|
|
|||||
|
|
Kutokuwa na majivuno |
Kuona haya |
|||
|
|
Kuirudisha amana |
Ubakhili |
Husda |
|
Tembelea http://mawaidha.info
Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Mwenyezi Mungu ametufunza adabu za namna nyingi ili ziwe pambo letu Waislam zikitupamba katika matendo yetu,
maneno yetu, na pia zikitupamba ndani ya nafsi zetu.
Mapambo ya ndani ya nafsi ni Tabia
njema. Na Adabu, ni yale maneno na matendo mema
yanayozidhihirisha.
Neno Adabu, asili yake linatokana na
neno ‘Maaduba’, na maana yake ni kualikwa chakula au kuitwa. Na neno
‘Adabu’, limetoholewa kutoka katika neno hilo ‘Maaduba’,
kwa sababu watu ‘Wanaitwa’ katika kuzifuata tabia njema na katika kuwa na
khuluka njema.
Khuluka njema ni msingi madhubuti
wa Umma. Ni kuendelea kwa Umma. Ni
tumaini la Umma. Ni uhai wa Umma.
Umma ukirudishwa nyuma kwa sababu
zozote zile za kilimwengu kisha ukapoteza tabia zake njema na khuluqa zake, si
rahisi tena kunyanyuka. Lakini Umma hata ukirudi nyuma namna gani, ikiwa bado
umeshikamana na khuluqa njema, basi tumaini la
kunyanyuka tena linabaki. Na hii ni kwa sababu Umma
wowote ukiacha tabia zake njema na kujifanya kama karagosi kwa kuonyesha kila
fani ya kuiga, na jeuri na utovu wa adabu, basi tamaa ya kunyanyuka tena
inapotea.
Mshairi alisema:
ÇäãÇ ÇáÇãã ÇáÇÎáÇÞ ãÇ ÈÞíÊ ÝÇä åã ÐåÈÊ ÇÎáÇÞåã ÐåÈæÇ
“Hakika ya umma
wowote ule ukitaka kubaki, basi lazima wawe na tabia njema. Tabia njema zao zikitoweka,
basi na wao watatoweka.”
Umma wa Kiislamu ni Umma uliolelewa
kwa Adabu na Tabia njema tokea Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alipoanza kuwalingania watu katika dini hii tukufu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akisema:
ÈõÚöËúÊõ áÃÊãøöãó ãóßóÇÑöãó
ÇáÃóÎúáÇóÞö
“Kwa hakika nimeletwa kuja kukamilisha (kufundisha) tabia njema”.
Huyu ni Mtume wetu mtukufu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) ambaye Mola wake alimsifia na kumwambia:
æÅäß áÚáì ÎáÞ ÚÙíã
“Na bila shaka una tabia njema kabisa”
Al Qalam – 4
Muislamu anatakiwa awe mwenye adabu na
mwenye heshima akiwaheshimu wakubwa wake na wadodo wake.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
<áíÓ ãäÇ ãä áã íÑÍã ÕÛíÑäÇ¡ æíÚÑÝ ÔÑÝ
ßÈíÑäÇ>
Hayupo pamoja nasi
asiyewahurumia wadogo wetu na asiyeijuwa heshima ya
wakubwa wetu.
Attirmidhy na Abu Daud
Na katika riwaya nyingine, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema kumuambia Ummu Salamah
(Radhiya Llahu anha):
íÇ Ãã
ÓáãÉ ÐåÈ ÍÓä ÇáÎáÞ ÈÎíÑ ÇáÏäíÇ æÇáÂÎÑÉ
Ewe Ummu Salamah,
Tabia njema imechukuwa kheri zote za dunia na akhera.
Attabarani
Muislamu asiyekuwa na adabu
anaudhuru Uislamu badala ya kuupa nguvu. Mamilioni ya watu waliingia katika
dini hii tukufu kwa kuvutiwa na Adabu na Tabia njema
za Masahaba (Radhiya Llahu anhum) waliozifungua nchi zao hizo, pamoja na
kuvutiwa na Adabu na Tabia njema za wale waliokuja baada yao.
Mataifa makubwa kama vile Indonesia
kwa mfano, mamilioni ya watu wake waliingia katika dini hii kutokana na tabia
njema za wafanya biashara wa Kiislam waliokwenda huko. Walikuwa
wakiuona uaminifu wao, ukweli wao, ucha Mungu wao. Ilikuwa mara tu
unapofika wakati wa Swala, walikuwa wakiwaona namna
gani wafanya biashara hao wakiacha kazi zao na kuelekea mwahali maalum kwa
ajili ya kufanya Ibada zao.
Imam Malik anasema:
“Umma huu hauwezi
kutengenea isipokuwa kwa kufuata mwenendo wa wenzao waliowatangulia”.
Kuwatii wazee wawili
Kuwatii wazee wawili ni miongoni
mwa Adabu zilizotiliwa mkazo sana na kusisitizwa katika Qurani na katika
mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).
Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuwatii na
kuwafanyia wema wazee wetu, na akazifanya haki za wazee - baba na mama
- kuwa katika daraja la pili baada ya haki Zake Subhaanahu wa Taala. Mwenyezi
Mungu amewajaalia wazee kuwa ni sababu ya kuwepo kwetu
hapa duniani, na kwa ajili hiyo wakapata tabu sana juu yetu.
Hasa Mama, aliyembeba mwanawe tumboni miezi tisa, akamzaa, kisha akahangaika naye na kutaabika naye,
tabu juu ya tabu. Tabu ya kubeba, tabu ya kuzaa, tabu ya kulea, kunyonyesha pamoja
na kukesha na kuhangaika naye kila mtoto anapolia au
kuugua.
Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Ametuamrisha kuwakirimu wazee
wetu wawili hao, kuwatumikia kuwainamishia bawa la unyenyekevu, pamoja na kuwaombea dua ili Mwenyezi Mungu awarehemu kama
walivyotulea huku wakiturehemu tulipokuwa watoto.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÞóÖóì
ÑóÈøõßó ÃóáÇøó ÊóÚúÈõÏõæÇú ÅöáÇøó ÅöíøóÇåõ æóÈöÇáúæóÇáöÏóíúäö ÅöÍúÓóÇäðÇ ÅöãøóÇ
íóÈúáõÛóäøó ÚöäÏóßó ÇáúßöÈóÑó ÃóÍóÏõåõãóÇ Ãóæú ßöáÇóåõãóÇ ÝóáÇó ÊóÞõá áøóåõãóÂ
ÃõÝøò æóáÇó ÊóäúåóÑúåõãóÇ æóÞõá áøóåõãóÇ ÞóæúáÇð ßóÑöíãðÇ 23 æóÇÎúÝöÖú áóåõãóÇ
ÌóäóÇÍó ÇáÐøõáøö ãöäó ÇáÑøóÍúãóÉö æóÞõá ÑøóÈøö ÇÑúÍóãúåõãóÇ ßóãóÇ ÑóÈøóíóÇäöí
ÕóÛöíÑðÇ 24
“Na
Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa; Msimuabudu yeyote ila
Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko
kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala
usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wanguMlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.”
Al israa- Bani Israil 23-24
Na Anasema:
æóæóÕøóíúäóÇ
ÇáúÅöäÓóÇäó ÈöæóÇáöÏóíúåö ÍóãóáóÊúåõ Ãõãøõåõ æóåúäðÇ Úóáóì æóåúäò æóÝöÕóÇáõåõ
Ýöí ÚóÇãóíúäö Ãóäö ÇÔúßõÑú áöí æóáöæóÇáöÏóíúßó Åöáóíøó ÇáúãóÕöíÑõ
“Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili.
Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya
udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia):Nishukuru Mimi na wazazi wako. Na kwangu
Mimi ndiyo marudio.”
Luqman 14
Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) yanakubaliana na mafundisho ya Qurani.
Alipoulizwa juu ya matendo anayoyapenda zaidi Mwenyezi Mungu
kupita yote, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) alisema:
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alisema:
"ÇáÕáÇÉ Úáì æÞÊåÇ Ëã ÈÑ ÇáæÇáÏíä
Ëã ÇáÌåÇÏ Ýí ÓÈíá Çááøå"
"Swala
ndani ya wakati wake, kisha kuwafanyia wema wazee wawili kisha jihadi katika
njia ya Mwenyezi Mungu."
Fathi l Bari (Sharhi ya Sahihul Bukhari)
Aliiweka amali hii ya kuwafanyia wema wazee wawili kuwa ni ya pili ikiitangulia hata Jihadi katika njia ya Mwenyezi
Mungu.
Na alipokuwa akizitaja amali ovu, akaitaja amali ya kuwaasi
wazee wawili kuwa ni ya pili baada kumshirikisha
Mwenyezi Mungu. Akasema:
ÞÇá ÑÓæá Çááå Õáì Çááå Úáíå æÓáã: (ÃáÇ ÃäÈÆßã ÈÃßÈÑ
ÇáßÈÇÆÑ). ÞáäÇ: Èáì íÇ ÑÓæá Çááå¡ ÞÇá: (ÇáÅÔÑÇß ÈÇááå¡ æÚÞæÞ ÇáæÇáÏíä - æßÇä
ãÊ߯Çð ÝÌáÓ ÝÞÇá - ÃáÇ æÞæá ÇáÒæÑ¡ æÔåÇÏÉ ÇáÒæÑ¡ ÃáÇ æÞæá ÇáÒæÑ¡ æÔåÇÏÉ ÇáÒæÑ).
ÝãÇ ÒÇá íÞæáåÇ¡ ÍÊì ÞáÊ: áÇ íÓßÊ.
Amesema Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
“Nikuambieni ni amali
zipi zilizo ovu kupita zote?”
Tukasema:
“Tuambie ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu”
Akasema:
“Kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwaasi wazee
wawili,”
Alikuwa ameegemea, akakaa vizuri, kisha akasema:
“Na kusema uongo, na kutoa ushahidi wa uongo…”
Akawa anayakariri maneno hayo mpaka tukasema
(nyoyoni);
“Yareti angenyamaza”
Bukhari na Muslim
Pakitokea mgongano baina ya haki ya Mwenyezi Mungu na haki
ya wazee, kwa mfano mzee awe ni mshirikina akimuamrisha mwanawe naye awe kama
yeye katika ushirikina huo, au katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa jambo lolote
lile, basi hapo haijuzu kumtii mzee, kwa sababu haki ya Mwenyezi Mungu ni kubwa
zaidi na tukufu zaidi. Lakini wakati huo huo kuasi au kumshirikisha Mwenyezi
Mungu kwao, kusikuzuwie kuwatendea mema na kusikufanye
ukawa unawapiga pande.
Mwenyezi Mungu anasema:
æóÅöä
ÌóÇåóÏóÇßó Úóáì Ãóä ÊõÔúÑößó Èöí ãóÇ áóíúÓó áóßó Èöåö Úöáúãñ ÝóáóÇ ÊõØöÚúåõãóÇ
æóÕóÇÍöÈúåõãóÇ Ýöí ÇáÏøõäúíóÇ ãóÚúÑõæÝðÇ æóÇÊøóÈöÚú ÓóÈöíáó ãóäú ÃóäóÇÈó
Åöáóíøó Ëõãøó Åöáóíøó ãóÑúÌöÚõßõãú ÝóÃõäóÈøöÆõßõã ÈöãóÇ ßõäÊõãú ÊóÚúãóáõæäó
“Na pindi wakikushikilia
kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anayeelekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyokuwa
mkiyatenda.”
Luqman -15
Ndugu
wa Nasaba (Al Arhaam)
Ndugu wa Nasaba ni wale ulohusiana
nao, jamaa zako, ikiwa ni katika wanaoweza kukurithi au wasioweza, unaoweza
kuoana nao au usioweza, lakini upo uhusiano wa nasaba baina yenu.
Mwenyezi Mungu Ametutahadharisha juu ya hatari ya kuwapiga
pande ndugu wa Nasaba Akasema:
ÃóíøõåóÇ
ÇáäøóÇÓõ ÇÊøóÞõæÇú ÑóÈøóßõãõ ÇáøóÐöí ÎóáóÞóßõã ãøöä äøóÝúÓò æóÇÍöÏóÉò æóÎóáóÞó
ãöäúåóÇ ÒóæúÌóåóÇ æóÈóËøó ãöäúåõãóÇ ÑöÌóÇáÇð ßóËöíÑðÇ æóäöÓóÇÁ æóÇÊøóÞõæÇú
Çááøåó ÇáøóÐöí ÊóÓóÇÁáõæäó Èöåö æóÇáÃóÑúÍóÇãó Åöäøó Çááøåó ßóÇäó Úóáóíúßõãú
ÑóÞöíÈðÇ
“Enyi
watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na
akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake
wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye
mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kuwaangalieni.”
Annisaa - 1
Hapa Mwenyezi Mungu anatutahadharisha tusije tukamuasi, na pia anatutahadharisha juu ya Jamaa zetu, tusije
tukawapiga pande na kuachana nao.
Mwenyezi Mungu pia ametutaka tushikamane na
kuendeana nao.
Mwenyezi Mungu anasema:
æóÅöÐú ÃóÎóÐúäóÇ ãöíËóÇÞó Èóäöí
ÅöÓúÑóÇÆöíáó áÇó ÊóÚúÈõÏõæäó ÅöáÇøó Çááøåó æóÈöÇáúæóÇáöÏóíúäö ÅöÍúÓóÇäÇð æóÐöí
ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúíóÊóÇãóì æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÞõæáõæÇú áöáäøóÇÓö ÍõÓúäÇð
æóÃóÞöíãõæÇú ÇáÕøóáÇóÉó æóÂÊõæÇú ÇáÒøóßóÇÉó Ëõãøó ÊóæóáøóíúÊõãú ÅöáÇøó ÞóáöíáÇð
ãøöäßõãú æóÃóäÊõã ãøöÚúÑöÖõæäó
“Na
tulipofunga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu;
na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu
kwa wema,na shikeni Swala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipo kuwa wachache tu
katika nyinyi; na nyinyi (pia) mnapuuza.”
Al Baqarah - 83
Na Akasema:
æóÃõæúáõæÇú ÇáÃóÑúÍóÇãö ÈóÚúÖõåõãú Ãóæúáóì
ÈöÈóÚúÖò
“Na
ndugu wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe”
Al Anfal – 75
Na Akasema:
ÝóÂÊö ÐóÇ ÇáúÞõÑúÈóì ÍóÞøóåõ æóÇáúãöÓúßöíäó
æóÇÈúäó ÇáÓøóÈöíáö Ðóáößó ÎóíúÑñ áøöáøóÐöíäó íõÑöíÏõæäó æóÌúåó Çááøóåö
æóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
“Basi
mpe jamaa haki yake na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa). Hayo ni bora kwa wale wanaotaka radhi ya Mwenyezi Mungu; na hao
ndio watakaofuzu”.
Ar Rum – 38
(Neno ‘Rahim’ maana yake ni ‘undugu
wa nasaba’)
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
“Mwenyezi Mungu amelitoa (au amelitohoa) jina
la ‘Rahim’ kutoka katika jina lake ‘Al Rahiym’, kisha
akasema:
“Atakayekuunga nitamuunga
na atakayekukata nitamkata”.
Na hii inamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu atamkata (kwa kutomrehemu) yule atakayeukata uhusiano na jamaa zake,
na atawaunga (kwa kuwarehemu) wale watakaouendeleza uhusiano huo.
Mtu anaweza kuona kuwa; katika kutembeleana kwa ajili ya kuunganisha uhusiano na ndugu wa nasaba pesa
nyingi zinatumika na wakati mwingi unapotea. Lakini Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ametufundisha kinyume na hivyo.
Katika hadithi ilisiyomuliwa na
Anas bin Malik (Radhiya Llahu anhu), Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Anayependa atandaziwe riziki (aongezewe riziki yake),
basi aendeleze uhusiano wake na ndugu zake wa nasaba
(jamaa zake alohusiana nao)”.
Bukhari
Na katika Hadith al Qudusiy, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenyezi Mungu ameiambia
Rahim; ‘Je utaridhika iwapo nitamuunga atakayekuunga na nitamkata
atakayekukata?”
Rahim ikasema:
“Ndiyo”
Mwenyezi Mungu Akasema:
“Basi hiyo ni haki yako”
Bukhari
Kuuendeleza uhusiano huu kunakuwa kwa kupendana,
kunasihiana, kufanyiana wema na uadilifu, kurudishiana haki zilizopotea,
kuwasaidia wale wenye shida kati yao, kujua hali zao, kusameheana katika makosa
yanayotokea baina yao mara kwa mara, kuombeana dua, na kwa ujumla kujaribu
kuwafanyia kila la kheri na kuwaepusha na kila shari kwa uwezo wote.
Iwapo katika ndugu, yupo au wapo wasiopenda kurudisha
uhusiano na ndugu kwa sababu ndugu yake au jamaa yake huyo anapindukia mipaka
katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na baada ya kujaribu kila njia katika kunasihi
kwa kutumia njia mbali mbali za hekima kujaribu kumweka sawa ndugu huyo bila
mafanikio, basi hapana ubaya kuepukana na mtu au watu wa aina hiyo, wakati huo
huo tukiendelea kuwaombea dua, huenda Mwenyezi Mungu akawahidi na kuwaongoza
katika haki.
Mwenyezi Mungu anasema:
æóÇÚúÈõÏõæÇú
Çááøåó æóáÇó ÊõÔúÑößõæÇú Èöåö ÔóíúÆðÇ æóÈöÇáúæóÇáöÏóíúäö ÅöÍúÓóÇäðÇ æóÈöÐöí
ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúíóÊóÇãóì æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÇáúÌóÇÑö Ðöí ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúÌóÇÑö
ÇáúÌõäõÈö æóÇáÕøóÇÍöÈö ÈöÇáÌóäÈö æóÇÈúäö ÇáÓøóÈöíáö æóãóÇ ãóáóßóÊú
ÃóíúãóÇäõßõãú Åöäøó Çááøåó áÇó íõÍöÈøõ ãóä ßóÇäó ãõÎúÊóÇáÇð ÝóÎõæÑðÇ
“Muabuduni Mwenyezi Mungu
wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na
masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita
njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika
Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri”.
Annisaa – 36
Na katika hadithi iliyotolewa na Bukhari, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
“Jibril alikuwa
akiendelea kuniusia juu ya Jirani, hata nilidhania atapewa haki ya kunirithi”
Kumfanyia wema jirani, ni kwa kutokumuudhi au kumkera.
Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Wallahi si Muislam
Wallahi si Muislam”,
Wakamuuliza:
“Nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?”
Akasema:
“Ambaye jirani yake haiepuki
shari yake”
Katika wema pia, ni kumfanyia jirani ihsani kiasi cha uwezo wako kwa
kumsaidia pale anapohitajia msaada wao, kwa kumjulia hali yake, kumpelekea
zawadi, yote hayo kiasi cha uwezo.
Kuwafanyia
wema mayatima na masikini
Mwenyezi Mungu anasema:
íóÓúÃóáõæäóßó
ãóÇÐóÇ íõäÝöÞõæäó Þõáú ãóÇ ÃóäÝóÞúÊõã ãøöäú ÎóíúÑò ÝóáöáúæóÇáöÏóíúäö
æóÇáÃóÞúÑóÈöíäó æóÇáúíóÊóÇãóì æóÇáúãóÓóÇßöíäö æóÇÈúäö ÇáÓøóÈöíáö æóãóÇ
ÊóÝúÚóáõæÇú ãöäú ÎóíúÑò ÝóÅöäøó Çááøåó Èöåö Úóáöíãñ
“Wanakuuliza
watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya
wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri
yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua”.
Al Baqarah - 215
Na akasema:
æóÅöÐóÇ
ÍóÖóÑó ÇáúÞöÓúãóÉó ÃõæúáõæÇú ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúíóÊóÇãóì æóÇáúãóÓóÇßöíäõ
ÝóÇÑúÒõÞõæåõã ãøöäúåõ æóÞõæáõæÇú áóåõãú ÞóæúáÇð ãøóÚúÑõæÝðÇ
“Na
wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa na mayatima na
masikini, wapeni katika hayo mali ya urithi, na semeni nao maneno mema”.
An Nisaa - 8
Na akasema:
ÝóÂÊö
ÐóÇ ÇáúÞõÑúÈóì ÍóÞøóåõ æóÇáúãöÓúßöíäó æóÇÈúäó ÇáÓøóÈöíáö Ðóáößó ÎóíúÑñ
áøöáøóÐöíäó íõÑöíÏõæäó æóÌúåó Çááøóåö æóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
“Basi
mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa”.
Ar Rum - 38
Na katika hadithi, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kujishughulisha kuwasaidia Vizuka na Masikini ni mfano wa anayepigana Jihadi katika njia ya
Mwenyezi Mungu, au mfano wa mwenye kufunga nyakati za mchana na kuswali nyakati
za usiku”.
Bukhari
Na katika hadithi nyingine Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mimi na mwenye kumlea
yatima tutakuwa (pamoja) Peponi kama hivi.” Akaashiria kwa kidole cha
shahada na cha kati.
Bukhari
Makatazo
katika kudharauliana, dhana, kupelelezana na kusengenyana
Mwenyezi kiburi hupata maradhi mengi
yakiwemo kudharau, kusengenya nk. Na hii ni kwa sababu mtu wa aina hii siku zote hujiona kuwa
yeye amekamilika, na kwa ajili hiyo huanza kuwatia wenzake kila aina ya ila,
wakati ukweli wa mambo ni kwamba yeye ndiye mwenye ila, na kwa ajili hiyo
utamuona anajaribu kutafuta ila za wenzake pamoja na makosa yao na kuwaonyesha
watu makosa hayo, ili ajionyeshe kuwa yeye amekamilika.
Mtu wa aina hii hupenda kuwadharau
wenzake na kuwacheka pale wanapokosea.
Haya yote yameharimishwa. Na Mwenyezi Mungu ametujulisha
kuwa mwenye kudharauliwa huenda akawa ni bora kuliko
mwenye kudharau, na ujinga wa mwisho ni mtu kumdharau yule aliye bora kuliko
yeye.
Mwenyezi Mungu Anasema:
íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ áóÇ íóÓúÎóÑú Þóæãñ ãøöä Þóæúãò
ÚóÓóì Ãóä íóßõæäõæÇ ÎóíúÑðÇ ãøöäúåõãú æóáóÇ äöÓóÇÁ ãøöä äøöÓóÇÁ ÚóÓóì Ãóä
íóßõäøó ÎóíúÑðÇ ãøöäúåõäøó
“Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau
wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao.”
Al Hujurat - 11
Na katika jambo baya la dharau ni
kule kuwavunjia watu heshima na kuwaita kwa majina ya kejeli.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóáÇ
ÊóáúãöÒõæÇ ÃóäÝõÓóßõãú æóáÇ ÊóäóÇÈóÒõæÇ ÈöÇáÇóáúÞóÇÈö ÈöÆúÓó ÇáÇöÓúãõ
ÇáúÝõÓõæÞõ ÈóÚúÏó ÇáÇíãóÇäö æóãóä áøóãú íóÊõÈú ÝóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáÙøóÇáöãõæäó
“Wala
msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya
kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini.
Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu”.
Al Hujurat - 11
Kuwasengenya watu, na maana yake ni kutafuta
makosa yao na upungufu wao, na kuyazungumza kwa wengine.
Waislamu wanatakiwa wawe wenye kupendana mfano wa mwili mmoja, kila mmoja amsitiri mwenzake na sio
kumfedhehesha.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
æóáÇ íóÛúÊóÈ ÈøóÚúÖõßõã
ÈóÚúÖðÇ
“Wala msisengenyane
nyinyi kwa nyinyi."
Al Hujurat - 12
Kwa hivyo Muislam anapomsengenya Muislam mwenzake au kumwita
kwa jina ovu, anakuwa kama amejifanyia mwenyewe, na hii ni kwa sababu Muislam
ni ndugu wa Muislam na Umma wa Kiislam ni Umma mmoja.
Katika mambo aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, ni kujiamulia mambo kwa dhana tupu, kwa sababu dhana
inaharibu uhusiano baina ya watu na kuwafanya watoe uamuzi kinyume na haki.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ÇÌúÊóäöÈõæÇ ßóËöíÑðÇ ãøöäó ÇáÙøóäøö Åöäøó ÈóÚúÖó
ÇáÙøóäøö ÅöËúãñ
“Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi”.
Al Hujurat - 12
Mwenyezi Mungu ametukataza pia kupelelezana kutaka kujua
siri za watu au kuona na kusikia yale ambayo wenyewe
hawapendi wengine wayasikie.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
æóáÇ ÊóÌóÓøóÓõæÇ
“Wala msipelelezane”.
Al Hujurat - 12
Katika kulifasiri neno ‘Kusengeya’ (Ghiyba), Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwauliza
Masahaba (Radhiya Llahu anhu):
"Mnajua
nini maana ya kusengenya (Ghiyba)? "
Wakasema:
"MwenyeziMungu na Mtume wake wanajua zaidi".
Akasema:
"(Kusengenya) ni kuzungumza juu ya nduguyo
(Muislam, akiwa hayupo) yale anayoyachukia".
Akaulizwa:
"Je! ikiwa (ila) ninayoizungumzia anayo
kweli?"
Akasema:
"Ikiwa anayo kweli, basi huko ndiko kusengenya, na ikiwa si kweli, basi
hayo ni madhambi makubwa zaidi (kwa kumsingizia uongo)”.
Muslim
Mafunzo
mbali mbali yaliyotungiwa sheria katika Uislamu
Mwenyezi Mungu ametuwekea sheria na
mafundisho mbali mbali katika mwenendo wetu na adabu zetu, na Muislam anatakiwa
ayafuate. Miongoni mwa mafundisho hayo ni;
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye
kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiama, amkirimu
mgeni wake.”
Bukhari na Muslim
Kuomba
ruhusa kabla ya kuingia
Katika mafundisho ya kiislamu ni
kuomba ruhusa kabla ya kuingia majumbani mwa watu.
Mwenyezi Mungu anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ áÇ ÊóÏúÎõáõæÇ ÈõíõæÊðÇ ÛóíúÑó ÈõíõæÊößõãú ÍóÊøóì
ÊóÓúÊóÃúäöÓõæÇ æóÊõÓóáøöãõæÇ Úóáóì ÃóåúáöåóÇ Ðóáößõãú ÎóíúÑñ áøóßõãú
áóÚóáøóßõãú ÊóÐóßøóÑõæäó
“Enyi
mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu
mpate kukumbuka”.
An Nur – 27
Mwenyezi Mungu anasema:
æóÅöÐóÇ
ÍõíøöíúÊõã ÈöÊóÍöíøóÉò ÝóÍóíøõæÇú ÈöÃóÍúÓóäó ãöäúåóÇ Ãóæú ÑõÏøõæåóÇ Åöäøó
Çááøåó ßóÇäó Úóáóì ßõáøö ÔóíúÁò ÍóÓöíÈðÇ
“Na
mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko
hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kuhisabu kila kitu”.
An Nisaa - 86
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Haki
ya Muislamu kwa mwenzake ni mambo matano;
1.
Kumtolea salaam,
2.
Kumtembelea anapoumwa,
3.
Kuhudhuria mazishi yake,
4.
Kuitikia wito anapokualika, na
5.
Kumwombea ndua anapokwenda chafya.
Bukhari na Muslim
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) pia ametufundisha namna ya kutoa salam, akasema:
“Aliyepanda (gari, mnyama nk.) anamsalimia anayekwenda kwa
miguu, (na) anayekwenda anamsalimia aliyekaa, watoto wawasalimie wakubwa na
wachache wawasalimie wengi”.
Bukhari
Na akasema:
“Umtolee
salamu unayemjua na usiyemjua”
Bukhari
Katika dini yetu tumefundishwa kusema; ‘Bismillahi’ kabla ya
kula, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusema;
‘Alhamdulillah’ baada ya kula, na pia tumefundishwa kula kwa mkono wa kulia.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alipomuona mtoto mdogo akila chakula ndani ya sinia ,
mara anakula kilicho chini yake na mara anakula kilicho mbali, akamwambia:
“Ewe kijana! Sema
Bismillah, kula kwa mkono wa kulia na kula kilicho karibu yako’
Bukhari na Muslim
Tumefundishwa pia kuwa mtu anapokwenda chafya aseme:
‘Alhamdulillah’, na yule atakayemsikia (akisema
Alhamdulillah) amwambie; ‘Yarhamuka Llah’, (Mwenyezi Mungu akurehemu). Kisha
yule aliyepiga chafya anamjibu mwenzake kwa kumwambia; “Yahdiykumu Llahu wa
yuslih baalakum”.(Mwenyezi Mungu akuhidi na astawishe
hali yako).
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
"ÅÐóÇ ÚóØóÓó ÃÍóÏõßõãú ÝóáúíóÞõá:
ÇáÍóãúÏõ áöáøóåö¡ æóáúíóÞõáú áóåõ ÃÎõæåõ Ãæú ÕóÇÍÈõåõ: íóÑúÍóãõßó Çááøóåõ¡
ÝÅÐóÇ ÞÇáó áóåõ: íóÑúÍóãõßó Çááøóåõ¡ ÝóáúíóÞõáú: íóåúÏöíßõãõ Çááøóåõ æóíõÕúáöÍõ
ÈÇáóßõãú"
“Mmoja wenu akienda chafya aseme:
’Alhamdulillah’ na amjibu ndugu yake na rafiki yake (kwa kumwambia;)
‘Yarhamuka Llah’, na akimwambia; ‘Yarhamuka Llah’
amjibu kwa kumwambia: ‘Yahdiykumu Llahu wa yuslih baalakum”.
Bukhari
Katika mafundisho ya Kiislam pia tumekatazwa kunon’gona watu
wawili ikiwa yupo wa tatu pamoja nao.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mnapokuwa watatu, wawili wasinon’gone wakamuacha wa tatu
wao, mpaka mchanganyike na watu (muwe wengi) kwa sababu (kutenda) hivyo,
kutamhuzunisha (wa tatu wenu)”.
Bukhari na Muslim
Dini yetu imetuamrisha na
kupendekeza kuwazuru wagonjwa.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Muislam anapomzuru ndugu yake Muislam, anakuwa ndani ya
bustani za Peponi mpaka atakaporudi.”
Muslim
Ni vizuri pia mtu anapomtembelea mgonjwa na
kabla ya kuondoka, asimame kuliani pake kisha aombe dua ifuatayo mara saba:
ÃÓÃáõ Çááøóåó ÇáÚóÙöíãó ÑóÈø ÇáÚóÑúÔö ÇáÚóÙöíãö Ãäú
íóÔúÝöíßó
“Namuomba Mola mtukufu Mola wa Arshi tukufu, akuafu”
Attirmidhy
Kula
na kunywa wima
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) ametukataza kula au kunywa tukiwa tumesimama wima.
Amesema Anas (Radhiya Llahu anhu):
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
ametukataza mtu kunywa akiwa amesima wima”. Anasema Qatada: ‘Tukamuuliza Anas; ‘Na kula je?’ Akasema; “Vibaya zaidi.”
Akimaanisha ‘kula wima’.
Muslim
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) ameharamisha mwanamume kuvaa dhahabu na vitambaa vya hariri.
Katika hadithi nyingi zilizomo katika Bukhari na Muslim na vitabu vingine sahihi kutoka kwa Masahaba mbali
mbali (Radhiya Llahu anhum) wamesema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
ametukataza kuvaa dhahabu na hariri, na (ametukataza pia) kunywa ndani ya
vyombo vya dhahabu na vya fedha, na akasema: “Vyombo hivi ni vyao hapa duniani
na vyenu huko akhera”
Bukhari na Muslim
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) pia ametufundisha namna ya kuwalea watoto, kuwahurumia
na kuwabusu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwabusu Al Hassan na Al Hussein (Radhiya
Llahu anhum), na alimkataza yule aliyesema kuwa ana watoto kumi na hajapata
kumbusu yeyote kati yao hata siku moja. Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimwambia:
“Asiyekuwa na huruma, hatohurumiwa.”
Bukhari
Rehma ya Muislam si kwa ajili kwa
wanadamu peke
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alitujulisha juu ya yule aliyekuwa na kiu, na baada ya
kunywa maji kisimani akamuona mbwa akihangaika mbele ya kisima, akajisemea
moyoni mwake:
“Bila shaka mbwa huyu ana kiu kikubwa”. Akachota maji kisimani na
kumnywesha. Mwenyezi Mungu akamghufiria madhambi yake yote.
Masahaba
(Radhiya Llahu anhu) waliposikia hayo wakamuuliza:
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata katika wanyama tunapata
thawabu?”
Akasema:
“Katika kila kiumbe kilicho hai mnapata thawabu (mkikifanyia
wema na kukihurumia).
Bukhari
Upole
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
ametufundisha kuwa wapole na wavumilivu katika kutatua matatizo yetu.
Alimfundisha Bibi Aisha (Radhiya Llahu anhu) hayo pale Bibi Aisha alipowatukana
Mayahudi na kuwalani. Akamwambia:
“Taratibu
ewe Aisha, Mwenyezi Mungu anapenda upole katika kila kitu”
Bukhari
Kisa chenyewe kilikuwa hivi:
Liliingia
kundi la Mayahudi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) na badala ya kumtolea salaam kwa kumuambia
"ASSALAAM alaykum, wakamuambia:
“ASSAAM
aleikum”, na maana yake NI; “Mauti yawe juu yenu.”
Walisema
hivyo wakidhania kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) hatotambua. Lakini Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akawajibu:
“Wa alaikum”. Bila
ya kuongeza neno lolote, na maana yake; “Na juu yenu
pia”.
Bibi
Aisha (Radhiya Llahu anha) aliyekuwa amekaa pamoja na
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) wakati ule akawajibu
kwa ghadhabu:
‘Alaykumu
assaam wa Llaana’
“Mauti
yawe juu yenu pamoja na laana”
Ndipo
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alipomwambia:
“Taratibu ewe Aisha, Mwenyezi Mungu anapenda upole katika
kila kitu.”
Anasema
Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha):
“Nikamwambia:
"Hukuwasikia walivyosema?”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akanijibu:
“Nimesikia,
ndio maana nikawajibu ‘Wa aleikum”
Na
maana yake “Na juu yenu”
Mwenyezi Mungu ametuamrisha tusaidiane wenyewe kwa wenyewe kwa wema na kwa uchaMungu, akasema:
æóÊóÚóÇæóäõæÇú
Úóáóì ÇáúÈÑøö æóÇáÊøóÞúæóì æóáÇó ÊóÚóÇæóäõæÇú Úóáóì ÇáÅöËúãö æóÇáúÚõÏúæóÇäö
“Na
saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika
dhambi na uadui”.
Al Maidah – 2
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amefananisha kushikamana kwa Waislam kuwa sawa na kushikamana kwa mwili mmoja,
na akafananisha kushikamana huko kuwa ni sawa na kushikamana kwa majengo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Waislam katika kuhurumiana kwao na kupendana kwao na
kupendeleana kwao ni mfano wa mwili mmoja, kinaposikitika kiungo (chochote kwa
kuumwa), basi mwili wote unashirikiana katika kukesha na kupata homa”.
Bukhari na Muslim
Na katika hadithi nyingine amesema:
“Waislam ni mfano wa majengo, yameshikamana na kuzuwiana
yenyewe kwa yenyewe (yasianguke)”.
Bukhari
Namima
(Kuchukuwa maneno ya huku na kuyapeleka kule)
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) ametuhadharisha juu ya tabia mbaya sana ya 'Namiyma',
nayo ni mtu kuchukua maneno ya huku na kuyapeleka kule kwa nia ya kufitinisha.
Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alipopita karibu na kaburi, aliwajulisha Masahaba (Radhiya
Llahu anhum) kuwa mwenye kaburi lile anaadhibishwa kwa sababu alikuwa akiishi
baina ya wenzake akiwa na tabia hiyo ovu.
Uislam unatufundisha pia ubora wa
kusaidia watu na kukidhi haja zao.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Anayejishughulisha na kuwasaidia ndugu zake, na Mwenyezi
Mungu atamsaidia. Na
atakayemuondolea Muislam mwenzake dhiki yake, basi Mwenyezi Mungu atamuondolea
dhiki katika dhiki zake za Siku ya Kiama. Na atakayemsitiri Muislam na Mwenyezi Mungu atamsitiri Siku ya Kiama”.
Muslim
Tabia, ni ule mwenendo alio nao
mwanadamu ndani ya nafsi yake. Mwenendo ambao si rahisi mtu kuweza
kuubadilisha, kwa sababu chimbuko lake ni ndani ya
nafsi yake, na hatimaye unageuka mwenendo huo kuwa ni sehemu ya dhati yake
asiyoweza kuachana nayo.
Baadhi ya maulama wa elimu ya nafsi
wanasema kuwa Tabia ya mtu ni mfano wa picha yake ikikuelezea ni nani yeye, na
anaweza kujulikana mtu undani wake kutokana na tabia zake.
Bila shaka tabia ziko ovu na ziko
njema.
Katika lugha ya kiarabu neno ‘Khalqu’ maana yake “Umbile” na neno “Khuluqu” maana yake “Tabia”. La mwanzo kwa kutumia ‘a’ ‘Khalqu’ na linatujulisha juu ya
umbile la nje la kiumbe. Ama la pili kwa herufi ‘u’
‘Khuluqu’ linatujulisha juu ya umbile la ndani la kiumbe.
Kwa hivyo neno ‘Khalqu’ (Umbile), linamaanisha sura inayo
onekana ya kiumbe na neno ‘Khuluqu’ ambalo kwa
kiswahili tunaita ‘Khuluka’ na maana yake ni tabia, linatujulisha juu ya zile
tabia ambazo si kitu cha kuonekana kwa jicho, bali zimo ndani ya nafsi yake
mwanadamu.
Kama tulivyoandika hapo mwanzo kuwa Tabia ziko aina mbili; Njema
na Ovu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alimuambia Ash'aj Abdul Qais (Radhiya Llahu anhu):
“Una mambo mawili ambayo Mwenyezi Mungu anayapenda; Upole na
Kutokuwa na pupa”.
Ahmed – Annasai – na Bukhari katika
Adabul mufrad (Fathu l
Miongoni mwa tabia njema, ni Kusema
kweli, Uaminifu, Ukarimu, Kutimiza Ahadi, Ushujaa na Subira. Bila shaka mwenye
tabia hizi anastahiki kukirimiwa na kupewa kila sifa
anayostahiki.
Miongoni mwa Tabia ovu ni; Kusema
Uwongo, Khiana, Uwoga, na Kusengenya.
Mwenye tabia hizi, bila shaka
anastahiki kila lawama.
Mwenyezi Mungu ametuwekea sheria inayowaita
(inayowalingania) watu katika Tabia njema na
kuwakataza Tabia ovu, ili nafsi zipate kutahirika na kutakasika na ili watu
waweze kuishi vizuri baina
Kwa ajili hii, utaona kuwa mafundisho mengi ya dini
yamezungumzia maudhui haya na hayakuacha kumpa sifa
anazostahiki kila mwenye tabia njema. Inatosha kauli yake Suhanahu wa Taala alipomsifia Mtume wake kwa kumwambia:
æóÅöäøóßó
áóÚóáì ÎõáõÞò ÚóÙöíãò
“Na bila shaka una tabia
njema kabisa”.
Suratul Qalam - 4
Mwenyezi Mungu akatutaka pia tuzikimbilie Rehema Zake na Pepo Yake aliyowatayarishia wacha Mungu katika waja wake
wenye sifa hiyo ya Tabia njema.
Mwenyezi Mungu ööAnasema:
æóÓóÇÑöÚõæÇú
Åöáóì ãóÛúÝöÑóÉò ãøöä ÑøóÈøößõãú æóÌóäøóÉò ÚóÑúÖõåóÇ ÇáÓøóãóÇæóÇÊõ æóÇáÃóÑúÖõ
ÃõÚöÏøóÊú áöáúãõÊøóÞöíäó. ÇáøóÐöíäó íõäÝöÞõæäó Ýöí ÇáÓøóÑøóÇÁ æóÇáÖøóÑøóÇÁ
æóÇáúßóÇÙöãöíäó ÇáúÛóíúÙó æóÇáúÚóÇÝöíäó Úóäö ÇáäøóÇÓö æóÇááøåõ íõÍöÈøõ
ÇáúãõÍúÓöäöíäó
“Na
yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo
ambayo upana wake tu ni sawa na upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari
kwa wachamungu.
Ambao hutoa wanapo kuwa na
wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia
ghadhabu, na wasamehevu
kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.”
Aal Imran – 133-134
Na katika aya ifuatayo, Mwenyezi amewasifia wenye kutimiza
ahadi, wavumilivu wakati wa shida, wakati wa madhara
na wakati wa vita, kuwa ni watu wenye Tabia njema.
Mwenyezi Mungu Anasema:
áøóíúÓó
ÇáúÈöÑøó Ãóä ÊõæóáøõæÇú æõÌõæåóßõãú ÞöÈóáó ÇáúãóÔúÑöÞö æóÇáúãóÛúÑöÈö æóáóÜßöäøó
ÇáúÈöÑøó ãóäú Âãóäó ÈöÇááøåö æóÇáúíóæúãö ÇáÂÎöÑö æóÇáúãóáÂÆößóÉö æóÇáúßöÊóÇÈö
æóÇáäøóÈöíøöíäó æóÂÊóì ÇáúãóÇáó Úóáóì ÍõÈøöåö Ðóæöí ÇáúÞõÑúÈóì æóÇáúíóÊóÇãóì
æóÇáúãóÓóÇßöíäó æóÇÈúäó ÇáÓøóÈöíáö æóÇáÓøóÂÆöáöíäó æóÝöí ÇáÑøöÞóÇÈö æóÃóÞóÇãó
ÇáÕøóáÇÉó æóÂÊóì ÇáÒøóßóÇÉó æóÇáúãõæÝõæäó ÈöÚóåúÏöåöãú ÅöÐóÇ ÚóÇåóÏõæÇú
æóÇáÕøóÇÈöÑöíäó Ýöí ÇáúÈóÃúÓóÇÁ æÇáÖøóÑøóÇÁ æóÍöíäó ÇáúÈóÃúÓö ÃõæáóÜÆößó
ÇáøóÐöíäó ÕóÏóÞõæÇ
“Sio
wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na
Magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na
Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali kwa kupenda kwake, jamaa na
mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa
anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao
vumilia katika shidana dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, hao
ndio wajilindao.”
Al Baqarah – 177
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) pia ametufundisha mengi juu ya umuhimu wa kuwa na Tabia
njema.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Wema (kutenda mema) ni (katika) Tabia njema”.
Muslim
Na akasema:
“Mbora wenu ni yule mwenye Tabia njema zaidi”.
Bukhari
Na akasema:
“Kwa
hakika, Muislam mkamilifu wa Imani ni yule mwenye
Tabia njema kupita wenzake”
Attirmidhiy na Al Hakim
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) pia ametujulisha kuwa Tabia njema ndiyo yenye uzito
zaidi juu ya mizani Siku ya Kiama.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna
chenye uzito zaidi juu ya mizani kuliko Tabia njema”
Bukhari, Abu Daud, Attirmidhiy na imesahihishwa
na Ibni Hibban
Tabia njema pia ni katika sababu
kubwa za kuingizwa katika Pepo ya Mwenyezi Mungu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alipoulizwa juu amali gani zinazowaingiza watu zaidi
Peponi akasema:
“Ucha
Mungu na Tabia njema”
Attirmidhiy na Ibni Hibban (Bukhari
katika Fathi l
Na akasema:
“Katika
wale ninaowapenda sana miongoni mwenu na watakaokuwa karibu nami Siku ya Kiama,
ni wale wenye Tabia njema, na katika wale ninaowachukia na watakaokuwa mbali
zaidi nami, ni wale wenye kusema maneno mengi yasiyo na maana na wenye
kuzungumza kwa kujinata (huku akiukaza ulimi na kuuregeza na kujifanya kuwa
yeye ni mfasihi kuliko wenzake) na wenye kuzungumza kwa kiburi.”
Attirmidhiy
Bila shaka mwenye Tabia na mwenendo
mwema pamoja na maneno mazuri yasiyo na kiburi, ni mwenye kupendeka zaidi mbele
ya wenzake.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hamtopendwa
na watu kwa ajili ya mali zenu, bali mtapendwa kwa
ajili ya ukunjufu wa nyuso zenu na Tabia zenu njema”.
Al Bazzaar
Tumesoma hapo mwanzo kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni mfano bora wa kufuatwa katika
Tabia njema, hata Mola wake Subhaanahu wa Taala Akamuambia:
æóÅöäøóßó
áóÚóáì ÎõáõÞò ÚóÙöíãò
“Na bila shaka una tabia njema kabisa”.
Suratul Qalam - 4
Masahaba wake (Radhiya Llahu anhum) na
adui zake, wote walikubaliana juu ya Tabia zake njema. Hajawahi hata siku moja
yeyote katika adui zake kumtuhumu Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuhusu jambo hili, bali Tabia zake njema
zilijulikana kila pembe ya dunia.
Anas bin Malik (Radhiya Llahu anhu) alimtumikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) miaka
kumi, na alikuwa hambanduki kila anapokwenda, na kwa ajili hiyo bila shaka
alikuwa akimjua vizuri sana Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam).
Tumsikilize nini anasema juu ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
Anasema Anas (Radhiya Llahu anhu):
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa mbora wa viumbe, mkarimu kupita wote na alikuwa shujaa kupita wote”.
Anaendelea kusema:
“Nimemtumikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) miaka kumi, wallahi
hajapata hata siku moja kuniambia:”Ah!”, na wala
hajapata kuniambia kuhusu jambo lolote nililofanya: ”Kwa nini umefanya,"
au "bora ungefanya hivi”.
Muslim
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala
Mwenyezi Mungu öööAnasema:
æóáÇ
ÊõØöÚú ßõáøó ÍóáÇÝò ãøóåöíäò. åóãøóÇÒò ãøóÔøóÇÁ Èöäóãöíãò. ãóäøóÇÚò áøöáúÎóíúÑö
ãõÚúÊóÏò ÃóËöíãò
“Wala
usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa.
Mtapitapi, apitaye
akifitini. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa
madhambi.
Mkavu, na juu ya
hayo, mshari, amejipachika tu.”
Al Qalam – 10 - 13
Katika kumkataza mwanawe tabia mbovu, Luqmaan mwenye hekima alisema:
æóáÇ
ÊõÕóÚøöÑú ÎóÏøóßó áöáäøóÇÓö æáÇ ÊóãúÔö Ýöí ÇáúÃóÑúÖö ãóÑóÍðÇ Åöäøó Çááøóåó áÇ
íõÍöÈøõ ßõáøó ãõÎúÊóÇáò ÝóÎõæÑò
“Wala
usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na
kujifakhirisha.”
Luqman – 18
Kujitahidi
katika kujipamba na Tabia njema
Baadhi ya wataalam wanasema kuwa; Tabia ni
mizizi iliyo ndani ya nafsi ya mtu. Ni kitu alichoumbwa nacho, na kwamba haiwezekani mtu kujirekebisha au hata kujaribu
kuzibadilisha tabia zake. Baadhi ya watu wakapata kisingizio kutokana na msemo huu, wakaona uzito kujitahidi katika kuzirekebisha
tabia zao.
Lakini ukweli ni kwamba zipo katika
Tabia njema ambazo mtu ameumbwa nazo ndani ya nafsi yake. Na mtu anapojaaliwa na kitu
Wakati huo huo zipo tabia njema ambazo mtu huzipata kwa kujaribu na kujitahidi,
“Una mambo mawili ambayo Mwenyezi Mungu anayapenda; Upole na
Kutokuwa na pupa”.
Al
Ash'aj, akamuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam):
“Ninazo (tabia hizo) tokea mwanzo (nimezaliwa nayo) au
nimezipata baadaye?”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamjibu:
“Tokea mwanzo”
Akasema:
“Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniumba na tabia mbili anazozipenda”.
Ahmed – Annasai – na Bukhari katika
Adabul mufrad (Fathu l
Katika kuisherehesha hadithi hii, anasema Ibni Hajar Al
Asqalani, mmoja wa Maulamaa wakubwa wa Kiislam:
“Kutokana na jawabu
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), tunaelewa kuwa zipo
katika Tabia mtu ameumbwa nazo, na zipo zile ambazo mtu anaweza kuzipata au
kujifunza”.
Fathi l Bari
Zipo dalili nyingi zinazothibitisha kuwa mtu anaweza
kuzipata au kujifunza.Tabia njema:
Kwanza:-
Tunaona kwa mfano mtu mwoga,
kutokana na kupewa mafunzo mengi na jitihada nyingi anageuka kuwa shujaa. Na
pia tunaona mara nyingine mtu mwongo, kwa mafunzo na
malezi bora, anageuka kuwa ni msema kweli. Kama vile tulivyoona wagomvi na watu waovu, baada ya kumjua Mola wao na kuongezeka imani
Pili:-
Tumeona pia mara nyingi wanyama
wanapopata mafunzo, hubadilisha Tabia zao. Tumeona kwa
mfano paka anapopata mafunzo maalum, huishi pamoja na mapanya, na mbwa anaishi
na paka, na pia tumeona kima wanapopata mafunzo maalum huweza kufanya mambo
mengi ya kiajabu. Ikiwa mwenendo wa wanyama unaweza
kubadilika, basi uwezo wa mwanadamu ni mkubwa zaidi.
Tatu:-
Mweyezi Mungu katika sehemu nyingi ametutaka tuzibadilishe
tabia zetu na kuwa na Tabia njema.
Mwenyezi Mungu ööAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÇÊøóÞõæÇú Çááøåó æóßõæäõæÇú ãóÚó ÇáÕøóÇÏöÞöíäó
“Enyi
mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.”
At Tawba – 119
Na Akasema:
æóÇÕúÈöÑú
æóãóÇ ÕóÈúÑõßó ÅöáÇøó ÈöÇááøåö æóáÇó ÊóÍúÒóäú Úóáóíúåöãú æóáÇó Êóßõ Ýöí ÖóíúÞò
ãøöãøóÇ íóãúßõÑõæäó
“Na
subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa
sababu ya Mwenyezi Mungu tu. Wala usiwahuzunikie; wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazo zifanya.”
An Nahl-127
Na Akasema:
æóÃóäÝöÞõæÇú
Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóáÇó ÊõáúÞõæÇú ÈöÃóíúÏöíßõãú Åöáóì ÇáÊøóåúáõßóÉö
æóÃóÍúÓöäõæóÇú Åöäøó Çááøåó íõÍöÈøõ ÇáúãõÍúÓöäöíäó
“Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala
msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu
huwapenda wafanyao wema.”
Al Baqarah - 195
Ingelikuwa Tabia za mtu haziwezi kubadilika, basi amri za
Mwenyezi Mungu pale anapotutaka tubadilishe Tabia zetu na
kuzifanya ziwe njema zitakuwa hazileti maana. Na kila mwenye akili timamu
anatambua kuwa Mwenyezi Mungu haamrishi jambo lisilo na
maana wala haamrishi yale tusiyoyaweza.
Mwenyezi Mungu Anasema:
áÇó
íõßóáøöÝõ Çááøåõ äóÝúÓðÇ ÅöáÇøó æõÓúÚóåóÇ áóåóÇ ãóÇ ßóÓóÈóÊú æóÚóáóíúåóÇ ãóÇ
ÇßúÊóÓóÈóÊú ÑóÈøóäóÇ áÇó ÊõÄóÇÎöÐúäóÇ Åöä äøóÓöíäóÇ Ãóæú ÃóÎúØóÃúäóÇ ÑóÈøóäóÇ
æóáÇó ÊóÍúãöáú ÚóáóíúäóÇ ÅöÕúÑðÇ ßóãóÇ ÍóãóáúÊóåõ Úóáóì ÇáøóÐöíäó ãöä ÞóÈúáöäóÇ
ÑóÈøóäóÇ æóáÇó ÊõÍóãøöáúäóÇ ãóÇ áÇó ØóÇÞóÉó áóäóÇ Èöåö æóÇÚúÝõ ÚóäøóÇ æóÇÛúÝöÑú
áóäóÇ æóÇÑúÍóãúäó ÃóäÊó ãóæúáÇóäóÇ ÝóÇäÕõÑúäóÇ Úóáóì ÇáúÞóæúãö ÇáúßóÇÝöÑöíäó
“Mwenyezi Mungu
haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri iwezavyo. Faida ya iliyo
yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake
pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie
tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu
Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na
utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.”
Al Baqarah - 286
Nne:-
Katika hadithi sahihi, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika ya elimu (mtu huipata) kwa kujifunza, na upole (mtu hujifunza) kwa kuwa mpole na
mtu anapoitafuta kheri ataipata, na anayejiepusha na shari, huepushwa nayo.”
Al Khatib, kutoka kwa Abi Huraira
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) pia alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu amuongoze katika
Tabia njema.
Katika dua ya kufungulia sala alikuwa akiomba kwa kusema:
æÇåÏäí áÃÍÓä ÇáÃÎáÇÞ áÇ íåÏí áÃÍÓäåÇ ÅáÇ ÃäÊ æÇÕÑÝ Úäí ÓíÆåÇ
áÇ íÕÑÝ Úäí ÓíÆåÇ ÅáÇ ÃäÊ
Na maana yake ni;
“Na uniongoze katika
Tabia njema, hapana aongozae katika Tabia njema isipokuwa Wewe. Na uniepushe na Tabia mbaya, hapana anaye epusha nazo isipokuwa Wewe.”
Muslim, Attirmdhy Annasai na
wengine
Mmoja katika maulamaa wa
1.
Subira
2.
Wema
3.
Ushujaa
4.
Uadilifu
1.
Mwenye Subira kwa
kawaida huwa mstahamilivu. Hupenda kuwaondolea wenzake udhia, huwa mwenye
huruma, mpole, na kwa kawaida mweye Subira hawi na
tabia ya pupa na uamuzi wa haraka.
2 Mtu Mwema daima
hujiepusha na utovu wa adabu na uovu katika vitendo na
matamshi, na pia huwa mwingi wa haya. Na tabia hii ya kuona haya ni nguzo muhimu
Wema pia humuepusha mtu na matendo
machafu, ubakhili, uwongo, kusengenya na kufitinisha watu kwa kuchukua maneno
ya huku na kuyapeleka kule.
3 Mtu Shujaa kwa kawaida hujiheshimu. Hapendi kuwakosea wenzake kama vile yeye alivyokuwa hapendi kukosewa. Shujaa pia huwa na tabia ya kuwatakia wenzake kheri, hata
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Ushujaa si kwa uhodari
wa kupigana mieleka, bali ushujaa ni mtu anayeimiliki nafsi yake wakati wa
ghadhabu”.
Huu ndio ushujaa, nao ni ufalme na
hawezi kuumiliki ufalme huo isipokuwa Shujaa peke yake.
4 Uadilifu, kama alivyosema Feiruz Abadi; Humfanya mwenye tabia hiyo
kuweza kufanya mambo yake yote kwa Uadilifu, kati na kati bila ya kupindukia
mipaka katika kutoa wala katika kuzuwia nk.
Mfano
wa tabia njema na ovu
Ukweli ndiyo njia ya ushindi na
mafanikio, na uwongo ndiyo njia ya kushindwa na upotofu. Hivi ndivyo dini yetu
inavyotufundisha na hivi ndivyo ilivyothibiti katika
maisha yetu na matendo yetu ya siku zote.
Kama yupo mwenye kudhania kinyume cha
hayo, basi amekosea. Akiwepo anayedhania kuwa uwongo ndio utakaomuokoa, na ukweli utamuangamiza, basi huyo bado hajaijua vizuri haki
na yuko mbali nayo kabisa.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) ametufundisha hayo katika hadithi iliyosimuliwa na
Abdillahi bin Masaood (Radhiya Llahu anhu).
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Shikamaneni na
ukweli, kwa sababu ukweli unaongoza katika wema, na wema kwa hakika unaongoza
katika Pepo, na mtu anaposema kweli na akawa anajilazimisha (kila anaposema)
kusema kweli, mpaka ataandikwa kwa MwenyeziMungu kuwa ni Msemakweli. Na
jiepusheni na uwongo, kwa sababu uwongo kwa hakika
unaongoza katika maovu, na maovu kwa hakika yanaongoza katika Moto. Na mtu
anaposema uwongo, na akawa anajilazimisha (kila
anaposema) kusema uwongo, mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa kuwa ni
Muongo”.
Bukhari na Muslim
Zifuatazo ni sifa walizopewa
waliosadiki na kuamini kikweli:
Mwenyezi Mungu öAnasema:
ãöäó
ÇáúãõÄúãöäöíäó ÑöÌóÇáñ ÕóÏóÞõæÇ ãóÇ ÚóÇåóÏõæÇ Çááøóåó Úóáóíúåö Ýóãöäúåõã ãøóä
ÞóÖóì äóÍúÈóåõ æóãöäúåõã ãøóä íóäÊóÙöÑõ æóãóÇ ÈóÏøóáõæÇ ÊóÈúÏöíáÇ
“Miongoni
mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na
Mwenyezi Mungu.Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala
hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.”
Al Ahzab – 23
Wale waliokadhibisha na kutoa ahadi
za uwongo, Mwenyezi Mungu Amesema juu yao:
æóãöäúåõã
ãøóäú ÚóÇåóÏó Çááøåó áóÆöäú ÂÊóÇäóÇ ãöä ÝóÖúáöåö áóäóÕøóÏøóÞóäøó æóáóäóßõæäóäøó
ãöäó ÇáÕøóÇáöÍöíäó. ÝóáóãøóÇ ÂÊóÇåõã ãøöä ÝóÖúáöåö ÈóÎöáõæÇú Èöåö æóÊóæóáøóæÇú
æøóåõã ãøõÚúÑöÖõæäó. ÝóÃóÚúÞóÈóåõãú äöÝóÇÞðÇ Ýöí ÞõáõæÈöåöãú Åöáóì íóæúãö
íóáúÞóæúäóåõ ÈöãóÇ ÃóÎúáóÝõæÇú Çááøåó ãóÇ æóÚóÏõæåõ æóÈöãóÇ ßóÇäõæÇú
íóßúÐöÈõæäó
“Na
miongoni mwao wapo walio muahidi Mwenyezi Mungu kwa kusema: Akitupa katika
fadhila yake hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika watendao mema.
Alipo wapa katika fadhila yake wakaifanyia
ubakhili na wakageuka, na huku
Wakipuuza, basi akawalipa unafiki kuutia
nyoyoni mwao mpaka Siku watapo kutana naye, kwa sababu
ya kuwa walimkhalifu Mwenyezi Mungu katika yale waliyo muahidi, na kwa sababu
ya kusema kwao uwongo.”
At Tawba – 75-77
'Ukweli', kama unavyotakiwa katika
mazungumzo na katika kutimiza ahadi, pia unatakiwa katika matendo. Kwa sababu
mtu anapoahidi kutenda jambo, kwa mfano anapomuahidi
Mwenyezi Mungu kutoa sadaka atakapojaaliwa kupata pesa, basi wakati unapowadia
lazima aitimize ahadi hiyo. Na siku zote mtu anatakiwa ajitahidi katika
kuudhihirisha ukweli katika kauli zake na matendo
yake, ili matendo hayo yadhihirishe yale yaliyo ndani ya nafsi yake.
Msema kweli siku zote hupendeza mbele
ya watu.
Wanamuaminisha hata mali zao. Ushahidi wake
unakubaliwa na unakuwa na uzito mbele ya wenzake.
Kinyume na muongo ambaye watu hawamsadiki, na ushahidi
wake haukubaliwi, na watu hawamuamini katika mali zao.
2-
Kutokuwa na majivuno
Atakayejichunguza akaijua asili yake aliyoumbiwa na Mwenyezi
Mungu, akauchunguza ulimwengu aliyezaliwa na kukuwa ndani yake, kisha akamjua
Mola wake mtukufu aliyemuumba yeye na aliyeumba ulimwengu wote, itambidi aondoe
majivuno yake, na amsitahi Mola wake mtukufu. Kustahi huko, kutaonekana matunda
yake katika kauli zake anazotamka na katika matendo
yake.
Tumsikilize Mwenyezi Mungu Akituelezea juu ya waja wake
wasiokuwa na majivuno.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÚöÈóÇÏõ
ÇáÑøóÍúãóäö ÇáøóÐöíäó íóãúÔõæäó Úóáóì ÇáÇóÑúÖö åóæúäðÇ æóÅöÐóÇ ÎóÇØóÈóåõãõ
ÇáúÌóÇåöáõæäó ÞóÇáõæÇ ÓóáÇãðÇ
“Na waja wa Arrahman (Mwingi wa Rehema) ni
wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu:
Salama!”.
Al Furqan - 63
Kiburi kinatokana na ujinga wa mtu
asiyeijuwa kadiri yake na asiyeijuwa kadiri ya Mola wake aliyemuumba. Kwa
sababu kila kitu hapa duniani ni cha kupita, hakina
thamani yoyote na hakistahiki mtu kutakabari kwa ajili yake.
Pesa zitaondoka, ufalme utaondoka, uzuri utatoweka na uhai haudumu milele. Hapana atakayebaki
isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Mwenyezi Mungu Anasema:
ßõáøõ
ãóäú ÚóáóíúåóÇ ÝóÇäò. æóíóÈúÞóì æóÌúåõ ÑóÈøößó Ðõæ ÇáúÌóáÇáö æóÇáÅßúÑóÇãö
“Kila
kilioko juu yake kitatoweka.”
Na atabakia Mwenyewe Mola
wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.”
Ar Rahman – 26 – 27
Kwa hivyo mwenye kiburi anajipachika
cheo asichostahiki. Anashindana na Mola wake katika
moja wapo ya sifa Zake, na Mwenyezi Mungu haridhiki na jambo hilo.
Katika Hadithul Qudusiy, Mwenyezi Mungu anasema:
“Kiburi ni (mfano wa)
vazi langu la chini, na utukufu ni (mfano wa) vazi langu la juu atakaye
(jaribu) kuninya’nganya moja kati ya hizo, nitamtupa Motoni na wala sijali.”
Muslim
Mwenye kiburi hawezi kufaidika na
wenye kuilingania haki, kwa sababu kiburi chake kinamzuwia asiweze kuikubali
haki, na matokeo yake hupata hasara kubwa.
Mwenyezi Mungu anasema:
ÓóÃóÕúÑöÝõ
Úóäú ÂíóÇÊöíó ÇáøóÐöíäó íóÊóßóÈøóÑõæäó Ýöí ÇáÃóÑúÖö ÈöÛóíúÑö ÇáúÍóÞøö æóÅöä
íóÑóæúÇú ßõáøó ÂíóÉò áÇøó íõÄúãöäõæÇú ÈöåóÇ æóÅöä íóÑóæúÇú ÓóÈöíáó ÇáÑøõÔúÏö
áÇó íóÊøóÎöÐõæåõ ÓóÈöíáÇð æóÅöä íóÑóæúÇú ÓóÈöíáó ÇáúÛóíøö íóÊøóÎöÐõæåõ ÓóÈöíáÇð
Ðóáößó ÈöÃóäøóåõãú ßóÐøóÈõæÇú ÈöÂíóÇÊöäóÇ æóßóÇäõæÇú ÚóäúåóÇ ÛóÇÝöáöíäó
“Nitawatenga
na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi
bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini
wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo
ni kwa sababu wamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo.”
Al Aaraf- 146
Na mwenye kiburi hupata hasara ya nafsi yake, kwa sababu yeyote mwenye sifa ya kuwa na kiburi, Mwenyezi
Mungu humdhalilisha.
Mwenyezi Mungu Anasema:
Åöäøó
ÇáøóÐöíäó íóÓúÊóßúÈöÑõæäó Úóäú ÚöÈóÇÏóÊöí ÓóíóÏúÎõáõæäó Ìóåóäøóãó ÏóÇÎöÑöíäó
“Kwa
hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu
wadhalilike”.
Ghafir (Al Muuminun) – 60
Mwenyezi Mungu anamdhalilisha mwenye kiburi, lakini wakati
huo huo asiye na kiburi Mwenyezi Mungu humtukuza na
kumkirimu.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) anasema:
“Mwenyezi Mungu humuongezea utukufu mja wake
anayesamehe, na mtu anapoondowa kiburi chake mbele ya Mwenyezi Mungu, basi
Mwenyezi Mungu humnyanyua”.
Muslim
Al Fudhail bin Abbas amemuelezea asiye na
kiburi kuwa na sifa zifuatazo;
“Mwenye kuikubali haki na
kuifuata. Hata ukiisikia kutoka kwa asiyekuwa na elimu,
(haki) lazima uikubali”.
Kitabu ‘Tahadhiyb mauidhatul Muuminin’
Lakini kiburi ni kinyume na hivyo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
“Kiburi ni kuipinga haki
na kuwadharau watu”.
Muslim
Wafuasi wa dini zote wanajulikana
kwa sifa zao maalum. Sifa ambazo wasiokuwa wao hawana.
Kwa mfano Mayahudi wanajulikana kuwa wana sifa ya khofu,
Manasara, wana sifa ya kupenda. Ama Waislamu, wao wana sifa ya aina yao peke
Katika kitabu chake Imam Malik kiitwacho Al Muwata- a anasema:
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Kila dini ina
khuluqa zake, na khuluqa za Uislamu ni kuona haya”.
Khuluqa njema inamuongoza mtu katika
kufanya amali njema, lakini khuluqa mbaya inamuongoza mtu katika maovu. Kwa hivyo anayemsitahi Mwenyezi
Mungu, hupenda kumtii, na kuepukana na kumuasi pamoja
na kumuabudu
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Msitahini Mwenyezi Mungu kama anavyopaswa
kustahiwa”
Attirmidhy
Na akasema:
“Kuona haya hakuleti
(kingine) isipokuwa kheri tupu”.
Bukhari na Muslim
Na kuona haya ni dalili ya kuwa na
imani.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Imani ina sehemu
sabini na zaidi. Sehemu ya juu kabisa ni kauli ya ‘La
ilaaha illa Llah’ na ya chini ni kuondoa udhia barabarani, na kuona haya ni
sehemu katika sehemu za imani”.
Bukhari na Muslim
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) siku moja alipokuwa akipita njiani, alimsikia mtu
akimnasihi ndugu yake apunguze kuona haya, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:
“Mwache, kwani kuona haya ni
dalili ya kuwa na imani”.
Bukhari na Muslim
Ikiwa kuona haya kunamsaidia mtu katika matendo ya kheri, kwa hivyo kutokuwa na haya kunaondoa vile vikwazo
vinavyomfanya mtu asitende maovu na kumfanya ateleze na kuanza kuyatenda maovu
hayo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Katika maneno yaliyonukuliwa kutoka kwa
Mitume iliyotangulia; (ni haya yafuatayo): “Ikiwa huna haya, basi tenda
utakalo”.
Bukhari
Juu ya kuwa kuona haya ni jambo la
kheri, lakini haya hizo zisimpeleke mtu akaacha kufanya matendo mema,
kukakataza maovu na kuuliza katika mambo ya dini yale asiyoyaelewa.
Ummu Salama (Radhiya Llahu anha) amesema kumwambia mumewe
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
“Ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Hatutaki tuone haya katika (kuijua) haki, je! Mwanamke anapoota anatakiwa kukoga?”
Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema: “Ndiyo,
atakapoyaona maji”
Bukhari
Kupendelea, nako ni mtu kumpendelea
kheri mwenzake kuliko nafsi yake. Na hii ni daraja
kubwa isiyoweza kufikiwa isipokuwa na watu wenye daraja kubwa. Masahaba (Radhiya
Llahu anhum) walizifikia daraja hizo, na Mwenyezi
Mungu ameshuhudia hayo pale Aliposema:
æóíõÄúËöÑõæäó
Úóáóì ÃóäÝõÓöåöãú æóáóæú ßóÇäó Èöåöãú ÎóÕóÇÕóÉñ
“Bali
wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.”
Hashr – 9
Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) amesimulia
kuwa; mgeni mmoja aliyetoka safari ya mbali alimwendea Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kumwambia:
“Mimi nimechoka sana”.
Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) (alitaka kumkirimu yeye mwenyewe, lakini)
hakuwa na chochote nyumbani kwake cha kuweza kumkirimu mgeni yule. Akawauliza
Sahaba zake (Radhiya Llahu anhum):
“Nani atakayemkirimu mgeni huyu usiku wa leo?”
Mmoja katika watu wa
Madina akasema:
“Mimi, ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu”.
Akamchukua na kwenda
naye mpaka nyumbani kwake na kumwambia mkewe:
“Tumkirimu, huyu ni
mgeni wa Mtume wa Mwenyezi Mungu”.
Katika riwaya nyingine, imepokelewa kuwa
alisema kumuuliza mkewe:
“Kuna chakula chochote
nyumbani?”
Mkewe akajibu:
“Hakuna chochote
isipokuwa chakula cha watoto wetu tu”.
Akasema:
“Wababaishe kwa
chochote kile, na njaa itakapowashika sana wakataka kula chakula chao cha
usiku, jaribu kuwalaza, watakapoingia wageni wetu nyumbani, zima taa, kisha
tujifanye
Wakawakaribisha, wageni wakala, na wao wakalala na njaa
Asubuhi yake alipokwenda kwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), Mtume akamwambia:
“Mwenyezi Mungu amefurahishwa na yale mliyowatendea wageni wenu usiku wa jana”.
Bukhari na Muslim
Tabia njema zilioje na nafsi njema
zilioje, kwa hakika watu hawa walikuwa na ukarimu usio na kifani.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) aliwapa sifa za aina ya pekee watu wa kabila la Al
Ash'ariy, na hili ni kabila la Sahaba maarufu Abi Musa Al Ash ary (Radhiya
Llahu anhu).
Akasema:
“Watu wa kabila la Al
Ash'ary wanapokuwa safarini sehemu za mbali kwa ajili ya kupigana Jihadi, watu
wao walioko Madina chakula cha watoto kikipungua, basi hukusanya kile
walichonacho katika kitambaa kimoja, kisha wakagawana sawa sawa baina
Bukhari na Muslim
Atakayesoma juu ya mwenendo wa
Waislam na kudurusu sira zao, akaona namna gani walivyokuwa wakikirimiana,
atatambua maana ya kauli yake Subhanahu wa taala öAliposema:
æóÇáøóÐöíäó
ÊóÈóæøóÄõæÇ ÇáÏøóÇÑó æóÇáÇíãóÇäó ãöä ÞóÈúáöåöãú íõÍöÈøõæäó ãóäú åóÇÌóÑó
Åöáóíúåöãú æáÇ íóÌöÏõæäó Ýöí ÕõÏõæÑöåöãú ÍóÇÌóÉð ãøöãøóÇ ÃõæÊõæÇ æóíõÄúËöÑõæäó
Úóáóì ÃóäÝõÓöåöãú æóáóæú ßóÇäó Èöåöãú ÎóÕóÇÕóÉñ æóãóä íõæÞó ÔõÍøó äóÝúÓöåö
ÝóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
“Na
walio na maskani zao na Imani yao kabla yao,
wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo
pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni
wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao
ndio wenye kufanikiwa."
H’ashr – 9
5
– Kuirudisha amana na kutimiza ahadi
Likiwepo kundi la watu wasiokuwa na
mwamana wala ahadi, basi watu wa aina hii hawawezi hata kidogo kuaminiana
wenyewe kwa wenyewe, na hali zao zinakuwa mfano wa wanyama. Hawajali kitu
isipokuwa kupata wanachokitaka hata kama kupata kwao
huko kutasababisha maafa kwa wenzao.
Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu ametuteremshia aya nyingi
zinazotuhimiza juu ya kuwajibika kurudisha amana za watu na
kutimiza ahadi.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú áÇó ÊóÎõæäõæÇú Çááøåó æóÇáÑøóÓõæáó æóÊóÎõæäõæÇú
ÃóãóÇäóÇÊößõãú æóÃóäÊõãú ÊóÚúáóãõæäó
“Enyi
mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na
Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.”
Al Anfal – 27
Na Akasema:
Åöäøó
Çááøåó íóÃúãõÑõßõãú Ãóä ÊõÄÏøõæÇú ÇáÃóãóÇäóÇÊö Åöáóì ÃóåúáöåóÇ
“Hakika
Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe”.
An Nisaa – 58
Na Anasema:
æóÃóæúÝõæÇú
ÈöÇáúÚóåúÏö Åöäøó ÇáúÚóåúÏó ßóÇäó ãóÓúÄõæáÇð
“Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.”
Al Israa (Bani Israil) – 34
Na Akasema:
æóÃóæúÝõæÇú
ÈöÚóåúÏö Çááøåö ÅöÐóÇ ÚóÇåóÏÊøõãú
“Na timizeni ahadi ya
Mwenyezi Mungu mnapo ahidi”.
An Nahl – 91
Na Akasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÃóæúÝõæÇú ÈöÇáúÚõÞõæÏö
“Enyi mlio amini! Timizeni ahadi.”
Al Maidah – 1
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) kaviingiza vitendo vya kusema uwongo, kuvunja ahadi na
kuikhini amana katika dalili za Unafiki.
Katika hadithi iliyosimuliwa na Abu
Huraira, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Alama za mnafiki ni tatu; Akizungumza husema uwongo,
akiahidi hatimizi na akiaminiwa hufanya khiana.”
Bukhari na Muslim
Na kutoka kwa Abdillahi bin Amru
bin Al Aas; kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Tabia nne, yeyote aliyekuwa nazo (tabia hizi) anakuwa
mnafiki halisi. Na aliyekuwa na moja kati ya tabia hizo, amekuwa na moja wapo ya tabia za
unafiki mpaka aiache (tabia hiyo); Anapoaminiwa hufanya hiana, anapozungumza
husema uwongo, anapoahidi huenda kinyume, na anapochukizwa huvuka mipaka
(katika ghadhabu).”
Bukhari na Muslim
Mwenyezi Mungu amewasifia wenye kujiepusha na ubakhili.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóãóä
íõæÞó ÔõÍøó äóÝúÓöåö ÝóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
“Na wenye kuepushwa na
ubakhili wa nafsi zao, hao ndio wenye kufaulu.”
At Taghabun – 16
Na wale waliojidanganya nafsi zao kwa
kuona kuwa katika ubakhili mna kheri, Mwenyezi Mungu anawaonya juu ya adhabu
kali inayowangojea.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
æóáÇó
íóÍúÓóÈóäøó ÇáøóÐöíäó íóÈúÎóáõæäó ÈöãóÇ ÂÊóÇåõãõ Çááøåõ ãöä ÝóÖúáöåö åõæó
ÎóíúÑðÇ áøóåõãú Èóáú åõæó ÔóÑøñ áøóåõãú ÓóíõØóæøóÞõæäó ãóÇ ÈóÎöáõæÇú Èöåö
íóæúãó ÇáúÞöíóÇãóÉö æóáöáøåö ãöíÑóÇËõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö æóÇááøåõ ÈöãóÇ
ÊóÚúãóáõæäó ÎóÈöíÑñ
“Wala
wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale
aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao (kufanya
ubakhili huko). La!, ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa
(madude ya kunasa shingoni) za yale waliyoyafanyia
ubakhili – Siku ya Kiama”.
Aali Imran – 180
Na öAkasema:
æóÇáøóÐöíäó
íóßúäöÒõæäó ÇáÐøóåóÈó æóÇáúÝöÖøóÉó æóáÇó íõäÝöÞõæäóåóÇ Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö
ÝóÈóÔøöÑúåõã ÈöÚóÐóÇÈò Ãóáöíãò. íóæúãó íõÍúãóì ÚóáóíúåóÇ Ýöí äóÇÑö Ìóåóäøóãó
ÝóÊõßúæóì ÈöåóÇ ÌöÈóÇåõåõãú æóÌõäæÈõåõãú æóÙõåõæÑõåõãú åóÜÐóÇ ãóÇ ßóäóÒúÊõãú
áÃóäÝõÓößõãú ÝóÐõæÞõæÇú ãóÇ ßõäÊõãú ÊóßúäöÒõæäó
“Na
wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii
katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.
Siku zitapo tiwa moto
katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao
na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni
mliyo kuwa mkilimbika.”
At Tawba – 34 – 35
Na ubakhili unaangamiza jamii, kwani kwa
ajili yake (ubakhili), damu nyingi zilimwagika, na heshima zilivunjwa.
Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim
kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Uogopeni ‘Jiepusheni’ na ubakhili, kwa sababu ubakhili
uliwaangamiza wale waliokuwepo kabla yenu, uliwafanya wamwage damu zao na
wakubali heshima za wanawake zao zivunjike”.
Kwa kawaida mwanadamu huipenda sana
mali yake. Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu ametuletea aya nyingi zikituelezea juu
ya thawabu pamoja na ujira mkubwa watakaoupata wale
watakaozitoa mali zao katika njia anazozipenda Mwenyezi Mungu na kuridhika
nazo.
Mwenyezi Mungu Anasema:
ãøóä
ÐóÇ ÇáøóÐöí íõÞúÑöÖõ Çááøåó ÞóÑúÖðÇ ÍóÓóäðÇ ÝóíõÖóÇÚöÝóåõ áóåõ ÃóÖúÚóÇÝðÇ
ßóËöíÑóÉð æóÇááøåõ íóÞúÈöÖõ æóíóÈúÓõØõ æóÅöáóíúåö ÊõÑúÌóÚõæäó
“Ni
nani atakeyemkatia Mwenyezi Mungu sehemu bora (ya mali
yake kwa kuwapa masikini na kutoa katika mambo mengine ya kheri) ili Mwenyezi
Mungu amzidishie mzidisho mwingi na Mwenyezi Mungu ndiye anayezuwia na ndiye
anayetowa na Kwake (nyote) mtarejeshwa.”
Al Baqarah – 245
Na Akasema:
æóÓóÇÑöÚõæÇú
Åöáóì ãóÛúÝöÑóÉò ãøöä ÑøóÈøößõãú æóÌóäøóÉò ÚóÑúÖõåóÇ ÇáÓøóãóÇæóÇÊõ æóÇáÃóÑúÖõ
ÃõÚöÏøóÊú áöáúãõÊøóÞöíäó. ÇáøóÐöíäó íõäÝöÞõæäó Ýöí ÇáÓøóÑøóÇÁ æóÇáÖøóÑøóÇÁ
æóÇáúßóÇÙöãöíäó ÇáúÛóíúÙó æóÇáúÚóÇÝöíäó Úóäö ÇáäøóÇÓö æóÇááøåõ íõÍöÈøõ
ÇáúãõÍúÓöäöíäó
“Na
yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo
ambayo upana wake ni sawa na mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu.
Ambao hutoa wanapo kuwa na
wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia
ghadhabu, na wasamehevu
kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.”
Aali Imran – 133 – 134
Na Akasema:
ÝóÃóãøóÇ
ãóä ÃóÚúØóì æóÇÊøóÞóì. æóÕóÏøóÞó ÈöÇáúÍõÓúäóì. ÝóÓóäõíóÓøöÑõåõ áöáúíõÓúÑóì
“Ama
mwenye kutoa na akamcha Mungu. Na akaliwafiki lilio jema.
Tutamsahilishia yawe mepesi.”
Al Layl – 5 – 7
Mtu hasidi ni mtu mouvu
Mtu hasidi si rahisi kupona kutokana na
maradhi yake hayo, ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akatutaka tujikinge Kwake
kutokana na shari ya hasidi anapohusudu.
Mwenyezi Mungu öAnasema:
Þõáú
ÃóÚõæÐõ ÈöÑóÈøö ÇáúÝóáóÞö 1 ãöä ÔóÑøö ãóÇ ÎóáóÞó 2 æóãöä ÔóÑøö ÛóÇÓöÞò ÅöÐóÇ
æóÞóÈó 3 æóãöä ÔóÑøö ÇáäøóÝøóÇËóÇÊö Ýöí ÇáúÚõÞóÏö 4 æóãöä ÔóÑøö ÍóÇÓöÏò ÅöÐóÇ
ÍóÓóÏó 5
1.
“Sema:
Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko,
2. Na shari ya alivyo viumba,
3.