(Manukato mazuri ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam))
Muhammad Faraj
Jina
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni mjukuu wa Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) na kipenzi chake,
mtoto wa pili wa Ali bin Abi Talib (Radhiya
Llahu anhu, ) na mama yake ni Bibi Fatimah binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Sallam).
Ndugu zake ni wengi, lakini mashuhuri katika hao ni
kaka yake Al-Hasan bin Ali (Radhiya Llahu anhuma) Khalifa wa tano wa
Waislamu.
Amesema Jaafar Al Sadiq (Radhiya Llahu anhu):
"Baina ya Al-Husayn na Al-Hasan kaka
yake ni twahara moja."
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikufa Shahiyd katika
mji wa Karbalaa -
Alizaliwa Madina tarehe 5 Shaaban mwaka wa 4 wa Hijri
na mara baada ya kuzaliwa alipelekwa kwa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) aliyemuadhinia na kumlisha tende baada ya
kuilainisha kwa mdomo wake mtukufu.
Alipotimia siku saba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) alimpa jina la Al-Husayn akamchinjia mbuzi wa Aqiqa
na kumuamrisha mama yake amkate nywele zote kisha azitolee sadaka kiasi cha
uzito wake.
Anasema Imam Ahmad katika Musnad yake katika
hadithi iliyopokelewa na Ali bin Abi Talilb (Radhiya Llahu anhu):
"Alipozaliwa Al-Hasan (Radhiya Llahu
anhu) alimpa jina la ami yake Hamza na alipozaliwa Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) alimpa jina la Jaafar. Anasema Aliy: "Akaniita Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) akaniambia:
'Nimeamrishwa nibadilishe majina ya hawa wawili.' Nikamuambia: "Mwenyezi
Mungu na Mtume wake ndio wenye kujua zaidi." Akawapa majina ya Al-Hasan na
Al-Husayn."[1]
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam) alipofariki dunia, Al-Husayn alikuwa na umri wa miaka mitano.
Abubakar (Radhiya Llahu anhu) Khalifa wa mwanzo wa Waislamu alikuwa
akiwapenda
1
Shaharbano
binti Yizd Jard bin Shahriyar Kisra (mama yake Ali Zayn Al Abdidiyn)
2
Laylah
binti Murrah Al Thaqafiyah (mama yake Ali Al Akbar)
3
Ummu
Jaafar Al Qadhaiyah (alifariki wakati wa uhai wa Ali bin Abi Talib
4
Ar-Rabaab
bint Mru'ul Qays Al Kilaabiyah (mama yake Abdullah Al Radhiy'a na Sakina bintil
Hussayn)
5
Ummu
Is'haq bin Talha bin Abdullah
2
Ali
Al Asghar ( 'mdogo' au As-Sajjaad)
3
Abdullah
Al Radhiy'a (au Ash-Shahiyd aliyeuliwa pamoja na baba yake
Karbalaa akiwa mtoto mchanga)
4
Ja’afar
5
Sakinah
6
Faatimah
1
Ruqayyah
2
Zaynab
Inasemekana pia kuwa alikuwa na Ali Al Awsat
(Ali wa kati) na Muhammad
Imepokelewa kutoka kwa Hani bin Hani kutoka kwa Ali
bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:
"Al-Husayn amefanana
Imepokelewa kutoka kwa Hammaad bin Zayd kutoka kwa
Hishaam kutoka kwa Muhammad kutoka kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) kuwa
alisema:
"Nilikuwepo siku ile Ibn Ziyad
alipokuja na kichwa cha Al-Husayn akiwa anakichocha kwa kijiti. Nikasema:
"Hakika amefanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Sallam)."
Kutoka kwa Abdullah bin Abi Yazid alisema:
"Nilimuona Al-Husayn bin Ali. Nywele
na ndevu zake zilikuwa nyeusi
Kutoka kwa Abi Nuumin alisema:
"Nilikuwa kwa Abdullah bin ‘Umar bin
Khattwaab, akaja mtu kuuliza juu ya damu ya mbu. Abdullah bin ‘Umar akamuuliza:
"Ni mtu wa wapi wewe?"
Akamuambia:
"Mtu wa
Abdullah bin ‘Umar akamuambia:
"Muangalieni mtu huyu, ananiuliza juu
ya damu ya mbu wakati wao ndio waliomuua mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam), na mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) akisema :"Al-Hasan na Al-Husayn ni manukato
yangu mazuri ya hapa duniani."
Kutoka kwa Abu Ayub Al Ansariy (Radhiya Llahu anhu)
amesema:
"Niliingia nyumbani kwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) nikawakuta Al-Hasan na
Al-Husayn wakicheza juu ya kifua chake. Nikamuuliza: "Unawapenda?"
Akaniambia: "Vipi nisiwapende wakati hawa ndio
manukato yangu mazuri ya hapa duniani."
Attabarani katika Muujam yake
Anasema Imam Adh-Dhahabiy katika 'Siyar aalam
an-Nubalaa' kuwa; hadithi kama hii zimepokelewa pia kutoka kwa Ibni ‘Umar
na Ibni ‘Abbaas na ‘Umar na Ibni Mas’uud na Malik bin Al Huwayrith na Abi
Sa’iyd na Hudhayfa na Anas na Jaabir (Radhiya Llahu anhum) kupitia njia
mbali mbali zenye kuipa nguvu.
Imepokelewa pia kuwa siku moja Al-Hasan na
Al-Husayn walipoingia msikitini, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alisema:
"Mwenye kupenda
kuwaangalia mabwana wa vijana wa Peponi awaangalie hawa."
Na kutoka kwa Imam Ahmad na Attabarani na
Attirmidhiy kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam)
alisema:
"Husayn ni mjukuu
katika wajukuu. Mwenye kunipenda basi ampende na Al-Husayn pia."
Imepokelewa pia katika hadithi sahihi kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) amesema:
"Al-Hasan na Al-Husayn ni mabwana wa
vijana wa Peponi."
Na akasema:
"Mola wangu mimi ninawapenda na Wewe
wapende pia."
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa
akimpenda na kumheshimu
Juu ya kutoridhika kwake siku ile kaka yake
alipojiuzulu ukhalifa kwa ajili ya kumuachia Mu’awiyah bin Abi Sufyan (Radhiya
Llahu anhu), Al-Husayn alinyamaza na hakushindana naye.
Al-Hasan (Radhiya Llahu anhu) alipofariki dunia
wakati wa ukhalifa wa Mu’awiyah, Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa
katika nchi ya
Mu’awiyah akiwa bado yuhai aliamua kumrithisha mwanawe
Yazid ukhalifa. Jambo
Watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) 'Ahlul Bayt' wana daraja kubwa
"Na walio kuja baada
Al Hashr- 10
Al-Husayn na kaka yake Al-Hasan (Radhiya Llahu
anhum) wao pia wana daraja kubwa
Tunaamini pia kuwa kuuliwa kwa Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) ni msiba mkubwa
"Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba
mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyo onekana na yanayo onekana! Wewe utahukumu
baina ya waja wako katika waliyo kuwa wakikhitalifiana."
Az-Z’Umar – 46
Mwenyezi Mungu Amependa kumnyanyua zaidi Al-Husayn na
kumpa daraja hiyo ya ushahiyd, na ametaka kuwadhalilisha waliyemuua na kuwalipa
wanachostahiki.
Anasema Shaykh Al-Islam Ibn Taymiyah:
"Mwenyezi Mungu Amemkirimu kwa
kumruzuku kifo cha shahiyd, na Amemdhalilisha aliyemuua na kila aliyeshirikiana
naye au kuridhika na kitendo hicho. Na yeye Al-Husayn anayo mifano mema kwa
waliomtangulia katika njia hiyo, na Mwenyezi Mungu Anasema:
"Na uwape habari njema wanaosubiri.
Ambao uwapatapo msiba husema:"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake
Yeye tutarejea."
Al Baqarah – 155-156
Katika kitabu cha 'Tariykh' cha Ibni Asakir,
imeandikwa; Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Kalbiy
amesema: "Mu’awiyah (Radhiya Llahu anhu) alisema kumuambia mtu
mmoja wa kabila la Kikureshi: 'Utakapoingia ndani
ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
ukaona vifungu vya watu wanasoma darsi, utakapoliona fungu ambalo watu
wanaosikiliza wametulia kimya kama kwamba ndege wametua juu ya vichwa vyao
wanaogopa wasiruke, basi ujuwe kuwa hapo ndipo penye darsi ya Abu Abdullah
(Al-Husayn) (Radhiya Llahu anhu), mahali hapo hapana mchezo hata kidogo.[3]"
Na katika Tariykh pia; Kutoka kwa Hammad bin
Salamah kutoka kwa Abil Muhzim amesema: "Tulikwenda
kusalia jeneza la mwanamke, na Abu Hurayrah (Radhiya Llahu anhu) alikuwa
pamoja nasi. Likaletwa na jeneza la mwanamume na kuweka ubavuni mwake na
kusaliwa. Tulipokuwa tukipeleka majeneza, Al-Husayn alichoka akakaa katikati ya
njia. Abu Hurayrah akakaa karibu yake huku akipangusa mchanga ulio miguuni mwa
Al-Husayn. Al-Husayn akamuambia: "Ewe Abu Hurayrah, kwa nini unafanya
hivi?" Abu Hurayrah akamuambia: "Niache. Kwani wallahi lau kama
wangekujua vizuri watu, basi wangekunyanyua juu ya mabega
Imepokelewa katika kitabu cha Tariykh pia kuwa;
Wakati wa ukhalifa wa ‘Umar bin Khattwaab (Radhiya Llahu anhu) zililetwa
nguo kutoka
Baada ya Ali bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu)
kuuliwa, watu wa mji wa Al-Kuufah -
Baada ya fungamano kumalizika, jeshi kubwa liliondoka
kuelekea Sham '
Aliondoka na jeshi kwa nia ya kufanya sulhu na watu wa
huko kwa sababu Al-Hasan (Radhiya Llahu anhu) anajulikana kuwa yeye ni
mtu asiyependa vita. Inajulikana pia kuwa tokea hapo mwanzo wakati watu wa Sham
walipokataa kuutambua ukhalifa wa baba yake, na baba yake alipoamua kupeleka
majeshi kwa ajili ya kupambana na watu wa Sham, Al-Hasan (Radhiya Llahu
anhu) alimnasihi
Dalili nyingine ni kule kumuondoa Qais bin Saad katika
uongozi wa jeshi na kuliweka chini ya uongozi wa Abdullah bin ‘Abbaas (Radhiya
Llahu anhuma).
Kutoka kwa Al-Hasan Al Basriy (Radhiya Llahu anhu) alisema:
"Nilimsikia Abubakar akisema:
"Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
alipokuwa akihutubia, akaja Al-Hasan. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) akasema: "Mwanangu huyu ni bwana. Na huenda Mwenyezi
Mungu kupitia kwake akasuluhisha baina ya makundi mawili ya Waislamu."
Al-Bukhaariy
Mu’awiyah na Al-Hasan hatimaye walikutana, na Al-Hasan
alikubali kumuachia ukhalifa Mu’awiyah, na mwaka ule ukaitwa 'Mwaka wa
umoja'.
Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alihukumu muda wa
miaka miwili na miezi mitatu kisha akafariki dunia.
Na ‘Umar (Radhiya Llahu anhu) alihukumu muda wa
miaka kumi, na ‘Uthmaan (Radhiya Llahu anhu) alihukumu miaka kumi na mbili na
Ali (Radhiya Llahu anhu) miaka mine na miezi tisa, na Al-Hasan (Radhiya
Llahu anhu) alihukumu muda
wa miezi sita.
Utawala wa Mu’awiyah (Radhiya Llahu anhu)
uliendelea kwa muda wa karibu miaka ishirini mpaka mwaka wa 60 Hijri, na wakati
wote huo hapakuwa na matatizo ya aina yoyote katika dola ya Kiislamu, bali
kulikuwepo na ufunguzi na kutekwa kwa nchi nyingi za kikafiri, na utulivu
ulienea katika maeneo yote ya dola kubwa ya Kiislamu.
Katika muda huo alifariki dunia Al-Hasan bin Ali (Radhiya
Llahu anhu), ikasemekana kuwa alitiliwa sumu ndani ya chakula chake, na
ukweli anaujuwa Mwenyezi Mungu peke yake, kwani hapana dalili yoyote yenye
isnadi sahihi yenye kutuhakikishia juu ya jambo
Katika mwaka wa 50 Hijri, Mu’awiyah (Radhiya Llahu anhu) alimteuwa mwanawe
Yazid kuwa khalifa wa Waislamu baada yake, akawataka watu wafungamane naye.
Maulamaa wengi wanasema kuwa hapa Mu’awiyah alikwenda
kinyume na mwenendo wa Makhalifa waongofu waliotangulia.
Wanasema kuwa fungamano
1-
Kuanzisha
uzushi mpya kwa kumrithisha mwanawe ukhalifa wakati hapo mwanzo ukhalifa
ulipatikana kwa mashauriano baina ya Waislamu kwa kumchagua mtu asiyekuwa na
uhusiano wa kiaila na Khalifa.
2-
Walikuwepo
wenye kuustahiki zaidi ukhalifa kuliko Yazid
Amesema Ibn Al-‘Arabiy:
"Mu’awiyah ameacha lililo bora zaidi,
nalo ni kujaalia Ukhalifa upatikane kwa mashauriano bila ya kumuingiza yeyote
katika watu wa aila yake, wachilia mbali mwanawe. Hata hivyo watu walikubali
kufungamana naye, na kwa ajili hiyo fungamanao lilikuwa sahihi kisheria[6].
Ibni Kathiyr alitaja kisa cha Abdullah bin Mutiy'a na
sahibu zake waliomuendea Muhammad bin Al-Hanafiyah mtoto wa Ali bin Abi Talib,
ndugu kwa baba wa Al-Hasan na Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhum), wakamuambia:
"Yazid hastahiki kuwa Khalifa kwa
sababu anakunywa pombe na hasali swala zake sawa sawa."
Muhammad bin Al Hanafiyah akasema:
"Mimi sikuyaona hayo mnayoyasema.
Nilionana naye na nilikaa kwake. Ni mtu anayesali swala zake sawa sawa na ni
mwenye kupenda kheri. Anapenda kujifunza elimu ya fiqhi na kufuata mafundisho
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam)."
Wakasema:
"Huenda alikuwa akifanya hayo mbele
yako tu."
Muhammad akasema:
"Anaogopa nini hata afanye hivyo?
Mlimsikia yeye mwenyewe akisema hivyo?"
Wakasema:
"Sisi tunaona hivyo tu, hata
Muhammad akawaambia:
"Mwenyezi Mungu amewakataza Waislamu
kusema bila dalili." Kisha akawasomea kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na
wao wanajua."
Al Zukhruf-86
Kwa hivyo zile habari kuwa Yazid alikuwa akinywa ulevi
ni uvumi tu, na hapana isnadi yoyote sahihi yenye kuthibitisha hayo. Kisheria
ni haramu kwa Muislamu kumtuhumu mwenzake bila ya dalili.
Na kutokana na kauli ya Muhammad bin Al-Hanafiya (Radhiya Llahu anhu), ambaye ni ndugu wa
Al-Hasan na Al-Husayn (Radhiya Llahu
anhu) tunapata dalili kuwa Yazid hakuwa hivyo.
Yazid alitawala mwaka wa 60 Hijri na wakati huo
alikuwa na umri wa miaka 36, na katika watu waliokataa kumtambua ni Al-Husayn
na Abdullah bin Az-Zubayr (Radhiya Llahu
anhum) ambao wakati huo walikuwepo Madina, na walipotakiwa kwa lazima
kumtambua Yazid waliondoka na kukimbilia Makkah.
Habari ziliwafikia watu wa
Wakaanza kumuandikia Al-Husayn bin Ali (Radhiya Llahu anhu) wote kwa pamoja
wakimuambia: "Sisi tunafungamana na wewe tu na hatumtaki mwengine
isipokuwa wewe."
Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) alipoona kuwa barua nyingi
Alipowasili huko na baada ya kuulizia na kufanya
upelelezi, Muslim alielewa ukweli kuwa watu wa huko hawamtaki Yazid, bali
wanamtaka Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu).
Alifikia nyumba ya mtu mmoja anayeitwa Hani bin
Uruwah, na makundi makubwa mkubwa ya watu yalikuwa yakimuendea kufungamana naye
kuwa wanamtaka Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) awe Khalifa wao.
Habari juu ya makundi hayo ya watu zilimfikia Nu’umaan
bin Bashir gavana wa Yazid wa Al-Kuufah, ambaye hakuonyesha kukasirishwa wala
hakujaribu kuwazuwia watu wala hata kumuarifu Khalifa Yazid.
Hata hivyo watu walizifikisha habari hizo kwa Yazid na
kumuarifu juu ya kutojali kwa Nu’umaan juu ya yanayotendeka huko, na Yazid
akaamua kumuondoa Nu’umaan katika ugavana na kumuweka badala yake ‘Ubaydullah
bin Ziyad aliyekuwa pia gavana wa mji wa
‘Ubaydullah aliwasili Al-Kuufah nyakati za usiku akiwa
amejifunika uso. Ikawa kila anapowasalimia makundi ya watu walikuwa wakimjibu:
"Wa alaykumussalaam ewe mwana wa binti yake Mtume wa Mwenyezi Mungu."
Wakimdhania kuwa ni Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu). Kwa sababu aliingia
usiku akiwa ameufunika uso wake.
‘Ubaydullah akaelewa kuwa ni kweli watu wanasubiri
kuwasili kwa Al-Husayn. (Radhiya Llahu
anhu).
‘Ubaydullah alipowasili katika kasri yake alimtuma mtu
mmoja aitwae ‘Aqiyl akapeleleze na kuwaletea jina la mkubwa wa mpango huo.
‘Aqiyl akawadanganya watu kuwa yeye ni mtu kutoka mji wa Hims aliyekuja na
Dinari elfu tatu kwa ajili ya kuchangia kuja kwa Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu). Akawa anauliza na kuuliza mpaka akaifikia
nyumba ya Hani bin Uruwah akaingia na kumkuta Muslim bin ‘Aqiyl humo.
Akafungamana naye na kumpa zile Dinari elfu tatu.
Akawa pamoja nao mpaka alipopata habari zao kwa
ukamilifu, ndipo aliporudi kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad na kumpa habari zote.
Baada ya watu wengi kufungamana naye, na kuhakikisha
kuwa mipango yote inakwenda kama ilivyopangwa, Muslim bin ‘Aqiyl alimuandikia
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu)
kumtaka aje
Ubeidullah bin Ziyad baada ya kutambua juu ya
matayarisho ya kuja kwa Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu), alituma askari kwenda kumkamata Hani bin Uruwah, na
walipomuendea na kumuuliza: "Yuwapi Muslim?" Hani akawajibu:
"Sijuwi yuko wapi. Wallahi lau
‘Ubaydullah akampiga Hani kisha akaamrishwa atiwe
jela.
Habari zikamfikia Muslim bin ‘Aqiyl aliyeondoka na
jeshi la watu wapatao elfu nne na kuizunguka kasri ya ‘Ubaydullah bin Ziyad, na
watu wa Al-Kuufah wote wakatoka na kumuunga mkono.
Wakati huo viongozi wa makabila makubwa ya Al-Kuufah
walikuwa ndani ya kasri ya ‘Ubaydullah aliyewataka wawatishe watu wao ili
waache kumuunga mkono Muslim.
Wakatoka na kuwatisha kuwa jeshi kubwa linakuja kutoka
Sham, jambo lililoingiza hofu ndani ya nyoyo zao, na kidogo kidogo, mmoja baada
ya mwengine wakaanza kuondoka na kumuacha mkono Muslim bin ‘Aqiyl. Alitoka na
jeshi la watu elfu nne akajikuta amebakiwa na watu wapatao thelathini tu, na
kulipopambazuka Muslim alijikuta amebaki peke yake. Wote wamekwishamkimbia.
Walipotambua kuwa Muslim amebaki peke yake, likatumwa
jeshi la watu wapatao sabini na kulizunguka hema lake. Walijaribu mara tatu
kuingia ndani ya hema lakini Muslim alipambana nao kwa upanga wake na kuwatoa
nje kila wanapojaribu.
Wakaamua kumrushia mawe, na yeye akaamua kuwatokea nje
na kupambana nao, akawaua wengi na mwisho wakakubaliana nae kuwa aondoke hapo
na kurudi alikotoka, na Muslim akakubali
Muslim akaondoka na kuanza kuzunguka katika barabara
za mji wa Al-Kuufah. Kiu kilimshika akagonga mlango wa nyumba ya mwanamke mmoja
wa kabila la Bani Kinda na kuomba maji.
Bibi alimuuliza: "Nani wewe?"
Akamuambia: "Mimi ni Muslim bin ‘Aqiyl."
Kisha akamuhadithia habari zake na namna watu walivyomuacha mkono na kwamba
Al-Husayn atakuja kwa sababu keshaarifiwa. Yule bibi akamkaribisha nyumbani
kwake, akamletea maji na chakula, lakini mwanawe akampelekea habari ‘Ubaydullah
bin Ziyad aliyetuma askari wengine wapatao sabini. Wakaizunguka nyumba na
Muslim akatoka na kupambana nao lakini hatimaye wingi uliushinda ushujaa,
akaishiwa nguvu ikambidi asalimu amri.
Wakamchukua na kumpeleka katika kasri ya ‘Ubaydullah
bin Ziyad huku akikabbir na kumtaja Mwenyezi Mungu.
‘Ubaydullah akamuuliza:
"Kipi kilichokuleta huku?"
Muslim akasema: "Fungamano na Al-Husayn bin Ali
liko juu ya shingo yetu."
‘Ubaydullah akamuambia: "Nitakuua."
Akasema: "Kabla ya kuniua niruhusu niusie."
Akamuambia: "Usia."
Akageuka huku na kule akamuona ‘Umar mtoto wa Sa’ad
bin Abi Waqaas. Akamuambia: "Wewe ndiye uliye karibu zaidi na mimi. Kwa
Rehma ya Mwenyezi Mungu nakuusia." Akamshika mkono, akaenda naye pembeni
kidogo na kumtaka amtume mtu kwenda kwa Al-Husayn na kumuambia kuwa arudi
alikotoka. ‘Umar akamtuma mtu kumjulisha Al-Husayn kuwa mpango wao
umekwishajulikana na kwamba watu wa Al-Kuufah wamekwenda kinyume na ahadi zao.
Katika maagizo ya Muslim ni kauli mashuhuri
"Rudi wewe na watu wa nyumba yako, na
wasikubabaishe watu wa Al-Kuufah. Watu wa Al-Kuufah wamekudanganya na wamenidanganya
mimi pia. Na mtu muongo hana rai."
Muslim bin ‘Aqiyl akauliwa siku ya Arafat na wakati
huo Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu)
aliondoka Makkah Sikukuu mosi kuelekea
Masahaba wengi walijaribu kumzuia Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) asiondoke, wakiwemo
Abdullah bin ‘Umar na Abdullah bin ‘Abbaas na Abdullah bin Amru bin Al Aas na
Abu Sa’iyd Al-Khudry na Abdullahi bin Az-Zubayr na Muhammad bin Al-Hanafiyah –
ndugu yake kwa baba (Radhiya Llahu anhum).
Wote hawa waliposikia kuwa Al-Husayn (Radhiya Llahu
anhu) anataka kwenda Al-Kuufah walimkataza.
1.
Abdullah
bin ‘Abbaas (Radhiya Llahu anhu) alimuambia: "Ingelikuwa
sioni vibaya kufanya hivyo mbele ya
watu, basi ningelikuzuia kwa nguvu zangu zote usiende huko. Bora ubaki hapa
usiende
2.
"Imepokelewa
kuwa Ibn ‘Umar (Radhiya Llahu anhu) alikuwa Makkah alipopata habari kuwa
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) keshaondoka kuelekea
3.
Abdullah
bin Zubayr (Radhiya Llahu anhu) naye alimuambia Al-Husayn: "Unakwenda wapi? Unakwenda kwa watu waliomuua baba yako
na ndugu yako? Usiende." Lakini Al-Husayn (Radhiya Llahu
anhu) alikataa katakata.
4.
Abu
Sa’iyd Al-Khudry (Radhiya Llahu anhu) naye alimuambia: "Ewe Aba
Abdullah! Mimi nakunasihi, na mimi nakuhurumieni. Nimesikia kuwa
wamekuandikieni baadhi ya wafuasi wenu huko Al-Kuufah wakikutakeni muende kwao.
Msiende. Nilimsikia baba yako akiwa Al-Kuufah akisema: "Wallahi nimewachoka na kuwachukia, na wao
wamenichoka na kunichukia, na mimi nimechoka nao na kuwachukia. Hawana utiifu hata
kidogo. Aliyekuwa pamoja nao amepata hasara kubwa. Wallahi hawana nia nzuri
wala azimio jema katika jambo, wala hawana subira mbele ya upanga."
5.
Alipokuwa
njiani kuelekea
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa njiani
akielekea
Alipopata habari za kuwasili kwa Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu), ‘Ubaydullah bin Ziyad alituma jeshi la watu wapatao elfu moja
chini ya uongozi wa Al Hurr bin Yazid At-Tamimiy kwenda kumzuia asiweze kuingia
Al-Kuufah. Na alipokutana naye karibu na mji wa Al Qadisiyah akamuuliza:
"Unakwenda wapi ewe mwana wa binti yake Mtume wa
Mwenyezi Mungu?"
Akamuambia: "Nakwenda
Akamuambia: "Basi mimi nakuamrisha urudi ili
Mwenyezi Mungu asinipe mtihani wa kupambana na wewe. Bora urudi ulikotoka, au
uende Sham alipo Yazid, lakini usiende Al-Kuufah."
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikataa na
akaendelea na safari yake kuelekea Al-Kuufah, na Al Hurr akawa anajaribu
kumzuia Al-Husayn.
Al-Husayn akamuambia: "Kaa mbali na mimi, akukose
mama yako."
Al Hurr akamuambia: "Wallahi neno
Al Hurr
akamuuliza: "Kitu gani kilichokuleta?"
Akamuambia:
"Barua zenu na wajumbe wenu."
Al Hurr
akasema: "Barua gani na wajumbe gani?
Al-Husayn
(Radhiya Llahu anhu) akasema: "Ewe ‘Uqbah zilete zile barua."
Akazitoa
barua nyingi
Al Hurr
akasema: "Sisi si katika waliokuletea barua hizi. Sisi tumeamrishwa
kukukamata na kukupeleka kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad.
Al-Husayn
(Radhiya Llahu anhu) akasema: "Mauti ni bora kuliko hayo." Akapanda
farasi wake, na sahibu zake nao wakapanda farasi wao na kuondoka kuelekea
Karbalaa huku jeshi la Al Hurr likimfuata na kujaribu kumzuia.
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) akaendelea na safari mpaka
alipowasili Karbalaa. Akauliza: "Panaitwaje mahali hapa?"
Wakamuambia: "Karbalaa". Akasema: "Kurab na balaa." Na maana yake ni (misiba na
balaa), na hii ilikuwa siku ya pili ya Muharram mwaka 61[9].
Kikosi kingine
cha jeshi la ‘Ubaydullah chini ya
uongozi wa ‘Umar bin Sa’ad kikawasili, na kumtaka Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) afuatane nao kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad. Al-Husayn alikataa na
kumtaka ‘Umar amruhusu ende Sham kwa Yazid. ‘Umar akataka muda ende kumshauri ‘Ubaydullah, na ‘Ubaydullah akakubali, lakini katika majlis yake palikuwepo na mtu
aitwae Shumar bin Dhil Jawshan aliyesema: "Hapana Wallahi! Tusimruhusu.
Sisi ndiye tutakayempeleka Sham." ‘Ubaydullah
akapendezewa na fikra hiyo, akasema: "Kweli, lazima tumpeleke chini ya
ulinzi wetu."
‘Ubaydullah akamuambia Shumar: "Nenda
wewe ukamlazimishe akubali kusalimu amri na kupelekwa kwa Yazid chini ya ulinzi
wangu, na ikiwa ‘Umar ataregarega basi chukua wewe uongozi."
Shumar
akaondoka na kuelekea mahali alipo Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) akiwa amezungukwa na jeshi la
‘Umar bin Sa’ad na Al Hurr bin Yazid At-Tamimiy, na alipojulishwa kuwa lazima
apelekwe Sham chini ya ulinzi wa askari wa ‘Ubaydullah bin Ziyad
alikataa akawaambia: "La Wallahi! Sikubali kusalimu amri kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad."
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa na watu sabini na
mbili wakati jeshi la
Akawanasihi
waliache jeshi la ‘Ubaydullah na
kuungana naye, na watu thelathini wakakubali kujiunga naye akiwemo kiongozi wao
Al Hurr bin Yazid At-Tamimiy.
Wakamuuliza
Al Hurr: "Wewe umekuja ukiwa kiongozi wetu na sasa hivi unatuacha
mkono?"
Akawaambia:
"Ole wenu! Mimi niliishauri nafsi yangu niingie Peponi au Motoni
nikachagua Peponi. Wallahi sitochagua kuingia Motoni hata
Ulipoingia
wakati wa Swalah, Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) aliwaswalisha makundi yote mawili Swalah ya adhuhuri baada
ya kuwauliza
Kabla ya
magharibi kuingia walijaribu kuingia ndani ya hema lake, na wakati huo
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa
amejinyosha kidogo juu ya tandiko huku akiwa ameushika upanga wake tayari kwa
hatari yoyote itakayomkabili. Dada yake alimsikia akisema: "Nimemuota
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam) aliyeniambia: "Leo utakuwa pamoja nami."
Kisha
Al-Husayn akawauliza: "Wanataka nini?" Watu wake wakamuambia:
"Hatujui." Akawaambia: "Kawaulizeni." Wakatoka watu ishirini juu ya farasi wao
akiwemo Al-‘Abbaas bin Ali bin Abi Talib ndugu yake Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) wakawauliza: "Mnataka
nini?" Wakasema: "Lazima akubali kusalimu amri kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad au apigane."
Wakawaambia: "Mpaka tumuulize kwanza."
Wakarudi
kwa Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) na
kumjulisha, akawaambia: "Tupeni muda wa usiku huu mmoja na kesho
tutakujulisheni. Niacheni nisali kwa ajili ya Mola wangu kwani mimi napenda
kusali kwa ajili ya Mola wangu Mtukufu."
Usiku kucha
wakawa wanasali huku wakimuomba Mwenyezi Mungu yeye pamoja na waliokuwa naye –
Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.
Asubuhi
yake kabla mapambano kuanza, Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) aliwahutubia wanawe na watoto wa ndugu zake aliokuwa nao,
akawaambia: "Nyinyi bora muondoke, nimekwishakupeni ruhusa."
Wakamuambia:
"Na watu watasema nini? Kuwa tumemuacha Shaykh wetu na kiongozi wetu na
bwana wetu na bin ami yetu bila ya kumhami? Hapana Wallahi hatutofanya hivyo,
bali tupo tayari kuzitoa nafsi zetu na za watu wetu na
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) akawakabili
adui zake, akauchukua msahafu na kuuweka mbele yake kisha akainyanyua mikono
yake juu kumuomba Mwenyezi Mungu na hapo ndipo mapambano yalipoanza.
Mishale na
mkuki ikaanza kuvurumishwa huku na kule, na jeshi kubwa la adui likaanza
kushambulia kwa nguvu upande wa Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) ambao juu ya uchache wao
walipigana kufa na kupona na wakaweza kuwashinda na kuwarudisha nyuma.
Watu wa
jeshi la Ibni Ziyad wakaomba msaada kutoka kwa wenzao. Kikawasili kikosi cha
watu wapatao mia tano. Ukaingia wakati wa Swala ya adhuhuri, na Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) akamuambia kiongozi wa upande
wa pili: "Waamrisheni wasimamishe vita ili tuswali Swala ya
adhuhuri." Wakakataa, na Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) pamoja na wenzake wakaswali Swala ya hofu huku wakiendelea
na mapambano.
Jeshi la upande
wa pili likaongezeka, wakapata nguvu na kuweza kumkaribia Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu), na watu wa
upande wa Al-Husayn walioelewa kuwa hawana uwezo wa kulishinda jeshi
Wakaanza
kuuliwa mmoja baada ya mwingine mpaka akabaki Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu)
peke yake. Alibaki muda mrefu akiwa amesimama mbele
Wakamzunguka
Radhiya Llahu anhu
aliyewakabili kwa upanga wake akipambana nao kwa ushujaa mkubwa akimuua kila
aliyejaribu kumsogelea. Akaendelea hivyo mpaka alipochoka na nguvu kuanza
kumuishia. Lakini juu ya kuchoka kwake waliogopa kumkaribia.
Shumar
akaanza kupiga kelele tena: "Muuweni, mkamateni." Na hapo ndipo mtu
mmoja aitwae Zara'a bin Shariyk alipompiga kwa ghafla tena kwa nguvu juu ya
bega lake la kushoto, na mwingine aitwae Sinan alimpiga kwa mkuki, na Al-Husayn
(Radhiya Llahu anhu) akaanguka,
na hapo ndipo walipoweza kumuendea na kumkata kichwa chake – Mwenyezi Mungu
atawashinda Inshaallah. Inasemekana aliyemkata kichwa chake ni Shumar. Na hii
ilikuwa siku ya Ijumaa siku ya ‘Ashuraa mwaka wa 61Hijri.
Kichwa
chake kikachukuliwa na kupelekwa Al-Kuufah kwa ‘Ubaydullah bin Ziyad, na kilipowasili akawa anakichokoa kwa kijiti
huku akikiingiza mdomoni mwake. Na Anas bin Malik (Radhiya Llahu anhu) aliyekuwepo katika majlis
hiyo wakati huo akainuka na kuondoka huku akisema kwa ukali: "Wallahi wewe
ni mtu mbaya. Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) akipabusu
mahali hao unapokipitisha kijiti."
Anasema
Abdul Malik bin ‘Umayr: "Niliingia kwa Ibni Ziyad nikakiona kichwa cha
Al-Husayn kimewekwa ndani ya chombo. Na Wallahi hazikupita siku nyingi
nikaingia kwa Al Mukhtar bin Abi Ubayd nikakiona kichwa cha Ibni Ziyad ndani ya
chombo mbele ya Al Mukhtar."
Tutasoma
juu ya Al Mukhtar kila tukiendelea mbele na kisa chetu.
Imepokelewa
kutoka kwa Al Amash kutoka kwa ‘Umara bin Umayr amesema: "Kilipoletwa
kichwa cha Ibni Ziyad pamoja na vichwa vya sahibu zake vikawekwa ndani ya
msikiti wa Al Rahbah, niliwasikia watu wakiseama: "Kesha kuja kesha kuja
tena." Nikaliona joka kubwa lililokuja na kuvipitia vichwa vyote
vilivyokuwepo kisha lilipowasili penye kichwa cha Ibni Ziyad likaingia ndani ya
pua yake na kubaki humo muda, kisha likatoka na kuondoka taratibu mpaka
likatoweka. Nyoka huyo huyo alirudia kufanya hivyo mara mbili au tatu."
Attimidhy
3939
Amesema
Ibrahim Al-Nukhaiy (Radhiya Llahu anhu): "Ningelikuwa
mimi miongoni mwa waliomuua Al-Husayn kisha nikaingia Peponi, ningeliona haya
kuuangalia uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)."
Attabarani.
Waliuliwa
pamoja na Al-Husayn (Radhiya Llahu
anhu)
wengi kati ya watu wa nyumba yake.
Katika
ndugu zake aliuliwa:
Jaafar na
‘Abbaas na Abubakar na Muhammad na Uthman.
Katika
watoto wake:
Ali Al
Akbar (huyu si Ali Zayn al Abidiyn) na Abdullah.
Katika
watoto wa Al-Hasan:
Abdullah na
Al-Qaasim na Abubakar
Katika
watoto wa ‘Aqiyl:
Ja’afar na
Abdullah na Abdur-Rahman na Abdullah bin Muslim na Muslim bin ‘Aqiyl aliyeuliwa
Al-Kuufah tokea mwanzo.
Katika
watoto wa Abdullahi bin Ja’afar:
Aun na
Muhammad
Watu kumi
na nane katika watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Sallam), wote waliuliwa kwa dhulma na uadui katika vita hivi
ambavyo idadi ya pande mbili hazikuwa sawa.
Lakini
ajabu ni kuwa miongoni mwa waliouliwa waliokuwa pamoja na Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) walibeba majina ya Abubakar bin Ali na ‘Uthmaan bin Ali na
Abubakar bin Hasan, lakini huwasikii kutajwa unaposikiliza kanda za kaseti za
Kishia au unaposoma vitabu vyao vilivyoandikwa juu ya kuuliwa kwa Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu), ili pasisemwe kuwa Ali bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu)
na watu wa nyumba yake waliwapa watoto wao majina ya Abubakar na ‘Umar na
‘Uthmaan, na kwamba Al-Hasan (Radhiya Llahu anhu) alimpa mwanawe jina la
Abubakar.
Kutoka kwa
Ummu Salamah (Radhiya Llahu anha) amesema:
"Jibril alikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
na Al-Husayn alikuwa pamoja nami. Akalia Al-Husayn. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
akaingia na kumuinamia. Jibril akamuuliza: "Unampenda ewe Muhammad?"
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
akasema: "Ndiyo nampenda."
Akasema:
"Hakika umati wako watamuua na ukitaka nitakuonyesha udongo wa ardhi
atakaouliwa juu yake." Akamuonyesha, na ardhi hiyo inaitwa Karbalaa."
Imam Ahmad
katika 'Fadhail'
Imepokelewa
kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Llahu
anhu)
kuwa amesema: "Nilimuota Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) katika
nusu ya mchana nywele zake zikiwa zimetimka na mwili wake umejaa vumbi huku
akiwa amebeba chupa ndani yake mna damu. Nikamuuliza: "Ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu, kitu gani hiki?"
Akasema:
"Damu ya Al-Husayn na sahibu zake, sijaacha kuifuatilia mpaka leo."
Anasema
‘Umarah: "Msimulizi wa hadithi hii; tukayahifadhi hayo tukagundua kuwa ile
ndiyo siku aliyouliwa."
Imam Ahmad
mlango wa 'Musnad Abdullah bin ‘Abbaas'
Na hivi
ndivyo alivyokufa Shahiyd Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) na aliyeamrisha kuuliwa ni ‘Ubaydullah bin Ziyad ambaye hajaishi muda mrefu naye pia akauliwa, na
aliyemuwa ni Al Mukhtar bin Abi Ubayd kwa kulipa kisasi cha Al-Husayn.
Al Mukhtar
alikuwa miongoni mwa waliomuacha mkono Muslim bin ‘Aqiyl kama walivyofanya watu
wa mji wa Al-Kuufah waliomtaka Al-Husayn (Radhiya
Llahu anhu) aje kwao wakamuahidi kuwa watapigana kwa ajili yake.
Wote
walimuacha mkono ‘Aqiyl akauliwa, hapana hata mmoja aliyekwenda kumsaidia. Na
alipokuja Al-Husayn (Radhiya Llahu
anhu)
hali ikawa ni ile ile wote walimuacha mkono akauliwa, hapana hata mmoja
aliyekwenda kumsaidia isipokuwa Al Hurr bin Yazid At-Tamimiy na wachache
aliokuwa nao, hawa ndio waliomsaidia, na wote hawa walitoka katika jeshi la
Ubaydullah bin Ziyad. Ama watu wa Al-Kuufah wote walimuendea kinyume wakamuacha
mkono, hapana hata mmoja aliyeunyanyua mkono wake kumsaidia. Na hii ndiyo
sababu kila mwaka wanaendelea kupiga vifua vyao na kufanya wanayofanya kwa
majuto ya makosa
1- Kuuliwa kwa Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni msiba mkubwa kwa
Waislamu wote, hasa kwa vile yeye ni mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) na kipenzi chake na manukato yake mazuri. Hata
hivyo Waislamu walikwishapitiwa kabla yake na misiba mingi sana ikiwemo kuuliwa
kwa Sayiduna Ali bin Abi Talib (Radhiya
Llahu anhu) baba yake Al-Husayn, ambaye bila shaka daraja yake ni kubwa
zaidi kupita ya Al-Husayn.
Kabla ya
hapo misiba mikubwa zaidi ilipatikana ya kuuliwa kwa Khalifa wa pili wa
Waislamu ‘Umar bin Khattwaab na Khalifa wa tatu ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Llahu anhum).
Kabla ya
wote hao, Mitume ya Mwenyezi Mungu
2- Haijuzu kwa Muislamu anapopatwa na msiba au
kwa ajili ya kumbukumbu ya msiba wowote kufanya
vitendo vinavyokwenda kinyume na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam)
"Hayupo
pamoja nasi atakayejipiga makofi ya mashavu akachana nguo zake na kutamka
maneno ya kijahilia (yaliyokuwa yakitamkwa na washirikina kabla ya
Uislamu)."
Al-Bukhaariy
Na akasema:
"Mimi
najitenga mbali na (kila) mwenye kupiga kelele na mwenye kukata nywele na
mwenye kuchana nguo." (anapokutwa na msiba).
Muslim –
Kitab al Iman
Na akasema:
"Kwa
hakika mwenye kuomboleza kwa kupiga kelele asipotubu atavalishwa siku ya Kiama
ngao ya
Muslim –
Kitab al Iman
Kwa hivyo
ni wajibu kwa kila Muislamu anapopatwa na msiba aseme
"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na
Kwake Yeye tutarejea."
Al Baqarah-156
3- Zipo riwaya zinazosema kuwa kichwa cha
Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) kilipelekwa
Sham kwa Yazid na kilipowekwa mbele yake, Yazid alilia
Na ziko
riwaya nyingine zinazosema kuwa; kichwa chake hakikupelekwa Sham, bali alizikwa
huko Karbalaa mahali alipofariki – Mwenyezi Mungu Ndiye Ajuae.
Anasema
Shaykh ‘Uthmaan Al-Khamiys katika kitabu chake 'Hiqbah mina ttariykh':
"Yazid
hakushiriki kabisa katika kuuliwa kwa Al-Husayn, wala hakutoa amri hiyo. Na
huku si katika kumtetea Yazid, bali Yazid alimtuma ‘Ubaydullah bin Ziyad kumzuia tu Al-Husayn
asiweze kuingia mji wa Al-Kuufah, na wala hakumuamrisha kumuua, bali Al-Husayn
mwenyewe alielewa hayo akataka aruhusiwe kwenda Sham kwa Yazid ili akauingize
mkono wake ndani ya mkono wa Yazid, lakini ‘Ubaydullah alikataa akashikilia kuwa lazima
asalimu amri kwake.
Funga ya
siku ya ‘Ashuraa haina uhusiano wowote na kuuliwa kwa Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) kama inavyodaiwa,
bali inatokana na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) kama ilivyosimuliwa katika Sahih
Al-Bukhaariy kuwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya
Llahu anhuma) alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Sallam) alipoingia Madina aliwakuta
Mayahudi wakifunga siku ya ‘Ashuraa akawauliza: "Kwa nini mnafunga siku hii?" wakamuambia:
"Hii ni siku tukufu ambayo Mwenyezi Mungu alimuokoa Musa na kaumu yake
akamzamisha Firauni na kaumu yake. Musa akafunga siku hii kumshukuru Mwenyezi
Mungu, na sisi tunafunga." Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi
wa Sallam) akasema: "Na sisi tunamsitahiki zaidi Musa kupita nyinyi."
Akafunga Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa Sallam) na akaamrisha watu wafunge.
Marejeo:
Siyar aalaam an Nubalaa - Imam
Adh-dhahaby
Hiqbah minat Tariykh - Shaykh Uthmaam Khamiys
Al Bidayah wan Nihayah - Imam Ibni Kathiyr
Maqtal Al_Husayn
- Naasir bn Muhammad Al
Ahmad
[1] Imam Ahmad na Abu Yaala na Al Bazaar na Attabarani
[2] Siyar aalam al Nubalaa (Imam Adh-Dhahabiy)
[3] Ibni Asakir katika 'Tariykh'
[4] Ibni Asakir katika 'Tariykh'184/183/14
[5] Hiqbah mina Tariykh (Shaykh ‘Uthman Al-Khamiys)
[6] Hiqbah mina Tariykh (Shaykh ‘Uthman Al-Khamiys)
[7] Al Bidaya wal Nihaya (Ibni Kathiyr)
[8] Maqtal Al-Husayn (Naasir bin Muhammad Al Ahmad)
[9] Abulr-Razzaq Al Musawiy al Muqrum (Man qatal l Hussain)