MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO
Muhammad Faraj Salim Al Saaiy
Tembelea http://mawaidha.info
Faatwimah (Radhiya
Llaahu ‘Anha)
Al-Ahnaf Bin
Qays (Radhiya Llaahu ‘Anhu)
Sababu Za
Kuharibika Kwa Tabia
“Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” ni msemo maarufu, na wengine wanasema “Mtu huvuna kile
alichopanda”.
Watoto wetu ndio vijana wa
siku za mbele na viongozi wa mustakbal. Ni mababa wa
watoto watakaokuja baada yetu. Ukiwalea vizuri kwa
mafundisho mema, unalea umma uliochipukia katika malezi mazuri, tabia njema,
hekima pamoja na Tawhiyd. Umma unaostahiki kuuongoza
ulimwengu. Umma alioutaja Mwenyezi Mungu Aliposema:
ßõäÊõãú ÎóíúÑó
ÃõãøóÉò ÃõÎúÑöÌóÊú áöáäøóÇÓö ÊóÃúãõÑõæäó ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóÊóäúåóæúäó Úóäö
ÇáúãõäßóÑö æóÊõÄúãöäõæäó ÈöÇááøåö æóáóæú Âãóäó Ãóåúáõ ÇáúßöÊóÇÈö áóßóÇäó
ÎóíúÑðÇ áøóåõã ãøöäúåõãõ ÇáúãõÄúãöäõæäó æóÃóßúËóÑõåõãõ ÇáúÝóÇÓöÞõæäó
“Nyinyi ndio Umma bora kuliko Umma zote
zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na manakataza
yaliyo maovu na mnamuwamini Mwenyezi Mungu. Na
Aali ‘Imraan – 110
Mtoto mdogo aliyekuwa akitembea alijikuta yupo nje
ya mji karibu na pango, akaamua kukaa juu ya ardhi, na
kilipomjia kikohozi akaisikia sauti ya kikohozi chake kikimrudia mwenyewe
(mwangwi wake– echo-). Kwa vile ni mara yake ya
mwanzo kusikia sauti ikimrudia, akadhani kuwa pana mtoto mwengine upande wa
pili au ndani ya pango anajaribu kumwigiza.
Akauliza kwa ukali: “Nani
wewe?!
Sauti yake mwenyewe ikamrudia: “Nani! Wewe?”
“Nakuuliza
nani wewe?” Sauti ikamrudia tena
Akasema kwa ukali zaidi: “Nakuuliza
nani wewe usokuwa na adabu?”
Sauti ikamrudia tena kwa
maneno yale yale aliyotamka.
Mtoto alikasirika
Mama yake akamwambia: “Mwanangu,
huo ni mwangi wako mwenyewe. Ni sauti yako mwenyewe ikikurudia, na wala hapana mtoto aliyekuwa akikuigiza. Na
Mfano huu unafaa kutumika katika mambo mengi
Anasema mama wa Waislam
Bibi ‘Aaishah (Radhiya Llaahu ‘anha):
“Faatwimah (Radhiya Llaahu ‘anha), amefanana
Na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)
anapokwenda kumtembelea binti yake huyo nyumbani kwake, Bibi Faatwimah (Radhiya
Llaahu ‘anha) naye hufanya
Haya ni mafundisho matukufu, kutoka kwa watukufu
wawili, Mmoja akiwa ni mbora wa viumbe vyote (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam),
na wa pili ni Bibi wa mabibi wa Peponi (Radhiya Llaahu ‘anha), yakitufundisha
juu ya heshima na uhusiano unaotakiwa baina ya mzazi na wanawe na namna mzee
anavyoweza kuvuna kile anachopanda.
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Hayuko
pamoja nasi asiyemheshimu mkubwa wetu na kumhurumia mdogo wetu”.
Siku moja ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu
‘anhu) alipoingia nyumbani kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi
wasallam) alimkuta amewaweka Al-Hassan na Al-Husayn (Radhiya Llaahu ‘anhum) mgongoni pake,
akasema:
“Utukufu
ulioje wa ngamia aliyepandwa.”
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)
akamjibu:
“Na utukufu ulioje wa wapandaji wake
(ngamia huyo).”
Mtu mmoja aliingia nyumbani kwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kumkuta akiwabusu
wajukuu zake, akasema: “Hivyo nyinyi
Mnawabusu watoto wenu?”
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akamuuliza:
“Kwani
nyinyi mnawafanyaje watoto wenu?
Yule mtu akasema:
“WaLlaahi nina
watoto kumi na sikupata hata siku moja kumbusu mmoja kati
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)
akamwambia:
“Nifanye
nini ikiwa Mwenyezi Mungu Ameondoa rehma katika moyo wako. Hakika Mwenyezi Mungu huwahurumia wale wenye huruma.”
‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu ‘anhu) siku
moja alikuwa amelala juu ya ardhi huku wanawe wanacheza na
kuruka ruka kifuani pake. Akaingia mmoja katika Magavana wake aliyekuwa
akihukumu katika mojawapo ya mikoa ya dola ya Kiislam na
kumuona katika hali ile, akashangaa na kusema:
“‘Umar! Simba wa Mwenyezi Mungu unafanya hivi
na wanao?”
‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) akamuuliza:
“Kweni
wewe unafanyaje na wanao?”
Akasema:
“Mimi nikiingia nyumbani mfano wa
simba, kila mmoja anajificha kwenye pango lake.”
‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) akamwambia:
“Bora
jiuzulu, usiifanye tena kazi yetu (ya Ugavana)”.
Yule mtu akauliza:
“Kwanini ewe amiri wa
Waislam?”
‘Umar akamwambia:
“Ikiwa
wanao unawafanyia hayo, watakuwa katika hali gani Waislam walio chini ya
utawala wako?”
Hii ni mifano michache ndani ya mafundisho mengi
yanayopatikana kutoka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) na Sahaba zake
(Radhiya Llaahu ‘anhum), yakitufundisha namna gani walivyowalea watoto wao kwa
mapenzi na huruma, watoto waliokuja kuwa wanaume kweli wakaweza kuzifungua nchi
mbali mbali Mashariki ya ardhi na Magharibi yake.
Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) anasema:
“Mwenyezi
Mungu Akiwatakia watu wa nyumba kheri, basi huingiza mapenzi baina
Wataalamu wanasema: ‘Akili ya mtoto, ni mfano wa chombo kitupu kinachosubiri kujazwa, na usipokijaza
mwenyewe kitajazwa na wengine, na hapo usiilaumu isipokuwa nafsi yako.
Usingoje akili ya mwanao ikatawaliwa na marafiki wabaya waliojaa nje.
Waarabu wanasema:
ÃæáÇÏäÇ
ÃßÈÇÏäÇ ÊãÔí Úáì ÇáÃÑÖ
“Watoto wetu ni maini yetu
yanayotembea juu ya ardhi.”
Mwenyezi Mungu Akitujulisha namna gani waliotutangulia
walivyokuwa wakivijaza vyombo hivyo, Anasema:
Ãóãú ßõäÊõãú
ÔõåóÏóÇÁ ÅöÐú ÍóÖóÑó íóÚúÞõæÈó ÇáúãóæúÊõ ÅöÐú ÞóÇáó áöÈóäöíåö ãóÇ ÊóÚúÈõÏõæäó
ãöä ÈóÚúÏöí ÞóÇáõæÇú äóÚúÈõÏõ ÅöáóÜåóßó æóÅöáóÜåó ÂÈóÇÆößó ÅöÈúÑóÇåöíãó
æóÅöÓúãóÇÚöíáó æóÅöÓúÍóÞó ÅöáóÜåðÇ æóÇÍöÏðÇ æóäóÍúäõ áóåõ ãõÓúáöãõæäó
Ãóãú
ßõäÊõãú ÔõåóÏóÇÁó ÅöÐú ÍóÖóÑó íóÚúÞõæÈó ÇáúãóæúÊõ ÅöÐú ÞóÇáó áöÈóäöíåö ãóÇ ÊóÚúÈõÏõæäó ãöä ÈóÚúÏöí
ÞóÇáõæÇ äóÚúÈõÏõ ÅöáóÜٰåóßó æóÅöáóÜٰåó ÂÈóÇÆößó ÅöÈúÑóÇåöíãó æóÅöÓúãóÇÚöíáó
æóÅöÓúÍóÇÞó ÅöáóÜٰåðÇ æóÇÍöÏðÇ æóäóÍúäõ áóåõ ãõÓúáöãõæäó
“Je! Mlikuwapo yalipomfikia Yaakubu mauti, alipowaambia wanawe “Je,
mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema; “Tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahimu na Ismaili na Is’haka; Mungu
Mmoja tu, na sisi tunanyenyekea kwake”
Al-Baqarah – 133
Siku moja Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alipanda
mnyama na alimpakia nyuma yake ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhiya Llaahu ‘anhu),
ambaye wakati huo alikuwa bado mdogo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akamwambia:
“Ewe
kijana! Mimi ninakufundisha maneno,
uyahifadhi (vizuri). Unapoomba, umuombe Mwenyezi Mungu (Allaah) (tu),
ukitaka msaada, uuombe kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Allaah)
(tu), na ujue (ya kuwa) hata
Hivi ndivyo tunavyotakiwa tuwalee watoto wetu, kwa kuizamisha imani ya Tawhiyd nyoyoni mwao, mtoto aijue
dini yake, ajuwe ya kuwa hapana wa kumuomba isipokuwa Allaah, hapana wa
kumtegemea isipokuwa Allaah, hapana wa kumkimbilia wakati wa shida isipokuwa Allaah.
Amuogope na kumtii MwenyeziMungu (Allaah), na hii ni
kwa sababu kumjua na kumuogopa Mwenyezi Mungu ndiyo elimu bora kupita zote.
Asiyemuogopa Mwenyezi Mungu hana maana wala hana mwamana hata kidogo, na anayemuogoga Mola wake kati yenu ni yule anayemjua Mola
wake
Mwenyezi Mungu Anasema:
ÅöäøóãóÇ
íóÎúÔóì ÇááøóÜåó ãöäú
ÚöÈóÇÏöåö ÇáúÚõáóãóÇÁõ
“Kwa hakika wanaomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake
ni wale wanachuoni (Maulamaa).”
Faatwir – 28
Mtu mmoja alikwenda kumshitaki mwanawe kwa Sayyiduna ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa alimpiga kofi
la uso. ‘Umar akamuuliza:
“Mwanao
huyu umemfundisha Qur-aan?”
Yule mtu akajibu: “Sijamfundisha”
“Umemfundisha
mafundisho ya Mtume?”
“Sijamfundisha”
“Umemfundisha
tabia njema za waarabu?”
“Sijamfundisha.”
‘Umar akamwambia: “Mwanao huyu
alikufananisha na ng’ombe, ndiyo maana akakupiga.”
Juu ya kuwa kuwafanyia wema wazee wawili ni jambo tukufu
Siku moja Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)
alipokuwa amekaa pamoja na Sahaba zake (Radhiya Llaahu
‘anhum), aliletewa maji, akanywa na kubakisha mengine ili wenzake nao wapate
kunywa. Kuliani pake alikaa mtoto mdogo, na kushotoni
watu wazima. Kwa mujibu wa sheria shari’ah
(tutofautishe sheria (za wanaadam) na shari’ah (za Allaah [Dini]), ugawaji lazima
uanze upande wa kulia na kuendelea upande huo huo wa kulia bila kujali ukubwa
wa mtu au umri wake.
Ili Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) aweze
kuwapa maji watu wazima walioko kushotoni pake kwanza, ilibidi amuombe ruhusa
mtoto yule aliyekaa kuliani kwake kwa kumwambia:
“Ikiwa
utaniruhusu nitawapa hawa kwanza (watu wazima walio kushotoni pangu).”
Yule mtoto akasema:
“Hapana WaLlaahi, sijitolei haki
yangu itokayo kwako (baraka zako) kumpa mtu yeyote yule.”
Hapana
kitendo kibaya kuliko mtu kutokuwa muadilifu baina ya watoto wake. Kumpendelea mmoja wao na kuwaacha wengine
wakitizama ni dhulma na kujenga uadui baina
Na
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alipomuona
mtu mmoja amempakata mwanawe wa kiume, na amemweka wa
kike mbele yake juu ya ardhi, akamwambia:
“Si
bora ungefanya uadilifu baina
Mtu mmoja alitaka kumpa sehemu ya
“Mimi sikubali mpaka kwanza umtake
shauri Mtume wa Mwenyezi Mungu.”
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi
wasallam) akamuuliza:
“Jee na
wanao wengine pia utawaandikia sawa na mtoto huyu?”
Yule Mtu akajibu:
“Hapana, namtakia huyu mmoja tu”
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi
wasallam) akamwambia:
“Mimi
siwi shahidi katika (jambo la) dhulma.”
Wazee mara nyingi huwa na
tabia ya kuwavunja moyo watoto kwa kuwashutumu na kulaumu kila wanapotenda
makosa madogo madogo, na kwa ajili hiyo watoto huingiwa na uwoga ndani
ya nyoyo zao na kuendelea na uwoga huo hadi ukubwani wakajihisi kuwa
wana kasoro mbele ya wenzao.
Mtoto anapokosea hukosolewa kwa
hekima kwa niyah ya kumjulisha kosa lake, na siyo kumshutumu na kumvunja moyo
na kuingiza uoga (ima kote iwe uoga au uwoga) ndani ya moyo wake akaogopa tena
kujaribu kufanya jambo.
Alipotawazwa ‘Umar bin ‘Abdil-Aziyz (Radhiya Llaahu
‘anhu) kuwa Khalifa wa Waislam, wajumbe na watu kutoka
sehemu mbali mbali za dola ya Kiislamu walikwenda kumpa hongera na kufungamana
naye. Mojawapo ya makundi hayo likiongozwa na kijana
mdogo liliwasili katika qasri ya ‘Umar bin ‘Abdil-Aziyz. Kijana aliinuka na kuanza kuhutubia kwa kumpa hongera ‘Umar mbele ya hadhara
ya watu waliomzidi umri.
‘Umar akamwambia:
“Mbona
umeinuka wewe mdogo wao, si bora mungelimchaguwa kiongozi aliye mkubwa wenu kwa
umri?”
Yule kijana akasema:
“
‘Umar bin ‘Abdil-Aziyz alifurahi
ÊóÚóáøóãú ÝóáóíúÓó ÇáãóÑúÁõ íõæáóÏõ ÚóÇáöãðÇ æóáóíúÓó ÃóÎõæ Úöáúãò ßóãóäú åõæó ÌóÇåöáõ
Na maana yake ni:
‘Jifunze,
kwani mtu hazaliwi akiwa na elimu.
Na aliye na elimu hawezi kuwa sawa na asiyekuwa na elimu.’
Kisha akasema: “Wameongoka
watu waliokuchaguwa uwe kiongozi wao.”
Kwa upande mwingine, kudekeza sana watoto hasa wa
kiume na kuwaendekeza kupita kiasi hadi kuwavalisha vidani na kukata mikato ya
nywele za watoto wa kiume kama wanawake na kuvaa nguo zilizofanana na za kike au
kuigiza staili za makafiri ni jambo lisilopendeza. Kuwaachia moja kwa moja bila ya kuwakosoa wanapokosa au kuwaongoza
wanapopotea njia si katika malezi mazuri.
Malezi yanatakiwa yawe kati na
kati,
Mwanamume wa Kiislamu
anatakiwa awe na sifa ya ushujaa na ucha Mungu, na ushupavu.
Mwenyezi Mungu Amewasifia wanaume kwa ushujaa wao na uwanaume wao Aliposema:
ÑöÌóÇáñ
ÕóÏóÞõæÇ ãóÇ ÚóÇåóÏõæÇ Çááøóåó Úóáóíúåö
“Wapo watu (wanaume kweli kweli) miongoni mwa
walioamini, waliotimiza ahadi waliyoahidiana na
Mwenyezi Mungu …”
Al-Ahzaab - 23
Luqmaan mwenye hekima alikuwa na
tabia ya kumuusia mwanawe mara kwa mara na kumfundisha tabia njema.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÅöÐú ÞóÇáó
áõÞúãóÇäõ áÇÈúäöåö æóåõæó íóÚöÙõåõ íóÇ Èõäóíøó áÇ ÊõÔúÑößú ÈöÇááøóåö Åöäøó
ÇáÔøöÑúßó áóÙõáúãñ ÚóÙöíãñ
“Na (wakumbushe), Luqman alipomwambia Mwanawe; na hali ya kuwa anampa nasaha. ‘Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu maaana shirki ndiyo dhulma kubwa.”
Luqmaan- 13
Na Akasema:
æáÇ ÊõÕóÚøöÑú
ÎóÏøóßó áöáäøóÇÓö æáÇ ÊóãúÔö Ýöí ÇáÇÑúÖö ãóÑóÍðÇ Åöäøó Çááøóåó áÇ íõÍöÈøõ ßõáøó
ãõÎúÊóÇáò ÝóÎõæÑò
“Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi
ardhi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi
kila anayejivuna na kujifakhirisha.”
Luqmaan – 18
Haya ni mambo
mawili ambayo mtoto wa Kiislamu anatakiwa afunzwe kujiepusha nayo, Ushirikina
na Kiburi.
Ushirikina ni dhambi isiyosameheka, na Kiburi
ni tabia Asiyoipenda Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).
Anasema mshairi:
Ikiwa umeumbika, kwa uzuri ulotimu,
Au umetajirika, pesa
nyingi tasilimu,
Kiburi
ukajivika. vazi lenye uhasimu,
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Mola mwenye
madaraka, Ndiye Mwenye kurehemu
Kukupa na kukupoka, ndiyo kaziye Karimu.
Humpa Anayetaka,
jamii ya wanaadamu,
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Waringa na
hekaheka, wenzio kuwashutumu,
Kwa kuziona fanaka,
Mola Alokukirimu,
Wazimu ukakushika,
ukawa huna fahamu,
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Usiipige mipaka,
wazazi kuwalaumu,
Zinduka ndugu
zinduka, wewe Sio marehemu,
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Kiburi ni mbaya shuka, kuivaa ni haramu.
Yapendeza kukumbuka,
msemo wenye kudumu,
Mpanda
ngazi hushuka, alacho kikawa sumu.
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Na mwanaadamu
yataka, bongo
Wazee walotamka,
maneno yalo muhimu,
Kulonama
huinuka, laini huwa kigumu.
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Kituoni nimefika,
nazikomesha nudhumu,
Yatosha naloandika,
kiburi ni jahanamu,
Ashikae atashika, asoshika
Si lazimu,
Kiburi kwa mwanaadamu, Si kitu chema kiburi.
Mara nyingi mtu anaporudi kutoka kazini akiwa
amebeba kichwani matatizo yake ya kazini, na anapowasili nyumbani na kukuta
mambo yameparaganyika, mke mkali, watoto wanafanya zogo, kazi zao za skuli
hawakuzifanya, wanapigana, na mengi katika matatizo yanayotokea mara kwa mara
majumbani, wakati huo mzigo unakuwa mzito sana juu yake, na ghadhabu zake zote
alizokuja nazo kutoka kazini huwamiminia watoto wake kwa kuwapiga vibaya sana.
Kuwapiga watoto kwa
ghadhabu kunaweza kuleta madhara kuliko manufaa.
Mtu anaporudi na akahisi
kuwa siku hiyo amekumbana na matatizo mengi na akaona kuwa ghadhabu zake ziko
karibu karibu, ni bora aanze kuomba msaada wa Mola wake kwa kusoma ile du’aa
aliyotufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
Çááøóåõãøó Åöäøöí ÚóÈúÏõßó æóÇÈúäõ ÚóÈúÏößó æóÇÈúäõ ÃóãóÊößó äóÇÕöíóÊöí
ÈöíóÏößó ãóÇÖò Ýöíøó Íõßúãõßó ÚóÏúáñ Ýöíøó ÞóÖóÇÄõßó ÃóÓúÃóáõßó Èößõáøö ÇÓúãò
åõæó áóßó ÓóãøóíúÊó Èöåö äóÝúÓóßó Ãóæú ÃóäúÒóáúÊóåõ Ýöí ßöÊóÇÈößó Ãóæú
ÚóáøóãúÊóåõ ÃóÍóÏðÇ ãöäú ÎóáúÞößó Ãóæú ÇÓúÊóÃúËóÑúÊó Èöåö Ýöí Úöáúãö ÇáúÛóíúÈö
ÚöäúÏóßó Ãóäú ÊóÌúÚóáó ÇáúÞõÑúÂäó ÑóÈöíÚó ÞóáúÈöí æóäõæÑó ÕóÏúÑöí æóÌáÇÁó ÍõÒúäöí
æóÐóåóÇÈó åóãøöí
Allaahumma inniy ‘abduka wabnu ‘abdika wabni amatika
– naaswiyatiy biyadika – maadhin fiyyaa hukmuka – ‘adlun fiyyaa qadhaauka – as-aluka
bikulli smin huwa lak – sammayta bihi nafsika – aw anzaltahu fiy kitaabika – aw
‘allamtahu ahadan min khalqik – aw istaatharta bihi fiy ‘ilmil ghaybi ‘indak – an taj’ala l Qur-aana rabiy’a qalbiy - wa nuura sadry – wa
jalaa-a huzniy – wa dhahaaba hammiy.”
Hapo Mwenyezi Mungu Atamuondolea dhiki na huzuni zake, na badala yake Atampa furaha na ataweza
kuyakabili matatizo ya nyumbani kwa utulivu na bila ya ghadhabu.
Mu’aawiyah alimuuliza Al-Ahnaf bin Qays (Radhiya Llaahu
‘anhum):
“Ewe
Al-Ahnaf akasema:
“Ewe Amiri wa Waislam, wao ni uti wa migongo yetu,
matunda ya nyoyo zetu, kipumbazo cha macho yetu, kwa ajili yao tunawashinda
adui zetu, na wao ndio watakaokuwa wazazi wa watakaokuja baada yetu, kwa hivyo
uwe kwao, mfano wa ardhi laini, na uwe mfano wa mawingu yanayowaletea kivuli. Wakikuomba, uwape, wakikuomba msamaha, uwasamehe, na wala
usiwanyime ulichonacho mpaka wakakuchukia na kukuona unachelewa kufa (ili
wakurithi).”
Mu’aawiyah (Radhiya Llaahu ‘anhu) akasema:
“WaLlaahi ewe Aba Bahr, wao ni
Usiku mmoja Waislam waliokuwa safarini kupigana Jihaad
wakiwa wamejipumzisha huku wakisikiliza hotuba ya ‘Abdullaah bin Mubaarak
(Radhiya Llaahu ‘anhu) ambaye ni mmoja katika Maulamaa
wakubwa wa Kiislam, akiwatia moyo pamoja na kuwajulisha umuhimu wa kupigana Jihaad.
Mmoja kati ya waliohudhuria akamuuliza:
“Ewe ‘Abdullaah, ipo ‘amali yoyote iliyo bora
kuliko hii tuliyokuwa nayo sisi? Tumo safarini kwa
ajili ya Jihaad na wakati huo huo tupo katika majlis ya elimu.”
‘Abdullaah bin Mubaarak akamwambia:
“Naam ipo. Yule aliyeamka usiku, akaenda kuwatizama wanawe
waliolala, na kuwafunika vizuri wale wasiojifunika.”
Haya ndiyo mapenzi na rehma tunayotakiwa kuwafanyia
watoto wetu ili nao wakue, wawe na huruma na ili wapate kuhurimiana ndugu kwa
ndugu, Waislam kwa Waislam na kuieneza rehma baina yao.
Baada
ya kufanya utafiti kwa kuwahoji waalimu, baadhi ya wazee, na watoto waliolazwa mahospitali
kwa ajili ya kutibiwa ili wasirudie kutumia unga na mihadarati, pamoja na wale
waliotiwa jela kwa ajili ya kujishughulisha na biashara hii ovu, wataalamu wamegundua
yafuatayo kuwa ni miongoni mwa sababu muhimu za kuharibika kwa mwenendo wa watoto:
1. Ugomvi
usiokwisha baina ya wazee mbele ya watoto (Watoto wasipopata mfano mwema wa kuufuata
katika wazee wao basi huutafuta mfano huo nje, na kwa ajili hiyo huwafanya
waimbaji, wana michezo, na wababe wa sinema kuwa ni mfano kwao bora wa kuigwa,
na kuanza kuvaa kama wao na kuchana michano yao pamoja na kutembea kama wao n.k.)
2. Kuoana
baina ya watu wa mataifa yasiyolingana ustaarabu wao.
3. Baba
na mama wanapoacha kuifanya kazi yo vizuri kwa
kutofuatilia habari za watoto wao kutaka kujua nini wanachofanya wakiwa shuleni
au nje wanapocheza na wenzao. Mshairi maarufu aitwae
Ahmad Shawqiy anasema: “Yatima
si yule aliyefiwa na wazee wake, bali yatima ni yule mwenye mama aliyeiacha
kazi yake na baba asiyejishughulisha naye.”
4. Kuruhusiwa
watoto kuwaiga na kuwapenda bila kipimo waimbaji na
wababe wa sinema n.k. katika mavazi
5. Marafiki
wabaya wana sehemu kubwa ya kuharibika kwa mwenendo wa
watoto. Kuwazuia watoto wasiende kwa rafiki zao ni jambo gumu sana, lakini mtu
anaweza kumuelimisha mwanawe na kumkumbusha mara kwa mara juu ya umuhimu wa
tabia njema na umuhimu wa kumtii Mola wake, ili mtoto nae kwa upande wake aweze
kuwaongoza rafiki zake.
6. Kuwaruhusu
watoto kutizama na kufuatilia filamu za fujo na zile
zenye kuonyesha utovu wa adabu.
7. Kutokujishughulisha
kwa mzee kupekua mikoba ya mwanawe ili ajue ni vitabu
vya aina gani anavyosoma. Kwa sababu marafiki wabaya wanaweza kumpa vitabu vya
utovu wa adabu na kuviingiza nyumbani na kusababisha
ndugu zake wengine nao kuviangalia.
8. Kutotembelea
skuli za watoto wao kwa ajili ya kujua mwenendo wao
pamoja na matatizo
9. Kutojishughulisha
na matokeo ya mwanawe katika mitihani, ikiwa amefeli
au amepasi yote kwake ni sawa tu, hii humfanya mtoto asiyashughulikie
10.
Kutendewa vibaya na waalimu pia kunawafanya watoto kutoipenda skuli.
11.
Ushirikiano baina ya skuli na wazee ni jambo muhimu
12.
Wazee kuwapenda watoto wengine na kutowashughulikia wengine.