KATIKA

KUTHIBITISHA KUONEKANA ALLAH

(SUBHAANAHU WATAALAA) KWA MACHO HUKO AKHERA

MAJIBU NA MAELEZO

Muandishi: Abul Fadhl Kassim Mafuta Kassim

Yaliyomo

Utangulizi 5

Pongezi Na Shukrani (1) 11

Pongezi Na Shukrani (2) 13

Shukrani 20

Mpangilio Wa Kitabu Hiki 22

Sura Ya Kwanza. 25

Vipi Tutamfahamu Mola Wetu Na Wapi Tuichukue Imani Ya Dini Yetu?. 25

Sura Ya Pili 34

Uchambuzi Yakinifu Juu Ya Elimu Ya Hadithi. 34

Masharti Ya Usahihi Wa Hadithi 37

Tuhuma Za Uwongo Dhidi Ya Ahli Sunna. 42

Majibu Yetu. 45

Tuhuma Ya Kwanza. 46

Majibu Yetu. 47

Tuhuma Ya Pili 51

Majibu Yetu. 52

Majibu Yetu. 59

Historia Ya Abul-Hasan Kwa Ufupi 60

Yaliyomo Katika Kitabu Al-Ibana. 63

Tuhuma Ya Tatu. 68

Majibu Yetu. 69

Majibu Yetu. 71

Tuhuma Ya Nne. 76

Majibu Yetu. 77

Sura Ya Tatu. 87

Chanzo Na Chimbuko La Upotevu. 87

Uchambuzi Yakinifu Juu Ya Suala La Majazi 93

Chanzo Cha Kutumbukia Katika Itikadi Batili 95

Majibu Yetu. 96

Je Wenye Kupinga Majazi Wana Hoja Za Kielimu?. 102

Hoja Yao Ya Kwanza. 102

Hoja Yao Ya Pili 104

Hoja Za Wenye Kuthibitisha Majazi 107

Majibu Ya Wenye Kupinga. 108

Hoja Yao Ya Tatu. 111

Sura Ya Nne. 116

Hoja Za Wenye Kuitakidi Kuonekana Allah Huko Akhera. 116

Hoja Ya Kwanza. 117

Jaribio La Kwanza La Kuipotosha Hoja Hii 123

Majibu Yetu. 125

Majibu Yetu. 128

Jaribio La Pili La Kupotosha Hoja Hii 135

Majibu Yetu. 137

Majibu Yetu. 141

Hoja Ya Pili 145

Jaribio La Kwanza La Kuipotosha Hoja Ya Pili 154

Juma Na Sheikh Wake Al-Qannubi Wamzulia Uwongo Sheikh Al-Bani. 167

Majibu Yetu. 168

Hata Mufti Wao Pia Asema Uwongo! 179

Kasoro Ya Pili Ya Hadithi Hii: 181

Nakala Kutoka Kwa Al-Qannubi. 181

Majibu Yetu. 181

Maana Sahihi Ya Neno Al-Ziyadah. 184

Majibu Yetu. 185

Majibu Yetu. 190

Mukhtasari 197

Hoja Ya Tatu. 198

Hadithi Ya Kwanza. 201

Sanadi Ya Hadithi Hii 206

Kuhusu Matni Ya Hadithi Hii: 206

Jaribio La Kwanza La Kupotosha Hadithi Hii 208

Majibu Yetu. 208

Tuhuma Yake Ya Pili Dhidi Ya Qais: 211

Majibu Yetu: 212

Majibu Yetu. 215

Jaribio Lake Jingine. 216

Majibu Yetu. 218

Ufahamu Wake Mbaya Juu Ya Hadithi Hii 225

Majibu Yetu. 227

Hadithi Ya Pili 236

Jaribio La Kwanza La Upotoshaji 245

Majibu Yetu. 245

Jaribio Lake La Pili 252

Majibu Yetu. 253

Jaribio Lake La Tatu. 255

Majibu Yetu. 256

Jaribio Lake La Nne. 259

Majibu Yetu. 260

Majibu Yetu. 262

Sura Ya Tano. 270

Hoja Za Wenye Kupinga Kuonekana Allah Kwa Macho Huko Akhera. 270

Majibu Yetu. 274

Hoja Yao Ya Kwanza. 276

Majibu Yetu. 278

Hoja Yao Ya Pili 297

Majibu Yetu. 298

Majibu Yetu. 304

Jaribio Lake Jingine La Upotoshaji 311

Majibu Yetu. 312

Hoja Yao Ya Tatu. 314

Majibu Yetu. 315

Hoja Yao Ya Nne. 317

Majibu Yetu. 318

Hadithi Wanayoitegemea. 324

Majibu Yetu. 325

Sura Ya Sita. 327

Kauli Za Baadhi Ya Maimamu Juu Ya Suala Hili. 328

Jaribio La Kuipotosha Kauli Hii 329

Majibu Yetu. 329

Hatima. 337

 

 

2008-02-25 Haki ya uchapishaji inamilikiwa na muandishi.

 

Ni ruhusa kwa mtu yoyote kukitoa copy na kukisambaza kitabu hiki kwa dhumuni la kufikisha ujumbe kwa waislamu kokote walipo.

Lakini hairuhusiwi kubadilisha chochote bila ruhusa ya muandishi wa kitabu hiki.

 

Abul-Fadhli Kassim Mafuta Kassim

 

 

KITABU HOJA ZENYE NGUVU KATIKA KUTHIBITISHA KUONEKANA ALLAH KWA MACHO HUKO AKHERA, MAJIBU NA MAELEZO.

 

MARKAZ SHEIKHIL-ISLAMI IBN TAYMIYYAH AL-SALAFIY,

P.O.BOX 398 TANGA,

MOBILE: 0715 615645 / 0784 615645.

BARUA PEPE: kassimmafuta@yahoo.com

PONGWE-TANGA.

TANZANIA.

UTANGULIZI

. . .

( )([1]) [ : : 102]. ( )([2]) [ : 1].

( )([3]) [ ȡ : 70 71].

ǡ .

 

Ama baada ya kumsifia mola wetu kwa sifa njema, sina budi kumswalia Mtukufu Mtume wetu Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam-, na swala na salamu hizo pia ziwafikie Aali zake, wake zake, maswahaba zake na wale wote walioiandama njia yao kwa wema mpaka siku ya malipo.

 

Kwanza, napenda kusema machache kuhusu kitabu hiki, sababu za kuandikwa kwake na madhumuni yake.

Sababu kuu na asili ya kitabu hiki ni majibu na maelezo dhidi ya kitabu kiitwacho; HOJA ZENYE NGUVU JUU YA KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU KWA MACHO cha Ndugu JUMA M. Al-Mazrui.

Maudhui ya kitabu hicho ni kama kinavyojieleza chenyewe katika anwani yake, nayo ni kupinga kuonekana kwa Allah kwa macho huko akhera, na hiyo ndiyo itikadi ya makundi mengi ya batili kama vile: Mutazila, Khawariji (Ibadhi), Shia, na wengineo.

Ndugu Juma M. Al-Mazrui muandishi wa kitabu hicho hakuleta jambo jipya, bali amejikakamua kwa kiasi kikubwa mno kuitetea itikadi hiyo batili inayopingana na mafundisho sahihi ya Quran na Sunna za Mtume wetu Muhammad-swalla llaahu alayhi wasallam-.

Baada ya kukisoma kwa utulivu na umakini kitabu hicho chenye kurasa 339 kutoka mwanzo hadi mwisho, sikuweza kuuvumilia upotoshaji alioufanya, ndipo nilipoamua kukirudia tena na tena kwa lengo la kuyadhibiti yale ambayo nimeyaona kuwa ndio mambo ya msingi aliyoyategemea muandishi huyo kwenye kitabu chake hicho kwa lengo la kutaka kuhakiki zaidi.

Baada ya kufanya utafiti wa kielimu ambao lengo lake lilikuwa ni kupata faida, nikaona kuwa ninaowajibu wa kuzitawanya faida hizi ili ziwafikie wengineo katika waislamu ambao wengi wao hawana uwezo wa kufanya utafiti wa kielimu kwa kutumia misingi sahihi mpaka kuufikia ukweli.

Kutokana na majukumu niliyonayo pamoja na ufinyu wa wakati, kazi hii niliiona kuwa ni ngumu mno hivyo nilikata tamaa, kwa sababu shughuli hii si ndogo na inahitaji muda wa kutosha, lakini mambo makuu manne ndiyo yaliyonipa moyo wa kukiandika kitabu hiki:

i) Amri zilizokuja kuhimiza kuibainisha haki, na makatazo yaliyokuja kuharamisha kuinyamazia batili.

 

ii) Hali ya hatari ambayo inayowakabili waislamu wengi hasa wale wasio na uwezo wa kufanya utafiti wa kielimu; ima kwa sababu ya udhaifu wa kielimu au kwa sababu ya uvivu wa kutafiti au kukosa nyenzo za kufanyia utafiti huo au kwa sababu nyinginezo, hivyo hawataweza kukabiliana kielimu dhidi ya ubabaishaji alioufanya ndugu Juma, na hatima yake wataingia kwenye dimbwi la batili kwa kudhania kuwa upotoshaji alioufanya ndugu Juma Mazrui kuwa ni haki.

 

iii) Kupambana kwa kalamu dhidi ya watu wa bida na wapotoshaji wote ni moja katika amali njema za kumweka mtu karibu na Mola wake kwa sababu ni katika sampuli za Jihadi.

 

iv) Na kwa kuwa suala hili linafungamana na kuhusiana na mambo ya itikadi, ambayo ndiyo msingi wa dini, bado tuna wajibu wa kuielimisha jamii hata kama hakujitokeza mpotoshaji.

Kwa kuyazingatia yote hayo, nilipata ari na hima ya kulikabili jambo hili kwa umakini, na kwa Tawfeeq ya Allah nikafanikiwa kukikamilisha kitabu hiki kwa salama.

Na zote hizo ni miongoni mwa fadhila nyingi za Mola wangu juu yangu, ninamuomba anijaalie niwe miongoni mwa wenye kumshukuru.

 

 

Muandishi.

 

 

Abul-Fadhli Kassim Mafuta Kassim.

 

 

 

.

. ѡ .

.

:

13/ /1430

8//2009

Rudi juu

PONGEZI NA SHUKRANI (1)

 

Sifa njema zote ni za Allah Bwana wa viumbe wote, na swala na salamu zimshukie mtukufu wa Manabii na Mitume, na Jamaa zake na Swahaba zake na waliowafuatia hao kwa wema mpaka siku ya malipo.

 

Ama baada ya yaliyotangulia.

 

Nimekitalii kitabu cha ndugu mbora Abul-Fadhli Kassim Mafuta Kassim, nikakikuta kuwa ni kitabu kilicho na faida kwa sampuli yake, katika kuwajibu Makhawariji wa Kiibadhi, pale mtunzi alipozileta HOJA ZENYE NGUVU katika kuthibitisha kuonekana Allah huko Akhera kwa macho, na akaufichua uwongo wa ndugu Juma Al-Mazrui na masheikh zake pamoja na ubabaishaji wao kwa hoja za wazi wazi kama vile jua lililokuwa katikati ya mchana.

 

Allah amlipe mtunzi kheri kwa sababu ya kuwatumikia waislamu, na ambariki katika elimu yake na juhudi zake kubwa katika kuitangaza itikadi ya Salaf na kuitetea.

 

Na swala na salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad na Jamaa zake na Maswahaba zake wote.

 

 

 

Al-Akhi Sheikh Abu Hashim Abdul-Qadir Ibn Hashim Ibn Abdul-Qadir Al-Musawaa

13 /Jumadal-Ulaa /1430 H.

8 /Mei / 2009 M.

Rudi juu

Pongezi na Shukrani (2)

 

Ama baada ya kukipitia kitabu cha ndugu yetu Abul fadhli Kassim Mafuta, kitabu chenye anuani ya kitabu HOJA ZENYE NGUVU katika kuthibitisha kuonekena Allah kwa macho huko akhera, majibu na maelezo, kitabu hiki nimekipitia chote kwa uwangalifu na insaafu, ni kitabu madhubuti kinacholingana na jina lake kwani makusudio yake makubwa ni kutetea itikadi sahihi ya Manabii na Mitume wote, itikadi ya AHLI SUNNATI WAL-JAMAA dhidi ya waandishi wa uwongo, walio dhidi ya itikadi hii safi, kwani kitabu hiki kimebainisha waziwazi kwa hoja sahihi juu ya upotovu wa mtunzi wa kitabu kiitwacho HOJA ZENYE NGUVU JUU YA KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU KWA MACHO cha ndugu JUMA AL-MAZRUI ambae ni miongoni mwa wafuasi wa mapote ya matamanio kwani ndugu Juma ndani ya kitabu chake hicho amemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake kama kawaida ya watu wa matamanio kumsifu Allah subhaanahu wataalaa kwa sifa ambazo ametakasika nazo za kutoonekana, ilhali Mwenyezi Mungu Subhaanahu wataalaa amejisifu yeye mwenyewe nafsi yake kwa sifa ya kuonekana huko akhera na pia akasifiwa na Mtume wake Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam kwa sifa hiyo hiyo ya kuonekana na hii ndio itikadi ya Maswahaba wa Mtume Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam na ndio itikadi ya Taabiina na wema waliofuata baada yao itikadi ya Ahli-Sunnat Wal-Jamaa.

Ndugu Juma Al-Mazrui ameandika kitabu hicho ili atetee itikadi yake ya kikhawarij kama ilivyo kawaida ya watu wa matamanio kabla ya kusoma na kufahamu jambo, wao kwanza ni kutetea itikadi zao vyovyote iwavyo kama vile walivyoipokea toka kwa mababu zao, lakini kwa rehema za Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa amejaalia katika umma huu kama anavyosema Mtume katika hadithi sahihi kwamba: HALITAACHA KUWEPO KUNDI KATIKA UMMA WANGU LENYE KUPIGANIA HAKI HAWATADHURIWA NA WASIOWASAIDIA NA WALA HATADHURIWA NA WANAOWAPINGA MPAKA KITAKAPO SIMAMA KIYAMA na watu hawa ni AHLI-SUNNAT WAL-JAMAA.

Ama ndugu Juma Mazrui mimi namlaumu sana kwa kufanya haraka kuandika kitabu hicho bila ujuzi wa dini, lakini baada ya lawama namuomba Mwenyezi Mungu amuongoze ndugu Juma na ampe maarifa na amtoe katika hali ya itikadi potofu, kwani kubwa la Juma ni kumuamini sana Said Mabruk Al-Qanuubi bila kumuelewa elimu yake na uwadilifu wake kwani inaonyesha bwana Juma hamfahamu bwana huyu Qannubi na ndio maana akampachika majina makubwa ya kielimu ambayo hastahiki jinsi alivyo, kwani Said Qannubi si mwengine zaidi ya kuwa ni mwanakasumba wa kikhawariji si mkweli, angelikuwa ni mkweli asingelifikia hali ya kunukuu hoja hai za ndani ya vitabu vya wanakasumba na watu wa matamanio na yeye kuzifanya hoja za kuwarudi Ahli-Sunnat wal-Jamaa.

 

Ama marudio anayorudiwa ndugu Juma ndani ya kitabu hiki ni malipo yatokanayo na chumo la mikono yake iliyoandika maandiko ya Qannubi ambaye ni mwanakasumba wa kikhawariji aliyeiajiri mikono yake juu ya kunukuu maneno ya watu wa matamanio wenye chuki dhidi ya wanasunnah, na maimamu wa Ahli-Sunnat.

Miongoni mwa watu anaowaiga Qannubi maandiko yao ni kama Al-kauthari, na Abuu Ghudah na Jamal-din Afghani ambaye si Muafghani bali ni Muirani, na Butwi na Al-Maliki katika watu wa hivi karibu na pia miongoni mwao hao ni pote la Muutazilah kwani wao ndio wanaopinga sana kuonekana kwa Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa kwani pote hili elimu yao yote imejengeka juu ya misingi ya mijadala ambayo asili yake ni vipimo vilivyo juu ya kufananisha kisichopo kwa kilicho kuwepo na miongoni mwa maigizo ya Qannubi ni pote la Jahmiyyah, Baatiniyya, Mashia Imamiyyah ndio maana utayakuta maandishi yao yote juu ya kutoonekana Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa wanayanukuu kwa mwana matamanio mkubwa adui wa Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa Abdul Jabbar al-Muutazili kwenye kitabu chake almughni, hasa katika zile hoja za kiakili alizozitaja Alkhalili kama alivyomnukuu Juma Mazrui katika kitabu chake Al-Haqu Addamigh ukurasa 67, kwamba kuona kwa macho ni kuingia sura ., na kadhalika amefananisha kuonekana Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa na kuonekana viumbe, ametakasika Mwenyezi Mungu na dhana zao.

 

Na vilevile Qannubi si mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu, lakini ni shujaa asiye na uwoga wala aibu na ndio maana utakuta mara nyingi hutoa hukumu juu ya hadithi kutokana na ushujaa wake mfano;- anasema kwamba hadithi ambazo zimepokewa zenye kuifasiri aya ya 22 na ya 23 za surat Al-Qiyamah ni dhaifu na za uwongo, na Juma Al-Mazrui akamfuata kiongozi wake Qannubi na ilhali hadithi hizo zote zilizokuja kutafsiri aya hizo ni Mutawatir kwa mujibu wa majio yake na kwa mujibu wa ushuhuda wa wanazuoni wa somo la hadithi, pia Qannubi kutokana na kutoelewa somo hili utakuta anamtia ila (dosari) mpokezi wa hadithi pasi na kuielewa ila ile kwamba haiwi hadithi ya mpokezi yule ni dhaifu, mfano amemwita imamu Zuhri kwamba ni Mudalis ili aidhoofishe hadithi zake bila kubainisha ni tadlis ipi ili muradi atetee matamanio yake.

 

Haya nimeyataja machache, lakini makosa ya namna hii ni mengi juu ya Qannubi na mfano wa hayo, na yote haya yanatokana na kasumba za kimadhehebu zinazompelekea Qannubi na mfano wake kuandika mambo wasioyajua ili watetee madhehebu yao kwa hali na mali, mfano Juma Mazrui, nikisema kwamba hana ujuzi katika somo la hadithi sitakosea, lakini hebu tumsikilize yeye mwenyewe anavyojieleza katika kitabu chake Hoja zenye nguvu katika ukurasa wa 194 anamwita mpokezi wa hadithi kwa jina ambalo sio lake, mpokezi huyu jina lake ni Ibn Halbas yeye akamwita Abu Halbas, mfano mwingine katika kitabu chake hicho katika ukurasa wa 69 amemwita Al-Duuriy, Al-Dauri na haya ni mengi mno kwenye maandiko ya Juma na haya ni kwa kuwa haja wahi kukaa na watu wa elimu hizi, labda aliwahi kukaa na Qannubi kisha akamuiga porojo zake na ndio maana akasema Ibnu-Halbas ni majhulil-ayn bila ya kubainisha ni majhul wa vipi, lakini yeye katika uibadhi wake Imamu wake aitwae Abuu Ubaidah Muslim Ibni Abi Karimah yeye ndiye Majhuli tena ni Majhulil-Ayn, mtu huyu ni kigano, lakini kwa kutojua kwao wanadhania yupo, sitaeleza mengi bali mengi yameshaelezwa ndani ya kitabu hiki na mwenye kutaka haya arudi kuangalia vitabu vya watu wa Sunnah kama kitabu Assunnah, Arrisalatu alhamawiyyatu alkubraa, Al-Aqidatu Atwahawiyah, na Minhaju Assunnah na vinginevyo.

 

Ama kitabu hiki cha ndugu yetu Abul-Fadhli ni kitabu kilichokusanya faida nyingi sana haswa katika somo azizi la hadithi na pia katika somo la lugha ya waarabu, faida ambazo hazipatikani katika vitabu vingi vilivyokwisha andikwa kwa lugha ya waswahili. Mwenyezi Mungu subhaanahu wataalaa amlipe ndugu yetu huyu kheri na amzidishie elimu na uongofu na kulingania dini ya Mwenyezi Mungu subhanahu wataalaa kwa hekima na elimu, kwani Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutakabali dua za watu wake na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam na Aali zake na Maswahaba zake.

 

Al-Akhi Sheikh Abuu Saam Seif .S. Al-Ghafriy.

Rudi juu

SHUKRANI

 

Ni Allaah peke yake ndiye wa kuhimidiwa na kushukuriwa, kwa hiyo sina budi kusema:

(Al-Hamdu lillaahi) kwa kuniwezesha kukiandika kitabu hiki na ninamuomba Allaah akijaalie kitabu hiki kiwe ni chenye kheri, faida na manufaa kwa waislamu wote hasa wasomi wa mambo ya dini na wale wenye kuitafuta elimu ya dini na kuyafuatilia mambo ya dini kwa ukaribu na wakawa wako tayari kutoa wakati wao na hali na mali zao kwa ajili ya elimu ya kuutafuta ukweli kupitia elimu ya dini.

Pamoja na hayo, pia ninawashukuru wale wote ambao wametoa juhudi zao kwa njia mbali mbali kwa ajili ya kufanikisha kutoka kwa kitabu hiki, ima kwa kutoa nasaha na ushauri wao, au kwa kuutumia wakati na mali zao.

 

Pia ninawashukuru ndugu zangu wapenzi:

Sheikh Abu Hashim Abdul-Qadir Hashim Al-Musawaa Al-Hashimiy.

Na Sheikh Abu Saam Seif .S. Said Al-Ghafriy.

Kwa kazi yao kubwa waliyoifanya ya kukipitia kitabu hiki na kwa nasaha zao na ushauri wao walioutoa. Pia ninamshukuru ndugu yangu mpenzi Sheikh Abu Arqam Abdallah Muhsin kwa kunishajiisha na kunipa moyo wa kukichapisha kitabu hiki wakati nilipomuonyesha nuskha ya kitabu hiki kabla ya kukichapa.

Mwisho ninamshukuru Ahli yangu Ummul-Fadhli kwa ustahamilivu wake na uzito alioubeba mpaka nikaweza kukimaliza kitabu hiki.

 

Abul-Fadhli Kassim Mafuta Kassim

Markaz Sheikhil-Islami Ibn Taymiyyah, Pongwe-Tanga Tanzania

25/SHAABAN/1428 H = 26/08/08 M.

Rudi juu

MPANGILIO WA KITABU HIKI

Nimekianza kitabu hiki kwa kumsifia Allah subhaanahu wataalaa Mola wetu mkarimu na kumswalia Mtume wetu Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam pamoja na Aali zake na Maswahaba zake wote.

Kisha nikalazimika kuzijibu baadhi ya tuhuma za uwongo ambazo amezileta ndugu Juma dhidi ya maulamaa wa kiislamu kama vile Ibnu Taymiyyah, na Ibnul-Qayyim Allah awarehemu kwa lengo la kutaka kuwachafua.

Kisha nikaweka mlango maalumu kwa ajili ya kuelezea kwa muhtasari uchambuzi wa elimu ya hadithi, na kanuni za upokezi wa habari.

Pia tukabainisha sababu za msingi za upotevu wa watu, na kuyabatilisha madai ya uwongo ya ndugu Juma pale alipodai kuwa chanzo na sababu ya upotevu ni kukataa kuwepo kwa majazi ndani ya Qurani.

Pia tumelazimika kujadili kielimu tena kwa muhtasari suala la Majazi kuwepo kwake na kutokuwepo na tofauti za maulamaa wa kiislamu juu ya suala hilo.

Kisha ndio tukaanza kuubainisha msimamo sahihi wa AHLI-SUNNA WALJAMAA, juu ya masala ya kuonekena Allah kwa macho huko akhera, na suala hili ndiyo maudhui mama ya kitabu hiki.

 

Na tumelizungumzia suala hili kwa namna tatu:

 

i) Kuithibitisha itikadi hii kupitia maandiko matakatifu ya dini yetu kama vile; Quran na Hadithi sahihi za Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- pamoja na kutoa maelezo kwa muhtasari juu ya maandiko hayo.

ii) Pia nimetumia kauli za Maswahaba na wanafunzi wa Maswahaba (Taabiina) na Maimamu wakubwa wa kiislamu kama vile Imamu Malik, Imamu Shaafiy, Imamu Ahmad bin Hanbal na wengineo kwa lengo la kuutilia nguvu msimamo wetu, na kuibatilisha dhana ya kwamba itikadi ya kuonekana Allah akhera kwa macho ni itikadi ya wale ambao ndugu Juma na kaumu yake anawaita kuwa ni Mawahabi.

 

iii) Kuzivunja baadhi ya hoja batili zilizotolewa na muandishi huyo hasa zile ambazo ndiyo msingi aliojengea juu yake itikadi yake hiyo potofu.

 

iv) Mwisho tukamalizia kwa kuweka Khatima.

Hayo yote nimeyafanya kwa ufupi mno, na sikutaka kumjibu hoja baada ya hoja au neno kwa neno kwa kuhofia kurefusha, hasa ukizingatia kuwa ndugu Juma Mazrui amekijaza kitabu chake maneno mengi ambayo si ya kweli na yasiyo na uzito katika misingi ya kielimu.

 

Rudi juu

SURA YA KWANZA

 

VIPI TUTAMFAHAMU MOLA WETU NA WAPI TUICHUKUE IMANI YA DINI YETU?

 

Hili ni swali muhimu mno na jawabu sahihi la swali hili ndiyo ufumbuzi wa matatizo mengi yaliyojitokeza katika umma wa kiislamu, kwa sababu waislamu wengi hawajui vipi watamfahamu mola wao muumba, na wapi wanatakiwa kuichukua dini yao !

 

Ama Ahlu Sunna wal Jamaa wao wanaitakidi kwamba:

Tutamjua mola wetu kwa vile alivyojielezea yeye mwenyewe katika kitabu chake (Quran tukufu) na vile alivyotuelezea mjumbe wake mtukufu katika mafundisho yake yaliyo sahihi.

Kwa kuyathibitisha yale yote ambayo Allah amejithibitishia mwenyewe au ambayo ameyathibitisha Mtume wake -swalla llaahu alayhi wasallam-, na kuzikanusha sifa ambazo Allah na Mtume wake swalla llaahu alaihi wasallam wamezikanusha, bila ya kupotosha, wala kupinga, wala kumfananisha yeye na chochote katika viumbe vyake, pamoja na kufuta dhana ya kwamba kuyathibitisha yale ambayo Allah amejisifia nayo kuwa ni kumfananisha yeye Jalla Jalaaluh- na viumbe vyake.

 

Na tunaichukua imani ya dini yetu kutoka kwenye Quran na Sunna (mafundisho) sahihi ya Mtume wetu Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- pamoja na kuuzingatia ufahamu wa Salaf Swaalih (wema waliotangulia) kama vile; Maswahaba na Taabiina (wanafunzi wa Maswahaba) na maulamaa waliokuja baada yao.

Na hivi ndivyo tulivyoamrishwa na Quran kadhalika Sunna sahihi za Mtume swalla llaahu alayhi wasallam.

 

 

Amesema Allah -azza wajalla-:

13

 

Na wanapoambiwa:aminini KAMA WALIVYOAMINI WATU wanasema;

Tuamini kama walivyoamini wapumbavu?....

Suratul-Baqarah aya ya 13.

 

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Masoud na Ibn Abbaas kwamba wamesema: Watu waliokusudiwa hapa ni maswahaba.

Tazama tafsiri al-Durrul-Manthuur juzuu ya 1 ukurasa 70-71.

 

Na maana ya aya hii ni kwamba makafiri na wanafiki walikuwa wakiambiwa kwamba wamuamini Allah kama walivyoamini Maswahaba wa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- wao kwa sababu ya kiburi, na jeuri zao walikuwa wakiwatukana Maswahaba kwa kuwaita wapumbavu, na hali ya kuwa wapumbavu ni wao !

 

Na amesema tena Allah:

Basi wakiamini KAMA MLIVYOAMINI NYINYI (maswahaba) basi watakuwa wameongoka.Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani.

Suratul Baqarah aya ya 137.

 

Katika aya hii Allah anawataka Ahlul-kitabi (Mayahudi na Wakristo) wamuamini Allah kama walivyoamini Maswahaba na waislamu wote kwa ujumla walio na imani kama ya Maswahaba, na kama wataasi wakenda kinyume na Amri hiyo, basi wao watakuwa ni waasi na ni wapinzani wa Allah.

Na amesema tena Allah:

 

 

Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na AKAFUATA NJIA ISIYOKUWA YA WAUMINI,tutamuelekeza alikoelekea mwenyewe,na tutamuingiza katika Jahannamu.....

Surat An Nisaa aya ya 115.

Amesema Allah:

 

Na wale waliotangulia, wakwanza katika Muhajirina na Answaari,na wale waliowafuata kwa wema, Allah ameridhika nao, na wao wameridhika naye.....

Suratut Tawba aya ya 100.

 

Kwa mujibu wa aya hizo zote tulizozitaja, tunatakiwa waislamu wote kuamini kama walivyoamini maswahaba wa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- pamoja na kuifuata njia waliyoipita.

 

Na kama imani zetu zitatofautiana na imani zao na njia yetu ikitofautiana na njia yao, basi tutakuwa ndani ya mashaka makubwa mno na upotevu uliowazi kama zilivyoeleza aya tulizozitaja.

 

Hivyo basi, tunapolizungumzia suala zima la kumuamini Allah Subhaanahu Wataalaa- ni lazima tujiulize maswali yafuatayo:

 

Je imani zetu zinaendana na mafundisho ya Quran na Sunna kama walivyofahamu wema waliotangulia (Salaf Swalih)?

Je hivi tunavyoitakidi ndivyo walivyoitakidi hao Salafu Swalihi (wema waliotangulia) au la?

 

Na kama jawabu likiwa la, basi tujue kwamba tumo ndani ya upotevu kwa kuifuata njia isiyokuwa ya hao waumini wa mwanzo.

 

Na bila shaka, wao wameifahamu vizuri Quran na walimfahamu vizuri Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- kuliko walivyomfahamu na wanavyomfahamu na watakavyofahamu watakaokuja baada yao, ndiyo maana Allah akawasifia wao na wale walioifuata njia yao kwa wema, na akawaahidi mambo mazuri.

Na wakati huo huo akawasema vibaya wale waliyoihalifu njia hiyo, na kuwaandalia makazi mabaya motoni -Allah atuepushe na adhabu zake-.

 

Hivyo basi, katika suala hili la kuonekana au kutokuonekana Allah kwa macho huko akhera pia tunatakiwa pale tunapozitazama aya na hadithi zinazo lizungumzia suala hili tuutangulize mbele ufahamu wa hao wema waliotutangulia (Salafu Swalihi) katika imani, vipi wao walizifahamu aya na hadithi hizo?

 

Na ilikuwaje imani yao juu ya suala hilo?

Je waliamini kwamba Allah ataonekena kwa macho huko akhera kama wanavyo amini Ahli Sunna?

Au Allah hataonekana kwa macho huko akhera kama ilivyokuwa itikadi ya makundi mengine kama vile: Jahmiyyah, Mutazila na wajukuu zao kama vile Shia, Ibadhi na wengineo miongoni mwa watu wa bida?

 

Inshaallah swali hili litajibiwa na kitabu chetu hiki, tafadhali fuatilia kwa makini na insafu utagundua ukweli juu ya suala hili.

Huenda mtu akatatizika au akatatizwa kwa kuambiwa: vipi tufuate njia ya hao waliotangulia (Maswahaba,Taabiina, na Maimamu waliokuja baada yao) na hali yakuwa wao wenyewe wametofautiana katika mambo mbalimbali?

 

Jawabu ni kwamba; tutashikamana na ufahamu wao katika mambo ambayo wameafikiana, na yale waliyotofautiana sisi tutaichukua kauli iliyoungwa mkono na maandiko sahihi, na wala haifai kuzusha kauli ya tatu zaidi ya kauli zao mbili zilizo tofauti.

 

Ama mambo ambayo hayakuwepo katika wakati wao katika yale ambayo yanafaa kutumia akili na rai, basi huo ndiyo uwanja wa kuogelea maulamaa katika kufanya ijtihadi na kutumia rai zao kwa mujibu wa kanuni na misingi ya kielimu.

 

Swali la kujiuliza ni; Je hao wema waliotangulia wametofautiana juu ya suala la kumuona Allah kwa macho huko akhera?

 

Jawabu ni kwamba:

Maswahaba Hawakutofautiana katika suala hili, bali wote waliafikiana kwamba watu wema watamuona mola wao kwa macho huko akhera kama lilivyo thibitishwa suala hilo na Quran na Sunna sahihi za Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-.

 

Na hakuna mtu yeyote aliyemuona, wala atakayemuona Allah kwa macho yake hapa duniani, na hivyo ndivyo wanavyoamini na kuitakidi Ahlu Sunna Wal-jamaa.

 

Lakini tofauti imekuja katika jambo ambalo ni nje ya maudhui yetu hii, jambo lenyewe ni: Je bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- alimuona Mola wake katika usiku aliokwenda mbinguni (Miraji) ?

Jawabu ni kwamba, kuna kauli iliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas -Allah amridhie- kwamba; bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- alimuona Mola wake katika usiku huo.

 

Wengi katika wanavyuoni wakayachukulia maneno yake hayo kwamba, makusudio yake ni kuwa bwana Mtume alimuona Mola wake kwa moyo wake, na wakategemea riwaya nyingine zilizopokewa kutoka kwa huyo huyo Ibn Abbas.

 

Ama kuhusu suala la kumuona Allah usingizini hili pia si katika maudhui ya kitabu hiki.

Rudi juu

 

SURA YA PILI

 

UCHAMBUZI YAKINIFU JUU YA ELIMU YA HADITHI.

 

Kabla ya kuanza kuzitaja hoja na dalili wanazozitegemea Ahli sunna wal- Jamaa juu ya kuonekana Allah kwa macho huko akhera, kwanza napenda kuzungumzia suala linalofungamana na elimu ya istilahi ya upokezi wa riwaya za hadithi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- na suala hili litakuwa katika nukta zifuatazo:

 

i) Kwanza, tufahamu kuwa mafundisho yote ya bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- ni wahyi (ufunuo) utokao kwa Allah, na Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- hazungumzi kwa matashi wala matamanio ya nafsi yake.

 

ii) Pili, mafundisho yote ya Mtume wetu Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- yamehifadhiwa katika vitabu vya maulamaa wa Ahlu Sunna wal-Jamaa kwa ufanisi mkubwa mno kiasi ambacho hakuna jambo lolote linalohitajika kubainisha itikadi au hukumu ya mambo ya dini ya kiislamu isipokuwa jambo hilo limedhibitiwa kwa ufanisi wa hali ya juu.

 

iii) Tatu, katika kuhakikisha kuwa mafundisho hayo sahihi ya dini ya kiislamu yanahifadhiwa na hayachanganyiki na upotofu wowote, maulamaa wa Ahli Sunna wal Jamaa wameweka misingi madhubuti juu ya usahihi wa mapokezi hayo ya riwaya za hadithi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- na ukweli wa wapokezi hao kama tulivyofundishwa na Quran tukufu pale aliposema Allah:

Enyi mlioamini ! akikujilieni mwovu (fasiki) na habari yoyote ichunguzeni basi.

al Hujraat (49) aya 6.

 

Kwa mujibu wa aya hii ni kwamba, si kila asemaye; amesema Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- atakuwa msemaji huyo ni mkweli, na atakayo yanukuu yatakuwa ni kweli maneno ya Mtume, bali ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua usahihi wa habari hiyo aliyoileta na udhaifu wake.

 

Kwa sababu hiyo, maulamaa wa hadithi baada ya kufanya utafiti wa kina pamoja na kutumia uzoefu wao wa muda mrefu, wakaweka misingi madhubuti inayowahusu wapokezi wa hadithi.

Pia wakaweka kanuni maalumu kwa ajili ya udhibiti wa njia sahihi za kukubaliwa hadithi na kurudishwa.

Na pia yakatumika maneno ya kiistalahi ambayo yanaleta maana maalumu na hayo yamejaa kwa wingi katika vitabu vyao.

 

Kwa mantiki hiyo, yeyote anayetaka kuzungumzia masuala yanayofungamana na elimu ya hadithi; usahihi wake na udhaifu wake, hana budi kuzijua kanuni hizo na maneno hayo ya kiistilahi.

Na kama hatafanya hivyo, basi lililobora kwake ni kunyamaza kuliko kusema, kwa sababu hatima yake ni kupotosha watu kwa kuzisahihisha hadithi zisizo sahihi au kuzidhoofisha hadithi zilizo sahihi na yote mawili ni balaa, hasa ukizingatia kwamba maneno ya Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- ni sheria.

 

Rudi juu

MASHARTI YA USAHIHI WA HADITHI

 

1) Uadilifu, ni lazima kila mpokezi wa hadithi za Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- awe ni mtu mwenye akili timamu,mwenye uwezo wa kupambanua mambo hata kama ni mtoto mdogo, awe mkweli, mcha mungu na wala asiwe mwongo, wala asiwe mwenye kufanya maasia kwa dhahiri wala asiwe na tabia mbaya zenye kuvunja heshima.

2) Hifdhi nzuri, mpokezi awe na uwezo wa kudhibiti maneno aliyo yapokea, bila ya kubadilisha chochote katika maana yake,au kukosea sana,au kubabaika kulikopetuka mipaka wakati wa kusimulia mapokezi hayo.

3) Kuungana kwa sanadi (msururu wa wapokezi) kwa kuwa kila mpokezi awe amepokea kutoka kwa aliye juu yake mpaka mwisho wake (kwa huyo ambaye habari hiyo imenasibishwa kwake, ima bwana -Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-, au swahaba, n.k.

4) Isiwe habari aliyoileta mpokezi huyo ni SHAADHUN (ni yenye kupingana na habari ya mpokezi mwingine aliye madhubuti au wengi zaidi kuliko yeye).

5) Wala isiwe na ila (kasoro iliyojificha) kama vile Idhtiraabu (mgongano baina ya wapokezi n.k) au kuwa ni habari Maqluub (yenye kugeuzwa)

 

Katika masharti haya tuliyoyataja, yako ambayo likikosekana moja tu basi hadithi haitakubaliwa,kama vile:

1-Kuwa mpokezi si muadilifu,kwa kuwa ni mwongo au asherati n.k.

2-Kupatikana kasoro kama vile mgongano katika sanadi (njia) au mgongano wa maneno katika habari hiyo, kisha ikawa imeshindikana kuziunganisha au kuipa nguvu njia moja juu ya nyingine.

 

Tanbihi:

Habari inaweza kuwa na njia nyingi, na katika njia hizo wakawepo wapokezi wasio madhubuti kwa kuwa wanakosea kiasi, au silsila (mtiririko) wa wapokezi haukuungana, kutokana na wingi wa njia hizo habari hiyo itapata uzito na kuhesabiwa kuwa ni sahihi, na kwa lugha ya kitaalamu huwa wanaiita HASANUN-LIGHAIRIHI.

 

Amesema Imamu An-Nawawiy:

 

Bali ile hadithi ambayo imekuwa ni dhaifu kwa sababu ya udhaifu wa mpokezi wake ambaye ni mkweli mwaminifu utaondoka (udhaifu huo) kwa kuja kwake kupitia njia nyingine na itakuwa ni HASAN (sahihi)

Na vile vile ukiwa udhaifu wake ni kwa sababu ya Irsaal (atakaposema TaabiI amesema Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-) pia udhaifu huo utaondoka kwa kuja (kupokewa) kwa njia nyingine.

 

Hivyo basi, inawezekana ukaifuatilia hadithi kisha ukazikuta takriban njia zake zote zina udhaifu, hapo hutakiwi kuwa na pupa na kuanza kuihukumu hadithi yote kuwa ni dhaifu, bali unatakiwa kuihukumu sanad husika tu, na useme kwamba sanad ya hadithi hii ni dhaifu.

 

Kwa sababu udhaifu wa sanad moja tu, si ushahidi wa udhaifu wa hadithi yote yenye njia nyingi.

Na kama ukitaka kuihukumu hadithi yote kwa njia zake zote unatakiwa ufanye kazi ya kuzikusanya sanad (njia) zote kisha ndiyo uichambue sanad moja baada ya nyingine kwa kufuata kanuni na taratibu za elimu ya hadithi (mustalahul-hadithi).

Na kama itakubainikia kuwa njia zote zina udhaifu, basi pia unatakiwa kuangalia sababu za udhaifu wake.

Je udhaifu wake ni mwepesi au mzito?

Kama ni mwepesi basi hadithi hiyo kwa kuzijumuisha njia zote hizo itakuwa ni Hasanun-Lighayrihi (sahihi) na itafaa kuifanya kuwa ni hoja ya kisheria, na wala haitohesabiwa kuwa ni dhaifu.

Hili ni jambo muhimu sana katika elimu ya hadithi kulifahamu na kulizingatia, lakini ndugu Juma kwa makusudi hakuuzingatia utaratibu huu kwenye kitabu chake Hoja zenye Nguvu kwa sababu anazozijua mwenyewe, kwani yeye ndiye aliyesema hivi:

kitaalamu ikiwa hadithi imepokewa na wapokezi wengine kabisa, lakini hadithi ni ile ile, basi huambiwa kuwa hadithi hiyo ina shahidi.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama Hoja zenye Nguvu ukurasa 70.

 

Lakini huko mbele -Inshaallah- utazigumdua sababu zilizomfanya ndugu Juma aupuuze utaratibu huu.

Rudi juu

 

TUHUMA ZA UWONGO DHIDI YA AHLI SUNNA

 

Kama ilivyokuwa kawaida ya watu wanaofuata matamanio ya nafsi zao katika mambo ya dini kama vile: Mayahudi, Manasara, Washirikina na kadhalika watu wa bida, huwa hawaachi kuwasema vibaya wale walioshikamana na njia sahihi na kuwataja kwa kebehi na uovu, tena mpaka kufikia kuwazulia uwongo.

 

Huu ndiyo mwenendo wao na sera yao tangu zamani, jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa hata ndugu Juma naye ameifuata njia hiyo ovu dhidi ya Ahli Sunna wal-Jamaa.

 

Amekianza kitabu chake kwa mashambulizi yasiyo na ukweli dhidi ya Ahli Sunna na maulamaa wao, tena bila ya kuwa na insafu wala uadilifu, bali chuki binafsi na uadui ndivyo vilivyomuongoza na kumsababishia kuacha kuyahakiki mambo kwa njia za kielimu, kwa mfano:

 

1-Hakuna kitu kingine zaidi ya chuki kilichomfanya awaite Ahlu Sunna kwa jina la Mawahabi, au Hashawiya, au Mujasima.

 

2- Hakuna kitu kingine zaidi ya chuki dhidi ya Ahli Sunna kilichomfanya awatie kasoro kwa mambo ambayo hayakuthibiti kuwa ndiyo itikadi yao, kama suala la kuwa Allah ana sura ya kijana, au ana viatu vya dhahabu na mengineyo.

 

3-Hakuna jambo jingine zaidi ya chuki na uadui lililompelekea kuwatuhumu baadhi ya wanavyuoni wa Ahli Sunna kama vile Ibn Taymiyyah na Ibn Al-Qayyim kwa sababu ya misimamo yao na kuwaita kuwa ni wanavyuoni wa kiwahabi! Maimamu wa Hashawiya! Mujasima! Na hali yakuwa hakuna tofauti yoyote baina ya misimamo yao hiyo na misimamo ya Maimamu wakubwa wa Ahli Sunna kama vile: Abu Hanifa, Imamu Malik, Imamu Shaafiy, Imamu Ahmad Ibn Hanbal, Imamu Bukhari, Imamu Muslimu, Imamu Abu Daud, Imamu Tirmidhiy, Imamu Abul-Hasan Al-Ashariy, Imamu Abdul-Qadir Jaylaaniy !!!

Kwamfano katika suala la sifa za Allah: kuwa Allah ana mikono miwili, ana macho mawili, ana uso, anacheka, ana mguu na nyinginezo katika sifa za Allah za ukamilifu ambazo amejisifia nazo au amesifiwa na Mtume wake swalla llaahu alayhi wasallam- utawakuta maimamu hawa wakubwa wanazithibitisha sifa hizo kama zilivyopokewa, na hivyo ndivyo anavyofanya Ibn Taymiyya na Ibn al-Qayyim.

 

Lakini Juma kwa sababu ya chuki zake dhidi ya Ibn Taymiyya na Ibn al-Qayyim akalizungumzia suala hilo kwa sura ambayo msomaji anaweza kudhania kuwa Ibn Taymiyya na Ibn al-Qayyim wana itikadi ambayo si ya kiislamu na wala hakuna muislamu yeyote mwenye itikadi hiyo ila Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibnul-Qayyim.

 

Kwa mfano amesema Juma:

Na itikadi hizi ambazo nitakutajia sasa hivi (Inshala) zimo hasa katika madhehebu ya kiwahabi na wao wamezirithi kutoka kwa maimamu wa madhehebu za Al-hashawiya Al-mujasima kama Ibn Taymiyya Ibn Qayyim Al-jawziya na wengineo.Mwisho wa kunukuu. Tazama kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 23.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Sisi tunasema kwamba msimamo wa Sheikhul-Islami Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim katika masala ya sifa za Allah hauna tofauti na msimamo wa Quran na Sunna, bali ndiyo msimamo wa maswahaba na wanafunzi wao, na ndiyo msimamo wa maulamaa wakubwa waliokuja baada ya wanafunzi wa maswahaba, kama vile: Abu Hanifa, Malik, Shaafiy, Ahmad bin Hanbal, Abul-Hasan al-Ashariy na wengineo katika maimamu wakubwa, kwa hiyo kumuita Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim kuwa ni maimamu wa Hashawiya Mujasima ni matusi dhidi maimamu hao wote waliotangulia kama tutakavyoona hapo mbeleni Inshaallah.

 

Rudi juu

TUHUMA YA KWANZA

 

Kisha akasema ndugu Juma katika ukurasa wa 23:

Falsafa ya Ibn Taymiyya kuhusu maumbile ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia kama alivyosema haya katika kitabu chake NAQDU MARATIBIL AL-IJMAA.

Nini maana ya sifa ya kutangulia? Sisi waislamu tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu tu ndiye mwenye sifa ya kutangulia, yaani kabla yake hapakuwa na kitu chochote: kila kilichopo tunapopajua na tusipopajua, tunapopaona na tusipopaona basi ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu.

Lakini itikadi ya Ibn Taymiyya wanaemwita Sheikh wa waislamu ni kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa navyo vitu ambavyo kutokana na hivyo ndio kaanzia kuumba maumbile yote.

Sasa suala ni kuwa hivi vitu vya nani? Je haoni yeye huyu Ibn Taymiyya kuwa falsafa hii inapelekea kurudi kwenye itikadi ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu zaidi ya mmoja?

Huyu ndiye ambaye Mawahabi wanamwita Sheikh Al-islam.

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Maneno yote haya ya ndugu Juma ni maneno ya uwongo yaliyojaa chuki dhidi ya mwanachuoni huyu mkubwa wa kiislamu, si kweli kwamba itikadi ya Ibn Taymiyya ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia.

Na wala maneno ya Ibn Taymiyya katika suala hili hayapelekei kwenye dhana ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja, lakini huo ni ufahamu mbaya wa ndugu yetu Juma uliosababishwa na chuki binafsi dhidi ya maulamaa wa Ahli Sunna hasa Ibn Taymiyya.

 

Katika kubatilisha madai haya ya uwongo ya Juma, hebu tukunukulie kidogo ndugu msomaji maneno ya Ibn taymiyya yanayohusu masuala haya ya maumbile, amesema Ibn Taymiyya:

- - ɡ - - (( )) 26

8/272

 

KILA KISICHOKUWA MOLA NI CHENYE KUZUKA KIMEPATIKANA BAADA YA KUTOKUWEPO, ay eye (Allah) Subhanah- ndiye mwenye kuhusishwa na kutangulia na azal, hakuna kitu katika viumbe vyake kilichokuwa ni chenye kutangulia, hata kama ikikadiriwa kuwa yeye (Allah) hakuacha kuwa ni mwenye kutenda, (lakini) hakuna kitu kilichotangulia kwa kutangulia kwake, bali hakuna kabisa katika viumbe (vyake ambavyo ) ni vyenye kutangulia, BALI HAKUNA KILICHOTANGULIA ILA YEYE (ALLAH) Subhaanah-.

Na yeye pekeyake ndiye mwenye kukiumba kila kisichokuwa yeye, kila kisichokuwa yeye ni chenye kuumbwa kama alivyosema Subahaanah-:

((Allah ni muumba wa kila kitu)). Surat Zumar aya ya 26.

Tazama kitabu Daru Taarudh juzuu ya 8 ukurasa wa 272 cha Ibn Taymiyya.

 

Ndugu msomaji, je kwa maneno haya umefahamu kwamba Ibn Taymiyya ana itikadi ya kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia kama anavyodai Juma?

 

Au umefahamu kwamba Ibn Taymiyya anasema kuwa kila kisichokuwa Allah ni chenye kuzuka na kimepatikana baada ya kutokuwepo?

 

Je kwa maneno haya ya Ibn Taymiyya umefahamu kwamba ana itikadi ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja kama anavyodai ndugu Juma kuwa sheikhul islam Ibn Taymiyya ana itikadi hiyo?

Au umefahamu kwamba ndugu Juma si mkweli?

Hebu yatupie jicho maneno mengine ya Sheikul-Islam Ibn Taymiyya tuone anavyosema:

" .. "

18/227-228

Kila kitu katika vitendo vyake hakuna budi kuwa ni chenye kutanguliwa na mwenye kutenda na ni chenye KUTANGULIWA NA KUTOKUWEPO. NA HAIWEZEKANI KUWA KITENDO FULANI KILIKUWEPO PAMOJA NA MTENDAJI TANGU MWANZO NA AZAL..

Mwenye kutenda (ambaye ni Allah) anakitangulia kila kitendo katika vitendo vyake na hilo linawajibisha kuwa KILA KISICHOKUWA YEYE (ALLAH) NI CHENYE KUZUKA NA NI CHENYE KUUMBWA.

Tazama Majmuul-Fatawa juzuu ya 18 ukurasa wa 227-228.

Bila shaka maneno haya yako wazi katika kuufichua uwongo wa ndugu Juma na wala hayahitajii maelezo.

Rudi juu

 

TUHUMA YA PILI

 

Kisha ndugu Juma akaleta tuhuma nyingine dhidi ya Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake (Ibn al-qayyim) kuhusiana na suala la sifa za Allah akasema:

Anasema Ibn Al-qayyim katika kitabu chake HADI AL-ARWAAH ukurasa wa 13 akitaja sifa za Mwenyezi Mungu anasema:

na kwamba yeye (Mwenyezi Mungu) ana mikono miwili bila ya mfano na ana macho mawili na ana uso. Naye Ibn Al-qayyim anasema kuwa kayanukuu maneno haya kutoka kwa Abul-hasan Al-ashari.

Lakini kudai kwamba maneno haya ni maneno ya Al-imamu Al-ashari ni kitu cha kutazama zaidi kwani wafuasi wa Al-imamu Al-ashari nao ni masuni kama mashafi hawakubaliani na haya.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama ukurasa wa 24-25 katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu dhidi ya maneno haya ya ndugu Juma yatakuwa katika nukta kuu tatu:

Nukta ya kwanza:

Suala kuwa Allah ana Mikono miwili bila ya mfano.

Ana Macho mawili bila ya mfano.

Ana Uso bila ya kuwa na mfano.

Hii si itikadi ya Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake peke yao, hiyo ndiyo itikadi iliyo elezewa na Quran na Sunna na ndiyo itikadi ya maswahaba na wanafunzi wao na ndiyo itikadi ya maimamu wakubwa wa kiislamu.

Amesema Imamu Shaafiy Allah amrehemu-:

 

" ....... (( )).

:

"........ (( )).

 

Allah Tabaaraka Wataalaah- ana majina na sifa ambazo zimetajwa na kitabu chake na amezielezea Mtume wake swalla llaahu alayhi wasallam- kwa uma wake zimetufikia (habari) kuwa yeye ni mwenye kusikia na ana mikono miwili kwa kauli yake (Allah) : Bali mikono yake (Mwenyezi Mungu) iwazi.

Na akasema tena (Imamu Shaafiy) Allah amrehemu-:

 

..Na yeye (Allah) ana Uso kwa sababu ya kauli yake (Allah):

((Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa Uso wake)).

Tazama kitabu Twabaaqatul-Hanabila juzuu ya 1 ukurasa wa 283-284 cha Imamu Ibn Abi Yaala.

Pia tazama kitabu Manhaju Imami Shaafiy fi Ithbatil-Aqidah ukurasa wa 370-378. cha Dkt. Muhammad al-Aqil.

 

:

.

: .

......".

1/ 166 772.

 

Amesema Imamu Abu Issa Al-Tirmidhiy Allah amrehemu- alipoitaja hadithi namba 772:

Na wamesema wengi katika wanavyuoni kuhusu hadithi hii na inayofanana na hii katika mambo ya sifa (za Allah) na kushuka Mola katika mbingu (iliyokaribu na) dunia, wamesema: zimethibiti riwaya nyingi kuhusu suala hili, na sisi tunaliamini na wala hatusemi kwa dhana na wala hatusemi vipi? Na hivi ndivyo ilivyopokelewa kutoka kwa Malik,Ibn Uyaina, na Abdullahi bin Mubarak kuwa wamesema kuhusu hadithi hizi: zipitisheni bila ya kuzipa namna.

Na hii ndiyo kauli ya wanavyuoni wa Ahli Sunna wal-Jamaa. Ama Jahmiya wao wamezipinga riwaya hizi na wakasema: huko ni kumfananisha Allah (na viumbe).

Na hali yakuwa ametaja Allah katika kitabu chake katika sehemu nyingi: (ametaja kuwa ana) Mkono, Usikivu, Uoni.

Lakini Jahmiya wakazitafsiri aya hizi tofauti na wanavyuoni, wakasema: Allah hakumuumba Adam kwa mkono wake, na (wakasema kuwa) maana ya mkono hapa ni nguvu.

Na amesema Ishaq bin Ibrahim: inakuwa ni kumfananisha Allah (na viumbe) atakaposema: Mkono (wa Allah) ni kama mkono au mfano wa mkono (wa kiumbe).

Tazama kitabu chake Jamiul-Tirmidhiy/Sunan Tirmidhiy hadithi namba 772.

[224-310]:

" , , : (( ))

: (( )) : (( )) : (( ))......".

224.

 

Amesema Imamu Abu Jafar Muhammad bin Jarir al-Tabariy aliyefariki mwaka [310 H]:

Kauli katika yale yaliyofahamika ujuzi wake katika sifa (za Allah) kwa habari, ni mfano wa kuelezea kwake (Allah) -Azza wajalla- kuwa yeye (Allah) ni mwenye kusikia mwenye kuona, na kwamba yeye (Allah) ana mikono miwili aliposema:

Bali mikono yake (Mwenyezi Mungu) iwazi.

 

Na kwamba yeye (Allah) ana Uso pale aliposema:

Na utabakia Uso wa Mola wako

 

Na kwamba yeye Allah ana Mguu, kwa kauli ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-: Mpaka atakapo weka Mola ndani yake Mguu wake

 

Na kwamba yeye (Allah) anacheka kwa kauli yake Mtume:

Na atakutana na Allah na hali ya kuwa anamchekea.

 

Tazama kitabu Mukhtasarul-Uluwi ukurasa wa 224.

[392-463]:

" : , , , , : ....".

" " 16/ 43-44. 272.

 

Amesema Imamu Abu Bakar al-Khatib al-Baghdadiy aliyefariki mwaka [463 H]:

Sisi tunaposema: (kuwa Allah ana) Mkono, Usikivu,na Uoni ni kuthibitisha sifa za Allah kama alivyo jithibitishia mwenyewe, na wala hatusemi maana ya mkono ni uwezo...

Tazama Mukhtasarul-Uluwi ukurasa 272.

 

Hizi ni baadhi ya kauli za maulamaa wa Ahli Sunna ambao wamemtangulia Ibn Taymiyya kwa karne nyingi.

Wao wanasema kuwa Allah ana Macho, Mikono miwili, Mguu, n.k. na hiyo ndiyo itikadi ya maimamu wote wanne: Abu Hanifa, Malik, Shaafiy, na Ahmad bin Habal, sasa kwanini ndugu Juma ainasibishe itikadi hii sahihi na Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim peke yao?

 

Kwani kuna kioja gani kwa mtu kumsifia Allah kwa sifa ambazo amejisifia nazo mwenyewe katika Quran na amesifiwa na Mtume wake swalla llaahu alayhi wasallam-?

Je wakumshangaa ni yule aliyehalifu hilo au yule aliyetii? Ama kweli walimwengu wana mambo !

 

Amesema tena Juma:

Lakini kudai kwamba haya ni maneno ya Al-imamu Al-ashari ni kitu cha kutazamwa zaidi kwani wafuasi wa Al-imamu Al-ashari nao ni masuni kama mashafi hawakubaliani na haya.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Kwa maneno haya ya ndugu Juma anatuwekea wazi zaidi namna asivyokuwa mtafiti mzuri wa mambo na huwa hukumu zake ni za kubuni.

 

Tangu lini mtu akahukumiwa kwa matendo ya watu wengine?

Kuwa wafuasi wa Abul-Hasan al-Ashari wako kinyume na itikadi yake, basi hiyo ndiyo hoja yakwamba hakusema maneno hayo?

Kwanini usiwashangae watu wanaodai kuwa ni wafuasi wa Imamu Shaafiy katika mambo ya twahara na swala lakini katika mambo la itikadi wamemfuata Abul-Hasan na wako kinyume na Imamu wao?

Kwanini wamemkwepa Imamu Shaafiy aliyefariki mwaka 205 H na kumfuata Abul-Hasan al-Ashariy aliyezaliwa mwaka 260 H na kufariki mwaka 324 H?

Abul-Hasan yeye amezaliwa nusu karne baada ya Imamu Shaafiy kufariki, je Imamu Shaafiy hakuwa na itikadi yoyote? Na je yeye alikuwa akimfuata nani?

Rudi juu

 

HISTORIA YA ABUL-HASAN KWA UFUPI

 

Abul-Hasan al-Ashariy jina lake kamili ni: Aliy bin Ismail bin Ishaq bin Salim bin Ismail bin Abdillahi bin Musa bin Abi Burda bin Abi Musa al-Ashariy, amezaliwa mwaka 260 H.

 

Mwanzoni mwa uhai wake alikuwa na itikadi ya Mutazila kwa muda wa miaka 40 na sababu yakuwa na itikadi hiyo ni sheikh wake aliyesoma kwake ambaye ni baba yake wa kufikia (mume wa mamake) jina lake ni Abu Aliy al-Jubbai, yeye alikuwa na itikadi potofu za Mutazila (itikadi za kupinga sifa za Allah) na hiyo ni itikadi iliyo anzishwa na Waasil bin Atwaa.

 

Kisha Imamu Abul-Hasan akaiwacha itikadi hiyo ya Mutazila na kuifuata itikadi ya Ibn Kullaabi kwa muda, na miongoni mwa itikadi za Ibn Kullaabi ni kumthibitishia Allah sifa saba tu, sifa ya: Uhai, Elimu, Uwezo, Utashi, Usikivu, Uoni, na kusema.

Na ama sifa nyingine zote kama vile Uso, Mikono miwili, Mguu na mfano wa hizo alizipa tafsiri potofu.

 

Alijifungia ndani kwake kwa muda wa siku kumi na tano kisha akatoka akaelekea msikiti mkuu wa Basra akapanda juu ya mimbari baada ya swala ya Ijumaa kisha akawaambia watu, nilijificha kwenu kwa muda kwa sababu nimezitazama dalili lakini zikawa sawa kwangu na haikunipambanukia haki na batili, nikamwomba Allah aniongoze ndipo akaniongoza kwenye haya niliyo yaweka humu kwenye vitabu hivi, na nimejivua na yale yote niliyokuwa nikiyaitakidi kama ninavyoivua kanzu yangu hii, kisha akaivua kanzu yake na akaitupa kwa watu, kisha akavitoa vitabu vyake akawapa watu.

 

Na miongoni mwa vitabu vyake ni al-Ibana an Usuli-Diyana na ndani ya kitabu hicho amesema wazi wazi kwamba msimamo wake huo ndiyo msimamo wa Salaf Swalih msimamo wa maimamu wakubwa kama vile: Malik, Shaafiy, Ahmad bin Hanbal na wengineo na kuwalingania watu washikamane nao.

 

Na wanavyuoni walio lithibitisha suala hili la kutubia kwake, kuacha misimamo hiyo potofu na kushikamana na msimamo wa Salaf Swalih na kuandika kitabu al-Ibana, ni hawa wafuatao:

1-  Abul-Qasim Aliy bin al-Hasan bin Hibatu-llaahi Ibn Asaakir aliyefariki mwaka 571 H, katika kitabu chake al-Tabyiin ukurasa wa 28.

2-  Imamu al-Baihaqiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 458 katika kitabu chake al-Itikad ukurasa wa 31na 32.

3-  Imamu al-Dhahbiy aliyefariki mwaka 748 H katika kitabu chake al-Uluwu ukurasa wa 160.

4-  Imamu Ibn al-Imadi aliyefariki mwaka 1098 H katika kitabu chake Shadharaatul-Dhahbi ukurasa wa 303.

5-  Imamu Abul-Hasan al-Sayyid Murtaza al-Zabidiy katika kitabu chake Ithafu Saadatil- Mutaqina juzuu ya 2 ukurasa 2.

6-  Imamu Ibn Kathir al-Qurashiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 774H, katika kitabu chake al-Bidayatu wal-Nihayah juzuu ya 11 ukurasa wa 187.

7-  Imamu Taaju-Din Abu Nasri Abdul-wahab bin Taqiyu-Din al-Subkiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 771 H, katika kitabu chake Twabaqaatu al-Shaafiiya al-Kubraa juzuu ya 2 ukurasa 246.

 

Na wengi katika maulama ambao hatukuwataja, wote hao wamekiri na kuthibitisha katika vitabu vyao tulivyo vitaja kuwa Abul-Hasan aliziwacha itikadi zote hizo potofu na kushikamana na itikadi sahihi ya Salaf Swalih na akatunga kitabu al-Ibana.

Rudi juu

 

YALIYOMO KATIKA KITABU AL-IBANA

 

Hebu tunukuu baadhi ya maneno yake kutoka kwenye kitabu hicho ili tuone je anayoyasema yeye yanatofauti yoyote na yale anayoyasema Ibn Taymiyya na mwanafuzi wake?Au chuki binafsi inafanya kazi yake?

 

Anasema Abul-Hasan baada ya kuzitaja itikadi potofu za watu wa bida na kuzipinga:

 

"

: , .

: , : , , , - .....

..... : (( )) 5.

: (( )) 27.

: (( )) 75.: (( )) :64.

: (( )) 14...".

MLANGO WA PILI

Katika kuibainisha kauli ya watu wa haki na sunna Ikiwa atasema mwenye kusema : mmeipinga kauli ya Mutazila, na kauli ya Qadariya (wenye kupinga Qadari) na kauli ya Jahmiya na kauli ya Haruuriya (miongoni mwao ni maibadhi) na kauli ya Raafidha (Shia) na kauli ya Murjia (wenye kuitakidi kuwa watu wote ni sawa katika imani) basi hebu tuelezeeni kauli yenu na msimamo wenu ambao mnaufuata.

 

Ataambiwa: Kauli yetu tunayoisema na msimamo wetu tunaoufuata ni kushikamana na kitabu cha Mola wetu na Sunna za Mtume wetu swalla llaahu alayhi wasallam- na yale yaliyopokelewa kutoka kwa mabwana wakubwa katika maswahaba na Taabiina (wanafunzi wa maswahaba) na maimamu wa hadithi, sisi ni wenye kushikamana na hilo na yale anayoyasema Abu Abdillahi Ahmad bin Muhammad bin Hanbal Allah autie nuru Uso wake na ainyanyue daraja yake na ampe thawabu kwa wingi- sisi ni wenye kuyasema..

 

Na jumla ya kauli ni kuwa sisi tunakiri kwamba .Allah yuko juu ya Arshi yake kama alivyosema: ((Allah mwingi wa rehma yuko juu ya Arshi)) Twaha aya ya 5.

 

Na kwamba yeye Allah ana uso bila kuwa na namna kama alivyosema: ((Na utabakia Uso wa Mola wako wenye utukufu)). Al-Rahman aya ya 27.

 

Na kwamba yeye ana mikono miwili bila ya kuwa na namna kama alivyosema Allah: ((Niliye muumba kwa mikono yangu miwili?)) surat Saad (38) aya ya 75.

Na akasema ((Bali mikono yake (Allah) iwazi)) al-Maida aya ya 64.

 

Na kwamba yeye ana jicho bila kuwa na namna kama alivyosema: ((Linakwenda(jahazi la Nuh) kwa uwangalizi wa macho yetu)) al-Qamar aya ya 14.

 

Tazama katika kitabu chake al-Ibana kuanzia ukurasa wa 38-44, chapa ya Daarul-Bayaan Damascus - Syria ya mwaka 2004.

 

Bila shaka ndugu msomaji kwa mujibu wa nukuu hizi utakuwa umefahamu kwamba itikadi anayoielezea Ibn Taymiyya ndiyo itikadi halisi ya Ahli Sunna, itikadi ya maimamu wakubwa waliotangulia ambayo ndiyo itikadi iliyoelezwa na kitabu kitukufu Quran na Sunna sahihi za Mtume Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam-.

 

Na hiyo ndiyo itikadi ya Imamu Abul-Hasan al-Ashariy, kama alivyojielezea mwenyewe katika kitabu chake, kwa hiyo maneno ya ndugu Juma yanayotilia shaka maneno ya Ibn al-Qayyim na kudai kuwa ni maneno ya kutazamwa, madai hayo hayana uzito wowote wa kielimu.

Rudi juu

 

TUHUMA YA TATU

 

Ndugu Juma hakuchoka kusema uwongo na kuwatuhumu maulamaa wa Ahli Sunna, bali akaamua kumzushia Imamu Ibn al-Qayyim tuhuma nyingine nzito, amesema ndugu Juma:

katika kuifasiri aya ya Mwenyezi Mungu inayosema kwamba:

 

" "

Wamemsahau Mwenyezi Mungu na yeye akawasahau.

Sura ya 9 aya 67.

Kaifasiri aya hii kuwa ni kusahau kweli kweli akasema: Zingatia kauli yake Mwenyezi Mungu (katika aya hio na ilio mfano wa hio) namna alivyofanya uadilifu kamili kwao akawasahau kama walivyo msahau !!!.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama ukurasa wa 25 wa kitabu chake.

 

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

Miongoni mwa mambo mabaya kabisa katika uislamu ni kumzulia mtu jambo asilolifanya au asilosema, na kama mtu mwenyewe ni mwanachuoni basi ubaya unakuwa maradufu.

Vitendo vya ndugu Juma anavyovifanya dhidi ya maulamaa ni hiyana na ni dhulma ambayo inamporomoshea mtu uadilifu wake na kumfanya asikubaliwe maneno yake.

Je ni kweli Ibn al-Qayyim anasema kuwa Allah anasahau kweli kweli?

Au Juma amekusudia kusema uwongo ili kupotosha?

 

Jawabu ni kwamba, si kweli kuwa Ibn al-Qayyim anaitikadi kwamba Allah anasahau, bali itikadi yake ni itikadi ya Quran na Sunna kuwa Allah hasahau, lakini ndugu yetu Juma alikusudia kupotosha kama ilivyo kawaida ya watu wa batili.

 

Na ushahidi wa kuwa Ibn al-Qayyim hana itikadi hiyo chafu ni pale alipokuwa akiitafsiri kauli ya Allah isemayo:

" (( )) 52 :

, "!!!!!

141 1424

 

[Ujuzi wake (karne hizo) uko kwa Allah] surat Twaha aya ya 52:

Makusudio ni kwamba matendo ya karne hizo (zilizopita) kufru zao na shirki zao zote zinajulika kwa Mola wangu amezidhibiti, amezihifadhi na ameziweka katika kitabu na atawalipa siku ya Qiyama, na hakuziweka katika kitabu kwa sababu ya kuogopea kusahau na kupotea

KWA SABABU YEYE SUBHANAH- HAPOTEI WALA HASAHAU!!!!!

Tazama kitabu chake Shifaul-Alili ukurasa wa 141 chapa ya Darul-kitabil- Arabi Beirut Lebanon,chapa ya kwanza mwaka 2004.

 

Swali, kwa mujibu wa maneno haya, je ndugu msomaji umefahamu kwamba Ibn al-Qayyim itikadi yake ni kuwa Allah anasahau au hasahau?

Je umegundua kwamba Juma al-Mazrui anaendelea kusema uwongo?

 

Pengine Juma mwenyewe au mtu mwengine katika wapenzi wake anaweza kusema: lakini maneno hayo siyo aliyo yanukuu kutoka kwa Ibn al-qayyim bali yeye amenukuu maneno mengine kwenye kitabu kingine ambayo Ibn al-Qayyim anaelezea kwa uwazi kuwa Allah anasahau kweli kweli!

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Sababu ya kunukuu kauli hiyo ya Imamu Ibn al-Qayyim ni kutaka kukuthibitishia ndugu msomaji kwamba Ibn al-Qayyim hana itikadi hiyo ya kikafiri ambayo ndugu Juma amembabatiza nayo.

 

Kisha ndiyo tutupie macho hayo maneno ya Ibn al-Qayyim aliyo yanukuu Juma, na tutakapoyatazama tunakuta kwamba Ibn al-Qayyim hakutoka nje ya ibara ya Quran na Sunna, na wala maneno yake hayamaanishi kuwa Allah anasahau kweli kweli. Na kama maneno hayo yanaleta maana hiyo, basi hata Quran yenyewe na Sunna zitakuwa zina maanisha hivyo.

 

Ibn al-Qayyim katika maneno yake ametumia ibara isemayo:

" "

Bi an-nasiyahum kamaa nasuuhu

Maana yake Kiswahili ni kwa kuwa amewaacha (amewapuuza) wao kama walivyo msahau (walivyompuuza)

Na ibara hiyo hiyo ndiyo iliyotumika katika Quran amesema Allah:

" "

 

Wamemsahau Allah naye akawaacha (akawapuuza) .

 

Na haya hapa ni maneno ya Ibn al-Qayyim kwa ukamilifu :

 

" (( )) : (( )) ".

1/210

 

Izingatie kauli yake al-Haq (Allah) Wamemsahau Allah na yeye akawaacha wao (katika adhabu), na kauli yake Wala msiwe kama wale ambao wamemsahau Allah na yeye akawasahaulisha nafsi zao (zingatia) namna alivyo wafanyia wao uadilifu kwa kuwa walimsahau na yeye akawaacha (katika adhabu).

Tazama kitabu Mukhtasaru Sawaaiqil-Murslah juzuu ya 1 ukurasa wa 210.

Hapa nataka kuelezea kitu kimoja muhimu kwa faida ya wasomaji:

 

Tulipo litafsiri neno Nasiya hum kwa maana ya kuacha, lengo si kutaka kuleta taawili na kupotosha.

Bali neno hili la kiarabu Nasiya ambalo limetasuliwa (limenyambuliwa) kutoka kwenye asili ya neno Al-Nisyaanu lina maana mbili na zote ni za asili.

 

Amesema Imamu Abul-Husain Ahmad bin Faaris aliyefariki mwaka 395 H, katika kamusi yake Mujamu Maqaaisil-Lugha ukurasa wa 987:

 

" : : , ".

987.

 

Nasiya: Nuni, Siin, na Yaau ni asili mbili zilizo sahihi: moja yao inafahamisha

Kughafilika na ya pili ni Kuacha kitu.

 

Kwa hiyo tumefahamu kuwa neno Nasiya lina maana mbili:

i)            Kughafilika.

ii)           Kuacha.

 

Na kwa mujibu wa kanuni na misingi ya elimu ya itikadi linapotumika neno lolote lenye zaidi ya maana moja: Maana moja inalingana na utukufu wa Allah, na maana ya nyingine hailingani na utukufu wake Allah, basi neno hili litachukuliwa kwa maana ambayo inalingana na utukufu wake Allah.

 

Kwamfano hapa limetumika neno Nasiyahum ambalo maana yake ima itakuwa :

(Allah) Amewasahau wao au (Allah) Amewaacha wao.

Tukitazama baina ya maana mbili hizi, ni ipi inayonasibiana na utukufu wake Allah Jalla Jalaaluh-?

Bila shaka kulitumia neno hili kwa maana ya kuacha ndiyo sahihi bali ni wajibu kufanya hivyo kwa sababu Allah hasahau kama ilivyotuelezea Quran na Sunna na alivyotuelezea Ibn al-Qayyim hapo nyuma.

Na hakuna shaka kwamba naye Ibn al-Qayyim amelitumia neno hili hapa kwa maana inayolingana na utukufu wake Allah, nayo ni kwa maana ya kuacha.

Na mtu akilitumia neno hili na jingine kama hili kwa utaratibu ule ule uliotumika katika Quran au katika Sunna hatakuwa na hatia wala hastahiki lawama, na hivyo ndivyo alivyofanya Ibn al-Qayyim, lakini kwa masikitiko makubwa jambo hili halikumfurahisha ndugu Juma na kaumu yake na wakalifanya hilo ni kosa kubwa lisilo na mfano !

Na -wali llaahil-hamdu- ukirejea sehemu mbali mbali katika vitabu vya Ibn al-Qayyim utaona anavyosema kwa uwazi kabisa kwamba:

"!

KWA SABABU YEYE (ALLAH) SUBHANAH- HAPOTEI WALA HASAHAU !

Tazama kitabu chake Shifaul-Alili ukurasa wa 141 chapa ya Darul-kitabil- Arabi Beirut Lebanon,chapa ya kwanza mwaka 2004.

 

Lakini ah ! tutazifanya nini sisi nyoyo zilizonyweshwa chuki, husda na uadui mpaka zikawa hazioni kwa waislamu wenzao ila shari tupu !

Lakini hii ndiyo sera ya watu wote wa bida tangu azal.

Ewe Mola wetu usijaalie ndani ya nyoyo zetu chuki na undani dhidi ya ndugu zetu walio amini, Allaahumma Aamin!

Rudi juu

TUHUMA YA NNE

 

Amesema Juma kuhusu Ibn al-Qayyim:

Na Ibn Al-qayyim akafikia kusema kuwa moto wa akhera kuna siku adhabu yake itakwisha kwa waislamu na wasio kuwa waislamu na utabaki mtupu bila ya mtu yeyote.

Na akainasibisha kauli hii kwa Sheikh wake Ibn Taymiyya na akaisifu kuwa kauli hii ndio inayokubaliana na Quran na suna.

Mwisho wa kunukuu. Tazama katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 25.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Ibn al-Qayyim kwenye kitabu chake Haadil-Arwaahi chapa ya Daarul-Kitabil-Arabi amenukuu mjadala ulio kuwa kati ya pande mbili: upande wa wasemao kuwa moto utakwisha na upande wa wasemao kuwa moto hautakwisha, kwa hiyo yeye kazi yake ilikuwa kunukuu hoja za pande mbili na ndiyo maana utaona anasema:

" "

Na wale (wanaosema kwa) kukata kudumu kwa moto wana njia sita.

Tazama Haadil-Arwaahi ukurasa wa 232.

 

Kisha akasema tena:

" ....".

Wamesema wenye kusema kwisha (kwa moto). Tazama kitabu Haadil-Arwaahi ukurasa 233.

 

Na mwisho alipofikia kuufunga mjadala huo akasema:

 

Kama ukiulizwa ni wapi umefikia unyayo wenu katika masala haya makubwa, ambayo ni makubwa kuliko dunia kwa mara nyingi?

Ataambiwa : tumefikia kwenye kauli yake Tabaaraka wataalaa-:

 

(( )) :107.

Kwa hakika Mola wako ni mwenye kufanya analo litaka..

Surat Huud aya ya 107.

Tazama Haadil-Arwaahi ukurasa wa 248.

 

Mpaka hapo inaonyesha kwamba Ibn al-Qayyim hakuunga mkono hoja ya upande wowote ule.

Lakini ukweli ni kwamba Ibn al-Qayyim amebabaika sana katika masala haya, na hakuwa na kauli ya wazi katika suala hili kwenye kitabu hiki.

Lakini tulipo yafuatilia maneno yake yaliyomo kwenye vitabu vyake vingine tukakuta kuwa ameuweka wazi msimamo wake juu ya masala haya kwa mfano kwenye kitabu chake Al-Waabilu al-Sayibu ukurasa wa 49 chapa ya al-Nasri, iliyohakikiwa na sheikh Ismail al-Ansaariy,amesema Ibn al-Qayyim:

 

" , , . , : , , - :

,

,

.

, , , , ".

49 , .

 

Na ama moto ni nyumba ya uchafu wa kauli na vyakula na vinywaji na ni nyumba ya wachafu, Allah -Taalaa- ataukusanya uchafu wenyewe kwa wenyewe kisha aurundike kama anavyorundika kitu ili kipandane chenyewe kwa chenyewe, kisha auweke katika Jahannam pamoja na watu wake.

Hakuna katika Jahannam ila uchafu. Na kwa vile wamekuwa watu katika tabaka tatu:

Usafi usio changanyikana na uchafu.

Na uchafu usio changanyika na usafi.

Na wengine wana uchafu na usafi.

Basi yamekuwa makazi yao pia ni (namna) tatu :

Makazi ya wasafi watupu (Peponi)

Makazi ya wachafu watupu (Motoni)

Na makazi haya mawili (Pepo na Moto) HAYATAKWISHA.

Na makazi ya wale walio na uchafu uliochanganyika na usafi ni makazi ambayo yatakwisha, nayo ndiyo makazi ya waliofanya maasia miongoni mwa waislamu. Na hatabakia katika Jahannam yeyote katika waislamu waliofanya maasia, wataadhibiwa kwa kiasi cha malipo yao kisha watatolewa motoni kisha wataingizwa peponi na,

HAYATABAKIA ILA MAKAZI YA WATU SAFI (PEPO) NA MAKAZI YA WATU WACHAFU (MOTO).

 

Kwa maneno haya ya Ibn al-Qayyim tunapata faida kwamba huko akhera watu watakuwa katika makundi matatu:

 

1-  Kuna watu wema walio safi kabisa, hawa makazi yao ni katika Janna (peponi).

2-  Kuna watu waovu walio wachafu kabisa nao ni makafiri, hawa makazi yao ni Jahannam (motoni).

3-  Na kuna watu ambao wamechanganya wema na uovu, na asili yao ni waislamu, hawa wataadhibiwa motoni kwa kadiri ya amali zao kisha watatolewa motoni na moto wao utazimwa.

 

Ama kundi la kwanza watu wa peponi wataishi katika neema za milele bila ya ukomo wala kwisha.

Na kundi la pili ambao ni makafiri wao wataadhibiwa motoni milele bila ya ukomo wala adhabu zao hazitakwisha.

Na hiyo ndiyo itikadi ya Imamu Ibn al-Qayim Rahimahu llaahu-

Kama utakuwa ndugu msomaji umesoma maneno yake kwa umakini, basi utakuwa umepata jawabu la kukutosha.

Halikadhalika yamenukuliwa maneno kutoka kwa sheikh wake sheikhul-islam Ibn Taymiyya kwamba anaitikadi hiyo, lakini kauli iliyo na nguvu ni kuwa msimamo wa Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim katika suala hili na mengineyo ni msimamo wa Salaf Swalih (wema walio tangulia).

Amesema Ibn Taymiyya:

 

" , , ".

1/146. 1406.

 

Kwa hakika neema za peponi na adhabu za motoni ni zenye kudumu, pamoja na kupata upya vyenye kuzuka ndani yake.

Tazama kitabu chake Minhaajus- Sunna kilicho chapishwa katika chuo kikuu cha Imamu Muhammad bin Suud al-Islamiyah Riyadh ya mwaka 1406 H.

:

" ".

1/581 . 18/308 , .

 

Amesema Ibn Taymiyyah -Allah amrehemu-:

Wameafikiana waliotangulia na maimamu wao na Ahli-Sunna wal-Jamaa wote kwamba kuna viumbe havitakwisha wala kutoweka kabisa, kama vile pepo,moto na vinginevyo.

Na hawakusema kuwa vitatoweka vitu vyote isipokuwa kundi la watu wa falsafa katika wazushi kama vile Jahmi bin Safwan na wale waliomuafiki miongoni mwa Mutazila na mfano wao.

Na hii ni kauli batili ambayo inatofautiana na kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake na maafikiano ya walio tangulia katika uma huu na maulamaa wake.

Tazama kitabu chake Bayaanu Talbisul-Jahmiya juzuu ya 1 ukurasa wa 581, kilicho chapishwa na Daarul-Qasimi- Riyadh, pia tazama Majmuu Fatawa juzuu ya 18 ukurasa wa 308.

 

Kwa maneno haya ya Ibn Taymiyya tumefahamu kuwa:

Msimamo sahihi wa Ahli Sunna ni kuwa pepo na moto havitakwisha Abadan.

Na msimamo wa watu wa bida ni kuwa pepo na moto vitakwisha.

Na msimamo huu wa kuwa moto utakwisha ni msimamo batili kwa mtazamo wa Ibn Taymiyya.

Kwa hiyo bila shaka msimamo wa Ibn Taymiyya katika jambo hili ni huo huo msimamo wa Ahli Sunna kwamba pepo na moto havitokwisha na ndiyo maana akaubatilisha msimamo wa wale wanaodai kuwa vitu hivyo vitakwisha.

Tena hasa ukizingatia kuwa maneno haya yamo katika kitabu kinachohesbiwa kuwa ni miongoni mwa vitabu alivyoviandika mwishoni mwa umri wake Bayaanu Talbisil-Jahmiya.

:

" .... ".

1/152-153 , .

 

Amesema Ibn Taymiyya:

Na haya ambayo wanayataja watu wengi miongoni mwa wanafalsafa waki-Jahmiya na mfano wao kuhusu mwanzo kuwa ni mfano wa mwisho na kwamba viwiliwili vya walimwengu vitakwisha hadi pepo na moto pia haya waliyo yazua wanafalsafa ni batili kwa itifaki ya waliotangulia katika uma huu na maimamu wake.

Tazama kitabu chake Bayaanu Talbisul-Jahmiya juzuu ya 1 ukurasa wa 152-153 kilicho chapishwa na Daarul-Qasimi- Riyadh.

Hapa Ibn Taymiyya anatuambia kuwa kauli ya wanafalsafa ya kudai kwamba vitu vyote vitakwisha na kutoweka kabisa, tena mpaka pepo na moto madai hayo ni batili.

:

" ...".

1/157.

Amesema tena Ibn Taymiyya:

Kisha (Allah) akatuelezea kubakia pepo na moto kubaki kwa itlaki (bila ya kuwa na mwisho) na wala hakutuelezea upambanuzi wa yale yatakayo kuwa baada ya hapo.

Tazama kitabu hicho hicho juzuu ya1 ukurasa 157.

Hapa Ibn Taymiyyah anatuambia kuwa; maandiko yamekuja kutuelezea kuwa pepo na moto zitabakia milele, na wala hayakutuelezea yatakayo tokea baada ya hapo.

 

Rudi juu

SURA YA TATU

 

CHANZO NA CHIMBUKO LA UPOTEVU

 

Ndugu msomaji kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya dini yetu hii ya kiislamu na ukawa unashughulishwa na kufuatilia matatizo yanayo usibu umma huu mtukufu, bila shaka utaziona athari za wazi wazi za tofauti za wafuasi wa dini hii tukufu, tena baadhi ya tofauti ni zile tofauti nzito ambazo huwezi kutoa hukumu kwamba wote hao waliotofautiana wako katika haki.

Na pengine unaweza kujiuliza ni nini sababu zilizowaingiza watu hawa katika tofauti hizi na itikadi potofu na batili?

Ndugu Juma M. Al-Mazrui yeye anadai kwamba chanzo cha watu kutumbukia katika itikadi za batili:

Ni kukanusha kwao kuwepo kwa MAJAZI katika lugha ya kiarabu na hasa katika Quran.

Tazama kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 32.

 

Bila shaka sababu hii aliyoitoa si sababu ya msingi wala haina uzito wowote kwa mtazamo wa kisheria, na hakuna muislamu yeyote yule, awe msomi au hata asiye msomi atakayekubaliana naye na hii sababu aliyoitoa, kwa kuwa ni sababu dhaifu ambayo haikuchunga vigezo vya kisheria.

Sisi kwa upande wetu tunasema kwamba:

Chanzo kikuu na chimbuko la kupotea kwa watu wengi mpaka kufikia kuingia katika itikadi potofu ni kuacha kuifuata njia ya Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- na kuuacha mwenendo sahihi wa wema waliotangulia katika kuifahamu dini.

 

Na hili ni jambo ambalo Allah na Mtume wake -swalla llaahu alayhi wasallam -wamelitahadharisha kwa ukali mno.

Amesema Allah:

...

Na atakayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na AKAFUATA NJIA ISIYOKUWA YA WAUMINI,tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu...

Surat An Nisaa aya ya 115

Kama utaizingatia aya hiyo hapo nyuma, utagundua kuwa kufuata njia isiyokuwa ya waumini ni moja miongoni mwa vyanzo vya upotevu katika umma huu.

Na hapana shaka kuwa, hakuna waumini waliokusudiwa hapo zaidi ya wale ambao Allah ametangaza kuwapa radhi zake, wao na wote wenye kufuata nyendo zao kwa wema pale aliposema:

 

.. .

Na wale waliotangulia,wakwanza katika Muhajirina na Answaari, na wale waliowafuata kwa wema, Allah ameridhika nao, na wao wameridhika naye.....

Suratul-Tawba aya ya 100.

 

Na kwa hakika isiyopingika hakuna wengine waliokusudiwa na haya hii zaidi ya Maswahaba ambao Allah amewataka watu wote wamuamini yeye Allah kama walivyomuamini watu hao

pale aliposema:

" "

Na wanapoambiwa:aminini KAMA WALIVYOAMINI WATU wanasema;hivi tuamini kama walivyoamini wapumbavu?....

Suratul Baqarah aya ya 13.

Na amesema tena Allah:

" "

Basi wakiamini KAMA MLIVYOAMINI NYINYI (maswahaba) basi watakuwa wameongoka.Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani.

Suratul Baqarah aya ya 137.

 

Pamoja na kuwa aya hizi tulizozitaja zinaeleza kwa uwazi ulazima wa kuifuata njia ya hao wema na kuwatahadharisha watu kufuata njia nyinginezo ambazo ndiyo chanzo cha upotevu wa watu na hatima yake ni kuingia motoni, lakini kwa makusudi kabisa ndugu Juma M. Al-Mazrui kaamua kuzifumbia macho aya hizo na kuzikwepa, kisha akaamua kuunda sababu nyingine ambazo ukizitazama kwa makini utagundua kuwa si sababu za msingi wala hazina uzito wowote katika mizani ya kielimu.

 

Pia ndugu Juma alitangulia kusema:

 

Na umma huu nao sasa umefika mbali katika kuitakidi mambo ya upotovu.Na chanzo chake ni itikadi mbili:

moja ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ataonekana,na la pili ni kuamini kuwa watu wataingia motoni kukoshwa dhambi zao tu:kisha wataingizwa katika pepo.

Tazama kitabu chake hicho ukurasa wa 17.

 

Ndugu Juma pia anadai kwamba miongoni mwa vyanzo vya upotevu ni watu kuitakidi kuwa Allah ataonekana huko akhera kwa macho. Na kadhalika kuitakidi kuwa waislamu waliomuasi Allah wataingia motoni kisha watatolewa !?

 

Itikadi zote hizi ambazo ndugu Juma ameziita kuwa ni vyanzo vya upotevu zimetajwa na Quran na Sunna sahihi za Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- na ndiyo itikadi ya Maswahaba wa Mtume Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam- na wafuasi wao walio wafuatia kwa wema.

Juma hakusema kwamba vyanzo vya upotevu ni:

Kutoshikamana na Quran na Sunna,

Kumtii shetani na askari wake,

Kufuata matamanio ya nafsi,Ujinga,Kiburi,

Kufanya israfu katika matumizi ya majazi ndani ya Quran, na kuzipotosha tafsiri za baadhi ya aya kwa madai kuwa kuna majazi.

Na nyinginezo miongoni mwa sababu zilizotajwa na Quran au Sunna.

Bali yeye ameamua kutaja mambo hayo kuwa ndiyo vyanzo vya upotovu, na hali ya kuwa yeye mwenyewe ana yakini kwamba hawezi kututhibitishia kielimu kwamba itikadi hizo ni vyanzo vya upotevu kivipi?

 

Lakini ninazidi kuamini kuwa upofu ni upofu wa moyo ! Ee Mola wetu tukinge na upofu wa macho na moyo Aamin-.

 

Ama kuhusu suala la majazi kuwepo kwake ndani ya Quran au kutokuwepo tutalitolea ufafanuzi kwa muhtasari katika sehemu hiyo ifuatayo inshaallah:

Rudi juu

UCHAMBUZI YAKINIFU JUU YA SUALA LA MAJAZI

Ama madai ya kwamba umma umeingia katika upotevu kwa sababu ya kuitakidi kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni madai batili kwa hoja tutakazo zitoa katika kitabu chetu hiki Inshaallaah.

Na ama kuitakidi kwamba kuna waislamu ambao wataingia motoni kisha watatoka kwa sababu ya shafaa (uombezi):

 

Suala hili limethibiti kwa hoja zenye nguvu katika kitabu (Quran) na sunna sahihi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-.

 

Ama madai yake ya uwongo kuwa suala la kupinga kuwepo kwa majazi ndani ya Quran kuwa ndiyo chanzo cha kupotea watu, ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

 

Suala kuwepo majazi na kutokuwepo kwake katika Quran na lugha ya kiarabu ni jambo ambalo maulamaa wametofautiana tangu zamani kama walivyotofautiana katika mambo mengine.

 

Ndugu Juma Al-Mazrui katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 32 amefanya jaribio la kutaka kuuficha ukweli huo ambao uko wazi tena mbele ya macho yake na akafanya upotoshaji kwa makusudi dhidi ya watu anaowaita Mawahabi (akiwa ana wakusudia Ahlu sunna wal Jamaa) kwa kudai kwamba watu hao wamepotea, na chanzo cha upotevu wao huo ni kukanusha kuwepo kwa majazi katika lugha na Quran.

 

Amesema ndugu Juma al Mazrui baada ya kichwa cha habari kisemacho:

Rudi juu

CHANZO CHA KUTUMBUKIA KATIKA ITIKADI BATILI

 

Kisha akasema:

Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, machoni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na hasa hasa katika Quran.

Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-jawziyya katika kitabu chake MUKHTASAR AL-SAWAAIQ AL MURSALA.

Na maana ya majazini kutumika neno tafauti na maana yake ya asili

Sasa wao Mawahabi wanakataa kuwa katika Quran hakuna majazi.

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu yatakuwa katika nukta tatu:

Nukta ya kwanza:

Ni kuhusu maelezo yake kuhusu neno Majazi,kwa ufupi ni kwamba maelezo ya Juma kuhusu majazi yana upungufu alitakiwa aseme hivi:

Majazi ni kutumia neno katika isiyokuwa maana yake ya asili pamoja na kuwepo dalili inayozuia kukusudiwa maana yake ya asili kwa mafungamano ambayo yapo baina ya neno la asili na neno ambalo si la asili.

 

Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:

 

1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.

 

2-Lazima kuwepo na QARINATUN MAANIATUN MIN IRADATI MAANAL ASLIY dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.

 

3-Lazima kuwepo na ALAAQAHmafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu.

 

Kwa mfano nikisema: Nimemuona Simba anamla Swala.

Kwa mujibu wa misingi ya lugha ya kiarabu neno Simbahapa limetumika katika maana yake ya asili.

Kwa sababu katika maneno haya hakuna QARINATUN MAANIATUN MIN IRADATI MAANAL ASLIY dalili yenye kuzuia kuikusudia maana ya asili.

 

Na yanapotamkwa maneno hayo kila mwenye kusikia atakuwa ameelewa moja kwa moja kwamba simba aliyekusudiwa hapo ni simba mnyama mkali wa porini na wala sivinginevyo.

 

Lakini mtu akisema; nimemuona simba kwenye uwanja wa mapambano ameshika upanga.

Bila shaka hakuna atakayedhania kwamba simba aliyekusudiwa hapa ni yule mnyama pori, na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; ameshika upanga maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake.

Kwa hiyo kusema tu;kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili,ni makosa kwa sababu tulizozitaja.

 

Nukta ya pili;

Sina shaka kuwa ndugu Juma na wengineo katika watu wa bida wanapokuwa wanataja neno;Mawahabi huwa wanawakusudia AHLU SUNNA WAL-JAMAA, nao ni wale ambao wanaziunga mkono hoja na dalili na kazi ya daawa alioifanya Sheikhul Islaam Muhammad bin Abdul Wahaab ambaye amezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H.

Swali, Je ni kweli kwamba hao ambao ndugu Juma anawaita mawahabi ndio wanaopinga majazi?

 

Maulamaa ambao wanapinga kuwepo kwa Majazi wako katika makundi mawili:

a) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika lugha na Quran.

b) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika Quran tu.

 

a) Hawa wafuatao ni baadhi ya maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na halikadhalika katika Quran:

 

1- Imamu Abu Ishaaq Ibrahim bin Muhammad bin Mihraan Al-Isfraayiiniy Al-Shaafiy aliyefariki mwaka 418 H.

 

2- Imamu Abu Aliy Al Hassan bin Ahmad bin Abdil-Ghaffaar Al-Fasawiy aliyefariki mwaka 377 H.

 

3-Sheikhul Islaam Abul Abbaas Ahmad bin Abdul-Haliim Ibn Taymiyyah aliyefariki mwaka 728 H.

4-Shamsud Din Abu Abdillahi Muhammad bin Abi Bakar mashuhuri kwa jina la Ibnul Qayyim al Jawziyyah aliyefariki mwaka 751 H.

 

b) Na hawa wafuatao ni maulamaa ambao wamepinga kuwepo kwa majazi ndani ya Quran tu, lakini wakathibitisha kuwepo kwake katika lugha ya kiarabu:

 

1-Muhammad bin Ahmad bin Abdillahi mashuhuri kwa Ibn Khuwayz Mindaad katika maulamaa wa madhehbu ya Ki-Maalik.

 

2-Imamu Abul Abbaas Ahmad bin Ahmad Al-Twabariy Al-Shaafiy mashuhuri kwa Ibnul-Qaadhiy aliyefariki mwaka 335 H.

 

Ndugu msomaji kama ukiutazama kwa makini mwaka aliozaliwa Sheikh Muhammad bin Abdil-Wahab na mwaka waliokufa maulamaa hawa tuliowataja utagundua kwamba ndugu Juma al-Mazrui ni mwongo.

 

Kwa mfano,baina ya Sheikh Muhammad bin Abdil Wahaab aliyezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H na baina ya Imamu Abu Ishaaq al Isfraayiiniy aliyefariki mwaka 418 H, ambaye ni miongoni mwa wanaopinga kuwepo kwa Majazi utaona kuwa baina yao kuna miaka takriban 697, kabla ya kuzaliwa huyo wanaedai kuwa ndiyo muasisi wa huo uwahabi! Kwa miaka hiyo tayari upingaji wa majazi ulikuwepo duniani.

 

Sasa utasemaje kwamba Mawahabi wanapinga majazi na hali yakuwa huyo muasisi wa huo mnaouita uwahabi amezaliwa miaka 697 baada ya kauli hiyo ya kupinga majazi ? au unataka kutuambia kwamba Imamu Abu Ishaaq Al-Isfraayiiniy alifufuka baada ya kuzaliwa Muhammad bin Abdul-wahab kisha akamfuata sheikh Muhammad bin Abdil-wahab ?

Au mnataka kutuambia kuwa hawa nao pia ni Mawahabi?

 

Rudi juu

JE WENYE KUPINGA MAJAZI WANA HOJA ZA KIELIMU?

 

Jambo muhimu la kulizingatia ni; je hao maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi, wamepinga kwa hoja na dalili za kielimu? Au ni kwa maneno matupu?

 

Jawabu ni kama ifuatavyo:

Ukirejea kauli za maulamaa hao waliopinga kuwepo kwa majazi ima katika lugha ya kiarabu na Quran, au katika Quran tu, utagundua kwamba kuna hoja za msingi walizozitoa ambazo haitakiwi kuzipuuza, bali inatakiwa zitazamwe kielimu na kwa jicho la insafu.

Hizi zifuatazo ni baadhi ya hoja zao:

Rudi juu

HOJA YAO YA KWANZA

 

Miongoni mwa hoja zao zinazowafanya kupinga kuwepo majazi katika lugha na halikadhalika katika Quran, ni kuwa maana ya maneno hufahamika kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context) na dalili za uhalisia.

Pia wakadai kuwa neno linapokuwa peke yake halileti maana kamili mpaka liwe katika sentensi, na linapo unganishwa katika sentensi huwa ule mtirirko wa maneno ndio unao ainisha maana husika ya neno hilo.

Mfano, neno "" Raasun lina maana nyingi, lakini maana zote zinaainishwa na mtiririko wa maneno, kwa mfano mtu akisema:

Raasul-Jabali, atakuwa hapa anakusudia kilele cha mlima.

Na kama atasema:

Raasul-Maali, atakuwa anakusudia msingi wa mali au rasilimali.

Na kama atasema:

Raasul-Insaani, atakuwa anakusudia kichwa cha binadamu.

Na maana zote za neno hili zimeanishwa na mtirirko wa maneno, na wala hakuna binadamu yeyote anaeweza kututhibitishia kwa hoja na dalili kwamba maana ya asili ya neno Raasi ni kichwa cha binadamu, na katika sehemu nyingine zote ni Majazi.

Rudi juu

HOJA YAO YA PILI

 

Itifaki iliyopo baina ya maulamaa wa lugha ya kiarabu kwamba mtu anaweza akayapinga maneno ambayo yanadaiwa kuwa ni majazi. Na kwa wakati huo huo akawa huyo mpingaji ni mkweli na yule mwenye kudai kuwa maneno hayo ni majazi pia akawa ni mkweli.

 

Kwa mfano mtu akisema kwa kutumia majazi:

 

Nimemuona simba ameshika upanga akiwa anamkusudia mtu shujaa, kama akitokea mtu mwingine akisema huo ni uwongo! huyo uliemuona wewe si simba, bali ni mtu shujaa, anakuwa huyu mwenye kutumia majazi ni mkweli na wakati huo huo huyu aliyepinga naye pia ni mkweli !

 

Kwa sababu hiyo wakasema wenye kupinga majazi:

 

Kwa mujibu wa itifaki hiyo ni kwamba mtu akisema kwamba ndani ya Quran kuna majazi atakuwa moja kwa moja ameshasema kuwa ndani ya Quran kuna vitu ambavyo kuna uwezekano wa mtu akasema kuwa ni uwongo na akawa huyo msemaji kwa wakati huo ni mkweli !

 

Na bila shaka hilo si sahihi kwa itifaki ya waislamu wote, kwa sababu wamekubaliana waislamu wote duniani tangu hapo kale hadi sasa kwamba hakuna kitu chochote ambacho kiko ndani ya Quran kinachofaa kukipinga bali ukiipinga herufi moja tu utakuwa tayari umekufuru.

Na hii itikadi ya kuwepo kwa Majazi ndani ya Quran inawafungulia watu mlango wa kuliingia jambo hilo la hatari.

 

Kwa mfano, pale aliposema Allah:

Na akaja Mola wako na Malaika safu safu.

Suratul-Fajri (89) aya ya 22.

Baadhi ya watu wakaigeuza maana ya aya hii wakasema hapana, hatakuja Mola Muumba wa kila kitu, bali itakuja amri yake!

 

Kwa madai kwamba eti kuna Majazul-Hadhfi majazi ya kuondosha kwa hiyo kuna kitu kimeondoshwa.

Na kitu kilichowapa ujasiri wa kukana kwao kuja kwa Allah siku ya Qiyama ni pale walipofunguliwa mlango huo na hicho kitu kiitwacho Majazi.

 

Kwa mfano, ukiwauliza kwa nini mmekimbilia kuitakidi kwamba hapo kuna majazi ? Na hali yakuwa majazi si asili na hairuhusiwi kuiwacha asili na kukimbilia kwenye majazi mpaka itakapo shindikana maana ya asili?

 

Wanadai kuwa asili imeshindikana, kwa sababu Allah hawezi kuja, na kitendo cha kuja kinaonyesha kuwa Allah ana mahali na hiyo ni sifa ya kiwiliwili, na kumpa Allah sifa hiyo ni kumfananisha na viumbe na kufanya hivyo ni kufru!!!

 

Madai haya si sahihi, kwa sababu kwanza, inatakiwa kukithibitisha kile ambacho Allah amejithibitishia nafsi yake kama anavyo stahiki, pamoja na kumtakasa na kufanana na viumbe, kama tutakavyo lifafanua suala hili mahali pake Inshaallah.

Rudi juu

 

HOJA ZA WENYE KUTHIBITISHA MAJAZI

 

Wakajitetea wenye kuthibitisha kuwepo majazi ndani ya Quran kwa kusema:

Majazi ni sehemu katika fasihi za lugha ya kiarabu, na hii Quran imeshuka kwa lugha ya kiarabu.

Na kila ambacho kinafaa kuwepo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Quran.

Na miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya lugha ya kiarabu ni haya majazi.

Kwahiyo, tunapata natija kwamba Majazi yamo katika Quran.

 

Rudi juu

MAJIBU YA WENYE KUPINGA

 

Wakawajibu wenye kupinga kuwepo majazi ndani ya Quran kama ifuatavyo:

 

Tumewakubalia (AL-MUQADDIMATU AL-SUGHRAA) kwamba majazi yamo katika lugha ya kiarabu, lakini hatuwakubalii (AL-MUQADDIMATUL-KUBRAA) kwamba kila kilichomo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Quran, bali sisi tunasema kinyume chake, kwamba; kuna baadhi ya vitu vimo katika lugha ya kiarabu, lakini havifai bali ni haramu kuitakidi kuwemo ndani ya Quran.

Kwa mfano;

Katika elimu ya balagha sehemu ya Badii katika sehemu ya Muhassinaatul-Maanawiyyah (vitu vyenye kupendezesha maana), kuna kitu kinachoitwa AL-HAZLU (mzaha/utani).

 

Kitu hiki kimo ndani ya lugha ya kiarabu, lakini huwezi kusema kwamba maadamu kimo kwenye lugha, basi kinafaa kuwemo ndani ya Quran, kwa sababu Allah anasema kuhusu Quran:

*

Kwa hakika hii (Quran) ni kauli kupambanua (13) Na wala si mzaha (14).

Suratul-Twaariq (86) aya ya 13-14

Miongoni mwa fani za lugha ya kiarabu ni suala la utani, lakini ndani ya Qurani hakuna utani na mwenye kuitakidi kuwa katika Quran kuna utani atakuwa tayari amekufuru.

Halikadhalika ndani ya lugha ya kiarabu kuna kitu katika milango ya elimu ya balagha kiitwacho al Rujuu kujirudi, msemaji anaweza kusema neno halafu hapo hapo anajikadhibisha mwenyewe kwa kuwa alisema maneno hayo bila ya uhakika, kutokana na kuweweseka, au hofu, au kuzidiwa na mapenzi n.k.

 

Halikadhalika kuna kitu kitachoitwa Husnu Taalili kutoa sababu ya kitu ambayo si halisia.

Mfano mtu akisema: Mvua imenyesha mjini kwetu kwa sababu ya kutuona haya.

 

Mambo haya na mengineyo ambayo sikuyataja, yamo katika lugha ya kiarabu lakini hayamo na wala hayafai kuwemo katika Quran, bali kuitakidi kuwemo ndani ya Quran ni ukafiri.

 

Kwa hiyo madai ya kwamba kila kilichomo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Quran, madai hayo hapa yanaporomoka.

" "

 

Na kwa kuzitumia njia za kimantiki (logic) wanasema kwamba;

Kichanguzi cha Kulliyyatun Muujibah ni Juziyyatun Saalibah

Kwamfano;

Kulliyatun Muujibah kama vile ukisema: kila ambacho kimo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo katika Quran.

 

Maneno hayo yanavunjwa na Juziyyatun Saalibah ambayo ni kusema:

Kuna vitu vingi vimo katika lugha ya kiarabu lakini havifai kuwemo kwenye Quran.

Na msingi huu (Juziyyatun Saalibah ukithibiti kwa hoja basi msingi huo wa kwanza (Kulliyyatun Muujibah) unaporomoka.

Na hapo nyuma tumekuthibitishia kuwepo katika lugha ya kiarabu vitu vingi ambavyo kudai kwamba vimo ndani ya Quran ni haramu.

 

Tazama maelezo hayo kwa urefu zaidi katika kitabu Manu Jawazil-Majaazi cha Imamu wa tafsiri katika zama hizi Sheikh Muhammad al-Amin bin Muhammad al-Shinqitwiy.

 

Rudi juu

HOJA YAO YA TATU

 

Pia ukitazama kwa makini utakuta kuwa hakuna vigezo na vidhibiti vya uhakika katika kuitolea Taarif (definition) sahihi Majaazi al-Mursal (Absolute Metaphor), na matumizi yake, na hilo linasababisha mgongano katika matumizi yake kilugha jambo ambalo ni muhali kuwemo katika Quran.

 

Kwa mfano mtu akisema: Nimeingiza kidole sikioni.

Kwa mujibu wa maelezo ya wenye kudai kuwepo majazi wanasema kuwa hapo kuna Majaazul-Mursal (Absolute Metaphor) na maana yake ni kwamba umeingiza baadhi ya kidole, kwa sababu kidole chote hakiingii sikioni, kwa hiyo utakuwa umekitaja kidole lakini makusudio ni baadhi yake.

Wakiwa wanaifanyia kazi Qaaidah (kanuni) iliyopo katikaMajaazil Mursali (Absolute Metaphor) isemayo:

Min Itlaaqil-Kulli wa Iraadatil-Baadhi (ni kukitataja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake).

 

Lakini ukifanya utafiti wa kina utagundua kwamba wenye kuitumia Qaaidah (kanuni) hii wameshindwa kuidhibiti kitaalamu, kiasi ambacho inafikia kuifanya sehemu kubwa ya lugha ya kiarabu kama si yote kuwa ni Majazi! Jambo ambalo si sahihi.

 

Kwa sababu wanakubaliana wataalamu wote wa lugha ya kiarabu kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi.

Na hilo linapingana na kanuni hiyo na nyinginezo za kimajazi.

 

Kwa kuitumia Qaaidah hiyo ya kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake, kunavunja itifaki hiyo.

Kwamfano, mtu akisema:

Nimekula wali, au

Nimekunywa maji, au

Nimekwenda Makka.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo yanakuwa maneno yote hayo ni Majazi hata kama wenye kuyathibitisha hawasemi hivyo, lakini kanuni hiyo waliyoiweka ndiyo inavyoelekeza, kwa sababu utaambiwa wewe umekula baadhi ya wali na hukula wali wote.

Na utaambiwa kuwa umekunywa baadhi ya maji na hukunywa maji yote.

Na umefika baadhi ya sehemu za jiji la Makka na hukufika Makka yote, pengine umefika Mina, Aziiziyyah, Ajyaad, Ghaza na katika msikiti mtukufu, lakini hukufika Misfala, wala Hafaair, wala Kaakiyyah na sehemu nyinginezo katika mitaa ya Makka, kwa hiyo ukisema nimefika Makka ni majazi kwa kuwa umetaja Makka lakini makusudio yako ni baadhi yake.

Halikadhalika ukisema nimekaa msikitini, au nyumbani, au darasani, au ofisini, maneno yote hayo ni majazi kwa sababu kiuhakika kabisa utakuwa hukukaa katika msikiti wote bali umekaa katika baadhi ya eneo la msikiti, au nyumba, au darasa, au ofisi.

 

Hivyo basi, kwa sababu ya kukosekana udhibiti ulio makini wa suala hili ndiyo baadhi ya maulamaa wakasema kuwa maneno yote hayo ni hakika na wala si majazi na mtiririko wa maneno (context) ndiyo ulio ainisha maana ya maneno hayo.

 

Pia maulamaa wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapowahoji na kuwapa changamoto (challenge) wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi hawapati majibu yoyote ya kuridhisha ndipo pale wakalipinga suala hili ili:

 

-Lugha ya kiarabu isichezewe.

-Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Quran kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Kwa sababu wamejitokeza baadhi ya watu wakazipotosha aya nyingi zinazotaja sifa za Allah kwa madai kwamba kuna majazi kwa madai ya kumtakasa Allah na sifa za viumbe na hatima yake wakaingia katika upotofu.

Mpaka hapo itabainika kwamba;

Kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Quran ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili zaidi kuliko kudai kinyume chake.

 

Na ama baadhi ya mifano ambayo hutolewa kama ni hoja ya kuwakandamiza wenye kupinga majazi Imamu Ibnul-Qayyim katika kitabu chake AL-SWAWAAIQUL-MURSALA ameyajibu kwa ufundi mkubwa mno.

Kadhalika Imamu wa Tafsiri na Usuul katika zama hizi sheikh Muhammad al-Amin al-Shanqitwiy pia amezijibu hoja nyingi tena kwa ufanisi wa hali ya juu kwa mwenye kutaka faida na arejee kwenye kitabu chake: MANU JAWAAZIL-MAJAZI

 

Na ukizitazama kwa makini hoja zao utagundua kwamba tofauti ni ya kimatamshi, hawa wameona utaratibu huo wauite Majazi, na kwa hakika hilo lina mapungufu mengi kama tulivyo thibitisha hapo nyuma.

Na wengine wameona wauite Usluubun min Asaalibil-Lugha (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

Rudi juu

SURA YA NNE

HOJA ZA WENYE KUITAKIDI KUONEKANA ALLAH HUKO AKHERA.

 

Hizi zifuatazo ni baadhi ya hoja za Ahli-Sunna wal-Jamaa katika kuthibitisha usahihi wa kuonekana Allah kwa macho huko akhera.

Mara baada ya kutaja hoja na dalili za Ahlu Sunna zenye kuthibitiha suala hili na kuzitolea maelezo Inshaallah tutafuatishia kutaja majaribio aliyoyafanya ndugu Juma M. Al-Mazrui dhidi ya hoja hizo kwa lengo la kuzipotosha na kisha yatafuata majibu yetu baada ya hapo ili kuthibitisha usahihi wa hoja hizo.

Rudi juu

 

HOJA YA KWANZA.

 

Miongoni mwa hoja za wenye kuthibitisha kuonekana Allah huko akhera kwa macho ni pale aliposema Allah;

 

" *** ".

Zipo nyuso siku hiyo ni zenye kungara* Ni zenye kumwangalia (kumuona) Mola wake.

Surat al-Qiyamah aya 22-23.

 

Aya hii ni miongoni mwa hoja zilizowazi ambazo Ahlu-Sunna wanazitegemea katika kuthibitisha kwamba watu wema watamuona Mola wao huko akhera kwa macho yao. Na kuna hoja nyingi zinazoipa nguvu hoja hii yenye kuthibitisha kuonekana Allah Azza wajallah- huko akhera kwa macho:

kuna hoja za ndani na hoja za nje.

 

Hoja za aina ya kwanza ni:-

Hoja za ndani, ni muweko wa neno hili katika upande wa kilugha, kwa sababu limetumika neno Naadhirah ambalo limenyambuliwa kutokana na asili ya neno Nadharan, na likawa neno hili limekuja baada ya herufi ILAA, na kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu linapokuwa neno hili limekuja baada ya herufi hiyo maana yake ya asili ni kutazama kwa macho. Na kwa bahati nzuri hata wale wenye kupinga kuonekana Allah huko akhera wanakubaliana na sisi katika hilo, na ushahidi wa madai haya ni kauli ya ndugu Juma M. Al-Mazrui aliposema katika ukurasa wa 53 wa kitabu chake, pale alipokuwa akielezea maana za neno AL-NADHARU:

 

Tukitazama maana ya neno hili: (al-nadharu) kupitia kiyoo cha Quran tunakuta ni:

1)Kutazama kikawaida kwa macho: NA HII NDIO MAANA YA MSINGI YA NENO HILO.. mwisho wa kunukuu.

Kama ndugu Juma anakubaliana na sisi kuwa neno AL-NADHARU maana yake ya asili ni kutazama kwa macho, basi anatakiwa pia akubali kwamba kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu ambazo wataalamu wote wa lugha hiyo wamekubaliana ni kuwa: maana ya kwanza inayozingatiwa katika matumizi ya neno ni kulitumia neno katika maana yake ya asili kwanza, kabla hatujakwenda katika maana nyingine.

Pamoja na kwamba inawezekana likatumika neno katika maana nyingine isiyokuwa ya asili, lakini mpaka ishindikane kutumika maana ya asili, kisha kuweko na dalili itakayotufahamisha kushindakana matumizi hayo ya asili ya neno hilo na kwenda nje ya asili yake.

Na sisi tukilitazama neno NAADHIRAH hapa tunaona kuwa bado haijashindikana kulitumia katika maana yake ya asili ambayo ni kutazama kwa macho, na wala hakuna hoja yoyote ya msingi yenye kutufanya tutoke nje ya asili ya neno hili, bali ni kinyume chake; kuna hoja nyingi zinazolipa nguvu neno hilo libaki katika matumizi yake ya asili ambayo ni (kutazama kwa macho). Kama vile kutajwa neno: "" Wujuuhun (Nyuso) katika aya tunayoijadili.

 

Hoja za aina ya pili ni:

Hoja za nje, nazo ni zile dalili ambazo zimekuja kwa wingi mno katika Qurani na Sunna, na kauli za maulamaa wakubwa katika Maswahaba, na wanafunzi wao na maimamu waliokuja baada yao, kauli ambazo ni tafsiri za aya hii na nyinginezo zinazosema kwamba Allah ataonekana kwa macho akhera. Ama kuhusu dalili za Sunna tutazitaja hapo mbeleni -Inshaallaah- hapa tutaitaja kauli moja ya Taabiyyun (mwanafunzi wa swahaba) ambaye ni Ikrimah bin Abdillahi rahimahu llaahu-.

Amesema Imamu Al-Tabariy katika kitabu chake JAAMIUL-BAYAAN

(mashuhuri kwa jina la Tafsirul-Twabariy) katika juzuu ya 29 ukurasa wa 228:

 

Ametusimulia Muhammad bin Mansour Al-Tusiy, na Ibrahimu bin Saad Al-Jauhariy (wote wawili) wamesema; ametusimulia Aliy bin Al-Hasan bin Shaqiq, amesema ametusilulia Al-Husain bin Waaqid kutoka kwa Yazid Al-Nahwiy kutoka kwa Ikrimah (amesema kuhusu kauli ya Allah):

 

" *** ".

Zipo nyuso siku hiyo zenye kungara* Ni zenye kumwangalia (kumuona) Mola wake.

Surat al-Qiyamah aya 22-23.

 

Akasema Ikrimah: Zitamtazama Mola wake Mlezi.

Bila shaka, tafsiri hii ya Ikrimah inaipanguvu hoja ya wale wanaosema kwamba watu wema watamuona Mola wao huko akhera kwa macho yao, na si rahisi kuwa haya ni mawazo yake binafsi, bali ni tafsiri ambayo ameipokea kutoka kwa sheikh wake swahaba mtukufu Ibn Abbaas radhiyallahu anhumaa- naye amemsikia bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- akitamka maneno hayo, na nina thubutu kusema hivi kwa sababu ya maandiko mengine ambayo yamepokewa kutoka kwa bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- ambayo yanaipa nguvu kauli hii.

 

Pamoja na kuwa hoja hii iko wazi katika kuithibitisha itikadi hii sahihi ya Ahli Sunna juu ya kuonekana Allah huko akhera kwa macho, lakini wapinzani wa hoja hii hawakuwacha kuitilia mashaka tena kwa madai ambayo ni dhaifu mno. Na haya yafuatayo ni baadhi ya madai yao yanayoonekana yana uzito kidogo:

Rudi juu

 

JARIBIO LA KWANZA LA KUIPOTOSHA HOJA HII

 

Katika kufanya jaribio la kuipotosha hoja hii inayozungumzia kuonekana kwa Allah huko akhera ndugu Juma M.Al-Mazrui ameleta madai mengi ambayo hayana msingi, na haya yafuatayo ni baadhi ya madai hayo:

 

1) Madai yake ya kwanza juu ya hoja hii ni kwamba, neno Naadhirah amabalo limetumika katika sura hii lina maana pana zaidi, kuliko kuona. Kwa sababu mtu anaweza kusema:

Nimeutazama mwezi lakini sikuuona.

Kwa hiyo neno kutazama halimaanishi kuwa lazima mtu aone.

Tazama ukarasa wa 50 katika kitabu chake.

 

Akiwa na maana kwamba, hata hao watakao mtazama Mola wao huko akhera kuna uwezekano wasimuone maana si lazima ukitazama ni sharti uone!!!

 

2) Madai yake ya pili ni kuhusu neno hili (nadharu) lina maana nyingi katika lugha ya kiarabu: haiwezekani kusema kwamba maana fulani ndio iliokusudiwa ila kwa dalili na ushahidi.

 

Na dalili ikiwa na maana nyingi basi ushahidi wake ni batili ila ikipata uzito kwa dalili nyingine nje ya hiyo au itapata uzito katika vifuatanishi vya maneno (context).

Tazama ukurasa wa 51,na 56 katika kitabu chake.

 

3) Hadithi zote ambazo zimepokewa zenye kuifasiri aya hii kuwa maana yake ni kumuona Mwenyezi Mungu ni hadithi batili na za uwongo !!!.

Tazama ukurasa wa 74-75 katika kitabu chake.

 

4) Akatoa dalili za kimaandishi zinazopingana na aya hiyo -kwa mtazamo wake- kama vile kauli yake Allah aliposema:

Macho hayamfikii naye anayafikia macho (yote).

Sura ya 6 aya ya 103.

Na hadithi isemayo :

Na hakuna kinachozuia baina ya watu na kumtazama Mola wao isipokuwa lile vazi la kibri chake.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu kuhusu madai yake ya kwanza, kwamba neno naadhira lina maana pana kuliko kuona kwa sababu mtu anaweza kutazama lakini asione, sisi tunasema hilo ni kweli, lakini neno Naadhira hapa limetumika kwa maana ya kuona kwa sababu hizi zifuatazo:

 

i) Hivi unadhania kwamba siku ya Qiyamah nyuso zitangara na kutoa nuru kwa kumtazama wasiemuona?

Unapomtazama unayempenda ambaye una shauku ya kumuona halafu usimuone je hiyo ni starehe au adhabu?

Je kutakuwa na tofauti gani baina ya wema na waovu katika hilo?

 

Makusudio makubwa ya kumuona Allah huko akhera ni Takrima watakayokirimiwa waja wema waliomuamini Mola huyo Mkarimu hapa duniani wakiwa hawamuoni Ewe Allah ! Turuzuku ladha ya kuuona uso wako mtukufu- Aamin-.

 

ii) Pia kuna ushahidi wa aya nyinyingine za Quran kama aya ya 26 katika surat Yunus na hadithi nyingi za Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- ambazo zimefikia kiwango cha MUTAWAATIR (Idadi kubwa ambayo ni muhali kuwa wapokezi wake wameafikiana kutunga uwongo) hadithi zote hizo zinaiunga mkono aya hii.

Kwa mfano kauli yake bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-aliposema:

Kwa hakika nyinyi mtamuona Mola wenu.

Hadithi hii ameipokea Imamu Al-Bukhari namba 7435, na maelezo yake Inshaallah yatakuja huko mbeleni.

 

Ama kuhusu madai yake ya pili, ni pale aliposema:

Neno hili (nadharu) lina maana nyingi katika lugha ya kiarabu: haiwezekani kusema kwamba maana fulani ndio iliokusudiwa ila kwa dalili na ushahidi.

Sisi tunasema kwamba bado kauli hii ya Juma si hoja ya kuibatilisha maana ya kutazama iliyobebwa na neno naadhirah, kwa sababu maana hiyo ndiyo ya msingi na ya asili kama alivyokiri Juma.

Na katika kanuni za lugha ya kiarabu, mtu aliyeshikamana na maana ya asili ya neno hana wajibu wa kuleta hoja wala dalili ili kuthibitisha kwanini ameshikamana na maana ya asili, bali anayetakiwa kuleta hoja ni yule anayedai kinyume cha asili, na wale wanaoitumia aya hii kuthibitisha kuonekana Allah, wao wameshikamana na maana ya asili ya neno hili. Kwa hiyo wenye kuitakidi kinyume chake na wakalitafsiri neno NAADHIRAH kwa maana ya KUNGOJEA badala ya maana ya asili KUTAZAMA wao ndio walio na wajibu wa kuleta hoja kwa nini wameikimbia maana hii ya asili na wakaamua kwenda nje ya asili bila ya hoja wala dalili yoyote yenye nguvu?

 

3- Madai yake ya tatu ni kwamba hadithi zote zilizokuja kuifasiri aya hii kuwa maana yake ni kumuona Mwenyezi Mungu ni hadithi batili na za uwongo! Kisha akaanza kuidhoofisha kauli ya Taabii Ikrimah kwa kusema:

Hadithi hii pia ni dhaifu ! na udhaifu wake ni kuwa katika wapokezi wake yumo HUSAIN BIN WAQID naye ni dhaifu wanavyuoni wa hadithi hawamkubali.

Anasema Ibn Hajar Al-asqalaani katika wanavyuoni wakubwa wa madhehebu ya Al-shafi:

AL-HUSAIN BIN WAQID AL-MARUZI, ABU ABDALLAH AL-QADHI alikuwa mkweli lakini anasahau na anakosea sana..

Mwisho wa kunukuu.

Tazama ukurasa wa 67 katika kitabu chake.

Rudi juu

 

MAJIBU YETU

 

Hapa ndugu Juma ametumia uwongo na lengo lake ni kuwadanganya wasio na taaluma ya kutosha katika mambo ya elimu ya hadithi.

Hapa ameidhoofisha kauli ya Taabii Ikrimah kwa madai ya kuwa mpokezi wake ambaye ni AL-Husain bin Waaqid anakosea sana!

 

Jawabu yetu dhidi ya maneno ya ndugu Juma yatakuwa kama ifuatavyo:

 

Kwa hakika mimi ninashangazwa sana na tabia hii ya kusema uwongo anayoitumia ndugu Juma, kwa kweli mimi ninashangazwa sana na tabia yake hii ! nikafikia kujiuliza inakuwaje mtu anaamua kuwadanganya watu katika mambo ya dini?! Kweli mtu huyo atakua ana nia njema? Au ana jambo jingine nyuma ya pazia?

Na uwongo wake huo uko pale alipodai kwamba Al-Husein bin Waaqid ni DHAIFU! Kisha akadai kuwa WANAVYUONI WA HADITHI NAO HAWAMKUBALI!!! Halafu maneno hayo akamsingizia Ibni Hajar kuwa ndiye aliyeyasema!

Je ni kweli Ibn Hajar amemdhoofisha mpokezi huyu? Hebu tuyatazame hayo maneno ya Ibn Hajar kuhusu mpokezi huyu, yeye anasema nini?

 

Anasema Ibni Hajar:

" ".

AL-HUSAIN BIN WAQID AL-MARWAZIY ABU ABDILLAHI AL-QADHIY NI THIQA (mwadilifu mwenye kuhifadhi) na ANA MAKOSA.

Tazama Al-Taqribu tarjama namba1492.

 

Hayo ndiyo maneno ya Ibni Hajar Al-Asqalaniy kuhusu Al-Husain Ibn Waaqid, sasa hebu tuanze kuyachambua kwa kuhoji:

Je Ibn Hajar amesema kuwa Husein ni THIQA (muadilifu mwenye uwezo mzuri wa kuhifadhi) Au amesema kuwa Husein ni DHAIFU?

Jawabu liko wazi katika maneno yake hayo hapo nyuma, kwa hiyo Juma analazimika kutueleza ni mahali gani Ibni Hajar amesema kuwa Husein ni dhaifu?

Huwenda Juma akawa ametatizika na kauli ya Ibn Hajar pale aliposema: ANA MAKOSA yeye haraka haraka kwa sababu ya nia yake mbaya akadhania kwamba kuwa makusudio ya Ibn Hajar ni kuwa Husein ANAKOSEA SANAA!

Na kama hiyo ndiyo sababu iliyomfanya ndugu Juma aseme kuwa Husein ni dhaifu, je hakuiona kauli ya Ibni Hajar aliyosema kuwa Husein ni THIQA kabla ya kusema anakosea?

 

ii) Lau kama Husein angekuwa na makosa mengi ya kumfanya awe ni dhaifu na asikubaliwe na wanavyuoni wa hadithi, kitaalamu ingesemwa Faahishul-ghalat au Kathirul-Khatai au Sayyiul-Hifdhi lakini maneno yaliyotumika hapo ni Lahu Auhaam (ana makosa) na hiyo si sababu ya kumhukumu mpokezi kuwa ni dhaifu, kwani ni nani asiyekosea na kutatizika?

 

iii) Ndugu Juma yeye amesema ni AL-MARUZI! Na kutamka hivi si sahihi, sahihi ni AL-MARWAZIY , na hii pia ni ishara tosha kwamba yeye si mtaalamu, na hayuko makini katika fani hii, maana makosa yake katika jambo hili ni mengi mno kushinda hayo makosa anayomsingizia nayo Husein Al-Marwaziy.

 

iv) Hebu tuwatazame maulamaa wa hadithi wanasema nini kuhusu Husein? Je ni kweli hawamkubali kama anavyodai ndugu Juma? Au huo ni uwongo wake alioubuni ili kuzihadaa akili za watu?

 

Amesema Imamu Abu Bakar Ahmad bin Muhammad Al-Athram;

Nilimuuliza Imamu Ahmad bin Hanbal: unasema nini kuhusu Al-HUSAIN BIN WAQID?

Akasema hana ubaya wowote kisha akamsifia sana.

 

Amesema Imamu Yahya Ibn Main: Husain ni THIQA (mwadilifu mwenye kuhifadhi vizuri).

Amesema Imamu Abu Zura: Husain hana ubaya wowote.

Amesema Imamu Al-Nasai: Husain hana ubaya wowote.

Amesema Imamu Abu Daud: Husain hana ubaya wowote.

Amesema Imamu Ibn Sad : Husain: alikuwa ni mwenye hadithi nzuri.

Amesema Imamu Ibn Hibbaan: alikuwa Husain ni miongoni mwa watu bora na mara nyingine hukosea katika mapokezi.

 

Tazama maelezo hayo yote katika vitabu vifuatavyo:

Sualaatul-Athrami ukurasa wa 61.

Al-Jarhu wal-Taadili juzuu ya 3 ukursa wa 306.

Tahdhibul-Kamaal juzuu ya 6 ukurasa wa 493.

Taarikhul-Duuriy juzuu ya 2 ukurasa wa 119.

Taarikhu Abi Zura ukurasa wa 208.

Tabaqaatu Ibn Sad juzuu ya 7 ukurasa wa 371.

Tahdhibul-Tahdhibi juzuu ya 1 ukurasa 543.

Al-Taqribu, tarjama namba 1392.

 

Ndugu msomaji, kwa mujibu wa kauli hizi za maulamaa hawa wakubwa wa hadithi, je ni kweli kwamba hawamkubali Husein kama anavyodai ndugu Juma Al-Mazrui? Au Juma amekusudia kudanganya?

Haya ni machache katika mengi ya uwongo aliyoyajaza kwenye kitabu chake alichokiita;

HOJA ZENYE NGUVU JUU KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU KWA MACHO sawa sawa angekiita HOJA ZA UWONGO JUU YA KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU... Bila shaka angekuwa amepatia zaidi.

 

Pamoja na kuwa ndugu Juma hapa ametumia maneno machache, lakini makosa yake ni mengi mno:

Kwanza amemzulia Ibn Hajar kwamba amesema kuwa Husein ni dhaifu, lakini tulipoyarejea maneno ya Ibn Hajar kuhusu Husein tukakuta maneno yake ni kinyume na alivyodai Juma.

Pili amewazulia uwongo maulamaa wa hadithi kwamba hawamkubali Husein, na hali ya kuwa madai hayo pia hayana ukweli.

4) Ama dalili za kimaandishi alizozitoa ndugu Juma kuonyesha kwamba zinapingana na aya hii, jawabu ni kwamba hazipingani bali ni ufahamu wake finyu, na hilo tutalielezea kwa kina -Inshaallah tutakapokuwa tunazijibu hoja zao.

Rudi juu

JARIBIO LA PILI LA KUPOTOSHA HOJA HII

 

Ndugu Juma amefanya majaribio mawili dhaifu mno ya ki-lugha kwa lengo la kutaka kuipotosha maana ya aya hii, akadai kwamba:

(a) Hakuna Muqaabala.

(b) Kuna al-Hasru.

Ni nini maana ya maneno haya? Fuatilia maelezo yafuatayo, Inshaallah utakubainikia uwongo wake.

 

Dhamira kubwa ya ndugu Juma ililenga katika kuubatilisha ushahidi uliobebwa na aya hii wa kuthibitisha kuonekana Allah kwa macho huko akhera, lakini wali llaahil-hamdu- hakufaulu na matokeo yake amewadhihirishia watu wenye elimu uwelewa wake mdogo katika suala hili na ufahamu finyu.

 

Hebu tuanze na huo Muqaabala

Amesema Juma:

Kanuni ya kwanza ni ile inayojulikana kuwa " " (muelekeo wa neno au maneno na kinyume chake).

Muqaabala ni; kuleta maana mbili au tatu zenye kuafikiana kisha ukaleta kinyume chake kwa mpangilio.

Kasha akatoa mifano takriban mitano, kisha akasema: katika aya hizi zote sehemu ya mwanzo ya aya ni tofauti na sehemu yake ya pili, nayo ni kinyume chake, na kila neno linaelekeana au linakabiliana na mwenzake kimaana. Huu ndio mukabala wa balagha ya kiarabu: yanapotajwa maneno fulani kisha yakaletwa mengine yanayo kabiliana na hayo yaliyotajwa mwanzo kimaana basi ni lazima yawe maneno ya kwanza ni kinyume cha maneno ya pili.

Tazama katika ukurasa wa 77 katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu

Kisha akasema tena:

Sasa kama tutafasiri kuwa nyuso za watu wema zinamuona Mwenyezi Mungu basi maana itakuwa hivi: kuna nyuso zinamuona Mwenyezi Mungu na kuna nyuso zinatazamia kuteremkiwa na adhabu. Tazama jinsi tafsiri ilivyokuwa haioani, na huo mukabala wa balagha ya kiarabu unavyopotea. Nyuso za watu wema zinamuona Mwenyezi Mungu wakati za watu wabaya zinatazamia kuteremkiwa na adhabu !!!.

Tazama kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 81.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu yatakua katika masuala mawili:

Suala la kwanza ni kuhusu (") Muqaabala, sisi tunasema kwamba: kuitafsiri aya hii kwa maana ya kumuona Allah hakuupotezi muqaabala, bali muqaabala upo isipokuwa Juma hakuutaka kwa sababu ni kinyume na itikadi yake, na yeye huwa anatanguliza kwanza itikadi yake kisha mambo mengine yatapimwa na anavyoitakidi, jambo likiafikiana na itikadi yake, hilo litakuwa ni zuri na linafaa hata kama ni baya lisilofaa, na kama haliafikiani na itikadi yake basi hilo ni baya na halifai hata kama ni mafundisho ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-, na mpokezi anayekubalika ni yule anayepokea riwaya ya kuipa nguvu itikadi yake hata kama ni dhaifu, na yule anayepokea kinyume na itikadi yake huyo ni dhaifu, mwongo, na anaghushi! Na umeshayaona pale alipomzulia Ibn Hajar ili amdhoofishe mpokezi mkweli anaekubalika (Husein Al-Waqidiy) na Inshaallah hayo utayaona kwa wingi huko mbeleni.

 

Sisi hapa tunasema kwamba:

Nyuso za watu wema siku ya Qiyama zitangara.

Kwa sababu watu wema watakua katika neema kubwa ya kumuona Mola wao.

 

Na nyuso za watu waovu zitajikunja.

Kwa sababu watu waovu watakua katika adhabu kali na huku wana yakini kwamba watafikwa na adhabu kubwa kuliko hiyo.

 

Kwa hiyo watu wema nyuso zao zitatoa nuru.

Na watu waovu nyuso zao zitakunjana.

 

Watu wema watakua katika neema kubwa.

Na watu waovu watakua katika adhabu kali.

 

Na huu ndiyo Muqaabala wenyewe, ambao Juma hakuutaka kwa sababu unapingana na itikadi yake ya kiibadhi.

Imamu Al-Aluusiy katika tafsiri yake Ruhul-Maaniy juzuu ya 29 ukurasa wa 75 anaitilia nguvu hoja hii kwa kusema:

" ...".

Na uthibitisho wa hilo ni kuwa yale wanayofanyiwa hao (waovu) ni muqaabala wa kumtazama Mola Subhaanah- kwa kuwa hilo ni ukomo wa neema, na hili (wanalo fanyiwa waovu) ni ukomo wa mateso.

Suala la pili ni masala ya () kutangulizwa mtendwa, amesema Juma:

Watu wa fani ya balagha wanaita hii kuwa ni:

" "

Kumtanguliza mtendwa badala ya mtenda.

Yaani kawaida ni kuwa atangulie mtenda sio mtendwa: mtendwa aje baadaye. Huu ndio utaratibu wa asili wa lugha ya kiarabu kama tulivyosema mwanzo.

Sasa je kama kutangulia mtenda ndio utaratibu wa asili wa lugha hii, inapokuja kinyume na hivi akatangulia mtendwa huwa inamaanisha nini?

Wanasema kitaalam kuwa hii inaonesha "" yaani kumuusisha mtenda na kitu kimoja tu na huwa hafanyi cha pili.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 83.

 

Kisha akasema tena:

Sasa ikiwa tutaifasiri kutazama hapa kwa maana ya kuona basi tafsiri haitokuwa sahihi: itapingana na uhakika ulivyo.

Kwanini? Kwa sababu tafsiri itabidi iwe hivi: (nyuso hizo) zinamuona Mola wake tu. Na huu si ukweli: ukweli ni kuwa watu huko kwenye kisimamo cha kiama na kwenye pepo wataonana na wataona kheri zilizoandaliwa katika pepo.

Yote haya yanaonesha kuwa makusudio ya aya hii si kuona.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama katika kitabu hicho ukurasa wa 85.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu ya maneno haya yatakuwa katika njia zifuatazo:

Njia ya kwanza:

Ninataka kumfahamisha ndugu Juma na wengineo kwamba: masala haya huwa mahali pake ni katika elimu ya balagha sehemu ya Ilmul-Maani mlango wa Al-Qasru.

Kuna njia nyingi za Al-Qasru moja katika hizo ni hii ya kumtanguliza mtendwa kabla ya mtenda, hili ni jambo ambalo linafahamika na wala halina upinzani.

Lakini jambo muhimu la kulijadili hapa, je matumizi ya lugha kwa utaratibu huu hayaleti ila maana moja tu nayo ni: "" kumhusisha mtenda na kitu kimoja tu akawa hafanyi cha pili kama anavyodai Juma?

Au anapotangulizwa mtendwa juu ya mtenda kuna malengo mengine kinyume na aliyoyataja Juma?

Sisi tunasema: naam, inawezekana akatangulizwa mtendwa kabla ya mtenda kwa malengo mengine kinyume na aliyoyataja Juma.

Inawezekana kuwa Juma ameghafilika, au hilo hajui, au anajua lakini amekusudia kupotosha.

Kwa mfano; kuna uwezekano wa kutangulizwa mtendwa kwa lengo la:

1-Kumpa umuhimu mtendwa ()

2-  Kuchunga utaratibu wa utungo wa maneno

( ) .

 

Na malengo mengineyo ambayo wanavyuoni wa fani ya balagha wameyaeleza kwa marefu na mapana kwenye vitabu vyao.

Na yote tuliyoyataja yana mifano tele kwenye Quran na maneno ya waarabu.

Labda hapa tutoe mifano miwili mitatu:

Mfano wa kwanza; amesema Allah:

 

{ }17}

Na ama Thamudi tuliwaongoza, wakapenda upofu kuliko uwongofu.

Surat Fussilat (41) aya ya 17.

 

Neno Thamudi hapa ni mtendwa kwa mujibu wa Qiraa (kisomo) cha baadhi ya wasomaji walipolisoma kwa Fatha ya Dali. Hapo neno Thamudi limetangulia na haki yake ilikua ni kuja baada ya mtenda, na huyo mtenda ni dhamiri (pronoun) aliyoambatana na Fiilu (kitendo) tuliwaongoza.

Kwa hiyo si makusudio ya aya hii kuuhusisha uwongofu wa Allah kwa kabila la Thamudi tu, kwa sababu ya kuwa mtendwa ametangulia, kwa sababu wapo watu wengine waliongozwa na Allah na wao si katika kabila la Thamudi, bali makusudio ni kuonyesha kwamba mtendwa hapo amepewa umuhimu na kupatilizwa.

Mfano wa pili; amesema Allah:

" "

5

Na wanyama hoa amekuumbieni

Suratun Nahl (16) aya ya 5.

 

Pia si makusudio ya aya hii kwamba Allah ametuumbia wanyama hoa pekee, bali hata wanyama pori pia amewaumba yeye.

 

Mfano wa tatu; amesema Allah:

" "

9

Basi Yatima usimwonee.

Suratul-Dhuhaa (93) aya ya 9.

Uonevu ni haramu kwa kila mtu, na si kwa yatima peke yake, na yaliyo haramu kumfanyia yatima ni mengi na si uonevu pekee, kwa hivyo huwezi kusema kwamba: haifai kumwonea yatima tu, kwa sababu mtendwa ametangulizwa, la hasha! Bali hata wengine wasiokua yatima pia ni haramu kuwaonea, pia huwezi kusema kwamba lililo haramu ni uonevu tu kwa yatima, lakini uovu mwingine wowote usio kuwa uonevu unaweza kumfanyia.

Kwa hiyo kitendo alichokifanya Juma si sahihi, kwa sababu yeye katika maneno yake ameleta dhana ya kwamba utaratibu huu wa kumtanguliza mtendwa kabla ya mtenda hauleti isipokuwa maana moja tu, nayo ni; kumhusisha mtenda na kitu kimoja tu, na dhana hiyo si ya kweli kwa maelezo tuliyo yatoa, na kwa maelezo hayo ndiyo unadhihirika ufahamu finyu alio nao Juma katika masala haya ya kielimu.

 

Pili, hadithi zilizo kuja kuizungumzia itikadi hii zinaukata mzozo huu kwa kuifafanua aya hii na nyinginezo, na kutuwekea wazi juu ya kuthibiti kwa jambo hili la kuonekana Allah kwa macho huko akhera.

Kwa hiyo hoja yetu hii bado imesimama na Juma na kaumu yake hawakufaulu katika majaribio yao ya kutaka kuiporomosha.

 

Hebu sasa na tuiangalie hoja ya pili:

Rudi juu

 

HOJA YA PILI

 

Miongoni mwa hoja zilizo na nguvu zinazothibitisha kuonekana kwa Allah huko akhera kwa macho ni kauli yake Allah Azza wajalla- aliposema:

 

{ }

26

Wale waliofanya mema watapata wema na ziada.

Surat Yunus (10) aya ya 26.

 

Katika aya hii limetajwa neno ziada, na wala haikuanishwa hiyo ziada yenyewe ni nini? wala hakikutajwa kiwango chake, na hilo ni katika mambo ya ghaibu hatuna njia ya kulifahamu ila kwa kupitia wahyi utokao kwa Allah, na tulipomrejea bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- tuanona anatwambia kuwa maana ya neno ziada lililotajwa katika aya hii ni: kumuona Allah huko akhera.

Na tafsiri hiyo imeelezwa kwa mapokezi haya yafuatayo:

:

:

{ }

 

Amesema Imamu Muslimu: Ametusimulia Ubaidu-llahi Ibn Maysarah, Amesema: ametusimulia Abdul-rahman bin Mahdi, amesema: ametusimulia HAMAD BIN SALAMAH, kutoka kwa Thabiti bin Aslam al-Bunani, kutoka kwa Abdul-Rahman Ibn Abi Laylaa, kutoka kwa Suheib, kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- amesema:

Watakapoingia watu wa peponi katika pepo atanadi mwenye kunadi: hakika nyinyi mna ahadi mbele ya Allah anataka kukutekelezeeni.

Watasema kwani hukuzingarisha nyuso zetu na ukatuokoa na moto na ukatuingiza peponi?

Akasema (Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-);

Kisha ataondoa pazia, kwa hakika hawajawahi kupewa kitu wanacho kipenda zaidi kuliko kumtazama yeye (Allah subhaanahu wataalaa).

Amesema Imamu Muslimu: ametusimulia Abu Bakri Ibn Abi Shaiba, ametusimulia Yazid Ibn Haroun, kutoka kwa HAMAD IBN SALAMAH kwa sanad hii hii na akazidisha (kwamba Mtume swalla llaahu alayhi wasallam) kisha akasoma:

Wale waliofanya mema watapata wema na ziada.

Tazama sahihul muslim hadithi namba 449.

:

:

{ }

.

 

Amesema Imamu Tirmidhiy: Ametusimulia Muhammad bin Bashaar Amesema: ametusimulia Abdul-rahman bin Mahdi, amesema: ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thabiti bin Aslam al-Bunani, kutoka kwa Abdul-Rahman Ibn Abi Laylaa, kutoka kwa Suheib, kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- kuhusiana na kauli ya Allah:

Wale waliofanya mema watapata wema na ziada.

Akasema (Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-):

Watakapoingia watu wa peponi katika pepo atanadi mwenye kunadi: hakika nyinyi mna ahadi mbele ya Allah anataka kukutekelezeeni.

Watasema kwani hakuzingarisha nyuso zetu na akatuokoa na moto na akatuingiza peponi?

Akasema (Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-);

Kisha litafunuka pazia. Akasema: Naapa kwa Allah ! Hajawahi kuwapa kitu wanacho kipenda zaidi kuliko kumtazama yeye (Allah subhaanahu wataalaa).

Tazama Jaamiul-Tirmidhiy hadithi namba 2552.

:

( :

: . :

 

Amesema Imamu Ibn Abi Asim: ametusimulia Hudba Ibn Khalid Ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thabiti bin Aslam al-Bunani, kutoka kwa Abdul-Rahman Ibn Abi Laylaa, kutoka kwa Suheib, kwamba Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- amesema kuhusiana na kauli ya Allah:

Wale waliofanya mema watapata wema na ziada.

Akasema Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-;

Watakapoingia watu wa peponi katika pepo, na wakaingia watu wa motoni katika moto, atanadi (mwenye kunadi): Enyi watu wa peponi! Hakika nyinyi mna ahadi mbele ya Allah anataka kukutekelezeeni.

Watasema ni ahadi gani hiyo? kwani hakuzingarisha nyuso zetu na akatuingiza peponi, na katuokoa na moto?

 

Akasema (Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-):

Kisha Allah atawaondolea pazia, watamtazama Allah ! Hakuna kitu walichopewa wanacho kipenda zaidi kuliko kumtazama yeye (Allah subhaanahu wataalaa), na HIYO NDIO ZIADA.

Tazama kitabu al-Sunna cha Ibn Abi Asim, ukurasa wa 217 hadithi namba 472.

 

Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa utafiti wa misingi ya mapokezi ya hadithi za Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- na wala haina kasoro yoyote. Pia maulamaa wa hadithi wameisahihisha na wala hakuna aliyeitia kasoro.

 

Ama kuhusu kasoro alizozitaja Juma al-Mazrui katika kitabu chake Hoja zenye nguvu kutoka kwa sheikh wake wa kiibadhi al-Qannubi, Inshaallah hapo mbele tutakuwekea wazi ili uzione hiyana na hila zinazofanywa na watu hawa, ima kwa sababu ya ujahili katika elimu ya hadithi au kwa sababu ya nia zao mbaya.

 

Ndugu msomaji, bila shaka ukiitazama hadithi hii kwa mazingatio utaona namna bwana Mtume Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam- alivyoifafanua kwa uwazi usio na kificho na kuibainisha maana sahihi ya aya 26 ya surat Yunus (10).

Basi ni nani aliyekosa haya akadai kuwa yeye anajua zaidi maana na makusudio ya kitabu cha Allah -tabaaraka wataalaa- (Quran) kumshinda bwana Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam?

Bila shaka hakuna muislamu yoyote atakayeweza kudai hilo, kwa sababu Allah yeye ndiye aliyemteua Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- kuwa wadhifa wake ni kuwabainishia watu yaliyomo ndani ya kitabu kitukufu (Quran) pale aliposema Allah:

" " 44.

Na tumekuteremshia wewe dhikri (Quran) ili upate kuwabainishia watu kile kilichoteremshwa kwao.

Surat al Nahli aya ya 44.

 

Na halikadhalika tunakubaliana waislamu wote kuwa hatuna hiyari katika kuufuata ubainifu wa mjumbe huyu mtukufu, bali ni wajibu wetu kuamini, kukubaliana, na kufuata yale yote aliyotufundisha kutoka kwa Allah subhaanahu wataalaa- kwa sababu mjumbe huyo hatamki kwa matamanio ya nafsi yake bali kila analolitamka ni kwa amri ya mola wake jalla jalaaluh.

 

Hivyo basi, kwa bayana hii ya bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- inatubainikia kwamba;

Allah atawakirimu waja wake waumini huko akhera kwa neema nyingi, na neema iliyo kubwa kuliko zote ni ile ya kumuona yeye Tabaaraka wataalaa kwa macho yao bila ya kuwepo kizuizi chochote, na hiyo ndiyo maana ya ziada iliyotajwa katika aya ya 26 ya sura ya 10 (surat Yunus).

Rudi juu

 

JARIBIO LA KWANZA LA KUIPOTOSHA HOJA YA PILI

 

Baada ya ndugu Juma kuona kuwa mapokezi hayo yamethibiti kwa njia zilizo sahihi kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- katika kuitafsiri aya ya 26 ya surat Yunus, na ikawa tafsiri yake inalingana na itikadi ya Ahli sunna yakuwa Allah ataonekana huko akhera kwa macho, na ikawa pia tafsiri hiyo inapingana na itikadi potofu ya kiibadhi yakwamba Allah hataonekana akhera kwa macho, ndipo hapo hiyana za kielimu zilipoanza kutoka kwa ndugu Juma M. Al-Mazrui huku akipata msaada kutoka kwa sheikh wake aliyemvika kilemba cha ukoka, naye si mwingine bali ni Said Mabruuk al-Qannubi, wakaanza kuyapotosha maandiko sahihi ili kuihami itikadi yao hiyo potofu kwa kutumia uwongo, hila na hadaa, subhaana llaah!

Sasa hebu nikunakilie maneno yake kuhusu hadithi hii kutoka katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu. Amesema katika ukurasa wa 111:

 

..na hapa nitakunakilia namna mbili tu katika maneno ya AL IMAMU SAID BIN MABRUK AL- QANNUBI IMAMU WA HADITHI ,FIQHI NA USULI uone jawabu yake juu ya hadithi hiianasema Al imamu Al qannubi:

Na hadithi hii ni batili na ubainifu wa haya ni kwa njia mbili:

Ni kuwa katika sanad yake yumo HAMAD BIN SALAMA, naye japo kuwa ni mkweli katika nafsi yake lakini

HIFDHI YAKE NI MBOVU:

ANASAHAU na

KUKOSEA na

AMECHANGANYIKIWA na KUBADILIKA MWISHONI MWA UMRI WAKE; kwahivyo yeye hafai kuwa hoja.

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu dhidi ya maneno haya ya Juma Al-Mazrui aliyoyanakili kutoka kwa sheikh wake Al-qannubi, sisi Inshaallah tutayajibu kwenye nukta mbili:

 

Nukta ya kwanza:

Ni kuhusu kauli yake ya kumuita Al-Qannubi kuwa ni Imamu wa hadithi.

Bila shaka kwa watu walio na maarifa juu elimu hii ya hadithi wanaifahamu daraja hii ya uimamu katika fani hii kwamba si kila mtu alipewa daraja hiyo bali walipewa watu wachache mno kama vile:

 

Sufyaan al-Thawry, Sufyaan bin Uyaina, Malik bin Anas, Ali bin al Madini, Ahmad bin Hanbali, Muhammad bin Ismail al Bukhari na wengineo wachache.

 

Kwa uthibitisho zaidi hebu fungua vitabu vya tarjama kisha usome kwa utulivu utaligundua hili ninalokueleza, hebu soma vitabu kama vile;

Tahdhibul kamal,ya al mizziy.

Tahdhibut Tahdhibi na al-Taqribu vya al Haafidh Ibn Hajar al-Asqalaani.

Mizanul-Itidaal ya Imamu al-Dhahbi n.k.

 

Pamoja na kuwa mlango wa kuitana hivyo haujafungwa, lakini je ni kila mtu anaweza kupewa wasifu huo hata wale wasiostahiki?

Lakini unajua ni kwanini ndugu Juma ameamua kumpa al-Qannubi daraja hiyo katika fani hii hususani alipokuwa akilizungumzia suala hili?

 

Si kwa nia nyingine bali lengo lake ni kumkuza mbele ya macho ya wasomaji ili aipe uhalali kazi aliyoikusudia kuifanya, nayo ni kazi ya kuyapotosha maandiko sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume mtukufu Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- yanayotufundisha kwamba Allah -subhaanahu wataala- ataonekana kwa macho huko akhera na kuyafanya maandiko hayo kuwa ni batili kwa sababu yanapingana na itikadi ya madhehebu yake ! ndiyo akaamua kumnyanyua na kumpa cheo cha uimamu katika hadithi ili msomaji aone kwamba kuna mwanachuoni mkubwa, tena Imamu wa hadithi na fiqhiameibatilisha hadithi hii !!! Na hakumpa cheo hicho kwa kuwa anastahiki, hapana! Kwa sababu hapo mbeleni Inshaallah utakubainikia ujahili wa mtu huyo aitwaye imamu wa hadithi katika elimu hii.

Nukta ya pili:

Ni madai yake kwamba Hamad bin Salama hifdhi yake ni mbovu, anasahau, anakosea na amechanganyikiwa na kubadilika mwishoni mwa umri wake.

Madai haya ya kwamba hifdhi ya Hamad bin Salama ni mbovu si madai ya kweli na mwenye kudai hilo anatakiwa alete ushahidi juu ya hilo, na hakuna ushahidi wowote juu ya madai hayo, bali kinyume chake ndio sahihi. Na Inshaallah tutayajibu maneno hayo kwa njia tatu:

 

Njia ya kwanza:-

Kauli za maulamaa wakubwa wa hadithi kuhusu hifdhi ya Hamad bin Salama:

 

1-Amesema Imamu Ahmad bin Hambali:

: .

Mtu madhubuti kuliko wote (waliopokea kutoka kwa ) Thabit ni Hamad bin Salama.

Na hadithi hii Hamad bin Salama ameipokea kutoka kwa Thabiti, lizingatie hilo kwa sababu ni jambo muhimu.

Na amesema tena Imamu Ahamd kuhusu Hamad bin Salama kuwa ni:

(Mtu) Madhubuti.

 

2-Amesema Imamu Yahya bin Main:

: .

Yeyote atakayetofautiana na Hamad bin Salama kuhusu (mapokezi kutoka) kwa Thabit kauli (ya kuchukuliwa) ni kauli ya Hamad.

 

Pia amesema tena:

(Hamad bin Salama) ni Thiqa (muadilifu mwenye hifdhi nzuri).

 

3-Amesema Al Imamu al Saajiy:

:

Alikuwa (Hamad bin Salama) ni mwenye kuhifadhi tena ni Thiqa (muadilifu) na ni mwenye kuaminiwa.

 

4-Amesema Ibn Saad:

:

Na alikuwa (Hamad) ni mtu Thiqa (muadilifu mwenye hifdhi nzuri) mwenye hadithi nyingi, lakini mara nyingine anasimulia hadithi Munkar.

Hapo limetumika neno la kiarabu Rubba nalo huleta maana ya uchache.

 

5-Amesema Al Ijliy:

:

(Hamad) ni: Thiqa (muadilifu mwenye hifdhi nzuri) mtu mwema mwenye hadithi nzuri.

 

6-Amesema Al Haafidh Ibn Hajar katika kitabu chake al Taqribu uk 195:

 

195 1636:

..".

Hamad bin Salama bin Dinar al Basriy Abu Salama ni Thiqa (muadilifu mwenye hifdhi nzuri) mcha mungu na ni mtu madhubuti zaidi (kati ya waliopokea kutoka) kwa Thabit, na hifdhi yake ilibadilika mwishoni mwa umri wake.

 

7-Amesema Imamu Aliy bin Abdillahi bin al-Madiniy sheikh wake Imamu al-Bukhariy:

:

Utakapomsikia mtu anamsema kwa ubaya Hamad bin Salama basi mtuhumuni (mtu huyo).

Juma Mazrui na sheikh wake Qannubi wanamsema vibaya Hammad, bila shaka wanafanya hivyo kwa sababu ya nia zao mbaya, na sisi tuna watuhumu kwa hilo.

 

Tazama maneno hayo ya maulamaa kwenye vitabu vifuatavyo:

Al-thiqaat cha Ibn Hibbaan juzuu ya 6 ukurasa wa 216.

Twabaqaatul-Kubraa cha Ibn Sad juzuu ya 7 ukurasa 282.

Taarikhu Thiqaat cha al-Ijliy ukurasa wa 131.

Mizaanul-Itidaal cha al-Dhahbiy juzuu ya 1 ukurasa 590-595.

Tahdhibut-Tahdhibi cha Ibn Hajar al-Asqalaaniy juzuu ya 2 ukurasa wa 10-13.

Al-Taqribu pia cha al-Hafidh Ibn Hajar al-Asqalaaniy, tarjama namba 1636.

 

Sasa hebu ndugu msomaji mtukufu linganisha kauli hizo za maulamaa hao wakubwa wa hadithi juu ya Hamad bin Salama na kauli za huyo al-Qannubi aliyevishwa kilemba cha ukoka na ndugu Juma! Bila shaka ukweli utakubainikia na hapo ndiyo utagundua kwamba kuna agenda ya siri baina ya huyo sheikh aliyesimikwa daraja ya uimamu (al-Qannubi) na mwanafunzi wake (Juma).

 

Njia ya pili:-

Ni kuhusu suala la kuwa Hamad bin Salama anakosea na anasahau, jawabu ni kwamba kukosea na kusahau ni katika tabia za kibinaadamu, hakuna mwanadamu yeyote asiyekosea au kusahau ila yule aliyekingwa na Allah -Tabaaraka wataalaa- asikosee wala kusahau.

Isipokuwa nataka ifahamike kwamba kukosea au kusahau kukizidi mno kupita kiasi hiyo itakuwa ni kasoro, lakini tumeona katika kauli ya Imamu Ibn Saad kuwa Hamad ana hadithi nyingi mno lakini ni mara chache kukosea. Haya ni nani huyo asiyekosea? Hebu na atutajie! Na ni nani huyo asiyesahau? Alisahau Adam baba wa watu wote seuze Hamad bin Salama?

 

Amesema Allah:

115

Na tulimpa ahadi (Nabii) Adam zamani,lakini alisahau wala hatukuona kwake azma.

Surat Twaha (20) aya ya 115.

 

Bali amesahau Musa bin Imran Mtume wa Allah, soma aya ya 73 katika surat al Kahfi (18). Kwa hiyo kusahau si kasoro katika upokezi wa habari, lakini ikithibiti kwamba mpokezi amesahau katika habari aliyoipokea, au kusahau kwake kumevuka mipaka bila shaka hiyo itakuwa ni dosari na itaathiri katika habari zake atakazo zipokea, hapa Juma na sheikh wake Qannubi hawajatuthibitishia kwa maandiko yoyote ya kielimu kuhusu kukosea kwa Hammad, je kumevuka mipaka au wameamua kumtuhumu tu? Na kama ndugu yangu msomaji umeyazingatia maneno ya maulamaa tuliyokutajia kuhusu Hammad utagundua kuwa ni kinyume na wanavyosema wazushi hawa.

Njia ya tatu:-

Ni kuhusu suala la kuwa Hamad amechanganyikiwa mwishoni mwa umri wake, suala hili ni kweli na wanavyuoni wamelitaja kwenye vitabu vyao na linaweza kuyatia kasoro mapokezi ya mpokeaji, lakini swali la msingi la kujiuliza ni wakati gani huko kuchanganyikiwa kutatia kasoro mapokezi hayo?

 

Ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

 

Hukumu ya riwaya za mpokezi aliyechanganyikiwa mwishoni mwa umri wake si moja bali iko katika namna tatu:

 

i)            Namna ya kwanza ni kuwa riwaya zote alizosimulia kabla ya kuchanganyikiwa na zikajulikana, riwaya hizo zitakubalika.

ii)           Namna ya pili ni zile riwaya ambazo amezisimulia baada ya kuchanganyikiwa hizo hazitokubaliwa.

iii)         Ni zile ambazo hazikujulikana kuwa amezisimulia kabla ya kuchanganyikiwa au baada yake, riwaya hizo hazitatumika mpaka zibainike, je zimesimuliwa kabla ya kuchanganyikiwa au baada?

 

Amesema Imamu al Nawawy:

" ".

 

Hukubaliwa (habari) zile ambazo zimepokewa kutoka kwa hao (walio changanyikiwa) kabla ya kuchanganyikiwa na hazitokubaliwa zilizokuwa baada yake, hata zile ambazo zimetiliwa shaka (kuwa ni baada au kabla pia hazitakubaliwa).

Tazama Taqtribun-Nawaawy pamoja na Tadribul-raawiy juzuu ya 2 ukurasa 372.

 

Kwahiyo hukumu hii ya ujumla iliyotolewa na ndugu Juma na sheikh wake aliyemvika kilemba cha ukoka Al-Qannubi dhidi Hamad bin Salama haikufuata kanuni za kielimu, kwa sababu walikuwa wana wajibu wa kuthibitisha kitaalamu kwamba mpokezi aliyepokea hadithi hii kutoka kwa Hamad bin Salamah amesimuliwa baada yakuwa tayari Hamad amechanganyikiwa, na wala si kwa kutoa hukumu kiujumla na hali ya kuwa jambo lina upambanuzi wa kielimu kama huu tulioutoa.

Na si Juma wala sheikh wake Qannubi anayeweza kufanya hivyo, na akijaribu ataumbuka, kwa sababu mpokezi aliyepokea hadithi hii kutoka kwa Hamad ibn Salama ni Abdul-rahaman bin Mahdi ambaye ni katika jumla ya wanafunzi wakubwa wa Hamad ambao wamepokea kutoka kwa sheikh wao Hamad bin Salama kabla ya kuchanganyikiwa.

 

Mpaka hapo ndugu msomaji utakuwa umegundua namna ndugu Juma na sheikh wake wanavyotumia ujanja ujanja katika masuala ya kielimu, na hakuna shaka kuwa kufanya hivyo ni kuwafanyia hiyana watu wasiojua na hiyo ni dhulma ya wazi.

Na hakuna budi kwa sheikh na mwanafunzi wake wakubali moja ya mambo mawili;

1-Wakubali kuwa wao ni waongo, wamekusudia kuwadanganya na kuwalaghai waislamu.

2-Au ni wajinga, wanasema katika elimu hii wasichokijua. Na kila watakalo lichagua kwao wao ni baya.

Rudi juu

JUMA NA SHEIKH WAKE AL-QANNUBI WAMZULIA UWONGO SHEIKH AL-BANI.

 

Miongoni mwa ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba Juma na sheikh wake Said Mabruk Al-qannubi wanasema uongo na lengo lao ni kuwadanganya waislamu kwa lengo la kuihami itikadi yao batili, ni hiki kitendo chao cha wazi cha kumzulia uwongo sheikh Al-Bani maneno ambayo hakuyasema.

Wamejaribu kuwadanganya waislamu kwamba sheikh Al-Bani pia anamsimamo kama wao dhidi ya Hammad Ibn Salamah, amesema Juma M. al-Mazrui katika kitabu chake Hoja zenye nguvu ukurasa wa 112 na hapa ninamnakili kama alivyoandika mwenyewe:

Na akasema Al-albani (mwanachuoni wa hadithi wa kiwahabi) katika kitabu chake AL DHAIFA juzuu ya 2 ukurasa wa 333:

hakika ya Hamad anakosea sana.

Rudi juu

Kisha akasema tena Juma:

Hii ni nakala kutoka katika kitabu ALTUFAN AL-JAARIF LI KATAAIB AL-BAGHYI WAL-UDWAAN juzuu ya 3 sehemu ya 1 ukurasa 308. cha Imam wa hadithi, fiqhi na usuli Al-huja Said bin Mabruk al-qannubi.

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu juu ya maneno haya ni kwa njia mbili:-

 

Njia ya kwanza:

 

Ni kama tulivyotangulia kusema hapo nyuma kwamba Juma na sheikh wake ima ni waongo au ni wajinga wasiofahamu maneno ya maulamaa, nimesema hivyo si kwa kutaka kuwakashifu na kuwadhalilisha, bali ninasema hivyo kwa sababu hii ifuatayo:

 

Maneno ya Sheikh Al-Bani -Allah amrehemu yako kinyume na anavyosema Juma aliyoyanukuu kutoka kwa sheikh wake Al-Qannubi, na ukiyarejea maneno ya sheikh Al-Bani utayaona yamekuja baada ya kuitaja hadithi isemayo:

Mwenye kuiacha sehemu ya unywele mmoja katika janaba na asiuoshe atafanywa kadha wa kadha huko motoni. 2/332.

Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa swahaba mtukufu Aliy Allah amridhie- na katika sanad yake yumo Atwaa bin Saaib na Hamad bin Salamah.

 

Kisha akasema (sheikh Al-Bani):

Amesema Imamu Ibn Hajar:

Sanadi ya hadithi hiyo ni sahihi kwa sababu Atwaa amepokea kutoka kwa Hamad kabla ya Hamad hajachanganyikiwa, lakini imesemwa kwamba; sahihi ni kuwa hadithi hii ni Mauquf kwa Aliy (maneno ya swahaba mtukufu Aliy na si maneno ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam).

 

Naye Imamu al-Nawawy akasema;

Hadithi hii ni dhaifu kwa sababu Atwaa amedhoofishwa, na Hamad anakosea.

Baada ya Sheikh Al-Bani kutoa maelezo ya maulamaa kuhusu hadithi hiyo ndiyo akaanza kulichambua kosa moja baada ya jingine lengo lake ni kuyachambua makosa ya kweli, na ambayo si makosa kwa mujibu wa misingi ya elimu ya mustalahul hadithi.

Kwa sababu kuna baadhi ya maulamaa kama Imamu Al-Nawawy wameona kuwa miongoni mwa makosa yaliyopelekea udhaifu wa hadithi hiyo ya kuoga janaba ni kuwa Hamad bin Salama anakosea.

Sheikh Al-albani akasema kumtetea Hamad na kuwajibu wale walioidhoofisha hadithi hiyo kwa sababu ya Hammad, na haya yafuatayo ni maneno ya sheikh Al-Bani:

 

" .

- ...".

2/332-333.

 

Hii ni sababu nyonge kama ilivyo sababu iliyotangulia kabla yake, kwa sababu Hamad bin Salama ni IMAMU miongoni mwa maimamu wa kiislamu ni THIQA (muadilifu mwenye hifdhi nzuri) tena ni HOJA na hakuna shaka yoyote katika hilo, na suala la kukosea halimtoi katika daraja hiyo, kwani ni nani asiyekosea?

Lau kama kila mpokezi zitakataliwa hadithi zake kwa sababu ya kuwa anakosea tu, basi wasingesalimika ila wachache miongoni mwa kundi kubwa la watu Thiqaat (wadilifu wenye hifdhi nzuri) tena katika watu waliomo katika sahihi mbili (Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim) wachalia mbali vitabu vingine.

Na kwenye hilo la kuzikubali hadithi za Hamad ndivyo walivyopita maulamaa wa hadithi waliotangulia na waliofuatia na miongoni mwa hao ni huyo Imamu al Nawawy- isipokuwa itakapothibiti kukosea kwake.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama Sil sila Dhaifa juzuu ya 2 ukurasa 332-333.

 

Hebu ndugu msomaji yasome tena maneno ya ndugu Juma ambayo amemnukuu sheikh wake al Qannubi kwa uangalifu, amesema bwana Juma:

 

Na akasema Al-albani (mwanachuoni wa hadithi wa kiwahabi) katika kitabu chake AL DHAIFA juzuu ya 2 ukurasa wa 333:

hakika ya Hamad anakosea sana.!!!

Mwisho wa kunukuu.

Ndugu msomaji, hebu linganisha maneno haya ya ndugu Juma na sheikh wake Al-Qannubi wanayodai kuwa ni maneno ya sheikh Al-Bani, na hayo maneno yenyewe ya sheikh Al-Bani ambayo tumeyakunukuu hapo juu kutoka kwenye kitabu chake, ukiliyanganisha utaona yanavyotofautiana na maneno ya sheikh Al-Bani, sheikh Al-Bani anasema:

HAMAD BIN SALAMA NI IMAMU MIONGONI MWA MAIMAMU WA KIISLAMU NI THIQA TENA NI HOJA NA HAKUNA SHAKA YOYOTE KATIKA HILO, NA SUALA LA KUKOSEA HALIMTOI KATIKA DARAJA HIYO, KWANI NI NANI ASIEKOSEA ?

 

Juma anadai kwamba sheikh Al-Bani amesema: HAKIKA HAMAD ANAKOSEA SANA na maneno hayo Juma anadai kwamba ameyanukuu kutoka kwa sheikh wake mkubwa Said Mabruk al-Qannubi!

Lakini jambo kubwa la ajabu ambalo linawashangaza wasomaji ni kuwa maneno ya sheikh Al-Bani yako kinyume chake na anavyodai Juma na al-Qannubi, Sheikh Al-Bani anasema: HAMAD NI IMAMU MIONGONI MWA MAIMAMU WA KIISLAMU, THIQA, TENA HOJA?!

Pia isitoshe sheikh Al-Bani amemtetea sana Hamad dhidi ya wale wenye kudai kwamba anakosea, akafikia kusema : basi ni nani asiekosea?.

Bila shaka ndugu msomaji kwa maelezo haya utakuwa umebainikiwa na uongo alioufanya Juma na sheikh wake al-Qannubi.Wameamua kufanya hivyo kwa makusudi baada kugundua kwamba sheikh Al-bani mwanachuoni mkubwa wa hadithi katika zama hizi, anayekubalika na waislamu wengi duniani tena kwa kiwango cha juu mno! Kwa hiyo wakaona wamtumie kama ngazi ili wafikie malengo yao mabaya, ndipo bila haya wala aibu wakaamua kumzulia uongo wa wazi.

 

Wameamua kumzulia uongo sheikh huyo ili msomaji akiyasoma maneno hayo moja kwa moja adhanie kwamba sheikh Al-albani naye ni miongoni mwa wanaomtia kasoro Hamad bin Salama na kumdhoofisha kwa sababu ya kukosea sana, na hali yakuwa hivyo sivyo kabisa ! bali ni uwongo mweupe kama jua la mchana wa saa sita. Na hapana shaka kuwa kitendo hiki ni kitendo kiovu tena cha kidhalimu, na huo si mwenendo wala sera za maulamaa waliosimama katika njia ya haki ambao lengo lao ni kutaka kuwaelimisha watu haki ili waifuate, bali hivyo ni vitendo vya watu wa batili waliofilisika katika hoja, kwa sababu siku zote mtu mkweli mwenye hoja zenye nguvu hayuko tayari kughushi wala kusema uongo katika suala lolote, wachilia mbali suala la dini, sasa inakuwaje mtu mwenye kudai uimamu na ijtihadi tena mcha Mungu awafanyie ghushi waislamu katika jambo la itikadi ya dini yao kwa sababu ya kulinda misimamo ya kimadhehebu na ukabila ?!

Bali kwa mujibu wa itikadi yao ya batili ya kikhawariji (kiibadhi) hiyo ni dhambi ya kumuingiza mtu motoni milele na wala hatoki tena, na hakuna wa kumuombea, na kama ataombewa basi maombi hayo hayatokubaliwa !

Na hapa Juma anajinyonga mwenyewe kwa kitanzi chake kwa sababu ya itikadi yao potofu, anasema katika kitabu chake KISIMAMO KATIKA SALA ukurasa wa 28 :

 

Na unajua Sheikh X. ni kitu gani kimewafanya wanazuoni wa kiibadhi wasiseme uwongo?

Ni kwa sababu ya itikadi yao kwamba MADHAMBI MAKUBWA YANAMUWEKA MTU MOTONI MILELE NA YANAMPOROMOSHEA MEMA YAKE, NA UWONGO NI KATIKA MADHAMBI MAKUBWA.

Mwisho wa kunukuu.

 

Tazama hapa namna wanavyojinyonga na kamba yao wenyewe! Je wewe ndugu Juma, na sheikh wako Al-Qannubi hamuogopi kukaa motoni milele kwa kusema uongo? Je hamuogopi kuporomoshewa amali zenu na kuanguka uadilifu wenu?

Hivi ndugu Juma kwa sababu ya uongo wenu kama huu ndiyo mnataka kufanya mijadala na maulamaa wakubwa kama Ibn Baz -kama mnavyodai- na mko tayari kwenda kuapa kwenye Kaaba?! Hamuogopi ?!

Hivi kweli mnaweza kudai kwamba mwanchuoni mkubwa kama al-Allaama sheikh Abdul-Aziz Ibn Baz awakimbie watu kama nyinyi wenye hoja dhaifu tena za uongo namna hii ?!!!

Kama mkiwa mmeweza kupotosha yaliyoandikwa vitabuni ambayo yako dhahiri shahiri, na mkaweza kuwazulia maulamaa mambo ambayo hawakusema, kweli mtashindwa kuzipotosha, na kuzigeuza habari zilizofanyika ndani ya ofisi tena kwa siri, tena mashahidi wa tukio hilo ni nyinyi wenyewe? Eti Ibn Bazi amkimbia Khalili! Kwa hoja gani alizonazo Khalili na wafuasi wake? Hoja zenyewe ni hizi za uwongo anazozitaja Juma kutoka kwa Qannubi na Khalili?

Vitabu vya Al-bani vimejaa ulimwenguni mashariki na magharibi, mmemzulia wazi wazi ! je mtashindwa kuzua yaliyofanyika ofisini kwa siri?

 

Ndiyo maana ukiyatazama maneno ya Juma kuhusu suala la kukutana Ibn Baz na Khalili utauona uongo unaelea juu juu, kwa mfano pale aliposema:

Kwa hivyo Al-khalili akamtaka Bin Baz ambaye kawaita maibadhi MAKAFIRI wende mbele ya Al-kaba Takatifu wakaombe hivi hivi, lakini Bin Baz akaogopa.

Na hii inatosha kuonesha kuwa hata yeye mwenyewe sh. Bin Baz hana hakika na itikadi yake.

Na kama si hivyo kipi kimemzuia kumtaka Mwenyezi Mungu aibainishe haki baina yake na watu ambao kawaita makafiri.!!!!

Mwisho wa kunukuu uwongo wa ndugu Juma.

Tazama kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 42.

 

Je ni kweli Ibn Baz amewaita maibadhi makafiri?

Ni mahali gani hapo? Kitabu gani ? Mbona hukututajia?

Vitabu vya Ibn Baz vimejaa tele hapa duniani, hebu tutajie kitabu kimoja ambacho Ibn Baz amesema maneno hayo, na hii ni chalenji nina kupa wewe Juma na masheikh zako Khalili, al-Qannubi, na Ahmad bin Suud al-Siyabi mtutajie ni mahali gani Ibn Baz amewaita maibadhi kuwa ni makafiri kwa uwazi kabisa, bila ya kuhitajia taawili.

Na haya ndiyo maajabu ya makhawariji hawa wa akhiril-zaman! Wanasema uongo wala hawana haya, na vitabu vyao vimejaa uongo.

Rudi juu

HATA MUFTI WAO PIA ASEMA UWONGO!

 

Kwa ushahidi zaidi hebu tukudokolee mfano mmoja wa uongo wao na mifano mingine itafuatia katika sehemu zake, ni pale mufti wao Khalili alipoamua kulipindua shairi la Ibnul-Qayyim kwa makusudi, kisha Juma naye akafuatia vivyo hivyo ! Ametaja al-Khalili katika kitabu chake AL-HAQU DAMIGH, naye Juma katika kitabu chake Kisimamo ukurasa wa 93 akasema hivi:

Na akasema katika NUNIA kuhusu wote ambao hawana itikadi ya kihashawiya (Kiwahabi) kwamba ni maaduwi ambao ukafiri wao ni mkubwa kuliko mushrikina (wenye kuabudu masanamu) Anasema (Ibnul-Qayyim):

 

***

Na muatil ni mwenye kuutangaza uadui *** na washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri.

 

Juma na mufti wake Khalili wameyapindua maneno haya ya Ibnul-Qayyim kwa makusudi, mimi ninawapa chalenji watuletee maneno haya, na mimi ninasema kwamba maneno haya hayamo katika NUNIA ya Ibnul-Qayyim.

Maneno yaliyomo katika NUNIA ni haya:

** *

 

Na muatila ni wenye kuutangaza uadui *** kwa sura ya kumtakasa Rahman (Allah mwingi wa rehma).

Haya ndugu msomaji ni machache kati ya mengi ya uongo yaliyojaa kwenye vitabu vya makhawarij (maibadhi) wa zama hizi, mpaka Mufti wao pia asema uongo! Na inaonekana kuwa Juma hasomi vitabu kwa kuhakiki mambo, bali yeye ananukuu kiupofu kutoka katika vitabu vya masheikh zake Khalili na Qannubi.

Hebu tuendelee kuyatupia macho maneno ya ndugu Juma al-Mazrui katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 113, kuhusu hadithi hii, anasema ndugu huyo:

Rudi juu

KASORO YA PILI YA HADITHI HII:

NAKALA KUTOKA KWA AL-QANNUBI.

 

Jambo la pili ni kuwa hadithi hii ina kasoro ya pili nayo ni kuwa "" (haitoki kwa Mtume (S.A.W.). Anasema Al imamu Al-tirmidhi hadithi hii HAMAD BIN SALAMA kainasibisha na Mtume (S.A.W.) (Wala haitoki kwake) na ameipokea (hadithi hii) Hamad bin Zaid na Sulaimaan bin Mughira kutoka kwa Thabit Al-banaani kutoka kwa Abdul-rahmaan bin Abi Leila (ni) KATIKA MANENO YAKE (yaani hadithi hii ni maneno ya Abdul-rahamaan bi Abi Leila na si maneno ya Mtume (S.A.W.)..

Kisha akasema tena ndugu Juma al Mazrui:

 

Mpaka hapa inatubainikia kwamba hadithi hii si ya kutegemea.

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Njia ya kwanza:

Kama tulivyotangulia kukutajia kauli za maulamaa wa hadithi kuhusu riwaya za Hamad bin Salama kutoka kwa Thabit al-Bunaani (hapa ndugu Juma amekosea kwa kumuita Al-banaan, na sahihi ni Al bunaani) kwamba yeye Hamad bin Salama ni mtu madhubuti zaidi kwa mapokezi kutoka kwa Thabit na iwapo atatokea mtu yeyote kupingana na mapokezi ya Hamad bin Salama kutoka kwa Thabit basi kauli ya kuchukuliwa ni kauli ya Hamad.

 

Na hapa tunaona kwamba Hamad bin Zaid na Sulaimaan Ibnul-Mughira wawili hawa wametofautiana na Hamad bin Salama katika riwaya hii kutoka kwa Thabit al-Bunaani.

Amesema Imamu Yahya bin Main:

: .

Yeyote atakayetofautiana na Hamad bin Salama katika (mapokezi yake kutoka) kwa Thabit, basi kauli (ya kuchukuliwa) ni kauli ya Hamad.

Tazama Mizanul Itidali 1/591.

Njia ya pili:

Hamad bin Zaid ni mashuhuri kwa tabia ya kuzifanya Mawquuf hadithi ambazo ni Mar fuu au kwa lugha nyingine ana tabia ya kuzinasibisha na Maswahaba kauli ambazo ni za Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- huwenda hapa pia amelifanya jambo hilo.

Amesema Imamu Yaaqub bin Shaibah:

Hamad bin Zaid ni madhubuti zaidi kuliko Hamad bin Salama na wote hao ni watu Thiqa isipokuwa Hamad bin Zaid ni maarufu kwa kuzifupisha isnadi na kuzifanya kuwa Mawqufu hadithi ambazo ni Marfuu...

Tazama Tahdhibul-Tahdhibi juzuu2 ukurasa 10.

 

Njia ya tatu:

Zimepokewa hadithi nyingine nyingi kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- na kauli nyingi kutoka kwa Maswahaba zinazoitilia nguvu hadithi hii ambayo katika sanadi yake yumo Hamad bin Salama ambaye ni mtu madhubuti zaidi katika riwaya za Thabit al-Bunaani kuliko wapokezi wote wanaopokea kutoka kwa Thaabit.

Mpaka hapo ndugu msomaji utakua umebainikiwa na majibu yetu juu ya sanadi ya hadithi hii dhidi ya upotoshaji uliofanywa na jamaa hawa, na -wali llaahil hamdu hoja zetu zimekubainikia dhidi ya hoja dhaifu za bwana Juma na sheikh wake.

Kisha ndugu Juma akazidhoofisha riwaya nyingine ambazo nyingi katika hizo wapokezi wake ni dhaifu, na hakuishia hapo tu, bali hata hadithi nyingine ambazo ni sahihi zilizopokelewa kwa njia nyingi lakini baadhi yake zina udhaifu pia amezidhoofisha, kinyume na ulivyo utaratibu katika taaluma ya elimu hii ya mambo ya hadithi.

Ndugu Juma yeye hakuzichunga kanuni hizo wala hakuzijali, na akazidhoofisha hadithi hizo bila ya kuheshimu kanuni za taaluma hii.

Rudi juu

MAANA SAHIHI YA NENO AL-ZIYADAH

 

Kisha akahitimisha maudhui kwa mukhtasari kwa kusema:

Mpaka hapa tumefikia mwisho wa mjadala wetu wa kuielezea aya ya 26 ya sura ya 10 yenye kusema:

Wale waliofanya mema watalipwa wema na ziada.

Pamoja na riwaya zake ambazo wamezitegemea wale wenye kuitakidi kumuona Mwenyezi Mungu katika tafsiri yao hiyo.Tumebainisha kwa ushahidi wa kielimu kuwa riwaya hizi zote ni batili: hakuna hata riwaya moja ambayo ni sahihi: zote zimesimuliwa na wapokezi madhaifu, wenye kughushi na waongo.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama ukurasa 132-133 katika kitabu chake.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Hayo ndiyo yalikuwa malengo yake makubwa ya ule mchezo wake mchafu wa kuzidhoofisha hadithi za Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-, aliamua kwa makusudi kuyapindisha baadhi ya maandiko na kupotosha maana zake ili afikie kwenye lengo hili, nalo si lengo jingine zaidi ya kupingana na tafsiri sahihi ya bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- alioitoa juu ya aya 26 ya surat Yunus !

Ili yeye atuletee tafsiri yake ambayo itaafikiana na madhehebu yake ya kiibadhi inayopinga kuonekana Allah huko akhera kwa macho, na ndiyo maana hakuufanya utafiti wake kuwa ni wa kielimu ulio na insafu (uadilifu), bali akatumia zaidi uongo na hila.

Lakini uhakika wa mambo si kama alivyodai ndugu huyo, kwamba hadithi zote zilizoitafsiri aya hii ni batili, bali ni kama tulivyokuthibitishia kielimu na uadilifu kwamba:

-Ziko riwaya ambazo wapokezi wake ni dhaifu na hakuna namna ya kuzipa nguvu.

 

-Na ziko riwaya nyingine ambazo wapokezi wake ni madhubuti, na kama kuna kasoro ndogo ndogo basi ni zile za kibinaadamu ambazo kiutaalamu haziyaathiri mapokezi yao bali zinaweza kukubalika kwa kujumuishwa na riwaya nyingine zinazozitiliana nguvu.

-Pia ziko riwaya ambazo ni sahihi na wala hazina shaka juu ya usahihi wake. Kama riwaya hii tuliyoitaja hapo nyuma.

Amesema tena ndugu Juma:

Na neno ZIADA ambalo limo katika aya hii, Mwenyezi Mungu hakusema ni ziada gani.

Na kwahivyo haitakiwi tudai katika mambo ya itikadi kitu ambacho hakina ushahidi sahihi.

Mwisho wa kunuku.Tazama katika kitabu chake hicho ukurasa wa 133.

 

Majibu yetu ni kwa njia mbili:

 

a) Kama yakiwa makusudio ya Juma ni kwamba hakuna aya ya Quran iliyoelezea maana ya neno ziada, hilo ni kweli.

 

b) Lakini kama anakusudia kuwa hakuna kabisa hata katika maneno ya mjumbe wa Allah, bila shaka hilo si kweli, kama tulivyolithibitisha hilo kupitia hadithi sahihi ya bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- alipokuwa akiitafsiri aya hii kama ilivyokuja katika hadithi hii ambayo:-

Imepokewa kutoka kwa Suheib, kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- amesema kuhusiana na kauli ya Allah:

Wale waliofanya mema watapata wema na ziada.

Akasema Mtume swalla llaahu alayhi wasallam:-

Watakapoingia watu wa peponi katika pepo atanadi mwenye kunadi: hakika nyinyi mna ahadi mbele ya Allah anataka kukutekelezeeni.

Watasema kwani hukuzingarisha nyuso zetu na ukatuokoa na moto na ukatuingiza peponi?

Akasema (Mtume swalla llaahu alayhi wasallam):

BASI LITAONDOLEWA PAZIA NA WATAMTAZAMA YEYE ALLAH NA HAWAJAWAHI KUPEWA KITU WANACHOKIPENDA MNO KULIKO HUKO KUMTAZAMA YEYE ALLAH NA HIYO NDIYO ZIADA.

Hadithi hii ni sahihi imepokewa na Imamu Muslimu tazama sahihul muslim hadithi namba 449.

 

Bila shaka tafsiri hii ya bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- inaukata mzozo uliopo baina ya wale wenye kuitakidi kuonekana Allah huko akhera kwa macho na wale wenye kuipinga itikadi hiyo.

Na haipingi hukumu hii ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- ila yule ambaye moyo wake umejaaa unafiki, kibri, na kufuata matamanio ya nafsi yake.

Ama kuhusu majaribio ya ndugu Juma ya kutaka kuidhoofisha hadithi hii bila shaka majaribio hayo yamefeli kama ilivyokudhihirikia katika uchambuzi wetu.

 

Kisha akasema tena:

Na kwa kutazama hizo kauli nyengine tofauti zilizosemwa basi utaona kuwa iliyokaribu na usahihi ni kauli ya Alqama bin Qais ambaye amesema kwamba ZIADA hapa ni kuzidishwa matendo ya watu wema aliyefanya moja akalipwa mara kumi ya wema wake...

Mwisho wa kunukuu.

Tazama katika kitabu chake Hoja zenye nguvuukurasa wa 133.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu hapa ni kwa njia tatu:

Njia ya kwanza:

Kila muislamu anatakiwa kuamini kwamba Allah ni mwingi wa fadhila mwingi wa huruma kwa waja wake, amewakirimu waja wake kwa fadhila nyingi hapa duniani, na ataendelea kuwakirimu zaidi huko akhera, atawapa waja wake fadhila nyingi mpaka waridhike.

Kwa kuwa yamekuja maandiko tofauti ambayo yanaelezea kuwa watu wema huko akhera watalipwa wema wao na ziada juu, tunatakiwa kuyakubali maandiko yote sahihi yaliyo tufahamisha hivyo, na kufanya hivyo si kuthibitisha mgongano baina ya maandiko hayo, ndiyo maana akasema Imamu Ibn kathir katika kitabu chake cha tafsiri alipokua akiitafsiri aya isemayo:

(26)

Na wale waliofanya mema watapata wema na ziada.Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila.Hao ndio watu wa Peponi. Humo watakaa milele. Yunus 26.

 

Akasema Ibn Kathir:

: { } ݡ .

 

Na kauli yake (Allah): ZIADA ni kuzidishiwa malipo ya matendo; jema moja utazidishiwa mema kumi mfano wake, mpaka ziada mia saba, na zaidi ya hapo. Pia ziada itakusanya yale yote atakayowapa Allah huko peponi: Makasri, Hurul-ain (wanawake wa peponi), radhi zake Allah, na yale aliyowafichia miongoni mwa vitulizo vya jicho na (ZIADA) ILIYO BORA KULIKO ZOTE, NA ILIYO JUU ZAIDI NI KUUTAZAMA USO WAKE ALLAH ULIOMTUKUFU. Kwa sababu hiyo ndiyo ziada kubwa kuliko vitu vyote walivyopewa, na hawakustahiki kupata hilo kwa sababu ya matendo yao, bali ni kwa fadhila zake (Allah ) na rehma zake.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama tafsirul Quranil adhim juzuu 4 ukurasa chapa ya kwanza ya daaru Ibn Hazm ya mwaka 1419=1998.

 

Kwa mujibu wa maneno hayo ni kwamba watu watapata ziada nyingi, na miongoni mwa ziada hizo ni: kwamba yule aliyefanya wema mmoja atalipwa mara kumi ya wema wake, na hali kadhalika atafadhiliwa kumuona mola wake -Jalla jalaaluh-, na kuyatafsiri maandiko kwa namna hii ni kuitumia ile kanuni ya upatanisho (the juristic law of reconciliation between the apparently conraditory texts) kanunni ya upatanisho baina ya maandiko ambayo dhahiri yake yanagongana, kanuni ambayo ndugu Juma pia ameikubali, na kuitumia kama alivyoielezea katika ukurasa wa 261 katika kitabu chake.

Lakini kwa masikitiko makubwa kabisa, ameshindwa au hakutaka kuifanyia kazi kanuni hiyo aliyoikubali mwenyewe na alipofika kwenye maandiko haya yaliyokuja kuitafsiri aya hii akaitupilia mbali kwa sababu haiendi sambamba na itikadi yake!

 

Njia ya pili:

Je, unajua ni kwanini ndugu yangu msomaji ndugu yetu Juma ameipa nguvu kauli ya Alqama bin Qais? Ni kwa sababu riwaya hiyo ina nguvu kuliko riwaya nyingine? Au ameipa nguvu kwa sababu inaafikiana na msimamo wake batili?

Jawabu ni hili hapa:

Ndugu Juma ameipa nguvu kauli ya Alqama bin Qais si kwa sababu kuwa ni sahihi na ina nguvu, bali ni kwa sababu inaafikiana na msimamo wake batili.

Na kama utaifanyia utafiti wa kielimu riwaya hiyo utaona kwamba miongoni mwa wapokezi wake ni IBN HUMAID (jina lake kamili ni; MUHAMMAD BIN HUMAID BIN HAYYAAN AL-TAMIMI AL-RAZI) kama alivyoeleza Ibn Jarir al-Twabariy katika kitabu chake cha tafsiri juzuu ya 11 ukurasa 125.

Ibn Humaid huyo huyo ndiye yule ambaye ndugu yetu Juma alimtia kasoro na kuidhoofisha riwaya yake, kama alivyoelezea katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa 123. Lakini hapa bwana Juma anaitaja riwaya yake na anaipa nguvu!

Hivi inakuwaje mpokezi mmoja huyo huyo ambaye ametuelezea kwa vishindo kwamba ni dhaifu, mwongo !!! Mara ghafla anakuja kutubadilikia na kutwambia kwamba riwaya yake ni sahihi tena ndiyo yenye nguvu !!! Je hapo kuna uadilifu?!

 

Kauli ya Juma kuhusu Ibn Huamid:

Hebu ndugu msomaji ni kunakilie maneno ya Juma alipokuwa akimuelezea Ibn Humaid, amesema Juma:

Sanad hii ni dhaifu sana kwa sababu ina msururu wa wapokezi madhaifu na waongo.

Kisha akasema:

1)  IBN HUMAID na jina lake kamili ni MUHAMMAD BIN HUMAID BIN HAYAAN AL-TAMIMI AL-RAZI.amesema Ishaq bin Mansur al-kuusaj! Akisimulia kauli ya Ali bin Mihran juu ya MUHAMMAD BIN HUMAID akisema kwamba; sijapata kuona mtu (anayejifanya) jasiri juu ya Mwenyezi Mungu (hamuogopi Mwenyezi Mungu) kuliko yeye alikuwa akizichukua hadithi za watu kisha akizigeuza Na akasema tena kuwa sijapata kuona mtu bingwa wa uwongo kuliko watu wawili: Sulaiman Al-shadhakuni na MUHAMMAD BIN HUMAID.!!! Mwisho wa kunukuu.

Tazama katika ukurasa wa 122-123 katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu.

 

Haya ndugu msomaji bila shaka umejionea mwenyewe namna watu hawa wanavyocheza karata tatu! Inakuaje mpokezi akipokea riwaya inayopingana na msimamo wa kiibadhi hafai ni dhaifu, anaghushi, muongo, na riwaya zake hazikubaliki, tena mpaka inafikia kiwango cha kuwazulia baadhi ya maulamaa uongo ilimradi dau lifike pwani.

Lakini mpokezi huyo huyo akipokea riwaya ambazo zinaafikiana na msimamo wa kiibadhi basi riwaya hizo hazina neno bali ndizo zenye nguvu!!!

Bila shaka ndugu msomaji mpaka hapa utakuwa umethibitisha yale niliyokuambia huko nyuma kwamba: hawa watu wako katika kutetea itikadi zao tu, tena si kwa uadilifu wala kwa hoja za kielimu, bali wako tayari kuupindisha ukweli kwa maslahi yao, mpokezi mkweli ni yule anayepokea riwaya za kuwaunga mkono wao, ama yule anayepokea riwaya kinyume na itikadi zao za kikhawariji basi huyo ni muongo,dhaifu, anaghushi na tuhuma nyingi za uongo.

Nadhani ndugu msomaji umejionea mwenyewe, mpokezi mmoja huyo huyo amepewa hukumu mbili tofauti! Huko nyuma riwaya yake ina nguvu, lakini hapa ni muongo na hakuna muongo kama yeye!!!

Siku zote mtu unapofanya utafiti wa kielimu, kwa lengo la kuwafaidisha watu na utafiti wako, basi ni lazima uwe na sifa kuu mbili:

1) Elimu ya kutosha juu ya jambo unalolifanyia utafiti.

2) Uwe mkweli na muaminifu katika utafiti wako.

 

Na sifa zote hizi Juma amezikosa, na kama mtu atakosa sifa moja kati ya hizo mbili lazima kutapatikana upotoshaji wa haki na wala ukweli hautakuwepo, sikwambii zikikosekana sifa zote mbili.

Lakini hilo halinishangazi sana kwa sababu hizo ndizo sera za Ahlul ahwaa (watu wanaofuata matamanio yao katika mambo ya dini).

Rudi juu

MUKHTASARI.

 

Kwa ufupi ni kwamba watu wema watakaoingia peponi, Allah -jalla jalaaluh- atawakirimu kwa neema nyingi mno na kubwa katika neema hizo ni kupata radhi zake na kumuona yeye -subhaanahu wataalaa- kwa macho yao.

 

Na miongoni mwa ushahidi wa jambo hilo ni aya hiyo ya 26 katika surat Yunus (10) aya ambayo imetafsiriwa na bwana Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- Mtume ambaye ametumwa kwa kazi hiyo ya kuwabainishia watu yale yaliyoletwa kutoka kwa mola wao, na katika tafsiri yake mjumbe huyo mtukufu anasema kwamba neno ZIADA lililotajwa katika aya hiyo maana yake ni KUMUONA ALLAH -subhaanah- huko peponi, na hilo limepokewa kwa mapokezi yaliyo sahihi kabisa ambayo hayana shaka ndani yake japokuwa ndugu Juma na kaumu yake walijaribu kuyatia dosari.

Kwa hiyo tunasema kwamba itikadi ya kuonekana Allah huko akhera ni itikadi sahihi ambayo imeelezewa na Quran tukufu kitabu ambacho hakiingiliwi na mambo batili, na Sunna sahihi za Mtume Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam, na wakaichukua itikadi hiyo Maswahaba zake watukufu Allah awaridhie.

Rudi juu

HOJA YA TATU

 

Hoja ya tatu wanayoitegemea Ahlu Sunna katika kuithibitisha kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni hadithi sahihi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam-.

 

Inshaallaha katika sehemu hii tutazitaja hadithi ambazo zimethibiti kutoka kwa bwana Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- kwa mapokezi yaliyo sahihi yasiyo na shaka yoyote kwa kuzingatia kanuni za mapokezi ya hadithi.

Na hadithi sahihi juu ya masala haya ziko nyingi mno, lakini hapa tutazitaja kwa uchache tu kwa lengo la kufupisha.

Ama kuhusu chalenji aliyoitoa Juma ya kutaka aletewe hadithi moja tu sahihi, ni chalenji ambayo haina uzito wowote wa kielimu, maana Juma amejigamba na kujisifu kwa kusema katika kitabu chake KISIMAMO KATIKA SALA ukurasa wa 22:

Chukua- kwa mfano, hadithi za kuonekana kwa Mungu: Hadithi hizi ziko kwa wingi, lakini na kuchalenj Sheikh X. wewe na wanazuoni wako uniletee hadithi moja tu sahihi inayosema kwa uwazi kwamba Mungu ataonekana.!!!

Mwisho wa kunukuu.

 

Tazama namna watu walivyo na jeuri na kiburi katika masala ya elimu ! badala ya kuomba msaada wa kuelimishwa juu ya masala ya kielimu asiyoyajua, yeye analeta lugha ya kiburi na jeuri, eti: nakuchalenj uniletee hadithi moja tu sahihi inayosema kwa uwazi kwamba Mungu ataonekana !!!

Mtu mwenyewe anayesema hivyo kazi yake kunukuu tu kutoka kwa masheikh zake wala hawezi kuyahakiki mambo ya kielimu, wakikosea naye anakosea, wakidanganya naye anadanganya kama ulivyojioenea.

Sisi tunamwambia ndugu Juma awache jeuri na kibri ajitahidi kusoma na kufanya utafiti zaidi kwa misingi ya uadilifu haki itambainikia badala ya kungangani kasumba za kujikweza na kufuata umadhehebu.

Na hizi zifuatazo ni baadhi ya hadithi sahihi zinazosema kwa uwazi kabisa kwamba watu wema watamuona Mola wao huko akhera kwa macho:

Rudi juu

HADITHI YA KWANZA

 

Hadithi hii imepokewa kwa njia nyingi, lakini kwa kufupisha tutazitaja baadhi ya njia hizo:

Njia ya kwanza:

:

...."

 

Amesema Imamu al-Bukhari:

Ametusimulia Amru bin Aun, amesema: ametusimulia Khalid na Hushaim, kutoka kwa Ismail, kutoka kwa Qais, kutoka kwa Jarir:

Tulikua ni wenye kukaa mbele ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- kwa ghafla akautazama mwezi, katika usiku wa mwezi mpevu, akasema:

Kwa hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona huu (mwezi) hamtasongamana katika kuuona..

Tazama Sahihul-Bukhari, hadithi namba 6882.

 

Njia ya pili:

:

:

...."

 

Amesema Imamu Muslimu -Allah amrehemu-:

Ametusimulia Zuhayr Ibn Harbi, amesema: ametusimulia Marwan Ibn Muawiya al-Fazaariy, amesema: ametusimulia Ismail Ismail Ibn Abi Khalid, amesema ametusimulia Qais Ibn Abi Hazim, amesema: nimemsikia Jarir Ibn Abdillahi anasema:

Tulikua ni wenye kukaa mbele ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam- kwa ghafla akautazama mwezi, katika usiku wa mwezi mpevu, akasema:

Kwa hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona huu (mwezi) hamtasongamana katika kuuona..

Tazama Sahihu Muslim, hadithi namba 1002.

 

Njia ya tatu:

:

.

 

Amesema Imamu Abu Daud -Allah amrehemu:-

Ametusimulia Isaq Ibn Ismail, amesema: ametusimulia Sufyani, kutoka kwa Suheil Ibn Abi Swaleh, kutoka kwa baba yake (Abu Swaleh) kwamba amemsikia yeye akisimulia kutoka kwa Abu Hurayra, amesema: walisema watu: Ewe Mtume wa Allah ! Je tutamuona Mola wetu siku ya Qiyama?

Akasema: Je mnadhuriana katika kuliona jua wakati wa mchana ambao hakuna mawingu?

Wakasema: hapana. Akasema (Mtume): Je mnadhuriana katika kuuona mwezi katika usiku wa mwezi mpevu na hali hakuna mawingu? Wakasema: hapana. Akasema (Mtume): Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hamtodhuriana katika kumuona yeye (Allah) kama msivyo dhuriana katika kukiona kimoja kati ya hivyo (jua na mwezi).

Tazama kitabu Sunan Abi Daud, hadithi namba 4105.

Rudi juu

Njia ya nne:

:

:

".

 

Amesema Imamu Ahmad Ibn Hanbal:

Ametusimulia Yahya Ibn Adam, ametusimlia Abu Bakri Ibn Ayyash, kutoka kwa Amashi kutoka kwa Abu Swaleh, kutoka kwa Abu Said al-Khudriy-Radhiyallaahu Anhu- amesema: amesema Mtume swalla llaahu alayhi wasallam-:

Kwa hakika nyinyi mtamuona Mola wenu -Azza Wajalla-, wakasema (Maswahaba): Ee Mtume wa Allah! Tutamuona Mola wetu?

Akasema (Mtume): Je mnadhuriana katika kuliona jua katika nusu ya mchana ? wakasema: Hapana.

Akasema (Mtume): Je mnadhuriana katika kuuona mwezi katika usiku wa mwezi mpevu? Wakasema: Hapana.

Akasema: basi nyinyi hamtadhuriana katika kumuona yeye (Mola wenu) kama ambavyo hamdhuriani katika kuliona (jua na mwezi mpevu).

Tazama katika kitabu Musnad cha Imamu Ahmda, hadithi namba 10697.

 

Kadhalika ameitaja hadithi hii Imamu al Bukhari katika Sahihul-Bukhari hadithi namba 7434.Na Imamu Muslimu katika Sahihi yake hadithi namba 182.Na Imamu Ibn Abi Asim hadithi namba: 443,444,445,446,447,448,449 mpaka 458.

Rudi juu

SANADI YA HADITHI HII

Ama kuhusu sanadi ya hadithi hii:

Sanadi yake ni sahihi na wala hakuna mwanachuoni yeyote wa hadithi aliyeitia dosari zaidi ya Juma na sheikh wake al-Qannubi na Inshaallah utaliona jawabu letu dhidi ya ubabaishaji wao.

Rudi juu

KUHUSU MATNI YA HADITHI HII:

 

Ama kuhusu maana ya hadithi:

Bila shaka hadithi hii iko wazi kabisa na wala haihitajii maelezo marefu ili ieleweke, isipokuwa kuna jambo muhimu la kutanabahisha nalo ni kwamba:

Bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- ametubainishia kuwa tutamuona Allah -Subhaanah- kwa uwazi kabisa bila ya kudhuriana wala msongamano wowote, kama vile ambavyo watu hawasongamani wala hawakanyagani katika kuutazama mwezi mpevu wa tarehe kumi na nne, na kama vile ambavyo watu hawasongamani wala hawakanyagani katika kulitazama jua la mchana ambao hakuna mawingu.

Na zimepokewa hadithi nyingi ambazo zina maana kama hii walizozipokea Maswahaba wengi kutoka kwa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam-, lakini kwa kufupisha tutosheke na riwaya hizi chache zilizo pokelewa kutoka kwa Maswahaba watatu wa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- (Jarir Ibn Abdillahi, Abu Said al-Khudriy na Abu Huraira Allah awe radhi nao, na mwenye kutaka ziada basi arejee vitabu vya hadithi.

Na muislamu yeyote mwenye imani ya kweli akifikiwa na habari yoyote ambayo ni sahihi kutoka kwa Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- hana budi kuikubali na kuusadiki ujumbe uliobebwa na hadithi hiyo na huo ndio ukamilifu wa Shahaadatu Anna Muhammadan Rasuulu-llahi (kukiri kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah) nayo ni:

Kuyaamini yote aliyokuja nayo mjumbe huyo na kuyasadikisha yote aliyoyaelezea kutoka kwa mola wake hata kama akili zetu duni hazikubali, na kadhalika kumtii Mtukufu huyo kwa kutenda mema aliyoyaamrisha na kuyaacha mabaya aliyoyakataza.

Rudi juu

JARIBIO LA KWANZA LA KUPOTOSHA HADITHI HII

Jaribio lake la kwanza ndugu Juma amelielekeza katika Sanadi ya hadithi hii, na akazielekeza tuhuma zake kwa mpokezi QAIS BIN ABI HAAZIM.

Amesema Juma al-Mzrui katika kitabu chake Hoja zenye nguvu ukurasa wa 253:

Hadithi hii imepokewa kupitia kwa Qais naye ni QAIS BIN ABI HAAZIM. Na mtu huyu wanavyuoni wengi wamemdhaifisha (wamesema kwamba ni dhaifu).

Mwisho wa kunukuu.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Katika itikadi ya makhawaarij (maibadhi) ni kwamba mtu akifanya dhambi kubwa kama vile kusema uongo, basi anakua kafiri na huko akhera ataingia motoni milele na hatoki katu. Sasa ajabu ni maibadhi hawa wa zama hizi kwa nini wanasema uongo?!!

 

Na ushahidi juu ya uongo wao ni huu ufuatao:

Ndugu Juma anadai kwamba Qais ni DHAIFU na wanavyuoni wengi wamemdhaifisha!!!

Maneno haya ni uongo na ukweli ni kwamba Qais ni THIQA (ni mtu muadilifu mwenye hifdhi nzuri) kwa mujibu wa kauli za maulamaa wa hadithi.

1-Amesema Imamu Yahya bin Main : THIQA.

 

2-Amesema Imamu Abu Daud: Mtu mwenye sanadi nzuri kuliko Taabiina wote (taabiina ni wafuasi wa maswahaba) ni Qais bin Abi Haazim.

 

3-Amesema Yaqub bin Abi Shaibah:

Alikuwa Qais ni katika Taabiina wa zamani mnona yeye ni mwenye ufanisi katika kupokea riwaya.

 

4-Amesema Ismail bin Abi Khalid:

Alikuwa (Qais) ni mtu madhubuti.

 

5-Na Imamu Ibn Hibbaana amemtaja miongoni mwa Thiqaat (watu madhubuti katika riwaya).

 

6-Amesema Imamu al-Dhahbiy :

Wameafikiana (maulamaa wa hadithi) juu ya kumfanya (Qais) kuwa ni Hoja na mtu YEYOTE ATAKAYEMSEMA VIBAYA BASI AMEJIUDHI MWENYEWE.

 

7-Na amesema al Hafidh Ibn Hajar:

Qais bin Abi Haazim al Bajaliy Abu Abdillahi al Kufiy ni THIQA.

 

Tazama vitabu vifuatavyo:

Taarikhul-Duuriy juzuu ya 2 ukurasa wa 95.

Kitabu Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan juzuu ya 5 ukurasa 307.

Tahdhibul-Tahdhibi juzuu ya 4 ukurasa wa 561 -586.

Al-Taqribu ukurasa 134-135, tarjama namba 6250.

 

Mpaka hapa madai ya Juma kwamba Qais ni dhaifu yatakuwa yameporoka.

Rudi juu

TUHUMA YAKE YA PILI DHIDI YA QAIS:

 

Amesema ndugu Juma:

Anasema Yaaqub bin Abi Shaiba QAIS ni katika wafuasi wa maswahaba wa mwanzo . na wamesema wanavyuoni wetu wengine wakamtukuza(na) wengine wakamshambulia na wakasema kuwa ana hadithi (nyingi) MUNAKiR.

Na anasema Ismail bin Abi Khalid, ambaye hadithi hii imepita kwake, kuwa: QAISaliishi mpaka akavuka miaka mia na ziada nyingi juu mpaka akaharibika fahamu na kurukwa na akili.

Na akasema Ibn Al Madini kaniambia Yahya bin Said kuwa QAIS BIN ABI HAAZIM hadithi zake ni MUNKAR, kisha akazitaja Yahya hadithi (zake nyingi ambazo ni) MUNKAR.kwahivyo kutokana na maneno haya hadithi hii haina usahihi wowote. !!!

Mwisho wa kunukuu.Tazama maneno hayo ya bwana Juma katika kitabu chake Hoja zenye nguvu ukurasa wa 253-254.

Rudi juu

MAJIBU YETU:

 

Majibu yetu Inshaallah yatakuwa kwa njia mbili:

Njia ya kwanza, ni kuhusu kauli ya Ibn al-Madini kuwa ameambiwa na Yahya bin Said kwamba Qais bin Abi Haazim hadithi zake ni MUNKAR.

 

Ameijibu tuhuma hii Imamu al-Dhahbiy pale alipoitaja kauli hiyo kwa kusema:

Kisha (Yahya bin Said) akazitaja hadithi ambazo ameziona kuwa ni munkar, lakini hakufanya kitu, bali hadithi hizo zimethibiti, na wala haishangazi kupwekeka nazo (kuwa amezipokea peke yake) kwa sababu ya upana wa aliyoyapokea, na miongoni mwa hadithi hizo ni (ile inayotaja habari za) Mbwa wa Hauab.

Tazama mizanul itidaal juzuu ya 3 ukurasa 392-393.

 

Maana ya maneno haya ya Imamu al-Dhahbiy ni kwamba si sahihi kusema kwamba Qais hadithi zake ni MUNKAR au hadithi zake nyingi ni MANAKIR kwa sababu ya kupwekeka kwake katika kupokea baadhi ya hadithi bila ya kushirikiana katika mapokezi hayo na watu wengine, kwa sababu Qais alikuwa na hifdhi pana na riwaya nyingi, na baada ya kuzifuatilia hadithi zake imegundulika kwamba ni hadithi sahihi na miongoni mwa hadithi hizo ni ile ambayo Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- alitabiri kwamba baadhi ya wake zake watabwekewa na mbwa pindi wafikapo mahali paitwapo Hauab na hiyo ni hadithi sahihi.

 

Maana nyingine ya neno Munkari:

Amesema al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu chake Tahdhiibul- Tahdhiibi juzuu ya 4 ukurasa wa 562 akiitafsiri kauli ya Yahya bin Said al Qattwaan:

" : ".

Na makusudio ya al-Qattwaan (aliposema) Munkar: ni kupwekeka mutlaki.

Maana ya maneno ya Ibn Hajar ni kwamba:

Siyo makusudio ya Imamu al-Qattwaan aliposema hadithi munkar kuwa maana yake ni hadithi ya mtu dhaifu aliyepingana na mtu Thiqa kama ilivyozoeleka katika elimu ya Mustalahul hadithi bali makusudio ni kupwekeka mpokezi katika mapokezi yake. Na si Imamu al-Qattwaan peke yake aliye litumia neno MUNKAR kwa maana ya kupwekeka, bali hata Imamu Ahmad bin Hanbal anakawaida ya kulitumia neno hilo kwa maana ya kupwekeka, na kulitumia neno hili kwa maana hii halileti ile maana ya kujeruhi iliyozoeleka katika elimu ya hadithi.

 

Amesema Imamu Ibn Hajar katika Hadyu Saar ukurasa wa 453 kuhusu matumizi ya Imamu Ahmad juu ya tamko hili:

" ...".

Na tamko hili (MUNKAR) analitumia Imamu Ahmad kwa yule ambaye analeta hadithi ngeni kwa watu wa rika lake...

 

Bado tunasisitiza kuwa, kuna muhimu mkubwa kwa mtu anayetaka kufanya utafiti wa mambo ya hadithi na riwaya, kusihi kwake na kutokusihi kuwa na utaalamu wa kutosha juu ya istilahi za maulamaa, bila ya hivyo, mtu atapoea na atawapoteza watu.

 

 

Njia ya pili:

Kuhusu kauli ya ndugu Juma al-Mazrui dhidi ya mpokezi Qais bin Abi Haazim pale aliposema:

Na amesema Ismail bin Abi Khalid, ambaye hadithi hii imepita kwake, kuwa: QAIS aliishi mpaka akavuka miaka mia na ziada nyingi juu mpaka akaharibika fahamu na kurukwa na akili.

Tazama katika kitabu chake Hoja zenye Nguvu ukurasa wa 254.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu ni kama ifuatavyo:

Tulishawahi kuijibu tuhuma kama hii wakati ndugu Juma alipomtuhumu nayo Hamad bin Salama na tukasema kwamba:

Mtu akichanganyikiwa mwishoni wa umri wake hazirudishwi riwaya zake zote, bali huangaliwa ni kina nani waliopokea kutoka kwake, na wakati gani wamepokea ?

Je wamepokea kabla ya kuchanganyikiwa au ni baada, rejea ufafanuzi tulioutoa hapo nyuma.

Hivyo basi tunamtaka bwana Juma atuthibitishie kwamba Ismail bin Abi Khalid amepokea kutoka kwa Qais baada ya Qais kuharibikiwa na akili.

Na kama hana ushahidi juu ya hilo basi anyamaze awaache wenye kujua waseme.

Kwa ufupi ni kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa misingi ya elimu ya hadithi na wala haina shaka yoyote, na bila shaka ndugu yangu msomaji utakuwa umebainikiwa na hila za ndugu Juma juu ya kutaka kuzipotosha hadithi za Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam- kwa sababu ya madai yake yaliyo dhaifu tena ya uongo.

Rudi juu

JARIBIO LAKE JINGINE

 

Pia ndugu Juma alifanya jaribio jingine la kutaka kumdhoofisha mpokezi mwingine ambaye ameipokea hadithi hii kutoka kwa Ismail kutoka kwa Qais, naye ni JARIR BIN ABDUL-HAMID BIN QURT.

 

Amesema Juma:

Na mpokezi mwengine ambaye si madhubuti humu ni:

2) JARIRI BIN ABDILHUMAID BIN QART AL-RAZI naye japo kuwa wanavyuoni wengine wamemkubali lakini pia kuna tofauti juu yake.

Anasema Al-imamu Ibn Hajar Al-asqalaani kuwa ikiwa riwaya ya Al-shadhkun ni sahihi basi Jarir alikuwa akighushi.

Na amesema Al-imamu Ahmad bin Hanbal kuwa hakuwa mtu mwenye hifdhi nzuri .

Na akasema Al-bayhakii kuwa ilinasibishwa kwake kuwa alikuwa na hifadhi mbaya mwishoni mwa umri wake. Kwa hivyo hadithi hii ni dhaifu pia.

Mwisho wa kunukuu.

Tazama kitabu chake Hoja zenye nguvu ukurasa wa 255.

Rudi juu

MAJIBU YETU

 

Majibu yetu ni kwa njia mbili:

 

Njia ya kwanza: ameliandika jina la mwanachuoni huyu kimakosa, sawa sawa ni: ABDUL-HAMID BIN QURT na siyo ABDULHUMAID BIN QART.

Lengo letu hapa ni kumuweka sawa tu, na sio kutaka kumdhalilisha ndugu yetu Juma kwa kumtia makosa kama haya, kwa sababu nimeshindwa kumvumilia maana makosa ya aina hii yamekua mengi mno tena yanakaririka, hivyo nimeona ni vyema kumtanabahisha ili atanabahi, na pia wengine wasiingie kwenye makosa aina hii.

Na watu wengi wanaoingia katika makosa haya na mfano wake utawakuta ni wale ambao wamevivamia vitabu vya elimu bila ya kuichukua kutoka kwa maulamaa waliobobea katika fani hii, ndiyo ukamuona mtu analitaja la jina mtu vile anavyodhania y