Kiongozi wa
Kabila la Janjaweed
Nitakubali ikiwa makundi yote yatakubali
kuweka silaha zao chini

Musa Hilal
Kutoka Islam Online
Akizungumza na Islam Online Bw. Musa Hilal kiongozi wa kabila la Waarabu la Janjaweed huko Sudan alisema kuwa watu wake watakubali kuweka silaha zao chini na kujisalimisha mbele ya serikali ya Sudan iwapo makundi yote yenye silaha huko Darfur yatakubali kufanya hivyo pia.
Akijibu tuhuma za seikali ya Marekani pamoja na azimio la Umoja wa Mataifa la hivi karibuni lionaloitaka serikali ya Sudan kuwalazimisha watu wa kabila la Janjaweed kusalimisha silaha zao serikalini katika muda usiozidi mwezi mmoja Bw.Musa alisema: Azimio la Umoja wa Mataifa la kuwataka watu wa kabila lake kutupa silaha zao chini lazima lijumuishe makundi yote yanayopambana huko Darfur na si kabila lake peke yake.
Miongoni mwa
makundi muhimu yanayopambana na
serikali ya
Akieleza juu ya kukubali kwake azimio la Umoja wa Mataifa linalohusu mkoa wa Darfur Bw. Hilal alieleza kutoridhika kwake juu ya ibara inayowataka watu wa kabila lake la Janjaweed peke yao kutupa silaha zao chini, akasema: Ikiwa ni watu wa kabila langu peke yao ndio wanotakiwa kuranya hivyo basi sitokubali hata kulisoma azimio hilo.. Kwa mantiki gani wanazungumza hawa kuwa sisi peke yetu tutupe silaha zetu chini kisha tuwe mawindo mepesi ya kuanzgamizwa na wengine?
Jina la Bw.
Hilal linabeba nambari 1 katika orodha iliyowekwa na Serikali
ya Kimarekani yenye majina ya
viongozi 7 wa makabila ya Janjaweed
ya Kiarabu. Orodha hiyo inawatuhumu
watu hao kuwa waliwaua na kuwaunguza watu wa makabila
ya Kiafrika katika mkoa wa
Hilal aitahadharisha serikali
ya Kimarekani
Hilal aliitahadharisha serikali ya Kimarekani
pamoja na
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuwa wasije wakaingia katika shimo la upotofu unaozushwa na makundi
ya waasi wa
Haki kwa
wote
Bw. Hilal
aliongeza kusema: Ikiwa wanataka kutoa uamuzi wowote
dhidi yangu, basi mimi
sina kipingamizi, lakini lazima kwanza ufanyike uchunguzi kwa njia ya
uadilifu, na ni wajibu wao
kuchgua kamati itakayotafuta ukweli bila ya upendeleo,
na isiwe kusudi
Alisema pia kuwa mahkama itakayohukumu kwa uadilifu itamtakasa na tuhuma za uongo walizomzulia.
Bw. Hilal
alipendekeza ufanyike mkutano utakaojumuisha makundi yote kwa ajili ya kupatanisha na kuweka misingi
ya amani na kuondoa matatizo
yote yaliyorimbikika. Alisema: Napendekeza litafutwe suluhisho la daima, na
pande zote - zile zenye asili
ya Kiarabu na zenye asili
ya Kiafrika zipate haki zao
sawa sawa. Na sisi hatuna chuki
dhidi ya kundi lolote lile
na wala
hatutaki kupewa na yeyote, si
serikali wala upinzani. Sisi tupo hapa tokea
mamia ya miaka iliyopita na hatutaki
jengine isipokuwa kubaki. Na maslahi yetu pia yaendelee
Sisi ndio tuliodhurika
zaidi
Bw. Hilal
alisema pia kuwa waliodhurika zaidi na
matukio ya
Akasema: Tokea
mwaka 1980 walikuwa wakieneza chuki dhidi yetu, wakitaka
Waarabu wafukuzwe nje ya Mkoa
wa Magharibi
ya
Aliendelea kusema:
Lakini serikali zote zilizotangulia ikiwemo hii ya
Muhammad Al Bashir zilipuuza
tahadhari zetu na kutuacha
peke yetu tukipambana na waasi wenye asili
ya Kiafrika waliopewa mafunzo ya kisasa ya
kupigana vita pamoja na silaha za
kisasa na wala hatukuwahi hata siku moja
kuusikia Umoja wa Mataifa ukisema
lolote kutaka tusishambuliwe
Bw. Hilal
alikanusha kuwa anapigana vita dhidi ya makabila ya
Kiafrika kwa ajili ya kuisaidia
serikali ya
Tulichowahi kufanya sisi ni kujiunga na jeshi la ukombozi pale serikali ilipotangaza kuunda jeshi la kupambana na waasi, na vijana wetu wapatao elfu 3 walijiunga na jeshi hilo ambalo ndani yake hayakuwepo makabila ya Kiarabu peke yake, bali makabila ya Kiafrika yanayotokana na makabila hayo ya Al For na Zaghawa na Samalit pia yalijiunga na jeshi hilo wale waliokuwa wakipinga uasi.
Alipoulizwa; Kwa nini basi hatuoni wakimbizi kutoka makabila ya Kiarabu katika kambi za Darfur Bw Hilal alisema: Walituunguzia vijiji vyetu vingi sana, na wengi kati ya watu wa makabila yetu iliwalibidi kuacha nyumba zao, lakini sisi Waarabu hatukubali kuwapeleka wanawake zetu na na watoto wetu katika kambi za wakimbizi wakaomba chakula na nguo kutoka katika jumuiya za kusaidia watu, bali sisi wenyewe tunawahami na kuwaweka katika majumba yetu na kuwalisha na kuwavisha katika chakula chetu.