KWA ELIMU
Imeandikwa
katika kitabu
kiitwacho 'Tuhufatul
Ahawazi kilichoandikwa
na mwanachuoni
maarufu AlMubarak
Furry - mlango wa 1804
"Yafuatayo
ni
maelezo yaliyoandikwa
na Ibnu Salah
katika utangulizi
wa hadithi
alizosimuliwa na Al
Zuhuriy kuwa
alimwambia;
"Nilikwenda
kwa Abdul
Malik bin Marawan (Khalifa
wa Waislam
wakati wa
utawala wa
Bani Umayyah)
akaniuliza;
'Unatokea
wapi ewe Al Zuhuriy?'
Nikamwambia;
'Natokea
Makkah'
Akaniuliza;
'Umemuacha
nani mwenye
kupendwa na
mwenye kufuatwa
huko Makkah?'
Nikamwambia;
"Ataa bin Abu
Rabah.'
Akaniuliza;
"Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
watumwa walioachwa
huru.'
Akaniuliza;
'Sababu
gani zilizomfanya
apendwe na
kufuatwa?'
Nikamwambia;
'Elimu
yake ya
dini na
riwaya.'
Akasema;
'Hakika
wenye elimu
ya dini
na
riwaya ndio wanaopaswa
kupendwa na
kufuatwa.'
Akaniuliza
tena;
'Nani
mwenye kupendwa
na
kufuatwa katika nchi
ya
Nikamwambia;
'Taus bin
Kiysan'.
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
watumwa walioachwa
huru.'
Akaniuliza;
'Sababu
gani zilizomfanywa
apendwe na
kufuatwa?'
Nikamwambia;
'Sababu
zile zile
zilizomfanya Ataa
apendwe na
kufuatwa.'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na kufuatwa
huko Misiri?'
Nikamwambia;
'Yazid bin Abu
Hubayb.'
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
watumwa walioachwa
huru.'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na mwenye
kufuatwa huko
Nikamwambia;
'Makahool.'
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
watumwa walioachwa
huru, alikumwa
mtumwa katika
Wanubi aliyeachwa
huru na
mwanamke wa
kabila la Hudhayl.'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na
kufuatwa katika Bara
ya Arabu (
Nikamwambia;
'Maymun bin
Maharan'
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
watumwa walioachwa
huru.'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na kufuatwa
huko Khurasan?'
Nikamwambia;
'Al Dhahaaq bin
Muzahim.'
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na
kufuatwa katika nchi
ya
Nikamwambia;
'Al Hassan
bin Abul
Hassan'.
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'
Akaniuliza;
'Nani
mwenye kupendwa
na
kufuatwa katika nchi
ya Al Koufa?'
Nikamwambia;
'Ibrahim Al
Nakhaiy'.
Akaniuliza;
'Ni katika
waarabu huyu au
katika watumwa
walioachwa huru?'
Nikamwambia;
'Ni katika
waarabu.'
Akanambia;
'Umenipumzisha
ewe Al Zuhriy!
wallahi
waliokuwa watumwa
watatamba na
kusikilizwa na
kuwashinda waarabu
mpaka utafika
wakati wao
watapanda juu
ya membari
na waarabu
watakuwa chini
Nikamwambia;
'Ewe Khalifa wa Waislamu! Hii
ni amri ya Mwenyezi Mungu.
Mwenye
kuihifadhi ndiye
atakayefuatwa na mwenye kuipoteza ataanguka.'