KWA NINI UISLAMU UMEHARAMISHA WANAUME KUVAA DHAHABU NA
HARIRI?
Leo ulimwenguni kote
kutokana na
kile kinachojulikana
Utamaduni
huu wa
vijana wa kiume kujipamba kwa kuvaa dhahabu
unakwenda kinyume na utamaduni wa
mila ya Kiislamu.
Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamume na Mwanamke
na kumpa kila mmoja maumbile
na tabia zinazotofautiana na mwenzake. Ikiwa hili linaashiria kitu, basi si
kingine bali
ni kutofautiana pia katika nafasi
na majukumu ya kila mmoja
wao. Nadharia inaonyesha kuwa tabia na
maumbile ya mwanaume ni ukakamavu
na ugumu, wakati ambapo tabia
na maumbile ya kike ni ulaini
na ulegevu. Uislamu unamtaka mwanaume aelekee katika mazingira yaliyo mbali na
udhaifu,unyonge na anasa zinazoweza
kumlegeza ili aweze kuwa imara
na mwenye nguvu katika kupambana
na harakati za maisha ya
kila siku, ambapo sehemu kubwa
ya jukumu
Sasa kwa kuzingatia kuwa madini ya
dhahabu na hariri ni vitu
vya anasa ambavyo humfanya mvaaji aonekane amependeza machoni mwake yeye mwenyewe
kwanza na machoni mwa wengine na
natija yake ni kuvaana na
maumbile ya kupendeza ambayo ni ulaini na
ulegevu. Pengine kwa njia
moja au nyingine hii ndio inaweza
kuwa hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri
kwa wanaume kwa kuwa inakubaliana
na tabia na maumbile
Hebu tujaribu kuwa wakweli,
tuwatie katika mizani ya haki
na uadilifu
wanaume wenye kuvaa dhahabu na
wasiovaa dhahabu, tutagundua nini? Bila ya shaka
mtakubaliana na
mimi kuwa ipo tofauti ya
dhahiri baina
Ni kweli usiopingika
kwamba kujua hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri
kwa wanaume, hii ni elimu
isiyo na manufaa na ni
ujinga usiodhuru. Usiulize hekima kwa kuwa
kumeshurutishwa katika kuulizia hekima ya amri au makatazo,
awe huyo muamrishaji/mkatazaji
analingana sawa na kufanana na
huyo muamrishaji/mkatazwaji
na hapa ni
suala la Mungu Muumba Muamrishaji na mwanadamu kiumbe
muamrishwa. Kwa mantiki hii mwanadamu
hana budi kuikubali na
kuipokea amri kwa kuwa Mola
wake ameamrisha/amekataza, kisha
baada ya kutekeleza aliloamrishwa ndipo anaweza kutafuata
kujua hekima/falsafa ya amri ile.
Lakini kule kujua hekima/falsafa iliyomo katika amri au katazo isiwe ni
sharti ambalo kwanza ni lazima litimizwe
kabla ya kuamrika au kukatazika. Muislamu wa
kweli anaambiwa na Mola wake:
"HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH
NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI, WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO. NA MWENYE
KAMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI (kabisa)." [33:36]
Kuharamishwa
uvaaji wa
dhahabu kwa wanaume kumethibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa
kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (SAW) -Rehema na Amani zimshukie.
1.
Amepokea (riwaya) Imamu Bukhaariy,
Muslim na Ahmad kwamba Mtume wa
Allah "Amekataza (kuvaa)
pete ya dhahabu".
2.
Imepokelewa kutoka kawa Ibn
Abbaas-Allah awawiye radhi-kwamba Mtume wa Allah aliiona pete ya dhahabu
kidoleni mwa mtu, akamvua na
kuitupa (huku) akisema " Mmoja
wenu analikusudia kaa la moto na
kulivaa mkononi?" Mtu yule akaambiwa
baada ya kwenda zake mtume
" Itwae pete yako unufaike
nayo. Akawajibu Wallah hapana, kamwe sitaichukua ikiwa aliyeitupa ni Mtume
wa Allah -Rehema na Amani zimshukie."
Muislam