MATOKEO YA
MWEZI WA RAMADHANI
Sameer Zulfikar Ramzan
FAT-HI MAKKA
Fat-hi Makka ni kule kuuingiza mji wa
Makka katika mikono mwa waislam kama inavyoeleweka kuwa Bwana Mtume Muhammad (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) baada ya kupewa utume alipata bughdha tele ikambidi kuuhama mji wa
Makka na kuhamia mji wa Madinah, na mji wa Makka ni mji mtakatifu na mji ulio
bora koliko mji yote duniani.
Zimekuja hadithi nyingi zenye kutuelezea
utukufu wa mji wa Makka mji aliozaliwa Bwana wetu Muhammad (Swallah Llahu alayhi
wa sallam), na mji huu
ndio uliokuwa ni
kitovu cha ushirikina kwa wakati huo ujulikanao wakati wa ujinga,
na ndio sababu kuu ya kuteremshwa Mtume Makka katikati ya ujinga ili aweze
kupambana nao kwa ufanisi zaidi, lakini matokeo yake Mtume (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) alifukuzwa
na kutaka kuuliwa na ndipo ikajiri kwa amri ya Allah kuuhama mji wa Makka na
kuhamia Madinah mji wa jirani yake.
Bwana Mtume alihama Makka akiwa na huzuni kubwa kwani alikuwa akiupenda mno mji huo na Allah
(Subhaanahu wa Ta’ala) akahakikisha ndoto ya Mtume wake kwa kuutia mkononi mji huo hali ya kuwa
yupo
hai.
Tarehe ya Fat-hu Makka na
sababu zake
Ilikuwa katika mwezi
wa Ramadhani mwaka wa nane tokea Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuhamia Madinah na
ilikuwa katika kumi la pili, na sababu
ya kutekwa huko ilikuwa ni kutokana na Makafiri wa Makka kutengua mkataba
walioekeana na Mtume (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) katika
mwaka wa sita yaani miaka miwili kabla ya tokeo hili. Mkataba huo ulikuwa moja katika
mikataba maarufu katika uislam ukijulikana
Makafiri katika kila zama
wanakuwa ni walalamishi na wenye kuvunja mikataba, Makafiri wa Makka walikiuka
kipengele kimoja cha mkataba ambacho kinasema kuwa
'pasiwepo na mapambano baina ya waislam na makafiri kwa muda wa miaka kumi'.
Na kipengele chengine walichoki khalifu kilikuwa
kinasema;
"kwa
yeyote anayetaka kuungana na Mtume katika makabila ya warabu basi ni ruhusa, na
yeyote anaye taka kuungana na Makureshi wa Makka ni ruhusa na watakuwa na hukumu sawa na watakaoungana nao
kwa kufanya kazi vipengele vyote vya
mkataba huo.
Sasa hebu na tuangalie matokeo ya
ubabaishaji kutoka
upande wa makafiri.
Watu wa kabila la Bani Bakri wakaungana na
Makureshi na Bani Khuzaah wakaungana na Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam), na ikijulikana kuwa
makabila haya mawili yalikuwa na gomvi lisilo kwisha. Hapo tena Bani Bakri
wakawafanyia uadui bani Khuzaah na kuwavamia usiku na kuwauwa wenzao
waliokubaliana kuwacha uadui ndani ya mkataba, na baya zaidi ni kwamba badhi ya
viongozi wa Makurshi walishiriki wakitoa msaada wa kila wa aina kwa Bani Bakri katika dhulma hii.
Mmoja kati ya hao Bani Khuzaah alisalimika
na akawahi kwenda kwa Mtum (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) kutoa khabari na
kuomba kunisuriwa, hapo tena Bwna Mtume akaazimia kuiteka Makka kwa hali yoyote
ikiwa kwa vita au kwa njia nyengine yeyote ile. Wakati huo Mtume Muhammad (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) alikuwa na wafuasi wengii walioingia katika
islam.
Juu ya tendo la kukhalifu mkataba
waliowekeana pande mbili, baadhi ya viongozi wa
ki-kureshi wakajuta na kujuwa kuwa kitendo walichokifanya kitasababisha
kutenguka kwa mkataba wao hapo tena wakamtuma Abu Sufyani aende Madinah
akautilie nguvu mkataba huo na kuonyesha kwamba wao hawaungani na hao wenzao
walio wauwa Waislam. Lakini kwenda kwake Madina kulikuwa bure pasipo na maana
pesa mbili maana Mtume (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) hakumjibu
kitu na alinyamza kimya kwani Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akisubiri kwa hamu
fursa hii ili aweze kuitia mkononi Makka na kumaliza nguvu za Makureshi na
kiburi chao.
Maandalizi ya kuuteka mji wa makka
Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) alifanya
maandalizi katika hali ya siri mno kiasi cha kwamba hata Waislam hawakujuwa
Mtume anakusudia kwenda wapi? Kwani
alikuwa hajawaambia lolote lile zaidi ya kuwa wawe tayari kujiandaa na vita, na kulikuwa hakuna anayethubutu kumuuliza, na Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuambia bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kuwa amuandalie vifaa vya kivita na
akamkataza asimwambie mtu wapi anakokusudia kwenda.
Hii ilikuwa ni hikma ya kivita, kwani Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) hakutaka
Makureshi wagundue azma yake, na iwe
nikuwateka kwa kuwashitukizia tu ikiwa ni moja ya mbinu za kivita inayotumika
hata nyakati hizi za sasa.
Tena hapo Bwana Mtume akatuma kikosi cha Waislam
kuelekea mbali na mji wa Madinah kujifanya wanapeleleza kitu, bila ya
wanaotumwa kujuwa lengo, na majamedari wa siku hizi nao waitumia mbinu hii vile
vile, Bwana Mtume kafanya hivi ili
waarabu washughulishwe na kikosi hiki na waone kuwa Mtume (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) azma yake ni
kupambana na watu wa miji mengine.
Maandalizi ya Waislam yalipotimia Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam)
akawaelezea Masahaba (Radhiya Llahu anhum) anakusudia kuelekea wapi na
akaomba dua;
“Ewe Mola
wadhibiti majasusi wasije kuwafikishia Makureshi khabari hizi”.
Na kabla
hawakutoka Madinah, uliteremka wahyi kumjulisha Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) yale aliyoyafanya
Hatib ya kutuma barua kwa Makuresh ikuwaajulisha jambo hili. Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam)
akamtuma Sahaba Ali na Sahaba Zubair na Mikdadi
(Radhiyallahu anhum), wamfuate huyo mjumbe mwenye barua nae ni mwanamke, na
watamkuta sehemu kaadha.
Wakatoka hadi hiyo sehemu na wakamkuta bibi huyo na kumtaka awape hiyo barua
aliyotumwa, na yule bibi akasema kuwa yeye hana kitu, na baada ya mjadala mrefu
wakamuambia;
"Imma utowe mwenyewe au tutakuvua
nguo", wakimaanisha kuwa wapo tayari kuitowa kwa
nguvu, na walikuwa na yakini kuwa bibi huyu anayo barua kwani amri ikishatoka
kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) basi inakuwa haina shaka.
Yule bibi alipoona kuwa ataadhirika, akaitoa barua hiyo kwenye
misuko yake ya nywele, na wakaichukuwa na kumpelekea Mtume barua hiyo, na Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipoamrisha ifunguliwe na isomwe ikagundulika kuwa kumenukuliwa kuhusu
kuuvamia mji wa Makka
Bwana Mtume akamgomba sahaba huyu nae
akajitetea na kuthibitisha kwamba hakufanya hayo kwa kutoka katika uislamu na
Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamsadiki aliyoyasema, lakini kama tunavyoisoma tarekhe ya
kiislam mara zote Syd Umar (Radhiya Llahu anhu) alikuwa ni mtu wa kuchukua maamuzi makali na
yakutisha na safari hii ikawa kama ilivyokuwa desturi yake akamuomba Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam)
amruhusu amuuwe kwani ni jasusi, lakini Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamkataza kwa sababu
huyo sahaba alipigana vita vya Badri.
MSAFARA UKIWA NJIANI
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akiwa yumo njiani kuelekea Makka
akakutanaa na ami yake bwana Abbas akiwa na aila yake wanaelekea Madinah wakiwa
washasilimu. Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akafurahishwa
Upande
mwengine Abu Sufyan aliamua kutoka Makka kupeleleza khabari, kwani kimya kilikuwa
kirefu wala hawakuwa wakifahamu Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) anaazimia kufanya nini? Akatoka Abu Sufyan hadi kufika sehemu ambayo akaja akapambana na
Bwana Abbas (Radhiya Llahu anhu) nae akiwa anamtafuta mtu wa kumpa khabari ili aweze
kawapelekea Makureshi ya kwamba wajisalimishe na alifanya hivyo baada ya kuomba
kwa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na kuruhusiwa kufanya hivyo na baada ya hapo bwana Abbas
(Radhiya Llahu anhu) akampakia Abu Sufyan katika farasi wake hadi kwa Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam), kwa bahati wakati huo sahaba Umar bin Khattab
(Radhiya Llahu anhu) alikuweko huku anatetemeka kumuona Abu Sufyani, na bila ya kusita
akamuomba Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amruhusu amkate kichwa chake, Bwana Abbas (Radhiya Llahu anhu) akasema kuwa yeye ndiye
aliyekuja na Abu Sufyan, na Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipoona kuwa Omar amekuja juu
akamuamrisha bwana Abbas aondoke na Abu Sufyan na arudi nae asubuhi ya siku ya pili yake.
Ilipofika siku ya pili bwana Abbas (Radhiya
Llahu anhu) alikwenda
pamoja na Abu Sufyan na Abu Sufyan akasilimu mbele ya
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema kuwaambia kina Abu Sufyan akawambie
watu wake kwamba;
“Atakaefunga mlango wa nyumba yake akabaki ndani
basi atakuwa na amani, na atakaeingia msikiti wa Makka atakuwa katika amani, na
atakaeingia nyumba ya Abu Sufyan atakuwa na amani.”
Na hili la mwisho bwana Abbas (Radhiya
Llahu anhu) ndie
aliyemuomba Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ampe kipaumbele Abu Sufyan kwa
sababu alikuwa mtu mwenye kupenda fakhari. Kisha Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) akamtaka bwana
Abbas (Radhiya Llahu anhu) apande nae kwenye kijabali ili awaone waislam
wote pamoja na nguvu walizokuwa nazo. Hapo tena wakawa wanapita makundi kwa
makundi, na kwa kufanywa hivyo ilikuwa ni kumfahamisha Abu Sufyan kuwa watu wa
Makka hawatoweza kupambana nao kutokana na nguvu kubwa walizokuwa nazo waislam
kwa wakati huo.
Abu Sufyan akarudi Makka na akawapa
khabari watu wa Makka na akawatahadharisha na kufanya ukaidi, kwani waislam wana
nguvu kubwa zisizo kifani ikiwa idadi
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akaingia Makka hali ya kuwa
nimwenye ushindi, na akaingia sehemu iliyo ya juu na huku akamuamrisha Khalid
bin Walid (Radhiya Llahu anhu) aingilie sehemu ya chini yaani upande mwengine akiwa pamoja na
waislam wengine na Mtume aliwakataza waislam wasipigane, lakini sahaba khalid
alipambana na baadhi ya makafiri ambao waliamua kutotii amri ya Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) na
wakaanza kuwapiga waislam, hapo dipo sahabi Khalid (Radhiya Llahu anhu) nae akaamua kupambana
nao hadi kuwashinda.
Kwa kweli hivyo hatuwezi kuvita kuwa
vilikuwa ni vita ila tu kuna watu wachache ambao
walikuwa ni wakarofi na kutaka kuonyesha ukaidi wao nakutaka kuonyesha kuwa wao
wana nguvu, wakauliwa wakaidi hao ikiwa idadi
Kuvunjwa kwa
masanamu
Baada ya waislam kuingia Makka nakufika
kwenye Al-Kaaba, Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuagizia mshika ufunguo wa Makka bwana Othman
bin Talha aulete ufunguo huo nae akatii na kuusalimisha pasi na pingamizi, bwana huyu alikuwa katika makafiri shupavu
(mkereketwa) na aliwahi kumtukana Mtume wakati alipokuwepo Makka na mara moja
Bwana Mtume alimtaka ampe ufunguo wa Al-Kaaba na alimkatalia kumpa funguo na
Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuambia itafika siku nitauchukuwa ufunguo huo nawe
utakuwa huna nguvu, na siku ilipowadia akautoa, na hapo tena ndipo Bwana Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) akaingia ndani ya Al-Kaaba na kuanza kuyavunja masanamu yote na kuyatupwa
nje.
Yasemekana kuwa yalikuwemo masanamu mia
tatu na sitini, na Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) aliyavunja
masanamu hayo kwa gongo
Mshika ufunguo siku hiyo alikuwa ni mtu dhalili kabisa na wakati huo akiwa bado ni kafiri
Mtume akamwambia;
"Hakika Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ameniaamrisha nikurejesheeni
ufunguo na hatokunyanganyeni isipokuwa dhalimu”.
Kutoka siku
hiyo ufunguo wa Al-Kaaba ukabaki mikononi mwa kabila
la mshika funguo huyo. Bwana huyu kuona hali hii ikamuingia imani na akasilimu hapo hapo. Tena ikatoka amri kwa
sahaba Bilal (Radhiya Llahu anhu) apande juu ya Al-Kaaba ili aadhini, na lengo ni kudhihirisha
uislamu mbele ya makafiri.
Baada ya adhana Mtume (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) akahutubia,
na mwisho akawauliza watu wa Makka alowateka; “Jee mnafikiri nitakufanyeni nini
leo ?
"Wakajibu;
"Wewe ni
ndugu mwema na ni mtoto wa ndugu yetu hivyo tunadhani utatufanyia wema tu”.
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akawaambia;
“Nendeni
hakika nyinyi mpo huru”.
Kutokana na
maneno haya wengi kati
Baada ya hapo wakaja watu makundi kwa makundi kutoa ahadi
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ya kumtii na kuwa pamoja naye. Na Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam)
alipokuwa akitufu Al-Kaaba
alitokezea bwana mmoja akawa anataka kumuuwa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam), akamvizia mpaka
akamfikia na hapo tena Bwana
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamgeukia na kumuuliza;
“Nani wewe, Fadhalah?”,
yule bwana akajibu
“Ndiye ni mimi”,
akaulizwa;
“Ulikuwa unakusudia nini kwenye nafsi
yako”,
akajibu;
“Nilikuwa namtaja Mola wangu”,
yaani alimdanyanya Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam)akacheka kisha
akamuambia; “Muombe msamaha Mola wako”.
Kisha baada ya hapo akamuwekea mkono wake
mtukufu kwenye kifua chake na akuondoa, na baada ya
hapo bwana Fadhalah akawa anasema kuwa;
“Hakuunyanyua mkono wake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kutoka kifuani kwangu illa ikawa
hakuna mtu nimpendaye katika dunia hii
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akakaa Makka siku kumi na tisa, kisha akawatazama Maansari (watu wa Madina) akawaona
kuwa wana huzuni kubwa, walidhani kuwa Mtume hatorudi tena Madinah, Mtume (Swallah
Llahu alayhi wa sallam)
akawaambia;
"Mimi
nitarudi Madinah na nitafia huko huko".
Wakafurahi kusikia hayo kwani huzuni zao ni kwamba watakosa kuishi nae. Mtume (Swallah Llahu alayhi wa
sallam) akarudi Madina
pamoja na Masahaba wake (RA) akiwa amefanikiwa kwa
yale yaliyotokea na ahadi aliyopewa na Mola wake.
Baadhi ya mafunzo
Kuna mafunzo mengi katika matukio haya, lakini
sisi tutagusia yale mazingatio yaliyo wazi zaidi.
Mbinu za
kijeshi.
Tunaona katika matokeo haya namna gani
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alivyokuwa akichunga maslahi ya kivita, hata ikawa haitaji sehemu
wanayoikusudia isipokuwa siku za mwisho na hili
linategemea ukubwa wa lile jambo lenyewe, kwa sababu angelilisimulia mapema
pengine MaQureshi wangejiandaa kwa vita na baadae pangekuwa na hali nyengine
siyo ile aliyoikusudia Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam)) nayo ni kuivamia Makka kwa amani.
Kusafika Makka na ushirikina
Hili halina ubishi kuwa Makka ilisafika na kushirikishwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) wakati wa uhai wa Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam)
hadi kufikia kusema kuwa haingii Makka isipokuwa Muislam, na hii ni kutokana na
utukufu wa mji huu. Pia kutakasika Al-Kaaba na
masanamu yaliyokuwemo ndani yake, jambo ambalo lilikuwa likimuudhi mno Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) tokea ujanani mwake.
Upole wa
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na usamehevu wake
Katika maisha ya Mtume (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) tunaweza
tukathibitisha mengi kuhusiana na upole wake na
usamehevu wake, na khasa katika matokeo
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hakutaka kuyawaza yale yaliyopita kuanzia kuteswa waislam hadi kufukuzwa yeye
na kupambana kwa vita pamoja na makafiri hao, yote hayo aliyaweka pembeni na
akataka kudhihirisha shakhsiya (personality) yake uungwana wake ambao amesifiwa
kwayo ndani ya Qurani kuwa;
“Hatuja
kutuma wewe Muhammad isipokuwa uwe ni rehema kwa walimwengu wote”.
Wengine hudhani Mtume
(Swallah Llahu alayhi wa sallam)kuja kwake ni rehma kwa waislam tu. Hapana, bali
kuja kwake ni rehma hata kwa makafiri, kwani mara ngapi alitakiwa awaapize na
uishe uonevu, lakini alikataa na hili lakuwasamehe ni kubwa zaidi maana alikuwa
na uwezo wakuamrisha alitakalo. Kuuliwa, kupigwa n.k lakini yote
hakuyataka.
Hii ni kuonyesha
usamehevu wake ulivyo na natija ya hatua yake hii ilikuwa ni kusilimu wengi
katika Ma-Qureishi baada tu ya kuachiwa huru.
Mungu
atujaalie tuwe ni wasamehevu