SAYID AL ISTIGHFAR

 

Tembelea: http://mawaidha.info/

 

Mwezi wa Ramadhani huo unaingia. Mwezi wa Rehma, mwezi wa Barka, mwezi wa Maghfira, mwezi wa kuepushwa na moto wa Jahannam.

Mwenyezi Mungu ametutunukia mwezi huu kama ni zawadi kutoka Kwake kwa ajili ya kututakasa, kuturehemu, kutughufuria madhambi yetu, kuzinyanyua darja zetu, kuzilainisha nyoyo zetu.

 

Kwa ajili hii inatupasa kuukabili ukarimu huu utokao kwa Mola wetu Mkarimu Subhanahu wa Taala kwa kujitakasa na kutubu kutokana na madhambi tuliyoyachuma miezi kumi na moja iliyopita huku tukimuomba atughufurie na huku tukimuahidi kutoyarudia tena madhambi hayo.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua."

Aali Imran – 135

 

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenyezi Mungu huifurahia toba ya mja wake kuliko mmoja wenu anapokuwa juu ya mnyama wake jangwani akamuangusha na kumkimbia."

Bukhari

Na katika riwaya ya Muslim na wengine:

"Mwenyezi Mungu huifurahia toba ya mja wake kuliko mmoja wenu anapokuwa juu ya mnyama wake jangwani akamuangusha na kumkimbia. Mnyama huyo akiwa amebeba chakula chake na maji yake, kisha mtu huyo akakata tamaa, akauendea mti na kuegemea chini ya kivuli chake akiwa keshakata tamaa ya kumuona mnyama wake tena. Na anapokuwa katika hali hiyo, ghafla anamuona mnyama wake mbele yake. Akazishika hatamu zake, kisha akasema kwa furaha: "Mola wangu Wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako". Alikosea kwa wingi wa furaha."

Muslim na wengine

Na maana ya Mwenyezi Mungu kuifurahia toba hiyo ni kuwa anaridhika na nia ya mja wake huyo juu ya kuwa alikosea kutamka.

 

Miongoni mwa dua za kuomba maghfira ni hii dua inayoitwa 'Sayyid al Istighfaar' (Dua bora ya kuomba Maghfira kupita zote) aliyotuusia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Dua ambayo ndani yake imekusanya maana zote za Toba na kukiri na kwamba hapana mwenye kusamehe makosa isipokuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

 

Imepokelewa kutoka Shaddad bin Aus (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Laahu alayhi wa sallam) amesema:

"Bwana wa kuomba maghfira ni kusema:

Çááøóåõãøó ÃóäúÊó ÑóÈøöí áÇ Åöáóåó ÅáÇ ÃóäúÊó ÎóáóÞúÊóäöí æóÃóäóÇ ÚóÈúÏõßó æóÃóäóÇ Úóáóì ÚóåúÏößó æóæóÚúÏößó ãóÇ ÇÓúÊóØóÚúÊõ ÃóÚõæÐõ Èößó ãöäú ÔóÑøö ãóÇ ÕóäóÚúÊõ ÃóÈõæÁõ áóßó ÈöäöÚúãóÊößó Úóáóíøó æóÃóÈõæÁõ áóßó ÈöÐóäúÈöí ÝóÇÛúÝöÑú áöí ÝóÅöäøóåõ áÇ íóÛúÝöÑõ ÇáÐøõäõæÈó ÅöáÇ ÃóäúÊó.

(Allahumma anta Rabbiy laa ilaaha illa Anta. Khalaqtaniy wa ana abduka. Wa ana alaa ahadika wa waadika ma statwaatu. Audhu bika min sharri ma sanaatu. Abu'u laka biniimatika alayya wa abu'u laka bidhanbiy, faghfirliy, fainnahu laa yaghfiru dhunuuba illa anta.)

 

Akasema: "Atakayesema hayo wakati wa mchana akiwa na yakini juu yake akafa siku hiyo kabla ya usiku kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi. Na atakayesema hayo wakati wa usiku akiwa na yakini juu yake akafa kabla ya asubuhi kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi."

Bukhari na Attirmidhy na Annasai na wengine

 

Maana ya yake

 

Ewe Allah. Wewe ni Mola wangu mlezi hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe

Çááøóåõãøó ÃóäúÊó ÑóÈøöí áÇ Åöáóåó ÅáÇ ÃóäúÊó

Umeniumba na mimi ni mja Wako

ÎóáóÞúÊóäöí æóÃóäóÇ ÚóÈúÏõßó

Na mimi nimo katika kutekeleza maamrisho Yako na waadi Wako niwezavyo

æóÃóäóÇ Úóáóì ÚóåúÏößó æóæóÚúÏößó ãóÇ ÇÓúÊóØóÚúÊõ

Ninajikinga Kwako na kila shari niliyoitenda

ÃóÚõæÐõ Èößó ãöäú ÔóÑøö ãóÇ ÕóäóÚúÊõ

Ninakiri Kwako kwa neema Zako juu yangu

ÃóÈõæÁõ áóßó ÈöäöÚúãóÊößó Úóáóíøó

Na ninakiri Kwako juu ya dhambi zangu

æóÃóÈõæÁõ áóßó ÈöÐóäúÈöí

Kwa hivyo unisamehe kwa sababu hapana mwenye kusamehe madhambi isipokuwa Wewe

ÝóÇÛúÝöÑú áöí ÝóÅöäøóåõ áÇ íóÛúÝöÑõ ÇáÐøõäõæÈó ÅöáÇ ÃóäúÊó.

 

Nakutakieni nyote na kila Muislamu Ramadhani njema ya mwaka huu na kila mwaka, huku nikimuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tufaidike na Ramadhani hii na nyingi zijazo. miaka baada ya miaka  -Amin

 

http://mawaidha.info/