|
Hadithi ya Al Jassaasah Imetafsiriwa na Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Utafiti mwingi
uliofanywa na wazungu wenye kufuatilia mambo ya ulimwengu wa Mashariki (Orientalists)
juu ya dini ya Kiislamu na juu ya Mtume wa Waislamu katika nadharia zao
wanaitakidi kuwa mengi kati ya yaliyomo ndani ya mafundisho ya dini ni miongoni
mwa itikadi zilizokuwepo wakati ule alioishi Mtume (Swallah Llahu alayhi
wa sallam). Kwa maana nyingine ni
kuwa kwa vile Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
aliishi karibu na Mayahudi na Manasara, akaingiliana nao, na wakaingia baadhi
Kusudi la nadharia yao
hii ni kuingiza shaka katika utukufu wa ujumbe huu wa mwisho kwa njia ya kuwaambia
watu kuwa; Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)
hakuja na kipya katika mambo ya Ghaibu na mambo ya Imani, na kwamba yote
anayofundisha ni katika itikadi na ibada zilizokuwepo tokea mwanzo. Utayaona hayo kwa
uwazi katika kamusi mbalimbali za maarifa na vitabu vilivyowekwa kwa ajili ya
kuwafundisha watu juu ya dini ya Kiislamu, elimu yake na viongozi wake
likiwemo kamusi maarufu 'Daairat al maarif al Islamiyah',
walioshirikiana kuliandika wengi katika watu maarufu wenye kushughulikia
mambo ya ulimwengu wa Mashariki. Tutakuta kwa mfano waliyoandika kuhusu 'Tamiym al
Daariy', ambaye yumo katika maudhui yetu haya. Anasema mtaalamu wa mambo ya ulimwengu wa Mashariki
kutoka Italia Levy Dalavida: "Na Tamiym alikuwa mfuasi wa dini
ya Kinasara kama walivyokuwa wengi kati ya waarabu wa Syria, akafanikiwa
kumfundisha Mtume juu ya ibada nyingi alizojifunza katika dini ya kinasara….
Na inasemekana kuwa Tamiym ndiye wa mwanzo kumhadithia Mtume visa mbalimbali
vya dini, Mtume akavisadiki na kuwahadithia watu." (Mwisho wa maneno ya Levy) Wakaja
wapungufu wa elimu waliofuata maneno haya ya wataalamu hawa wa ulimwengu wa
Mashariki na kuyakubali maneno Sisi
hatukanushi kuwa zipo hadithi nyingi za watu wa kitabu, pamoja na tafsiri zao
zilizojipenyeza ndani ya vitabu vyetu, na hizi ni habari na visa maarufu
ziliokwishatajwa na maulamaa na kuzibainisha kwa watu. Lakini kutumia
kisingizio hiki kwa ajili ya kuzikataa hadithi sahihi zilizothibiti, au
kuzitumia kwa ajili ya kuwatuhumu Masahaba (Radhiya Llahu an'hum),
walioisimamia na kuisimamisha dini hii, ni jambo lisilokubaliwa na Muislamu
yeyote. Mjadala uliozushwa zaidi kuhusu
riwaya za Tamiym ni juu ya kisa cha Al Jassasah kilichomo ndani
ya Sahih Muslim. Kisa hiki kilisimuliwa na Na kisa chenyewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) alikaa juu ya membari huku akicheka akasema: "Kila mtu aushikilie vizuri mswala wake. Kisha
akasema: "Mnajua kwa nini nimekukusanyeni (nimekuiteni)?" Wakasema:
"Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaojua." Akasema:
"Mimi wallahi sikukuiteni kwa ajili ya kukupendezesheni wala
kukutisheni, lakini nimekuiteni kwa sababu Tamiym Al Daariy aliyekuwa
akifuata dini ya kinasara amekuja kufungamana na mimi na kusilimu. Na
amenihadithia hadithi inayokubaliana na niliyokuwa nikikuhadithieni juu ya Masiyh
Ad Dajjal. Amenihadithia kuwa: "Tulipanda merikebu baharini
pamoja na wanaume thelathini wa kabila la Lakhm na Judham, na mawimbi yakatuchezea
baharini mwezi mzima, mpaka tulipokifikia kisiwa wakati wa magharibi na watu
wakakaa ukingoni mwa merikebu (au juu ya ngalawa ya kushushia watu).
Wakaingia kisiwani wakamkuta mnyama mwenye nywele nyingi Wakasema: "Ole wako! Nani
wewe?" Akasema: "Mimi ndiye
Jassaasah." Wakasema: "Nini
Jassaasah?" Akasema: "Enyi watu, nendeni
kwa huyu mtu kijijini hakika yeye atakuwa na hamu kubwa ya kujua habari zenu."
Akasema: "Alipotutajia jina Tukamuambia: "Ole wako, nani
wewe?" Akasema: "Mumekwishazijua
habari zangu, nihadithieni juu yenu. Ni nani nyinyi?" Wakasema: "Sisi ni watu katika
waarabu, tulisafiri kwa merikebu na ikasadifu bahari kuchafuka. Mawimbi
yakatucheza muda wa mwezi kisha tukateremka katika kisiwa chako hiki. Tukakaa
ukingoni mwa merikebu na tulipoingia kisiwani tukakutana na mnyama mwingi wa
nywele hajulikani wapi mbele wapi nyuma kwa wingi wa nywele tukamuuliza, 'Ole
wako, Nani wewe?' Akasema: 'Mimi ni Jassaasah', tukamuuliza: 'Nini
Jassaasah?' Akatuambia nendeni kwa mtu huyu kijijini atakuwa na hamu ya kujua
habari zenu. Ndipo tulipokujia wewe haraka
na tulimuogopa, tukidhania kuwa anaweza kuwa shetani.' Akasema: Nipeni habari za mitende ya
Biysan.' Tukamuuliza: 'Nini katika habari
zake unataka kujua?' Akasema: 'Nataka kujua juu ya tende
zake. Zishamea? Tukamuambia: 'Ndio'. Akasema: "Hivi karibuni
zitaacha kumea." Akasema: "Nipeni habari za
bahari ya At Twabariyah." Tukamuuliza: "Nini katika
habari zake unataka kujua?" Akasema: "Yamo maji ndani
yake?" Wakasema: "Maji mengi Akasema: "Hakika hivi
karibuni maji yake yatatoweka." Akasema: "Nipeni habari za Ain
Zaatar." Wakasema: "Nini katika habari
zake unataka kujua?' Akasema: "Katika chemchem
yake yamo maji? Wakasema: "Ndiyo, maji mengi
Akasema: "Nipeni habari za Mtume
wa wasiojua kusoma wala kuandika amefanya nini?" Wakasema: "Ameondoka Makka
na kuhamia Yathrib (Madina)." Akasema: "Wamempiga vita
waarabu?" Tukasema: "Ndiyo.' Akasema: "Na yeye amewafanya
nini.? Tukamjulisha kuwa amehamia kwa
waarabu wengine wenye kumuunga mkono na kumtii." Akawaambia: "Yashatokea
hayo?" Tukasema: "Ndiyo." Akasema: "Ama ni bora kwao
kumtii. Na mimi nitakupeni khabari zangu. Mimi ndiye Al Masiy'h, na hivi
karibuni nitapewa idhini ya kutoka na nitatoka na kutembea juu ya ardhi, na wala
sitoacha kijiji ila lazima nikipitie katika muda wa siku arubaini isipokuwa
Makkah na Tiybah (Madina), miji hii ni haramu kwangu kuingia ndani
yake. Kila ninapotaka kuingia katika mojawapo ya miji hiyo, ananikabili
Malaika aliyeshika mkononi mwake upanga ulionolewa akinizuwia. Hakika katika
kila pembe yupo Malaika mwenye kuilinda miji hiyo. Akasema Fatimah: Fatima
binti Qays (Radhiya Llahu an'ha) "Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) alisema huku akichocha
gongo Akasema: "Kwa hakika
imenifurahisha hadithi ya Tamiym kwa kuwa inakubaliana na yale
niliyokuhadithieni na juu ya Madina na Makkah. Hakika atatokea katika bahari
ya Akasema: Maimamu na maulamaa wamekiingiza
kisa hiki ndani ya vitabu vyao katika milango ya sifa za Tamiym (Radhiya
Llahu an'hu) 'Al Iswaabah' 1/368 na katika Fathil
Bari 12/46 na Imam Annawawiy katika Sharhi ya Muslim. Amesema Ibnu Hajar katika Al Iswaabah:
"Ni mashuhuri miongoni mwa Masahaba, alikuwa katika dini ya Manasara
akenda Madina kusilimu." Juu ya kuwa kuwemo hadithi hii
ndani ya Sahih Muslim inatosheleza kulazimika kuikubali, kutokana na daraja
yake na namna umma wote wa Kiislamu ulivyozipokea hadithi zake. Na wapokezi
wote wa hadithi hii ni watu wenye kuaminika, hapana hata mmoja kati yao
mwenye kutuhumiwa, hata hivyo hadithi hii imesimuliwa pia na Imam Ahmad na
Abu Ya'ala na Ibnu Majah, na Abu Daud, na imepokelewa pia kwa njia ya
Masahaba wengine wasiokuwa Fatima binti Qays (Radhiya
Llahu an'ha) kama vile Abu Hurairah na Bibi Aisha na Jabir (Radhiya
Llahu an'hum) ikiwa ni dalili ya kupokelewa kwa njia mbali mbali
na wingi wa njia zake, kwa sababu hadithi hii haikutolewa na Imam Muslim
peke yake na wala haikusimuliwa na
Fatima bint Al Qays peke yake. Amesema Al Hafidh (Mwenyezi Mungu
amrehemu) katika Al Fat'h (13/323):
"Wamekubaliana kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa
sallam) anapokubali linalotendwa au kutamkwa mbele yake asilipinge ni dalili
kuwa jambo Ama kudai kuwa haya si katika
mambo ya dini ambayo Mitume haijakingwa katika kumsadiki mtu muongo, Isitoshe, kama aliyohadithia
Tamiym (Radhiya Llahu an'hu) ni kisa
cha uongo ingewezekana kweli wahyi usiteremshwe kukikanusha kisa hicho na
kuubainisha ukweli wake, kama ilivyowahi kutokea mara nyingi wakati wanafik
na wenzao walipokuwa wakisema kinyume na waliyoficha nyoyoni mwao, na wahyi
ukawa unateremka kuwafedhehesha na kubainisha uongo wao? Juu ya kuwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) kesha hadithia mara nyingi juu
ya Ad Dajjal na kuteremka kwa Isa bin Maryam (Alayhis Salaam) katika zama
za mwisho akihukumu kwa uadilifu kwa kutumia sheria ya Mtume wetu (Swalla
Laahu alayhi wa sallam), na kwa mikono yake atamuua Ad Dajjal. Yote haya yamesimuliwa kwa njia
nyingi Hata kama tutachukulia kuwa
hadithi hii ni katika Israiliyat, basi ni katika zile sahihi zinazokubalika
ambazo tunapaswa kuzikubali kutokana na kukubaliana na sheria yetu. Dalili ya maneno haya ni kauli ya
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) aliposema: "Na
amenihadithia hadithi inayokubaliana na niliyokuwa nikikuhadithieni juu ya
Masiyh Ad Dajjal…" Na wengi katika wafasiri
wameitafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu: "Na kauli (ya kuja
kwa Kiama) itakapowathibitikia tutawatolea mnyama katika ardhi
atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya zetu.' An Naml - 82 Wanasema kuwa myama huyo ni huyu
Al Jassaasah aliyetajwa katika hadithi ya Tamiym, Kwa kumaliza tunasema kuwa
hadithi ni sahihi, na inazipa nguvu hadithi za Ad Dajjal na zile za dalili ya
kukaribia kwa Siku ya Kiama. Kwa hivyo kumtuhumu Tamiym (Radhiya
Llahu an'hu) kuwa ni muongo na kwamba kaja kuuchafua uislamu ni
tuhuma mbaya kwa sahaba huyu mtukufu (Radhiya
Llahu an'hu) ambaye sira yake inashuhudia kuwa ni
mcha Mungu na mwingi wa kufanya ibada na wema, bali ni kumtuhumu Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) pamoja na ujumbe wake,
na hili linatosha kuwa ni dhambi kubwa na uovu ulio dhahiri. |