Tembelea http://mawaidha.info
Imepokelewa katika Athar kuwa
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) siku moja
alipokuwa safarini alikutana na
mtu aliyemuomba afuatane naye, na Nabii Issa alikubali.
Walipokuwa njiani Nabii Issa alinunua mikate mitatu, akala mmoja,
akampa mwenzake mkate mwingine, kisha akamwambia:
"Na mkate huu wa tatu tuubakishe, utatusaidia mbele ya safari."
Usiku ulipoingia na
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) alipojipumzisha na usingizi kumchukuwa,
yule mtu aliuchukua ule mkate wa tatu
uliobaki akaula.
Alipoamka akamuuliza:
“Uwapi mkate tuloubakisha?”
Yule mtu akajibu:
“Sijuwi”
Walipokuwa wakiendelea na
safari wakatokezewa na mnyama mkali sana,
na maisha yao yakawa hatarini,
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) akanyanyua mikono juu na
kuomba dua, na yule mnyama
akatoweka.
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) akamwambia mtu yule:
“Kwa utukufu
wa Yule Aliyetuokoa
na hatari ya mnyama mbaya
huyu, niambie nani aliyekula mkate?”
Yule mtu akajibu kama alivyojibu
pale mwanzo:
“Sijuwi”.
Wakaendelea na safari, na
walipowasili kandokando ya bahari. Nabii
Issa (Alayhi ssalaam) alimuomba Mola wake, akaanza kutembea juu ya bahari
pamoja na
mwenzake yule, na walipokuwa katika
hali ile akamuuliza tena:
“Kwa utukufu
wa aliyetuwezesha kutembea juu ya
bahari, tafadhali niambie nani aliyeula
mkate ule?”.
Yule mtu akajibu
vile vile:
“Sijuwi”.
Baada ya kuvuka bahari,
wakatembea kidogo, kisha wakapumzika karibu na
jabali, na Nabii Issa (Alayhi ssalaam) akamuomba Mola wake na lile
jabali likageuka kuwa dhahabu, kisha
akamuambia mtu yule:
“Jabali hili la dhahabu tutaligawa sehemu tatu.
Sehemu moja itakuwa yangu,
moja yako, na sehemu moja
tutampa yule aliyekula mkate”.
Yule mtu akasema:
“Mimi ndiye niliyekula
mkate!”.
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) akamuambia:
“Basi dhahabu yote chukua
wewe”.
Yule mtu alipokuwa amekaa chini ya jabali
lake la dhahabu huku akitafakari, wakapita majambazi wawili.
Majambazi:
“Dhahabu ya nani hii?”
“Yangu”.
“Dhahabu yote yako peke
yako?”
“Ndiyo”.
Majambazi:
“Unaonaje tukagawana sehemu tatu, kila mmoja
wetu achukue sehemu moja?”
Yule mtu baada ya kuwahisi kuwa
ni watu
wabaya, akawakubalia, kisha akawaambia:
“Sote tuna njaa, mnaonaje nikienda kununua mikate tupate kula,
kisha tusikilizane namna ya kuichukuwa
dhahabu yetu?”
Majambazi wakakubali.
Baada ya yule mtu kuondoka, majambazi
wakaanza kupanga ukhabithi wao.
“Unaonaje akirudi tu, tumshambulie
kwa visu na mapanga, tumuulie
mbali kisha tuichukuwe sisi dhahabu yote?”
Wakakubaliana.
Na yule mtu alipokuwa akienda kununuwa mikate akawa anawaza na kufikiri;
“Kwa nini
nigawane nao dhahabu ile, wakati
nimepewa peke yangu? Ah! Bora nitawatilia
sumu katika mikate hii, wafe,
kisha niichukue dhahabu yote peke
yangu”.
Alipowasili na mikate
yake ya sumu,
wale majambazi walimvamia na kumshambulia kwa visu na
mapanga na kumuua, kisha wakakaa
chini ya mti na kuanza
kula mikate ile iliyotiwa sumu.
Wakafa wote watatu.
Nabii Issa (Alayhi ssalaam) siku ya pili
alipokuwa akirudi safarini akifuatana na wanafunzi
wake, alipita mahali pale na kuona maiti
tatu, akasema kuwaambia wanafunzi wake;
“Tamaa
ndiyo iliyowauwa watu hawa”.