HUYU ANATAHARUKI
Muhammad Faraj
Huyu anataharuki na yule anakimbia
Wazama hawaibuki kwa anasa za dunia
Ana tabu makhuluqi dunia kun'gan'gania
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Anadhani haondoki milele atabakia
Hajali hashughuliki ya
kesho kufikiria
Atapoitwa na Haki hana
pa kukimbilia
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Hapana kitachobaki wala
kitachosalia
Ila
Wajihi wa Haki uso wa Mola
Jalia
Huwezi sema
sitaki wala hata kukimbia
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Kila kitu
tahiliki Qurani yatuambia
Sasa kwa nini hutaki mbegu njema kufukia
Upate njema
riziki na rehema
za Jalia
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Allahu wetu
khaliqi mengi katutunikia
Sisahau yako
haki sehemuyo ya dunia
Na hayo uyadiriki Mola
alivyousia
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Kwa wema
uwe shabiki watu kuwatunukia
Hata asostahiki wewe uwe maridhia
Ufisadi ni halaki iepuke
yake njia
Kila kitu
tahiliki ila uso wa
Jalia
Mola wetu
warehemu walokwisha tangulia
Nanyi mlobaki
humu msidhani tabakia
Angebaki muadhamu habibi wetu Nabia
Hapana atayebaki ila uso wa
Jalia