MWANACHUONI WA KARNE – SHAYKH
AL-ALBAANIY
Muhammad Baawazir (16 Muharam
1428H – 04 Februari 2007M)
1332H-1420H 1914M-1999M
NASABA YAKE: Al-Albaaniy (Kwa sababu asili yake ni
mtu wa
KUN-YAH YAKE: Abu ‘Abdir-Rahmaan (maana yake ni ‘baba
wa ‘Abdur-Rahmaan’)
WAKE ZAKE: Alioa wake wane; watatu wa mwanzo walimzalia
watoto, na wa nne ‘Ummu Al-Fadhwl’ hakujaaliwa kuzaa, na ndiye aliyekuwa naye
hadi mwisho wa maisha yake.
WATOTO WAKE: Aliruzukiwa watoto 13; wakiwa 7 wa
kiume na 6 wa kike. Wa kiume ni: ‘Abdur-Rahmaan, ‘Abdul-Latwiyf,
‘Abdur-Razzaaq, ‘Abdul-Muswawwir, ‘Abdul-Muhaymin, Muhammad na ‘Abdul-A’alaa.
Wa kike ni: Aniysah, Aasiyah, Salaamah, Hassaanah, Sakiynah na HibatuLlaah.
Mwanachuoni Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn bin
Nuuh An-Najaatiy Al-Albaaniy ni mmoja kati ya Maulamaa wakubwa wa Kiislam
katika zama hizi. Anahesabika kuwa ni mwanachuoni wa Hadiyth maarufu kabisa
katika fani ya elimu ya Jarh na Ta’adiyl.[1]
Shaykh Al-Albaaniy vilevile ni hoja katika elimu ya
Mustwalahul-Hadiyth.[2]
Na wanachuoni wamemsifu na kumwelezea kwamba kwa elimu yake hiyo, karejesha
kumbukumbu za zama za kina Imaam Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy, Ibn Kathiyr na
wengineo miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa fani hiyo.
Alikuwa na kumbukumbuku kali ya kuweka vitu
kichwani na kuhifadhi mengi. Kumbukumbu inayotukumbusha wema waliotangulia kama
kina Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) na waliofuatia kama Imaam
Al-Bukhaariy, Imaam Ash-Shaafi’y, Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyah, Imaam Ibn
Kathiyr, Imaam An-Nawawy na wengineo (Allaah Awarehemu wote).
KUZALIWA NA KUKUA KWAKE
Alizaliwa mwaka 1332H – 1914H katika mji wa
Ashkodera ambao kwa wakati huo ulikuwa ni mji mkuu wa
Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy alianza
masomo yake ya awali katika madrasah ya Al-Is’aaf Al-Khayriyah hapo
KUJIFUNZA KWAKE ELIMU YA HADIYTH
Alitunukiwa shahada ya juu ya
elimu ya Hadiyth kutoka kwa Shaykh Raaghib At-Twabbaakh, mwanachuoni mkubwa wa
Halab katika wakati huo. Hapo ni wakati alipokutanishwa naye kupitia Shaykh
Muhammad Al-Mubaarak ambaye alimjulisha Shaykh At-Twabbaakh kuhusu kijana huyo
(Al-Albaaniy) jinsi alivyokuwa mahiri katika elimu ya Hadiyth. Na baada ya
Shaykh At-Twabbaakh kumjaribu na kulithibitisha
Aliingia kwenye fani hiyo ya Hadiyth akiwa na miaka
ishirini. Aliathirika
Hapo ndipo ilipoanza safari ndefu ya kusoma vitabu
mbalimbali. Nikatolesha nakala ya maudhui hiyo iliyofanyiwa uchambuzi wa kina
katika jarida
Shaykh Al-Albaaniy alijifunza pia kwa baba yake
elimu ya kutengeneza saa hadi akawa fundi mzuri maarufu kwa kazi hiyo. Ikawa
ndiyo kazi impatiayo rizki yake ya halali. Akiwa ni fundi na hapo hapo ni mtafutaji
elimu. Hali hiyo ikaendelea hivyo hadi alipoamua kutenga siku mbili tu za
kufanya kazi hiyo ya utengenezaji wa saa kwa ajili ya kupata rizki yake, na
siku zote zilizobaki zikawa ni za kutafuta elimu. Elimu hiyo alikuwa
akiichukulia katika maktaba kubwa ya mji huo wa
Elimu ya Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) zilikuwa zina athari kubwa
Na kwa sababu hiyo ndivyo alivyoanza kuyaacha na
kuyaweka pembeni madhehebu ya Kihanafi aliyokulia nayo na aliyosomeshwa na baba
yake. Na alikuwa baba yake (Allaah Amrehemu) akivutana
VITABU VYAKE
Maktaba za Kiislam zimeneemeka kwa vitabu vingi vya
Shaykh haswa vile vikubwa vyenye mijalada mingi vya ‘Silsilatul Ahaadiyth
Asw-Swahiyhah’ na ‘Silsilatul Ahaadiyth Dhwa’iyfah wal Mawdhuw’ah’ na kitabu
chake cha Swalah kiitwacho ‘Swiftatus Aswalaat An-Nabiy’ ambacho kimepokelewa
kwa nguvu
Pia Shaykh ana vitabu maarufu sana vya Hadiyth
vyenye kuvifanyia sharh, tahkiki, na hata kubainisha yale ya sahihi na ya
dhaifu ndani ya vitabu hivyo, kama alivyofanya kwenye vitabu Sunnan
At-Tirmidhy, Sunnan Ibn Maajah, Sunan Abu Daawuud n.k. Vilevile ana mijalada
mingi ya vitabu
Kazi zake za uandishi kuhusu masuala ya Hadiyth zinazidi
zaidi ya mia.
Baadhi ya vitabu vyake
vilivyoenea sana ni:
1- Silsilatu Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (Mijalada
1-11)
2- Silsilatu Ahaadiyth Adhw-Dhw’iyfah wal
Mawdhuw’ah (Mijalada 1-14)
3- Al-Irwaa Al-Ghaliyl (Mijadala 1-9)
4- At-Targhiyb wa Tahiyb (Mijalada 1-4)
5- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan Abu Daawuud
(Mijalada 1-4)
6- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan At-Tirmidhy
(Mijalada 1-4)
7- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan Ibn Maajah
(Mijalada 1-4)
8- Mukhtaswar Swahiyh Al-Bukhaariy
9- Mukhtaswar Swahiyh Muslim
10- Sharhu Al-‘Aqiydah Atw-Twahaawiyah
11- Ahkaam Al-Janaaiz
12- At-Taswul: Anwa’uhu wa Ahkaamuhu
13- Kitaabu As-Sunnah
14- Swalaatu At-Taarawiyh (Qiyaamu Ramadhwaan)
15- Tamaamul-Minnah Fiyt-Ta’aliyq ‘Alaa
Fiqhis-Sunnah
16- Ghaayatul-Maraam Fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal
wal Haraam
17- Adaabu Az-Zafaaf [4]
18- Swifatu Asw-Swalaatin-Nabiy[5]
KUENEZA KWAKE ELIMU
Na baada ya Al-Imaam, Al-Muhadith, Shaykh Abu
‘Abdir-Rahmaan Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy kupata elimu yake akaanza kuwasiliana
na watu kwa ajili ya kueneza Da’awah. Alibeba bendera ya Tawhiyd na Sunnah, na
akatembelea Mashaykh wengi waliopo
Hali hiyo ya kusimamia haki na kupambana na batili
ilimjengea Shaykh heshima kubwa na vipenzi wengi ingawa pia hawakukosekana
wapinzani wasiotaka haki. Waliompinga ni wale wenye kufuata hawaa za nafsi zao,
kasumba za kimadhehebu, mapenzi ya bid’ah na wapinzani wa Sunnah za Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na Mashaykh wa aina hiyo
walijaribu kumpinga na kumtilia fitna serikalini na kusababisha Shaykh kutiwa
jela mara kadhaa, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1967M kwa muda wa mwezi mmoja,
na kisha akaja kufungwa tena kwa muda wa miezi sita.
Kilipoanzishwa chuo kikuu cha Madiynah Al-Munawarah
huko Saudi Arabia, mwanachuoni mkubwa huko, Shaykh Muhammad Ibraahiym Aalu
Shaykh aliyekuwa Rais wa baraza la Maulamaa na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho,
alimchagua Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni mwalimu wa elimu ya Hadiyth na vigawanyo
vyake katika chuo hicho.
Miongoni mwa athari zake Shaykh Al-Albaaniy,
aliweka msingi na kanuni ya fani la somo la elimu ya ‘Isnaad’ na akawa
ndiye wa kwanza kabisa kufanya hivyo katika vyuo vyote vya Kiislam, na chuo cha
Madiynah Al-Munawarah kikawa ni kinara cha vyuo vingine kwa
Tukio
Uongozi wa chuo ulimlazimisha Shaykh kulaani
kitendo hicho, lakini Shaykh hakutoa kauli yoyote kuhusu tukio
Hata hivyo, baada ya miaka kadhaa wakamuomba tena
arejee nchini Saudia na kufundisha tena, na Shaykh bila kuwa na kinyongo kwa
dhulma aliyofanyiwa awali, aliitikia wito huo na kurejea na kufanya kazi yake
kwa Ikhlaasw kubwa. Haukupita muda akasimamishwa tena!
Pamoja na matukio hayo, inatubainikia wazi kuwa
Shaykh hakuwa ni
SAFARI ZAKE
Shaykh (Allaah Amrehemu) alihama kutoka
Katika kukaa kwake hapo
Akarejea tena Damascus na ziara yake ya mwisho ya
nchi ya United Arab Emirates ilikuwa ni mwaka 1989M ambako alikwenda kukaa nje
ya mji kwenye Jumuiya ya Daarul-Birr kwenye shamba la kiongozi wa Jumuiya hiyo
na kufanya darsa zake mbalimbali hapo katika msikiti uliokuwepo hapo ambao
baadaye ulipewa jina la Shaykh kwa kumbukumbu za ziara zake za kielimu hapo, na
pia kuuenzi mchango wake na elimu yake kubwa.
Katika mwaka 1419H, mwaka mmoja kabla ya kifo
chake, Waislam duniani walifarijika kuona Shaykh akitambuliwa kimataifa kwa
kupewa tunzo kubwa la kielimu na mchango katika Dini, itambulikanayo kama,
‘Tunzo La Mfalme Fayswal La Kimataifa’. Ambalo kinatolewa kila mwaka katika
mchango wa nyanja mbalimbali za jamii, na kwa upande wa Dini hutolewa kwa yule
mwanachuoni mkubwa katika Ummah wa Kiislam katika elimu maalum ya Dini. Na
mwaka huo Ash-Shaykh, Al-Imaam, Al-Muhadith, Al-‘Alaamah Al-Albaaniy (Allaah
Amrehemu) alitunukiwa jaiza hiyo kwa mchango wake mkubwa wa elimu ya Hadiyth na
vigawanyo vyake.
Tunzo
Hiyo itakumbukwa na wengi kuwa ilikuwa ni hadhi
kubwa ya heshima ya kuukubali mchango wake wa Dini hii aliyopewa na nchi ya
Saudi Arabia pamoja na kwamba walimfukuza nchini humo mara mbili kutokana na
msimamo wake thabiti usioyumba wa kusimamia Al-Kitaab (Qur-aan) na As-Sunnah
pamoja na misimamo yake mingine ya kielimu iliyokuwa ikipingana na Mashaykh wa
Saudiyah. Alikuwa anajali zaidi kumridhisha Mwenyeezi Mungu tu Pekee. Pamoja na
hivyo, Mashaykh wa Saudiyah walikuwa wakimheshimu
UPINZANI
Mmoja katika waliokuwa wakikesha kumpiga vita
Shaykh, ni mwanachuoni wa Kisufi aitwaye ‘Aliy bin Hasan As-Saqaaf ambaye
alikuwa huko
As-Saqaaf alitunga vitabu kumkosoa Shaykh kwenye masuala
ya Hadiyth, na pia baada ya yeye kuona mafanikio makubwa ya kuenea na
kununuliwa kwa wingi kitabu cha Shaykh kiitwacho ‘Swifatus-Swalaat An-Nabiy’,
As-Saqaaf akaandika kitabu dhidi ya hicho! Hata hivyo, vitabu vyake vilijibiwa
kielimu
As-Saqaaf licha ya kumshambulia Shaykh Al-Albaaniy,
vilevile kuna mengi kayaandika kwenye vitabu vyake kushambulia baadhi ya
Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum).[6]
Shaykh Al-Albaaniy katika sifa zake kubwa ni
kukabiliana na wote wanaopingana naye na kufanya nao mijadala yenye hoja na
dalili. Na hivyo ndivyo alivyofanywa kwa Shaykh As-Saqaaaf. Alikwenda nyumbani kwa
Shaykh As-Saqaaf baada ya mapatano ya kwenda kujadili mada kuhusu ‘At-Tawasul’,
na alipofika kwake akakuta kinyume na alivyotarajia kwa kudhani kuwa Shaykh
As-Saqaaf ni katika ‘wajukuu wa Mtume’ kama ajiitavyo, ingawa vitendo
alivyovikuta – kama anavyosema mwenyewe – havikuwa kama vya babu yake [yaani
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)], kwani vitendo vyake
vilikuwa vya kiburi, ukubwa, ufakhari na kupenda kutukuzwa.
Shaykh Al-Albaaniy alipotaka waanze mjadala huo
uliomleta hapo, As-Saqaaf akawa anazunguka huku na kule kwa mada zingine bila
kuzungumzia walichopanga awali. Na Shaykh kwa utulivu, alivumilia yote na
mwisho kuondoka bila kufikia alilolifuata. Na baada ya hapo, Shaykh As-Saqaaf
akawa anamtukana Shaykh Al-Albaaniy kwenye kanda, vitabu na majukwaani. Shaykh
Al-Albaaniy hakuwahi kumtukana wala kuandika vitabu vya kumtukana
Tukio moja lilinidhirishia utukufu wa hali ya juu
Shaykh aliwapokea vizuri
Huo ni mfano wa mwanachuoni wa aina ya nadra
Vilevile Shaykh Al-Albaaniy aliwahi kujadiliana na
mahasimu zake wengine kama Shaykh Ramadhaan Al-Buuti ambaye anapinga
UHUSIANO WAKE NA WANACHUONI
Imaam Al-Albaaniy alichunga
Mifano mizuri ya hili, ni barua zake kwa Mashaykh
maarufu kama Shaykh Muhammad Mitwaliy Ash-Sha’arawiy (Allaah Amrehemu)
aliyekuwa Misr, Shaykh Sayyid Saabiq (Allaah Amrehemu) aliyekuwa Misr vilevile,
Shaykh Yuusuf Al-Qaaradhwaawiy (Mmisr) ambaye hivi sasa ni Mufti wa nchi ya
Qatar na kiongozi wa Umoja wa Maulamaa Duniani. Pia aliwahi kukutana nao uso
kwa uso.
Vile vile aliandika vitabu vya kusahihisha Hadiyth
zilizomo kwenye vitabu vya Mashaykh hao.[9]
Pia alikuwa anawasiliana na Mashaykh wakubwa wa Saudia
FADHILA NA MEMA YAKE
Shaykh Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) alikuwa ni
mwenye kufuata mwenendo wa watangu wema (Salafus-Swaalih), akifuata
matendo
Alikuwa hastahi katika haki, akiitangaza haki
katika vitabu vyake na mihadhara yake. Na hii ni sifa ya nadra
Sifa hiy ndio waliyokuwa nayo Maimaam wanne wa
Sunnah, ambao misimamo
Walikuwa na kauli nyingi kuhusu hayo, hapa
nitaziorodhesha chache:
Imaam Abu Haniyfah (Allaah Amrehemu)
"Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni sahihi, basi
hiyo ndiyo madhehebu yangu" "Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kukubali rai
zetu ikiwa pindi hawatojua wamezipata kutoka wapi".[10]
Katika riwaya nyingine: "Imekatazwa mtu ambaye
hajui dalili zangu kutoa hukmu kutokana na maneno yangu"
Katika riwaya nyingine imeongezwa: "….Kwani
sisi ni wanaadamu, tunasema jambo siku moja na kulirudisha siku ya pili
yake".
Imaam Maalik naye (Allaah Amrehemu)
"Hakika mimi ni mwanaadamu: Ninafanya makosa
(mara nyingine) na ninakuwa sahihi (mara nyingine). Kwa hiyo, tazameni rai
zangu: zote ambazo zinakubaliana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, zikubalini; na
zote ambazo hazikubaliani na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, basi zipuuzeni".[11]
Imaam Ash-Shaafi’iy (Allaah Amrehemu)
"Ukiona katika maandishi yangu jambo ambalo ni
tofauti na Sunnah ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), basi
zungumza kwa kurejea Sunnah ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) na acha niliyoyasema mimi"
Katika usimulizi mwengine: " …basi ifuate
(Sunnah) na usitazame tena pembeni kufuata usemi wa mwingine yeyote"[12]
Na akasema:
“Hadiyth ikipatikana kuwa ni sahiyh, basi hiyo ndio
madhehebu yangu"[13]
Imaam Ahmad bin Hanbal (Allaah Amrehemu)
Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au
Ash-Shaafi'iy au ya Awzaa’iy, wala Thawriy, lakini chukueni kutoka
walikotoa"[14]
Na sifa hii ndio iliyomfanya Shaykh kupendwa na
kupata wafuasi wengi kila pande ulimwenguni. Na ndiyo iliyomfanya kupata wenye
chuki dhidi yake.
Shaykh ameacha athari kubwa katika elimu ya Hadiyth
hadi imefikia sasa wanachuoni wengi wanapotaja Hadiyth basi hawaachi kutaja
usahihi au udhaifu wa Hadiyth hiyo kwa mujibu wa uchambuzi wake.
Alikuwa haachi kufunga Swawm za Sunnah haswa za
Jumatatu na Alkhamiys katika maisha yake ila tu alipokuwa safarini.[15]
Nyumba yake ilikuwa ‘ingia toka’ ya watu wa kila
aina waliokuwa wakija kwake kutafuta elimu, kuuliza masuala ya Dini, kutatuliwa
masuala ya kijamii, kifamilia, na hata kuhitaji misaada mbalimbali pamoja na
kuwa hali ya Shaykh ilikuwa ya wastani, hata hivyo, alikuwa haachi kuwasaidia
wanaomfuata kwa shida.
Shaykh alikuwa baadhi ya nyakati akitaja jinsi
alivyokuwa siku za nyuma akiokota makaratasi njiani au kadi zilizotupwa au
kupekua kwenye sehemu zilitupwa karatasi ambazo alikuwa akizitumia kuandikia
Hadiyth. Yote ni kutokana na hali ya umaskini na shida kwa kutokuwa na uwezo wa
kununua madaftari ya kuandikia.
Alikuwa akichunga
Sifa yake ya kujifunza ilikuwa haina mithali!
Alikuwa akitumia zaidi ya masaa kumi na nane (18) kwa siku katika maktaba yake
kupitia na kufanya rejea mbalimbali, kutafiti na kuandika! Muda aliokuwa
akikatisha masomo yake na utafiti wake ulikuwa ni wa kuswali na kula kidogo.
Waliobahatika kukutana na Shaykh wanashuhudia
utaratibu wake na heshima yake na ucha Mungu wake wa hali ya juu. Alikuwa
haachi fursa bila kumfundisha mtu kitu kipya au kumkosoa makosa yake kwa
utulivu na busara. Siku moja alipokuwa Hospitali amelazwa, Daktari aliyekuwa
amenyoa ndevu zake zote akaingia na kumpa dawa na baada ya kumaliza akiwa
anaondoka, akamuomba Shaykh amuombee Du’aa, Shaykh akaomba na kusema “Namuomba
Allaah Akupendezeshe kwa kile kinachompendeza mwanaume”
[Makusudio ya Shaykh hapa yalikuwa ni kuwa yule
Daktari apendezeshwe kwa kuongozwa kuweka ndevu, kwani ni jambo lililosisitizwa
Alikuwa Shaykh kila alfajiri akipita na gari
Kwa kuchelea kwake ‘Riyaa’, wakati mmoja alijiwa na
ujumbe wa watu kutoka
Alikuwa akiendesha baiskeli yake kutoka
Alikuwa akiingia msikitini siku ya Ijumaa, akiswali
Raka’ah mbili mbili za Naafilah (Sunnah) na akiendelea hadi Khatwiyb
atakapopanda minbar kuanza kutoa Khutbah.[18]
Shaykh inasemekana alikuwa katika daraja ya Al-Haafidh
(Mwanachuoni wa Hadiyth aliyehifadhi Hadiyth laki moja (100,000) pamoja na
mnyororo wa wapokezi wake na ‘mutuun’ zake (maneno ya kila Hadiyth).
Hayo yanaelezwa na Shaykh ‘Ashiysh aliyemuuliza suala
Katika wasia wake Shaykh alitoa hadiya maktaba yake
ya vitabu na kazi zake za uandishi kuitunuku Chuo Kikuu Cha Madiynah Al-Munawarah
kama anavyosema katika wasia wake: “Nimeiachia maktaba yangu – vyote vilivyomo,
vikiwa ni vilivyochapishwa tayari, au nakala, au kazi nilizoziandaa
kuchapishwa; kwa maandishi ya mkono wangu, au ya mwengine aliyeniandikia – kwa
kuipa maktaba ya Jaami’atul-Islaamiyah (Chuo Cha Kiislam) kilichopo
katika mji wa Madiynah Al-Munawarah. Kwa sababu ni kumbukumbu nzuri na chuo
hicho wakati nilipokuwa huko nikifundisha, kwa kulingania kwake kwa msingi wa
Kitaab (Qur-aan) na Sunnah kwa kufuata mwenendo (Manhaj) wa wema
waliotangulia (Salafus-Swaalih)”.[20]
Alikuwa hapendi kuitwa mwanachuoni na mara nyingi
akijiita ‘Twaalibul-‘Ilm’ Mtafutaji elimu.
Siku moja mwanamke kutoka
Shaykh alipambana na kila aina ya upotofu na moja
ya aliokumbana nayo ni mtu mwenye kudai utume. Kwa utulivu bila hasira wala
kutaka kumlaani na kumshambulia pamoja na kuwa ni dai la ukafiri ulio wazi.
Shaykh alimsikiliza kwa makini na kumuuliza maswali na kuzikatakata hoja zake
hadi mwisho baada ya masaa, yule mtu akaomba Tawbah kwa Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala). Unaweza kusikiliza mjadala huo hapa.[22]
Alijiwa na watu waliokuwa wakimtukana na kumuita
kafiri, na bila kukasirika na kugombana nao akajadiliana nao kwa upole na
mapenzi na ilipofika wakati wa Swalah wakakataa kuswalishwa naye, yeye
hakukasirika bali aliomba mmoja wao aswalishe na yeye atamfuata! Baada ya
Swalah hiyo wakaendelea na mjadala na ilipofika Swalah nyingine, wao wenyewe
wakamuomba Shaykh awaswalishe!! Akawa kwao si kafiri tena, bali mwanachuoni
mwenye kuheshimiwa kabisa na wao.
Alikuwa mtu wa kawaida
Katika
kipindi cha maisha yake, alifanya tafiti nyingi na kuzichambua taqriban nyororo
30,000 za wasimulizi wa Hadiyth (isnaad) za Hadiyth zisizo na idadi,
akiwa ametumia kiasi cha miaka 60 ya umri wake kusoma na kupitia vitabu vya
Sunnah na kuwa karibu navyo kwa muda wote huo, na mawasiliano ya nyanja hiyo,
na pia kuwa karibu na Maulamaa wa elimu hiyo.[23]
Wanachuoni
wengi walimuheshimu
Aliwaheshimu
[Kwake Allaah tumetoka na Kwake ndio
tutarejea. Ee Allaah, nilipe kwa msiba wangu huu na nibadilishie bora kuliko
hicho (ulichokichukua)]
Hii ni Du’aa inayoombwa na yule aliyepewa taarifa ya kifo
KIPINDI CHA MWISHO CHA MAISHA YAKE
Shaykh (Allaah Amrehemu) hakutulia kutafuta elimu
hadi umri wa miaka 86, akisoma, akifundisha, akielimisha akiandika vitabu,
akiandika barua kwa wanachuoni wenzake kuwapongeza, kuwanasihi, kuwakosoa
makosa ya vitabuni mwao au fatwa zao. Hakuwa hadi umri huo akiacha kutafiti
masuala ya Hadiyth, akipangua sahihi na dhaifu na za kutungwa, aliweza kuvigawa
vitabu vingi vikubwa vya Hadiyth kama vya Maimaam Abu, Dawuud, Ibn Maajah,
At-Tirmidhy, An-Nasaaiy na wengineo, akaweza kuvigawa Sahihi zake na Dhaifu
zake na kuwasaidia kuwarahisishia wenye elimu na wanafunzi katika uandishi wao
na katika tafiti zao.
Shaykh ameshukuriwa sana kwa kazi hiyo iliyosaidia
Ummah leo hii, na kuamsha Ummah leo kujua Hadiyth sahihi na dhaifu na pia
kuwafanya wengi wapate kuwa karibu na kuifuatilizia elimu ya Hadiyth na sayansi
yake. Aliyafanya yote hayo – kwa sababu
moyo wake ulikuwa umefungamana nayo hayo kwa mapenzi ya juu – na hakuacha hadi
taqriban miezi miwili ya mwisho ya maisha yake, alipokuwa dhaifu akiugua
kitandani. Pamoja na magonjwa mazito yaliyomdhoofisha
KIFO CHAKE NA JINSI KILIVYOATHIRI
UMMAH
Alizikwa siku hiyo hiyo aliyofariki, pamoja na kuwa
alizikwa usiku, lakini idadi ya watu ilikuwa kubwa kuweza kuzidi maelfu kwa
maelfu. Aliswaliwa katika ‘Muswallaa’ (Eneo la wazi la kuswaliwa nje ya
msikiti)
Wanachuoni, watafuta elimu, wanafunzi, na watu wa
kawaida wote waliathirika
WANAFUNZI WAKE MAARUFU
Wanafunzi wake ni
wengi mno na miongoni mwao maarufu katika Mashaykh ni hawa ambao baadhi
Shaykh Muqbil
bin Haadiy Al-Waadi’iy (
Dkt. ‘Umar
Sulaymaan Al-Ashqar (
Shaykh ‘Aliy
Hasan ‘Abdul-Hamiyd Al-Halabiy (Jordan)
Shaykh Saalim
Al-Hilaaliy (Palestina)
Shaykh Hamdiy
‘Abdul-Majiyd
Shaykh Muhammad
‘Iyd ‘Abbaasy
Shaykh Muhammad
Ibraahiym Shaqrah (
Shaykh ‘Aliy
Khushshaan
Shaykh Muhammad
Jamiyl Zaynuu (
Shaykh
‘Abdur-Rahmaan ‘Abdus-Swamad
Na waliojifunza
kwake kwa njia isiyo ya moja kwa moja ni:
Shaykh Muhammad
Hasaan (Misr)
Shaykh Abu
Is-haaq Al-Huwayniy (Misr)
SIFA NJEMA WALIZOTOA MAULAMAA KWA
MUJADDID WA ENZI HII SHAYKH MUHAMMAD NAASWIR-UD-DIYN AL-ALBAANIY (ALLAAH
AMREHEMU)
SHAYKH ‘ABDUL-‘AZIYZ BIN BAAZ [ALIYEKUWA
MUFTI WA
Sikumuona mtaalamu wa Hadiyth za Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika enzi yetu ya leo chini ya qubah la mbingu
"Mwenyezi
Mungu Hutuma kwa Ummah huu mwanachuoni katika kila miaka mia mtu wa kupiga
msasa mambo ya dini Yake".[26] Aliulizwa ni
nani mpiga msasa wa karne hii? Akajibu: Ninadhani Shaykh Muhammad
Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ndiye mpiga msasa
wa enzi hii. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
MWANACHUONI MKUBWA MUHAMMAD IBN
SWAALIH
Yale niliyoyajua kuhusu
Shaykh na ambayo ni kidogo wakati nilipokuwa nakutana naye, ni kuwa yeye ana
shime ya hali ya juu ya kutumia Sunnah na kupiga vita bid’ah; sawasawa katika
‘Aqiydah au matendo. Ama kwa kusoma kwangu vitabu vyake, hakika nimemjua vyema
kwa hayo. Yeye ana elimu kubwa ya Hadiyth kwa upande wa Riwaayah na Diraayah,
na Mwenyezi Mungu Amewanufaisha watu wengi kutokana na yale aliyoyaandika kwa
upande wa elimu, mfumo na mwelekeo katika taaluma ya Hadiyth. Na hii ni faida
kubwa
MWANACHUONI MKUBWA MFASIRI
MUHAMMAD AL AMIYN ASH-SHANQIYTWY (ALLAAH AMREHEMU)
Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz
Al-Haddaah anasema:
"Hakika Mwanachuoni
mkubwa Ash-Shanqiytwy anamtukuza Shaykh Al-Albaaniy utukuzo wa kushangaza.
Anapomuona anapita nailhali yeye yuko katika darsa yake katika Msikiti wa
Madiynah, husimamisha darsa lake, husimama na kumsalimia kwa ajili ya
kumuheshimu".
MTUKUFU SHAYKH ‘ABDUL-MUHSIN
AL’ABAADIY (ALLAAH AMHIFADHI)
Bila shaka Shaykh
Al-Albaaniy, alikuwa ni katika Maulamaa wa kipekee walioumaliza umri wao katika
kuitumikia Sunnah, kuitungia vitabu, kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,
kuinusuru ‘Aqiydah ya kisalafiya, kuipiga vita bid'ah, na kuitetea Sunnah ya
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Yeye ni katika Maulamaa
wazuri wenye sifa za kipekee. Sifa zake zimeshuhudiwa na watu maalumu na watu
wa kawaida. Na hakuna shaka yoyote kwamba kumpoteza mwanachuoni
SHAYKH ‘ABDULLAH AL-UBAYLAAN
(ALLAAH AMHIFADHI)
Ninajipa pole mwenyewe, na
ninawapa pole ndugu zangu Waislamu kote duniani kwa kufariki Imaam Mwanachuoni
Mkubwa Mhakiki Mcha Mungu Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy. Ukweli
ni kwamba maneno hayawezi kumzungumzia mtu huyu. Ninachoweza kukisema ni kuwa
yeye hakukulia katika mazingira ya kisalafiya, lakini pamoja na hivyo, amekuwa
ni katika walinganiaji wakubwa wa usalafiya, na kufanya mambo kwa mujibu wa
Sunnah, na kutahadharisha mambo ya bid'ah. Hata Shaykh wetu ‘Abdullah
Ad-Duwaysh anayezingatiwa kuwa ni katika wahifadhiji wachache
MUFTI WA ZAMANI WA SAUDIA
MWANACHUONI MKUBWA SHAYKH MUHAMMAD BIN IBRAAHIYM AAL SHAYKH (ALLAAH AMREHEMU)
Anasema kuhusu Shaykh
Al-Albaaniy (Mwenyeezi Mungu Amrehemu): "Yeye ni mwana Sunnah, mpiganiaji
haki, na mwenye kupambana na watu wasiofuata haki".
MWANACHUONI MKUBWA SHAYKH ZAYD BIN
FAYYAADH (ALLAAH AMREHEMU)
Hakika Shaykh Muhammad
Naaswiru-ud-Diyn Al-Albaaniy ni katika Maulamaa wakubwa waliochomoza katika enzi
hii. Yeye alizishughulikia Hadiyth, njia zake, wapokezi wake na kiwango chake
cha kuwa ni sahihi au si sahihi. Na hii ni kazi kubwa ya kheri iliyomaliziwa
masaa na kutolewa juhudi kubwa. Na yeye ni
MWANACHUONI MKUBWA SHAYKH MUQBIL
AL-WAADI'IY (ALLAAH AMREHEMU)
Hakika katika taaluma ya
Hadiyth, hakuna mtu
((Mwenyezi Mungu
Hutuma kwa Ummah huu mwanzoni mwa kila miaka mia mtu wa kupiga msasa mambo ya
Dini Yake)).[27]
MWANACHUONI
MKUBWA WA MISR MUHIBUD-DIYN AL-KHATWIYB (ALLAAH AMREHEMU)
“Na katika walinganiaji wa
Sunnah ambao wametoa maisha
MWANACHUONI MKUBWA WA HADIYTH
Katika moja ya barua walizokuwa wakiandikiana na
Shaykh Al-Albaaniy katika masuala ya kitafiti ya Hadiyth, alikiri kuwa Shaykh
Al-Albaaniy ni mwanachuoni mkubwa kabisa wa Hadiyth.
MWANACHUONI MKUBWA HAMUUD BIN
ABDULLAH AT-TUWAYJIRIY (ALLAAH AMREHEMU)
Al-Albaaniy kwa sasa ni
bendera juu ya Sunnah. Kumkosoa yeye ni
PROFESA AMIYN AL-MISRIY (ALLAAH
AMREHEMU) ALIYEKUWA MKUU WA KITENGO CHA MASOMO YA JUU KATIKA CHUO KIKUU CHA
KIISLAMU
Ni moja kati ya mikosi ya
dunia hii kuchaguliwa watu
NA KATIKA WALIOMSIFU BAADA YA KUFA
KWAKE NI:
WAZIRI WA MASUALA YA KIISLAMU,
AL-AWQAAF, ULINGANIO NA UONGOZI SHAYKH SWAALIH BIN ‘ABDUL-‘AZIYZ BIN MUHAMMAD
AALU SHAYKH
Alisema: "Shukrani ni za
Mwenyezi Mungu kwa hukumu Zake na uwezo Wake ((Hakika
sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea)).[28]
Hakuna shaka kwamba kumpoteza Mwanachuoni Mkubwa Shaykh Muhammad
Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ni msiba. Kwani yeye ni katika wanachuoni wakubwa
wa Ummah na mabingwa wa Hadiyth. Kwa Maulamaa hao (Shaykh Al-Albaaniy),
Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameilinda Dini hii na Akaieneza Sunnah kupitia
kwao…."
KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA
ULIMWENGU WA KIISLAMU HUKO MAKKAH AL-MUKARRAMAH SHAYKH DKT. ‘ABDULLAH BIN
SWAALIH
Hakuna shaka yoyote kwamba
kufariki Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ni hasara kubwa kwa Ummah
wa Kiislam. Vielelezo vya ushahidi na michango yake ni mingi na mikubwa kupitia
elimu yake katika taasisi kubwa za Kiislam
TUME YA KUDUMU YA TAFITI ZA
KITAALUMA NA UTOAJI FATWA
SWALI: Siku hizi watu
wanazungumza
JIBU: Mtu huyu anajulikana kwetu kwa elimu yake, mchango
wake, kuitukuza kwake Sunnah na kuitumikia. Pia anajulikana kwa kuunga kwake
mkono madhehebu ya Ahlus-Sunnah wal Jama’ah katika kutahadharisha ukasumba, na
ufuataji bila dalili, na vitabu vyake vyenye faida. Lakini yeye kama walivyo
Maulamaa wengineo, si mtu aliyetakaswa na makosa. Yeye anakosea na kupatia.
Tunamtarajia alipwe thawabu mbili katika alilolipatia, na thawabu moja ya
kujitahidi akikosea kama ilivyothibiti toka kwa Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kuhukumu anapohukumu
akajitahidi na akapatia, basi ana thawabu mbili, na anapohukumu akajitahidi na
akakosea, basi ana thawabu moja)). Tunamuomba Allaah Atupe sisi
tawfiyq, nyinyi na yeye, tuweze kusimama imara mbele ya haki na kuepukana na
vipotoshi vya fitna. Kwa Allaah ndio tawfiyq. Na Rehma ziwe juu ya Nabii wetu
Muhammad, Ahli zake na Maswahaba wake.[29]
TENZI KUMHUSU
SHAYKH AL-ALBAANIY
Hakika anayeinusuru Sheria ya
Mola wetu,
hunusuriwa kama ulivyosema
wahyi.
Na hakika tumemwona mhakiki wa
enzi yetu,
naye ni mwanachuoni wa Hadiyth
Naaswir Al-Albaaniy.
Ni yule ambaye wewe umekamia kumpinga,
ewe dhalimu, achana na uasi.
Watu waliokasumbika na
kushabikia madhehebu,
na kwa Manhaj na ‘Aqiydah ya
kikuhani…
Watu waliokasumbika na
kushabikia madhehebu,
na kwa kazi yenye mabaki yasiyosalia…
Wote hao wametangaza hasira zao,
kwa kutukana na kuchafulia watu heshima katika
ardhi.
Qiyaamah chao kimewaka moto na wote wamesimama,
lakini Shaykh Naaswir amesimama imara ngangari.
Ameeneza elimu bora kabisa katika enzi yetu,
ameeneza Sheria ya Ar-Rahmaan.
Hakulifanyia kasumba wala kulishabikia dhehebu
lolote,
bali amewasifu na kuwapa haki zao Maimaam wote
waliomtakasia Ar-Rahmaan.
Ingawa mahasidi na wenye chuki wamesema mbovu,
lakini hata hivyo, Mwenyezi Mungu Amewanufaisha
watu kwa elimu yake.
Wamesema yeye ni mshairi, mimi
nikasema nampenda,
na hususan kwa Naaswir Al-Albaaniy.
Ni bendera ya wakati wetu, basi siwezi kuishusha na
kuidharau haki yake,
ni Shaykh wa Mashaykh, mwenye akili ya kimola.
Yeye ndiye mkarabati wa zama,
na hakika imekuja, habari sahihi inayoishilia kwa
aliye karibu.
Nyakati zote yeye ni mwalimu,
anayelingania Sheria ya Mola wetu Ar-Rahmaan.
Yeye ndiye Imaam
sina shaka kabisa, na naapa kwa Yule Aliyeniumba.
Naye ndiye amekuwa ni wa kipekee katika wakati
wake,
kwa Fiqh, Hadiyth na Qur-aan.
Ameitetea na kuipigania
mteuliwa na mchaguliwa.
Ni Bid’ah ngapi alizozipiga vita,
bid’ah zilizoupakaza uso wa dini yetu kwa adha na
fitina.
Analingania Tawhiyd na Ucha Mungu,
ameshasema mara nyingi
Kwani hiyo ni faradhi, wajibu
na lazima,
hatuwezi kuongoka tukimfuata
mwingine ikiwa amali zitafaa katika mizani.
TANBIHI KUTOKA KWA MWANDISHI WA
HISTORIA HII
Pamoja na kuwa Shaykh Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu)
alikuwa ni mwanachuoni wa aina yake, na hoja katika Ummah katika elimu ya
Hadiyth, ila ni muhimu tusisahau kuwa alikuwa ni mwanaadam na hupata na
kukosea. Hatupaswi kufanya
Hatutoweza kumsahau kwa wepesi Shaykh wetu huyu
mtukufu, kwa elimu yake inayowanufaisha mamilioni leo hii na itakayowanufaisha
vizazi kwa vizazi hadi siku ya mwisho. Allaah Amrehemu na Amwandalie nyumba
bora huko katika pepo Yake ya Firdaws inshaAllaah. Aamiyn
[1] Ni fani ya Hadiyth inayohusiana na
uaminifu wa wasimulizi wa Hadiyth na inakusanya habari zao zinazothibitisha
uaminifu au udhaifu wa hao wasimulizi.
[2] Sayansi ya Hadiyth
[3] Hayaatul Al-Albaaniy, Muhammad
Ash-Shaybaaniy. Al-Albaaniy mwenyewe anayeeleza hayo pia kwenye vitabu vyake ‘Mukhtaswar
Al-‘Uluww’ na ‘Tahdhiyrus-Saajid’.
[4] Kitabu hichi tumekwishakitafsiri kwa
Kiswahili na kiko katika kuchapishwa.
[5] Kinaandaliwa kwa lugha ya Kiswahili.
[6] Daf-u Shubuhaat At-Tashbiyh, uk.237
[7] Mawaidha na maswali na majbu ya Silsilatul
Hudaa wan Nuur
[8] Bid’atut-Ta’aswub Al-Madh-habiy,
Shaykh ‘Iyd Al-‘Abbaasiy. Na pia nakala ya mjadala huo unapatikana kwenye
mtandao.
[9] Tamaamul Minnah Fiy Takhriyj Ahaadiyth
Fiqhi As-Sunnah, Ghaayatul-Maraam
Fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal Haraam.
[10]
Ibnul-'Aabidiyn katika al-Haashiyah 1/63, na katika inshaa yake Rasm
al-Mufti 1/4 kutoka Mkusanyiko wa Insha za Ibnul-'Aabidyin. Shaykh Swaalih
Al-Fulaaniy katika al-Iyqaadhw al-Himaam, uk.62. Na hii imeelezewa na
Imaam Ibn 'Abdul-Barr kutoka Abu Haniyfah na kutoka kwa maimaam wengine".
[11] Ibn 'Abdul Barr katika Jaami'ul Bayaan Al-'Ilm,
2/32, ibn Hazm akinukuu kutoka kwake katika Usuul-Al-Ahkaam 6/149, na
hali kadhaalika Al-Fulaaniy, uk.72.
[12] Harawiy katika Dhamm Al-Kalaam 3/47/1,
Al-Khatwiyb katika Al-Ihtijaaj bi Ash-Shaafi'iy 8/2, Ibn 'Asaakir
15/9/10, An-Nawawiy katika Al-Majmuu' 1/63, Ibn al-Qayyim 2/361, na
Al-Fulaaniy, uk.100, usimulizi wa pili ni kutoka Hilyah Al-Awliyaa ya
Abu Nu'aym.
[13] Nawawi katika Al-Majmuu' 1/63,
Ash-Sha'raaniy 1/57, akitoa chanzo chake
[14] Al-Fulaaniy, uk.113, na Ibn Al-Qayyim
katika I'laam Al-Muwaqi’iyn.
[15] Samiyr bin Amiyn
Az-Zuhayriy, Muhadith Al-‘Aswr, uk.39.
[16] Samiyr bin Amiyn
Az-Zuhayriy, Muhadith Al-‘Aswr, uk.30.
[17] Shaykh Husayn Al-‘Awaaishah, Swafahaat
Baydhwaa Min Hayaati Shaykhina Al-Albaaniy, uk.38
[18] Samiyr bin Amiyn Az-Zuhayriy, Muhadith
Al-‘Aswr, uk.39.
[19] Shaykh Husayn Al-‘Awaaishah, Swafahaat
Baydhwaa Min Hayaati Shaykhina Al-Albaaniy, uk.40.
[20] Samiyr bin Amiyn
Az-Zuhayriy, Muhadith Al-‘Aswr, uk.78.
[21] Indama Bakaa Al-Albaaniy
(RahimahuLlaah) ÚäÏãÇ Èßì ÇáÃáÈÇäí ..! [ÑÍãå Çááå]
[22] Munaadhwarah Ma’a Rajul-id-Da’aa
An-Nubuwah ãäÇÙÑÉ ãÚ ÑÌá ÇÏÚì ÇáäÈæÉ
[23] Abu Hudhayfah: 20
Points Regarding Shaykh al-Albaanee
[24] Abu Hudhayfah: 20 Points Regarding
Shaykh al-Albaanee
[25] Swahiyh Muslim, Mjalada 2, Uk.632 (Mulhaq
Al-Aswaalah Fiy Wafaat Mujaddid Al-Qarn Wa Muhadith Al-‘Aswr, 25 Jumaadah
Al-Aakhirah 1420, Uk.3.
[26] Imepokewa na Abu Daawuud,
na imeelezewa kuwa ni sahihi na Al-‘Iraaqiy na wengineo
[27] Imepokewa na Abu Daawuud,
na imeelezewa kuwa ni sahihi na Al-‘Iraaqiy na wengineo.
[28] Al-Baqarah: 156
[29] Al-Lajnatud Daaimah
Lil-Buhuuth Al-‘Ilmiyah wal-Iftaa, Fatwa Fatwa
12/244.