
327 na Bihaar al Anwaar (27/33).
5.
Itikadi kuwa Imam anao uwezo wa kufufua maiti makaburini mwao. Soma kitabu cha Usuwl
al Kaafi (1/457) na Baswaair Adarajaat
(76).
Kwa
hivyo itikadi kama hizi unadhani zinamuongoza mtu
katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu au katika kumshirikisha? Hii ni shirki ambayo hata makafiri wa Makka hawakuwa
wakiikubali.
Haydar: Nia ndiyo muhimu katika matendo
yoyote katika kukubaliwa na kukataliwa kwa matendo, na haya ndiyo aliyosema
Imam Khomeini.
Khaled: Nitazidi
kuwadhihisha; katika kitabu chake Al Khomeini kiitawacho Kashf al Asraar
Uk. 42 amesema: "Baada ya
kubainika kuwa shirki ni kumuomba asiyekuwa Mola wa
ulimwengu kwa kuitakidi kuwa yeye ndiye Allah! Kwa hivyo yaliyo duni ya haya
hayahesabiwi kuwa ni shirki. Na hapana tofauti baina
ya aliye hai na aliyekufa. Kwa mfano kuliomba jiwe
siyo katika shirki juu ya kuwa kitendo hicho ni
baatil." Na Mwenyezi Mungu Ametujulisha kuwa
watu wa Makka hawakuwa wakiyaomba masanamu wakiitakidi
kuwa hiyo ni miungu, kama alivyosema Khomeini, bali wao waliyafanya masanamu
hayo kuwa ni walinzi tu wenye kuwakaribisha karibu na Allah. Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÇáÐöíäó ÇÊøóÎóÐðæÇ ãöä Ïõæäöåö
ÃóæúáöíóÇÁó ãóÇ äóÚúÈõÏõåõãú ÅöáÇøó áöíõÞóÑøöÈõæäóÇ Åöáóì Çááøóåö ÒõáúÝóì } (ÇáÒãÑ : 3)
Na wale wanao wafanya
wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate
kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.
Unadhani walipofanya vile, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwaacha waendelee tu
kwa sababu hawakuwa wakiitakidi kuwa ni miungu? Angelifanya hivyo, basi
ingewezekana, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) aliwakataza na akapambana nao na akawabainishia kuwa
hii ndiyo shirki kubwa.
Haydar: Unataka kuniambia kuwa Imamu, Mwenyezi
Mungu amtukuze hakuwa akielewa maana ya shiriki, au alikuwa akiwaruhusu watu wa
kawaida kufanya hivyo?
Khaled: Mimi
siye nitakayetoa hukmu katika hilo, bali Mwenyezi
Mungu ametupa akili na vifua vinavyoweza kupambanua baina ya haki na upotovu.
Kwa hivyo inatubidi tufahamu kuwa Maimamu
Mwenyezi Mungu awarehemu walikuwa ni watu wema, tunawapenda kwa sababu ya
mapenzi yetu kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kwa ajili wao
wanafuata mafundisho yake. Na hatuwapi isipokuwa daraja
wanayoistahiki. Na tunajikinga kwa Mwenyezi
Mungu katika kuwanyanyua na kuwageuza miungu kama alivyosema Al Koshy Uk. 224
Amesema Jaafar bin Muhammad: "Wallahi sisi si chochote isipokuwa ni watumwa wa Mwenyezi Mungu aliyetuumbana
akatuchaguwa, na wala hatuna uwezo wa kudhuru wala kunufaisha. Tukipata rehma,
basi kwa Rehman Zake na tukiadhibiwa, basi kwa dhambi
zetu. Wallahi hatuna hoja yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, wala hatuna dhima, na sisi tutakufa na tutazikwa na tutafufuliwa na
kusimamishwa na kuulizwa. Ole wao, wanana nini Mwenyezi Mungu awalani hawa,
walimuudhi Mwenyezi Mungu wakamuudhi Mtume wake katika kaburi lake, na Amiri wa Waislamu na Fatima na Al Hassan na Al Hussayn na
Aliy bin Al Hussayn na Muhammad bin Aliy Swalawaatu Llahu alayhim. Nashuhudia
mbele yenu kuwa mimi ni mja ninayetokana na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na sina dhima mbele ya Mwenyezi
Mungu, nikimtii atanirehemu na nikimuasi ataniadhibu adhabu kali."
Khaled: Bado
ningali nastaajabu kwa wale wenye kuzifasiri aya za
Qurani kinyume na maana yake iliyo sahihi, na wanatoa ushahidi wa hadithi
dhaifu katika kuthibitisha jambo lisilokuwemo ndani ya kitabu cha Mwenyezi
Mungu.
Haydar: Unaweza kunipigia mfano katika haya
unayoyasema?
Khaled: Kauli
Yake Mwenyezi Mungu aliposema:
ÅäãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóå áöíõÐúåöÈó Úóäßõãõ
ÇáÑøöÌúÓó Ãóåúáó ÇáúÈóíÊö æóíõØóåøöÑóßõãú ÊóØúåöíÑðÇ } (ÇáÃÍÒÇÈ : 33)
Iwapi hapa dalili ya kuthibitisha kuwa Maimamu wamekingwa?
Haydar: Dalili hapa ni kwa kuifahamu maana ya
aya hii na siyo kwa yaliyoandikwa. Kwa sababu atakayemwakilisha Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) lazima awe aliyekingwa asije
akaharibu katika kuifikisha risala. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyomkinga Mtume
wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam), katika kuifikisha risala, kwa hivyo pia
Maimamu wakakingwa kwa sababu wao ndio waliousiwa baada yake Alayhi Swalaat wa
ssalaam.
Khaled: Kukingwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni wajibu kwa ajili ya kuifikisha risala,
kutokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:
æóãóÇ íóäØöÞõ Úóäö Çáúåóæóì Åöäú åõæó
ÅöáÇøó æóÍúíñ íõæÍóì } (ÇáäÌã : 3-4)
An Najm – 3-3
Sasa ni nani aliyewajibisha
kwa watu wengine maalum baada ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)? Kama ipo habari yoyote juu ya jambo hilo,
basi lazima iwe sahihi na mutawaatir iliyopokewa kwa njia nyingi sahihi na
yenye kueleweka na kufahamika na iliyoenea baina ya watu. Kwa kukosekana hayo,
hiyo itikadi ya kukingwa haina dalili yoyote.
Haydar: Lakini lazima ieleweke kuwa aya hii
imeteremshwa hasa kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy (Alayhissalaam) ambao
ndio waliousiwa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) baada yake.
Khaled: Kwanza lazima ieleweke kuwa aya hii
haikuteremshwa kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy, na dalili ni kwamba Allah
alipoiteremsha aya hii aliiteremsha pamoja na aya nyingine zikiwasifia wake wa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam), kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akainuka na kumwita Fatima na Aliy na Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya
Llahu anhum) akawafunika na shuka yake, kisha akaisoma tena aya hii ili
iwaingize nao pia ndani yake na ili nao wapate baraka za aya hii pamoja na wake
wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Ikiwa kweli aya hii inamaanisha
kutwahirika kwao, kwanini basi Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) airudie.
Kwa nini airudie tena ile dua wakati kitendo kishakamilika kwa kutakaswa kwa
amri ya Allah
Haydar: Lakini aya ina dalili mbili za
kukingwa kwa Maimamu. Ya kwanza ni kutumiwa mfumo wa maneno ya wingi wa wanaume
Aliposema:íØåÑßã badala ya kutumia wingi wa wanawake.
Na ya pili ni maana ya neno 'Al Rij's'ÇáÑÌÓ uchafu, na maana yake ni kuwakinga na uchafu na maovu.
Ikafahamika kuwa aya hii ni kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy peke yao.
Khaled: Sababu ya kutumika kwa mfumo wa maneno ya wingi wa wanaume
badala ya kutumiwaä ya wanawake katika neno íØåÑßã ni kwa
sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mwenyewe pia yumo
katika waliotakaswa katika aya hii, kwa sababu yeye ndiye mkubwa wa ukoo, na
siku zote anayehutubiwa ni mkuu wa ukoo ambaye daraja yake katika nyumba ni
kubwa kupita wake zake, ili iweze kuwaingiza wote kwa pamoja.
Haidar: Mwenyezi Mungu Anasema:
{ ÃóØöíÚõæÇ Çááøóåó
æóÃóØöíÚõæÇ ÇáÑøóÓõæáó æóÃõæúáöí ÇáÃóãúÑö ãöäßõãú } (ÇáäÓÇÁ : 59)
59. Enyi mlio amini!
Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika
nyinyi.
Annisaa – 59
Na kwa vile inajulikana kuwa
Uimamu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni wa
Aliy (Radhiya Llahu anhu) ikaamrishwa kuwa atiiwe kama anavyotiiwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
Khaled: Muislamu haifasiri Qurani kwa rai yake, bali anaziangalia kauli za maulamaa mbali
mbali, kwa sababu maana ya aya hiyo iko wazi kabisa. Na kumtii Mwenyezi Mungu
kunatofautiana na kumtii Mtume wake (Swallah Llahu
alayhi wa sallam). Na wenye madaraka kuwatii kwao ni
kutokana na kutimiza kwao yale waliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na hawana twaa ya aina
nyingine. Ama kuhusu kuchaguliwa Aliy (Radhiya Llahu anhu) na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa Amiri wa
Waislamu, haya ni maudhui mengine ambayo tutayazungumzia baadaye. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ameusia
juu ya watu wa nyumba yake aliposema: "Nakukumbusheni
Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu." Na maana yake ni kuwa 'Muzijuwe haki zao.' Na Masahaba waliwahesimu kwa heshima wanayoisahiki kwa kuwapenda na kuwaheshimu.
Haidar: lakini kwa nini mnakuwa wakali hivi
mnapozungumza juu ya kadhia ya yule anayehesabiwa kuwa ni mwakilishi wa Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ambaye tumeusiwa juu yake.
Khaled: Utanisameh kama unahisi katika
mazungumzo yangu pana ukali ndani yake, kwani sisi ni watu wenye kuitafuta haki
Inshaallah, na ujuwe
ewe ndugu Haidar, yareti mambo haya yangelimalizikia katika kuchaguliwa na
kuusiwa, bali mambo yamekuwa hata akawa anapewa daraja ya Mitume, ikiwa si
daraja kubwa kupita hizo.
Khalid: Nakuona
rangi yako imebadilika tokea uliporudi kutoka katika Al Husayn iat (kupiga
jauseni)?
Haydar: Yeyote atakayekaa na kutafakari
akaukumbuka msiba wa Imam Al Husayn alayhi ssalaam lazima moyo wake utajaa
huzuni.
Khalid: Lakini
karne nyingi sana zishapita tokea msiba huu
ulipotokea, kwanini basi nyinyi mumo tu bado mnaendelea kuufanyia kumbukumbu
msiba huu kila mwaka?
Haydar: Si haramu mtu kuhuzunika wala kulia,
kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alitokwa na machozi alipofiwa na mwanawe, na alilia pia siku ile Hamza (Radhiya
Llahu anhu) alipouliwa na alitokwa na machozi pale baadhi ya Masahaba
walipofariki dunia. Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alihuzunika kwa misiba hiyo unadhani upo msiba mkubwa duniani ambao
watu wanapaswa zaidi kulia kwa ajili yake kuliko msiba wa Abu Abdullah
alayhissalaam (Imam Al Husayn )?
Khalid: Katika
Uislamu, huzuni na kilio kwa ajili ya misiba si jambo
linalohukumiwa na hisia peke yake, kwani jambo hili limewekewa sheria maalum na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Haydar: Namna gani?
Khalid: Huzuni
na kutoa pole kwa mtu aliye karibu ni siku tatu, na
mke anayo eda maalum inayojulikana, ama kuhusu kulia, basi Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amekwishatujulisha namna yake kutokana na
kauli yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) siku ile aliyofariki mwanawe Ibrahim
aliposema;
“Kwa
hakika moyo unahuzunika, na jicho linatokwa na machozi
lakini hatusemi ila yale tu anayoridhika nayo Mwenyezi Mungu, na sisi kutokana
na kufarikiana nawe ewe Ibrahim tunahuzunika”.
Hatukupata
kusikia hata siku moja au kusoma kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) alirudia tena kulia au kuhuzunika kutokana na kifo cha
mwanawe huyo au kutokana na kifo cha ammi yake aliyekuwa akimsaidia au kutokana
na mke wake Bi Khadija (Radhiya Llahu anhu) au juu ya Hamza wala hata juu ya
yeyote miongoni mwa Masahaba.
Haydar: Kwa nini unakasirika mimi ninapomlilia Al
Husayn alayhi
ssalaam?
Khalid: Kwanza
siku ya Ashura inajulikana kuwa ni siku ambayo ndani yake Mwenyezi Mungu
alimuokoa Nabii Musa (AS) kutokana na Firauni, na kwa ajili hiyo Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akaamrisha watu wafunge siku
hiyo kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, na akaongeza kuwataka watu wafunge
siku ya tisa pia kwa ajili ya kwenda kinyume na namna Mayahudi walivyokuwa
wakifunga.
Pili - Mwenyezi Mungu amekadiria siku kama hiyo
auliwe Al Al Husayn (Radhiya
Llahu anhu), lakini hapana hukmu yoyote ya kisheria inayozungumza juu ya
kuitukuza au kuifanyia kumbukumbu siku hiyo kila mwaka kutokana na kifo hicho,
na mwanadamu anakipokea kwa moyo wa imani kile alichokadiriwa na Mwenyezi
Mungu. Sasa nani aliyetufundisha sisi tuirudie huzuni ya kuuliwa kwa Al Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu) kila mwaka inapofika siku kama hii?
Wakati huo huo kufunga siku hii ya Ashura
kumethibiti kwa dalilim tena ndani ya vitabu vyote vya
Ahlu Sunnah takriban na pia imethibiti katika vitabu vya madhehebu ya Kishia.
Katika kitabu cha madhehebu ya Kishia kiitwacho ‘Al
Istibsaar’ kilichoandikwa na Al Tuusi, na huyu Al
Tuusi anaitwa ‘Baba wa taifa la kishia’.
Imethibiti katika kitabu chake
cha Al Istibsaar juzuu ya 2 ukurasa wa 134 na katika kitabu kiitwacho ‘Wasail
al Shia’, kutoka kwa Abi Abdullah alayhi ssalaam kutoka kwa baba yake kuwaAliy alayhi
ssalaam amesema;
“Fungeni siku ya Ashura siku ya tisa na siku ya kumi kwani funga hiyo inafuta madhambi ya
mwaka mzima”.
HADITHI
NYINGINE
Kutoka kwa Abal Hassan (AS) kuwa amesema;
“Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alifunga siku ya Ashura.”
HADITHI
NYINGINE
Kutoka kwa
Jaafar kutoka kwa babake alayhima ssalaam kuwa amesema;
“Funga ya
Ashura inafuta dhambi za mwaka mzima”.
Huoni basi namna gani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alivyokuwa
akiitilia mkazo funga hii na pia ImamAliy (Radhiya Llahu anhu) na Jaafar (Radhiya
Llahu anhu). Wote hao wanatilia mkazo funga hiyo? Na
hii ni dalili kutoka katika vitabu vyenu wenyewe kuwa
funga hii ya Ashura ni katika mafundisho aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Haydar: Kweni
nani aliyekuambia kuwa Mashia hawaifungi siku hii na
kwamba hawafanyi ibada mbali mbali za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu?
Khalid: Kufunga
kuna wakati wake maalum, nao ni kutoka pale alfajiri
inapoingia hadi jua linapozama pamoja na nia. Hahesabiwi mtu kuwa amefunga
ikiwa atakaa na njaa mpaka wakati wa adhuhuri kisha
ale vyakula vizuri vizuri huku akisema;
“Siku
ya leo mimi nina huzuni.”
Haydar: Kwa nini unashadidia katika kulikataza
jambo hili wakati nina hakika kuwa halimpeleki mtu
kufanya maasi?
Khalid: Mambo
mnayoyatenda siku kama hii ambayo ni kinyume na
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hawezi
kuyakubali mtu yeyote mwenye akili timamu, yakiwemo yafuatayo;
1.
Kulia na kuomboleza.
2.
Kuchana
nguo na kujipiga makofi ya uso.
3.
Kujipiga
vifua kwa minyororo na visu mpaka damu kumwagika.
4.
Kauli za
kumsifia Al Al Husayn (Radhiya
Llahu anhu) zinazopindukia mipaka.
5.
Kuwalaani
na kuwatukana Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam).
6.
Kuibatilisha
amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) ya kufunga siku hii ya Ashura na kuwakataza watu wasifunge.
7.
Kuchinja
na kupika vyakula na kugawa kwa jina la Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu).
8.
Kuzika
mbegu ya chuki ndani ya nyoyo za watu wa kawaida,
jambo linalosababisha mfarakano baina ya umma.
9.
Kuharimisha
kufunga ndoa katika siku hii na kuharimisha
kuingiliana baina ya mtu na mkewe, na mengi mengineyo yenye mfano huu
mnayofanya katika siku kama hii.
Haydar: Lakini dhulma alofanyiwa Al Husayn alayhi ssalaam
inaumiza sana moyo na kuujaza huzuni kubwa sana, na Waislamu hawajapata
kupambana na msiba mkubwa kuliko huu.
Khalid: Msiba
mkubwa kuliko yote uliowasibu Waislamu ni kuondokewa
na Mtume wao (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kama ilivyoelezwa na Addarimiy na
Imam Malik kuwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimwambia;
“Atakayekutwa na msiba, basi aukumbuke msiba wangu (wa kufa kwangu),
kwani huo ni msiba mkubwa kupita (misiba) yote.”
Haydar: Naogopa nisije nikakufahamu vibaya kama
kwamba kusudi lako ni kuwa Msiba wa Al Husayn alayhi ssalaam hauna athari yoyote ile
ndani ya nafsi zetu.”
Khalid: Al Al
Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni kipenzi
cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na bwana wa vijana
wa Peponi, aliuliwa kwa dhulma akiwa shahid na Inshaallah mahali pake ni katika
Firdaws al Aala. – Subhanallah! – kwa hili sisi
hatukhitilafiani, na si msingi wa hitilafu baina yetu, isipokuwa hitilafu yetu
ni kuwa; Nani aliyetoa amri hii au fatwa hii, au nani aliyejuzisha kufanya yale
maovu yanayotendeka katika siku kama hii ya Ashura, mambo yaliyokatazwa hata
katika vitabu vya maulamaa wenu wa Kishia.
Katika
kitabu kiitwacho ‘Al Bihar’, 103/82 anasema Al Majlisi;
“Kuomboleza
ni katika matendo ya Ujahilia”.
Na
Ibni Babaweh al Qummy naye pia katika kitabu chake kiitwacho ‘Man la
yahadhuruhul Faqiyh’ (271/2) anasema;
“Katika
maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) yenye miujiza ndani yake ambayo hakupata kutamka mwingine kabla yake
ni kuwa; “Kuomboleza ni katika matendo ya Ujahilia”.
Na akaongeza kusema kuwa; Anapata dhambi hata yule
aliyehudhuria na asifanye matendo hayo.
Haydar: Nitapata dhambi ikiwa nitahudhuria hata
bila kupiga vifua wala kulia kwa sauti kubwa?
Khalid: Ndiyo,
ukihudhuria katika vikao kama hivi kisha usiwanasihi
watu wala kuwaongoza katika mema, bila shaka unapata dhambi. Hata Al Hur al
Aamily katika kitabu chake kiitwacho ‘Wasail al Shia’ (915/2) amesema;
“Kutoka
kwa Imam Al Sadiq kutoka kwa baba yake alayhimu ssalaam kuwa amesema;
“Amekataza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
kupiga kelele katika misiba na amekataza kuomboleza na kusikiliza
(maombolezo).”
Vipi
Muislamu anakubali kujifananisha na watu wa zama za
Ujahilia na kuwaiga matendo yao na akaacha mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)?
Hamuoni kuwa katika mwahali mwa maombolezo ya namna hii hakuzidishi
imani yoyote katika nyoyo za watu? Bali kinyume chake vikao hivi
vinazidisha chuki na mfarakano baina ya Waisalmu kila
mwaka. Na tatizo kubwa zaidi ni kuwa kila jeraha hilo
linapoanza kutaka kupona, unaingia mwaka mwingine na watu huanza tena
kukusanyika na kulichoma kisu kovu lake na kusababisha kufunguka tena kwa
jeraha hilo.
Kwa nini basi hamuyaachi hayo mkafuata uongofu
aliokuja nao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) badala ya kufuata wale wanaotaka kulizamisha jahazi hili na
kuwazamisha umma huu?
Khalid: Huoni
basi ewe ndugu yangu Haydar kuwa kuiadhimisha siku ya kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu) kunazalisha fikra za hatari ambazo hawezi kuzikubali Muislam yeyote
mwenye akilia timamu?
Haydar: Bora ungenifafanulia zaidi maneno yako
haya.
Khalid: Kuwa
na nia nzuri tu peke yake na kupenda mambo ya kheri
bila kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu kunaweza kumpeleka mtu katika njia
mbaya akajikuta anakwenda kwa kupepesuka bila ya nuru ya kumuongoza. Na hivi
ndivyo walivyofanya baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi, wakamnyanyua Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu) pamoja na kaburi lake katika daraja kubwa kuliko aliyopewa na Mwenyezi
Mungu.
Haydar: Maneno yako haya ni
makali, na mimi sitokubali mpaka unibainishie kwanza, ama sivyo nitakutuhumu
kuwa umewatukana maulamaa wetu.
Khalid: Nilikuwa
nikiwasikia sana watu wa madhehebu ya Sunni wakisema kuwa; Mashia wanapolizuru
kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)
wanalitukuza sana na wanalipa daraja kubwa sana kupita hata daraja na mapenzi
wanayoipa nyumba ya Mwenyezi Mungu ‘Al Kaaba’, na wanaitakidi kuwa penye kaburi
la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) pana
baraka nyingi sana zisizopatikana mahali pengine popote duniani. Na mimi nilikuwa nikidhani Masunni walikuwa wanazidisha chumvi
katika maneno yao hayo ya kuwatuhumu Mashia, na kwa ajili hiyo nikaamua
kuutafuta ukweli kwa kufanya utafiti wangu mwenyewe. Ndipo nilipogundua kuwa
yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na Masunni juu ya Mashia juu ya kulitukuza
kaburi la Al Husayn ni
machache sana ukilinganisha na mengi niliyoweza kuyajua.
Haydar: Huu wallahi ni
uongo unaowasingizia watu wanaoikubali shahada ya Laa ilaaha illa Llah
Muhammadan Rasulu Llah.
Khalid: Imeandikwa
katika kitabu kiitwacho ‘Furu-ul Kafi’, (1/324) na katika kitabu ‘Thawabul
aamal’ cha Ibni Babaweyh ukursa wa 56 na katika ‘Kamil al Ziarat cha Ibni
Kooloweyh (161) na ‘Wasail al Shia’ (348/10) kuwa;
“Ziara ya kaburi la Al Husayn ni sawa na
Hija ishirini pamoja na Umrah (ishirini)”.
Na imeandikwa pia katika
‘Tahdhiyb al Ahkam’ kilichoandikwa na Al Tusiy (16/2)
na ‘Wasail al Shia’ (348/10) kuwa mmoja katika Mashia alimwambia Imam wake;
“Mimi nimehijii mara
kumi na tisa na nimefanya Umrah mara kumi na tisa.”
Imam akamwambia;
“Ongeza bado Hija moja
na ufanye Umra niyingine ili uweze kuandikiwa thawabu ya ziara moja tu ya
kaburi la Al Husayn .”
Na hii maana yake ni
kuwa bora mtu alizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) mara moja kuliko
kuhangaika kwenda Makka akahiji Hija ishirini, ikimaanisha pia kuwa maulamaa
wenu wanapendekeza watu kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko kuhiji nyumba ya
Mwenyezi Mungu.”
Haydar: Huenda wanakusudia kuwakumbusha tu watu
wasije wakasahau kwenda kulizuru kaburi la Al Husayn .
Khalid: Ningependa
kukuuliza suali; Unadhani wanalijuwa kweli mahali lilipo kaburi la Al Husayn ?
Haydar: Unasema nini ewe Khalid, unataka
kuifuta historia na ukweli wake?
Khalid: Unajuwa
vizuri kuwa mimi sipendi kuongea maneno matupu bila ya
dalili. Ama kuhusu mahali lilipo kaburi laAliy (Radhiya Llahu anhu) imeandikwa
katika kitabu ‘Tahadhiyb al Kamal’ (305/13) kutoka kwa
Abu Jaafar al Sadeq amesema;
“Kaburi
laAliy halijulikani lilipo.”
Na imeandikwa katika
Tarikh al Baghdadi (138/1) kutoka kwa Mutin kuwa
amesema;
“Lau kama Mashia
wangelimjua aliyezikwa ndani ya kaburi hili wanalolizuru nje ya mji wa Al Kufa
(wakidhani kuwa ni kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)) basi wangelilipiga kwa mawe. Hili ni kaburi la Al
Mughira bin Shuuba.”
Na hii ni kwa sababu
hapana hata mtu mmoja mwenye kujua uhakika wa mahali alipozikwa Al Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu) baada ya kuuliwa.
Haydar: Juu ya uhakika uliotaja, hata hivyo mimi sidhani kama watu wanalitukuza kaburi hilo kiasi cha
hivyo unavyosema wewe, isipokuwa watu wanahimizwa tu ili wasipuuze ziara ya
kwenda huko.
Khalid: Turudie
mazungumzo yetu juu ya thawabu anazopata mtu aliyezuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), kwani yareti mambo
yangesimama hapo kuwa thawabu zake ni sawa na thawabu za Hija ishirini, bali
katika vitabu vingine thawabu zake zimefikia kuwa sawa na Hija themanini, na
haya yameandikwa katika kitabu kiitwacho ‘Thawabul aalmaal’ ukurasa wa 52 na
katika ‘Wasail al Shia’, imeandikwa kuwa thawabu za kulizuru kaburi la Al
Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni sawa na
Hija mia moja tena hija yenyewe iwe pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) 350/10).
Na katika hiyo hiyo
‘Wasail al Shia’, zimekuja riwaya nyingine zinazosema kuwa thawabu zake ni sawa
na Hija elfu zilizokubaliwa, Umra elfu zilizokubaliwa, Ujira wa mashahidi elfu
moja waliokufa katika vita vya Badar, thawabu za watu elfu waliofunga, thawabu
za sadaka waliopewa watu elfu zikakubaliwa pamoja a thawabu za watu elfu
waliotenda mema kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.
Haya
yote yameandikwa katika ‘Wasail al Shia’ (353/1), ‘Kamil al Ziarat uk.
143 na Bihar al Anwar (18/110).
Haydar: Maneno haya maana yake ni kupunguza shani ya kuikusudia nyuma ya Mwenyezi Mungu.
Khalid: Kama
nilivyokwambia ewe ndugu Haydar kuwa sisi tumekwishajulishwa kiasi cha thawabu
tunazopata tukenda kuhiji Makka, na pia tukisali ndani
ya msikiti mtukufu wa Makka. Lakini kama itakavyokuwa, hatuwezi kuzifikia
thawabu mnazozipata nyinyi mnapokwenda kulitembelea kaburi la Al Al Husayn mara moja tu.
Kwa sababu maulamaa wenu wanaifadhilisha ziara ya kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko Hija, kama
ilivyoelezwa katika kitabu cha ‘Furu-ul Kafi (324/1) na kama alivyoeleza Attusi
katika kitabu cha ‘Tahadhiyb’ (16/2) na kama walivyoeleza wengi miongoni mwa
maulamaa wenu waliosema; “Atakayelizuru kaburi la Al Husayn akiwa anaijuwa vizuri haki yake katika siku
isiyokuwa sikukuu Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija ishirini zilizokubaliwa, na
atakayelizuru siku ya Sikukuu Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija ishirini na Umra
ishirini, na atakayelizuru siku ya Arafat akiwa anaijuwa vizuri haki yake
Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija elfu moja na Umra elfu moja pamoja na thawabu
za kupigana vita elfu vya jihadi pamoja na Mtume aliyetumwa au Imam muadilifu”.
Haydar: Juu ya yote hayo katika nyoyo zetu
tunaipenda nyumba ya Mwenyezi Mungu mapenzi yasiyo na
mfano.
Khalid: Lakini
katika vitabu vyenu yako baadhi ya maandishi yanayoufadhilisha mji wa Karbala kuliko Al Kaaba na kuliko mji wa Makka, kwa mfano
maneno aliyoandika Al Majlisi katika kitabu cha ‘Bihar al Anwar’ (101-107)
kutoka kwa Abu Abdullah kuwa alisema;
“Mwenyezi Mungu
aliifunulia wahyi Al Kaaba akaiambia; ‘Lau kama si
udongo wa Karbala nisingekufadhilisha, na lau kama si kwa heshima ya yule
aliyezikwa Karbala nisingekuumba, na wala isingejengwa nyumba unayojifakharisha
nayo, basi powa tena tulia na uwe mkia usiotakabari juu ya ardhi ya Karbala, ama
sivyo nitakughadhibikia kisha nitakutumbukiza katika moto wa Jahannam”.
Haydar: Haya tena wallahi ni
maneno ya ajabu ndiyo kwanza leo nayasikie.
Khalid: Kauli
hizi ni sahihi inayotiliwa nguvu na kuungwa mkono na
maulamaa wengi wanaojulikana miongoni mwa Mashia.
Haydar: Ikiwa zinapatikana thawabu zote hizi kwa nini basi ziara hii isitajwe ndani ya kitabu cha
Mwenyezi Mungu?
Khalid: Jawabu
yako utaipata ndani ya kitabu cha Bihar al Anwar (101-290) imeandikwa;
“Mtu mmoja alimuuliza
Imam; ‘Mwenyezi Mungu amewafaridhishia watu kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu
lakini haikuitaja ziara ya Al Husayn alayhi ssalaam.”
Imam akampa jibu
linaloonyesha kama kwamba kuna utata kidogo ndani
yake. Alisema;
“Juu
ya kuwa haikutajwa, lakini Mwenyezi Mungu ametaka kuijaalia iwe hivyo.”
Kuna kukiri wazi wazi
kuliko huko juu ya uongo wa riwaya hizi zisizokuwa na
isnadi wala ukweli?
Haydar: Juu ya yote uliyoyataja, lakini mimi naitakidi kuwa watu wa kawaida miongoni mwa Mashia na
wale wanaopenda ukweli wanaienzi na kuitukuza nyumba ya Mwenyezi Mungu na
kwamba ndani yake mna thawabu nyingi sana na nyoyo zao siku zote zina shauku ya
kuiendea nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Khalid: Fadhila
hizi zinazotajwa juu ya kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) zimewafanya watu
wengi wawe na shauku kubwa ya kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko waliyokuwa nayo ya
kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha ‘Wasail
al Shia’ kuwa;
“Wallahi
nilitamani nisingehiji na badala yake ningekwenda kumzuru”.
Wanazusha hadithi nyingi
za uongo juu ya fadhila za Karbala hata wakazua hadithi inayosema kuwa eti
ndani yake udongo huo mna ponyo, kama alivyosema
Khomeni katika kitabu chake kiitwacho Kashf al Asrar uk. 62
Haydar: Tufanye nini mbele ya hadithi hizi
nyingi zinazopokewa na watu wa kawaida katika Mashia
wanaopenda kufanya mambo ya kheri hata wakatamani kuwazuru watu wa nyumba ya
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Khalid: Muislamu
mwenye kumpenda Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hafuati matamanio ya
nafsi yake, bali hutumia akili pamoja na dalili zilizo wazi zinazotokana na
hadithi sahihi zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam), na hata kama atawapenda watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) lakini anatakiwa asiende kinyume na yale
yaliyothibiti. Ni vizuri pia kama atafuata yale aliyofanyaAliy (Radhiya Llahu
anhu) kwa sababu yeye aliishi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) na kwa sababu yeye anayajua vizuri zaidi matendo ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Yareti kama
Shia wa kawaida atafanya hayo basi atapata kheri nyingi sana ndani yake.
Ujuwe pia ewe ndugu Haydar
kuwa riwaya hizi hazikuja ila baada ya kubaidika zama za Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na zama za waloziandika hadithi hizo na
hii niyo sababu ya kujaa kwa habari za uongo ndani yake, na kuenea kwake uongo
huo, na wakati huo hapakuwa na wanaoitetea dini ya Mwenyezi Mungu.
Khalid: Hebu
tuzungumze juu ya kulia kwenu kwa ajili ya kuuliwa kwa Al Husayn
(Radhiya Llahu anhu), kuomboleza,
kupiga vifua, kujipiga vichwani mpaka damu kuwatoka na mambo mengi mnayofanya
kila mwaka katika mwezi huu wa Muharrahm katika Al Husayniyat.
Haydar: Mambo haya si mageni na wala si uzushi,
ingawaje jina lake ni jipya, lakini mambo yote hayo yalikuwa yakijulikana tokea
wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na ilikuwa ikijulikana kuwa Al
Husayn alayhi ssalaam atauliwa tokea
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipomhadithia binti yake Al Zahraa
juu ya kuuliwa kwa mwanawe na
alimuonesha hata udongo wa ardhi atakayouliwa juu yake, na hali kadhalikaAliy bin
Al Husayn alipowasili Madina alipiga
kambi na wanawake wakakaa hapo, akamwita mshairi akawa anasoma mashairi ya
kuomboleza kifo cha Al Husayn na akaweka
msiba mahali hapo karibu miaka thelathini na nne.
Khalid: Hebu
tuyaangalie mambo kwa utulivu. Tokea pale Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alipowajulisha juu ya yale yatakayomsibu mjukuu wake alitamka hayo kwa ajili ya
kutoa habari tu au alikusudia kuweka sheria maalum?
Haydar: Kuna tofauti gani?
Khalid: Kama ilikuwa kwa ajili ya
kutoa habari tu, basi haiwezi kuchukuliwa kuwa ni amri iliyowekewa sheria. Kwa
mfano; tumejulishwa kuwa Siku ya Kiama ni sawa na miaka elfu hamsini. Habari
hizi haziwezi kuwekewa sheria yoyote ile juu yake katika hukmu za halali na
haramu.
Kwa hivyo
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipotupa habari ya kifo cha Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa akitujulisha tu,
na ilikuwa wajibu wetu sisi kusadiki yale aliyotujulisha, lakini hatukuambiwa
tena na sisi tuanzishe au tuzushe hukmu nyingine za kisheria juu ya yale
yaliyotendeka siku hiyo, ama sivyo Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
angetuamrisha kufanya hivyo pale alipotujulisha juu ya kuuliwa kwa mjukuu wake.
Ama kuhusu
ile riwaya yaAliy bin Al Husayn kuwa
alimwita mshairi aliyekuwa akisoma mashairi ya kuomboleza na kwamba aliendelea
kufanya hivyo kwa muda wa miaka thelathini na nne takriban, riwaya hii haina
isnadi sahihi – yaani hadithi hii ni dhaifu – na kufanya matendo kama hayo si
katika yale aliyotufundisha babu yake ambaye ni Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam), bali kinyume chake ametukataza kufanya hivyo.
Haydar ; Lakini
ukichunguza vizuri juu ya yaliyomsibu Al Husayn alayhi ssalaam kwa jicho la kutafakari,
ungejuwa kuwa alifanya jambo asilopata kulifanya kiumbe chochote kingine. Kwani
yeye alitoka akiwa amekasirishwa na dhulma iliyokuwa ikitendeka wakati wake,
hata akawa mfano bora wa kuigwa na kwa ajili hiyo hata mwahali mwengi kumeitwa
kwa jina lake (Al Husayniyat).
Khalid ; Ewe ndugu Haydar,
kwanza -
Hili jina la Al Husayniyat (sehemu zinazopigwa jauseni) halikuja isipokuwa
katika miaka ya mwisho ya utawala wa Kiislamu katika dola ya Kibuweihiyah kwa
mfano. Na jambo hili halikuwepo zama za Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) wala wakati wa watoto wa Al
Husayn (Mwenyezi Mungu awarehemu).
Pili –
Huoni kuwa kutokana na jina hili, ni dalili ya kupindukia mipaka katika
kumtukuza kwenu Al Husayn (Radhiya Llahu
anhu). Kwanini hamujaita kwa mfano Aliyat au Alawiyat au Muhammadiyat, kwa vile
wao ni bora kuliko Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), jambo ambalo sidhani kama
yeyote mwenye akili timamu anaweza kulipinga.. Kwa nini mkalipa jina la Al
Husayn (Radhiya Llahu anhu)?
Tatu - Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipata
adhabu nyingi sana kutoka kwa makafiri hata ikambidi auhame mji wa Makka. Na
katika mji wa Taif Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipigwa mawe, na mara
nyingi alikosewa kuuliwa, lakini hatukupata kumsikia hata siku moja
akiwachochea watu kufanya zogo, isipokuwa aliwataka kupigana Jihadi chini ya
bendera yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Nne – Al
Husayn (Radhiya Llahu anhu) aliuliwa
tokea mwaka wa 61 Hijri (miaka 61 baada ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) kuhama kutoka Makka kwenda Madina), kwa nini basi tusijishughulishe
kufanya zile ibada zilizokuwa zikifanywa wakati ule au kabla yake?
Tano - Kwa
nini Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)
asitoke kwenda kupigana na Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu) juu ya kuwa Mu'awiyah
alikuwa Khalifa wa Waislamu kwa muda upatao miaka ishirini?
Sita – Kwa
nini Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)
asitoke kwenda kupigana na Yazid mpaka zilipoanza kumfikia zile barua kutoka
Iraq?
Saba – Kwa
nini Al Hassan (Radhiya Llahu anhu) asiende kupigana na Mu'awiyah baada ya
kumpa ukhalifa yeye mwenyewe?
Nane – Yupo
Imam yeyote mwingine aliyetoka kwenda kupigana na Khalifa yeyote wa Kiislamu
baada ya Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)?
Haydar ; Kuna
ubaya gani ikiwa watu fulani watajikusanya kwa ajili ya kuwakumbuka watu wa
nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)?
Khalid ; Hapana
kilicho bora kuliko kufuata mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) katika kuwalingania kwake watu na katika kupigana Jihadi, na
tunatakiwa daima tuwe tunachukua ibra katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo;
“Hakika
nyinyi mnayo ruwaza njema (mfano mwema wa kuufuata) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu
kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi
Mungu sana.”
Al Ahzab – 21
Je, haya
yote yanapatikana katika vikao vyenu hivi?
Na pia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo ;
“Wanaoamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni
wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kusimamisha Sala na
kutoa Zaka na hawamuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.”
At Tawba - 18
Mwenyezi Mungu Subhanahu
wa Taala anawasifia hapa wale wanaoamirisha misikiti Yake kwa kumdhukuru na kwa
kufanya matendo ya kumtii, lakini hatuwaoni wale wanaohudhuria vikao kama hivi
vya Al Husayniyat (vikao vya kupiga jauseni) kuwa ni watu wenye kuijaza
misikiti, wala hatuwaoni kuijaza misikiti hata katika mwezi wa Ramadhani, jambo
lililohimizwa katika dini na pia maulamaa wengi wamesema juu yake na hata aalim
maarufu wa Kishia Al Amiliy amesema katika Wasail (185/50) kuwa; Bin Mahran
alimuuliza Imam wake juu ya umuhimu wa kusali ndani ya mwezi wa Ramadhani,
akamjibu;
“Usali kama unavyosali katika miezi mingine, isipokuwa ndani ya
mwezi wa Ramadhani mja anatakiwa azidishe katika Sunnah zake kama akipenda. na kama ataweza basi azidishe katika mwanzo wa mwezi huo
rakaa ishirini kuliko alivyokuwa akisali katika miezi mingine”.
Haydar: Lakini
ndani ya Al Husayniat (vikao vya jauseni) mna mafunzo makubwa sana katika
kuwaelimisha watoto hukmu za dini yao na kuwalea malezi bora yenye baraka ndani
yake.
Khalid: Yareti
hayo unayosema yangekuwa yanatendeka kweli basi yangekubaliana na mafunzo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam), lakini ndani ya vikao hivyo juu ya kuwa yanakuwepo baadhi ya
mawaidha na nasaha lakini mengi yanayotendeka humo ni matusi, laana na kuzika
mbegu za chuki ndani ya nyoyo za Mashia dhidi ya ndugu zao Masunni. Na yareti
maneno hayo yangekuwa yanasemwa na watu wa kawaida,
lakini la kusikitisha ni kuwa laana na matusi hayo yanafundishwa na maulamaa
wakubwa wanaojulikana
Khalid: Usisahau kuniletea na
mimi chakula mnachogawiwa katika Ashura.
Haydar: Bila
shaka, vipi nitakusahau na wewe ni rafiki yangu?
Khalid: Hukubaliani
namimi kuwa kuihusisha siku kama hii kwa matendo kama
haya pamoja na kufunga nusu siku, kuwa haya yote yanahitajia dalili za kisheria
ili yakubalike kuwa ni ibada anayopata mtu thawabu ndani yake?
Haydar: Unataka kuwakosowa Mashia kwa sababu
wanatoa sadaka na vyakula katika siku kama hii kwa ajili ya Al Husayn alayhi ssalaam
huku wakitegemea ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu?
Khalid: Chakula
hakina makosa yoyote, mtu akitaka anakula na asipotaka
hali, lakini kadhia yetu sisi ni ile nia ya kutoa sadaka hizo na
ile nia ya kuwachinja wanayama katika siku hiyo, pamoja na
matendo mbali mbali wanayohangaika kuyatenda ndani ya siku hiyo. Kwa sababu mtu
anapochinja kwa ajili ya mtu fulani na si kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu, huyo anapata dhambi hata kama atapiga bismillahi pale
anapochinja.
Haydar: Unataka kuniambia kuwa wewe unaweza
kuzisoma nia za watu?
Khalid: Mtu
anatakiwa matendo yake yalingane na nia yake, kwa
sababu Muislamu anapokuja akachinja siku ya Karbala na mtu huyo hana kawaida ya
kuchinja isipokuwa katika siku hii tu, tunaelewa wazi kuwa hakuchinja isipokuwa
kwa mnasaba wa siku hii. Na chochote ambacho msingi wake ni
batili basi siku zote kitabaki kuwa batil, kwa sababu haikuja katika sheria ya
Kiislamu hukmu ya mtu kuchinja mnyama kwa ajili ya kumbukumbu ya kuuliwa kwa
mtu.
Haydar: Kama kwamba umesahau yale niliyokwambia
kuwa wanyama wanaochinjwa na vyakula vinavyopikwa ni kwa ajili ya kuwalisha
waliohudhuria shughuli hizi za jauseni waliokuja kwa ajili ya kupata ibra na
kujifunza juu ya kuuliwa kwa shahid Abu Abdullah Al Al Husayn
alayhi ssalaam?
Khalid: Kwa
hivyo kusudi lote hilo ni kuwakusanya Waislamu katika siku hii ya Kerbala siku
aliyouliwa Al Husayn (Radhiya
Llahu anhu)?. Je, ninaweza kukuuliza suali moja?
Haydar: Tafadhali uliza.
Khalid: Ipo dalili yoyote kutoka
kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ya kuihusisha siku hii ya Ashura kwa
ibada maalum?
Haydar: Ninavyojuwa
mimi ni kuwa hapana dalili yoyote isipokuwa juu ya kufunga siku hii kama
ulivyonambia wewe mwenyewe hapo mwanzo.
Khalid: Sasa ikiwa hapana dalili
yoyote ile, nani huyu basi aliyethubutu kutoa fatwa kama hii ya kuwataka
Waislamu wawe wanakula baada ya adhuhuri katika siku hii ya Ashura, au nani
aliyetoa fatwa ya kuwataka Waislamu wawe wanajipiga vifua kwa mikono na kwa
visu na vijembe na damu nyingi kumwagika? Na nani aliyetoa fatwa ya kuirudia
huzuni hii kila mwaka kuwa watu wawe wakijikusanya na kulia na kuomboleza huku
wakijipiga makofi ya uso na kuchana nguo zao? Na nani huyu mwenye akili nyingi
aliyetoa fatwa hii ya kuwataka watu waache ibada zao zilizowekewa sheria na
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na badala yake kujishughulisha na mambo
kama haya yenye kupoteza wakati wa watu bila manufaa yoyote?
Haydar ; Huenda
ikawa mmoja katika Masahaba (Radhiya Llahu anhu) au katika watu wa nyumba ya
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kufanya haya?
Khalid: Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) aliuliwa mwaka wa 61
baada ya Hijra na baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhu) walikuwepo wakati
huu, kwanini basi tusisikie kuwa hata mmoja wao aliwahi kufanya matendo kama
hayo kutokana na mnasaba huo? Na je, Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kwa mfano angeliuliwa
siku ya Sikukuu, tungeacha kuisherehekea siku hiyo pia na kuvaa nguo nyeusi
katika siku ya furaha ?
Haydar: Kama
kwamba unauona msiba huu kuwa ni mdogo sana?
Khalid Nani
aliyekwambia kuwa kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya
Llahu anhu) ni msiba mdogo? Bali msiba huu ni mkubwa sana na dhulma kubwa sana
imepita, na kila aliyeshiriki katika mauaji haya atapata kwa Mwenyezi Mungu
kile anachostahiki. Lakini msiba upi unadhani ulio mkubwa zaidi; kufariki kwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) au msiba wa Al Husayn (Radhiya
Llahu anhu) au hata kuuliwa kwaAliy bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu)? Juu ya
ukubwa wa msiba wao lakini hatufanyi lolote isipokuwa kufaidika na ibra
inayopatikana katika kuwakosa kwa njia isiyokwenda kinyume na sheria.
Haydar ; Lakini
Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) ametupa
funzo kubwa la namna ya kupambana na wapotofu.
Khalid ; Ndugu yangu
mpenzi, unataka tujifunze kutokana na haya juu ya namna ya kupambana na
serikali zinazotutawala au namna ya kuupigania ukubwa, na je Masahaba waliokuwa
wakiishi wakati wake walikubaliana naye kuhusu jambo hilo, Sahaba kama vile
Ibni Abbas na wengine (Radhiya Llahu anhu)? Lazima utambuwe ewe Haydar kuwa
utawala wa Bani Umayya umewekwa na Imam Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) baada ya kujishusha
ukhalifa wake na kumkabidhi Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu).
Sasa je,
unataka tuwafunze watoto wetu namna ya kuzipindua serikali? Na kwa nini
tuiadhimishe siku aliyouliwa Al Husayn tu (Radhiya Llahu anhu) wakati wapo wengi
walio watukufu kupita yeye waliouliwa pia kwa dhulma?
Haydar: Sisi
hatumhusishi Al Husayn peke yake
(Mwenyezi Mungu awe radhi naye), bali tunajitahidi kufanya maombolezo ya kila
mtu mwema.
Khalid: Ikiwa haya unayoyasema ni
kweli ewe ndugu Haydar, basi itatukuta kazi kubwa ya kufanya maombolezo na
hafla za misiba kwa ajili ya watu wema wengi wakiwemo watu wa nyumba ya Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) na wengineo. Na kama tutahesabu misiba iliyowakuta watu
wema tokea siku aliyoumbwa Adam (AS) mpaka siku ya leo, basi idadi yao itazidi
idadi ya siku za mwaka mzima, bali huenda idadi hiyo ikazidi idadi ya saa za
mwaka mzima. Hivyo sisi tumeumbwa kwa ajili hiyo ?
Haydar: Katika
mazungumzo yaliyopita ulitaka tuzungumze juu ya uadilifu wa Masahaba, ukasema
kuwa watu hawa hawasemi uongo. Utasemaji nikikuuliza juu ya Sahaba ambaye
zimepokelewa kutoka kwake hadithi nyingi kupita kiasi. Kupita hata uwezo wake?
Khalid: Kama
kwamba unataka tuzungumze juu ya hadithi za Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) zilizopokelewa kutoka kwa baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhu)?
Haydar: Ndiyo, tuzungumze juu ya Masahaba
wanaohusika na elimu ya hadithi.
Khalid: Si
bora tuzungumze juu ya aalim wa hadithi mashuhuri kupita wote katika Masahaba?
Haydar: Nani
unayemkusudia ?
Khalid: Namkusudia
Abdul Rahman bin Sakhar al Dousiy, yule Sahaba aliyejitolea kuifanya kazi ya
elimu hii ya hadithi.
Haydar: Mara ya mwanzo leo nalisikia jina hili.
Khalid: Hulaumiki,
kwa sababu Sahaba huyu anajulikana zaidi kwa umaarufu wake kuliko kwa jina
lake. Nakusudia Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu).
Haydar: Nishamkumbuka! mwanachuoni wetu maarufu
aitwae Al Husayn Sharafuddin Al Mousawiy
alizungumza juu yake katika kitabu kizuri sana kiitwacho ‘Abu Hurairah’, na
akabainisha ndani yake udhaifu wa riwaya zake mtu huyu.
Khalid: Kabla
sijasema lolote kuhusu kauli yako hii, ningependa kukuuliza suali moja. Umewahi
kusoma chochote juu ya Sahaba huyu mtukufu (Radhiya Llahu anhu) katika vitabu
vya Masunni?
Haydar: Kusema kweli sijapata kusoma chochote,
isipokuwa nimekwishasikia mengi sana juu yake mtu huyu kutoka kwa wanavyuoni
wetu, na wote wanasema kuwa hadithi zilizopokelewa kutoka kwake zote si sahihi.
Hata hivyo na tuzungumze juu yake, lakini kwa utulivu, na suali langu la mwanzo
nataka kujua ; mtu huyu amesilimu mwaka gani?
Khalid: Inajulikana
kuwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesilimu mwaka wa saba baada ya Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) kuhajiri kwenda Madina na umri wake wakati ule ulikuwa
miaka thelathini, na alikuwa akiishi al Suffah (mtaa ulioshikamana na
nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) mahali walipokuwa wakiishi
masikini na wacha Mungu), na alikuwa daima pamoja na Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam), hambanduki, kila anapokwenda alikuwa naye mpaka siku ile Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alipofariki dunia.
Haydar: Lakini kinachostaabisha ni ule uwezo
wake wa kuhifadhi hadithi hata akaweza kuhifadhi hadithi nyingi kuwapita
Masahaba wote.
Khalid: Hii
inatokana na dua aliyoombewa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pale Abu
Hurairah (Radhiya Llahu anhu) alipomuendea Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) kumshitakia udhaifu wake wa kuhifadhi, na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akamwambia; ‘‘Itandaze nguo yako’’, na alipoitandaza (Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akamuombea dua) kisha akamwambia; ‘Sasa jifunike nayo
kifuani pako’, akajifunika na tokea siku hiyo hakusahau tena hadithi.
Haydar: Hadithi hii ngeni kwangu, je umewahi
kuifanyia tahakiki ewe ndugu Khalid ?
Khalid: Hadithi
hii imesimuliwa na Bukhari na wengineo kwa hivyo ni sahihi Alhamdulillah, na
hadithi hii haimo ndani ya vitabu vya maulamaa wa Kisunni peke yao, bali imo
hata ndani ya vitabu vya hadithi vya Kishia.
Imeandikwa
katika kitabu cha ‘Al Kharaij’ (1/75) na katika ‘Bihar al Anwar’ (18/913)
mlango wa ‘Miujiza ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kukubaliwa kwa
dua zake’ kuwa; Abu Hurairah alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam); ‘Mimi nasikia kutoka kwako hadithi nyingi kisha nazisahau’
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia; ‘Tandaza guo lako lote’,
akatandaza kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akauweka mkono wake
ndani yake kisha akamwambia; ‘Jifunike nalo’, ‘nikajifunika’ anasema Abu
Hurairah; ‘na tokea siku hiyo sijasahau tena hadithi’.
Haydar: Lakini kinachoshangaza ni kuwa Abu
Hurairah huyu amesimuliwa hadithi nyingi zisizoweza kulingana na muda wake
mfupi tokea aliposilimu.
Khalid: Kwa
kuanzia ndugu Haydar, ningependa kukuuliza iwapo unazijuwa idadi ya hadithi
alizozisimuliwa Abu Hurairah?
Haydar: Maelfu kwa maelfu ya hadithi.
Khalid: Jaribu kunipa idadi sahihi, kwani
katika vitabu sita maarufu vya Masunni na katika Muwata-a cha Imam Malik
hadithi za Abu Hurairah zilizopokelewa ndani yake idadi yake ni 2218
zilizokubaliwa na katika vitabu vya Sahih Bukhari na Sahih Muslim mna hadithi 609
tu za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) na walizokubaliana juu yake Bukhari na
Muslim ni 326, ziko wapi sasa hizo hadithi maelfu kwa maelfu?
Haydar: Si mimi ninayesema hivyo, haya ni
maneno ninayowasikia maulamaa wetu wengi wanapozungumza juu ya mtu huyu.
Khalid: Masahaba
wengi na maulamaa wengi pia wamemsifia sana Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu)
na wameisifia elimu yake pia, mfano wa Abu Saeed al Khudary (Radhiya Llahu
anhu) aliposema;
‘Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema kuwa ‘Abu Hurairah ni chombo cha
elimu.’
Imam Shafi naye alisema;
“Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) hodari wa kuhifadhi kupita wote wenye
kuhifadhi hadithi katika wakati wake”.
Ama Imam Bukhari yeye
amesema yafuatayo juu ya Abu Hurairah; “Maulamaa wapatao mia nane wamepokea
hadithi kutoka kwake, na alikuwa hodari wa kuhifadhi kupita watu wote wa elimu
ya hadithi wa zama zake.”
Haydar: Lakini anacholaumiwa Abu Hurairah ni
kuwa hapana mtu yeyote duniani aliyewahi kusimulia hadithi nyingi kuliko yeye. Hapana
mwanadamu yeyote anayeweza kuhifadhi hadithi nyingi kama hizo.
Khalid: Kwanza
kabisa uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi unatokana na baraka za ile dua
aliyoombewa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Pili Mtu
aliyekiwishajitolea kutafuta elimu na kusikiliza hadithi za Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) ataweza kweli kushindwa kukusanya idadi hiyo ya hadithi?
Tatu Abu Hurairah (Radhiya
Llahu anhu) alikuwa na wanafunzi wengi waliopokea kutoka kwake hadithi hizo.
Nne Hadithi
alizozisimuliwa Abu Hurairah zimo ndani yake maneno ya Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) na zingine ni juu ya matendo ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) na nyingine ni juu ya matendo ya baadhi ya Masahaba yaliyokubaliwa na
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Tano
Zipo hadithi ambazo Abu Hurairah amesimulia juu ya aliyoyasikia kutoka kwa
Masahaba (Radhiya Llahu anhu) yale ambayo Masahaba hao waliyasikia kutoka kwa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Sita
zipo hadithi nyingi pia zisizosihi isnadi, yaani hadithi alosingiziwa tu Abu
Hurairah kuwa amesimulia wakati yeye hakuzisimulia hadithi hizo.
Saba
kupania kwake Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kwa ajili ya kuifanya kazi hii
tu. Yaani kuzikusanya hadithi za Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam).
Nane Ulizungumza juu ya uwezo wake wa kuhifadhi hadithi ukasema kuwa hapana mwanadamu anayeweza
kuhifadhi namna hiyo. Sasa mimi nitakuuliza suali; Uwezo upi unaoshangaza
zaidi, ule wa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuhifadhi hadithi elfu chache
alizozisikia kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa muda wa miaka
mitano au ule wa yule aliyehadithia maelfu kwa maelfu ya hadithi?
Haydar: Pengine unawakusudia Maimamu wetu!
Khalid: Wala si katika Maimamu, bali hawa ni watu wa kawaida tu na hawaifikii hata chembe
daraja ya Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu), na mmoja wao ni Aban Bin Taghalab
ambaye Al Sadeq amesema juu yake; “Hakika Aban Bin Taghalab amesimulia hadithi
zangu 30,000, kwa hivyo na nyinyi zisimulieni”.
Na mwengine Muhammad bin Muslim bin Rabah,
huyu amesema juu yake An Najashi katika kitabu chake kiitwacho Al Rijal ukurasa
wa 163 kuwa; ‘Muhammad amepokea kutoka kwa Al Baqer hadithi 30,000 na amepokea
kutoka kwa Al Sadiq hadithi 16,000.’
Na mwengine Jaber bin Yazid al Juafiy
aliyesimulia hadithi nyingi sana za watu wa Nyumba ya
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ambaye Al Koshy katika tarjima yake
uk.194 akimnukuu mtu huyu ameandika yafuatayo; “Nimehadithiwa hadithi 50,000
hajapata kuzisikia mwengine isipokuwa mimi”.
Na Al Hurr al Amiliy ameandika katika
hitimisho la kitabu chake kiitwacho ‘Wasael’ (20/151) kutoka kwa Jabir
yafuatayo; “Kuwa yeye amehadithiwa hadithi 70,000 kutoka kwa Al Baqer na
amehadithia hadithi zipatazo140,000.
Sasa tukirudia suali
lako; Je hadithi alizozisimulia Abu Hurairah zinaweza hata kukaribia idadi ya
hadithi alosimulia mtu huyu? Kwa kukupa habari tu,
Abu l Al Husayn huyu
ameandika kitabu kiitwacho ‘Al Muraja-at’ ambacho ndani yake amewasifia sana na
kuwatetea watu hawa walohadithia maelfu kwa maelfu ya hadithi, kwa nini basi
asingefanya uadilifu angalau kidogo akamtetea na Abu Hurairah (Radhiya Llahu
anhu) pia?
Haydar: Lakini wapokeaji wa
hadithi wa madhehebu ya Kishia Mwenyezi Mungu awarehemu wanajulikana kuwa ni
watu wema na waadilifu na wanajulikana pia kwa uwezo wao mkubwa wa kuhifadhi.
Tafadhali usizikanushe fadhila hizi ewe Khalid.
Khalid: Ama
kuhusu uwezo wa kuhifadhi, jambo hili halina haja hata kuzungumza juu yake,
kwani hadithi zilizoandikwa ndani ya vitabu vyenu vya asili zinagongana na
kupingana. Ama kuhusu wema wao lau kama ungesoma kidogo tu katika vitabu vya
kishia mfano kitabu kiitwacho ‘Rijal al Koshy’, nk. ungeujuwa vizuri wema wao
watu hawa waliohadithia hadithi kwa maelfu. Na
hapa nakunukulia riwaya iliyoandikwa katika kitabu hiki cha ‘Rijal al
Koshy’ uk. 95 inayomzungumzia juu ya mmoja wa watu hao aitwae al Uqaili.
Anasema Al Koshy: “Al Uqaili alikuwa miongoni mwa masahaba wa Amiri l Muuminin,
na alikuwa mlevi wa kutupwa lakini alikuwa akihadithia hadithi kama alivyokuwa
akizipokea.”
Na Abu Hamza al Thamali
Thabit bin Dinar naye pia alikuwa mlevi kama ilivyoandikwa katika kitabu hicho
cha Al Koshy uk. wa 76.
Ali bin Hamza al
Batainiy alikuwa akiiba pesa za Al Maasum na khums wanazolipa maimamu wa
kishia, na hata amefikia kulaaniwa na kuambiwa kuwa ni muongo. Yote haya
yanapatikana katika kitabu kiitwacho ‘Al Waqifiyah dirasah tahaliyliyah
(1/418)’. Na wengi wengineo. Kwa hivyo katika vitabu vya Mashia si muhimu kwao
uadilifu wa msimuliaji wa hadithi, inatosha tu msimuliaji huo awe ni mtu
anayewapenda Ahli l Bayt basi hadithi zake zitakubalika na si muhimu hata kama
atakuwa muongo au mlevi au mwizi au awe fasiqi namna gani.
Haydar: Juu ya yote uliyosema ewe ndugu Khalid,
lakini hizi riwaya za Abu Hurairah hazikubaliwi na maulamaa wetu na hii ndiyo
sababu huwezi kuziona ndani ya vitabu vyetu.riwaya za mtu huyu.
Khalid: Ndugu
Haydar naona bora nimalize mazungumzo haya mazuri baina yetu kwa kukujulisha
kuwa Mashia waliotangulia walikuwa wakiziandika na kuzifanyia kazi hadithi za
Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu), na pia maneno yake na fatwa zake zote hizo
zilikuwa zikiandikwa na maulamaa wengi wa mwanzo wa Kishia na walikuwa
wakizifanyia kazi pia na utazikuta kwa mfano katika kitabu cha Mirza Al Husayn Nuri al Tubrusi katika kitabu chake kiitwacho
Mustadrak al Wasael. Ndani ya kitabu hicho ameandika hadithi nyingi za Abu
Hurairah (Radhiya Llahu anhu) katika mlango wa ‘Al Ijarah’ (14/28), bali Sheikh
al Mufiyd pia ameandika hadithi nyingi za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu)
katika kitabu chake kiitwacho Al Amaliy na utazikuta katika ukurasa
111-112-113.
Na Sheikh Al Saduq naye
pia katika kitabu cha ‘Maaniy al akhbar’ ukurasa wa 80-90 ameandika hadithi
zake, na pia katika kitabu ‘Ikmal al din’, ukurasa wa 136, na katika kitabu cha
Al Khiswal wa thawab al aamal pia na katika vitabu vingi vinginevyo. Kwa nini basi unakanusha tu kabla ya hata kuangalia
kwanza ndani ya vitabu? Daima mimi husema
kuwa tatizo la vijana wa Kishia wenye kupenda kheri huwa hawapendi kusoma vile
vitabu vya asili vya Kishia na pia hawaulizi dalili kutoka kwa mashekhe wao,
bali wao wanasema tu kila wanachoambiwa na wale mashekhe wanaopenda kuzungumza
bila dalili.
Haydar: Unataka kuniambia kuwa yote wanayosema wanavyuoni wetu juu
ya mtu huyu si ya kweli?
Khalid: Ndiyo ewe ndugu Haydar, kwani maulamaa
wote wa Ahlu Sunnah wamekubaliana juu ya ukweli wa riwaya zake Sahaba huyu
mtukufu (Radhiya Llahu anhu), na pia maulamaa wa Kishia waliotangulia nao pia
wamezikubali riwaya zake, na kama utasoma vitabu vyenu vilivyoandikwa na
maulamaa wa zamani basi hutamuona yeyote kati ya maulamaa wenu mwenye kumchukia
au mwenye kuzikataa riwaya zake isipokuwa mtu mjinga ambaye Mwenyezi Mungu
hakumfungua kifua chake apate kunufaika na elimu iliyo sahihi. Na lau kama utamuuliza yeyote anayemtukana au anayejaribu
kumuondolea hadhi yake Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) ‘Kwa nini unamchukia
Sahaba huyu namna hii? Umesoma nini juu sira ya Sahaba huyu?
Ameukosea nini Uislamu?’ Hutoweza kupata jawabu yoyote itakayokukinaisha, kwani tuhuma zote hizo
zinatokana na ujinga wa watu wachache wasiosoma chochote katika vitabu vya
Kisunni wala vya Kishia.
Haydar: Lakini anayezitoa makosa hadithi za Abu
Hurairah hufanya hivyo kwa ajili ya kuitakia kheri elimu hii ya hadithi isije
ikaingia ndani yake hadithi zisizo sahihi.
Khalid: Wanaojaribu
kumtia ila Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kusudi lao hasa ni moja tu; nalo
ni kuitia ila Sunnah iliyotahirika ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam). Na kwa vile hawakupata njia nyingine ya kuitia ila, wakaona
bora wawatie ila waliotunukulia Sunnah hiyo, na kwa vile Abu Hurairah (Radhiya
Llahu anhu) ndiye mashuhuri kupita wote na ndiye aliyesimulia riwaya nyingi
zaidi kupita wote ndiyo sababu wakawa wanajaribu kumtia ila.
Ijulikane
kuwa watu kama Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) na walio mfano wake katika
Masahaba watukufu (Radhiya Llahu anhu), Mwenyezi Mungu ndiye aliyewajaalia
kuifanya kazi hii ya kutufikishia Sunnah hii tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam). Sunnah ambayo ndani yake yamo mafundisho na sheria
anayoipenda Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo. Na sisi tunawapenda kwa ajili
hiyo na kwa ajili ya mengi mema waliyo nayo.
Ndugu
msomaji,
Baada
ya mazungumzo matulivu haya pamoja na maneno yenye hekima yaliyoegemzewa dalili
zilizo wazi kutoka katika vitabu vikubwa vinavyotambulikana pamoja na masdari
zinazotegemewa, hatuna budi kuikubali haki na kufikiri vizuri kabla hatujatoa
uamuzi wowote juu ya upande mwengine.
Inajulikana
pia na kila mtu kuwa mazungumzo baina ya Shia na Sunni siku zote yanakuwa
makali yaliyojaa shutuma na mwisho wake huwa hayaleti manufaa yoyote.
Kabla
ya mazungumzo yoyote baina ya pande mbili hizi, zinawajibika pande zote zijaalie
na kuzihusisha nia zao ziwe halisi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala, na kusudi la mazungumzo yao liwe kwa ajili ya kuifikia njia ya haki, na
njia ya kuifikia haki ni moja tu, nayo ni ile tuliyoitumia katika mazungumzo
yetu haya.katika kuleta hoja na dalili zenye nguvu pamoja na ufasaha wa maneno.
Msomaji
ataona kuwa katika mazungumzo haya hamna ndani yake ujeuri wala matusi dhidi ya
mtu yeyote, isipokuwa tu tumezitaja fatwa mbali mbali na kuzungumza juu yake.
Huenda
mazungumzo haya yakawa hayakujadili mambo yote yanayopaswa kuyajadiliwa baina
ya Shia na Sunni, lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutoa
mwangaza katika mambo mengi, pamojua na kutuwezesha kuwajilsha watu juu ya yale
yasiyokuwa yakijulikana.
Namuomba
Mwenyezi Mungu azijaalie kurasa hizi ziwe zenye manufaa kwa watu na hatuna haja
ya chochote isipokuwa tu watu wote wawe wafuasi wa Muhammad (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) kwa kufuata dalili zilizo sahihi, huku tukimuomba Mwenyezi
Mungu atufufuwe sote chini ya kivuli cha Uislamu tukiwa kama ndugu
tunaopendana.
Mwenyezi
Mungu ni muweza wa yote hayo, na mwisho kabisa wa maneno yetu tunasema
‘Alhamdulillahi rabbil aalamiyn’, na sala na salaam zimfikie Mtume wetu
Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pamoja na aali zake na Sahaba zake
wema.