Mapenzi ya Ahli Sunnah juu ya Ahlil Bayt

(Watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)

 

Mapenzi yetu Hadithi ya shuka Nani Ahlul Bayt? Al Mahdi na ‘‘Umar Utangulizi
Fadhila Makhsusi Fadhila za ujumla Fadhila za Ahlul Bayt Elimu ya Ghaibu Watu wa Ukoo
Ibni  Abbas (Radhiyal llahu anhuma) Al Abbas (Radhiya Llahu anhu) Al Hassan na Al Hussayn Fatima (Radhiya Llahu anha) Aly (Radhiya Llahu anhu)
Aly bin Musa ‘Al Ridha Musa bin Jaafar ‘Al Kadhim Jaafar As Sadeq Al Baaqer Ali Zeiynul Aabidiyn
Tafsiri ya Al Iyashi Nani Mnafiki Nani Sahaba Wake zake Muhammad bin Musa ‘Al Jawaad
    Hitimisho Wajibu wetu Kuoleana

               Utangulizi

Mmoja katika wana falsafa wa zamani alisema:

“Haki yote haiwezi kumilikiwa na upande mmoja, wala makosa yote hayawezi kuwepo upande mwingine, bali kila upande husibu sehemu yake. Mfano wa kundi la vipofu waliopelekwa mbele ya tembo wakatakiwa wamguse mwili wake, kisha kila mmoja aelezee umbile lake.

Katika muda mfupi waliopewa, hapana aliyewahi kukamilisha kuushika mwili wote. Kila mmoja alifanikiwa kugusa sehemu tu.

Aliyeushika mkonga akidhani kuwa amemshika tembo wote akasema: “Mwili wa tembo ni mrefu mfano wa gogo la mti”,

Aliyeshika mgongo akasema:

“Hapana, bali mwili wa tembo ni mfano wa jabali dogo”,

Aliyeshika sikio akasema:

“Nilivyouona mimi mwili wa tembo ni mpana, duara na laini”.

Kila mmoja anahadithia juu ya ile sehemu aliyodiriki kuishika katika muda mfupi ule akidhani anatoa maelezo kamili. Wote wamesema kweli, lakini kila mmoja amehadithia sehemu tu ya ukweli anoujua yeye akidhani kuwa ndio ukweli wote.”

 

Hitilafu husababishwa na mambo mengi, yakiwemo upeo wa kufahamu, kupenda, matamanio ya nafsi, mielekeo ya elimu, ya kifikra, kuiga waliotangulia, kupenda umaarufu, kupenda ukubwa, hitilafu za ustaarabu. Wengine huiga waliyowakuta nayo wazee wao, na wengine wanafuata mafundisho ya walimu wao wanaowaamini n.k. Na wengine huiendeleza hitilafu kwa sababu ya ubishi au kiburi tu, hata kama wataiona haki mbele yao.

Si vibaya kuhitilafiana, kwa sababu Mwenyezi Mungu Ametuumba kila mmoja na akili yake pamoja uwezo wake wa kufahamu.

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

æóáóæú ÔóÇÁ ÑóÈøõßó áóÌóÚóáó ÇáäøóÇÓó ÃõãøóÉð æóÇÍöÏóÉð æóáÇó íóÒóÇáõæäó ãõÎúÊóáöÝöíäó .ÅöáÇøó ãóä ÑøóÍöãó ÑóÈøõßó æóáöÐóáößó ÎóáóÞóåõãú.

«Na Mola wako Mlezi Angelipenda Angewafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana, Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi Amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu Amewaumba.»

Huud-118-119

Anasema Al Hasan Al Basry: æóáöÐóáößó ÎóáóÞóåõãú maana yake ni kuwa; Amewaumba ili wakhitalifiane.

 

Wenye kukhitilifiana wanaweza kusikilizana na kufahamiana ikiwa hapana chuki baina yao, lakini chuki inapoingia, hayapatikani tena masikilizano wala kufahamiana. Chuki inaondoa mapenzi na inavunja uhusiano mwema na inaendeleza bughudha na kuondoa uwezekano wowote wa masikilizano.

 

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) usiku mmoja aliamka uso wake ukiwa mwekundu huku akisema:

 

áÇ Åöáåó ÅöáÇø Çááå¡ æóíúáñ ááÚóÑóÈö¡ ãöäú ÔóÑó ÞóÏö ÇÞúÊóÑóÈ

Laa ilaaha illa Llah, Ole wao Waarabu kwa shari iliyo karibu

Alirudia maneno haya mara tatu.

 

Maulamaa wanasema kuwa;‘Hii ilikuwa ishara kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) juu ya hitilafu itakayotokea baada yake’.

 

Hitilafu iliyopo hivi sasa baina ya Shia na Sunni inakula kibichi na kikavu.

Mamia ya Waislamu wanauliwa kila siku huko Iraq, na wanaendelea kuuliwa, na mamilioni wengine wamejeruhiwa. Mamilioni wamekwishaihama nchi yao, na mamilioni hawana kazi wala bazi.

Lebanon, nchi iliyojaa neema, nchi ya elimu na ziraa. Nchi ya historia na sanaa, leo kila kitu kimesimama katika nchi hii kwa sababu ya fitna ya umadhehebu. Nchi haina serikali, ina majeshi mawili, kila moja linadai kuwa wao ndio wenye kuipenda nchi. Ina makundi mawili, kila moja linalituhumu jingine kuwa ni vibaraka. Watu hawaelewi wanapelekwa wapi, kila siku mapambano ya risasi na mabomu.

Huko Yemen, maelfu ya watu wamekwishapoteza maisha yao katika mapambano baina ya majeshi ya serikali na makundi ya watu wa kabila la Houthi wenye kufuata madhehebu ya Shia Ishnaashariyah.

Hii ni fitna iliyopenyezwa katika mwili wa Waislamu kwa ajili ya kuwagawa. Inatumiliwa na kuchochewa na wale wasiopenda kuuona umma wao umetulia huku ukipiga hatua katika kuziendeleza nchi zao na kuwaelimisha watu wao.

Na katika kila pembe ya ulimwengu chuki hizi zinaanza kupasua njia kidogo kidogo na ni Mwenyezi Mungu peke Yake Anaelewa wapi yataishia.

 

Mambo yaliyotokea miaka elfu moja mia nne iliyopita yanaendelea kuwagawa na kuwafarikisha Waislamu hadi hivi sasa katika karne hii ya satellite na computer.

Umma huu ni Umma mmoja, Mungu wetu ni Mungu Mmoja, na Dini yetu ni moja na Mtume wetu ni mmoja, Lengo letu ni moja na adui yetu ni mmoja, kwa nini basi hatuungani tukawa kitu kimoja?

Ikiwa kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni Ushia, basi sisi sote ni Mashia, na ikiwa kuwapenda Masahaba (Radhiya Llaahu ‘‘anhum) ni Usunni, basi sote tuwe Masunni. Waislamu hawatakuwa na kheri yoyote ikiwa watawachukia watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ambao Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ametuamrisha tuwaswalie kila tunapomswalia.

 

Na Waislamu hawatakuwa na kheri yoyote ikiwa watawachukia Sahibu zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) (Radhiya Llaahu ‘anhum), ambao baada ya kufariki dunia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), wao ndio walioibeba bendera na kuueneza Uislamu kila pembe ya ulimwengu.

Waislamu wanatakiwa waone fahari kubwa kila wanapotajwa Masahaba hawa watukufu (Radhiya Llaahu ‘‘anhum), kwa sababu wao ndio waliotuletea Uislamu. Wao ndio waliotufikishia Qur-aan tukufu ambayo ni Nuru itokayo kwa Mola wetu.

Mwenyezi  Mungu Amewajaalia wao kuwa ndiyo sababu ya kutufikia dini hii kote huku tuliko. Kwa juhudi yao kubwa na kujitolea kwao mhanga kwa hali na mali waliuwezesha Uislamu kuingia na kuenea na kufuatwa na kupendwa Arabuni kote, Iran, Asia, Afrika hadi Ulaya na Marekani.

Wangelikuwa watu hawa ni makafiri basi wangelituletea ukafiri badala ya Uislamu. Wangelituletea misalaba na masanamu badala ya Qur-aan na Swalah na salamu (amani ?).

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) kuwa hitilafu baina ya madhehebu ya Kiislamu si katika kiini cha dini na asili ya mafundisho yake, kama vile kuabudiwa Mwenyezi Mungu Mmoja na kwamba Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni Mtume Wake. Hitilafu haikuwa juu ya Qur-aan tukufu, kwani AlhamduliLlaah Waislamu wote kwa pamoja wanaamini kuwa Qur-aan hii tuliyonayo hivi sasa ndiyo ile ile aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) miaka elfu moja mia nne iliyopita bila ya kubadilika.

Tunaelewa kuwa walikuwepo baadhi ya Maulamaa wachache wa madhehebu ya Kishia mfano wa Nuwriy At-Tubrusiy aliyeandika kitabu ‘Faslu l Khitwaab fiy ithbaat tahriyf kitaab Rabbil Arbaab’, akidai ndani ya kitabu hicho kuwa Qur-aan hii tuliyonayo ilibadilishwa na kupunguzwa na kuzidishwa, lakini AlhamduliLlaah katika wakati wetu huu hapana tena anayeziamini kauli hizo hata miongoni mwa wengi kati ya Mashia, ikiwa si wote, na kama watakuwepo basi watakuwa wachache sana.

 

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) pia kuwa hitilafu hii haikuwa katika kuharamisha au kuhalalisha mambo yanayojulikana katika dini kuwa ni ya dharura kama vile uharamu wa Pombe, kula nyama ya nguruwe n.k.

Hapana shaka yoyote kuwa ipo hitilafu juu ya baadhi ya mambo yanayohusiana na Itikadi ‘Aqiydah’, kama vile kumuomba mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kuyatukuzu makaburi ya watu wema.

Naelewa pia kuwa wapo wanaojinasibisha na Ahlus Sunnah wenye kuwaomba wengine wasiokuwa Mwenyezi Mungu na kuyatukuza makaburi ya watu wema, lakini tofauti iliyopo baina ya Sunnah na Shia ni kuwa Maulamaa wa Ahlus Sunnah wanayakemea na kuyakataza mambo haya, wakati maulamaa wa Shia wanayanyamazia na kuyapa kipaumbele.

 

Al Mahdi na ‘‘Umar

Anasema Dr. Ahmed Al Kaatib mwanachuoni wa Kishia kutoka Iraq ambaye ni mwalimu katika vyuo vikuu mbali mbali vya dini huko Iraq, Kuwait na Iran na ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Majadilianao ya Ustaarabu, 'Al Hiwaar al Hadhwaariy', ambayo makao yake makuu yapo London, alisema:

"Nimefanya utafiti ulionipa uhakika kuwa hitilafu iliyopo baina ya Sunnah na Shia hauna msingi wowote na imenithibitikia baada ya kuidurusu kadhia hii kuwa hitilafu zilizokuwepo ni za kisiasa tu na wala si za itikadi.

Baada ya kufanya utafiti wangu ulionichukua muda mrefu sana imenithibitikia kuwa hitilafu iliyokuwepo baina yetu (Shia na Sunnah) ni juu ya Imam Al Mahdi na pia yale madai kuwa ‘‘Umar (Radhiya Llaahu ‘‘anhu) alimpiga Bibi Faatwimah Az Zahraa (‘Alayhas Salaam) siku ile watu walipofungamana na Abu Bakr (Radhiya Llaahu ‘anhu).

Baada ya kumaliza utafiti wangu," anaendelea kusema Ahmed Al Kaatib ambaye hadi hivi sasa ni mwalimu mkubwa wa madhehebu ya Shia Ithnaashariyah; "imenidhihirikia kuwa madai hayo kuwa ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) alimpiga Bibi Faatwimah (Alayhas Salaam) hayana msingi wowote na kwamba ni uzushi ulioenezwa na kuandikwa katika vitabu mbali mbali vya historia kwa ajili ya kuipa nguvu nadharia ya Uimamu, nadharia ambayo inafutika ikithibiti kuwa ‘Aliy (Radhiya Llaahu ‘anhu) alikubali kwa hiari yake kufungamana na Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan (Radhiya Llaahu ‘anhum) walipochaguliwa kuwa Makhalifa, kwa sababu angelikuwa Imam ‘Aliy (‘Alayhis Salaam) amechaguliwa na Mwenyezi Mungu, basi asingekubali kufungamana nao kwa hiari yake.

Wazushi wa kisa hicho walidai kuwa Aliy (Alayhis Salaam) alikubali kufungamana na Abu Bakr baada ya Umar kuingia kwa nguvu nyumbani kwake na kumpiga mkewe ambaye ni  Bibi Faatwimah (‘Alayhas Salaam) binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) mpaka mimba ikamtoka."

Anasema Ahmed Al Kaatib:

"Nilikifanyia uchunguzi kisa hiki lakini sijakikuta katika kitabu chochote chenye kutambulika na kuaminika miongoni mwa vitabu vya Kishia kama vile Al Kafi na vyenginevyo.

Kinachokikanusha zaidi kisa hicho ni ule uhusiano mzuri uliokuwepo baina yao hadi kufikia kuwa ‘Aliy na Faatwimah (‘Alayhimas Salaam) walimuozesha binti yao Ummu Kulthum kwa ‘Umar.

Itawezekanaje basi, kwa mama akubali kumuozesha binti yake mtu aliyempiga mpaka mimba ikamtoka?"

"Ama kisa cha Uimamu," anaendelea kusema Ahmed Al Kaatib: "Hata Ayatollah Sistani ametamka kuwa jambo hili si katika mambo ya msingi wa dini kwa Shia, na kwamba linaweza kujadiliwa.

Nilifuatilia vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa Kishia katika karne ya tatu na ya nne na ya tano Hijri nikaona kuwa hapana ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Imam huyu alizaliwa, na kwamba Sayed Murtadha na Al Umani na wengine wanasema: "Sisi tunaona kuwa haya ni mambo ya kukisia tu kwa dalili za kiakili na hatuna dalili za kielimu zisizopingika.

Kwa hivyo nadharia ya kuwepo kwa Imam wa kumi na mbili mwenye kusimamia, anayetokana na Imam Husayn (Radhiya Llaahu ‘anhu) aliyepewa jina na Muhammad bin Hasan Al Askary na nadharia ya kutoweka kwake, si katika itikadi za Ahlul Bayt, bali wamenasibishwa nazo na baadhi ya waandishi.

Na hivi sasa kwa vile serikali ya Iran imeamua kuipa nguvu nadharia ya Utawala wa mwanachuoni 'Wilayat al Faqiyh' na imeamua kufuata nidhamu ya kuchagua viongozi wa dini kwa njia ya kushauriana, 'Shuura' na kuchagua viongozi wa nchi kwa njia ya demokrasia (democracy), kwa hivyo haya yanafuta ile kauli ya kuwa kiongozi lazima awe aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, na badala yake mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi ikiwa watu wataridhka naye na kumchagua, (pia siyo lazima awe katika ‘Ahlul Bayt’)

 

Kwa ajili hiyo ile khitilafu iliyokuwepo baina ya Shia na Sunnah juu ya Uimamu sasa itakuwa ishaondoka pia kwa sababu Shia hawaamini tena juu ya ulazima wa kuwepo Imam aliyetoweka akaingia ndani ya pango na wala hawasubiri tena kutoka pangoni alipoingia miaka elfu moja iliyopita ili wapate kuisimamisha dola ya Kiislamu.

Na lile sharti ya kuwa Imam mwenye kuwaongoza Waislamu lazima awe Aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na awe aliyekingwa asiyefanya makosa anayetokana na ukoo maalum, nayo pia imeondoka kwa sababu kiongozi hivi sasa anachaguliwa kwa njia ya uchaguzi au kwa kushauriana ‘Shuura’."

Mwisho wa maneno ya Al Kaatib

(Website ya Al Arabiyah.net. Tarehe 27 May 2008)

 

Anasema mwanachuoni mwengine maarufu Dr. Musa al Musawiy katika kitabu chake ‘Ash Shi’ah wat Tas’hiyh’’:

«Baada ya utafiti mkubwa nilioufanya katika kulichambua tatizo hili la hitilafu kubwa iliyopo baina ya Shia Ithanaashariyah na Ahlus Sunnah, nimegundua kuwa yale yaliyotokea baada ya kufariki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) siyo sababu ya hitilafu hii kubwa, wala si kwa sababu ya kuwa ‘Aliy (Alayhis Salaam) ndiye anayestahiki ukhalifa baada ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), kwa sababu nawaona wenye kufuata madhehebu ya Shia Zaydiyah wapo kwa mamilioni katika ulimwengu na wanaishi kwa wema na mapenzi na masikilizano baina yao na  Masunni.

Kwa hivyo sababu ya hitilafu baina ya Shia Ithnaashariyah na Madhehebu mengine ya Kiislamu ni ule msimamo wao dhidi ya Makhalifa walioongoka na kuwatukana kwao na kuwalaani, jambo ambalo halipo upande wa Shia Zaydiyah na makundi mengine. Lau kama Shia Ithnaashariyah walingelifuata mwenendo wa Shia Zaydiyah basi hitilafu ingelipungua sana na tatizo lingekuwa dogo. Lakini Shia Ithnaashariyah wameingia katika shimo la kuwatukana Makhalifa walioongoka na kuwalani na kuwashambulia,  jambo linalosababisha hitilafu hii izidi na kuongezeka.»

Ash Shi’ah wat Tashiyh’. Uk.4

 

Kutokana na maelezo haya ya Maulamaa wa Kishia, inatubainikia kuwa laiti kama wafuasi wa Shia wangeliacha mwenendo wa kuwatukana na kuwalaani Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pamoja na wake zake Mama wa Waislamu, na lau kama wataacha mwenendo wa kuwatukana na kuwalaani Waislamu wenzao katika siku za Muharram na kuwaapiza kwa kula viapo kuwa lazima watalipa visasi vya kuuliwa kwa Al Husayn, basi sehemu kubwa ya chuki baina ya makundi mawili haya yangeondoka.

 

Masunni wanawaheshimu sana na kuwatukuza watu wote wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na wanawaheshimu pia Masahaba wake (Radhiya Llaahu ‘anhum), na wanaamini kuwa wote hao ni watu bora ambao Mwenyezi Mungu Ameridhika nao, kama ilivyoandikwa katika Qur-aan tukufu.

Masunni wanajitenga na kila aliyeshiriki katika vile vita vilivyosababisha kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llaahu ‘anhu), na wanajitenga na wote waliomuua na waliosababisha kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llaahu ‘anhu) na aila yake, na wanaamini kuwa wameuliwa kwa dhulma na kwa uadui, na kwamba wote wamekufa Shahiyd.

Wakati huo huo Masunni wanashangazwa wanaposikia vilio na maneno ya kulipwa visasi katika vikao vya Al Husayniyah. Maneno kama vile:

íÇ áÊÇÑÇÊ ÇáÍÓíä

Maneno yanayohimiza kulipwa visasi kwa ajili ya kuuliwa Al Hussayn (Radhiya Llahu anhu).

Wanajiuliza; visasi hivyo watalipiwa nani wakati wote waliomuua Al Husayn (Radhiya Llaahu ‘anhu) wamekwishafariki dunia.

 

Al Hurr bin Yazid At-Tamimiy keshakufa, ‘Umar bin Dhil Jawshan keshakufa, Zara'a bin Shariyk keshakufa, ‘Umar bin Sa’ad  keshakufa, Ubaydullah bin Ziyad naye pia keshakufa, na wote walioshiriki katika vita vile wamekwisharudi kwa Mola wao tokea miaka elfu moja mia nne iliyopita.

Maneno haya ya kuhimiza kulipa visasi yanatafsiriwa na Ahlus Sunnah kuwa wao ndio wanaokusudiwa, na haya ni katika chuki zilizopandikizwa na wasiopenda kuwaona Waislamu wa kila  Madhehebu wakiishi pamoja kwa kupendana na kushirikiana katika kuziendeleza mbele dola zao.

 

Nani Ahlul Bayt?

Mojawapo ya hitilafu kubwa baina ya Sunnah na Shia ni juu ya tafsiri ya neno 'Ahlul Bayt'. (Watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Wakati Shia wanasema kuwa Ahlul Bayt ni Aly bin Abu Talib na Fatima binti Muhammad na wanawe (Radhiya Llahu anhum) peke yao, Ahlus Sunnah wanaitakidi kuwa Ahlul Bayt ni wote hao waliotangulia kutajwa pamoja na wake wa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na binti zake waliobakia wasiotambuliwa na Shia, na pia wajukuu zake na baadhi ya waliohusiana naye katika ukoo wake.

Imeandikwa katika kamusi maarufu "Lisanul Arab" kuwa; mke na jamaa za mtu ni Ahli Bayti yake.

Na katika Qurani tukufu, Mwenyezi Mungu anawataja wake wa mtu kuwa ni Ahli yake.

Mwenyezi Mungu anasema:

ÞóÇáõæÇú ÃóÊóÚúÌóÈöíäó ãöäú ÃóãúÑö Çááøåö ÑóÍúãóÊõ Çááøåö æóÈóÑóßóÇÊõåõ Úóáóíúßõãú Ãóåúáó ÇáúÈóíúÊö Åöäøóåõ ÍóãöíÏñ ãøóÌöíÏñ

"Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa kutukuzwa."

Hud-73

Maulamaa wote wanasema kuwa neno (Watu wa nyumba), katika aya hii anakusudiwa Sarah mke wa Nabii Ibrahim (Alayhi ssalaam).

 

Na Akasema:

ÅöÐú ÑóÃóì äóÇÑðÇ ÝóÞóÇáó áöÃóåúáöåö ÇãúßõËõæÇ Åöäøöí ÂäóÓúÊõ äóÇÑðÇ

"Alipo uona moto, akawaambia watu wake (Ahli yake): Ngojeni! Mimi nimeuona moto."

Taha-10

Inajulikana hapa pia kuwa neno (Ahli yake) anakusudiwa mke wa Nabi Musa (Alayhi ssalaam) aliyekuwa amefuatana naye katika safari hiyo.

 

Na Mwenyezi Mungu akasema pia:

ÞóÇáóÊú ãóÇ ÌóÒóÇÁ ãóäú ÃóÑóÇÏó ÈöÃóåúáößó ÓõæóÁðÇ ÅöáÇøó Ãóä íõÓúÌóäó Ãóæú ÚóÐóÇÈñ Ãóáöíãñ

 

"Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewa adhabu chungu."

Yusuf-25

Neno (Ahlika katika aya hii) na maana yake ni 'mkeo' aliyekusudiwa ni mke wa Al Aziz.

Kwa hivyo dalili zote zinaonyesha kuwa neno Ahlul Bayt au Ahl linatumika zaidi kwa maana ya mke.

Na katika Surat Al Ahzab kuanzia aya ya 28 hadi ya 33 Mwenyezi Mungu anasema:

íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáäøóÈöíøõ Þõá áøöÃóÒúæóÇÌößó Åöä ßõäÊõäøó ÊõÑöÏúäó ÇáúÍóíóÇÉó ÇáÏøõäúíóÇ æóÒöíäóÊóåóÇ ÝóÊóÚóÇáóíúäó ÃõãóÊøöÚúßõäøó æóÃõÓóÑøöÍúßõäøó ÓóÑóÇÍðÇ ÌóãöíáðÇ¡ æóÅöä ßõäÊõäøó ÊõÑöÏúäó Çááøóåó æóÑóÓõæáóåõ æóÇáÏøóÇÑó ÇáúÂÎöÑóÉó ÝóÅöäøó Çááøóåó ÃóÚóÏøó áöáúãõÍúÓöäóÇÊö ãöäßõäøó ÃóÌúÑðÇ ÚóÙöíãðÇ

"Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri.

 

Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa."

 

íóÇ äöÓóÇÁ ÇáäøóÈöíøö ãóä íóÃúÊö ãöäßõäøó ÈöÝóÇÍöÔóÉò ãøõÈóíøöäóÉò íõÖóÇÚóÝú áóåóÇ ÇáúÚóÐóÇÈõ ÖöÚúÝóíúäö æóßóÇäó Ðóáößó Úóáóì Çááøóåö íóÓöíÑðÇ¡ æóãóä íóÞúäõÊú ãöäßõäøó áöáøóåö æóÑóÓõæáöåö æóÊóÚúãóáú ÕóÇáöÍðÇ äøõÄúÊöåóÇ ÃóÌúÑóåóÇ ãóÑøóÊóíúäö æóÃóÚúÊóÏúäóÇ áóåóÇ ÑöÒúÞðÇ ßóÑöíãðÇ

"Enyi wake wa Nabii! Atakaye fanya uchafu dhaahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Na miongoni mwenu atakeye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu."

íóÇ äöÓóÇÁ ÇáäøóÈöíøö áóÓúÊõäøó ßóÃóÍóÏò ãøöäó ÇáäøöÓóÇÁ Åöäö ÇÊøóÞóíúÊõäøó ÝóáóÇ ÊóÎúÖóÚúäó ÈöÇáúÞóæúáö ÝóíóØúãóÚó ÇáøóÐöí Ýöí ÞóáúÈöåö ãóÑóÖñ æóÞõáúäó ÞóæúáðÇ ãøóÚúÑõæÝðÇ

"Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema."

æóÞóÑúäó Ýöí ÈõíõæÊößõäøó æóáóÇ ÊóÈóÑøóÌúäó ÊóÈóÑøõÌó ÇáúÌóÇåöáöíøóÉö ÇáúÃõæáóì æóÃóÞöãúäó ÇáÕøóáóÇÉó æóÂÊöíäó ÇáÒøóßóÇÉó æóÃóØöÚúäó Çááøóåó æóÑóÓõæáóåõ ÅöäøóãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóåõ áöíõÐúåöÈó Úóäßõãõ ÇáÑøöÌúÓó Ãóåúáó ÇáúÈóíúÊö æóíõØóåøöÑóßõãú

ÊóØúåöíÑÇð

" Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba (ya Mtume), na kukusafisheni baarabara."

 

Ahlu Sunnah wanasema kuwa; kama vile katika aya zote zilizotangulia, kila anapotajwa Ahli ya mtu hukusudiwa mke, na katika aya hizi pia Mwenyezi Mungu anapotaja Ahli anawakusudia wake zake Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Ukizisoma kwa utulivu aya hizi utaona kuwa kuanzia aya ya 28 Mwenyezi Mungu anazungumza na wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam):

Mwenyezi Mungu anasema : "Ewe Nabii! Waambie wake zako….”, Akaendelea: "Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine.” Akaendelea kuwahutubia: «Kaeni majumbani mwenu» «Toeni Zaka». «Mt'iini Mwenyezi Mungu». Mpaka Aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba (ya Mtume), na kukusafisheni baarabara." Yote haya wanaambiwa wake zake Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuanzia aya ya 28 hadi 33.

Hivi ndivyo ulivyo mfumo wote wa aya hizi zilizokamatana na haziwezi kutenganishwa isipokuwa kama mtu anataka kuvuka mipaka na kwenda kinyume na nassi.

 

Mtu anaweza kuuliza: ‘Kwa nini basi Mwenyezi Mungu Ametumia ‘sigha’ (mfumo wa maneno) ya wingi wa wanaume na wanawake kwa pamoja aliposema:

ÅöäøóãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóåõ áöíõÐúåöÈó Úóäßõãõ ‘Ankum’

Ikiwa Amewakusudia wake za Mtume (Swallah Llahu alyhi wa sallam) kwa nini asitumie sigha ya wanawake peke yao akasema:

ÅöäøóãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóåõ áöíõÐúåöÈó Úóäßõä  ‘Ankunnaõ

Kwa nini asitumie sigha ya wanawake kama alivyotumia katika aya nyingine zilizomo ndani ya mfumo huu?

Majibu ni kuwa; Aya za mwanzo Mwenyezi Mungu Alipozungumza juu ya hukmu za kisheria na makatazo na maamrisho yanayowahusu wake za Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alitumia ‘Nuun’ ya wanawake Úäßä  lakini alipozungumza juu ya wema anaotaka kuuingiza ndani ya nyumba ile pamoja na kuwasafisha watu wa nyumba ile barabara, alimuingiza pia na mwenye nyumba ambaye ni mwanamume naye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ili kheri hiyo iwaenee wote. Na kawaida katika lugha ya kiarabu wanapotajwa wanawake na wanaume kwa pamoja hutumiwa wingi wa wanaume Úäßã ‘Ankum’

Nani wanaostahiki zaidi kusafishwa na kutakaswa kuliko wake zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), watu wa nyumba yake, mama wa Waislamu, na wanaostahiki pia ni jamaa zake, watu wa aila yake. Kwa sababu Mtume wetu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) anastahiki kuwa pamoja na kila kheri na kila jema na kila kilicho bora, na anastahiki zaidi kuwa pamoja na watu wema, naye haridhiki isipokuwa awe pamoja na watu wema, kwani wema lazima siku zote uwe katika mtiririko mmoja.

Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala alitaka kuwatakasa wake zake na jamaa zake, akamtunukia haya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

 

Ikiwa tumemkubali mke wa Nabi Musa (Alayhissalaam) katika aya tuliyotangulia kuitaja kuwa ni Ahli yake na tukamkubali mke wa Al Aziz kama ilivyokuja katika aya kuwa ni Ahli yake na tukamuingiza Sarah mke wa Nabi Ibrahim (Alayhissalaam) kuwa ni Ahli yake, juu ya kuwa katika aya ile Mwenyezi Mungu alitumia mfumo ule ule wa wingi wa wanaume na wanawake kwa pamoja Aliposema:

ÑÍãÉ Çááå æÈÑßÇÊå Úáíßã Ãåá ÇáÈíÊ

Alitumia neno (ÚáíßãAlaykum)

Kama alivyotumia (Úäßã Ankum) katika Suratul Ahzab aliposema:

ÅöäøóãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóåõ áöíõÐúåöÈó Úóäßõãõ ÇáÑøöÌúÓó Ãóåúáó ÇáúÈóíúÊö

Ikiwa tumewakubali wake wa Mitume wote hao kuwa ni watu wa nyumba, tunalazimika pia kuwakubali wake wa Mtume wetu Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa ni watu wa nyumba yake.

 

Hadithi ya shuka na dalili katika Hadithi

Kutokana na haya inafahamika zaidi tafsiri ya ile hadithi maarufu inayoitwa Hadiyth al Kisaa na maana yake ni hadithi ya nguo au hadithi ya shuka, wakati Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipowaingiza ndani ya shuka ile Aly na Bibi Fatima na Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum), kwa ajili ya kuwaingiza na wao katika zile baraka zilizoteremshwa ndani ya aya ile ya Surat al Ahzab.

Hadithi inasimulia kuwa baada ya kuwaingiza wote hao ndani ya shuka, akasema:

"Ãááåãøó åÄáÇÁ Ãåá ÈíÊí ÝÇÐåÈ Úäåã ÇáÑÌÓ æØåÑåã ÊØåíÑÇð

"Mola wangu hawa ni watu wa nyumba yangu, waondolee uchafu na uwasafishe baarabara."

Na Ummu Salama (Radhiya Llahu anha) mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipoingiza kichwa chake ndani ya shuka hiyo akasema:

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu na mimi ni katika watu wa nyumba yako.»

Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuambia:

ÊäÍí ÝÅäß Úáì ÎíÑ

"Wewe umo katika kheri wewe umo katika kheri."

Na maana yake ni kuwa Ummu Salama na wake wenzake wote wamekwisha tajwa na Mwenyezi Mungu katika aya hiyo na kwamba wao wamo katika kheri hiyo ya kusafishwa na kutakaswa.

Ndiyo maana akaambiwa:

"Wewe umo katika kheri wewe umo katika kheri."

Dalili nyingine inayothibitisha kuwa wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni katika watu wa nyumba yake imo katika Bukhari na Muslim na Attirmidhy na Annasaiy na wengine kama ilivyopokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipoulizwa na Masahaba:

"Vipi tukuswalie?

Akasema:

"Semeni:

Çááåã Õá Úáì ãÍãÏ æÃÒæÇÌå æÐÑíÊå¡ ßãÇ ÕáíÊ Úáì ÅÈÑÇåíã¡ æÈÇÑß Úáì ãÍãÏ æÃÒæÇÌå æÐÑíÊå¡ ßãÇ ÈÇÑßÊ Úáì Âá ÅÈÑÇåíã Åäß ÍãíÏ ãÌíÏ

"Mola wangu mswalie Muhammad na wake zake na vizazi vyake, kama ulivyomswalie Ibrahim, na umbariki Muhammad na wake zake na vizazi vyake kama ulivyowabariki watu wa nyumba ya Ibrahim hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa uliye Mtukufu."

Ikajulisha kuwa mke wa mtu na vizazi vyake ni watu wa nyumba yake.

 

Ikiwa mtu hajatoshelezwa na dalili zote tulizozinukuu kutoka katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam), basi ipo dalili nyingine katika Sahih al Bukhari itakayoondoa shaka yoyote iliyobaki kwa mwenye kuutafuta ukweli bila ya chuki moyoni mwake.

Inajulikana kuwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alisingiziwa uwongo katika kisa mashuhuri kinachojulikana kwa jina la Haadithatul If’k , uwongo ambao Mwenyezi Mungu aliteremsha aya katika Qurani tukufu kuukanusha, na wakati huo huo aya hizo ziliwaonya Waislamu kutorudia tena kueneza uvumi huo, na zikawatahadharisha juu ya adhabu kali itakayomfikia mwenye kurudia tena.

Wakati ule Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipanda juu ya membari yake kuhutubia, akasema:

"íÇ ãÚÔÑ ÇáãÓáãíä ãä íÚÐÑäí ãä ÑÌá ÞÏ ÈáÛäí ÃÐÇå Ýí Ãåáí¡ ÝæÇááøå ãÇ ÚáãÊ Úáì Ãåáí ÅáÇ ÎíÑÇð¡ æáÞÏ ÐßÑæÇ ÑÌáÇð ãÇ ÚáãÊ Úáíå ÅáÇ ÎíÑÇð¡ æãÇ ßÇä íÏÎá Úáì Ãåáí ÅáÇ ãÚí"

“Enyi Waislamu! Nani atakayenipumzisha na mtu aliyeniudhi katika Ahli yangu, kwani Wallahi sijaona kwa Ahli yangu isipokuwa kheri tupu, na hakuwa akiingia kwa Ahli yangu isipokuwa akiwa pamoja nami.”

Bukhari

Atakayechunguza, ataona kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amelitaja neno Ahly (watu wa nyumba yangu) katika hotuba hii fupi mara tatu, zote zikimaanisha mkewe Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha), ikituthibitishia kuwa neno Ahly lina maana ya mke.

 

Sisi tunawakubali na tunawapenda na tunawapa heshima kubwa na tunawatambua watu wote wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah LLahu alayhi wa sallam), wale wanaokubaliwa na Shia na pia wasiokubaliwa na Shia kuwa ni katika Ahlul Bayt kama vile ami zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah LLahu alayhi wa sallam), watoto wa ami zake pamoja na watoto wao (Radhiya Llahu anhum), hawa ambao Shia hawawatambui kuwa ni watu wa nyumba yake (Swallah LLahu alayhi wa sallam), kama walivyotajwa katika hadithi iliyotangulia, nao ni kama ifuatavyo:-

1.      Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam)

2.      Wake zake

3.      Binti zake wote

4.      Watu wa nyumba ya Al Abbas bin Abdulmuttalib

5.      Watu wa nyumba ya Aqiyl bin Abu Talib

6.      Watu wa nyumba ya Aly bin Abu Talib

7.      Watu wa nyumba ya Jaafar bin Abu Talib

Hawa wote wametajwa katika hadithi iliyotolewa na Muslim wakati Zeid bin Al Arqam (Radhiya Llahuanhu) alipoulizwa:

‘Wake zake si katika watu wa nyumba yake?’

Akasema:

‘Wake zake ni watu wa nyumba yake. Lakini watu wa nyumba yake (waliokusudiwa hapa) ni wale walioharimishwa kupokea sadaka.’

Akaulizwa:

‘Nani hao.

Akasema:

‘Hao ni watu wa nyumba ya Aly na watu wa nyumba ya Aqiyl na watu wa nyumba ya Jaafar na watu wa nyumba ya Abbas (Radhiya Llahu anhum).’

Kwa hiyvo watu wa nyumba hizo juu ya kuwa wengine hawakuwemo ndani ya ile shuka lakini wametajwa kuwa ni watu wa nyumba yake (Swallah LLahu alayhi wa sallam).

Wake zake bila shaka wanaingia katika watu wa nyumba yake kwa sababu ya kutajwa katika Suratul Ahzab kama ilivyotangulia, na ndiyo maana katika kuikamilisha aya hiyo Mwenyezi Mungu akasema :

{ æóÇÐúßõÑúäó ãóÇ íõÊúáóì Ýöí ÈõíõæÊößõäøó ãöäú ÂíóÇÊö Çááøóåö æóÇáúÍößúãóÉö Åöäøó Çááøóåó ßóÇäó áóØöíÝÇð ÎóÈöíÑ}

‘Na watajieni (watu) yasomwayo majumbani mwenu katka Aya za Mwenyezi Mungu na hikima (ya Mtume), kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri na Mjuzi wa mambo ya dhahiri.’

Al Ahzab-34

Na maana yake ni kuwa zifanyieni kazi zile aya zilizoteremshwa ndani ya nyumba zenu, kwa sababu Mwenyezi Mungu amezihusisha nyumba zenu kwa kuteremsha aya Zake, tofauti na nyumba nyingine. Na Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) ndiye anayehusika zaidi kwa sababu hazikupata kuteremshwa aya juu ya kitanda cha yeyote miongoni mwa wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) isipokuwa kwake.

 

Na watoto na wajukuu wa Al Hassan bin Aly na Al Hussayn bin Aly na Abdillahi bin Abbas na Muhammad bin Al Hanafiyah (mtoto wa Sayiduna Aly kwa mke mwengine), na Al Abbas bin Aly na wajukuu zao na wajukuu wa wajukuu zao, wote hao pia ni miongoni watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na hii ni kwa wale waliokuwa Waislamu.

Abu Lahab juu ya kuwa ni ami yake Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), lakini yeye hayumo katika Ahli yake kwa sababu hakuwa Muislamu.

Nabi Nuh (Alayhissalaam) allipomuona mwanawe amekimbilia jabalini na maji yanaanza kumfikia alimuomba Mwenyezi Mungu amuokowe.

Mwenyezi Mungu anasema :

æóäóÇÏóì äõæÍñ ÑøóÈøóåõ ÝóÞóÇáó ÑóÈøö Åöäøó ÇÈõäöí ãöäú Ãóåúáöí æóÅöäøó æóÚúÏóßó ÇáúÍóÞøõ æóÃóäÊó ÃóÍúßóãõ ÇáúÍóÇßöãöíäó {45}þ ÞóÇáó íóÇ äõæÍõ Åöäøóåõ áóíúÓó ãöäú Ãóåúáößó Åöäøóåõ Úóãóáñ ÛóíúÑõ ÕóÇáöÍò ÝóáÇó ÊóÓúÃóáúäö

ãóÇ áóíúÓó áóßó Èöåö Úöáúãñ Åöäøöí ÃóÚöÙõßó Ãóä Êóßõæäó ãöäó ÇáúÌóÇåöáöíäó {46)

“Na Nuhu alimuomba Mola wake akasema: ‘Ewe Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu. Na hakika ahadi yako ni haki. Nawe ni Mwenye haki kuliko mahakimu (wote).

Akasema (Mwenyezi Mungu), “Ewe Nuhu! Huyu si miongoni mwa watu wako. Yeye ni (mwenye) mwendo usiokuwa mzuri. Basi usiniombe ambayo huyajui . mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga.”

Hud-45-46

Mwenyezi Mungu alimkatalia na kumuambia kuwa huyo si mwanawe, wala si katika watu wa nyumba yake kwa sababu ya kuukanusha ujumbe aliokuja nao Nabi Nuh (Alayhissalaam).

 

Shia hawakubali kuwaingiza wengine isipokuwa wale tu waliotajwa katika hadithi ya shuka pamoja na maimamu kumi na mbili waliofuata wa madhehebu ya Ithnaasheri kwa sababu wanaamini kuwa hao ndio viongozi wa Waislamu waliotakaswa wasiotenda makosa watakaowaongoza Waislamu baada ya kufa kwa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mpaka Siku ya Kiama.

 

Mapenzi yetu kwa Ahlul Bayt

1-     Watu wa Ukoo

Ahlus Sunnah wanawapenda na kuwaheshimu watu wa ukoo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na wamewaweka katika daraja ya juu wanayoistahiki.

Hawa ni binti zake wote, pamoja na Bibi Fatima Al Zahraa na wanawe Al Hassan na Al Hussayn na watu wa ukoo wake tuliotangulia kuwataja kuwa ni katika Ahlul Bayt wakiwemo Aly bin Abi Talib na watu wa nyumba yake, na Al Abbas bin Abdulmuttalib na watu wa nyumba yake, na Aqiyl bin Abi Talib na watu wa nyumba yake na Jaafar bin Abi Talib na watu wa nyumba yake (Radhiya Llahu anhum).

Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwasafisha barabara watu hawa na akatuamrisha katika kitabu chake kitukufu kuwapenda, na pia Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ametuamrisha tuwapende.

Katika Sahih Muslim imeelezwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipowahutubia watu mahali panapoitwa Ghadiyr aliwaambia:

          { æÃåá ÈíÊí¡ ÃÐßÑßã Çááå Ýí Ãåá ÈíÊí¡ ÃÐßÑßã Çááå Ýí Ãåá ÈíÊí }.

«Na watu wa nyumba yangu. Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.»

Muslim

 

Mwenyezi Mungu anasema:

((Åöäøó Çááøóåó æóãóáÇÆößóÊóåõ íõÕóáøõæäó Úóáóì ÇáäøóÈöíøö íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ÕóáøõæÇ Úóáóíúåö æóÓóáøöãõæÇ ÊóÓúáöíãðÇ))

«Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu»

Al Ah’zaab -56

Ilipoteremshwa aya hii Masahaba (Radhya Llahu anhum) walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam):

«Vipi tukuswalie?»

Akawaambia:

«Semeni:

{Çááåã Õá Úáì ãÍãÏ æÚáì Âá ãÍãÏ¡ ßãÇ ÕáíÊ Úáì ÅÈÑÇåíã æÚáì Âá ÅÈÑÇåíã Åäß ÍãíÏ ãÌíÏ¡ æÈÇÑß Úáì ãÍãÏ æÚáì ãÍãÏ¡ ßãÇ ÈÇÑßÊ Úáì ÅÈÑÇåíã æÚáì Âá ÅÈÑÇåíã Åäß ÍãíÏ ãÌíÏ}.

Mola wangu Mswalie Muhammad na Aali ya Muhammad, kama ulivyomswalia Ibrahim na aali ya Ibrahim hakika Wewe ni Msifiwa na Mwenye kutukuzwa. Na umbariki Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali ya Ibrahim hakika Wewe ni Msifiwa na Mwenyeye kutukuzwa.”

Anasema Ibnul Qayyim katika kuisherehesha hadithi hii:

Kuwaswalia Aali zake ni katika kukamilisha kumswalia Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kwa sababu kufanya hivyo ni katika kumfurahisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na Mwenyezi Mungu anamuongezea daraja na heshima (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

 

Imepokelewa kuwa Abubakar Al Siddiq (Radhiya Llahu anhu) alisema:

[[ÇÑÞ龂 ãÍãÏÇð Ýí Âá ÈíÊå]].

“Mpeni heshima  Muhammad kwa (kuwaheshimu) watu wa nyumba yake.”

Na alisema pia:

[[æÇááå áÃä ÃóÕöáó ÞÑÇÈÉ ÑÓæá Çááå Õáì Çááå Úáíå æÓáã ÃÍÈ Åáí ãä ÃÕá ÞÑÇÈÊí]]

“Wallahi, kuwasiliana na jamaa zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni bora kwangu kuliko kuwasiliana na jamaa zangu.”

Bukhari

Na ile hadithi isemayo: « Fatima ni Bibi wa wanawake wa Peponi.»

Imepokelewa kutoka kwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha).

 

Imepokelewa pia kuwa siku ile Abu Sufyan alipokuja kusilimu mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), Umar bin Khataab (Radhiya Llahu anhu) alimuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam):

«Huyu hapa Abu Sufyan amekuja mwenyewe kwa miguu yake, niruhusu nimkate kichwa chake».

Al Abbas (Radhiya Llahu anhu) ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema:

«Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi namuingiza Abu Sufiyan katika himaya yangu.»

Al Abbas akakaa karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na alipomuona Umar (Radhiya Llahu anhu) anashikilia kutaka kumkata kichwa Abu Sufyan, Al Abbas akamuambia:

«Taratibu ewe Umar angelikuwa huyu ni katika watu wa kabila lako la Bani Uday bin Kaab usingelishikilia namna hii, lakini kwa vile huyu ni mtu (wa kabila langu) anayetokana na ukoo wa Abdu Manaf.»

Umar akasema kumuambia Al Abbas (Radhiya Llahu anhum):

«Taratibu ewe Abbas, kwani Wallahi naapa kuwa siku uliyosilimu wewe ilikuwa bora kwangu kuliko angelisimu baba yangu Al Khattab, kwa sababu naelewa kuwa kusilimu kwako kulimfurahisha sana Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).»

Attabarani, Al Bidaya wal Nihayah- Ibni Kathiyr na Siyrat Ibn Hisham

 

Hadithi hizi na nyingi nyingine zinatufundisha namna gani watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) walivyokuwa wakiwapenda Masahaba, na pia Masahaba walivyokuwa wakiwapenda watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na zinatufundisha pia namna gani Ahlu Sunnah walivyojishughulisha kuzitafuta na kuziandika hadithi zinazowahusu watu wa \nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

 

Masahaba na pia ‘Tabi’iyna’ (waliokuja baada yao) walijishughulisha sana kutafuta na kuziandika fadhila za watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ili watakaokuja baada yao wazijuwe na kuzichunga na kuzifuata. Na hii ndiyo sababu utakaposoma kitabu chochote katika vitabu vya Ahli Ssunnah hukosi kuona ndani yake mlango maalum uliohusishwa kwa ajili ya sifa za Ahlul Bayt. Utayakuta haya katika vitabu vya Hadiyth na vitabu vya Aqida na hata katika vitabu vya Tariykh ‘historia’.

Imam Bukhari kwa mfano, amehusisha mlango maalum juu ya fadhila za Imam Aly (Radhiya Llahu anhu), na amehusisha mlango wa fadhila za Bibi Fatima (Radhiya Llahu anha) nk.

Imam Muslim katika mlango wa Fadhila za Masahaba ameandika juu ya fadhila za Maimam Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum).

Imam Attirmidhy na Ibni Maajah na Imam Ahmad bin Hanbal na Ibni Kathiyr na Attabariy na Ibni Taymiyah na Adh’dhahabiy na wengine, wote hawa katika vitabu vyao wameandika kwa mapana na marefu juu ya fadhila za Maimam hawa wawili ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amewaita ‘Mabwana wa vijana wa Peponi.’

Hizi zote ni dalili wazi juu ya heshima tunayowapa watu wa nyumba hii tukufu (Radhiya Llahu anhum).

Elimu ya Ghaibu na Kukingwa

Anasema Ayidh Al Qar’niy katika kitabu ‘Mawaddat Ahlil Bayt inda Ahlis Sunnah:

«Sisi tunawaheshimu na tunawaenzi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), lakini hatuamini kama wanavyoamini Shia kuwa wao wanajua elimu ya Ghaibu na wamekingwa hawafanyi makosa nk. Tunaamini kuwa mwenye kujuwa ghaibu ni Mwenyezi Mungu peke yake.

Mwenyezi Mungu anasema:

Þá áÇ íÚáã ãä Ýí ÇáÓãæÇÊ æÇáÃÑÖ ÇáÛíÈ ÅáÇ Çááå" [Çáäãá: 65]

Sema: “Hakuna aliyeko katika mbingu na ardhi ajuaye Ghayb (yasiyotokea) ila Mwenyezi Mungu."

An Naml-65

Na akasema:

Þá áÇ Ããáß áäÝÓí äÝÚÇ æáÇ ÖÑÇ ÅáÇ ãÇ ÔÇÁ Çááå æáæ ßäÊ ÃÚáã ÇáÛíÈ áÇÓÊßËÑÊ ãä ÇáÎíÑ æãÇ ãÓäí ÇáÓæÁ Åä ÃäÇ ÅáÇ äÐíÑ æÈÔíÑ áÞæã íÄãäæä

Sema: “Sina mamlaka ya kujipa nafuu wala ya kujindolea madhara ila apendavyo Mwenyezi Mungu; na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia mema mengi; wala isingalinigusa dhara. Mimi si chochote ila ni muonyaji na mtoaji wa habari njema kwa watu wanaoamini.”

Al Aaraf-188

 

«Na tunaamini kuwa aliyekingwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) peke yake.

Mwenyezi Mungu anasema:

æóÇááøåõ íóÚúÕöãõßó ãöäó ÇáäøóÇÓö

“Na Mwenyezi Mungu amekukinga“

Al Maidah-67

Sisi tunaamini kuwa hapana yeyote aliyekingwa (Maaswum ãÚÕæã), si katika watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wala katika Masahaba wake, kwa sababu zifuatazo:-

1.      Hapana nassi iliyo wazi isiyopingika inayoeleza juu ya kukingwa kwao. Lau kama ingekuwepo basi tungelifuata bila matatizo wala kipingamizi.

2.      Hapana hata mmoja katika watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyedai kuwa yeye amekingwa, akawataka watu waamini hivyo, isipokuwa katika vitabu ambavyo maulamaa wote kama vile Ibni Kathiyr na Ibni Hajar na Adhahaby na wengineo wamesema kuwa hadithi hizo si dhaifu tu, bali maudhui. (zimepachikwa).

3.      Hapana hata mwanachuoni mmoja katika maulamaa wetu aliyesema hivyo, juu ya kukhitalifiana kwao katika mambo mengi, lakini juu ya jambo hili hapana hitilafu baina yao.

4.      Lau kama wangelikuwa wamekingwa, basi wasingelikubali kukosolewa na mtu yeyote katika Ijtihadi zao. Kwa mfano kama Aly (Radhiya Llahu anhu) angelikuwa amekingwa, basi asingelikubali kukosolewa na Abubakar au Umar au Uthman (Radhiya Llahu anhum), na anapokosolewa angelisema kwa mfano; ‘Vipi mnanikosoa wakati mimi nimekingwa?’

Lakini Aly alikuwa akiwakosoa na wao walikuwa wakimkosoa, akiwaheshimu na wao wakimuheshimu, akiwapenda na wao wakimpenda.

5.      Maulamaa wanasema kuwa ÇáÊØåíÑ  ‘kusafishwa’ kama ilivyokuja katika aya, maana yake si kukingwa, bali ni kusafishwa na kutakaswa. Na  si kila aliyetakaswa amekingwa akawa hafanyi makosa, ama sivyo basi kila aliyesifiwa kuwa ametakaswa au amesafishwa atakuwa amekingwa. Kama ilivyokuja katika hadithi:

æÇÌÚáäí ãä ÇáÊæÇÈíä æÇÌÚáäí ãä ÇáãÊØåÑíä

Na unijaalie niwe miongoni mwa waliotubu na unijaalie niwe miongoni mwa wenye kujitakasa.

Na  Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutubu na anawapenda wenye kujitakasa, lakini haimaanishi kuwa hao wamekingwa hawafanyi makosa.

6.      Kama Muislamu atachukua elimu yake kutoka katika Qurani na Mafundisho ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) peke yake bila ya kuchukua kutoka kwa watu wa Ahlul Bayt, huyo Uislamu wake unakuwa sahihi na hauna dosari yoyote. Wangelikuwa Ahlul Bayt wamekingwa ‘Maasumiyn’, basi ingelimuwajikia kila Muislamu kuchukua elimu kutoka kwao.

7.      Kwetu Ahlus Sunnah, Abubakar na Umar ni viumbe bora kupita wote  baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Na Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mara zote alikuwa akiwatanguliza mbele ya Aly. Alikuwa akimuacha Abubakar aswalishe na Aly akiswali nyuma yake, na hapana hata mmoja katika Ahlis Sunnah aliyewahi kusema kuwa Abubakar amekingwa (Maaswum ãÚÕæã). Itakuwaje basi awe mwengine asiyekuwa yeye?

8.      Imepokelewa kuwa Aly (Radhiya Llahu anhu) aliwasifia waliojitenga katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, na alijuta kwa yaliyotokea katika vita vya ngamia na vita vya Swiffiyn. Angelikuwa amekingwa asingetenda matendo kisha akajuta.

9.      Imepokelewa kuwa Aly (Radhiya Llahu anhu) alipanda juu ya membari katika mji wa Al Kufa akasema:

«Namshitakia Allah dhiki zangu na matatizo yangu.»  Kisha akasema:

«Wana daraja zao kwa Mwenyezi Mungu Muhammad bin Maslamah na Usama bin Zeyd na Saada bin Abi Waqaas. Kama ni shari basi ndogo, na kama ni kheri basi ni nyingi (kwa kujitenga kwao na fitna).»

Naye ni mkweli (Radhiya Llahu anhu), lakini angelikuwa Maasuwm basi asingetamka haya. Asingewasifia waliojitenga na  fitna ile wakati yeye mwenyewe alikuwemo ndani yake.

 

10. Siku ya Saqiyfah, siku ile baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kufariki dunia, wakati Waislamu walipojumuika na kumchagua Abubakar kuwa Khalifa wao, hapana hata mmoja aliyejitokeza akasema : «Jamani tunaye aliyekingwa hapa, kwa hivyo yeye ndiye anayestahiki kuchaguliwa.» Hilo halijatokea, na siku ile walikuwepo waliopigana vita vya Badar na pia walikuwepo wale ambao Mwenyezi Mungu alitangaza kuridhika nao chini ya mti. Inaingia akilini kweli kuwa watu wote hao waliosifiwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Qurani tukufu, na wakasifiwa na Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wafanye njama dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wasallam)?

(Mwisho wa maneno ya Ayidh Al Qar’niy)

Mawaddat Ahlil Bayt inda Ahlis Sunnah Uk.317-322

 

Fadhila za Ahlul Bayt

Tunaweza kugawa fadhila za Ahlul Bayt katika mafungu mawili:-

1.      Fadhila za ujumla

2.      Fadhila makhsusi

 

Kwanza Fadhila za ujumla

Fadhila za ujumla mfano wa hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliposema:

          { æÃåá ÈíÊí¡ ÃÐßÑßã Çááå Ýí Ãåá ÈíÊí¡ ÃÐßÑßã Çááå Ýí Ãåá ÈíÊí }.

«Na watu wa nyumba yangu. Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.»

Muslim

Na fadhila zilizotajwa katika Surat al Ahzab:

ÅöäøóãóÇ íõÑöíÏõ Çááøóåõ áöíõÐúåöÈó Úóäßõãõ ÇáÑøöÌúÓó Ãóåúáó ÇáúÈóíúÊö æóíõØóåøöÑóßõãú ÊóØúåöíÑÇð

"Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba (ya Mtume), na kukusafisheni baarabara."

 

Ndani yake fadhila hizi wanaingia wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kwa sababu wao ndio waliokusudiwa, na pia wanaingia Sayiduna Aly na Bibi Fatima na Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum) kupitia hadithi ya Al Kisaa.

Fadhila za ujumla zinapatikana pia katika kutoa shahada ndani ya Swala wakati wa kusoma Tahiyatu, tunaposema:

Çááåã Õá Úáì ãÍãÏ æÚáì Âá ãÍãÏ

"Mola wangu mswalie Muhammad na Aali yake Muhammad”

Na yote haya yanatokana na fadhila zao na daraja yao mbele ya Mwenyezi Mungu.

 

Fadhila Makhsusi

Wafuatao ni baadhi ya watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na hawa ni maimamu kumi na mbili wa Shia:-

1.      Aly bin Abu Talib

2.      Al Hassan

3.      Al Hussayn

4.      Aly bin Al Hussayn (Zeinul Abedeen)

5.      Muhammad bin Aly bin Al Hussayn (Al Baqer)

6.      Jaafar Al Sadeq

7.      Musa Al Kadhim

8.      Aly Ridha

9.      Muhammad Al Jawaad

10. Aly Al Haadi

11. Al Hassan Al Askary

12. Muhammad (Imam wa kumi na mbili wanayemsubiri)

 

Hawa tunaweza kuwagawa makundi manne.

1-     Kundi la mwanzo ni Masahaba (waliomuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)), nao ni Aly na Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum).

2-     Kundi la pili ni maulamaa wacha Mungu miongoni mwa maulamaa wa Ahlis Sunnah wal Jama’a nao ni:

 1-Aly bin al Hussayn

2-Muhammad Al Baqer

3-Jaafar al Sadeq

4-Musa Al Kadhem

5-Ali Ridha

6-Muhammad Al Jawaad

3-     Kundi la tatu; hawa ni wacha Mungu lakini si katika maulamaa na inawatosha fahari ya kuwa wanatoka katika nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na wanayo haki ya kwenda penye kaburi la Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na kusema:

‘Assalaam alayka ewe baba yangu.’

Na hawa ni: Aly Al Haadi na Al Hassan Al Askary.

4-     Sehemu ya nne ni mtu asiyezaliwa wanayemsubiri, naye ni Muhammad bin Al Hassan.

 

Aly bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu)

Wa mwanzo wao ni Aly bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu) ambaye ni mtoto wa ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na mume wa Bibi wa mabibi wa Peponi Fatima (Radhiya Llahu anha) binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Na Aly (Radhiya Llahu anhu) ni Khalifa wa nne muongofu, na ni katika wale kumi waliobashiriwa kuingia Peponi.

Ndani ya Bukhari na Muslim ipo hadithi kutoka kwa Abul Abbas Sahal bin Saad Al Saidiy (Radhiya Llahu anhu), aliyesema kuwa siku ya vita vya Khaibar, Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alisema:

(áÃÚØíä åÐå ÇáÑÇíÉ ÛÏÇ ÑÌáÇ íÝÊÍ Çááå Úáì íÏíå¡ íÍÈ Çááå æÑÓæáå æíÍÈå Çááå æÑÓæáå)

"Nitampa bendera hii kesho, mtu ambaye atatupa ushindi Mwenyezi Mungu kwa mikono yake. (Mtu huyo) Anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

Anaendelea kusema Sahal (Radhiya Llahu anhu):

"Usiku kucha watu walikuwa wakiwaza wakitaka kujua ni nani huyo mwenye kupendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake atakayepewa bendera hiyo. Asubuhi yake watu wote wakaamkia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), kila mmoja akitamani apewe yeye bendera siku hiyo".

Baada ya watu kujikusanya mbele yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akauliza:

"Yuwapi Aly bin Abi Talib?...."

Bukhari na Muslim

Na akasema pia (Swallah Llahu alayhi wa sallam) juu ya Aly (Radhiya Llahu anhu):

áÇ íÍÈß ÅáÇ ãÄãä¡ æáÇ íÈÛÖß ÅáÇ ãäÇÝÞ

«Hakupendi isipokuwa muumini na hakuchukii isipokuwa mnafiki »

Na sisi Wallahi tunampenda na kumuenzi na kumheshimu yeye na mkewe na watoto wake wote (Radhiya Llahu anhum). Hadithi zake zimejaa ndani ya vitabu vyetu. Hekima yake tunaitumia na tunawafunza watoto wetu. Mashairi yake yaliyojaa mafunzo ya kheri na busara tunayasoma na kuyarudia na tunamfunza kila mmoja wetu.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema pia:

{ÃãÇ ÊÑÖì Ãä Êßæä ãäí ÈãäÒáÉ åÇÑæä ãä ãæÓì} æÒÇÏ ãÓáã: { ÅáÇ Ãäå áÇ äÈí ÈÚÏí}

Bukhari

 «Hutoridhika ukiwa wewe kwangu upo katika daraja ya Harun kwa Musa» na Muslim akaongeza: «Isipokuwa hapana Mtume baada yangu».

 

Hadithi zote hizi na nyingi nyingine zimo ndani ya vitabu vya Ahlis Sunnah zikituhakikishia kuwa hatuna uzito wowote kwetu katika kuzitaja au kuziandika ndani ya vitabu vyetu na hata kuzisema hadharani, bali ni fahari kwetu kufanya hivyo, kwa sababu hawa ni watu wa nyumba ya Mtume wetu Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

 

Fatima (Radhiya Llahu anha)

Bibi Fatima (Radhiya Llahu anha) binti yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Kipenzi chake (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Manukato yake mazuri aliyesema juu yake :

{Åä ÝÇØãÉ ÈÖÚÉ ãäí íÄÐíäí ãÇ ÂÐÇåÇ}

«Hakika Fatima ni sehemu inayotokana na mimi kinaniudhi kinachomuudhi»

Muslim

Na akasema kumuambia Fatima:

{ÃãÇ ÊÑÖí Ãä Êßæäí ÓíÏÉ äÓÇÁ ÇáãÄãäíä¡ Ãæ ÓíÏÉ äÓÇÁ åÐå ÇáÃãÉ}

«Huridhiki ukiwa wewe ni Bibi wa wanawake waumini, au Bibi wa wanawake wa umma huu»

Na katika Bukhari :

ÝÇØãÉ ÓíÏÉ äÓÇÁ Ãåá ÇáÌäÉ

« Fatima ni Bibi wa wanawake wa Peponi»

 

Al Hassan na Al Hussayn

Tunawaheshimu na kuwapenda pia Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum), na ndani ya vitabu vya Ahlus Sunnah utakuta maelezo mengi juu ya wajukuu hawa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyokuwa akitamka mbele ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum). Alikuwa akisema:

Çááåã Åäí ÃÍÈåãÇ ÝÃÍÈåãÇ

‘Mola wangu kwa hakika mimi ninawapenda na Wewe wapende’

Attirmidhiy

Na akasema:

ÇáÍÓä æÇáÍÓíä ÓíÏÇ ÔÈÇÈ Ãåá ÇáÌäÉ

‘Al Hassan na Al Hussayn ni mabwana wa vijana wa Peponi’

Attirmidhy na Ahmad na Al Hakim na wengine

 

Al Abbas bin Abdul Muttalib (Radhiya Llahu anhu)

Huyu ni ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah llahu alayhi wa sallam) aliyesema juu yake:

Úã ÇáÑÌá Õäæ ÃÈíå

‘Ami yake mtu ni sawa na baba yake

Attirmidhy

 

Abdillahi bin Abbas (Radhiya Llahu anhuma)

Huyu ni mtoto wa ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyemuombea dua nzuri aliposema:

{Çááåã Úáãå ÇáÊÃæíá æÝÞåå Ýí ÇáÏíä}

“Mola wangu mpe elimu ya kujuwa uhakika wa mambo na mjaalie awe na fiq-hi katika dini."

Ahmad

 

Ali Zeiynul Aabidiyn (Radhiyal Llahu anhu)

Huyu ni Aly bin Al Hussayn bin Aly bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhum) ambaye amesema Imam Al Zuhry juu yake:

‘Sijapata kumuona mtu kutoka kabila la Quraysh aliye bora kupita yeye.’

Na alisema Said bin Musayib:

‘Sijapata kumuona mcha Mungu kupita huyu.’

 

Muhammad bin Aly bin Al Hussayn ‘Al Baaqer’ (Radhiyal Llahu anhu)

Amesema juu yake Abu Naeem:

‘Alikuwa mtu wa kuaminika, mwingi wa elimu na hadithi.’

 

Jaafar bin Muhammad (Radhiyal Llahu anhu)

Huyu ndiye Jaafar As Sadeq bin Muhammad Al Baqer ambaye Imam Abu Hanifa alisema juu yake :

‘Sijapata kuona mtu mwenye elimu ya fiq’hi kupita Jaafar bin Muhammad.’

Amesema pia juu yake Ibni Hibban :

‘Mwenye kuaminika asiye na mfano.’

Amesema Imam Adhahaby :

« Imam As Sadeq ni Shekhe katika Mashekhe wa Kikureshi anayetokana na ukoo wa Bani Hashim na ni miongoni mwa maulamaa wao.»

 

Musa bin Jaafar ‘Al Kadhim’ (Radhiyal Llahu anhu)

Huyu ni mtoto wa Jaafar As Sadeq (Radhiya Llahu anhu)

Amesema juu yake Ibni Tayimiyah:

« Mashuhuri kwa kufanya ibada na kuhiji.»

Akasema Abu Hatim Al Razi:

« Ni mwenye kutegemewa msemakweli, Imam katika maimamu wa Kiislamu.»

Amesema juu yake Ibni Kathiyr:

« Alikuwa mwingi wa kufanya ibada na mwenye kuheshimika.»

Anasema Adhahaby katika ‘Siyar’ kuwa siku moja Harun Al Rashiyd alipokuwa katika Hija alikwenda mbele ya kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na alikuwa pamoja naye katika safari hiyo Musa bin Jaafar Al Kadhim (Radhiya Llahu anhu). Harun Al Rashiyd alipofika penye kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema kwa ufahari mbele ya watu: “Assalaam alayka ewe mtoto wa ami yangu.” Harun Al Rashiyd anatokana na ukoo wa Al Abbas bin Abdul Muttalib (Radhiya Llahu anhu). Musa bin Jaafar naye akasogea mbele ya kaburi hilo kisha akasema: “Assalaam alayka ewe baba yangu.”

Uso wa Harun Al Rashiyd ulibadilika. Akamtizama kisha akamuambia: “Hili Wallahi ni la kujionea fahari.”

 

Aly bin Musa ‘Al Ridha’

Amesema juu yake Ibni Hibban:

« Huyu ni miongoni mwa mabwana wa Ahlul Bayt na katika wenye hekima.»

Na Adhahaby amesema juu yake :

« Alikuwa mwenye shani kubwa mwenye kustahiki ukhalifa.»

 

Muhammad bin Aly bin Musa ‘Al Jawaad’

Amesema juu yake Ibni Taymiyah:

«Alikuwa miongoni mwa watu wema na mkarimu sana, na kwa ajili hii alipewa jina la Al Jawaad. Na alikuwa mwenye kuheshimika sana.»

 

Yote haya yanabatilisha zile kauli kuwa Masunni hawawapendi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Alipotuhumiwa Abdullah mwana wa Imam Muhammad bin Abdul Wahaab kwamba alisema kuwa watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hawana haki yoyote” akajibu:

“Subhana Llah huu ni uongo mkubwa. Waliotuzulia haya au kutunasibisha nayo wamesema uongo mtupu juu yetu.”

 

Na hivi ndivyo ilivyo kwa wote wanaotokana na ukoo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na pia wajukuu wote wa Sayiduna Aly (Radhiya Llahu anhu), wote tunawapenda bila kuwafarikisha na wote wamepewa sifa wanazozistahiki ndani ya vitabu vya Sunni ikiwa ni dalili wazi kuwa watu hawa tunawaenzi na kuwaheshimu.

 

Shia juu ya kudai kwao kuwa wanawapenda na kufuata mwenenendo wa watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), lakini ukweli ni kuwa wao wanawafarikisha na kuwatenga wengine. Kwa sababu watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kwao ni Aly na Fatima na Al Hassan na Al Hussayn na watoto wao na wajukuu zao peke yao, na wengine wasiokuwa hao wamewatoa katika sifa hii.

Aly (Radhiya Llahu anhu) alioa wake wengine akazaa nao watoto wengi, lakini Mashia hawahesabu watoto hao kuwa  ni Ahlul Bayt.

Watoto wengine wa Aly (Radhiya Llahu anhu) kama vile Muhammad bin Al Hanafiyah, Abubakar bin Aly, Umar bin Aly na Uthman bin Aly na Abbas, wote hawa ni watoto wa Sayiduna Aly (Radhiya Llahu anhu).

Wamewatoa pia mabinti wengine wa Aly kama walivyowatoa mabinti wengine wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), nao ni Zeinab na Ruqayah na Ummu Kulthum, kama walivyowatoa wake wa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hapo mwanzo.

 

2-     Wake zake

Sisi tunaamini kuwa wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni katika watu wa nyumba yake, na kwamba wao ni mama zetu.

Mwenyezi Mungu anasema:

(( ÇáäøóÈöíøõ Ãóæúáóì ÈöÇáúãõÄúãöäöíäó ãöäú ÃóäúÝõÓöåöãú æóÃóÒúæóÇÌõåõ ÃõãøóåóÇÊõåõãú ))[ÇáÃÍÒÇÈ:6]

«Nabii ana haki zaidi kwa Waislamu kuliko nafsi zao.na wakeze ni mama zao.»

Al Ahzab -6

Na akaharamisha kuwaoa baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Mwenyezi Mungu anasema:

(( æóãóÇ ßóÇäó áóßõãú Ãóäú ÊõÄúÐõæÇ ÑóÓõæáó Çááøóåö æóáÇ Ãóäú ÊóäúßöÍõæÇ ÃóÒúæóÇÌóåõ ãöäú ÈóÚúÏöåö ÃóÈóÏðÇ))

«Wala haikupasieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.»

Al Ahzab-53

Tunawapa heshima kubwa mama zetu hawa, na wa mwanzo wao ni Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha. Wa mwanzo kuamini, aliyemsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kwa hali na mali huku akimpa moyo na kumliwaza kila anapopatwa na masaibu au shida. Bibi Khadija ndiye aliyeambiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam):

"Åä Çááøå ÃãÑäí Ãä ÃÈÔÑ ÎÏíÌÉ ÈÈíÊ Ýí ÇáÌäÉ áÇ ÕÎÈ Ýíå æáÇ äÕÈ"

“Mwenyezi Mungu ameniamrisha nimpe bishara njema Khadija juu ya nyumba yake Peponi ya Lulu, hamna zogo ndani yake wala tabu (yoyote).”

Bukhari na Muslim

Na kutoka kwa Aly bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema:

ÎíÑ äÓÇÆåÇ ãÑíã ÈäÊ ÚãÑÇä¡ æÎíÑ äÓÇÆåÇ ÎÏíÌÉ ÈäÊ ÎæíáÏ

«Mwanamke bora (katika zama zake) ni Maryam binti Imran, na mwanamke bora (katika zama zake) ni Khadija binti Khuwaylid»

Bukhari na Muslim

Kisha anafuatia Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha), binti wa Abubakar Al Siddique (Radhiya Llahu anhu), Bibi aliyetakaswa kutoka mbingu ya saba baada ya mnafiki yule aliyejitwika sehemu yake kubwa katika uzushi wake ambaye ni Abdullahi bin Ubay bin Saluul kueneza uvumi mbaya juu ya mama huyu wa Waislamu kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Maulamaa wote wamekubaliana kuwa kumsingizia uwongo bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) katika kile kisa cha uwongo alichozuliwa (hadithi ya "Al-Ifki") wakati MwenyeziMungu kishamtakasa, basi anakuwa si Muislamu tena.

MwenyeziMungu anasema:-

Åöäøó ÇáøóÐöíäó ÌóÇÄõæÇ ÈöÇáúÅöÝúßö ÚõÕúÈóÉñ ãøöäßõãú áóÇ ÊóÍúÓóÈõæåõ ÔóÑøÇð áøóßõã Èóáú åõæó ÎóíúÑñ áøóßõãú áößõáøö ÇãúÑöÆò ãøöäúåõã ãøóÇ ÇßúÊóÓóÈó ãöäó ÇáúÅöËúãö æóÇáøóÐöí Êóæóáøóì ßöÈúÑóåõ ãöäúåõãú áóåõ ÚóÐóÇÈñ ÚóÙöíãñ {11} áóæúáóÇ ÅöÐú ÓóãöÚúÊõãõæåõ Ùóäøó ÇáúãõÄúãöäõæäó æóÇáúãõÄúãöäóÇÊõ ÈöÃóäÝõÓöåöãú ÎóíúÑÇð æóÞóÇáõæÇ åóÐóÇ ÅöÝúßñ ãøõÈöíäñ {12} áóæúáóÇ

ÌóÇÄõæÇ Úóáóíúåö ÈöÃóÑúÈóÚóÉö ÔõåóÏóÇÁ ÝóÅöÐú áóãú íóÃúÊõæÇ ÈöÇáÔøõåóÏóÇÁ ÝóÃõæúáóÆößó ÚöäÏó Çááøóåö åõãõ ÇáúßóÇÐöÈõæäó {13} æóáóæúáóÇ ÝóÖúáõ Çááøóåö Úóáóíúßõãú æóÑóÍúãóÊõåõ Ýöí ÇáÏøõäúíóÇ æóÇáúÂÎöÑóÉö áóãóÓøóßõãú Ýöí ãóÇ ÃóÝóÖúÊõãú Ýöíåö ÚóÐóÇÈñ ÚóÙöíãñ {14} ÅöÐú ÊóáóÞøóæúäóåõ ÈöÃóáúÓöäóÊößõãú æóÊóÞõæáõæäó ÈöÃóÝúæóÇåößõã ãøóÇ áóíúÓó áóßõã Èöåö Úöáúãñ æóÊóÍúÓóÈõæäóåõ åóíøöäÇð æóåõæó ÚöäÏó Çááøóåö ÚóÙöíãñ {15} æóáóæúáóÇ ÅöÐú ÓóãöÚúÊõãõæåõ ÞõáúÊõã ãøóÇ íóßõæäõ áóäóÇ Ãóä äøóÊóßóáøóãó ÈöåóÐóÇ ÓõÈúÍóÇäóßó åóÐóÇ ÈõåúÊóÇäñ ÚóÙöíãñ {16} íóÚöÙõßõãõ Çááøóåõ Ãóä ÊóÚõæÏõæÇ áöãöËúáöåö ÃóÈóÏÇð Åöä ßõäÊõã ãøõÄúãöäöíäó {17}  æóíõÈóíøöäõ Çááøóåõ áóßõãõ ÇáúÂíóÇÊö æóÇááøóåõ Úóáöíãñ Íóßöíãñ {18} Åöäøó ÇáøóÐöíäó íõÍöÈøõæäó Ãóä ÊóÔöíÚó ÇáúÝóÇÍöÔóÉõ Ýöí ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ áóåõãú ÚóÐóÇÈñ Ãóáöíãñ Ýöí ÇáÏøõäúíóÇ æóÇáúÂÎöÑóÉö æóÇááøóåõ íóÚúáóãõ æóÃóäÊõãú áóÇ ÊóÚúáóãõæäó {19} æóáóæúáóÇ ÝóÖúáõ Çááøóåö Úóáóíúßõãú æóÑóÍúãóÊõåõ æóÃóäøó Çááøóå ÑóÄõæÝñ ÑóÍöíãñ {20}þ

"Hakika wale walioleta uwongo huo (wa kumsingizia bibi AishaRadhiya Llahu anha) mkewe Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa amezini)) Ni kundi miongoni mwenu (ni jamaa zenu) msifikiri ni shari kwenu bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aloyachuma katika madhambi yao na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kubwa (zaidi).

Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?

Kwa nini hawakuleta mashahidi wane? Na ilivyo kuwa hawakuleta mashahidi wane basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na

Akhera, bila ya shaka ingeli kupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyo jiingiza. Mlipoupokea (uwongo huo mkawa mnautangaza) kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

Na kwa nini mlipo yasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhaanaka (Mola wetu) Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa!?

Mwenyezi Mungu anakuonyeni msirudi kabisa (msirejee tena) kufanya kama haya, ikiwa nyinyi ni Waumini! (Waislamu) kweli.”

An Nur– 11-17

 

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala katika aya hizi ametumia neno; ‘Subhaanaka katika kumtakasa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kutokana na uwongo aliozuliwa, na neno hili ‘Subhanaka’ Mwenyezi Mungu analitumia katika kukanusha uongo mkubwa tu, Anaponasibishwa na mwana au mshirika.

Mwenyezi Mungu amesema:

ÓõÈúÍóÇäóßó åóÐóÇ ÈõåúÊóÇäñ ÚóÙöíãñ

(Mola wetu) Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa!?’

 

Anasema Az Zamakhshary:

“Alipokanusha kuwa hana mwana wala mshirka alisema:

æóÞóÇáõæÇú ÇÊøóÎóÐó Çááøåõ æóáóÏÇð ÓõÈúÍóÇäóåõ Èóá áøóåõ ãóÇ Ýöí ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö ßõáøñ áøóåõ ÞóÇäöÊõæäó

“Na wanasema:”Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto” ‘Subhaanahu’ Ameepukana na hilo bali ni vyake hivyo vilivyomo mbinguni na ardhini . Vyote vinamtii Yeye.”

Al Baqarah-116

Na akasema:

ãóÇ ßóÇäó áöáøóåö Ãóä íóÊøóÎöÐó ãöä æóáóÏò ÓõÈúÍóÇäóåõ

 “Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kufanya mtoto; ‘Subhanahu’ Ametakasika.”

Maryam-35

 

Amelitumia neno ‘Subhanahu’ kwa ajili ya kujitakasa na kukanusha kuwa anaye mwana, na amelitumia neno hilo hilo ‘Subhanahu’ katika kuukanusha uwongo aliozuliwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha).

 

Miongoni mwa wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) pia ni Ummu Salamah (Radhiya Llahu anha), mama yetu mtulivu wa tabia, mwenye akili yenye uwezo wa kupima mambo, mwingi wa hekima ambaye Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mara nyingi alikuwa akichukuwa ushauri wake katika baadhi ya mambo. Alimshauri siku ile ya Sulhu ya Hudaibiya na akapata ushauri mwema kutoka kwake.

Hawa na wake zake wengine wote ni mama zetu. Ni watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kama ilivyokuja katika aya za Surat al Ahzab, na kama tulivyoona katika dalili mbali mbali kutoka katika Qurani tukufu na katika Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Inatuwajibikia kuwapenda na kuwaenzi na kuwaheshimu mama zetu hawa.

 

Baada ya kumalizika vita vya Ngamia (Waqaat al Jamal), Aly (Radhiya Llahu anhu) aliamua kumuacha huru Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha). Wafuasi wake wakamuuliza:

«Inakuwaje halali kumwaga damu zao na haiwi halali kwetu mali zao na mateka wao?»

Aly (Radhiya Llahu anhu) akasema:

«Yupi kati yenu atakayefurahi Mama wa Waislamu awe mateka wake?»

Wote wakanyamaza.

 

Ikiwa ni haramu kumsema vibaya Muislamu yeyote, basi inakuwa vibaya zaidi kuwasema vibaya watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wakiwemo wake zake na watu wa ukoo wake pamoja na wajukuu wake na wajukuu wa wajukuu wakiwemo Al Hassan na Al Hussayn na Abdullah bin Al Hassan na Aly bin Al Hassan na Muhammad bin Alyn a Jaafar bin Muhammad na Musa bin Jaafar na Aly bin Musa Al Ridha na waliobaki, na pia Sahaba zake (Radhiya Llahu anhum) wote kwa pamoja wa Makkah na wa Madina, na wale ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amewabashiria Pepo, na pia viongozi wetu wa dini.

 

Haiwezekani ukapatikana umoja wa Waislamu ikiwa kundi lolote litakuwa shughuli yao kubwa ni kuweka vikao vya kila mwaka kuwalani na kuwatukana Watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wakiwemo wake zake, au Sahaba zake (Radhiya Llahu anhum), kwa sababu hawa ni viongozi wetu waliokuwa naye tokea siku ile ya mwanzo. Hawa ni mifano mema kwetu, walioisimamia dini hii na kuieneza ulimwenguni kote, na hawa ndio waliotufikishia dini hii baada ya kujitolea mhanga roho zao na mali zao.

 

Wakati huo huo sisi tunaamini kuwa watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wanatoka katika nyumba bora kupita zote, lakini pia tunaamini kuwa hapana ajuaye Ghaybu isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Mwenyezi Mungu anasema:

(( Þõáú áÇ íóÚúáóãõ ãóäú Ýöí ÇáÓøóãóæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö ÇáúÛóíúÈó ÅöáøóÇ Çááøóåõ  ))[Çáäãá:65].

“Sema: ‘Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye Ghayb ila Mwenyezi Mungu.”

An Naml-65

Na anasema:

(( æóÚöäúÏóåõ ãóÝóÇÊöÍõ ÇáúÛóíúÈö áÇ íóÚúáóãõåóÇ ÅöáøóÇ åõæó ))[ÇáÃäÚÇã:59]

“Na ziko Kwake (Mwenyezi Mungu tu) funguo za siri (Ghayb) hakuna azijuaye ila Yeye tu.”

Al An-Am-59

 

 

Nani Sahaba – kilugha na kidini

Katika kamusi la lugha ya Kiarabu, neno ‘Sahaba’, maana yake ni Rafiki, Mwenzi wake, Sahibu nk.

Katika dini, neno ‘Sahaba’ maana yake ni Mwislamu aliyemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), akamfuata na kumuamini na akafariki katika imani hiyo.

Na hii ina maana kuwa, yeyote aliyewahi kumouna Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na asimuamini, basi hawezi kuingia katika maana ya neno ‘Sahaba’.

 

Nani Mnafiki – kilugha na kidini

Katika kamusi la lugha ya kiarabu, neno ‘Mnafiki’ maana yake ni mtu mwenye kigeugeu au mwenye kuwa na sura mbali mbali: Leo hivi kesho vile.

Katika dini, neno ‘Mnafiki’ maana yake ni yule anayejidhihirisha kuwa ni Muislam na kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), wakati undani wake ni kafiri na adui wa Mwenyezi Mungu na adui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

 

Baada ya tafsiri hii fupi ya nani Sahaba na nani Mnafiki, tutakubaliana kuwa maneno hayo mawili hayawezi kuwa na maana moja, (hayawezi kwenda sambamba) Kilugha wala Kidini.

Kwa sababu Sahaba ni yule aliyemuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akafariki dunia akiwa Muislam, wakati Mnafiki ni mwenye kujidhihirisha kama ni Mwislam wakati ndani ya nafsi yake ni kafiri.

Kwa hivyo haiwezekani Sahaba akawa Mnafiki na wala Mnafiki hawezi akawa Sahaba.

Sasa Mtu anaweza kuuliza:

'Vipi tutaweza kutofautisha baina ya Sahaba na Mnafiki?'

 Majibu:

Mnafiki ana sifa na alama maalum tulizojulishwa katika Qurani na katika Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na kwa ajili hiyo tunaweza kutofautisha baina yake na Sahaba.

Wanafiki ni watu;

‘Wanaoeneza ufisadi ardhini, kuifanyia istihzai dini, kuwafanyia istihzai wacha Mungu, ni wavukaji mipaka katika kufanya maasi wenye kuununua upotofu (upotevu) kwa uongofu, wavivu katika kufanya ibada, hugeuka geuka, mara Waislamu mara makafiri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

ãøõÐóÈúÐóÈöíäó Èóíúäó Ðóáößó áÇó Åöáóì åóÜÄõáÇÁ æóáÇó Åöáóì åóÜÄõáÇÁ

“Wanayumba yumba baina ya huku (kwa Waislam) na huko (kwa makafiri). Huku hawako wala huko hawako)”.

Annisaa-143

Na katika sifa za wanafiki pia ni;

‘Kuwa hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Akhera na kwamba Waislam wanapopata kheri yoyote au mafanikio, wao wanahuzunika, na hufurahi pale Waislamu wanapopata tabu au wanapokumbwa na masaibu au mitihani.

Huchukizwa na kutoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na hufurahi wanaporudi nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) peke yake vitani.

Wameingia katika dini kwa ajili ya kujikinga wasiambiwe kuwa wao ni makafiri, na wanapenda kuwadhuru Waislam na kuwafarikisha. Na katika sifa za unafiki ni kuwa; wanaiahirisha swala mpaka nyakati zake za mwisho na hawahudhurii Swala za jamaa na kwamba wanaionea uzito kabisa Swala ya Alfajiri na ya Ishaa’.

 

Hizi ni baadhi tu ya sifa za Wanafiki alizozitaja Mwenyezi Mungu katika Qurani tukufu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika mafundisho yake.

Bila shaka Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni watu walio mbali kabisa na sifa hizi. Hawa ambao Mwenyezi Mungu Amewaambia:

ßõäÊõãú ÎóíúÑó ÃõãøóÉò ÃõÎúÑöÌóÊú áöáäøóÇÓö ÊóÃúãõÑõæäó ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóÊóäúåóæúäó Úóäö ÇáúãõäßóÑö æóÊõÄúãöäõæäó ÈöÇááøåö

“Nyinyi ndio umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu”.

Aali Imran- 110

Na Akasema juu yao:

íÇ ÃíåÇ ÇáäÈí ÍÓÈß Çááå æãä ÇÊÈÚß ãä ÇáãÄãäíä

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na wale walokufuata katika hao walioamini”.

Al Anfal-64

Na Akasema juu yao:

ãøõÍóãøóÏñ ÑøóÓõæáõ Çááøóåö æóÇáøóÐöíäó ãóÚóåõ ÃóÔöÏøóÇÁ Úóáóì ÇáúßõÝøóÇÑö ÑõÍóãóÇÁ Èóíúäóåõãú ÊóÑóÇåõãú ÑõßøóÚÇð ÓõÌøóÏÇð íóÈúÊóÛõæäó ÝóÖúáÇð ãøöäó Çááøóåö æóÑöÖúæóÇäÇð

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja), wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake).”

Al Fat-h- 29

Na Akasema:

æóÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú æóåóÇÌóÑõæÇú æóÌóÇåóÏõæÇú Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóÇáøóÐöíäó ÂæóæÇú æøóäóÕóÑõæÇú ÃõæáóÜÆößó åõãõ ÇáúãõÄúãöäõæäó ÍóÞøÇð áøóåõã ãøóÛúÝöÑóÉñ æóÑöÒúÞñ ßóÑöíãñ

“Na wale walioamini wakahama (kuja Madina) na wakaipigania dini ya Mwenyezi Mungu (Nao ni Muhajir); na wale waliowapa (Muhajir) mahala pa kukaa na wakainusuru dini (ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake).(nao ni Ansar) Hao ndio Waislam wa kweli. Watapata msamaha (wa Mwenyezi Mungu) na kuruzukiwa kuzuri (kabisa huko Akhera)”.

Al Anfal – 74.

Masahaba wa Makka (Radhiya Llahu anhum) ndio walioamini, wakahama, na wakapigana jihadi. Na Masahaba wa Madina (Radhiya Llahu anhum) ndio waliowapa mahala pa kukaa na wakainusuru dini.

Baada ya maelezo haya kutoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi, asije mtu akatuambia kuwa Masahaba na wanafiki ni kitu kimoja. Hakika haya ni matusi makubwa kabisa!

Hawawezi kuwa wanafiki watu ambao Mwenyezi Mungu Amesema juu yao; “Nyinyi ndio umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni).”

Hawawezi kuwa wanafiki watu ambao Mwenyezi Mungu Ameshuhudia kuwa ni “Wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja), wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake).”

Hawawezi kuwa wanafiki watu ambao Mwenyezi Mungu Mwenyewe Anashuhudia  kuwa “Hao ndio Waislam wa kweli.”

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                       

 Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alisema:

"áÇ ÊóÓõÈøæÇ ÃóÕúÍóÇÈöí¡ ÝóæóÇáøÐöí äóÝúÓöí ÈöíóÏöåö áóæú Ãóäø ÃóÍóÏóßõãú ÃóäúÝóÞó ãöËúáó ÃõÍöÏò ÐóåóÈÇð ãóÇ ÃóÏúÑóßó ãõÏø ÃóÍóÏöåöãú æóáÇó äóÕöíÝóåõ".

"Msiwatukane Sahaba wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hata mmoja wenu atajitolea katika njia ya MwenyeziMungu kugawa dhahabu ukubwa wake mfano wa jabali Uhud, basi hatofikia gao lao wala hata nusu ya gao lao".

Bukhari na Muslim

Na akasema:

ãä ÓÈ ÃÕÍÇÈí ÝÚáíå áÚäÉ Çááå æÇáãáÇÆßÉ æÇáäÇÓ ÃÌãÚíä

“Atakayewatukana Masahaba wangu, basi itampata laana ya Mwenyezi Mungu na (laana ya) Malaika na (laana ya) watu wote”.

((Attabariy, katika ‘Al Kabeer’, Abi Naeem katika ‘Al Hiliya’ na Abi Asim, na hadithi hii pia inapatikana katika ‘Silsila za hadithi sahihi kilichoandikwa na Sheikh Al Albani)).

Na akasema (Swallah Llahu alayhi wa sallam):

“Nihifadhieni Masahaba wangu, kisha wale waliowafuatilia kisha wale waliofuatilia”.

Imam Ahmad, Ibni Majah, na Al Haakim.

 

Ikiwa Masahaba waliokuwa wengi wanatuhumiwa kuwa ni watu wenye kigeugeu na unafiki, hii italeta maana kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hakuweza kuwalea na kuwafundishsa vizuri Masahaba wake (Radhiya Llahu anhum) wakaijuwa haki, na kwamba yeye ni mlezi asiyefanikiwa, aliyeshindwa kuifanya kazi yake ya kuwalea Masahaba (Radhiya Llahu anhum).

Haikubaliki akilini abadan kuwa baada ya kuishi nao muda mrefu wote huo alifanikiwa kuwalea na kuwafundisha Masahaba watatu tu au wasiozidi saba?

 

Kila anayesoma na kuidurusu sira (historia) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), anaelewa kwamba wakati Waislam walipokuwa Makka hapakuwa na unafiki, na hii ni kwa ajili ya adhabu kali walizokuwa wakipata waliosilimu wakati ule. Na inajulikana pia kwamba unafiki ulianza kujitokeza baada ya Waislam kuhamia Madina, na baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kupata nguvu, na dini ya Mwenyezi Mungu kuanza kutambulika kila mahala.

Na inaeleweka pia kwa kila mwenye kuidurusu sira ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuwa Abubakar, Umar na Uthman na wengineo ni miongoni mwa Masahaba walioingia katika dini ya Mwenyezi Mungu tokea siku za mwanzo, wakapata tabu na shida kama walivyopata wenzao, na hii ni dalili wazi kuwa walikuwa mbali na sifa ya unafiki.

Mwenyezi Mungu amewafedhehesha wanafiki kwa kuwateremshia Suratul Munafiqun na At Tawba; akaelezea ndani ya sura hizo juu ya hali zao na vitimbi vyao; na akatuelezea yale yaliyofichika nyoyoni mwao katika kuwachukia Waislam, na ndiyo maana Surat at Tawba ikaitwa 'Sura ya Kufedhehesha'. Katika sura hiyo Mwenyezi Mungu alitaja pia sifa za Masahaba (Radhiya Llahu anhum) na akatujulisha kuridhika kwake nao. Na huu ni ushahidi utokao Kwake Subhanahu wa Taala.

Ama Suratul Munafiqun, hii imeteremshwa kwa ajili ya kutujulisha juu ya mkubwa wa wanafiki na kiongozi wao aitwae Abdillahi bin Ubay bin Salool na wenzake.

Anasema Zayd bin Al Arqam (Radhiya Llahu anhu):

"Nilikuwa vitani, nikamsikia Abdillahi bin Ubay akisema:

“Msitoe mali kuwasaidia waliokuwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu mpaka watakapomwondokea pale alipo, na tutakaporudi Madina yule mtukufu (akimaanisha yeye Abdillahi bin Ubay ‘mkuu wa wanafiki’kuwa ni mtukufu) atamtoa (katika mji wa Madina) yule aliyedhalilika (akimaanisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam kuwa eti ndiye aliyedhalilika)”.

Nikamhadithia ami yangu hayo niliyoyasikia (au Umar) naye akamhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam): Akaniita na mimi nikamhadithia. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamtuma mtu amuite Abdillahi bin Ubay pamoja na wenzake, wakaapa na kukanusha yale waliyosema, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hakunisadiki na akamsadiki yeye. Nikaona dhiki sijapata kuona mfano wake. Nikakaa nyumbani kwangu, lakini haujapita muda Mwenyezi Mungu akateremsha Suratul Munafiqun, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamtuma mtu aniite, akanisomea (Sura hiyo) kisha akaniambia:

“Mwenyezi Mungu amesadikisha maneno yako ewe Zeyd”.

Bukhari.

 

Tafsiri hii pia inapatikana katika kitabu cha tafsiri cha Mashia kiitwacho ‘Maj maa l bayan fiy tafsiyri l Quran’, kilichoandikwa na Imam Al Tubrusy ambaye ni miongoni mwa maulamaa wakubwa wa Kishia. Na katika kitabu hicho, ameelezea sababu ya kuteremshwa Suratul Munafiqun kuwa ni juu ya Abdillahi bin Ubay ‘mnafiki’ na wenzake …..

(Maj maa l bayan fiy tafsiyr l Qur an ukurasa 85)

Kisha Mwanachuoni huyu wa Kishia akazitaja riwaya zile zile alizozielezea Imam Bukhari zinazothibitisha hoja hiyo.

Inajulikana wazi kuwa Abdillahi bin Ubay pamoja na wafuasi wake walikuwa wakijulikana na Masahaba wote (Radhiya Llahu anhum) kuwa ni wanafiki, na mtu yeyote anaposoma Surat at Tawba ataona kuwa sura hiyo imeelezea juu ya vituko mbali mbali walivyokuwa wakivifanya wanafiki hao kiasi ambapo ilikuwa ikijulikana wazi mbele ya kila mtu kuwa wao ndio waliokusudiwa.

Kwa mfano kuanzia aya ya 44 hadi 49 ya sura hiyo Mwenyezi Mungu anasema:

áÇó íóÓúÊóÃúÐöäõßó ÇáøóÐöíäó íõÄúãöäõæäó ÈöÇááøåö æóÇáúíóæúãö ÇáÂÎöÑö Ãóä íõÌóÇåöÏõæÇú ÈöÃóãúæóÇáöåöãú æóÃóäÝõÓöåöãú æóÇááøåõ Úóáöíãñ ÈöÇáúãõÊøóÞöíäó {44} ÅöäøóãóÇ íóÓúÊóÃúÐöäõßó ÇáøóÐöíäó áÇó íõÄúãöäõæäó ÈöÇááøåö æóÇáúíóæúãö ÇáÂÎöÑö æóÇÑúÊóÇÈóÊú ÞõáõæÈõåõãú Ýóåõãú Ýöí ÑóíúÈöåöãú íóÊóÑóÏøóÏõæäó {45} æóáóæú ÃóÑóÇÏõæÇú ÇáúÎõÑõæÌó áÃóÚóÏøõæÇú áóåõ ÚõÏøóÉð æóáóÜßöä ßóÑöåó Çááøåõ ÇäÈöÚóÇËóåõãú ÝóËóÈøóØóåõãú æóÞöíáó ÇÞúÚõÏõæÇú ãóÚó ÇáúÞóÇÚöÏöíäó {46} áóæú ÎóÑóÌõæÇú Ýöíßõã ãøóÇ ÒóÇÏõæßõãú ÅöáÇøó ÎóÈóÇáÇð æáÃóæúÖóÚõæÇú ÎöáÇóáóßõãú íóÈúÛõæäóßõãõ ÇáúÝöÊúäóÉó æóÝöíßõãú ÓóãøóÇÚõæäó áóåõãú æóÇááøåõ Úóáöíãñ ÈöÇáÙøóÇáöãöíäó {47}þ áóÞóÏö ÇÈúÊóÛóæõÇú ÇáúÝöÊúäóÉó ãöä ÞóÈúáõ æóÞóáøóÈõæÇú áóßó ÇáÃõãõæÑó ÍóÊøóì ÌóÇÁ ÇáúÍóÞøõ æóÙóåóÑó ÃóãúÑõ Çááøåö æóåõãú ßóÇÑöåõæäó {48} æóãöäúåõã ãøóä íóÞõæáõ ÇÆúÐóä áøöí æóáÇó ÊóÝúÊöäøöí ÃóáÇó Ýöí ÇáúÝöÊúäóÉö

ÓóÞóØõæÇú æóÅöäøó Ìóåóäøóãó áóãõÍöíØóÉñ ÈöÇáúßóÇÝöÑöíäó {49}

“Hawatakuomba ruhusa wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wasende kupigana Jihadi kwa mali yao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua wachaMungu.

Wasio muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zikatia shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao.

Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa!

Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu.

Tangu zamani walitaka kukutilieni fitna, na wakakupindulia mambo juu chini, mpaka ikaja Haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu, na wao wamechukia”.

Na miongoni mwao wapo wanao sema: ‘Niruhusu wala usinitie katika fitina’. Kwa yakini wao hivyo wamekwisha tumbukia katika fitina. Na hakika Jahannamu imewazunguka.”

At Tawba – 44-49

Inaeleweka na kila mtu kuwa Masahaba wote walitoka kwenda vitani siku hiyo ya vita vya Tabuk (vita ambavyo aya hizo zinazungumzia juu yake), na waliobaki nyuma ni Aba Dhar na Aba Khaythamah (Radhiya Llahu anhum), kisha nao pia wakenda kujiunga na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pamoja na wenzao, na walikutana nao njiani kabla ya kuwasili uwanja wa vita.

Na ineleweka pia kuwa miongoni mwa waliobaki nyuma ni Kaab bin Malik, Hilal bin Umayyah na Mirara bin Rabia (Radhiya Llahu anhum), nao ni katika watu wa Madina na inajulikana na kila mtu kuwa Mwenyezi Mungu aliwasamehe Masahaba hao kama ilivyoelezwa katika kisa cha ‘Wale watatu waliongojeshwa’.

Ama wengine waliobaki Madina wasiende vitani walikuwa wakijulikana kuwa ni katika wale wanafiki waliomuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuomba udhuru wa uongo, au wale waliokuwa na udhuru wa kutopigana Jihad kwa ajili ya ugonjwa au udhuru mwingine unaokubalika.

Na haya tulieleza hapo mwanzo katika kisa cha Kaab (Radhiya Llahu anhu)  kuwa katika waliobaki pale Madina wasende vitani hakuwa akimuona aliye kufu yake isipokuwa wenye udhuru au wale waliokuwa wakijulikana kuwa ni Wanafiki.

Na hii ni dalili kuwa wanafiki walikuwa wakijulikana na Masahaba.

 

Na katika sura hiyo hiyo ya At Tawba, Mwenyezi Mungu Anatujulisha kuridhika kwake na Masahaba waliotangulia kuingia katika Uislamu miongoni mwa Wahajir (watu wa Makka waliohamia Madina) na Ansaar (Watu wa Madina waliowapokea Wahajir wa Makka) na akawatayarishia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele.

Mwenyezi Mungu anasema:

æóÇáÓøóÇÈöÞõæäó ÇáÃóæøóáõæäó ãöäó ÇáúãõåóÇÌöÑöíäó æóÇáÃóäÕóÇÑö æóÇáøóÐöíäó ÇÊøóÈóÚõæåõã ÈöÅöÍúÓóÇäò ÑøóÖöíó Çááøåõ Úóäúåõãú æóÑóÖõæÇú Úóäúåõ æóÃóÚóÏøó áóåõãú ÌóäøóÇÊò ÊóÌúÑöí ÊóÍúÊóåóÇ ÇáÃóäúåóÇÑõ ÎóÇáöÏöíäó ÝöíåóÇ ÃóÈóÏÇð Ðóáößó ÇáúÝóæúÒõ ÇáúÚóÙöíãõ

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”

At Tawba 100

Sasa tizameni ndugu zangu, vipi Mwenyezi Mungu anatuelezea juu ya kuridhika kwake na Masahaba katika Muhajir na Ansar kinyume na wanavyotuhumiwa unafiki, na kwamba walirudi nyuma na kukufuru, akiwemo mbora wa Masahaba wote Abubakar Al Siddique (Radhiya Llahu anhu).

Sisi tunaridhika na wote alioridhika nao Mwenyezi Mungu, na tunawafanyia uadui maadui wote wa Mwenyezi Mungu, na tunafuata yale tuliyofundishwa na Mwenyezi Mungu pamoja na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Mwenyezi Mungu anasema:

áóÞóÏ ÊøóÇÈó Çááå Úóáóì ÇáäøóÈöíøö æóÇáúãõåóÇÌöÑöíäó æóÇáÃóäÕóÇÑö ÇáøóÐöíäó ÇÊøóÈóÚõæåõ Ýöí ÓóÇÚóÉö ÇáúÚõÓúÑóÉö ãöä ÈóÚúÏö ãóÇ ßóÇÏó íóÒöíÛõ ÞõáõæÈõ ÝóÑöíÞò ãøöäúåõãú Ëõãøó ÊóÇÈó Úóáóíúåöãú Åöäøóåõ Èöåöãú ÑóÄõæÝñ ÑøóÍöíãñ {117}þ

“Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu.”

Attawba 117

Mwenyezi Mungu ni mpole kwao na anawarehemu na ameridhika nao na anawasifia namna walivyosimama pamoja na Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) katika saa ile ya dhiki (vita vya Tabuk), na huu ni ushahidi utokao kwa Mwenyezi Mungu Asiye mshirika.

 

Utayakuta haya pia katika vitabu vya wanavyuoni wakubwa wa Kishia (Ithnaasheri) waliotamka ukweli ndani ya baadhi ya vitabu vyao vinavyotambulika.

 

Tafsiri ya Al Iyashi

Anasema Abu Nasr Muhammad bin Masaud, anayejulikana kwa jina la ‘Al Iyashi’ katika tafsiri yake juu ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

Åöäøó Çááøåó íõÍöÈøõ ÇáÊøóæøóÇÈöíäó æóíõÍöÈøõ ÇáúãõÊóØóåøöÑöíä

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa.’

Al Baqarah – 222

Alisema:

"Kutoka kwa Salaam anasema: ‘Nilikuwa kwa Abu Jaafar (Muhammad Al Baqer Alayhi ssalaam- Imam wa tano kwa Shia) akaingia Hamran bin Ayun na kumuuliza baadhi ya mambo, na alipotaka kuondoka, Ayun akamuuliza Abu Jaafar:

'Tuelezee Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu, sisi tunapokuwa nawe nyoyo zetu hulainika na nafsi zetu zinakuwa mbali na dunia, tunadharau kila kilichomo mikononi mwa watu katika mali, lakini tunapotoka na kuchanganyika na watu na kufanya biashara, tunaanza kuipenda tena dunia.’

Abu Jaafar akasema:

"Nyoyo zinashindwa na mambo baadhi ya wakati, na wakati mwengine mambo yanakuwa mepesi.’ Kisha Abu Jaafar (Alayhi ssalaam) akaendelea kusema: ‘Kwa hakika Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu walisema:

‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunajiogopea unafiki’ akasema: “Kwa nini mnaogopa?”

Wakasema:

“Sisi tunapokuwa nawe ukatukumbusha, huwa na uoga, na nyoyo zetu zinalainika tukaisahau dunia, hatuitamani, hata hufikia kuwa tunaiona akhera Pepo na Moto mbele yetu. Lakini mara tunapotoka kwako na kuingia majumbani mwetu na kuanza kuwabusu watoto wetu na kuonana na wake zetu na mali zetu, tunaanza kubadilika hali zetu kinyume na pale tunapokuwa nawe, kama kwamba hatukuwa na kitu. Je! Hutuogopei unafiki?"

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akawaambia:

Kabisa sikuogopeeni hilo, kwani hizi ni katika hatua za shetani akijaribu kukupendezesheni dunia, Wallahi lau kama mungebaki katika hali ile mliyokuwa nayo pale mlipokuwa nami, basi Malaika wangekusalimieni majiani na mungekuwa mnatembea juu ya maji, na kama mungelikuwa hamtendi madhambi na kumuomba Maghfira Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu angeliumba viumbe vingine ili wafanye madhambi kisha wamuombe maghfira ili apate kuwaghufiria, kwani Muislam siku zote yupo katika mtihani, hukuisikia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

Åöäøó Çááøåó íõÍöÈøõ ÇáÊøóæøóÇÈöíäó

‘Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu?’

 na isemayo:

æóÃóäö ÇÓúÊóÛúÝöÑõæÇú ÑóÈøóßõãú Ëõãøó ÊõæÈõæÇú Åöáóíúåö

“Na ili muombe msamaha kwa Mola wenu kisha mtubie (mrejee)?"

Hud 3

(Tafsir Al Iyashi Juz1 uk.128)

 

Katika riwaya hii, anatubainishia Al Iyashi katika tafsiri yake kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ameshuhudia kuwa hawaogopei Sahaba zake unafiki. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hasemi kwa matamanio ya nafsi yake.

Kwa hivyo mwenye kumuita Sahaba yeyote kuwa ni mnafiki, mtu huyo atakuwa ana moja katika mawili:-

1-     Ama anakwenda kinyume na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

2-     Au anajua zaidi kupita Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Ikiwa tunautaka umoja wa Waislamu kikweli na kuiondoa chuki iliyopo, basi nawaomba ndugu zetu Mashia waache kuwakufurisha Masahaba au kuwaita wanafiki na kuwaapiza, na badala yake tumfanye Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa ni ruwaza njema kwetu, kuwa ni mfano mwema kwetu wa kuigwa, na tuwapende kama alivyokuwa akiwapenda Swallah Llahu alayhi wa sallam.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwapenda Swahaba zake (Radhiya Llahu anhum). Na watu wa nyumba yake 'Ahlul Bayt' (Radhiya Llahu anhum) nao pia walikuwa wakiwapenda Maswahaba (Radhiya Llahu anhum), na Maswahaba nao walikuwa wakiwapenda Ahlul Bayt.

Huyu hapa Imam Al Hassan Al Askari, ambaye ni Imam wa kumi na moja wa Shia alipokuwa akiwafahamisha watu daraja ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum)  mbele ya Mwenyezi Mungu alisema:

‘Miongoni wa masuala aliyouliza Musa (Alayhi Ssalaam) kumuuliza Mwenyezi Mungu alisema:

‘Wapo Masahaba wa Mtume yeyote wa Mwenyezi Mungu walio bora kuliko Masahaba wangu?'

Mwenyezi Mungu akamjibu:

“Ewe Musa kwani hujui kuwa ubora wa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad juu ya Masahaba wa Mitume yote ni sawa na ubora wa watu wa nyumba ya Muhammad juu ya watu wa nyumba za Mitume yote, na mfano wa ubora wa Muhammad juu ya Mitume yote?”

 Tafsiri ya Al Hassan Al Askary uk.11(Tafsiri ya Surat Al Baqarah

 

Ndani ya kitabu kitukufu kwa Shia kiitwacho ‘Nahaj al Balaghah’, Sharhi ya Muhammad Abdo Uk. 225, imeandikwa kua Imam Aly alisema:

“Nimewaona Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam), na sioni yeyote kati yenu aliyeshabihiana nao. Walikuwa wakati wa asubuhi utawaona nywele zimetimka kwa sababu ya kusimama kwao usiku kucha wakisujudu na kusimama (kwa kuswali), wanaomba huku wakisujudu, na wanapolala, na wanapokumbuka akhera yao utawaona wanasimama kama kwamba wamesimamia makaa ya moto. Na anapotajwa Allah basi macho yao yanatoa machozi mpaka nyuso zao zinaroa, na wanainamisha vichwa vyao chini mfano wa miti iliyopinda kwa upepo mkali wa kimbunga kwa kuhofia adhabu na kutarajia thawabu”.

 

Ama Ibarahim Al Thaqafi ambaye ni katika maulamaa wakubwa wa Shia, katika kitabu chake kiitwacho ‘Al Ghaaraat’ Juzuu ya 1 Uk.177 akimnukuu Aly (Radhiya Llahu anhu):

“Aliulizwa Aly: ‘Ewe Amiri wa Waislam, tuelezee juu ya Sahibu zako.’

Akauliza:

“Juu ya sahibu zangu wepi?”

Wakamwambia:

“Juu ya Sahaba wa Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam).”

Akasema:

“Masahaba wa Muhammad wote ni sahibu zangu”.

 

Tunamuomba msomaji arudie marejeo yote tuliyonukuu kutoka katika Qurani tukufu na kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na kutoka kwa maulamaa wa pande zote mbili ili imbainikie heshima ya Masahaba hawa wakiwemo Makhalifa watatu wa mwanzo wa Waislam mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na mbele ya maulamaa waliotangulia wa pande zote mble, kisha ajiulize; ni kwa maslahi ya nani mtu anaweza kuthubutu kuwatukana au kuwazulia uongo na kuwawekea vikao vya kila mwaka kuwalani na kuapa juu ya kulipa visasi.

Bali hata Sayiduna Al-Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa katika nchi ya Constantinople akipigana jihadi, na wakati huo Mu’awiyah (Radhiya Llahu anhu) ndiye aliyekuwa Khalifa wa Waislamu. Kwa hivyo Masahaba na Watu wa Nyumba ya Mtume (Radhiya Llahu anhum) walikuwa wakishirikiana na kupendana na kunasibiana na walikuwa pamoja katika jihadi yao dhidi ya maadui wa Uislamu.

 

Siku moja kundi la watu lilikwenda kwa Imam Aly Zeinul Abideen (Radhiya Llahu anhu) na walikuwa wakiwasema vibaya Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam); Abubakar, Umar na Uthman (Radhiya Llahu anhum).

Aly Zeinul Abideen (Radhiya Llahu anhu) akawauliza:

“Kwanza nielezeni ni nani nyinyi? Nyinyi ni katika wale Wahajir (Watu wa Makka) waliohama mwanzo waliotolewa majumbani mwao na katika mali zao wakitaka fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi zake na wakamnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake?”

ÇáøóÐöíäó ÃõÎúÑöÌõæÇ ãöä ÏöíÇÑöåöãú æóÃóãúæóÇáöåöãú  íóÈúÊóÛõæäó ÝóÖúáÇð ãøöäó Çááøóåö æóÑöÖúæóÇäÇð æóíóäÕõÑõæäó Çááøóåó æóÑóÓõæáóåõ

Al Hashr -8

Wote kwa pamoja wakasema: “La, sisi si katika hao”

Akawauliza tena:

“Basi nyinyi ni katika watu waliofanya maskani yao hapa (Madina) na wakautakasa Uislamu (wao barabara) kabla ya (kuja ) hao (Muhajirin) na wakawapenda hao waliohamia kwao”.

æóÇáøóÐöíäó ÊóÈóæøóÄõæÇ ÇáÏøóÇÑó æóÇáúÅöíãóÇäó ãöä ÞóÈúáöåöãú íõÍöÈøõæäó ãóäú åóÇÌóÑó Åöáóíúåöãú

Al Hashr -9

Wakajibu:

“La! Sisi si katika hao”

Kisha Imam Aly Zeinul Abideen (Radhiya Llahu anhu)  akawaambia:

“Nyinyi wenyewe mumeshuhudia kuwa si katika hawa wala si katika wale. Basi na mimi ninashuhudia pia kuwa nyinyi si katika kundi lile la tatu ambalo Mwenyezi Mungu Amesema juu yao:

æóÇáøóÐöíäó ÌóÇÄõæÇ ãöä ÈóÚúÏöåöãú íóÞõæáõæäó ÑóÈøóäóÇ ÇÛúÝöÑú áóäóÇ æóáöÅöÎúæóÇäöäóÇ ÇáøóÐöíäó ÓóÈóÞõæäóÇ ÈöÇáúÅöíãóÇäö æóáóÇ ÊóÌúÚóáú Ýöí ÞõáõæÈöäóÇ ÛöáøÇð áøöáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ÑóÈøóäóÇ Åöäøóßó ÑóÄõæÝñ ÑøóÍöíãñ

“Na Waliokuja baada yao (wakawa wanapendana na Waislamu waliotangulia wanawaombea dua) wanasema; ‘”Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia (kufa) katika Uislamu. Wala usijaaliye katika nyoyo zetu undani kuwafanyia Waislamu (wenzetu). Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole sana, Mwenye Rehema mno”.

Al Hashr – 10

Katika aya hizi Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa watu wa Makka waliacha majumba yao na mali zao na watu wao kwa ajili ya kutaka fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi zake, na kwa ajili ya kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na akashuhudia kuwa ni wakweli.

Na Mwenyezi Mungu anashuhudia pia watu wa Madina waliutakasa Uislamu baraabara, juu ya kuwa walifikiwa na wageni wazito na hawakuwa na mali ya kutosha, waliwapokea wageni hao kwa moyo mkunjufu, wakahiari kujinyima wao kwa ajili ya kuwakirimu wageni.

Kisha Mwenyezi Mungu Akatuamrisha tuliokuja baada yao kuwaombea maghfira na akatutaka tusijaaliye ndani ya nyoyo zet undani wowote juu yao.

 

Imepokelewa kutoka kwa Yahya bin Kathiyr kutoka kwa Jaafar bin Muhammad bin Aly bin Al Hussayn kutoka kwa baba yake ((Radhiya Llahu anhum) kuwa amesema:

« Alikuja mtu kwa baba yangu akamuambia : ‘Nihadithie juu ya Abubakar.’ Akasema: ‘Unauliza juu ya Al Siddique.’ Akasema yule mtu : ‘Mwenyezi Mungu akurehemu, na wewe pia unamuita Al Siddique ?’ Akamuambia : ‘Akukose mama yako wewe. Ameitwa As Siddique na aliye bora kupita mimi na wewe, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na Watu wa Makkah na watu wa Madina. Asiyemuita kwa jina la Al Siddique basi Mwenyezi Mungu hatosadiki kauli yake duniani wala akhera. Nenda, tena umpende Abubakar na Umar.»

 

Imeandikwa katika Nahj Al Balaghah pia kuwa Aly (Radhiya Llahu anhu) alimuandikia Muawiyah bin Abi Sufiyan (Radhiya Llahu anhu) akimuambia:

Kwa Muawiyah:

"Bisimillahi Rahmaani Rahiym,

Amma baad, kwa vile watu wote wamefungamana nami katika mji wa Madina, basi nawe pia uliyeko huko Sham (Syria) unalazimika kufungamana nami. Na hii ni kwa sababu watu waliofungamana nami ni wale wale waliofungamana na Abubakar na Umar na Uthmaan. Kwa hivyo aliyehudhuria hana haki ya kulikataa na asiyehudhuria hana haki ya kulipinga. Kwa hakika ushauri ni wa Muhaajirin na Answaar (Watu wa Makkah na wa Madina). Wanapokubaliana wote juu ya mtu na kumchagua kuwa Imam wao, na Mwenyezi Mungu Anaridhika na uchaguzi wao.

Nimemtuma kwako Jariyr, naye ni katika watu wa Imani na watu waliohajir, kwa hivyo fungamana nami - Walaa quwwata illa billaah!!".

Nahjul-Balaaghah- uk. 427 mlango wa 6

Subhanallah! Huyu hapa Aly (Radhiya Llahu anhu) anakiri mwenyewe kuwa hapana mwenye haki ya kupinga uchaguzi wa watu wa Makka na wa Madina na kwamba Mwenyezi Mungu ameridhika na kuchaguliwa kwa Abubakar na Umar na Aly (Radhiya Llahu anhum) kwa sababu wote wamechaguliwa kwa njia hiyo.

 

Kuoleana

Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ameoa mabinti wa Abubakar na Umar. Na Uthman alioa mabinti wawili wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), Mabibi Ruqayya na Ummu Kulthum, na alijulikana kwa jina la 'Dhiy Nnurayn', na maana yake ni Mwenye Nuru mbili kwa sababu ya mabinti hao wawili (Radhiya Llahu anhum).

Alihuzunika sana alipofariki mkewe wa pili Bibi Ummu Kulthum (Radhiya Llahu anha) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipomuona katika hali ile akamuuliza:

"Kipi kinachokuliza ewe Uthman?"

Uthman akajibu:

"Ninalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu kumekatika kunasibiana kwangu na wewe."

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

"Usilie ewe Uthman, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, lau kama nina mabinti mia wanakufa mmoja baada ya mwengine, basi ningekuozesha mpaka wasibaki katika mia hao hata mmoja."

Attabarani na wengine

 

Hii ni katika dalili za mapenzi makubwa yaliyokuwepo baina ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) pamoja na watu wa nyumba yake juu ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimuoa Bibi Aisha binti wa Abubakar Al Siddiquqe na alimuoa Hafsa binti wa Umar bin Khatab na alimuoa pia Ummu Habiybah Ramlah binti Abu Sufyan (Radhiya Llahu anhum).

 

Aly (Radhiya Llahu anhu) alimuozesha binti yake Ummu Kulthum kwa Umar bin Khatab.

(Al Kafi/346/5)

Alipouliwa Jaafar bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu), mkewe Asmaa binti Umays (Radhiya Llahu anha) aliolewa na Abubakar Al Siddique na alipofariki Abubakar (Radhiya Llahu anhu), Bibi Asmaa aliolewa na Aly bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu).

Jaafar Assadiq ni mjukuu wa Abubakar As Siddique, kwa sababu Muhammad Al Baqer mjukuu wa Al Hussain alimuoa Um Farwah mjukuu wa Muhammad bin Abubakar, na kutokana na ndoa hiyo akapatikana Jaafar As Sadiq. Kwa hivyo Jaafar ni mjukuu wa Abubakar na mwanawe Musa Al Kadhim anakuwa pia mtoto wa mjukuu wa Abubakar na kwa njia hii Maimam wote waliofuata wa Shia ni wajukuu wa Abubakar Al Siddique (Radhiya Llahu anhum jamiy’an)

Imepokelewa kuwa Jaafar Al Sadeq alikuwa akisema:

“Amenizaa Abubakar mara mbili.”

Siyar aalam al Nubalaa

 

Abaad bin Uthman bin Affan alimuoa Ummu Kulthum binti yake Abdullah bin Jaafar bin Abi Talib.

Shia wa Ahlul Bayt/141

Sakina binti Al Hussayn bin Aly bin Abi Talib aliolewa na Masaab bin Al Zubair bin Al Awaam.

Tabaqaat ibn Saad183/5

(Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote)

 

Majina ya watoto

Aly bin Abi Talib aliwapa wanawe majina ya Abubakar na Umar na Uthman.

Kashf al Ghumah 2/67

Al Hassan bin Aly alimpa mmoja wa watoto wake jina la Abubakar.

Kashf al Ghumah 2/198

Musa bin Jaafar alikuwa na watoto aliowapa majina ya Aisha na Umar.

Kashf al Ghumah 3/29

 

Wajibu wetu

Itakuwa siku ya furaha kubwa tutakapowaona wafuasi wa Sunni wakipeana mikono na wafuasi wa Shia kwa furaha bila kinyongo wala undani. Lakini hatuwezi kulifikia lengo hilo ikiwa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wataendelea kutukanwa na kukashifiwa na kulaaniwa.

Hatuwezi kulifikia ikiwa watu wataendelea kulizuru kaburi la Majusi Abu Lulua aliyemuua Khalifa wa Waislamu na Sahibu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) Umar bin Khataab (Radhiya Llahu anhu) na kuliita kaburi la Majusi huyo ‘Babu Shujaa ddiyn’ ‘Mlango wa shujaa wa  dini.’

Dini gani wakati mtu huyu hakuwa Muislamu? Kwa nini wanakubali kuisherehekea siku ambayo Mmajusi aliyekuwa akiabudu moto alimuuwa Khalifa wa Wasilamu?

Narudia mwito wa Sheikh Al Qaradhawi aliposema : «Enyi viongozi wa Shia wenye akili na hekima, upigeni vita mnasaba huu kwa ajili ya umoja wa Waislamu. Inatosha jamani kueneza chuki kwa mambo yaliyotokea miama 1500 iliyopita.»

Msisahau kuwa Umar huyu ni ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amemuowa bini yake Hafsa (Radhiya Llahu anha), na Umar huyu huyu ni mume wa Ummu Kulthum binti Aly bin Abi Talib (Radhiya Llahu anhu).