WITO
KWA MASHIA WENYE AKILI
Shaykh Mamduuh Al-Harbiy
Imepitiwa na Kurekebishwa Kwa Kiswahili Na Muhammad Faraj Na
Muhammad Baawazir
Napenda kuzungumza katika mlango huu kuhusu maudhui
haya ninayopenda kuyaita, “Wito Kwa Mashia Wenye Akili”. Na mazungumzo
yangu ni ibara ya utata mwingi nilioupata katika madhehebu haya ya kishia, na
nimependa kuwahutubia nao hao wenye akili, hao ambao wanatafiti haki miongoni
mwa vizazi vya Mashia pengine watapata jawabu katika utata huu ambao nimeuona
umejaa katika vitabu vya Kishia. Na huo ni utata unaobainisha mgongano katika
itikadi hii, na huenda nikaifafanua kwa haraka haraka kwani ni mengi ya
kuandikwa, na nataka kutoka kwa hao wenye akili wanaofanya utafiti wa haki
wajivue na wafanye ikhilasi kwa nia zao kwa ajili ya Allaah Ta’alaa na
wachambue utata huu ikiwa ni kweli wako hivyo. Na mimi sishuku kuwa wao
wanatafuta ukweli.
Miongoni Mwa Utata Unaopingana Kwa Mashia.
Kwanza: Mashia
wanaamini kuwa ‘Aliy ni Imamu aliyehifadhiwa ‘Ma’aswuum[1],
kisha tunamwona kwa kukiri kwao wenyewe kuwa amemuozesha mwanawe wa kuzaa Umu
Kulthuum, dada wa Hasan na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamuozesha ‘Umar bin
Khatwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) Na hili limethibitika kwenye vitabu vyao
vyenye kutegemewa kwa Mashia, yaani: Kuthibitika kwa ndoa hii imeandikwa katika
kitabu cha Kulayn kinachoitwa, ‘Al-Kaafi’ katika Juzuu ya Sita Uk. 115 na vile
vile katika kitabu: “Tahdhiibul-Ahkaam” cha Tuus, na kitabu, “Al-Istibsaar”.
Vile vile na vitabu vingi vyenye kutegemewa kwa hiyo
ikiwa ‘Aliy bin Abi Twaalib na yeye ni Imamu Ma’aswuum aliye hifadhiwa
anamuozesha binti yake Umu Kulthuum dada yake Hasan na Husayn kwa ‘Umar bin
Khatab. Kwa hiyo Mashia itawalazimu moja ya mambo mawili kila utamu wa mawili
hayo ni uchungu.
Ya Mwanzo: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) sio Ma’aswuum, kwa
kuwa amemuozesha mwanawe kwa kafiri, na hii inatengua misingi ya madhehebu ya
Shia bali inaonyesha kuwa wengine miongoni mwa Maimamu sio Ma’aswuum.
Ya Pili: Inalazimika kuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab ni Muislamu
ambaye ‘Aliy ameridhia kumuozesha mwanae na kuwa mkwewe, na hili linapinga
itikadi ya Shia, kwa kumkosoa kwake na kumkufurisha ‘Umar, na jawabu hizi mbili
ndio msingi wa utata huu.
Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu
‘anhuma) walikuwa makafiri, kisha tunaona kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye
ni Imamu Ma’aswuum ameridhia ukhalifa wao, kwa hiyo hili linalazimisha kuwa sio
Ma’aswuum kwa sababu aliwabai’ (aliwapa mkono wa utii) makafiri na wala
hakuwaasi, na alikiri ukhalifa wao, na jambo hili yaani! Kukubali kuwabai hawa
makafiri wawili madhalimu – Allaah Atulinde – kuna vunja huko kuhifadhiwa – na
ndani yake ni kusaidia udhalimu (dhulma). Na hili halitokei kwa Ma’aswuum
abadani.
Ama jambo jingine:
Ni kuwa kitendo cha ‘Aliy ni kitendo cha sawa wakati alipowabai’ Abu Bakr na
‘Umar kwa kuwa makhalifa hawa wawili walikuwa waumini, wa kweli waadilifu kwa
hiyo Mashia katika
Utata Mwengine: ‘Aliy alioa wanawake wengi baada ya kifo cha
Faatwimah, na hapa tunataka tusikilize vizuri utata huu, na tunataka jawabu la
wazi toka kwa wanazuoni wa Kishia. Ninasema: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu)
alioa wanawake wengi baada ya Faatwimah na wanawake wote hao wamemzalia watoto mfano wao ni ‘Abbaas bin
‘Aliy bin Abi Twaalib, ‘Abdullaahi Bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, Jaafar bin ‘Aliy
bin Abi Twaalib, ‘Uthmaan bin Ali bin Abi Twaalib, hao wote mama yao ni mjakazi
Binti Hizaam ni Daarim. Na hili limetajwa katika kitabu, ‘Kashful-Ghummah Fil
Ma’arifatil – Aimmah’ cha ‘Aliy Al-Arbaly na huyo ni katika Maimamu wa
wanazuoni wa Kishia, na pia yuko pia katika watoto wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu) ‘Ubaydullah bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi
Twaalib na huyu nae mama yao ni Laylaa bint Masuud Daaramiyah, hili pia
amelitaja Al-Arbaly katika ‘Kashful-Ghummah’ Na pia yupo Yahya yaani: Miongoni
mwa watoto wa ‘Aliy bin Abi Twaalib na Muhammad Al-Asghar na ‘Aun bin ‘Aliy bin
Abi Twaalib na mama yao ni Asmaa binti Umaysi.
Pia yuko Ruqayyah binti Ali bin Abi Twaalib, yupo pia
‘Umar bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na ‘Umar huyu alikufa akiwa na miaka thelathini
na tano na huyu ni tumbo moja na Ruqayyah binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama
Pia yupo Ummu Hassan binti ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu) na Ramlah Al-Kubraa binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama
Utata Mwengine: Ndani ya kitabu cha ‘Nahjul-Balaaghah’ ukurasa wa
136, Na hicho ni kitabu cha kutegemewa kwa Mashia, imeandikwa kuwa ‘Aliy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa ukhalifa, akasema: “Niacheni na tafueni
Mwengine”, Imamu Ma’aswuum wa kwanza kwa Mashia anasema niacheni tafuteni
Mwengine.
Nasema: Hii
inaonyesha ubatilifu wa madhehebu ya Shia, kwa kuwa vipi anakataa ukhalifa na
huu ukhalifa ni faradhi kutoka kwa Allaah tena ya lazima kama vitabu vya Shia
vinavyodai, na vipi ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaikataa nguzo ya kwanza kwa
Mashia, nayo ni nguzo ya Uimamu? Anasema: ‘Niacheni tafuteni Mwengine?’
Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Faatwimah
(Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye ni Mtoto wa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
naye Bibi mtukufu. Mashia wanadai kuwa Bi-Faatwimah amedhalilishwa wakati wa
uongozi wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kiasi cha kuvunja mbavu yake wakati watu wakiunguza nyumba yake na
kusababisha kutoka kwa mtoto wake kabla hajazaliwa ambae alikuwa alikusudiwa
aitwe kwa jina la Al-Muhsin au Muhsin, swali tata ni kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib
alikuwa wapi Bi-Faatwimah akifanyiwa haya yote? Alikuwa wapi Simba wa Masimba?
Alikuwa wapi shujaa yule? Kwa nini hakuchukua haki ya mke wake Bi-Faatwimah (Radhiya
Allaahu ‘anha) binti wa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Hili
ni tatizo na swali muhimu lapasa kujibiwa.
Utata Mwengine. Tumepata mengi kutoka kwa wakuu wa Kiswahaba
wanaingiliana kwa kuoza na kuoa na si hivyo tu bali hata kinyume chake wameoana
na Ahlul-Bayt (‘Alayhimus Salaam) Hususan Abu Bakr na ‘Umar, na hili
limeafikiwa na wana historia na baina ya wenye kuhamisha habari kutoka kwa
Sunni na kutoka kwa Shia, kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amemuoa ‘Aaishah (Radhiya
Allaahu ‘anha).
Na vile vile amemuoa Hafswah bint ‘Umar (Radhiya
Allaahu ‘anhu) naye akamuozesha mwanawe Ruqayyah, Kisha Umu Kulthuum kwa
Khalifa wa tatu Bwana mkarimu, mwenye staha ‘Uthmaan Bin ‘Affaan (Radhiya
Allaahu ‘anhu) na kwa ajili hiyo alipewa Laqab[2] ya Dhuu Nurayn (mwenye nuru mbili).
Kisha mwanawe ‘Uthmaan bin ‘‘Affaan aitwae Abaan
alimuoa Ummu Kulthum binti ‘Abdullaah bin Jaafar bin Abi Twaalib. Kadhalika
Marwaan Bin Abaan bin ‘‘Uthmaan alimuoa Umul-Qasim bint Husayn bin ‘Aliy bin
Abi Twaalib. Kadhalika Zayd bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Salama binti
Al-Husayn na ‘Abdullaah bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Faatwimah bint Al-Husayn
bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu).
Inatutosha kutaja Makhalifa watatu (Radhiya Allaahu
‘anhum) bila ya kuwataja wengine. Swali linalojitokeza hapa ni kwa nini
kukosolewa huku kwa Makhalifa hawa watatu peke
Ama waliowaita watoto wao kwa jina la ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Maimamu
miongoni mwao ‘Aliy kama tulivyotaja punde, alimwita mwanae ‘Umar Akbar na mama
yake kama tulivyotaja ni Ummu Habiib binti Rabiiah, ‘Umar huyu aliuawa maeneo
ya Karbalaa Tuff yaani katika usiku pamoja na ndugu yake Husayn (Radhiya
Allaahu ‘anhu) wala haitajwi kabisa kuwa ‘Umar alikufa kwa kuuawa –akiwa
Shahidi – kwa Allaah, wala hatajwi katika maombolezo ya Husayniyaat wakati wa
msiba wa Husayn na wakati wa kupokea taazia (rambirambi) ambayo inaitwa rambi
rambi ya Husayn, hawamtaji ‘Umar.
Kadhalika Hasan bin ‘Aliy aliwaita wanawe majina ya
Abu Bakr na’Umar na hili lipo katika vitabu vya Shia ‘Al-Irshaad’ cha Mufiid,
ukurasa wa 194 na vile vile katika kitabu cha ‘Muntahal-Aamal’ Juzuu ya
Utata Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’
sikilizeni vizuri, nasema: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’ kuwa
Maimamu wanajua lini watakufa na kuwa wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao, na
hili limeandikwa katika ‘Usuulul- Kaafi’ cha Kulayn Juzuu ya Kwanza, ukurasa wa
258 Kulayn aliweka mlango kwa kauli yake, ‘Hakika Maimamu wanajua lini
watakufa, na wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao’.
Kisha akataja Majlisy katika kitabu chake ‘Bihaaru
Al-Anwaar’ Juzuu ya 3, ukurasa wa 364, Anasema:
“Hakika Maimamu wanajua lini watakufa. Na kuwa wao watakufa kwa hiari
Na vile vile ametaja Al-Hurul Al-’Amily, ‘Kuwa iwapo Imamu
huyu Ma’aswuum anajua ghaibu, kwa hiyo atajua kinacholetwa kwake, katika
vyakula na vinywaji, na akijua kuwa chakula au maji kina sumu atajiepusha
nacho. Na hapana budi ajiepushe nacho, na akila chakula hicho atakufa hali ya
kuwa amejiua kwa kuwa yeye kwa itikadi ya Shia, anajua kuwa chakula hiki kina
sumu akila atakuwa amejiua’. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) amesema kuwa, “Mwenye kujiua mwenyewe ni mtu wa motoni”, Je Shia
wanaridhia hili.
Kuhusu Maimamu, nyinyi mnasema kuwa: “Maimamu wanajua
ghaibu, na wanajua lini watakufa.”
Majlisy anasema: “Hawi Imamu isipokuwa amekufa kwa kuuwawa au kwa sumu.”
Kwa hiyo akiletewa chakula nae anajua kina sumu akala,
huku kutakuwa ni kumtukana Imamu huyu, kwani atahesabiwa ni punguani, na hali
ya kuwa wao wametakaswa na hili. Kwa hiyo tunataka majibu ya mushkeli huu.
Utata Mwengine: Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijiuzulu
kwa Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika wakati ambao wafuasi wakimnusuru walikuwa
wakikusanyika kwake na kuunda jeshi na neema kukusanya itakayomuwezesha
kuendeleza vita dhidi ya Mu’aawiyah katika hali hii ndugu yake Husayn alitoka
kwa ajili ya kupigana na Yazid akiwa na watu wa chache katika familia yake,
katika wakati ambao angeweza kujisalimisha. haiwezekani mmoja wao kuwa katika
haki na mwengine kuwa katika batili, kwa sababu iwapo Hasan alijiuzulu pamoja
na kuwa na nguvu na jeshi lenye kumuwezesha vita, kwa ukweli kutoka Husayn bila
nguvu akiwa dhaifu pamoja na kuweza kwake kujisalimisha, hili lilikuwa ni
batili na kosa kwake yeye Husayn kwa kuwa kama Husayn kutoka pamoja na udhaifu
wake ni haki, basi kujiuzulu Hasan pamoja na nguvu alizokuwa nazo ni batili.
Na hili linawaweka Shia katika eneo wasilohusudiwa
ndani yake, kwa kuwa wao wamesema: Hao wote Hasan na Husayn walikuwa katika
haki, kiukweli ni kwamba wao wamekusanya mambo mawili yenye kupingana na kauli
hii inavunja misingi ya Itikadi ya Shia kwani wakisema ubatili wa Hasani
italazimika mbali wa Uimamu wake na wakisema ubatilifu wa Uimamu wake italazimu
kubatilika Uimamu wa baba yake kwani ndie aliyemteua. Na yeye ndie aliemsimika
baada yake kama Shia wanavyoitakidi, na
Mushkeli Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake (Al-Kaafii) Juzuu
ya
Nikamuuliza:
“Ni kitu gani hiki kinachoitwa msahafu wa Fatima?”
Akasema:
“Msahafu, ndani yake mna mfano wa Qurani yenu hii mara tatu!
Wallahi hamna ndani yake yaliyomo ndani ya Qurani yenu hii hata herufi moja”.
Sikiliza vizuri, Imamu anaapa na kusema, ‘WaLlaah
hakuna herufi moja iliyomo kwenye Qur-aan yenu’ Nikasema: ‘WaLlaahi hii ni
elimu’ akasema, ‘Ehee, Hakika hiyo ni elimu…’
Kwa hivyo: Je Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) alikuwa anajua msahafu wa Faatwimah?
“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa
hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake.”
(5:67)
Huu ni mushkeli mkubwa Enyi ndugu zangu tunataka
jawabu.
Mushkeli Mwengine:
Katika Juzuu ya Kwanza ya kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn kuna majina ya watu
waliopokea Hadithi toka kwa Mtume zinazotegemewa na Mashia Hadithi za Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na juu ya ali zake na Swahaba zake
na amani, na wamepokea kauli za Ahlul Bayt miongoni mwao ni majina yafuatayo:
hao ni wapokezi wa kitabu, ‘Al-Kaafi’ cha Kulayn watu waliopokea Hadithi za
Shia, sikiliza vizuri majina na mnapata nini ndani yake? Mufadhal bin ‘Umar –
Ahmad bin ‘Umar Halabi, ‘Umar bin Abaan ‘Umar bin Adhiinah – ‘Umar bin
Abdil-Aziyz – Ibrahim bin ‘Umar –’Umar bin Handhalah – Musa bin ‘Umar – ‘Abbaas
bin ‘Umar na jina lililokusanya majina
yote haya ni jina la ‘Umar ni sawa sawa kama ni jina la mpokezi au jina la baba
yake.
Mushkeli ni kwa vipi hao wapokezi wataitwa kwa jina la
‘Umar nae ndie adui mkuibwa wa? Ahlul Bayt.
Mushkeli Mwengine: Allaah Anasema:
“…Na wabashirie wanaosubiri, Wale
ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye
hakika tutarejea.” (2:155-156)
na Anasema tena,
“…na wanao vumilia katika shida na
dhara na wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wajilindao.” (2:177)
Subira ni jambo kubwa imetajwa katika Nahjul
Balaaghah. Athari hii: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema baada ya kufa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimhutubia yeye (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ali anasema kwa tamshi hili, ‘Lau
usingekuwa umekata kubabaika na ukaamrisha subiri tungelia kwako maji ya Shani
nyingi’
Hili limo katika (Nahjul Balaaghah) kadhalika katika
(Al-Mustadrak) na imetajwa tena kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
‘Mwenye kupiga mapaja yake wakati wa msiba basi amali zake zimepotea’, hili
limo ndani ya kitabu “Al Khiswaal) cha Sudduuk ukurasa wa 621 na katika kitabu,
‘Wasaail Shay Twaan’.Ali ndio Imamu wa mwanzo kwa Shia ana waonya wafuasi wake
akiwaambia: Mwenye kupiga mkono wake wakati wa msiba juu ya paja lake amani yake imeanguka, na vile vile
Husain Imamu wa zama zake na Imamu wa
dunia (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamwambia dada yake Zaynab katika Karbalaa kama
alivyopokea mwenye kitabu ‘Muntahal
Al-Aamaal’ kwa lugha ya Kifursi kimefasiriwa kwa lugha ya Kiarabu kinapatikana katika juzuu ya
kwanza ukurasa wa 248.
Husayn anasema: Na yeye ni Imamu wa tatu kwa Mashia
akimuusia Dada yake Zaynab anasema: Ewe dada yangu, nakuapia kwa Allaah wajibu
wako kuhifadhi kiapo hiki, nikiuwawa basi usichane nguo zako (kwa kulia),wala
usiparure uso wako kwa kucha zako, wala usiomboleze maangamizi juu ya Shahada yangu (Kufa kwangu Shahid)
anamuapia Allaah.
Abu Jaafary Qamy amenakili: Kuwa amiri wa waumini
(‘Alayhis Salaam) amesema katika ambayo wafuasi wake walikuwa anawausiana
Hili liko katika kitabu “Man
laYahdhuruhul-faqiih” na vile vile katika kitabu, ‘Wasaail’ cha Harul
Al-Aamily, na tukihitaji kuainisha utajo wake Al-Hurul Aamiliy katika,‘Wasaail
Shiiah’ Juzuu ya pili ukurasa wa, 916
Qamy ametaja ndani ya kitabu, ‘Man laYahdhuuruhul-Faqiih’ katika Juzuu ya
kwanza ukurasa wa 232
Amiri wa waumini
anawajuza wafuasi wake na anasema: ‘Msivae nguo nyeusi kwa kuwa hiyo ni
vazi la firauni msivae nyeusi kwa kuwa ni vazi la Firauni’ na imekuja katika tafsiri Swaafy katika kutafsiri kauli yake
Taalaa: “…wala
hawatakuasi katika jambo jema…,” (60:12) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) aliwabai wanawake kuwa wasivae nguo nyeusi, wala wasichane nguo wala
wasinadi maangamivu, bali katika kitabu (Furu’ul-Kaafiy) cha Kulayn kuwa yeye
alimuusia Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) akasema: “Mimi nitakapokufa
usirarue uso, wala usiteremshe nywele wala usiniomboleze kwa maangamivu, wala
usinisImamuishie maombelezaji” yaani usilete watu watakaoniomboleza kwa kupiga
mayowe, na hili ni kama
lilivyotajwa katika
kitabu, ‘Al-Kaafii’ Juzuu ya pili ukurasa wa 528.
Na huyu Sheikh wa Shia Muhamad bin Husain bin
Babawayhi Al-Qamy aliyepewa jina la Suduuq kwa Mashia anasema: Katika matamshi
ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo hayakutanguliwa ni: “Kuomboleza (An-Niyaaha)
ni katika amali za Jahiliya” kama wanavyopokea wanazuoni wao, Majlisy An Nuury
na wanazuoni wao wengi toka kwa Mtume (Swalaah llwahu alayhi Wasallam) kuwa amesema: “Sauti mbili
zimelaaniwa Allaah anazichukia mayowe wakati wa Msiba (Yaani mayowe wakati wa
msiba) na kughani wakati wa neema”
Swali na mushkeli ambao na wauliza wenye akili wa
Mashia baada Ya riwaya zote hizi kwa nini Shia wanahalifu haki iliokuja na
wanajipiga katika kumbukumbu yao katika Husainiyaat kwa kujitoa damu na kupiga
na kuchana mifuko? Sasa tumkubali nani tuwakubali wao au tumkubali Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Ahlul Bayt wake watoharifu
(Radhiya Allaahu ‘anhum).
Utata Mwengine:
Tatbiyr: Maana
yake ni kujitoa damu kichwani kama wafanyavyo Shia katika Siku ya Ashura -
nasema: Iwapo kujitoa damu na kujipiga vifua na kuchana nguo na kujiliza kwa
sauti kuna ajira kubwa mbele ya Allaah, basi vipi Masheikh wenye kuvaa nguo
nyeusi ambao ni kizazi cha Husayn (‘Alayhis Salaam)
Utata Mwengine: Ibada haiwi isipokuwa kwa Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) kujivunja na kujinyenyekeza katika daraja za kuabudu hakuwi isipokuwa
kwa Allaah Taalaa; Allaah Anasema: “Bali Allaah muabuduni” Na hapa kuna
mushkeli, kwa nini Shia wanajiita mja wa Husayn (AbduHusayn), mja wa ‘Aliy (AbduAli),
mja wa Zahraa (Faatwimah) na mja wa lmam? Kwa nini hawakujiita hivyo Maimamu Ma’aswuum
Utata Mwengine: Alipotawazwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) hatukumuona
kutofautiana na Makhalifa waongofu kabla yake, na kuchukia uongozi, hatukumuona
akimhalifu Abu Bakr, wala ‘Umar wala ‘Uthmaan hakuwatolea watu Qur-aan zaidi ya
ile iliyokuwa kwao na hakupinga chao chochote, bali kauli zake zilikuwa nyingi
juu ya mimbari. ‘Kheri ya ummah huu baada ya Nabii wake ni Abu Bakr na ‘Umar’
hakuhalalisha Mutah wala hakurudisha fadak,
na hakuwahalalishia watu Mut-ah katika Hajj, wala hakuongeza haya njooni
katika amali ya kheri –katika adhana wala hakuondoa – Swalaah ni bora kuliko
usingizi– na kama Abu Bakr na ‘‘Umar wangekuwa makafiri walionyang’anya
ukhalifa kwa Ali kama Shia wanavyodai, kwa nini hakulibainisha hilo aliposhika
uongozi, na alikuwa na nguvu na ulinzi (Radhiya Allaahu ‘anhu)! Kwa nini
hakubainisha na alikuwa na nguvu mkononi mwake? Bali kwa ukamilifu tumemuona
akifanya kinyume cha hayo yote, aliwasifu wote wa tatu, na kawataja kwa wema
aliposema: “Bora ya ummah baada ya Mtume wake ni Abu Bakr na ‘Umar” Nawaambia
hao wenye akili, basi itoshe au itutoshe yale yaliowatosha nyinyi ‘Aliy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) pale alipowasifu wale watatu, (Radhiya Allaahu ‘anhum).
Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Mu’aawiyah alikuwa kafiri, kisha
tunamuona Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anajiuzulu ukhalifa na yeye
ni Imamu Ma’aswuum, Imamu wa pili Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma)
anajiuzulu kwa ajili ya kafiri mpinga dini, na hili ni kinyume na ‘Ismah kama mnavyodai au kuwa Mu’aawiyah (Radhiya
Allaahu ‘anhu) ni Muislamu aliyestahili muadilifu.
Mushkeli Mwengine: Ni kuhusu swali tunalolifikiria vizuri, na hiyo ni
alama ya wazi kwa Shia kwa ujumla wake – Ithnaa ‘Ashariya (Maimamu kumi na
mbili) swali linasema: Je, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alisujudia kijiwe (turbah) cha Husayn ambao Mashia wanasujudia hivi sasa? na
udongo huo unaitwa turba Karbalaa? Je Mtume alisujudia kijiwe kile?
Ikiwa wanazuoni wa Shia watasema: Ndio, tutasema: Huu
ni uongo hili halikuthibitika toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam). Leteni dalili zenu ikiwa nyinyi mnasema kweli na
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
hakusujudia kijiwe cha Husayn, basi kwanini nyinyi mnasujudia udongo kwenye
udongo wa Husayn kwa nyuso zenu? Pamoja na kujua kuwa mapokezi ya Kishia
yanataja kuwa Jibril (‘Alayhis Salaam) alikuja na kifumba cha mchanga wa
Karbalaa na imekuja katika baadhi ya athari,
kuwa ardhi hii ni ambayo au imechanganyika na damu ya Husayn, au damu yake
tohara (Radhiya Allaahu ‘anhu) imechanganyika na udongo huu, hapo alilia kama
zinavyosema riwaya, kwa hiyo kwanini basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) hakuusujudia? Je, Shia
wameongoka zaidi kuliko Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?
Utata huu unahitaji jibu.
Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Swahaba wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliritadi baada ya mauti yake (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakageuka baada Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) Swali: Je Swahaba walikuwa kabla ya mauti yake walikuwa ni
Ithnaashariah kisha wakabadilika kuwa Sunnah iliyosImamuishwa?”Au wao kabla ya
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa Ahlu Sunnah? Kisha
wakabadilika kuwa Shia Ithnaashariah? Kwa kuwa kubadilika ni kutoka hali moja
hadi nyingine tunataka jibu kwenye swali hili.
Walikuwa Waislamu kisha wakaritadi wakageuka
wakabadilika kama zisemavyo riwaya za Shia, kuanzia zama za Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je Swahaba walikuwa Shia Ithna ‘Ashariyah,
kisha baada yake wakabadilika kuwa ahlu Sunnah au walikuwa ahlu Sunnah na juu
ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakati huo
ushia ulikuwa bado haujafahamika na kujitokeza? Tunataka jawabu katika hili.
Utata Mwengine: Inajulikana kuwa Hasan (Radhiya Allaahu ‘anhu) yeye
ni mtoto wa ‘Aliy na mama yake ni mwema Mtukufu Bi-Faatwimah (Radhiya Allaahu
‘anha) Na yeye ni miongoni mwa watu waliofunikwa (nguo) ya Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Shia na yeye vile vile ni katika Maimamu
Ma’aswuum Shani yake katika hilo ni shani ya ndugu yake Husayn (Radhiya Allaahu
‘anhu). Hapa kuna utata ambao tunataka utatuliwe: Kwa nini Uimamu umekatwa au
kuzuiwa kwa watoto wa Hussan na ukaendelea kwa watoto wa Husayn? Baba yao ni
mmoja mama yao mmoja na wote hao ni Mabwana, mabwana wa watoto wa vijana wa
peponi, bali Hasan anamzidi Husayn katika jambo moja yeye amemzidi Husayn umri,
na yeye ndiye mtoto wa kwanza kwa baba yake, kwa nini umekatwa na kuzuiwa kwa
watoto wa Hasani nakuwekwa kwa watoto wa
Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Utata huu unahitaji majibu na ufafanuzi na
uchambuzi wa kielimu.
Utata Mwengine: Kwa nini ‘Aliy hakuswalisha Swalaah japo moja katika
maradhi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amekufa
ndani yake ikiwa yeye ni Imamu wa baada yake
Utata Mwengine: Nyinyi mnasema: Sababu ya kupotea Imamu wenu wa
kumi na mbili nae ni Muhamad bin Hasan
Askary katika Saradib ni hofu ya dhulma, kama ilivyokuja katika riwaya zenu
nyingi khofu ya dhulma basi kwa nini kupotea huku kunaendelea pamoja na
kutoweka hofu hii, kwa kuwepo dola za Kishia kutawala kwa mujibu wa historia?
Kama Dola Al-‘Abidiyiin Fatimiyah, Buwayhiiyiina, Swafin na mwisho ile dola ya
Irani ya sasa ambayo nayo ina mitambo ya nyukilia, kwa nini asitoke hivi sasa?
Na nyie mnasema ikiwa yeye hakujificha isipokuwa kwa hofu ya madhalimu na
mashambulizi ya majabari, na zimekwishawahi kusImamua Dola za kishia jabari
zenye nguvu, kwa nini asitoke sasa na
kuna shia wenye nguvu wa kuweza kumnusuru, na kumlinda katika dola zao”?
Utata Mwengine: Kulayn ameandika mlango maalumu katika, ‘Al-Kaafii’
kwa anuani! “Hakika wanawake hawarithi chochote katika ardhi” Imepokewa ndani
yake toka kwa Abu Jaafar amesema: “Wanawake hawarithi chochote ardhini wala
katika ‘Iqari kitu chochote.” Hili ni katika juzuu ya Suba ukurasa wa 127
katika kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn.
Tunsi katika, ‘Tahdhib’ katika juzuu ya tisa ukurasa
wa 254 toka kwa Maysarah kauli yake! Nilimuuliza Abu Abdillaah (a.s) kuhusu
wanawake, nini haki
Toka kwa Muhamad bin Muslim toka kwa Abu Jaafar
amesema, “Wanawake hawarithi ardhi wala katika ekari”.
Na kutoka kwa Abdul Malik bin A’ayun toka kwa mmoja
wao (‘Alayhis Salaam) yaani – mmoja wa Maimamu Ma’aswuum kwa Mashia –
amesema:wanawake hawana chochote katika (“Ad-Dar wal ‘Iqaar” Nyumba
na mali isiyohamishika kama vile ardhi na mashamba nk.)” katika riwaya hii hakuna uhusisho au
kufunga, si kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) wala kwa Mwengine, juu yahili
haistahiki kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) kudai urithi wa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa riwaya ya Shia kwa kuwa Shia
wanamkosoa Abu Bakr wanasema: kuwa yeye alinyang’anya urithi wa Fadak, au anachomiliki Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika
mirathi yake katika Fadak pia kila lililokuwa la Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) hilo ni la Imamu zingatia kuwa imekuja katika
riwaya za Kishia kutoka kwa Muhamad bin Yahya toka kwa Ahmad bin Muhammad toka
kwa Amri bin Shammar toka kwa Jabir.
Toka kwa Jaabir kuwa Abu Jaafar (‘Alayhis Salaam)
amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah
amemuumba Adamu akamkatia kipande cha dunia kwa hivyo lililokuwa la Adam
(‘Alayhis Salaam) ni la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na
lililokuwa la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni la Maimamu
katika kizazi cha Muhammad.” Na hili pia liko katika ‘Usuulul Kaafi’ cha Kulayn
‘Kitabul Hujuh’ mlango kuwa ardhi yote ni ya Imamu (‘Alayhis Salaam) Juzuu
ukurasa wa 476.
Imamu wa kwanza baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa Shia ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa
hiyo mwenye haki ya kudai ardhi ya Fadak
ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu)
na sio Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) na hatukumuoa ‘Aliy akifanya
Utata Mwengine: Ahlu Sunnah na Shia walikubaliana pamoja na tofauti
Nasema: Hapa kuna utata! Je ushujaa wa
‘Aliy ulikoma baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
mpaka ambai Abu Bakr kisha ambai baada yake ‘Umar kisha baada yake ‘Uthmaan bin
Afaan, (Radhiya Allaahu ‘anhu) Je alishindwa japo mara moja katika minbari na
akaogopa kupanda japo mara moja na kusema kuwa ukhalifa umeporwa kwake yeye, na
kuwa yeye ndie mwenye haki, kwa nini hakufanya hivyo? Na yeye ndie wasii wa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwanini hakudai haki
yake?. Na yeye ndie yule shujaa ajulikanae na yeye alikuwa na wafuasi wengi wa
kumnusuru wanaompenda, ambao watajazana pembeni yake la angelisema katika
mimbari ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? kwa nini
hakufanya hili (Radhiya Allaahu ‘anhu)?
Utata Mwengine? Hadithi ya Kisaai (shuka iliyowafunika watu wanne
katika familia ya ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwasifu kwao kwa utoharifu.
Wanne hao ni ‘Aliy, Faatwimah, Hasan na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhum) wote. Swali,
ni ipi dalili ya kuwaingiza wengine katika utoharifu wa uhifadhi (‘Ismah) ikiwa
Hadithi ya Mtume iko wazi kwa kuwa toharisha hao wanne, katika nyumba ya Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu)
Faatwimah, Hasan, na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) wote? Basi ni ipi dalili ya
kuwaingiza wengine katika utoharifu na Ismah na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) hakuweka wazi isipokuwa katika hao wanne tu? Hili ni
tatizo, tunataka jibu lake.
Utata Mwengine: Shia wanapokea toka kwa Imamu Jaafari As-Swadiq
(Radhiya Allaahu ‘anhu) nae ndio Muasisi wa madhehebu ya Jaafariyah kwa mujibu
wa itikadi
Maneno haya yanaweza kutoka kwa mtu mjinga lakini
hayawezi kutamkwa na Imamu ambaye Shia wanamzingatia kuwa msomi zaidi katika
wakati wake. Kwa hiyo tunataka mkajibu juu ya mushkeli huu.
Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu)
anamchukia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wanazuoni wa Kishia wanadai katika
Husayniyaat zao, kongamano na vikao vyao wanasema kuwa: ‘Umar (Radhiya Allaahu
‘anhu) anamchukia ‘Aliy chuki kubwa mno, pamoja na hili tunapata kuwa ‘Umar
(Radhiya Allaahu ‘anhu) anatawalisha ‘Aliy Madiynah wakati alipotoka kupokaa
funguo za Baytil Maqdis. Vipi yatakuwa haya? ‘Umar anamchukia ‘Aliy wala
hampendi, na alipotoka ‘Umar kupokea funguo za Baytil Maqdis alimtawalisha Madiynah,
naye ni ‘Aliy bin Abi Twaalib ambae hampendi na anamchukia
Utata Mwengine:
Sikilizeni vizuri enyi Mashia wenye akili. Wanazuoni wa Shia wanaona kuwa
viungo vya Swalaah ni vinane, paji la uso, pua, viganja viwili, magoti mawili,
nyayo mbili, na viungo hivi vinapasa kugusa ardhi katika hali ya kusujudu na
haya yametajwa katika kitabu cha, ‘Wasaail Shiah’ cha Hurul Al-Aamily Juzuu 3
ukurasa wa 598, kadhalika wanasema uwajibu wa kusujudu juu ya kisicholiwa wala
kuvaliwa, kwa ajili hii wanaweka Turbah chini ya maji ya nyuso zao, chini ya
kiungo kimoja katika viungo hivi nane. Swali: Kwa nini Shia hawaweki Turbah iliyochanganywa
na damu tukufu ya Husayn chini ya viungo nyote vya kusujudu? Kwa nini
wameukhusisha uso peke yake katika kusujudia udongo huu wa Karbalai?
Na hali yakuwa nyinyi mmeamrishwa kusujudu juu ya
viungo vyote vinane, paji la uso, pua viganja, nyao, na magoti. Kwa nini uso tu
mlio wameukhusisha na huu udongo wa Husayn Karbalaai? Na hakuna dalili ya
kuhusisha? Huku ni kupingana! Na utata
huu tunataka jawabu.
Imekuja katika baadhi ya riwaya za mushkeli Mwengine
mfano wa kitabu (Al-Ghiibah) katika kitabu,
‘Al-Ghibah’ cha At-Tuusi: Kuwa Shia –wanadai katika baadhi ya riwaya kuwa Mahdi
wao wa kumi na mbili ni Muhammad bin Hasan Al-Askari atakapo tokea katika
Sirdaab yake Akhir Zamaan (Mwisho wa zama) hakika huyo atahukumu kwa hukumu ya
watu wa Dawuud.
Utata: Iko
wapi shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yenye
kufuta sheria zote zilizotangulia? Kwa nini anahukumu kwa sheria ya watu wa
Daudi? Na shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iko
wapi?
Utata Mwengine: Sikilizeni vizuri, Shia wanaitikadi kuwa Maimamu
wanabebwa na mama zao katika mbavu zao na kuzaliwa kwa mapaja
Utata Mwengine: Shia wamepokea kuwa Abu AbdiIlaah Jaafar Swaadiq
amesema: Mwenye jambo hii ni mtu hamwiti kwa jina lake isipokuwa Kafiri na hili liko katika “Al-Anwaar An-Nuumaniyah’
na imepokewa kwa Abu Muhammad Hasan Al-Askary kuwa amesema kwa mama yake Mahdi:
“Utabeba mimba ya mtoto wa kiume, na jina lake Muhamad yeye atasImamua baada
yangu” Je, huu sio mvutano hili
limetajwa katika, ‘Al-Anwaar An-Nuumaaniyah’ ukurasa wa 55 Juzuu ya Pili yaani
baada ya kurasa mbili za hadithi ya kwanza, kwa kuwa Hadithi ya kwanza ipo
Juzuu ya Pili ukurasa wa 53. Na hivi sasa katika riwaya ya kwanza Abu Abdillah
Jaafar Swaadiq anasema: Mwenye jambo hili ni mtu hamwiti kwa jina lake
isipokuwa Kafiri.Yaani: Hatataja jina
Utata Mwengine: Na
swali jingine, lau mtu anataka kuwa Shia, Lau mimi nataka kuwa Shia hivi sasa
ni madhehebu gani ambayo nitayafuata, au ni madhehebu yepi ninanayopaswa
kuyafuata kati ya madhehebu mengi ya Kishia? Baina ya Imamuia Ismailiyah, kwa
tofauti zao nyingi; Ismailiya Arkani au Ismailiya Mukarima au baina ya
Ismailiya Buhrah na Ismailiya Nasiiriyah, au baina ya ‘Alawiya na Zaidiyah, au
baina ya Duruuz, na makundi mengi ya Kishia. Kwa hiyo ni kundi lipi la Shia
ninaloweza kulifuata, na kuliamini kwani yote yanajinasibisha kwa watu wa Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na wote wanakubali Uimamu wa
‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na wote ni adui wa Swahaba na wote wanaitakidi Uimamu
wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwa yeye ni nguzo na kuwa yeye ni khalifa
baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila mwanya wowote ule, na kuwa pamoja nao
wana asili ya dini na wanasifu Maimamu kwa hiyo ni madhehebu gani nitakayoyafuata? Imamuiyah
Ithnaashariah? Au Ismailiya kwa aina zake au Naswiiriya Alawiyah? Au Duruuz
katika baki ya Fatimiyah? Haya yanahitaji ithbaati.
Utata Mwengine: Wakati Shia wanapotaka kuthibitisha Uimamu wa
Ithnaashariyah wao wanatoa dalili ya Hadithi ya Kisaai ambayo Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja watu wanne tu swali: Faatwimah
ametajwa kwa Hadithi Sahihi kwa uwazi kwanini amewekwa mbali na Uimamu na wala
hatajwi katika Maimamu wa kishia? Hao wametajwa amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) ‘Aliy na Faatwimah Hasan, Husayn kwanini mmemtoa Faatwimah
katika Maimamu kumi na mbili? Huu ni mushkeli unataka jawabu.
Utata Mwengine: Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) hakupiga makofi alipokufa mwanae Ibrahimu? Kwa nini hakujipiga
Utata Mwengine: Shia wanaitakidi kuwa Swahaba wengi walikuwa
makafiri na wanafiki walioritadi
isipokuwa wachache, na hili wanalolisema wengi wa katika wanazuoni wa kishia (Al-Mu’amamiyn
– wenye vilemba), katika itikadi zao, na Mashia wenye akili wanakiri haya yote,
ikiwa Swahaba waliriadi isipokuwa wachache mno miongoni mwao kuna waliokuwa wanafiki na baada ya
mauti ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa watu saba
tu, kwa sababu katika vitabu vya Shia kikiwemo
cha Kulayni kuwa Swahaba waliritadi isipokuwa saba kwa hiyo waumini ni
saba au kwa uchache wa hali ni wachache mno, kwa hiyo basi kwa nini basi hao
walioritadi wasiwavamie na kuwashambulie hao wachache wanyonge, na kuwauwa
wote? Na kwa nini basi hali haikurudi kwenye ukafiri na ujahiliya
Utata Mwengine: Shia wanasema: Kulia juu ya Husayn ni Sunnah. Je,
kulia huku kumejengwa juu ya dalili au hawaa (matamanio ya nafsi)? Ikiwa ni kwa
dalili basi iko wapi dalili hiyo? Hili jambo moja, iko wapi hiyo dalili
inayojuzisha kumlilia Husayn tukijua Husayn alimuusia dada yake asimlilie kwa
kupasua nguo wala asijipige wakati Husayn atakapokufa. Dalili hiyo iko wapi?
Kisha mbona hajafanya hivyo yeyote miongoni mwa Maimamu wa Ahlul Bayt ambao
mnadai kuwa mnawafuata na mnaenda juu ya uongofu wao, tunataka jawabu.
Utata Mwengine: Shia wanaamini kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni
bora kuliko mwanae Husayn, na iwapo hali iko hivyo ni kwa nini hamumlilii kwa
kukumbuka mauaji yake kama ambavyo mnalia kwa Husayn, nae aliyeuawa kama
alivyouwawa Husein kwa nini
hamlii kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mkajitoa
damu mkajipa na kutoa rambi rambi kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam)? Na yeye ni mtukufu wa
wote? Na yeye ameuwawa kwa kupewa sumu na Mayahudi. Kwa nini msiba wenu huu
mnauita Husayniyaati kwa nini msiunasibishe kwa Imamu wenu wa kwanza ‘Aliy na
ukaitwa, ‘Alawiyaati au Muhammad ukaitwa, ‘Muhamadiyaati’ kwa nini
mnaunasibisha kwa Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Kwa nini hamfanyi Husayniyati
aina nyingi au sehemu za kupokea rambi rambi,
Utata Mwengine: Iwapo Uimamu wa ‘Aliy ni Uimamu wa wanawe baada yake
nguzo ambayo haikamiliki imani ila kwa imani hiyo. Na aliyeamini hivyo
amekufuru na anastahiki Jahanamu, kama
Wakati ambao tunaiona Qur-aan Tukufu kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
mengine ameyaweka wazi katika nguzo na wajibu ambao huo sio Uimamu kwa Mashia,
kama Swalaah Zakaah, Swawm na Hajj, bali (Subhaanahu wa Ta’ala) ameweka wazi katika Qur-aan baadhi ya Mubahaat
(yaliyoruhusiwa), kama kuwinda kwa mfano kwa hiyo iko wapi nguzo kubwa? Uko
wapi uzito mkubwa? Na huo ni Uimamu kwa nini haujaletwa wazi katika Qur-aan?
Ikiwa ni kwa kiwango hiki cha utukufu. Na umuhimu wake mkubwa katika dini ya
Allaah. Tunataka jawabu juu ya hili.
Utata Mwengine: Shia wanaitakidi kuwa Qur-aan imeondolewa baadhi ya Aayah
na imebadilishwa baadhi ya Aayah wakati wa Abu Bakr na ‘Umar. Wanapokea kwa Abu
Jaafar kuwa aliambiwa: Kwa nini ‘Aliy aliitwa Amirul Muumiinina? Alijibu:
Allaah ndio aliomwita na hivi ndivyo alivyoshusha katika kitabu chake,
“Na pale Mola wako Alipowaleta katika wanaadamu
kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao,
akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Na ya kuwa Muhammad ni Mtume wangu na ‘Aliy ni Amiri wa Waumini” Hili ni limo
katika usuul Al-Kaafii” (1:412)
Kulayn anasema katika tafsiri yake ya Ayah, “Basi wale walio muamini yeye” (7:157) yaani: Maimamu,
“na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa
pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa. ” (7:157) yaani! ambao wamejiepusha masanamu kuyaabudu
hii ni kauli ya Kulayni, kisha anasema Jibti na Twaghuti ni fulani na fulani.
Hili limo ndani ya Al-Kaafii ukurasa wa 429 Angalia katika
kitabu cha Al-Kaafii hakutaja majina ya haya Matwaghuti mawili kwa sababu Al-Kulayn,
(mwandishi wa kitabu hicho) alikuwa wakati wa udhaifu na unyonge; yeye ni
Muhamad bin Yakub Al-Kulayni akasema – fulani na fulani wakati ambapo
Al-Majlisiy Sheikh wa dola ya Swafawiyah katika wakati wa nguvu na ulinzi
alisema katika kitabu chake, “Bihaar-ul-Anwaar’ Juzuu 23 ukurasa wa 306,
‘Muradi wa Fulani na Fulani ni Abu Bakr na ‘Umar. Na hivi ndivyo Al-Majlisiy
alivyoona kuwa ‘Umar na Abu Bakr ni mashetani, Allaah atukinge. Imekuja kaika
tafsiri yake kwa kauli yake Taalaa:
“Wala msifuate
nyayo za Shetani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.” (2:168)
wamesema: Hatua za shetani WaLlaahi ni utawala wa
fulani na fulani. Na imepokewa kuwa Abu ‘Abdillaahi amesema:
“Na mwenye kumtii Allaah na Mtume wake katika utawala
wa ‘Aliy hakika huyo amefuzu kufuzu kukubwa”
Amesema: Hivi ndivyo ilivyoshuka, hili limo ndani ya
“Usuul-ul-Kaafi” Juzuu ya
Kadhalika imepokewa kwa Abu ‘Abdillaahi (‘Alayhis
Salaam) amesema: Jibrili ameshuka kwa Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) na ali zake kwa aya hizi,
“Enyi mliopewa kitabu aminini yaliyoteremshwa kwa
‘Aliy ni nuru ilio wazi” angalia vizuri “kwa Ali nuru ya wazi” hili limo ndani ya “Usuulul Kaafi” Juzuu ya
Athari na Hadithi ni nyingi katika kuwatusi Mashaykh
wawili na kuwa wao walipondoa na waliibadilisha kitabu cha Allaah. Hapa kuna
swali au mushkeli kwa Mashia, mimi nalipeleka kwa Mashia wenye akili ili
watafiti ndani yake. Ikiwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhum)
wamepondoa Kitabu cha Allaah katika Aayah hizi, basi kwanini ‘Aliy (Radhiya
Allaahu ‘anhu) hakuzinyoosha baada ya kuwa Khalifa wa Waislamu kwa kuweka wazi
jambo hili. Kwa nini hakusema wakati wa ukhalifa wake na nguvu zake, na baada
ya kufa Abu Bakr na ‘‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa nini hakusema: Abu Bakr
na ‘Umar wamepondoa na kuibadilisha Quran hii, na usawa ni kadha wa kadha
katika dini ya Allaah Taalaa?
Kwanini hakuzirudisha Aayah hizi katika Qur-aan
Utata Mwengine: Abul Faraj Al-Asfahany ametaja katika “Maqaatil
Twaalibiyn” ukurasa wa 88, 142 na 188 chapa ya Beiruti na Al-Arbaly pia
imetajwa hivyo katika ‘Kaashiful-Ghummah’ Juzuu 2 ukurasa wa 66 na Majlisy
katika, Jalaa-ul-Uyuun ukurasa wa 582 kuwa Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi Twaalib
alikuwa ni miongoni mwa waliouawa katika Karbalaa angalia vizuri hao watatu ni
wanazuoni wa Kishia wametaja katika vitabu vyao kuwa Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi
Twaalib ni miongoni mwa waliouwawa katika Karbalaa pamoja na ndugu yake Husayn
(Radhiya Allaahu ‘anhu) na vile vile ameuawa pamoja na mtoto wa Husayn bin
‘Aliy ambae jina lake ni Muhamad Al-Asghar aliyekuwa maarufu kwa kun-ya Abu
Bakr wote hao waliuawa pamoja na Husayn.
Utata na Swali: Kwa nini Shia wanaficha jambo hili kwa wafuasi wao?
Kwa nini Shia wanazuoni wao wanaficha jambo hili kwa wafuasi wao wala hawatilii
mkazo isipokuwa kifo cha Husayn? Je ni kwa kuwa majina
Utata Mwengine: Ilikuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) kuna watu wanaomuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) mara moja katika maisha yao, kisha wanaenda kwenye miji yao,
na hili limepokewa kwa njia mutawaatir katika vitabu vya Ahlu Sunnah na Shia
anakuja Swahaba au mtu anamwona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) mara moja kisha anarudi wala hamuoni tena baada ya hapo, na hao ambao
hawakumuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka akafa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara au akafa yeye hao
hawakusikia uongozi wa ‘Aliy wala wanawe na wajukuu zake mimi nauliza! Je
Uislamu wao ni pungufu. Wanazuoni wa Shia wakisema: Ndio tunawaambia: Lau ni
hivyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angestahiki zaidi
kusahihisha Uislamu wao, na angewabainishia
jambo la Uimamu katika kikao cha kwanza ili wasije wakafa na hali ya
kuwa wao wameacha nguzo ya Imamuah, hiyo nguzo kubwa, haifai kwa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
afiche nguzo hii muhimu na hali ya kuwa anajua huyu yu mchungaji au huyo ‘bedui’ atarudi kwenye miji yao na
hatarudi tena kabisa, hatujamuona Mtume akifanya hivyo, na hili linathibitisha
na kuonyesha kuwa Immah sio nguzo katika nguzo za dini hii.
Utata Mwengine: Ulamaa wa Shia hawawezi, na mimi siongei na Shia wa
kawaida, kwa kuwa Shia wa kawaida ni watu wenye kufuata tu na miongoni mwao
kuna wengi wenye ikhlasi na ukweli na mimi ninapoelekeza maneno yangu
nayaelekeza kwa wajuzi wanaowaathiri watu wa kawaida nasema: Shia (wanazuoni)
hawawezi kukataa kuwa Abu Bakr ‘Umar, ‘Uthmaan, walimbai’ Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti na kuwa Allaah Taalaa ameeleza katika
Qur-aan kuwa amewaridhia na amejua yalio nyoyoni mwao kadhalika. Allaah
Anasema,
“Kwa hakika
Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na
alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa
kwa Ushindi wa karibu.” (48:18)
Kwa hiyo Allaah anawaridhia hata hao watatu, na amejua
yalio nyoyoni mwao miongoni mwa imani, tauhidi na ukweli na usafi na basi vipi
itafaa kwa wanazuoni wa Kishia baada ya hapo, kukufuru habari ya Allaah
alioitoa katika Qur-aan, na kudai kinyume chake ni kama kwamba wanasema, Ewe,
Mola wewe hujui kitu kutoka kwao kama tujuavyo sisi, sisi tunajua kuwa wao ni
Wazandiki na tunajua ya kuwa wamebadilisha dini, tunajua ya kwamba wamepotosha
dini hii, nawe hujui haya yote’ Allaah atukinge na hili na huu ni mushkeli
unaotaka majibu.
Utata Mwengine: Mara nyingi mara kwa mara wanazuoni wa Kishia
wamekuwa wakitaja katika kueleza mauaji ya Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa
amekufa akiwa na kiu kikali, katika vita na imekuja katika baadhi ya riwaya
kwamba alikuwa akisema, “Enyi Shia wangu kila mnywapo maji ni kumbukeni kwa
kila mnywapo maji ni kumbukeni” na kwa ajili hiyo utaona Shia wanaandika katika
mabirika na mafriji ya maji ibara ifuatayo: “Kunywa maji na kumbuka kiu cha
Husayn” Haya ni maneno mazuri.”
Swali na Mushkeli kwa wakati huo huo, madamu Maimamu
kwa mujibu wa ufahamu wa Shia wanajua ghaibu, je
Utata Mwengine: Dini ya Uislamu ilikamilika wakati wa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kauli yake Taalaa: “Leo nimekukamiliishieni Dini yenu.” (5:3) Na
madhehebu ya Shia yamedhihirika baada ya kufa Mtume (Radhiya Allaahu ‘anhu)
tunataka jawabu sahihi la kielimu na uthibitisho wa kielimu juu ya jambo hili
Allaah Anasema, “Leo
nimekukamiliishieni Dini yenu” (5:3)
na madhehebu ya shia ilisImamua baada ya kutawafu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) Je, tutatatuaje tatizo hili?
Utata Mwengine: Ikiwa ‘Aliy na wanawe wana miujiza hiyo ambayo
inapokewa katika vitabu vya Shia kuwa miujiza hiyo inawanufaisha na hata sasa
inawanufaisha na wao hata kama wamekufa kama wanavyodai kuwa wao wana miujiza,
‘Aliy bin Abi Twaalib Husayn na Hasan, na hao wanawanufaisha watu na wako
katika makaburi yao, swali: Kwa nini hawakujinufaisha wenyewe na miujiza hiyo
wakiwa hai, Tumemuona ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) Ukhalifa wake haukutulia
kisha akafa kwa kuuwawa, tumemuona Hasan
kadhalika amelazimika kujiuzulu Ukhalifa kwa Mu’aawiyah Mzandiki mkubwa
kwa Shia? Na ambae Mashia wengi wanamwona kuwa ni shetani, kwanini alijiuzulu
kwa ajili yake Mu’aawiyah?
Utata Mwengine: vipi Mtume atazikwa mbele ya Abu Bakr na ‘Umar na
kwa mtazamo wa Shia ni makafiri na
Muislamu hazikwi mbele ya kafiri hili
lilikuwaje?
Vipi atazikwa Mtukufu zaidi wa viumbe wa Allaah na
mbora aliyekanyaga kwa nyayo zake ardhi Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) azikwe mbele ya makafiri? Hili likoje? Vipi liwe kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) Na kwa nini Allaah hakumhifadhi katika ujirani wa makafiri
katika mauti yake (s.a.w.) ? Kwa nini
hakumlinda kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Kwanini
hakumhifadhi kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuzikwa
na makafiri? Kisha alikuwa wapi ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) simba wa masimba
kwenye hayo yote? Kwanini hakuzuia jambo hili kubwa na kuzuia kuzikwa na
kupigana kwa ajili yake? Muhamad (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anazikwa baina ya makafiri wapinzani
waliopondoa na kubadilisha sheria na wakaondoa Qur-aan na wakaritadi baada ya
mauti ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Vipi ‘Aliy (Radhiya
Allaahu ‘anhu) anyamaze kwenye hili?
Huu ni utata unahitaji dalili na ufafanuzi wa uwazi.
Utata Mwengine: Wanazuoni wa Kishia wanadai kuwa andiko kuhusu Uimamu
wa ‘Aliy na ustahiki wa Uimamu wake limethibitika katika Qur-aan. Lakini Swahaba
walificha. Kauli hii iko katika riwaya nyingi za Shia, kuwa Uimamu wa ‘Aliy (Radhiya
Allaahu ‘anhu) na ukhalifa wake umethibitika katika Qur-aan Tukufu isipokuwa swahaba
wameficha na kunyamazia. Madai hayo ni batili, kwa kuwa sisi hatukuwaona
Maswahaba wakificha Hadithi inayothibitisha na Shia juu ya Uimamu wa ‘Aliy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) mfano wa Hadithi, “Wewe kwangu ni kama daraja la Haruna
kwa Musa” (Muslimu 4418) Na nyingine miongoni mwa Hadithi
zinazofanana na hayo kwa nini Maswahaba hawakuficha Hadithi hii, kama
walivyoficha jina la ‘Aliy katika Qur-aan Tukufu. Na dalili iko katika kitabu
cha Allaah Taalaa? Hili linahitaji ufafanuzi kwa vile ni utata (mushkeli).
Utata Mwengine: Kwa kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhum.)
wamefanikiwa katika majaribio ya kikhabithi
Utata Mwengine: Shia wanapokea toka kwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu) kuwa alipotoka kwa Swahaba zake
akiwa na huzuni anapojua alisema: “Nyie
vipi mko katika zama ambazo ndani yake mipaka inakiukwa, na mali inafanywa
mpokezano na mawalii wa Allaah
wanafanyiwa uadui na wanatawalishwa ndani yake adui wa Allaah? Wakasema: ewe,
Amiri wa waumini, vipi tukizikuta zama hiyo tufanyeje? ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu.) alisema: kuweni
Hili limo ndani ya kitabu “Nahjus Saadah” Juzuu ya 2
Swali Na Mushkeli:
Taqiyah ya Shia iko wapi hapa? Kwanini ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) Imamu Ma’aswuum
kwa Shia ana waamuru wafuasi wake wasubiri hata wakichomwa kwa msumeno na
kusulubiwa juu ya mbao, kisha anasema: Mauti juu ya utii ni bora kuliko uhai juu
ya uasi. Iko wapi Taqiyah hapa wanayoinadi Shia?
Utata Mwengine: Ni nani ambae
alimlazimisha Abu Bakr katika kusuhubiana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) katika Hijra yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam)? Lau angekuwa mnafiki kama wasemavyo
Shia kuhusu Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa nini akimbie watu wake makafiri na wao
wana nguvu katika Makkah?
Na iwapo ni masilahi ya kiduiia kwa kuwa hao (Shia)
mara nyingine anasema:Hakutoka isipokuwa Masilahi ya kidunia, tunawaambia: Ni
maslahi gani aliokuwa akiyatarajia Abu Bakr pamoja na Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika saa
ile?
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alitoka peke yake akiogopa? Pamoja na kuwa anaweza kujipeleka kwenye kifo
kutokana na makafiri ambao hawakumsadiki? Hili linahitaji ushahidi wa kutosha
wa kumtuhumu Abu Bakr kuwa hakutoka isipokuwa unafiki. Ni jambo gani la
kumtuhumu na kumlazimisha kutoka na asibakie pamoja na familia yake, wanawe,
shangazi zake, miongoni mwa makafiri katika Makkah? Mnasema kuwa hakutoka
isipokuwa kwa masilahi ya kidunia, Ni masilahi gani hayo ya kidunia aliyokuwa
akitaka, kwa ajili yake pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam)? Hakuna masilahi ya dhahiri ya kidunia.
Utata Mwengine: Swali jingine
ikiwa Swahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliritadi baada ya mauti ya Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi kwa nini walipigana na
walioridadi katika wafuasi wa Musaulamah al-Kadh-dhaab na wafuasi wa Tulayha
bin Khuwaylid na wafuasi wa Al-Aswad ‘Insy na wafuasi wa Sajaah na wengine na
wakawarudisha kwenye Uislamu. Kwa nini hawakuwanusuru hao wapingaji ambao
walidai Utume katika wakati huo madamu ni mfano wao wameritadi
Utata Mwengine: Tumemuona ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuwakufurisha
mahasimu wake, hata wale Khawaarij ambao walimpiga vita na kumuudhi na
kumkufurisha ‘Aliy hakuwakuwafurisha wao. Kwa nini basi Shia hawamuigi ‘Aliy na
wao ndio ambao wanawakufurisha wabora wa Swahaba wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam)?
Shia wanawakufurisha viumbe bora wa Allaah baada ya
Mitume nao ni Swahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Utata Mwengine: ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa kwa
makubaliano ya watu wa Sunnah na Shia akishauriana na ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu) katika mambo mengi na hili lipo ndani ya
‘Nahjul Balaaghah’ ukurasa wa 325 na 340 uhakiki wa Subhi Swaalih! Lau
‘Umar angekuwa dhalimu
Utata Mwengine: Imethibitika kwa makubaliano kuwa Salmaan Farsiy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa Amiri wa Madaain katika wakati wa Ukhalifa wa
‘Umar na vile vile Amaar bin Yaasir alikuwa Amiri wa Kufah katika ukhalifa wa
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Shia wanadai kuwa Salmaan Farisy na Amaar bin
Yaasir walikuwa wanusuru wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na walikuwa ni katika
kundi lake, na kama ‘Umar kwao angekuwa Murtad, dhalimu jeuri dhidi ya ‘Aliy
kwanini Salmaan alikubali na kwa nini Amaar alikubali, kwa nini walikubali kuwa
maamiri katika ukhalifa wa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Kwa
nini Anmaar aliafikianakuwa Amiri wa Kufah? Na kwa nini Salmaan alikubali kuwa
Amiri wa Madaain? Je inafaa kwao kumsaidia dhalimu na Murtadi na Allaah
Anasema: “wala msiwasaidie ambao wamedhulumu” Huu ni mushkeli tunataka
jawabu.
Mushkeli Mwengine: Kuna swali liliulizwa kwa mmoja wa Shia sikilizeni
vizuri, “Enyi Shia wenye akili, enyi mnaotafuata ukweli. Enyi mnaotarajia kuwa
ni wapokezi wa bendera ya Mtume (Swalaah Allaahu ‘alayhi Wasallam) Siku ya Qiyaamah,
Shia mmoja aliambiwa! Je Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
hakutuamrisha kuchagua wake wema? Na kuwa na wakwe watukufu katika watu, hakuwa
na jawabu isipokuwa alisema: Ndio, bila
shaka, akaambiwa: Je unaridhia kuwa na mkwe mtoto wa zina? Akasema, Najilinda
kwa Allaah kuwa na mkwe mtoto wa zina akaambiwa nyie mnasema: au wanazuoni wa
Shia wanasema katika vitabu vyao wanadai uongo kuwa, ‘Umar bin Khatwaab alikuwa
mtoto wa zinaa na jina lake lilikuwa ni Swahaak hilo amelitaja Bahrany katika kitabu
“Al- Kashkuul” Juzuu ya 3 ukurasa wa 212 na anadai kuwa mwanazuoni huyu wa
Kishia ni Imatullah Al-Jazairy anadai: Nasema kwa uhakika wote: “Kuwa ‘Umar
alikuwa hatulii isipokuwa kwa maji ya wanaume”. Allaah atukinge, bali Shia
wanadai kuwa binti yake Hafswah alikuwa mnafiki khabithi
Hapa kuna swali: Unadhania Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) anakuwa mkwe wa mtoto wa zina? Allaah atukinge, au anaridhia mwenyewe
mke fisadi mnafiki? WaLlaahi nyie mnamzulia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam), Enyi Mashia na mnaridhia kwa Mtume yale msiyoyaridhia kwa
Nafsi zenu wenyewe. Tunataka jawabu juu ya mushkeli huu.
Utata Mwengine: Malik bin Ashtur mmoja wa wakuu wa Swahaba wa ‘Aliy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) nao ni miongoni mwa wanaotukuzwa na Shia, anasema: Enyi
watu – Hakika Allaah Mtukufu anakutumieni Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa mbashiri muonyaji. Na amekuteremshieni kitabu
ndani yake kuna halali na haramu, faradhi na Sunnah, kisha akamfisha akiwa
ameekeleza wajibu wake kisha amemfanya Khalifa wa watu Abu Bakr naye ataenda
mwendo wake na kufuata Sunnah zake. Na Abu Bakr akamwachia ‘Umar naye
akiendelea kufuata Sunnah hiyo. Hili limo ndani ya kitabu “Malik bin Ashtar
Khutwabuhu wa Aaraauhu ukurasa wa 89”.
Swali hapa ni: Malik bin Ashtur anamsifu Abu Bakr na ‘Umar kwa
wanayostahili, pamoja na haya Shia wanajitia upofu juu ya sifa hizi wala
hawataji katika vikao vyao na katika Husayniyaat zao, ambazo haziishi kuwatusi
Abu Bakr na ‘Umar kwanini wanaficha?
Utata Mwengine: Kwanini Shia
wanampa (‘Iswmah) uhifadhi kwa Faatwimah na kuizuia kwa dada zake Ruqayyah na
Umu Kulthuum? Na wao ni watoto wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam)
Mushkeli Mwengine: Shia anapoambiwa: Kwa nini ‘Aliy (Radhiya Allaahu
‘anhu) alinyamaza kuhusu kugombania Ukhalifa baada ya kifo cha Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nae ni
Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Maimamu ni Ma’aswuum, imekuja kwa
makubaliano yanatengua hii ‘Iswmah’
chukua kwa njia ya mfano kama Hasan bin ‘Aliy anamkhalifu baba yake
‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika
kutoka kwake kupigana na wanaodai damu ya ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) bila shaka
mmoja wao yuko sawa na Mwengine amekosea na wote hao ni Maimamu wawili, Ma’aswuum
kwa Shia, hili ni jambo geni, vile vile Husayn amemkhalifu Hasan katika kadhia
ya Sulhu pamoja Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) na bila shaka mmoja wao yuko
sawa na Mwengine amekosea na ajabu wote hao ni Maimamu wawili ambao hawakosei.
Utata Mwengine:
Iliposhuka kauli Yake, Ta’alaa:
“58. Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe” (4:58)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
aliwaita Bani Shaybah na akawapa funguo za Kaabah, na kumwambia, “Chukueni enyi
Bani Twalhah milele na milele katika nyinyi hadi Siku ya Qiyaamah
hatukunyang’anyeni isipokuwa dhalimu”.
Hili analisema katika Shani inafungana na ulinzi wa
Kaabah, basi kwanini hakusema katika Shani ya Ukhalifa wa ‘Aliy (Radhiya
Allaahu ‘anhu) na hilo ni jambo kubwa zaidi kwa Waislamu na juu yake kuna
Masilahi ya Waislamu wengi, bali Imani inasImamua juu yake, kwa nini
hakumwambia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ‘Chukua Ewe ‘Aliy, chukua Uimamu
kwako wewe na kizazi chako milele na milele hatakupokonyeni isipokuwa dhalimu’.
Kwa nini hakulisema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) na badala yake amesema katika usImamuizi wa Kaabah?
Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa ‘Aliy
(Radhiya Allaahu ‘anhu) anayo nakala ya Qur-aan iliyopangiliwa kwa jinsi
ilivyoshuka. Kwa nini ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa Khalifa baada ya
‘‘Uthmaan hakutoa msahafu huu Kamili?
Utata Mwengine: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alishiriki katika vita
dhidi ya walioritadi zama za Ukhalifa wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)
akachukua kijakazi katika mateka wa Bani Hanifah na baadae kijakazi hicho
kilizaa mtoto aliyeitwa Muhammad Bin Al Hanafiyah hii inalazimika kusema kuwa
‘Aliy ameridhia ukhalifa wa Abu Bakari vinginevyo asingeshiriki kwa radhi yake
katika jambo hili. Lau kama isingekuwa Ukhalifa wa Abu Bakr ni wa kisheria basi
asingeshiriki katika jambo hili na kumchukua kijakazi (As-Sabiyah) aliyekuja na
Muhammad bin Hanafiyah.
Utata Mwengine: Shia wanadai katika simulizi zao. Kuhusu Mahdi
aliyejificha na huyo ni Imamu wa kumi na mbili, Muhammad bin Hasan Al-Askari
wanataja: kuwa yeye alipozaliwa ndege walimshukia toka mbinguni wakipangusa
mbawa zao kwenye kichwa chake na uso wake na mwili wake. Kisha wanaruka, baba
yake alipoambiwa hivyo alicheka, akasema: Hao ni Malaika wa mbinguni wanashuka
kupata baraka kwa mtoto huyu na hao ndio wanusuru wake atakapotoka. Hili lipo
ndani ya kitabu cha “Raudhatul-Waadhiin” ukurasa wa 260.
Swali na utata: Madamu malaika ndio wanusuru wake basi kwanini ana
hofu na kuingia katika Sirdaab? Huu ni utata na mushkeli.
Utata Mwengine: Shia ambao wanadai kuwa Allaah amerefusha Umri wa
Mahdi wao anangojewa mamia ya miaka, kwa ajili ya haja ya viumbe – bali
ulimwengu wote – lau Allaah angerefusha uhai wa yoyote kwa ajili ya mahitaji ya
viumbe kwa huyo, basi angerefusha miaka ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) basi kwa nini hakurefusha muda wake (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) isipokuwa ni kwamba amekamilisha sheria kwake yeye (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Mushkeli Mwengine: ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alichagua watu sita
katika wafuasi wake kwa ajili ya Shura baada ya kufa kwake, kisha watatu katika
wao wakajitoa. Kisha Abdur-Rahmaan akajitoa wakabaki wawili. ‘Aliy (Radhiya
Allaahu ‘anhu) na ‘Uthmaan (Radhiya
Allaahu ‘anhu) kwanini ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) tangu mwanzo hakutaja mbele yao kuwa
yeye ni wasii wa Khalifah toka kwa Mtume
wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je, alikuwa anamhofia
yoyote baada ya mauti ya ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu)?
Haya ndio tuliojaaliwa enyi ndugu zangu katika kutaja
baadhi ya utata na matatizo na maswali kuhusu madhehebu haya yenye kugongana.
Ninawaomba mashie wenye akili wafanye utafiti kuhusu mas-ala haya tata huenda
yakawarudisha katika haki waliyokuwa nayo Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na watu watukufu wa nyumba yake.
Namuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atuthibitishie
katika Kitabu chake na katika Sunna ya kipenzi chake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam).
Ee Allaah! Jaalia mwisho wa maneno yetu tusemayo pindi
tutakapotoka hapa duniani ni neno hili tukufu lililobarikiwa, “Laa Ilaaha Illa
Allaah Muhammadun RasuuluLlaah”
Kadhalika tunamuomba Ar-Rahmaan kwa ukarimu Wake Atujaalie
makaburi yetu kuwa ni bustani katika bustani za peponi, na Atufufue siku ya Qiyaamah
nyuma ya bendera ya kipenzi Chako Muhammad bin ‘Abdillaah (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) miongoni mwa Maswahaba zake, watu wa nyumba yake
waliotoharika kwa hakika yeye ni Mkarimu na tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala).