Ya Habibi ya Nabiya
Makka ulikozaliwa, Madina
ukapokewa
Kwa mashada ya mauwa, Ya Habibi ya Nabiya
Maka ilikochomoza, nuru
ya Mola Muweza
Madina ikaangaza, kisha kote kueneya
Ulikuja na risala, kutoka
Kwake Taala
isomwe kila mahala, kila pembe ya
duniya
Ni Risala kamilifu, Yake Mola
Mtukufu
aso mwana wala kufu, yenye kunawiri
njiya
Yote ukayatimiza, hapana
ulichosaza
tena bila kupunguza, kamili
kutufikiya
Ukatufunza shahada, akhlaqi
na ibada
na kutoa misaada, kwa wenye
kuhitajiya
Allahu katakasika, Mola aso
mshirika
ni shahada ya hakika, na wewe wake
nabiya
Hiyo ndiyo ya awali, alotufunza
rasuli
ni nguzo iliyo ghali, nyoyoni
mwetu jamiya
Swala akatufundisha, asubuhi hadi Isha
zote twazikamilisha, nyakati
zikiingiya
Twaziswali kwa wakati, kwa ikhilasi na
dhati
tena bila hatihati, Ya Rabbi
takabaliya
Kisha tutowe na Zaka, wakati unapofika
kwa hesabu kila mwaka, nisabu ikitimiya
Ilitiliwa mkazo, tajiri
na walo nazo
tugawe bila vikwazo, tuwape
wahitajiya
Kisha kutoa sadaka,
hiyo kama
tukitaka
mali inatakasika, na
kurudisha afiya
Kuhiji Maka ni nguzo, kwa kila mwenye
uwezo
hiyo haina mchezo, yataka
kuipaniya
Kaaba nyumba tukufu, nyumba kongwe
takatifu
hapo lazima utufu, shoti saba
kutimiya
Nyumba hiyo ipo Maka, ni
mji wenye baraka
Dhambi hapo hufutika, Mola Ametuambiya
Arafati ndiyo hija, huko
nako kwakungoja
kwake aliye Mmoja, dua zinaelekeya
Siku hiyo ikifika, watu
tena patashika
machozi yamiminika, wakiomba na
kuliya
Labeka Rabi labeka, Mola uso
mshirika
Arafati tumefika, nawe
watushuhudiya
Mwenye sifa ya uluwa, La
ilaaha illa Huwa
ziwe zitakavyokuwa, dhambi
utatufutiya
Uturudishe tukiwa, kama
tulivyozaliwa
ndivyo tulivyoambiwa, na
Muhammadi nabiya
Kisha Mina siku tatu, wanakusanyika
watu
wanapiga jamaratu, na kuchinja
adhuhiya
Yabaki shughuli moja, hiyo pia
yakungoja
ni shoti saba za hija, tawafu na
sayi piya
safari ikishafika, ukataka
kuondoka
usibaki hapo Maka Widaa
itabakiya
Hiyo ni tawafu moja, ukesha
moja kwa moja
Hapana tena kungoja Garini
utaingiya
Hizo ndizo nguzo zake, na hiyo risala
yake
kutoka kwa Mola wake, ni
amana ya Jaliya
Ni nzito kweli kweli, Ilikataa
jabali
wewe ukaikubali, kubeba
ukairidhiya
Mola amekuhitari, mbele ya wote
bashari
uifikishe habari, kwa
jini na insiya
Anachokitaka huwa, Mwenyewe
kakuchaguwa
kwa sababu akujuwa, kipenzi chake
nabiya
Mwenye khuluqa adhimu, mpole tena karimu
kwa uma wake rahimu, kuliko kila nabiya
Ni mwenendo mtukufu, ulotimu
kamilifu
mkweli muaminifu, mwenye sifa
maridhiya
Mfano wa Quruani, inotembea njiani
kakufundisha Manani, utukufu wa tabiya