Yaliyomo
Siku
ile alipofukuzwa Peponi na kutolewa katika rehma ya Mwenyezi Mungu, Ibilisi
aliapa kuwa atazifisidi ibada za wanadamu na kuwakalia juu ya kila njia iliyonyoka.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
ÞóÇáó
ÝóÈöãóÇ ÃóÛúæóíúÊóäöí áÃóÞúÚõÏóäøó áóåõãú ÕöÑóÇØóßó ÇáúãõÓúÊóÞöíãó
“Akasema
(Ibilisi); ‘Kwa kuwa umenihukumia upotofu (upotevu) basi nitawakalia (waja
Wako) katika njia Yako iliyonyoka (ili niwapoteze).”
Al
Aaraf – 16
Ibilisi
hawaandami waliokwishapotoka, lakini moyo wake unaungulika kila anapowaona
walio juu ya njia iliyonyoka wakiswali na kufanya ibada zao sawa kama
walivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.
Ili
kuzifisidi ibada zao, Ibilisi hutumia hila nyingi zikiwemo:-
1.
Kuwatia wasi wasi.
1.
Kuwafanya wahisi tabu au dhiki
wanapoanza kufanya ibada.
2.
Kuwapambia ibada za uzushi na
kuwafanya waongeze au wapunguze.
Katika
kitabu chake kiitwacho ‘Talbis Iblis’ (Upambaji wa Ibilisi), mwanachuoni
maarufu Sheikhul Islam Ibni Taymiyah anasema:
“Juwa ya kwamba mlango mkubwa
anaopitia Iblisi katika kuwaharibia Waislam ibada zao ni mlango wa ‘ujinga
katika dini’. Iblisi huwaingilia watu kwa kupenya kupitia mlango huo kwa raha
zake huku akiwa amestarehe kabisa. Kwani Ibilisi keshawaharibia wengi miongoni
mwa wafanyao ibada kwa ajili ya kutokujuwa kwao namna ya kumuabudu Mola wao
kama anavyotaka kuabudiwa. Ama wale wenye kufahamu, Ibilisi huwaingilia kwa
kuibia ibia tu.”
Mmoja katika maulamaa wakubwa aitwae Matraf
bin Abdullah amesema:
“Fadhila ya elimu ni kubwa
kupita fadhila ya ibada”.
Na hii ni kwa sababu elimu ni nuru
inayomuongoza mja kuijuwa njia sahihi ya kumuabudu Mola wake bila kupunguza
wala kuvuka mipaka. Na Mwenyezi Mungu amekwisha tuelimisha kupitia kwa Mtume
wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam), namna gani anatutaka tumuabudu.
Mwenyezi Mungu Anasema:
Ëõãøó
ÌóÚóáúäóÇßó Úóáóì ÔóÑöíÚóÉò ãøöäó ÇáÇãúÑö ÝóÇÊøóÈöÚúåóÇ æóáÇ ÊóÊøóÈöÚú ÃóåúæóÇÁ
ÇáøóÐöíäó áÇ íóÚúáóãõæäó
“Kisha tumekuweka juu ya Sharia ya amri yetu, basi ifuate, wala
usifuate matamanio ya wale wasiojua (kitu).”
Al Jathiya – 18
Ibilisi pia humfisidia mtu ibada zake kwa
kumtia wasi wasi akiwa ndani ya ibada na kumfanya ahisi kama kwamba hajaifanya
vizuri, hajaikamilisha, ina kasoro, udhu wake haukutimia nk. Na kutokana na
hayo humfanya aongeze katika Swala au katika udhu, akidhani kuwa hiyo ndiyo sahihi
inayomridhisha Mola wake, bila kuelewa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Ibada yoyote isiyokuwa na amri ya Mwenyezi
Mungu au ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) haifai na
haina uzito wowote juu ya mezani.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
Þõáú
åóáú äõäóÈøöÆõßõãú ÈöÇáÃÎúÓóÑöíäó ÃóÚúãóÇáÇ. ÇáøóÐöíäó Öóáøó ÓóÚúíõåõãú Ýöí
ÇáúÍóíóÇÉö ÇáÏøõäúíóÇ æóåõãú íóÍúÓóÈõæäó Ãóäøóåõãú íõÍúÓöäõæäó ÕõäúÚðÇ.
“Sema;
‘Je! Tukujulisheni wenye hasara katika vitendo (vyao)?. Hao ambao bidii zao
(hapa duniani) zimepotea bure katika maisha ya dunia, nao wanafikiri kwamba
wanafanya amali njema !”
Al
Kahf – 103 – 104
Katika
kuzifasiri aya hizi, anasema Ibni Kathiyr kuwa; Aliy bin Abi Talib (Radhiya
Llahu anhu) amesema:
“Aya hii inamsibu kila mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu kinyume
na mafundisho ya Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na huyo anakuwa
mbali na njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu, akidhani kuwa amali yake hiyo
inakubaliwa, wakati ukweli ni kuwa anafanya makosa, na amali zake hizo
zinapotea bure.”
Mwenyezi
Mungu pia Anasema:
Þõáú
Åöä ßõäÊõãú ÊõÍöÈøõæäó Çááøåó ÝóÇÊøóÈöÚõæäöí íõÍúÈöÈúßõãõ Çááøåõ æóíóÛúÝöÑú
áóßõãú ÐõäõæÈóßõãú æóÇááøåõ ÛóÝõæÑñ ÑøóÍöíãñ
“Sema; ‘Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni;
(hapo) Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye rehema”.
Aali
Imran – 31
Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:
íóÇ
Ãóåúáó ÇáúßöÊóÇÈö áÇó ÊóÛúáõæÇú Ýöí Ïöíäößõãú æóáÇó ÊóÞõæáõæÇú Úóáóì Çááøåö
ÅöáÇøó ÇáúÍóÞøö
“Enyi
watu wa kitabu msipindukie mipaka katika dini yenu wala msiseme juu ya Mwenyezi
Mungu ila yaliyo kweli”.
An
Nisaa – 171
Na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ametukataza kuvuka
mipaka katika ibada na kuifanya iwe nzito, kwani yeye (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) ameletwa ili kutuwepesishia na si kuyafanyia mambo kuwa magumu.
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mumeletwa ili muwepesishe na hamkuletwa kuyafanya mambo yakawa
magumu”
Bukhari
– Attirmidhy – Al Bayhaqi – Annasaiy – Imam Ahmad
Na
katika hadithi iliyopokelewa na Imam Ahmad na Annasai, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Msipindukie mipaka katika dini kwani kilichowaangamiza
waliokuja kabla yenu ni kupindukia mipaka katika dini”.
Dalili
juu ya ubaya wa kuzusha au kupindukia mipaka katika ibada imo katika hadithi ifuatayo
iliyopokelewa na Bukhari na Muslim na kusimuliwa na Anas (Radhiya Llahu anhu)
inayosema:
“Watu watatu walikwenda katika kila nyumba ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kuwauliza wakeze (wakitaka kujuwa)
namna gani Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akifanya ibada zake,
na baada ya kujulishwa, mmoja wao akasema:
“Sisi wapi na Mtume wapi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amekwisha samehewa madhambi yake yote yaliyotangulia na
yanayokuja. Ama mimi nitakuwa nikiswali usiku kucha wala sitolala”.
Mwengine akasema:
“Na mimi nitafunga siku zote na wala sitokula mchana tena”.
Wa tatu akasema:
“Ama mimi sitofunga ndoa kabisa (ili niweze kufanya ibada zangu
vizuri).”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
aliporudi na kuhadithiwa, alipanda juu ya membari akasema:
“Nimesikia kuwa watu wanasema hivi na vile. Ama yule anayemjuwa
Mwenyezi Mungu zaidi na kumuogopa zaidi kuliko wote ni mimi. Lakini mimi
ninafunga na ninakula. ninaamka usiku kuswali na (pia) ninalala, na ninaoa
wanawake. Kwa hivyo yeyote atakayekwenda kinyume na mafundisho yangu basi huyo
hayuko pamoja nami”.
Hadithi
hii inatufundisha umuhimu wa kufuata na ubaya wa kuzusha. Umuhimu wa
kusahilisha na ubaya wa kuchupa mipaka katika ibada kwa kisingizio cha
kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu, hata kama nia ni njema. Nia pekee
haitoshi ikiwa ndani yake hamna muongozo wa mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), kwa sababu Mwenyezi Mungu haridhiki na
ibada yoyote isipokuwa ile tu Aliyoitolea amri Yake.
Baadhi
ya watu hawaridhiki wanapotawadha kwa kuosha viungo vyao mara tatu kama
tulivyofundishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Ibilisi anawatia wasiwasi na utawaona wakizidisha idadi ya kuosha kwa
kisingizio cha kuondoa wasiwasi, wakati ukweli ni kuwa huko kuongeza kwao ndio
wasiwasi wenyewe.
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amekataza kuyafanyia israfu
maji.
Siku moja alipomuona mmoja katika Sahaba zake (Radhiya Llahu
anhu) akitawadha, alimuuliza:
“Kwa nini unafanya israfu katika maji?”
Sahaba (Radhiya Llahu anhu) akauliza:
“Kwani hata katika maji pana israfu?”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamuambia:
“Ndiyo. Hata kama unatawadha penye mto wa maji yanayokwenda.”
Imam
Ahmad
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kutawadha kwa kuosha
viungo vyake mara moja moja, aliwahi pia kutawadha kwa kuviosha mara mbili
mbili na mara tatu tatu. Kwenda kinyume na hayo ni kupindukia mipaka katika
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Mtu
mmoja alimuuliza Imam Ahmad bin Hanbal:
“Ninaweza kuongeza zaidi ya mara tatu katika udhu?”
Imam akamjibu:
“La, huwezi. Hafanyi hivyo isipokuwa mwenye maradhi (ya wasi
wasi).”
Imepokelea
kutoka kwa Abu Daud kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
“Kutakuwa na watu katika umati wangu wanaopindukia mipaka katika
kujitwahirisha na katika kuomba dua”
Na
akasema:
“Hakika katika kutia udhu, pana shetani (mwenye kuwatia watu
wasiwasi) anayeitwa Al Walahan, kwa hivyo jiepusheni na wasiwasi wa udhu”.
Attirmidhy
Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:
Åöäøóåõ
áÇó íõÍöÈøõ ÇáúãõÚúÊóÏöíäó
“Yeye
(Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao mipaka”.
Al
Aaraf - 55
Kwa
vile kuzidisha katika udhu wa mwenye wasiwasi ni katika uchupaji wa mipaka,
basi huo unaingia katika zile ibada asizozipenda Mwenyezi Mungu.
Anasema
Ibni Qudama, katika kitabu chake kiitwacho “Dhammi l Muwaswasiyn”:
“Ukimuuliza mwenye wasi wasi kwa nini unatawadha zaidi ya mara
tatu?
Atakujibu: 'Akiba ya maneno, pengine nimekosea au nimepunguza
idadi ya kuosha viungo vyangu.'
“Mtu anaweza kuipa sababu anayoitaka,” anaendelea kusema
mwanachuoni huyo. “Lakini suali linakuja; “Je! Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) au Sahaba zake (Radhiya Llahu anhum) walikuwa wakifanya
hivyo?"
Bila shaka jawabu itakuwa ;’La. Hawakuwa wakifanya hivyo’. Kwa
sababu kusema kuwa walikuwa wakifanya hivyo, ni kuwazulia uongo."
Iwapo
tutakiri kuwa hawakuwa wakifanya hivyo, basi itatulazimu na sisi kuacha
mwenendo huo, kwani kuuendeleza ni kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)”.
Katika
wasiwasi ni pale mtu anapokuwa ndani ya Swala akasikia mingurumo tumboni mwake,
akadhani kuwa upepo umekwishamtoka, akaamua kuvunja Swala na kwenda kutawadha
kwa dhana tu.
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ametukataza kufanya hivyo
aliposema:
“Mmoja wenu anaposikia sauti tumboni mwake akatia shaka, je
kimetoka kitu (upepo) au hakijatoka? Basi asivunje Swala isipokuwa kama (ana
hakika kuwa) amesikia sauti (ikitoka) au harufu”.
Muslim
Imepokelewa pia kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuwa; huwa anahisi kila anaposwali kama
kwamba upepo unamtoka. Akajibiwa kuwa asivunje Swala mpaka asikie sauti au
harufu.
Bukhari
na Muslim
Katika
Musnad ya Imam Ahmad na Sunan za Abu Daud, Imeelezwa na Abu Saeed Al Khodary (Radhiya
Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Shetani humjia mtu katika Swala yake na kumfanya ahisi kama
kwamba ametoa upepo, basi mtu asiivunje Swala yake mpaka asikie sauti au
harufu”.
Na
katika Sunan ya Abu Daud, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
“Shetani anapomjia mtu na kumwambia kuwa udhu wako umevunjia”.
Basi naye asema (moyoni pake); “Muongo wewe”, isipokuwa pale anaposikia harufu
kwa pua yake au sauti kwa sikio lake”.
Katika
kitabu chake kiitwacho; “Dhammi l Muwaswasiyn” , anasema Ibni Qudama:
“Kwa ajili ya kuyapiga vita maradhi ya wasi wasi, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anatuamrisha kumkadhibisha
shetani, juu ya kuwa kitendo hicho (cha kutoka upepo) kinaweza kuwa kimetokea
kweli. Vipi basi mtu anakubali kumfuata shetani pale uongo wake unapokuwa
dhahiri, pale anapoambiwa na shetani kuwa; “Hukutawadha vizuri au hukutia nia
sawa nk., wakati anajuwa kuwa huo ni wasi wasi wa shetani tu, na kwamba
anajaribu kumchezea”.
Katika
kutia nia ya Swala, shetani hupata upenyo pia wa kuwachezea watu na kuwakosesha
thawabu nyingi sana.
Utamuona
mtu anafunga Swala kisha anaivunja. Na mwengine huendelea hivyo mpaka Imamu
anaporukuu, hapo ndipo huifunga Swala kwa haraka na kurukuu pamoja naye.
Ameweza
kuihudhurisha nia kwa haraka pale Imamu aliporukuu, wakati alishindwa kufanya
hivyo tokea mwanzo wa Swala.
Hii
ni njia moja wapo ya shetani kumkosesha thawabu nyingi kama anglifunga Swala
pamoja na Imamu.
Wengine
kabla ya kufunga swala utawasikia wakinyanyua sauti zao wakitamka maneno Fulani
na kushadidia maneno hayo, kisha husema; “Allahu
Akbar”, kisha huivunja Swala na kuanza kutamka tena maneno hayo akidhani
kuwa amekosea kuyatamka, na akidhani pia kwamba maneno hayo yamepangwa na Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam), na kwamba akiyakosea Swala yake inabatilika.
Utamuona
akiendelea kukubali kuchezewa na shetani na kumkosesha thawabu nyingi za
kujiunga na Imamu mapema.
Ukweli
ni kuwa maneno hayo anayotamka, anayodhani kuwa ndiyo nia ya swala, hayajapata
kutamkwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), wala na
Sahaba zake watukufu (Radhiya Llahu anhum).
Anasema
Ibnu l Qayim:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
anapotaka kuswali husema:
“Allahu Akbar”, kisha hufunga Swala. Hakuwa akisema kitu kabla
yake kama vile; “Uswaliy fardha sswalaati l Ishaa….” Au kauli zozote katika
zile wanazozitamka watu hivi sasa. Hapana hadithi Sahihi wala hata dhaifu
inayotujulisha kuwa kitendo hiki kimetendwa na Sahaba yeyote au Taabi'i au
mmojawapo wa maimamu wanaojulikana kwa ucha Mungu wao. Hapana hata mmoja wao
aliyewahi kutamka kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
akifanya hivyo kabla ya kufunga Swala….”
(Kitabu
‘ Al Qaulu l mubiyn fiy akhtaa l musalliyn)
Anasema
Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha):
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
anapotaka kuswali huanza kwa kusema:
“Allahu Akbar.”
Muslim
– 1/357 na 498
Kutoka
kwa Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu), anasema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alipomuona mtu mmoja akikosea katika Swala alimuambia:
“Unapotaka kuswali, tia udhu kisha elekea kibla kisha sema;
“Allahu akbar”, kisha soma utakachoweza kusoma katika Qurani”.
Bukhari
na Muslim
Ama
Abdillahi bin Umar bin Khataab (Radhiya Llahu anhu) alisema:
“Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akianza kuswali kwa kusema “Allahu akbar.”
Bukhari
2/221 na 738
Hizi
ni dalili chache katika nyingi zinazotujulisha kuwa kitendo cha kuitamka nia
hakikuwepo katika mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam), na kwa ajili hiyo tusimpe fursa shetani kutuingilia na kutufisidia Swala
zetu au kutukosesha thawabu za kujiunga mapema na Imamu kwa kupitia mlango huo.
Imepokelewa
kutoka kwa Ibni Aqiyl, kuwa siku moja aliulizwa na mmoja katika watu wenye
maradhi haya ya wasiwasi:
“Mimi kila ninapotawadha, huhisi kama kwamba sijatawadha vizuri,
na kila ninapofunga Swala huhisi kama sikuifunga vizuri, nifanye nini?”
Ibni Aqiyl akamjibu:
“Wacha kuswali, kwa sababu wewe huna lazima ya kuswali”.
Alipoulizwa kwa nini alijibu hivyo, alisema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
‘Haandikiwi dhambi wala thawabu mwendawazimu mpaka awe na akili
…”, na mtu aliyetawadha akahisi kuwa bado hajatawadha, kisha
akafunga Swala akahisi kuwa bado hajaifunga, huyo akili zake si sawa. Huyo ni
mwendawazimu, na mwendawazimu halazimiki kuswali”.
(Talbis
Iblis – Ibni Taimia Uk.169)