USIA
Mtungaji : Sh. Abdulla
Bakathir (Kadara) Mola amrehemu
Lamu . Mwaka unakadiriwa 1960
Kwa jina la Mwenyezi Mungu , mwingi wa rehema
mwenye kurehemu
1. Bisimillahi kutubu - Ina la Mola Qaribu - Alompesi
kujibu - Alomoumba kwa niya.
2. Nandike na Rahamani -
Mrahamu masikini - Na matajiri bengini - Kwa
3. Nandike na Arrahimu -
Wema alowakirimu - Kuwapa njema ilimu - Wakaweza kutumiya
4. Kisa naleta himdi - Kwa neema na
kuzidi - Umati wa Muhamadi - Nami nikawa mmoya
5. Ninashukuru kwa haki -
Alonipa tawfiki - Wanangu na marafiki - Kuwapa huu wasiya
6. Ina Bahiya Durari - Yenye na
tabia nzuri - Mimi nimeifasiri - Ipate kuwaeleya
7. Na mukisa kuipata - Somani bila matata - Pamoya
na kufuata - Yote nalowandikiya
8. Maradhi yamenishika - Siku sita zimefika - Siyaweza
kutamka - Maneno kukuuswiya
9. Watu wakidirikana - Henenda wakiagana - Ghafula
huepukana - Pasi na kukusudiya
10. Mengi nimekuuswiya - Ila
sikukwandikiya - Sasa hini nipokeya - Mwanangu utatumiya
11. Mauti kwetu ni haki -
Wala usingiye dhiki - Na ikiwa nimebaki - Na mengine takwambiya
12. Kwani mimi si wachuma - Kuna siku nitakoma - Ni
sasa kwa hini huma - Awtani tatembeya
13. Lakini naomba Mungu - Nishike wano wanangu - Nizike
na mama zangu - Kisa yapo taifiya
14. Ikiwa nimeondoka - Usipende kuzunguka - Baraza
zenye dhihaka - Sio nzuri kuongeya
15. Wanenapo masikini - Tukuonapo ndiyani - Twamkumbuka
fulani - Mayondi yatakwingiya
16. Wakikwalika harusi - Ukiwa nayo nafasi - Nenda
ungiye upesi - Palo pema kukaliya
17. Pindi wakubwa wayapo - Nafasai tena haipo - Huinika
wewe hapo - Heshima ukamwekeya
18. Ule alokualika - Mno atafurahika - Takua kihangaika
- Nafasi kuizengeya
19. Usiketi ziatuni - Wala tini mlangoni - Itiye
uwandazini - Nafasi itatokeya
20. Wenendapo karamuni - Usiswifu ya
fulani - Kunena si
21.
22. Pengine huwa hakuna - Nae hawezi kunena -
Hutahayari maana - Si uzuri kumwambiya
23. Mahala usoalikwa - Tahadhari na
kufika - Japo kwa mjomba kaka - Kwenenda nakuzuwiya
24. Akiwa alisahau - Hakika hakudharau - Kikuiliya
hiyau - Inika andama ndiya
25. Ukitoka hadharani - Sikae mabarazani - Fuliza kwako
nyumbani - Pija hodi kisa ngiya
26. Uchambiwa ningojeza - Usingie
na kufuza - Wala kisa kuuliza - Ni mtu gani nambiya
27. Situngie mivunguni - Maghala za zipembeni - Kufuli
zimo nyoyoni - Wata fafani kungiya
28. Kiwa wewe wapoteza - Na yeye zake tauza - Ukiwa
unatengeza - Naye atakuwekeya
29. Siulize majirani - Ayao kwangu
ni nyani - Kweli haipatikani - Wasiwasi utangiya
30. Kufuli ya mwanamke - Huwa nayo mume wake - Isha
akirudi kwake - Mke hendi kutembeya
31. Mume kenda senemani - Mke henda
kwa jirani - Arudipo hatamani - Kuzungumza na ndiya
32. Yule yamempendeza - Alikokwenda kuteza - Jirani
huku meyaza - Maovu amemwambiya
33. Watu huhishimiyana - Ndipo hapo hupendana - Ukali
kujibizana - Hupitisha kupoteya
34. Simtukane mkeo - Kiwa mbele ya wanao - Au watu
wangiyao - Wakawa watasikiya
35. Kikuudhi hadhirani - Sidhihirishe usoni - Ngoja
mkingiya ndani - Nena kwa kutaradhiya
36. Kiwa mekuwa mkali - Sinene mara ya pili - Epuka
wenende mbali - Tasahau mara moya
37. Si aibu usishike - Kumrai mke wake - Mtume
ni kazi yake - Kwa wote wake tisiya
38. Na upatapo kijana - Teza nae wewe
39. Shika mwanangu mpenzi - Kijana kuwa azizi - Twabiya
ni ya muyezi - Ndiyo takayotumiya
40. Boi akiwa mpevu - Khaswa likiwa
na nguvu - Afadhali mpe livu - Mngine wewe zengeya
41. Nguo zako matambara - Usimpe hata mara - Zikiwa
hazina sura - Kheri zungu kupuliya
42. Boi akiwa nyumbani - Nasivae leso tini - Kheri umpe
kiguni - Au kitambi kipiya
43. Boi kiwa na maneno -
Mazuri yaso mfano - Muyuwe hafai neno - Ni mpuzi nakwambiya
44. Mtafute mtatufu - Asokuwa na
harufu - Wala asiwe mchafu - Wa mwili na wa tabiya
45. Akiwa mtu mzima - Kumi na
tatu mekoma - Mfukuze kwa salama - Wewe mngine zengeya
46. Na ulalako chumbani - Sikaribishe mgeni - Na ukiwa
kitandani - Siwate mtu kungiya
47. Kitanda cha mke wako - Kukiona waliyoko - Mama
hata ndugu zako - Ni aibu nakwambiya
48. Ila ukosapo budi - Kuna
mambo yamezidi - Kula ayao harudi - Lazima ataingiya
49. Na ungiyapo chumbani - Sauti na
iwe tini - Aliyoko ukumbini - Asiwe wa kusikiya
50. Ukiwa na mtumishi -
Sifanye nae ubishi - Usizidishe uteshi - Walau kumrukiya
51. Nasiyuwe siri zako - Walau aibu yako - Atakuondolea
mbeko - Ni swalaha takwambiya
52. Siri siweke moyoni - Wala sitie bengini - Wala
simpe jirani - Fahamu itaeneya
53. Siri isipite kanwa - Wala kwa
mato kuonwa - Siri ni isiyonenwa - Inenwapo hueneya
54. Mtu nasikupe siri - Kisa akakukariri - Simpe mtu
khabari - Kataa kuisikiya
55. Mwambiye alokuyuza - Mbona wewe hukuweza - Kwangu
umeitangaza - Nami watu tawambiya
56. Boi akija chumbani - Nasimame mlangoni - Nasitie
guu ndani - Hata kukufagiliya
57. Alfajiri amka - Wakati usiyatoka - Kuku achanda
kuwika - Muwe mwawika pamoya
58. Inuka ungie choni - Uswali rakaateni - Usome
arubaini - Ya hayyu Ya Qayyumiya
59. Uchelewapo kwamka - Yuwa mbele limetoka - Watu
wametiarika - Nyumbani wameeneya
60. Kwanda sitoke chumbani - Imunike kiyooni - Uchafu
ulo usoni - Uoshe ulokungiya
61. Usipite kwa ziyatu -
Penye hadhara ya watu - Za miti huwa si mtu - Hishima huwavundiya
62. Ila kwa kuzoweyana - Au
wawe ni zijana - Hapo makosa hapana - Waweza kuivaliya
63. Shai kunwa ukumbini - Sipende kunwa chumbani - Paka
tungu mivunguni - Fahamu wataeneya
64. Saa itie majira - Ijaribu kula mara - Ukichelewa si
sura - Kazini kwenda kungiya
65. Uingiyapo kazini - Wape watu gudi moni - Kwa furaha
za usoni - Pamoya na kutekeya
66. Wote waite mabwana - Au
waite manana - Furaha ukiziona - Kila siku endeleya
67. Yaliyokhusu siyasa - Sizungumze kabisa - Ngojeya
kazi ikisa - Na wengine endeleya
68. Mno siifanye tamu - Utakuwa maadumu - Kanwani usiwe
sumu - Watu watakutukiya
69. Itiye mwao matoni - Itowe mwao ndimini - Barizi
mwao nyumbani - Shikiyo utakaliya
70. Siiza uitiwalo - Sikiza uambiwalo - Teuwa ulitakalo
- Yesapo kukueleya
71. Ukenda nyumba ya mtu - Ukaona kuna zitu - Usinene
nami kwetu - Yako mambo
72. Uwate kumuuliza - Kitu hiki wewe huza - Mno
kimenipendeza - Au kuomba kimoya
73. Wala sikae kitini - Kilokabili chumbani - Na
uketipo mezani - Wata zitu kutezeya
74. Mzungu akikwalika - Mezani akakuweka - Chakula boi
kaweka - Na mai kuwatiliya
75. Uma shika kushotoni - Kisu shika kivulini - Kijiko
kiwe yamini - Ni uzuri wa kuliya
76. Kitambaa kushotoni - Kiwe mwako mkononi - Zambatazo
mdomoni - Ukawa utafutiya
77. Kiwa ni Mtaliani -
Huifunga na shingoni - Na nta moya mezani - Uchafu kuzuwiliya
78. Wakikweteya khamri - Usinwe wambiye sori -
Atafahamu uzuri - Huipendi kutumiya
79. Tahadhari siteuke - Katika hadhara yake - Afadhali
uondoke - Faraghani kimbilya
80. Kuteuka ni aibu - Ni
kama shuzi swahibu - Wahindi na Waarabu - Wao wanaifanyiya
81. Ila wasitaarabu - Ambao wana adabu - Mve kwao
ni aibu - Zitabuni wametiya
82. Kuteuka hadhirani - Ni kama
shuzi mwendani - Khususa kwa Ungujani - Na Maka na Misiriya
83. Ukiweko hadhirani - Sitie zanda puani - Sitiye
masikiyoni - Na meno kutotoleya
84. Usiikune matako - Usishike mbele yako - Ziwiya
mikono yako - Hadhirani kutezeya
85. Muhindi akikwalika - Kawa chumbi akaweka - Kwanda
kwa chanda andika - Na ulimini kutiya
86. Ladu tamu huya kisa - Usile hata zikesa - Wali huya
kwa matasa - Hula ukiengezewa
87. Ukiwako hadhirani - Ndi akaya usoni - Sighadhibike
mwandani - Makofi ukaitiya
88. Mtatuwe kwa raufu -
Utowe yako hanchifu - Usoni futa uchafu - Mara moya takimbiya
89. Ukiwako hadhirani - Au ukawa mgeni - Chakula kiko
mezani - Na paka tini huliya
90. Chakula kilichowekwa - Tonge usimpe paka - Na kuku
wa kuzunguka - Hufai kuwatiliya
91. Wewe walikusudiwa - Kula tonge uchambuwa - Kuku
wake awayuwa - Mwenyewe tawatiliya
92. Nyumba ya watu swahibu - Kiwa mekuya gharibu -
Usimwambiye karibu - Kiwa umetanguliya
93. Kwako akiya mgeni - Mpe mai gilasini - Kisa
muoneshe choni - Na pa kupumzikiya
94. Kiyeta simu mgeni - Simngojee nyumbani - Mfuatiye
stani - Au mtu kumwekeya
95. Kiwa mtu wa barani -
Simbo una mkononi - Pokeya uweke ndani - Ndipo naye taingiya
96. Kiwa ni wa Mambasani -
Tanga na Uungujani - Begi una mkononi - Boi au wewe pokeya
97. Wageni furaha kwao - Ni kupata nyumba
98. Nyumba ikiwa na hodi -
Mgeni siku hazidi - Huwa si yake kasidi - Ni dhiki zimemngiya
99. Ukiwa wewe mgeni - Umeshukiya nyumbani - Sichelewe
chakulani - Ni yambo lina udhiya
100. Sichelewe kwenda kula - Na wakati
wa kulala - Na uchalikwa mahala - Na mapema humwambiya
101. Huu ni wangu waswiya -
Mwanangu nakuusiya - Iwapo utaugwiya - Utaepuka balaya
102. Na mtu akikutaka - Nende kule waloshuka - Kwao
yakimalizika - Na wewe watakwambiya
103. Akikwambiya mwendani - Hapa mekuya
fulani - Amekutaka fulani - Mwende mukale pamoya
104. Nguo zako piga pasi - Teuwa njema libasi - Sita
wa robo jilisi - Tayari wa kumwendeya
105. Ukenda kwake nyumbani - Simwandame hata ndani -
Kwanda kaa barazani - Mpaka wambiwe ingiya
106. Hapo kikuweka ndani - Kikuweka kitandani - Au
ukiwa kitini - Sikatae nakwambiya
107. Sinene ukiitesha - Kunena hapa patosha - Sikiza
akikwamrisha - Ni kwake umeingiya
108. Tena uwazungumze - Maneno yawapendeze - Urongo
usiuzuze - Ya kweli ukiwambiya
109. Kiwa wamekupulika - Kwa furaha
na kuteka - Kuwengeza wametaka - Ni bora kuendeleya
110. Kiwa hawakusikiza - Ni heri ukanyamaza - Si bora
kuwaengeza - Asotaka kusikiya
111. Usiwe kutetemeka - Kwa wakati
wa kuteka - Heh tatu zikifika - Kiteko kimetimiya
112. Wala sifunuwe kanwa - Watu ndani wakaona - Wala
usiteke
113. Towa salamu mwendani - Wenendapo barazani - Upite
ukae ndani - Wakikwambiya kungiya
114. Wakitonena karibu - Sikae nao swahibu - Wala sione
ajabu - Wana siri nakwambiya
115. Wakiwa wazungumza - Kwanda nenda pulikiza - Mpaka
wakiuliza - Khabari utawambiya
116. Usende ukaitiya - Maneno kwa
kukatiya - Wao wametanguliya - Sizungumze sikiya
117. Unenapo barazani - Siakie mayamini - Wallahi tena
fulani - Ni kweli nalokwambiya
118. Wendapo taaziyani - Popote na
karamuni - Sitoke mbele mwandani - Ila wakikuambiya
119. Waandazi wakikoma - Mwenyewe atasimama - Hasanta
atasema - Hapo utaitokeya
120 Ikiwa utaondoka - Kabula kumalizika - Asopata
atatoka - Kwa wandazi ni udhiya
121. Ukiwa huna makini - Sitoke kwako nyumbani - Ukenda
makaramuni - Watu kuwaharibiya
122. Wenendapo karamuni - Nyama ngumu ya kanwani -
Sirudishe sahanini - Ni uchafu nakwambiya
123. Ukiweko chakulani - Mifupa kibakulini - Duhu
lilomifupani - Usiigonge sikiya
124. Usisonde zilizomo - Ukatongowa midomo - Au
kurudisha mumo - Wesapo kuutumiya
125. Karamu iliyo nzuri - Yenye mai ya sukari - Ziwili
sinwe khatari - Hutosha kunwa kimoya
126. Yatiwapo gilasini - Zanda usitie ndani - Tumiya
kwa kushotoni - Kiwa wavuli huliya
127. Utumiya wa vulini -
Ukiwa swafi mwandani - Pumzi sitie ndani - Gilasi ukitumiya
128. Utotowazo menoni - Zisirudi matumboni - Wala
sishike zandani - Kisa ukazangaliya
129. Sende kwa mtu mtana -
Kwa siku za joto
130. Ingoje kumi na nusu -
Ufanye kwake julusu - Haikupati nuhusu - Waweza kuikaliya
131. Kwa mtu sende mtana - Au asubuhi
132. Baada hapo nendani - Kwa swahibu
na jirani - Imenena Qur-ani - Ilahi ametwambiya
133. Na safarini ukiwa - Kwenu peleka baruwa - Hali
wapate kuyuwa - Yote yalokujiriya
134. Kwa mama mwenye jamali - Na mkeo
wa halali - Kwa bashasha mbalimbali - Usitanganye
pamoya
135. Baruwa na iwe tamu - Ya
kuwatowa hamumu - Yale yatiayo hamu - Sipende kuwandikiya
136. Watiliye ya furaha - Na maneno ya mzaha - Mazuri
yenye nasaha - Ya faida kutumiya
137. Siarifu ya huzuni - Kuwaweka kitandani - Umbali
hawakuoni - Wakabaki na kuliya
138. Usiwate mfukoni - Deri buku ndiyani - Yajiriyo
duniyani - Upate kuwandikiya
139. Andika uyatakao - Ya haraka na
kituo - Ya kesho au ya yeo - Na uloazimiya
140. Ukiweko safarini - Una kitu cha nyumbani - Rafiki
simuamini - Kumpa kukupekeya
141. Akiwa rafiki yako - Nawe una mke wako - Simtoleze
ni miko - Au utaiyutiya
142. Sinene namuamini - Hawezi huyu kukhini - Fahamu
kuna shetani - Fitina tawatiliya
143. Zulekha mkumbukeni - Ni mwanamke amini - Yusufu
kungiya ndani - Kwa nguvu kaishikiya
144. Kamtiya aibuni - Kafungwa na
gerezani - Hata Mungu kabaini - Zulekha kaikiriya
145. Mke wa rafiki yako -
Mumewe kondowa miko - Usingie kama kwako - Ila na yeye pamoya
146. Na mungiyapo nyumbani - Kitwa inamiya tini -
Simtazame usoni - Mke wa nduyo sikiya
147. Fahamu kutizamana - Kunako khatari
148. Mambo yako ya nyumbani - Sizungumze ndiyani -
Sishitaki majirani - Wala mamako akiya
149. Kizere aso kuruba - Kwako asiwe suhuba -
Tawatiliya mswiba - Wa kuteta mara moya
150. Huwa hana la kunena - Ila
kutiya fitina - Na kukumbuka ujana - Wake alokitumiya
151. Uonapo amefuza - Kuya kuizungumza - Ni kheri
mkampuza - Musende kumsikiya
152. Angiyapo ondokani - Muingiliye chumbani - Mumuwate
ukumbini - Kwa uzuri kumwambiya
153. Simrukiye kizere - Wala simteze shere - Wala
simtume bure - Na wewe yatakujiya
154. Kizere ni mabruki -
Kiwa kizere cha haki - Zingine ni zishiriki - Simuamini mmoya
155. Lakini siwatukiye - Maneno siwaambiye - Iwa
na hadhari naye - Mambo kukuharibiya
156. Jirani tumeusiwa - Yataka kuwangaliwa - Haifai
kuudhiwa - Mtume ameziwiya
157. Zigari sinunuweni - Kuwapa wano nyumbani - Fahamu
wako jirani - Wane watamliliya
158. Musikangeni mituzi - Kwa thaumu
na ziyazi -
159. Hufai kutamanisha - Kwa mituzi ya kupisha -
Himtiya mshawasha - Na wane humliliya
160. Umrahamu jirani - Akiwa ni
masikini - Kwa wali kibakulini - Na wane kuwangaliya
161. Hadhira yako nyumbani - Kwanda mwambie jirani -
Kisa ngia mtaani - Kisa mbele endeleya
162 Sipende watu adhimu - Na suhuba za hakimu -
Watakuzidisha hamu - Na dhiki zitakungiya
163. Kiwa mumefuatana - Watu wote watanena - Apenda
makuu
164. Kiwa watu wamenena - Siri ikijulikana - Hukutuhumu
fitina - Ni wewe umeitiya
165. Usipende matajiri - Katukiya mafakiri - Wenye
twabiya nzuri - Suhuba zao zengeya
166. Wagonjwa watizameni - Sipitali
na nyumbani - Lakini musikaeni - Muda ukaendeleya
167. Muwee kumkaliya - Mara dhiki humwingiya - Hawezi
na kukwambiya - Twaa kiyasi sikiya
168. Kwake ngiya mara moja - Ila
kikwambiya ngoja - Pengine huwa na haja - Chooni ataka ngiya
169. Uwapo ni msafiri -
Rafikiyo una gari - Nauli ikikaswiri - Usende ukarukiya
170. Siteze na yake
171. Na safari za malori - Kufunikwa tonobari -
Usiingie si nzuri - Zina na mwingi udhiya
172. Na ungiyapo relini - Tikiti kata sekani - Singie
za rahisini - Kisa zitakutukiya
173. Sasa nitatia koma - Siwezi tena kusema - Rabbi
mnusuru mama - Na umbu langu pamoya
174. Nina umbu masikini - Alomwingi
wa imani - Uzito wangu kitwani - Yeye amenipokeya
175. Muawini Ya Karima - Kwa zijana waso mama - Wao
wanamsukuma - Na yeye huwatapiya
176. Ilahi ndiwe muweza - Nina mamangu ajuza -
Muhifadhi kwa kufuza - Na maisha ya afiya
177. Nimechoka siyakoma - Mikono hunitetema - Siku
nyingi nina huma - Hunu ni wangu wasiya
178. Huu ni wasiya wangu -
Kuwausiya wanangu - Kwani huona utungu - Kiwa mepotoka ndiya
179. Penda awe mtukufu - Huyu mwanagu Yusufu - Na watu
wamsharifu - Kiutumiya waswiya
180. Waswiya si wake pweke - Ni yeye
na ndugu zake - Na marafiki wandike - Pamoya na
kutumiya
181. Alotunga ina lake - Wamwita rafiki zake - Kadara
ni yeye pweke - Alotangaa duniya
182. Na lengine mashuhuri - Abdalla Bakathiri - Apenda
mno safari - Hadiriki kutuliya
183. Mtuze Rabbi Manani - Katika wake watani - Mpe kazi
na makini - Za baraka na afiya
184. Umondolee husuda - Tengeza zake ibada - Mrejeze
kama ada - Imwekelee duniya
185. Na jamii Isilamu - Walo kisiwa cha Amu - Na
wengine walo humu -
186. Na walio
187. Na Waunguja Rabbana - Uwape kusikizana - Uhuru
ukilingana - Wawe wote hali moya
188. Uwondolee fitina - Isilamu kupijana - Litetewalo
hapana - Ni fitina zimengiya
189. Swalla llahu wasalama
- Zishuke kwa wake tumwa - Nimedhoofu kwa huma - Rabbi tatupa afiya.
MAANA
7. Mukisa : mukisha
15. Mayondi : majonzi
17. Huinika : wainukie
24. Hiyau : sasa hivi ; Inika :
inuka
26. Uchambiwa : ukiambiwa ;
Kufuza : kuingia moja kwa moja
27. Situngie : usichungulie ;
Fafani : kujipeleka mbelembele ( kujua
39. Muyezi : mlezi
42. Kiguni : kikoi ; Kitambi :
kikoi
44. Mtatufu : mwenye makini (
mtulivu)
51. Mbeko : heshima
53. Kanwa : kinywa
57. Achanza : akianza
59. Yuwa : jua
60. Imunike : jiangalie
63. Tungu : chungu nzima (wengi ,
tele)
66. Manana : mabibi
70. Siize : usikatae
72. Huza : unauza (kuuza)
75. Kuvulini : kuliani ( mkono wa
kulia , kuume)
81. Mve : kuteuka
83. Zanda : vidole
85. chumbi : chumvi
86 Huja kisa : huja baadae
87. Ndi : nzi
95. Simbo : fimbo
107. Ukiitesha : ukijichekesha
108. Usiusuze : usiuzuwe
117. Siaike : usiape
123. Duhu : mafuta yaliyo ndani
ya mfupa
135. Yatiayo hamu : yatiayo wasi
wasi
151. Amefuza : amekuja moja kwa
moja
157. Zigari : vigari ( toys) ;
Wano : wanao ; Wane : wanawe
167. Muwee : mgonjwa