JIHAAD
|
Kuwaajibika |
||||
|
|
||||
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) amesema:
“Mtakapouziana
kwa riba, mkajishughulisha na biashara, mkaridhika na kilimo, na mkaiacha
jihadi (wakati wenzenu wanauliwa), Mwenyezi Mungu atakuteremshieni udhalilifu
mtakaoshindwa kuuondoa mpaka (pale) mtakaporudi katika dini yenu.”
Abu Daud na
Imam Ahmed
Na imetolewa
na Muslim na Abu Daud na An Nasaai na Al Haakim na Al Bayhaqiy kutoka kwa Abu
Hurairah (Radhiya Llahu anhu) pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayekufa
bila kupigana (jihadi) na wala (hata) kumpitikia moyoni mwake (nia ya kupigana)
jihadi, (akifa) anakufa akiwa na sehemu ya unafiki.”
Waislamu ni umma uliochaguliwa na Mwenyezi
Mungu kwa ajili ya kuuongoza ulimwengu na walimwengu na kulinyanyua juu neno la
Mwenyezi Mungu, lakini Waislamu leo wamekuwa watu dhalili kupita umma zote
zinazotembea juu ya ardhi. Kila anayetaka kuzifanyia silaha zake majaribio au
kujipima nguvu, anazielekeza silaha hizo na nguvu hizo kwa Waislamu. Tumeyaona
hayo yakitokea sehemu mbali mbali ulimwenguni, zikiwemo Bosnia, India,
Afghanistan, Palastina na sasa Iraq, na hivi sasa Ghaza.
Kote huko na katika sehemu mbali mbali ulimwenguni Waislamu wanadhalilishwa,
wanauliwa, watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume, na majumba yao yanabomolewa
mbele ya kamera za television na mbele ya macho ya kila mtu, bila watu kujali
wala hata nyoyo kusituka. Kisha Waislamu hao hao eti wanakimbilia kupeleka
mashitaka yao Umoja wa Mataifa wakitegemea kupata msaada, wakati wote hao
(Marekani, Mayahudi na Umoja wa Mataifa) ni kitu kimoja.
Na hii
inanikumbusha kile kisa cha chui na kima:
Inasemekana kuwa
chui alikuwa akipenda kumuonea kima na kumpiga bila sababu yoyote, na kila
anapomuona alikuwa akitafuta kisingizio chochote cha kumpiga makofi ya uso kima
yule.
Alikuwa mara
nyingine akimwambia; “Kofia yako iko wapi! Mbona
leo hujavaa kofia, si nilikwambia lazima uivae? Kesho lazima nikuone nayo,”
humwambia hivyo huku akimtandika makofi na mateke.
Siku ya pili
kima anapokuja akiwa amevaa kofia, chui yule yule humvamia na humpiga makofi
huku akimwambia:
“Kwa
nini umevaa kofia! Si nilikwambia usiivae?”
akiivaa anapigwa na asipoivaa anapigwa.
Hali
ikaendelea hivyo mpaka siku ile kima alipochoka kuonewa, akaamua kumshitaki
chui kwa mfalme simba bila kujuwa masikini kuwa simba na chui wote ni kitu
kimoja.
Mfalme simba
akamwita chui pembeni na kumwambia kwa kumnong'oneza:
“Wewe vipi ndugu
yangu! unampiga mwenzio bila kumtafutia kisingizio kinachokubalika? Tizama mimi
kwa mfano; ninapotaka kumpiga punda nafanya nini? Humtuma aniletee matufaha, na
yeye bila kuniuliza hukimbia na kuniletea matufaha mekundu, mimi hapo humtandika
makofi na kumwambia:
“Nani
aliyekuaambia uniletee matufaha mekundu?”
Hapo yeye
hukimbia na kurudi haraka akiwa ameniletea matufaha ya kijani, na hapo namtandika
tena makofi na kumwambia:
“Nani
aliyekwambia uniletee matufaha ya kijani?”
na kwa njia hii namtandika makofi kwa raha zangu.”
Chui akaona
kuwa hii ni fikra nzuri, akaondoka na kwenda moja kwa moja mpaka kwa kima
akamwambia:
“Nenda
kaniletee matufaha sasa hivi, tena mbiyo!”
Lakini kima
anakhitalifiana na punda, kima alimuuliza chui:
“Unata
nikuletee matufaha rangi gani? Mekundu au kijani au manjano?
Chui kuona
ameshindwa hila akarudia pale pale:
“Mbona
leo hujavaa kofia eh?”, Ngumi!
Teke!
Na
hii ndiyo hali yetu Waislamu baada ya kuyaacha mafundisho ya dini yetu, na
kuiacha jihadi na kuyakimbilia maisha ya dunia, Mwenyezi Mungu ametusalitishia
udhalili ikawa kila safihi anapotaka kujipima nguvu zake anakuja kututandika
sisi ngumi na makofi yake, na sisi tunakimbilia kwa mfalme Simba (Mmarekani) au
kwa chui (Umoja wa Mataifa) na kumbe wote hao ni kitu kimoja waliokwishaamua
kumpiga vita kila anayetaka kuisimamisha bendera ya Laa ilaaha illa Llah.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusimamishie kiongozi wa kheri, awe katika utawala
wake kiongozi huyo anaheshimiwa kila mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu, na
anadhalilishwa kila mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu. Awaunganishe umma chini ya
bendera ya Laa ilaaha illa Llah na kuihuisha Jihadi ambayo kwayo pekee umma huu
utarudisha heshima yake - Amin.
Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
"Hivi
karibuni mtakuja zungukwa na mataifa, mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula
chao (wanavyokaa kuizunga sinia ya chakula)." Tukasema: "Kwa sababu
ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu siku hiyo?" Akasema: "Hapana,
nyinyi siku hiyo mtakuwa wengi, lakini mtakuwa (mumegawanyika) muko mbali mbali
mfano wa takataka zinazokumbwa na maji ya mvua. Mwenyezi Mungu ataondoa haiba
yenu kutoka katika vifua vya adui yenu, na ataingiza ndani ya nyoyo zenu Al
Wahan (udhaifu)." Mmoja akauliza: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,
ni kitu gani hiki Al Wahan?" Akasema: "Kuipenda kwenu dunia na
kuyachukia mauti."
Imam Ahmed
katika Musnad yake
Hadithi hii
ni muujiza katika miujiza ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) juu ya hali yetu hivi sasa. Kama kwamba alipokuwa amekaa pale msikitini
kwake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akihadithia hadithi hii, alikuwa akiiona
hali yetu hivi sasa kama tulivyo.
Maadui wa
Waislamu wanatutuhumu kuwa tunaongezeka kwa wingi, na wanazihadaa serikali zetu
zikubali kutupa dawa za kuzuwia uzazi. Hii ina maana kuwa idadi yetu
inaongezeka, lakini juu ya wingi wetu, hatuna maana yoyote. Hatuna faida
yoyote. Maadui wa Mwenyezi Mungu wanatuuwa, wanatudhalilisha, wanatutenganisha,
wanatugawa, wanatugombanisha, na sisi hatuna la kufanya, bali hatuwezi kufanya kitu.
Wanatusukuma wanapotaka, na wanatuendesha wanavyotaka. Tumekuwa mfano wa
takataka zinazokumbwa na kusukumwa na maji ya mvua huku na kule.
Na muujiza
mwingine uliomo ndani ya hadithi hii ni kule kuungana dhidi yetu kwa mataifa
yote. Wamarekani, wazungu wa Ulaya, Mayahudi, Wajapani na maadui wa Mwenyezi
Mungu walioko Magharibi na Mashariki ya ulimwengu, wote wamejikusanya na
kutuzunguka, mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao. Wote wamekula kiapo
kuupiga vita Uislamu. Wakati huo huo sisi tumo katika starehe zetu, kama kwamba
hapana kinachotokea. Kila mmoja anakiogopea kiti chake, anaiogopea mali yake,
anauogopea mustakbali wake, anaiogopea nafsi yake. Tunaipenda
dunia na tunayachukia mauti.
Tunafaidika
na hadithi hii pia ile balagha, ule ubingwa wa kutumia lugha uliotumika katika
kuwaelezea maadui wa Mwenyezi Mungu, pale (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema:
"mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao."
Na hii inatuonyesha njaa waliyonayo maadui hawa, na tamaa yao kubwa juu
ya mali za Waislamu na utajiri wao. Wanakuja kwa nguvu zao zote na kwa
ujabaruti na ujeuri mkubwa na kibri huku wakiwasaidia Mayahudi kwa nguvu zao
zote ili waweze kuzinyakua mali hizo na uchumi huo na ardhi.
Na muujiza
mwingine ni kule kufanya kwao wanavyotaka bila kujali masikitiko yetu wala
huzuni zetu wala lawama zetu wala hata vilio vyetu. Wanafanya
wanavyotaka. Wanapiga wanavyotaka, wanabomoa
wanavyotaka, kama kwamba ardhi yote na Waislamu wote ni milki yao. "Mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao."
Hata Masahaba
(Radhiya Llahu anhum) walishangazwa waliposkia, wakauliza:
"Kwa
sababu ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu siku hiyo?" Walishanga. Vipi tutakuwa katika hali hii, vipi maadui
wataweza kutupiga wakati idadi yetu ni kubwa kupita yao. Bila shaka tutakuwa
wachache wakati huo. Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akawaambia: "Hapana, (bali) nyinyi
siku hiyo mtakuwa wengi, lakini mtakuwa mumefarakana mfano wa takataka
zinazokumbwa na maji ya mvua."
Izingatie
vizuri kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
aliposema "nyinyi siku hiyo mtakuwa
wengi", na hii maana yake ni kuwa mwili wa Waislamu ni mwili mmoja.
Tokea wakati ule mpaka wakati huu, sisi sote ni kitu kimoja.
"ãËá ÇáãÄãäíä Ýí
ÊæÇÏåã æÊÑÇÍãåã ßãËá ÇáÌÓÏ ÇáæÇÍÏ ÅÐÇ ÇÔÊßì ãäå ÚÖæ ÊÏÇÚì áå ÓÇÆÑ ÇáÌÓÏ ÈÇáÍãì
æÇáÓåÑ"
Mfano
wa Waislamu katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao ni mfano wa mwili mmoja,
kinapoumia kiungo kimoja basi viungo vyote vilivyobaki vinashirikiana (nacho
kiungo hicho) kwa homa na kukesha.
Bukhari na
Muslim
Hivi ndivyo
alivyotufundisha Mtume wetu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
Na katika
hadithi hii ya kuzungukwa na maaduwi tunaweza kuujuwa ugonjwa wetu na pia kuijuwa
dawa yetu.
Maradhi yetu
ni kuwa mbali na Mwenyezi Mungu, mfarakano wetu, na kuipenda kwetu dunia.
Na dawa yetu ni
kurudi kwa Mola wetu Subhanahu wa Taala. Turudi katika dini yetu. Tuirudishe imani
yetu na kumtegemea Mwenyezi Mungu peke Yake. Tumuogope Yeye tu, na tuache kuuogopa
uluwa na mali na ufalme na vitu kama hivi visivyo na thamani yoyote mbele ya
Mwenyezi Mungu. Tuache kuuthamini ulimwengu na kuyaogopa mauti.
Tuwalee
watoto wetu malezi ya Kiislamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na ya Mtume Wake
(Swalla Llahu alayhi wa sallam). Tuwafundishe taariykh yetu.
Kurudi kwa
Mwenyezi Mungu na kurudi katika mafundisho ya dini Yake ndiyo jambo la pekee
linaloweza kuturudishia heshima yetu na utukufu wetu.
Neno Jihadi, asili yake linatokana na juhudi, tabu, mashaka. Kwa mfano
tunasema; ‘Amejitahidi’, ‘amefanya juhudi’, yaani amezitumia nguvu zake na
uwezo wake wote katika kutimiza jambo fulani, na haya yote yanapatikana katika
mapambano ya kivita.
Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa watu
wote, akamuamrisha kuwalingania katika uongofu na katika dini ya haki, na
wakati wote alipokuwa Makka alikuwa akiwalingania watu kwa hekima na kwa
mawaidha mema, na kwa ajili hiyo ilibidi apambane na kila aina ya uadui, udhia
na mateso kutoka kwa watu wa kabila lake baada ya kuuona utukufu na uluwa wao
umo hatarini.
Wakati wote huo Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala alimtaka awe akipambana na
uadui huo kwa subira, uvumilivu na kwa kusamehe msamaha mzuri.
Mwenyezi
Mungu anasema:
ÝóÇÕúÝóÍö
ÇáÕøóÝúÍó ÇáúÌóãöíáó
“Basi
msamehe msamaha mzuri (kila anayekufanyia ubaya).”
Al Hijr – 85
Na akasema:
æóÇÕúÈöÑú
áöÍõßúãö ÑóÈøößó ÝóÅöäøóßó ÈöÃóÚúíõäöäóÇ
“Na
ungoje hukumu ya Mola wako, na hakika wewe uko mbele ya macho Yetu.”
At Tur – 48
Na akasema:
ÝóÇÕúÝóÍú
Úóäúåõãú æóÞõáú ÓóáÇãñ
“Basi
wasamehe wewe na uwambie (maneno ya) salama.”
Az Zukhruf –
89
Na akasema:
Þõá áøöáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ íóÛúÝöÑõæÇ áöáøóÐöíäó áÇ íóÑúÌõæä
ÃóíøóÇãó Çááøóåö
“Waambie
wale walioamini wawasamehe wale wasioziogopa siku za Mwenyezi Mungu (za kuwatia
adabu wabaya).”
Al Jathiyah - 14
Mwenyezi Mungu hakumtaka Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aukabili
ubaya wao kwa ubaya, wala udhia kwa udhia na wala hakumuamrisha kuwapiga vita
wanaoipiga vita daawa hiyo, au kuwapiga vita wale wanaowatesa Waislamu, bali
alikuwa akimwambia Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
ÇÏúÝóÚú
ÈöÇáøóÊöí åöíó ÃóÍúÓóäõ ÇáÓøóíøöÆóÉó äóÍúäõ ÃóÚúáóãõ ÈöãóÇ íóÕöÝõæäó
“Ondosha mabaya (unayofanyiwa) kwa (kulipa)
mema; Sisi tunajua wanayoyasema.”
Al Muminun –
96
Muda wote huo
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala alimuamrisha Mtume wake (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) apigane jihadi kwa Qurani na kwa hoja zilizo wazi.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
æóÌóÇåöÏúåõã
Èöåö ÌöåóÇÏðÇ ßóÈöíÑðÇ
“Na ushindane nao kwa (Qurani) hii mashindano
makubwa.”
Al Furqan –
52
Lakini baada ya kupita miaka kumi na tatu huku mateso yakiongezeka, na makafiri
kuzidisha uonevu na kuwadhalilisha Waislamu, na hatimaye kufanya njama za
kumuuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hata
akalazimika kuhamia Madina na kuwaamrisha Masahaba wake (Radhiya Llahu anhu) pia
kuhamia huko, hapo ndipo Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Alipoteremsha kauli
Yake isemayo:
æóÅöÐú
íóãúßõÑõ Èößó ÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú áöíõËúÈöÊõæßó Ãóæú íóÞúÊõáõæßó Ãóæú
íõÎúÑöÌõæßó æóíóãúßõÑõæäó æóíóãúßõÑõ Çááøåõ æóÇááøåõ ÎóíúÑõ ÇáúãóÇßöÑöíäó
“Na
(kumbuka ewe Muhammad) walipokufanyia hila wale waliokufuru ili wakufunge au
wakuue au wakutoe, na wakafanya hila (zao barabara) Na Mwenyezi Mungu
akazipindua hila hizo. Na Mwenyezi Mungu ni mbora wa kupindua hila (za watu
wabaya).”
Al Anfal – 30
Kisha Akasema:
ÅöáÇøó
ÊóäÕõÑõæåõ ÝóÞóÏú äóÕóÑóåõ Çááøåõ
“Kama
hamtomnusuru (Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), basi
Mwenyezi Mungu alimnusuru.”
At Tawba – 40
Baada ya kuhamia Madina, makao makuu ya dola mpya ya Kiislamu, na baada ya
makafiri kuwaendea huko huko na kuwafanyia mbinu na hila mbali mbali, ndipo
Mwenyezi Mungu aliipotoa amri ya kupigana Aliposema:
ÃõÐöäó
áöáøóÐöíäó íõÞóÇÊóáõæäó ÈöÃóäøóåõãú ÙõáöãõæÇ æóÅöäøó Çááøóåó Úóáóì äóÕúÑöåöãú
áóÞóÏöíÑñ 39 ÇáøóÐöíäó ÃõÎúÑöÌõæÇ ãöä ÏöíóÇÑöåöãú ÈöÛóíúÑö ÍóÞøò ÇáÇ Ãóä
íóÞõæáõæÇ ÑóÈøõäóÇ Çááøóåõ æóáóæúáÇ ÏóÝúÚõ Çááøóåö ÇáäøóÇÓó ÈóÚúÖóåõã ÈöÈóÚúÖò
áøóåõÏøöãóÊú ÕóæóÇãöÚõ æóÈöíóÚñ æóÕóáóæóÇÊñ æóãóÓóÇÌöÏõ íõÐúßóÑõ ÝöíåóÇ ÇÓúãõ
Çááøóåö ßóËöíÑðÇ æóáóíóäÕõÑóäøó Çááøóåõ ãóä íóäÕõÑõåõ Åöäøó Çááøóåó áóÞóæöíøñ
ÚóÒöíÒñ 40 ÇáøóÐöíäó Åöä ãøóßøóäøóÇåõãú Ýöí ÇáÃóÑúÖö ÃóÞóÇãõæÇ ÇáÕøóáÇÉó
æóÂÊóæõÇ ÇáÒøóßóÇÉó æóÃóãóÑõæÇ ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóäóåóæúÇ Úóäö ÇáúãõäßóÑö
æóáöáøóåö ÚóÇÞöÈóÉõ ÇáúÃõãõæÑö 41
“Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa
sababu wamedhulumiwa. Na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.
Ambao wametolewa majumbani (mijini) mwao
pasipo haki ila kwa sababu wanasema “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu.”
Na kama Mwenyezi Mungu asingaliwakinga watu,
baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangalivunjwa mahekalu na makanisa na nyumba
nyengine za ibada na misikiti ambamo jina la Mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi.
Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia dini yake. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda.
Wale ambao tukiwamakinisha (tukiwaweka uzuri)
katika ardhi husimamisha Sala na wakatoa Zaka na wakaamrisha yaliyo mema na
wakakataza yaliyo mabaya. Na marejeo ya mambo ni kwa Mwenyezi Mungu.”
Al Hajj 39 –
41
Katika aya
hizi zimetajwa sababu tatu ambazo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu ametoa ruhusa
ya kupigana vita:-
Ya kwanza - Kwa sababu ya kudhulumiwa
kwa kushambuliwa na kutolewa majumbani mwao pasipo haki kwa sababu wanasema
“Mola wetu ni Mwenyezi Mungu”.
Ya pili – Lau kama Mwenyezi Mungu asingaliwakinga kwa kuwaamrisha kupigana
jihadi, bila shaka yangalivunjwa mahekalu na makanisa na nyumba nyengine za
ibada na misikiti ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi.
Ya tatu – Sababu ya Waislamu kupewa nusura ya Mwenyezi Mungu na kumakinishwa
(kuwekwa uzuri) katika ardhi ni kwa ajili ya Kusimamisha Swala na Kutoa Zaka na
Kuamrisha mema na Kukataza mabaya.
Jihadi imefaridhishwa katika mwaka wa pili wa Hijra aliposema Mwenyezi Mungu:
ßõÊöÈó
Úóáóíúßõãõ ÇáúÞöÊóÇáõ æóåõæó ßõÑúåñ áøóßõãú æóÚóÓóì Ãóä ÊóßúÑóåõæÇú ÔóíúÆðÇ
æóåõæó ÎóíúÑñ áøóßõãú æóÚóÓóì Ãóä ÊõÍöÈøõæÇú ÔóíúÆðÇ æóåõæó ÔóÑøñ áøóßõãú
æóÇááøåõ íóÚúáóãõ æóÃóäÊõãú áÇó ÊóÚúáóãõæäó
“Mumelazimishwa kupigana vita (kwa ajili ya
dini). Nalo ni jambo zito kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri
kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu ndiye
anayejua, (lakini) nyinyi hamjui.”
Al Baqarah –
216
Kupigana
Jihadi ni Fardhi Kifaya na wakati mwingine inakuwa Fardhi Aiyn.
‘Fardhi aiyn’ ni yale ambayo kila Muislamu analazimika kuwa nayo au kuyatenda,
na hasameheki asiyetenda hata kama kundi la watu wengine watalisimamia jambo
hilo na kulikamilisha, kwa mfano; Imani, SWala, Tohara, Kutoa Zaka, Kufunga,
Kuhiji nk. Haya yanaitwa Fardhi aiyn na kila Muislamu analazimika kuwa nayo au
kuyatenda na si halali kwa mtu yeyote kutoyapa umuhimu.
Maana ya
Fardhi Kifaya
Ama ‘Fardhi kifaya’ ni yale
matendo ambayo Waislamu wanalazimika kuyatenda ingawaje si lazima litendwe na
Waisalmu wote, kwani linapotendwa na kundi miongoni mwao, basi waliobaki
wanasameheka, kwa mfano;
KATIKA DINI;
Kujifunza
elimu ya dini kwa ajili ya kuwasomesha wengine, Kumswalia maiti, Kuadhini nk.
KATIKA
MAISHA;
Kulima, Utabibu,
Ufundi na yaliyo na mfano wake, mambo ambayo yakikosekana, maisha ya wanadamu yanakuwa
hatarini.
Kama vile kuamrisha mema, kukataza mabaya, Kuitisha Jihadi, na Kuyapiga vita
maovu na yale yaliyoharamishwa nk.
Jihadi inaingia katika Fardhi kifaya ambayo haimwajibikii kila mtu iwapo
litatokea kundi la watu miongoni mwao litakaloweza kuwapiga vita maadui na
kuiondoa shari yao bila kuhitajia msaada wa waliobaki.
Katika kutafuta elimu, Mwenyezi Mungu Anasema:
æóãóÇ
ßóÇäó ÇáúãõÄúãöäõæäó áöíóäÝöÑõæÇú ßóÂÝøóÉð ÝóáóæúáÇó äóÝóÑó ãöä ßõáøö ÝöÑúÞóÉò
ãøöäúåõãú ØóÂÆöÝóÉñ áøöíóÊóÝóÞøóåõæÇú Ýöí ÇáÏøöíäö æóáöíõäÐöÑõæÇú Þóæúãóåõãú
ÅöÐóÇ ÑóÌóÚõæÇú Åöáóíúåöãú áóÚóáøóåõãú íóÍúÐóÑõæä
“Wala haiwapasi Waislamu kutoka wote
(katika miji yao wakaja Madina wakaiwacha miji yao mitupi). Lakini kwa nini
halitoki kundi (tu) katika kila taifa miongoni mwao (lende Madina kwa Mtume)
kujitalimisha vyema dini na (kisha wakaja) kuwaonya weziwao (waliosalia makwao)
watakapowarudia, ili wapate kujihadharisha (na wao na mabaya).”
At Tawba –
122
Ama kuhusu
Jihadi, Mwenyezi Mungu Anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÎõÐõæÇú ÍöÐúÑóßõãú ÝóÇäÝöÑõæÇú ËõÈóÇÊò Ãóæö
ÇäÝöÑõæÇú ÌóãöíÚðÇ
“Enyi Mlioamini! Shikeni hadhari yenu (juu
ya maadui zenu msikhadaike). Tokeni (kwenda vitani) makundi moja moja au tokeni
nyote pamoja (kama atakavyokuambieni Mtume).”
An Nisaa – 71
Na Akasema:
áÇøó
íóÓúÊóæöí ÇáúÞóÇÚöÏõæäó ãöäó ÇáúãõÄúãöäöíäó ÛóíúÑõ Ãõæúáöí ÇáÖøóÑóÑö
æóÇáúãõÌóÇåöÏõæäó Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÈöÃóãúæóÇáöåöãú æóÃóäÝõÓöåöãú ÝóÖøóáó
Çááøåõ ÇáúãõÌóÇåöÏöíäó ÈöÃóãúæóÇáöåöãú æóÃóäÝõÓöåöãú Úóáóì ÇáúÞóÇÚöÏöíäó
ÏóÑóÌóÉð æóßõÜáÇøð æóÚóÏó Çááøåõ ÇáúÍõÓúäóì æóÝóÖøóáó Çááøåõ ÇáúãõÌóÇåöÏöíäó
Úóáóì ÇáúÞóÇÚöÏöíäó ÃóÌúÑðÇ ÚóÙöíãðÇ
“Hawawi sawa Waislamu wanaokaa wasende
vitani, isipokuwa wenye dharura. (Hawawi sawa) na wale wapiganao katika njia ya
Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewafadhilisha
katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa
nafsi zao kuliko wakaao (wasende kupigana). Ingawa Mwenyezi Mungu ameahidi wote
(kupata) wema. Lakini Mwenyezi Mungu amewafadhilisha – wale wapiganao kuliko
wakaao – kwa ujira mkuu.”
An Nisaa – 95
Na katika Sahihi Muslim kutoka kwa Abu Said Al Khudary (Radhiya Llahu anhu)
amesema kuwa; Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alituma
ujumbe kwenda kwa watu wa kabila la Hudhayl kuwaambia; “Atoke (kwenda vitani)
katika kila wawili mtu mmoja na ujira watapata wote wawili.”
Sahih Muslim Kitab al Imara – mlango
wa Fadhail ianat al ghazi fiy sabili Llah – hadithi nambari 38
Na hii ni kwa
sababu ikimwajibikia kila mtu, basi mambo mengi ya kidunia yenye maslahi kwa
wanadamu yataharibika, ndiyo maana ikawajibika kwa baadhi yao tu.
Jihadi inakuwa Fardhi aiyn katika sehemu tatu;
Ya kwanza –
ni pale mwenye kuwajibika kupigana anapokuwa vitani keshasimama katika msitari
pamoja na wenzake, hapo analazimika kupigana.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÅöÐóÇ áóÞöíÊõãú ÝöÆóÉð ÝóÇËúÈõÊõæÇú
“Enyi mlioamini!
Mkutanapo na jeshi (la makafiri) kazaneni barabara (wala msikimbie).”
Al Anfal – 45
Na öAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÅöÐóÇ áóÞöíÊõãõ ÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú ÒóÍúÝÇð ÝóáÇó
Êõæóáøõæåõãõ ÇáÃóÏúÈóÇÑó
Enyi
Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo.”
Al Anfal - 15
Ya pili –
Adui anapoingia katika nchi ya Kiislamu, wanalazimika watu wote wa nchi hiyo
kwa pamoja kutoka na kupambana naye, na si halali kwa mtu yeyote kurudi nyuma
asitimize wajibu wake huo wa kupigana na adui, na hii ikiwa haiwezekani kumtoa
adui huyo bila kushirikiana wote kwa pamoja.
Mwenyezi
Mungu Anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÞóÇÊöáõæÇú ÇáøóÐöíäó íóáõæäóßõã ãøöäó ÇáúßõÝøóÇÑö
æóáöíóÌöÏõæÇú Ýöíßõãú ÛöáúÙóÉð æóÇÚúáóãõæÇú Ãóäøó Çááøåó ãóÚó ÇáúãõÊøóÞöíäó
“Enyi
mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu (kwanza kwani ndio wenye
madhara na nyinyi zaidi), na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi
Mungu yu pamoja na wacha- Mungu.”
Al Tawba –
123
Ya tatu –
Mwenye kuhukumu anapotangaza Jihadi analazimika kila mwenye kuwajibika kupigana
kuuitikia mwito huo, na haya yanatokana na hadithi iliyosimuliwa na Ibni Abbas (Radhiya
Llahu anhu) aliposema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) amesema:
áÇ åÌÑÉ
ÈÚÏ ÇáÝÊÍ æáßä ÌåÇÏ æäíÉ æÅÐÇ ÇÓÊäÝÑÊã ÝÇäÝÑæÇ
“Hapana kuhajir tena (kutoka Makka kwenda
Madina) baada ya Waislamu kuuteka (mji wa Makka) isipokuwa (kilichokuwepo ni)
jihadi na nia (ya kupigana jihadi), na mnapoitwa muitikie (mwito).”
Sahih Bukhari – juzu ya 2 mlango wa
‘Fadhila za jihadi.’ Hadithi nambari 2631
Na maana yake
ni kuwa mnapotakiwa kwenda kupigana Jihadi, basi lazima muitikie mwito huo.
Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taala ööööAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ãóÇ áóßõãú ÅöÐóÇ Þöíáó áóßõãõ ÇäÝöÑõæÇú Ýöí ÓóÈöíáö
Çááøåö ÇËøóÇÞóáúÊõãú Åöáóì ÇáÃóÑúÖö ÃóÑóÖöíÊõã ÈöÇáúÍóíóÇÉö ÇáÏøõäúíóÇ ãöäó
ÇáÂÎöÑóÉö ÝóãóÇ ãóÊóÇÚõ ÇáúÍóíóÇÉö ÇáÏøõäúíóÇ Ýöí ÇáÂÎöÑóÉö ÅöáÇøó Þóáöíáñ
“Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa
“Nendeni (kupigana) kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu” mnajitia uzito katika
ardhi? Je, mumekuwa radhi na maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe
za maisha ya dunia kwa (mkabala wa maisha ya) Akhera ni kidogo tu.”
At Tawba – 38
Anawajibika kupigana jihadi kila Muislamu mwanamume, mwenye akili timamu,
aliyekwishabaleghe, mwenye afya njema mwenye uwezo wa kuwaachia watu wake kiasi
cha mali inayowatosha mpaka pale atakaporudi.
Kwa hivyo
haimwajibikii asiyekuwa Muislamu, mwanamke, mtoto mdogo, mwenda wazimu na
mgonjwa, na kwa ajili hiyo hana lawama yeyote katika hawa asipoutikia mwito wa
jihadi kutokana na udhaifu wao au umasikini wao au umri wao au kutokuwa na
akili zao ambao huenda kuwepo kwao katika uwanja wa mapambano kukasababisha
madhara zaidi kuliko manufaa.
Mwenyezi
Mungu Subahanahu wa Taala Anasema:
áøóíúÓó
Úóáóì ÇáÖøõÚóÝóÇÁ æóáÇó Úóáóì ÇáúãóÑúÖóì æóáÇó Úóáóì ÇáøóÐöíäó áÇó íóÌöÏõæäó
ãóÇ íõäÝöÞõæäó ÍóÑóÌñ ÅöÐóÇ äóÕóÍõæÇú áöáøåö æóÑóÓõæáöåö ãóÇ Úóáóì
ÇáúãõÍúÓöäöíäó ãöä ÓóÈöíáò æóÇááøåõ ÛóÝõæÑñ ÑøóÍöíãñ
“Hapana
lawama kwa wanyonge, wagonjwa, na wasio pata cha kutumia, maadamu wanamsafia
nia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.”
At Tawba - 91
Na Anasema:
áóíúÓó
Úóáóì ÇáÃÚúãóì ÍóÑóÌñ æáÇ Úóáóì ÇáÃóÚúÑóÌö ÍóÑóÌñ æóáÇ Úóáóì ÇáúãóÑöíÖö ÍóÑóÌñ
“Kipofu hana lawama, wala kiguru hana
lawama, wala mgonjwa hana lawama.”
Al Fat-h 17
Na kutoka kwa
Abdullah bin Omar (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:
“Nilipelekwa
kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) siku ya Uhud
(aniruhusu nikapigane) na wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi na nne
lakini hakuniruhusu.”
Sahih Muslim – kitabu cha ‘Imara’
mlango unaobainisha kubaleghe – hadithi nambari 1868
Na hii ni kwa
sababu jihadi ni ibada na haimwajibikii isipokuwa aliyebaleghe.
Imeelezwa na
Maimam Ahmed na Bukhari kutoka kwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kuwa
amesema:
“Nilisema
(Nilimuuliza) - ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; wanawake wanawajibika kupigana
jihadi?” akanijibu: “Jihadi (yao ni ile) isiyokuwa na kuuana ndani yake - Hija na Umra.”
Musnad ya Imam Ahmed
juz. 6 – Hadithi za Bibi Aisha (Radhiya Llahu anhu)
Fathul Bari – Sharhi
ya Sahih Bukhari Juz. 4 mlango wa Hija ya wanawake.
Na katika
riwaya nyingine kuwa alisema:
“Lakini
jihadi iliyo bora ni Hija iliyokubaliwa.”
Imesimuliwa
na Al Waahidi na Al Sayutiy katika ‘Al Dur al Manthur’ kuwa Mujahid amesema;
“Ummu Salamah (Radhiya Llahu anha) alisema; “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam), (kwa nini) wanaume (tu) wanateka miji (wanapigana
jihadi) na sisi hatuteki na sisi tunapata nusu ya urithi (tu)?”
Mwenyezi
Mungu akateremsha kauli Yake:
æóáÇó
ÊóÊóãóäøóæúÇú ãóÇ ÝóÖøóáó Çááøåõ Èöåö ÈóÚúÖóßõãú Úóáóì ÈóÚúÖò áøöáÑøöÌóÇáö
äóÕöíÈñ ãøöãøóÇ ÇßúÊóÓóÈõæÇú æóáöáäøöÓóÇÁ äóÕöíÈñ ãøöãøóÇ ÇßúÊóÓóÈúäó
æóÇÓúÃóáõæÇú Çááøåó ãöä ÝóÖúáöåö Åöäøó Çááøåó ßóÇäó Èößõáøö ÔóíúÁò ÚóáöíãðÇ
“Wala
msitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume
wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma.
Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila
kitu.”
An Nisaa – 32
Imepokelewa
pia kutoka kwa Ikrimah (Radhiya Llahu anhu) kuwa alisema:
"Wanawake
waliuliza juu ya jihadi wakasema: “Tunatamani lau Mwenyezi Mungu angejaalia na
sisi pia tuwe tunapigana jihadi ili tupate cho chote katika ujira (mwema) kama
wanavyopata wanaume.” Ndipo Mwenyezi Mungu alipoiteremsha aya hiyo.
Hata hivyo
hapana ubaya ikiwa wanawake watatoka kwa ajili ya kuwatibia walioumia au kwa
ajili ya shughuli za mfano wake.
Kutoka kwa
Anas (Radhiya Llahu anhu) amesema; “Siku ya (vita vya) Uhud Waislamu walishindwa wakiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam), nilimuona (siku hiyo Bibi) Aisha binti Abubakar na
Ummu Suleyum wakiwa wamekunja mikono ya kanzu zao nikiviona visigino vya miguu
yao (huku wakiwa wanakwenda mbio) huku (na kule) wakibeba viriba vya maji
migongoni mwao na kuwanywesha watu, kisha wanarudi na kuvijaza tena kisha
wanarudi kuwanywesha watu (tena).”
Muslim juz. 3 Mlango wa ‘Kupigana
jihadi wanawake pamoja na wanaume.’ Hadithi nambari 1811
Kutoka kwa
Anas pia anasema;
“Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akipigana vita akiwa
pamoja na Ummu Suleyum na wanawake wengine katika watu wa Madina, waliokuwa
wakiwanywesha watu maji na kuwatibia majeruhi.”
Muslim juz.3
Mlango wa ‘Kupigana jihadi wanawake pamoja na wanaume.’ Hadithi nambari 1810
Abu Daud juz.
3 mlango wa ‘Wanawake wanapigana vita’. Hadithi nambari 2529
Attirmidhiy
juz. 3 mlango wa ‘Wanawake kwenda vitani’ hadithi nambari 1623
Jihadi
iliyowajibika haihitajii ruhusa ya wazee, ama jihadi ya kujitolea lazima
ipatikane ruhusa ya wazee wawili au ya mmoja wao.
Amesema Ibni
Masaud (Radhiya Llahu anhu):
“Nilimuuliza
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam); ‘Amali (ibada) ipi
inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu?
Akasema:
“Swala
katika wakati wake”.
Nikamuuliza
(tena):
“Kisha
ipi?”
Akaniambia:
“Kuwatii
wazee wawili.”
Nikamuuliza
(tena):
“Kisha
ipi?”
Akaniambia:
“Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Sahih Bukhari
juz.1 Kitabu cha ‘Nyakati za Sala’, mlango wa ‘Fadhila za kusali katika wakati
wake’, hadithi nambari 504
Sahih Muslim
– juz. 1 Kitabu cha ‘Imani’, mlango wa ‘Imani juu ya Mwenyezi Mungu ndiyo amali
bora kupita zote’, hadithi nambari 85
Na Ibni Omar (Radhiya
Llahu anhu) amesema:
“Alikuja
mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kumuomba
amruhusu kwenda kupigana jihadi, akamuuliza; ‘Wazee wako wahai?’ Akasema;
‘Ndiyo’, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:
‘Basi jihadi yako iwe katika (kuwahudumia) wao’.
Abu Daud na
Annasai na Attirmidhy aliyeisahihisha.
Na katika
kitabu kiitwacho ‘Shar-atul Islam’, (imeandikwa):
‘Na
haijuzu kwenda kupigana jihadi isipokuwa yule tu asiyekuwa na matatizo ya
kuwahudumia wanawe na wazee wake, kwa sababu hayo ni bora kuliko kupigana
jihadi, bali ndiyo jihadi iliyo bora.’
(Bila shaka
hii ni katika jihadi isiyowajibika, ama katika jihad ya ‘fardh aiyn’ yaani
jihadi iliyowajibika, basi hapana haja ya kuomba ruhusa kwa mtu yeyote kama
ilivyotangulia kuelezwa).
Haruhusiwi kwa
anayedaiwa kwenda katika jihadi isiyowajibika isipokuwa baada ya kumuomba
ruhusa mwenye kumdai au aweke rahani mali inayotosheleza kulipa deni hilo au
aweke mdhamini, kwa sababu katika hadithi ya Abu Qatadah (Radhiya Llahu anhu)
iliyomo ndani ya kitabu cha Imam Ahmed na pia katika Sahih Muslim (aliulizwa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)): ‘Unaonaje
nikiuliwa katika (jihadi) katika njia ya Mwenyezi Mungu, nitasamehewa madhambi
yangu yote?’
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:
“Ndiyo
(utasamehewa) ikiwa utauliwa ukiwa katika subira huku ukitegemea ujira mwema
(kutoka kwa Mwenyezi Mungu), isipokuwa (kama una) deni, hakika Jibril ameniambia
hayo (hivi punde).”
Ahmed na
Muslim
Kutoka kwa
Abdullah bin Omar (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenyezi
Mungu anamghufiria aliyekufa shahiyd madhambi yake yote isipokuwa deni.”
Pamoja na
deni zinaingia pia dhulma alizowadhulumu watu, kama vile kuuwa na kula mali za
watu pasipo haki na mfano wake.
Inajuzu
kutaka msaada wa wanafiki na wavunjao amri katika vita dhidi ya makafiri, na
hii ni kwa sababu Abdullahi bin Ubay na wanafiki wenzake walikuwa wakienda
vitani pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na
pia kisa cha Abu Muhjan al Thaqafi aliyekuwa mlevi, aliyepigana katika vita
dhidi ya dola ya Kifursi ni mashuhuri sana.
Ama kutaka
kupigana vita pamoja na makafiri, jambo hili lina khitilafu ndani yake miongoni
mwa maulamaa wa Kiislamu.
Ma Imam Malik
na Ahmed wanasema:
“Haijuzu
kutaka msaada wao, wala kusaidia katika jambo lolote.”
Imam Maalik
akaongeza:
‘Isipokuwa
kama watakuwa wakiwahudumia Waislamu tu, hapo inajuzu.’
Imam Abu Haniyfa
yeye anasem:
“Inawezekana
kutaka msaada wao na wanaweza kutoa msaada wowote ule sharti uwe Uislamu ndio
wenye nguvu, ama ikiwa ushirikina ndio wenye nguvu, basi inachukiza”.
Imam Shafi
yeye anasema:
“Inajuzu
kwa masharti mawili;
Kwanza
– Waislamu wawe wengi na washirikina wawe wachache.
Pili
– Wawe wanajulikana washirikina hao kuwa wana fikra nzuri na muelekeo mzuri juu
ya Uislamu. Na watakapotakiwa msaada wao, wasipewe katika sehemu ya ngawira,
bali wapewe malipo maalum bila kushirikishwa katika ngawira.”
Kutoka kwa
Mus'aab bin Saad bin Abi Waqaas amesema:
“Baba
yangu alidhani kuwa ana fadhila zaidi kuliko waliokuwa chini yake, Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:
“Kwani
mungepata ushindi na kupata riziki bila ya (dua za) madhaifu miongoni mwenu?”
Bukhari na
Annasai
Katika
Annasai imeandikwa kwa lafdhi ifuatayo:
“Hakika
Mwenyezi Mungu huwanusuru umma huu kwa madhaifu wao, kwa Dua zao na Swala zao
na ikhalsi yao.”
Na kutoka kwa
Abu al Darda-a (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Nilimsikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:
“Niitieni
masikini wenu, kwa hakika mnapata rizki na mnapata ushindi kwa (dua) za
madhaifu wenu.”
Maimamu wote
wa Ahlus Sunnah
Kutoka kwa
Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Huenda
mwenye nywele zilizotimka (kwa umasikini), anayefukuzwa milangoni (kwa
kudharauliwa) anapomuomba Mwenyezi Mungu atamkubalia (dua yake).”
Ahmed na
Muslim
Fadhila
zinazopatikana katika Kupigana Jihadi isiyokuwa ya waajib kwa ajili ya
kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuimakinisha hidaya Yake juu ya ardhi, na
kwa ajili ya kuimakinisha dini ya haki ni nyingi kupita fadhila zinazopatikana
katika kuhiji Hija ya nyongeza baada ya mtu kuhiji Hija yake ya lazima, au Umra
ya nyongeza, au Swala za Sunnah au Saumu ya Sunnah.
Juu ya yote
hayo, jihadi imekusanya kila aina ya ibada za kiroho na kiwiliwili, kuikinai
dunia, kuihama nchi na kuyahama matamanio na hii ndiyo maana ikapewa jina la
‘Ucha Mungu’, kwani imekuja katika hadithi kuwa; ‘Ucha
Mungu wa umma wangu ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Na ndani yake
mna kuitakasa nafsi, kuitakasa mali, na kumuuzia Mwenyezi Mungu nafsi, na haya
yote ni matunda ya mapenzi na imani na yakini na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu
Subhanahu wa Taala.
Mwenyezi
Mungu anasema:
Åöäøó
Çááøåó ÇÔúÊóÑóì ãöäó ÇáúãõÄúãöäöíäó ÃóäÝõÓóåõãú æóÃóãúæóÇáóåõã ÈöÃóäøó áóåõãõ
ÇáÌóäøóÉó íõÞóÇÊöáõæäó Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóíóÞúÊõáõæäó æóíõÞúÊóáõæäó æóÚúÏðÇ
Úóáóíúåö ÍóÞøðÇ Ýöí ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóÇáÅöäÌöíáö æóÇáúÞõÑúÂäö æóãóäú ÃóæúÝóì
ÈöÚóåúÏöåö ãöäó Çááøåö ÝóÇÓúÊóÈúÔöÑõæÇú ÈöÈóíúÚößõãõ ÇáøóÐöí ÈóÇíóÚúÊõã Èöåö
æóÐóáößó åõæó ÇáúÝóæúÒõ ÇáúÚóÙöíãõ
“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali
zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu -
wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na
Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini
kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.”
At Tawba -
111
Dini ya
Kiislamu imeitukuza ibada hii ya Jihadi, na ikatunabahisha juu umuhimu wake
katika sura nyingi zilizoteremshwa Madina na ikawalaumu wanaoiacha na
wanaoipinga na kuwapa sifa za unafiki na wenye maradhi moyoni.
Kutoka kwa
Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Nikujulisheni
juu ya aliye bora kupita wote? Mtu aliyeshika hatamu za farasi wake
(akimuelekeza) katika njia ya Mwenyezi Mungu (kupigana jihadi). Nikujulisheni
juu ya anayefuatiya? Mtu aliyejitenga akiwa na mbuzi wake akitoa haki ya
Mwenyezi Mungu katika mbuzi hao. Nikujulisheni juu ya mtu muovu kupita wote?
Mtu anayeombwa kwa jina la Mwenyezi Mungu kisha hatowi (juu ya kuwa anao
uwezo).”
Alipoulizwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam): ‘Mtu yupi aliye bora?’
Akajibu:
“Muislamu anayepigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake na
mali yake.”
Wakamuuliza:
“Kisha yupi?”
Akasema:
“Muislamu katika bonde mojawapo akimcha Mwenyezi Mungu na anawaepusha watu na
shari yake.”
Amehadithia
Attirmidhiy kuwa mtu mmoja alitamani ajitenge (awe mbali na watu huku akifanya
shughuli za ibada peke yake), akamuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) juu ya jambo hilo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) akamwambia:
“Usifanye
hivyo, kwa sababu mmoja wenu anaposimama (tu) katika njia ya Mwenyezi Mungu
(wakati wowote anapokuwa katika jihadi), ni bora kuliko akiswali nyumbani kwake
muda wa miaka sabini. Hampendi nyinyi Mwenyezi Mungu akughufirieni kisha
akuingizeni Peponi? Piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu. Atakayepigana
katika njia ya Mwenyezi Mungu (muda wa) kiasi cha kumkamua ngamia maziwa tu, imemwajibikia
Pepo.”
Attirmidhy
Kutoka kwa
Abu Saiyd al Khodary (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Ewe
Abu Saiyd! Atakayeridhika kuwa Mola wake ni Allah, na Islamu dini yake, na
Muhammad Mtume wake, amewajibika kuingia Peponi.”
Abu
Saiyd akastaajabu kwa maneno hayo akasema:
“Yarudie
tena (maneno hayo) kwa ajili yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.”
Kisha
(Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)) akasema:
“Na
mengine anamnyanyua kwayo mja wake daraja mia, na baina ya kila daraja mbili
(umbali wake) sawa na umbali wa mbingu na ardhi.”
Akauliza:
“Nini
hicho ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?”
Akasema:
“Ni
Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema pia:
“Hakika huko Peponi zipo daraja mia, Mwenyezi
Mungu amewatayarishia wapiganao Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na baina
ya kila daraja mbili umbali wake sawa na umbali wa mbingu na ardhi. Na
mnapomuomba Mwenyezi Mungu, muombeni (Pepo ya) Al Firdaus, kwani hiyo ipo kati
kati ya Pepo, sehemu ya juu ya Pepo, na juu yake ipo Arshi ya Al Rahman, na
kutoka hapo inapasuka (inaanzia) mito ya Peponi.”
Kutoka kwa
Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:
“Aliulizwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
“Kipi
chenye thamani kupita jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?”
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:
“Hamukiwezi.”
Akaulizwa
suali hilo mara mbili au tatu na kila anapoulizwa alikuwa akijibu:
“Hamukiwezi.”
Mara
ya tatu akasema:
“Mfano
wa anayepigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mfano wa aliyefunga
(aliyebaki akiwa amefunga), (na) akaswali nyakati za usiku huku akiomba na
kusoma aya za Mwenyezi Mungu bila kuchoka katika Swala yake wala kuacha kufunga
mpaka atakaporudi yule aliyekwenda kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi
Mungu.”
Maimamu
watano
Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hajeruhiwi
mtu (anapopigana jihadi) katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu
anamuelewa kila anayejeruhiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa atakuja
siku ya kiyama huku jeraha lake likiwa linamwaga damu, na rangi ni rangi ya
damu lakini harufu ni harufu ya miski.”
Amesema
Muhammad bin Ibrahim katika hadithi ndeefu yenye shairi refu ndani yake kuwa:
“Kisha
nikakutana na al Fudhail bin Iyadh akaniambia:
“Wewe
ni katika wanaoandika hadithi?”
Nikamwambia;
“Ndiyo’.
Akaniambia;
“Basi iandike hadithi hii (kama) ujira wako kwa kutuletea kitabu cha Abi Abdul
Rahman. Kisha Al Fudhail bin Iyadh akaanza kunihadithia yafuatayo:
“Amenihadithia
Mansur bin Al Muatamir, kutoka kwa Abi Saleh, kutoka kwa Abi Hurairah (Radhiya
Llahu anhu) kuwa mtu mmoja alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam); “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nifundishe jambo nitakalopata
ndani yake thawabu ya mpigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Akasema:
“Unaweza
uwe unaswali (moja kwa moja) bila kuchoka, na ufunge (moja kwa moja) bila kula
chakula?”
Akasema:
“Ewe
Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi ni dhaifu nisiyeweza kufanya yote hayo.”
Kisha
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:
“Basi
naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, lau kama utafanya yote
hayo basi (bado) hutouifikia (daraja) ya mpigana jihadi katika njia ya Mwenyezi
Mungu.
Hujaelewa bado kuwa Mpigana jihadi anapokuwa
juu ya farasi (akiwa amekaa tu juu yake) huku amezishika hatamu anaandikiwa
thawabu?.”
Na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kuwaambia Masahaba wake:
“Walipofariki
ndugu zenu katika vita vya Uhud, Mwenyezi Mungu alizijaalia roho zao ndani ya
mwili (mfano) wa ndege wa kijani, wanaiendea mito ya Peponi na wanakula katika
matunda yake na wanakaa katika tundu za dhahabu zilizotundikwa katika kivuli
cha Arshi. Walipoona ladha nzuri ya vyakula vyao na vinywaji vyao na makazi yao
wakasema:
“Nani
atakayewajulisha ndugu zetu (waliopo duniani) juu yetu kuwa tuko hai Peponi
tunaruzukiwa, ili wasije kufanya ulegevu katika jihadi?”
Mwenyezi
Mungu Akasema:
“Mimi
nitawajulisha juu yenu.”
Ndipo Alipoteremsha
kauli Yake:
æóáÇó ÊóÍúÓóÈóäøó ÇáøóÐöíäó ÞõÊöáõæÇú Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö
ÃóãúæóÇÊðÇ Èóáú ÃóÍúíóÇÁ ÚöäÏó ÑóÈøöåöãú íõÑúÒóÞõæäó . ÝóÑöÍöíäó ÈöãóÇ ÂÊóÇåõãõ
Çááøåõ ãöä ÝóÖúáöåö æóíóÓúÊóÈúÔöÑõæäó ÈöÇáøóÐöíäó áóãú íóáúÍóÞõæÇú Èöåöã ãøöäú
ÎóáúÝöåöãú ÃóáÇøó ÎóæúÝñ Úóáóíúåöãú æóáÇó åõãú íóÍúÒóäõæäó 0 íóÓúÊóÈúÔöÑõæäó
ÈöäöÚúãóÉò ãøöäó Çááøåö æóÝóÖúáò æóÃóäøó Çááøåó áÇó íõÖöíÚõ ÃóÌúÑó
ÇáúãõÄúãöäöíäó
“Wala
kabisa usiwadhanie waliouliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali
hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.
Wanafurahia
aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado
hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala
hawatahuzunika.
Wanashangilia
neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira
wa Waumini.”
Aal Imran –
169 – 171
Na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Roho
za mashahidi zimo ndani ya miili (mfano wa miili) ya ndege (yenye rangi ya)
kijani, wanatembezwa (wanaingia na kutoka) Peponi wanavyotaka.”
Na akasema:
“Shahidi
hahisi maumivu ya kuuliwa isipokuwa mfano wa mmoja wenu anavyohisi maumivu ya
kufinywa.”
Na akasema:
“Jihadi
iliyo bora, ajeruhiwe farasi wako na imwagike damu yako.”
Kutoka kwa
Jabir bin Atiq kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Mashahidi
ni (aina) saba gheri ya aliyeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu:
Aliyekufa
kwa maradhi ya tauni ni shahidi, aliyezama (aliyekufa kwa kuzama) shahidi,
mwenye maradhi yanayosibu sehemu za mbavu ni shahidi (aliyekufa kwa maradhi
hayo), aliyekufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi, aliyekufa kwa kuungua -
shahidi, aliyekufa kwa kuangukiwa na nyumba - shahidi, na mwanamke aliyekufa
katika uzazi - shahidi.”
Ahmed – Abu
Daud – Annasai kwa isnadi iliyo sahihi
Na kutoka kwa
Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) amesema:
“Wepi
mnaowahesabu kuwa ni mashahidi miongoni mwenu?”
Wakasema:
“Ewe
Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliyeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi.”
Akasema:
“Basi
mashahidi katika umati wangu watakuwa wachache.”
Wakasema:
“Wepi
hao basi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?”
Akasema:
“Atakayeuliwa
katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi, na atakayekufa katika njia ya
Mwenyezi Mungu ni shahidi (yaani akiwa katika kumtii Mwenyezi Mungu), na
atakayekufa kwa maradhi ya tauni ni shahidi, na atakayekufa kwa maradhi ya
tumbo ni shahidi na aliyezama ni shahidi.”
Muslim
Na kutoka kwa
Said bin Zeid kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Atakayeuliwa
kwa ajili ya (kuihami) mali yake ni shahidi, na atakayeuliwa kwa ajili ya
(kuipigania) dini yake ni shahidi, na atakayeuliwa kwa ajili ya (kuwahami) watu
wake ni shahidi.”
Ahmed na
Attirmidhiy na akaisahihisha.
Wanasema
wanavyouni kuwa watu wote hawa wanahesabiwa kuwa ni mashahidi juu ya kuwa
hawakufa katika vita vya jihadi ya kuipigania dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa
siku ya Akhera watapata thawabu sawa na waliokufa katika Jihadi, isipokuwa hapa
duniani wataoshwa na kusaliwa (kama maiti wa kawaida).
Anayepigana
jihadi ya kweli ni yule ambaye nia yake ni kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu
na kuinyanyua bendera ya Haki na kuiondoa batili na kujitolea mhanga nafsi yake
kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.
Ama ikiwa nia
ya kupigana Jihadi ni nyingine katika mambo ya kidunia tofauti na hayo
yaliyotajwa, basi hiyo haiwezi kupewa jina la Jihadi.
Kwa hivyo
atakayepigana kwa ajili ya kupata cheo, au kwa ajili ya ngawira, au apate
kuonekana ushujaa wake, au kwa ajili ya kujulikana, basi huyo hana chake katika
ujira wowote utokao kwa Mwenyezi Mungu na wala hatopata thawabu.
Kutoka kwa
Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Alikuja
mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema
(akauliza):
“Mtu
anapigana kwa ajili ya kujipatia ngawira (mali inayotekwa katika vita), na
mwengine apate kusifiwa, na mwengine apate kuonesha ushujaa wake, yupi kati yao
(anahesabiwa kuwa) yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu?”
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:
“Atakayepigana
ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, huyo yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Imesimuiwa na
Abu Daud na Annasai kuwa mtu mmoja alisema:
“Ewe
Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje mtu anayepigana kwa ajili ya kutaka ujira na
umaarufu, anapata nini?”
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):
“Hapati
chochote.”
Akauliza
suali hilo mara ya tatu ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alipomwambia:
“Hapati
chochote. Hakika Mwenyezi Mungu haikubali amali (matendo) yoyote ikiwa haikuwa
halisi kwa ajili ya kutaka radhi Zake.”
Nia ni uhai
wa amali yoyote ile, na chochote kinachotendwa bila ya nia basi amali hiyo
inakuwa amali isiyo na uhai wala uzito wowote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Amesimuliwa
Bukhari kutoka kwa Abullahi bin Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) kuwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika
amali zote (huhesabiwa kutokana) na nia, na hakika ana kila mja (malipo) ya
aliyoyanuwia.”
Nia ndiyo yenye
kunyanyua daraja ya matendo, kwani mtu anaweza kuifikia daraja ya waliokufa
shahiydi hata kama hakufa vitani.
Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayemuomba
Mwenyezi Mungu kwa nia ya kweli afe shahidi, Mwenyezi Mungu atamfikisha
katika daraja za waliokufa shahidi hata kama atakufa kitandani pake.”
Na akasema:
“Hakika
katika mji wa Madina kuna makundi ya watu ambao hamkwenda mwendo (vitani), na
hamkuyakata mabonde isipokuwa walikuwa mabondeni (sawa kama nyinyi),
yamewazuwia maradhi.”
Ikiwa nia ya
kupigana jihadi si kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, bali kwa ajili
ya kutafuta manufaa ya kidunia, basi si kama mtu huyo atakosa thawabu tu, bali
atakuwa amejitafutia adhabu siku ya Kiama.
Kutoka kwa
Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Nilimsikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:
“Wa
mwanzo kuhesabiwa siku ya Kiama ni mtu aliyekufa shahidi katika vita, ataletwa
na kujulishwa neema alizoneemeshwa na baada ya kuzijuwa ataulizwa:
“Umezifanyia
kazi gani neema hizi?”
Atasema:
“Nimepigana
jihadi kwa ajili yako mpaka nikafa shahidi.”
Ataambiwa:
“Umesema
uongo, bali ulipigana ili pasemwe kuwa wewe ni mjasiri na pashasemwa.”
Kisha
pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni.
Na
mtu (mwengine) aliyejifundisha elimu akaijuwa (vizuri), akasoma na qurani, (mtu
huyo) ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa;
“Umezifanyia
kazi gani neema hizi?”
Atasema:
“Nimejifunza
elimu nikafundisha na kwa ajili yako nikasoma qurani.”
Ataambiwa:
“Umesema
uongo, bali ulijifunza elimu ili pasemwe kuwa wewe ni aalim. Ukasoma qurani ili
pasemwe kuwa wewe ni msomaji mzuri, na pashasemwa.”
Kisha
pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni.
Na
mtu (mwengine) Mwenyezi Mungu amempa wasaa, akampa kila aina ya mali, ataletwa
na kujulishwa juu ya neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa:
“Umezifanyia
kazi gani neema hizi?”
Atasema:
“Sijaacha
njia unayopenda mtu atowe katika mali yake ila mimi nimetowa kwa ajili yako.”
Ataambiwa:
“Umesema
uongo, bali umetoa ili pasemwe kuwa wewe ni mkarimu na pashasemwa. Kisha
pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni”.
Katika mipaka
baina ya ardhi ya Waislamu na ya makafiri kwa kawaida panakuwa na upenyo,
upenyo ambao adui anaweza kuutumia kwa ajili ya kujipenyeza na kuingia ndani ya
ardhi ya Waislamu. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuzilinda vizuri sehemu
hizo ili adui asiwezi kuzitumia na kuwashambulia kwa urahisi.
Uislamu
umetilia mkazo sana kuzilinda sehemu hizo na pia umetilia mkazo kuwatayarisha
Waislamu ili wawe wapiganaji hodari, na kwa ajili hiyo kazi hii ya kulinda kwa
ajili ya kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ikapewa jina la (Al
Ribaat), na uchache wake ni muda wa saa moja na ukamilifu wake ni siku
arubaini, na fadhila nyingi sana zinapatikana katika kuzilinda sehemu zenye
hatari zaidi.
Maulamaa
wamekubaliana kuwa fadhila zake ni nyingi kupita fadhila za kuswali msikiti wa
Makka.
Hadithi
zifuatazo zinatujulisha juu ya fadhila za jukumu hili:-
Kutoka kwa
Salman (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa; alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akisema:
“Ribaat
ya siku moja na usiku wake ni bora kuliko kufunga mwezi mzima na kuswali usiku
wake, na mtu akifa (akiwa katika jukumu hilo), amali zake zitaendelea kuandikwa
na riziki yake ataendela kupata na atasalimika na fitna (za kaburi).”
Muslim
Na akasema:
“Kila
maiti amali zake zinakatika isipokuwa aliyekufa akiwa analinda mipaka ili adui
asiweze kuingia katika nchi ya Kiislamu (Muraabitan), kwa hakika huyu amali
zake zinaendelea kuandikwa mpaka siku ya Kiama, na anaepushwa na mitihani ya
kaburi.”
Uislamu
umetilia mkazo kujifunza kurusha (mkuki, mshale, kupiga risasi, mabomu nk.), na
pia kujifunza fani mbali mbali za kupigana kwa nia ya Jihadi katika njia ya
Mwenyezi Mungu, na ukapendekeza pia kufanya mazoezi ya viungo na ya kutumia
silaha kwa nia hiyo hiyo.
Kutoka kwa
Uqbah bin Amer (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Nilimsikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akiwa juu ya membari
akisema:
æóÃóÚöÏøõæÇú
áóåõã ãøóÇ ÇÓúÊóØóÚúÊõã ãøöä ÞõæøóÉò
“Basi
waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mnazoweza (silaha).”[1][1]
‘Hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika
nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha.”
Muslim
Na kutoka kwa Uqba (Radhiya Llahu anhu) pia alisema:
“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akisema:
“Mtawezeshwa kuziteka nchi nyingi, mmoja wenu
asishindwe kuutumuia mshale wake (asijifunze kuutumia kwa ajili ya mchezo tu –
bali kwa ajili ya kupigana jihadi). Hakika Mwenyezi Mungu huwaingiza Peponi
watu watatu kwa mshale mmoja - aliyeutengeneza (kwa nia ya jihadi), anayempa
(anayekaa nyuma yake au pamoja naye na kumpa pale mishale inapomalizika), na
mrushaji katika njia ya Mwenyezi Mungu.”
Uislamu umeshadidia sana katika kuchukizwa na mtu
anayejifunza kutumia upinde au silaha yoyote kisha akasahau namna ya kuitumia
silaha hiyo bila udhuru unaokubalika kisheria.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Atakayejifunza kutupa, kisha akasahau hayupo
pamoja nasi.”
Na akasema:
“Mchezo wowote anaocheza mtu ni batil (yaani
hapati thawabu ndani yake), isipokuwa (mchezo wa) upinde (na mshale), na
kumzowesha farasi wake (pamoja na kumfundisha), na kucheza na watu wa nyumba
yake (kwa kuzungumza na mkewe na kutaniana naye), hayo ni katika mambo ya haki
(anayopata thawabu ndani yake).”
Anasema Al Qurtubiy:
“Maana ya hadithi hii na Mwenyezi Mungu ndiye
ajuwae zaidi, ni kuwa; Kila mchezo unaopoteza wakati wa mtu usio na faida,
hauna thawabu yoyote ndani yake, na kuachana nao ni bora zaidi, isipokuwa mambo
matatu haya, juu ya kuwa ni mchezo, lakini yanampatia mtu thawabu kwa sababu ya
faida inayopatikana ndani yake. Kwa sababu katika kutumia upinde na mshale na
kumfundisha farasi mbinu mbali mbali za kivita, na mtu kuzungumza na kutaniana
na mkewe kunaweza kumfanya awe mcha Mungu wa kweli. Na kwa ajili hii mambo
matatu haya yakawa yanaweza kumpatia mtu thawabu.”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alisema:
“Enyi wana wa Ismail! rusheni (mishale) kwani
baba yenu alikuwa mrushaji.”
Na kujifunza kupanda farasi na kutumia silaha ni katika
fardhi kifaya inayoweza kuwa fardhi aiyn.
Yafuatayo ni mambo anayowajibika kuwa nayo kiongozi wa
jeshi.
1- Kushauriana na wenzake na kutaka rai zao, na asiwe
akijiamulia bila kuwashauri, na hii inatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema;
“Na shauriana nao katika mambo.”
Al Imran – 159
Na kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Sijapata kumuona mtu anayependa kutaka
ushauri wa Masahaba wake kupita Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).”
Imam Ahmed na Imam Shafi (Radhiya Llahu anhu).
2-
Upole na kuwarahisishia mambo.
Anasema Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha):
“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akisema:
“Yeyote atakayepewa uongozi wa umma wangu basi
awe mpole juu yao, awe mpole juu yao.”
Na imepokelewa kutoka kwa Muaqal bin Yasar kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Hapana amiri yeyote aliyepewa uongozi juu ya
Waislamu, kisha asijitahidi juu yao (katika kuwa mpole kwao na katika
kuwatafutia manufaa) wala asiwanasihi, (kwa kuwaamrisha mema na kuwakataza
mabaya) isipokuwa hatoingia Peponi.”
Na amesimulia Abu Daud kutoka kwa Jabir (Radhiya Llahu anhu)
kuwa amesema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) alikuwa akirudi nyuma katika misafara kwa ajili ya kuwasaidia walio
dhaifu (kwa kuwashika mikono au kushika hatamu za wanyama wao na kuwatanguliza
mbele ili wawe pamoja na wenzao), na kuwapakia juu ya ngamia (wake na wa
wengine wendao kwa miguu).”
3-
Kuamrisha mema na kukataza maovu ili
watu waepukane na kumuasi Mwenyezi
Mungu.
4-
Kulikagua jeshi mara kwa mara apate
kuwajuwa vizuri askari wake, na kuwajuwa wale wanaowavunja moyo wenzao wasitake
kwenda vitani, na wale wanaosababisha choko choko katika jeshi, kwa kusema kwa
mfano; ‘hatuna silaha za kutosha wala nguvu za kutosha.’ Na pia apate kuwajuwa
wale wanaotoa siri za jeshi.
5-
Kupashana habari na viongozi.
6-
Kuchaguwa sehemu zinazofaa kwa ajili
ya kupiga kambi.
7-
Kutuma wapelelezi kwa ajili ya
kujuwa hali za adui.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa anapotaka kushambulia mahali akiwababaisha adui kwa kuwajulisha kama
kwamba anataka kushambulia mahali pengine.
Alikuwa pia akiwatuma wapelelezi wamletee habari za adui, na
alikuwa akilipanga vizuri jeshi lake.
Amesema Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu):
“Bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) ilikuwa nyeusi
na ya jeshi ilikuwa nyeupe.”
Abu Daud
Kutoka kwa Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa anapompa uongozi yeyote katika Masahaba wake katika baadhi ya mambo
alikuwa akimwambia:
“Wapeni watu bishara njema (juu ya rehma ya
Mwenyezi Mungu na kusamehe kwake) wala miswape habari za kuwachukiza (kwa
kuwatisha na kuwaogopesha), na mambo muyafanye (yawe) mepesi, msiyafanye
(yakawa) magumu.”
Na pia kutoka kwa Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:
“Alinituma Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) mimi na Muadh kwenda Yemen akasema:
“Wepesisheni mambo wala msifanye yakawa
magumu, wapeni watu bishara njema wala miswape habari za kuwachukiza,
wahiyarisheni, na msikhitilafiane.”
Bukhari na Muslim
Kutoka kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Nendeni kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa kufuata mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu,
wala msimuuwe mzee mkongwe, wala mtoto mdogo, wala mwanamke (ila kama ni
mwanajeshi), wala msiendeane kinyume katika ngawira, na mchange pamoja ngawira
zenu, na mtengeneze na mfanye mema kwa sababu Mwenyezi Mungu anawapenda
watendao mema.”
Abu Daud
Omar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alimwandikia Saad bin
Abi Waqaas (Radhiya Llahu anhu) na askari wake wengine akiwausia yafuatayo;:
“Amma baad -
Mimi nakuamrisha wewe pamoja na askari ulio nao kumcha Mwenyezi Mungu
katika kila jambo, kwa sababu kumcha Mungu ni silaha bora kupita zote mbele ya
adui, na ni mbinu yenye nguvu kupita zote kati vita. Na nakuamrisha wewe pamoja
na ulio nao mchunge msije kufanya maasi kuliko mnavyomchunga adui yenu, kwa
sababu madhambi ya wanajeshi yana hatari zaidi juu yao kupita adui wao. Kwa hakika
Mwenyezi Mungu huwapa ushindi Waislamu kwa sababu maadui ni watu wenye kumuasi
Mwenyezi Mungu, ama sivyo sisi hatuna nguvu za kuwashinda, kwa sababu idadi yao
ni kubwa kuliko idadi yetu, na silaha zao ni kali kupita silaha zetu. Kwa hivyo
tukiwa sawa nao katika kufanya maasi, basi wao watatushinda kwa nguvu zao, kwa
sababu tunapewa ushindi kutokana na fadhila zetu na si kwa nguvu zetu.
Na mjuwe kuwa katika msafara wenu mna
(Malaika) wenye kuhifadhi wanaojuwa kila mnalotenda, kwa hivyo muwaonee haya,
na msiwe wenye kumuasi Mwenyezi Mungu mkiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na
wala msiseme kuwa; ‘Kwa vile adui wetu wana shari kupita sisi kwa hivyo
hawataweza kupewa ushindi juu yetu,’ kwani huenda watu wakasalatishiwa
(wakapelekewa) na kushindwa na adui aliye mbaya kupita wao kama pale Bani
Israil walipomuasi Mwenyezi Mungu akawapelekea Majusi (wanaoabudi moto)
wakaingia mijini mwao kila upande, ikawa ahadi iliyoyotimizwa.
Muombeni Mwenyezi Mungu akusaidieni katika
nafsi zenu kama mnavyomuomba akupeni ushindi juu ya adui yenu, namuomba
Mwenyezi Mungu anipe mimi na nyinyi yote hayo.
Na kuweni wapole kwa Waislamu katika mwenendo
wao wala msiwakalifishe mambo mazito yatakayowataabisha.”
Mpigana jihadi anatakiwa amuombe Mwenyezi Mungu ampe ushindi
kwa sababu ushindi umo mikononi mwake Subhanahu wa Taala, na huu ndio uliokuwa
mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na mwenendo
wa Masahaba baada yake (Radhiya llahu Anhum).
Kutoka kwa Abu Daud kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema:
“Mawili hayarudi patupu; Dua baada ya
muadhini, na (dua) katika vita pale wapiganaji wanapovamiana.”
Mwenyezi Mungu Amesema:
ÅöÐú
ÊóÓúÊóÛöíËõæäó ÑóÈøóßõãú ÝóÇÓúÊóÌóÇÈó áóßõãú
“(Kumbukeni) mlipokuwa
mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni.”
Al Anfal – 9
Imepokelewa kutoka kwa (Maimamu) watatu (wa elimu ya
hadithi) kutoka kwa Abdullah bin Abi Aufiy kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) katika siku mojawapo alipokuwa akiwasubiri maadui,
alisubiri mpaka wakati wa zawal (kidogo baada ya adhuhuri), kisha akasimama
kuwahutubia watu akasema:
“Enyi watu! Msitamani kukutana na adui, na
muombeni Mwenyezi Mungu usalama, na mtakapokutana naye (adui) basi muwe wenye
subira (wavumilivu) na jueni kuwa Pepo ipo chini ya vivuli vya panga.”
Kisha akasema:
“Mola wangu uliyekiteremsha kitabu, mwenye
kuyasukuma mawingu, uliyewashinda makundi (katika vita vya Ahzabu), washinde na
utupe ushindi juu yao.”
Na katika dua zake wakati wa vita (alikuwa akisema):
“Mola wangu wewe ndiye msaidizi wangu na
unipaye ushindi, kwako naelekea na nategemea na kwa ajili yako napigana vita.”
Imepokelewa na maimamu wa Ahli Ssunnah
Dini ya kiisalmu inawaita watu katika uongofu utokao kwa
Mwenyezi Mungu ili wafaidike na uongofu huo na ili wapate maisha mema ya hapa
duniani na ya kesho akhera.
Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu ameupa umma wa kiislamu jukumu
la kuinyanyua dini yake, na kuwafikishia watu wahyi wake kwa ajili ya kuuongoza
na kuukomboa ulimwengu.
Na kwa ajili hii ndiyo umma huu ukawa umma bora kupita umma
zote zilizodhihirishiwa watu, na ukawa mbele ya watu wengine ukiongoza mfano wa
mwalimu na wanafunzi wake, na kwa ajili hiyo lazima uwe na uwezo wa kujihifadhi
na wa kujidumisha, na pia uwezo wa kupambana kwa ajili ya kujipatia haki yake na ili uweze kuchukuwa
nafasi yake iliyowekewa na Mwenyezi Mungu.
Na kila mwenye kupunguza asitimize wajibu wake katika kujipatia
haki yake hiyo, basi anahesabiwa kuwa amefanya makosa makubwa ambayo Mwenyezi
Mungu humdhalilisha kwayo au kumfutilia mbali.
Uislamu umekataza ulegevu na kutaka amani (kwa makafiri)
ikiwa lengo halijafikiwa, kwa sababu kutaka amani katika wakati kama huu
haitokuwa na maana yoyote wala tafsiri nyingine isipokuwa ni uoga na kuridhika
kuishi kama watu duni.
Katika haya Mwenyezi Mungu Anasema:
ÝóáÇ
ÊóåöäõæÇ æóÊóÏúÚõæÇ Åöáóì ÇáÓøóáúãö æóÃóäÊõãõ ÇáÇóÚúáóæúäó æóÇááøóåõ ãóÚóßõãú
æóáóä íóÊöÑóßõãú ÃóÚúãóÇáóßõãú
“Basi msiregee na kutaka
suluhu (piganeni nao maadui zenu) maana nyinyi ndio mtakaoshinda; na Mwenyezi
Mungu yu pamoja nanyi; wala hatakunyimeni (thawabu za) vitendo vyenu.”
Muhammad – 35
Na maana ya neno ‘mtakaoshinda’ maana yake ni kuwashinda na
kuwa juu yao katika itikadi, ibada, mwenendo na tabia njema, elimu, na matendo.
Amani ya kweli haipatikani bila ya nguvu na uwezo wa
kupigana vita, na hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akaweka sharti kuwa lazima
adui aache kuwapiga vita waislamu na kuwafanyia uadui ili dhulma ipate kutoweka
juu ya ardhi na ili mtu asiteswe kwa ajili ya dini yake.
Likiwepo mojawapo katika sababu hizo, basi Mwenyezi Mungu
ametoa idhini ya kupigana vita. (yaani ikiwa waislamu wanapigwa vita au
wanadhulimiwa au wanafanyiwa uadui au wanateswa kwa ajili ya itikadi yao basi
wanaruhusiwa kupigana vita).
Hapana dini yoyote iliyowapa idhini watu wake kuingia katika
mapambano na kupigana vita kwa ajili ya kuisimamisha haki na kwa ajili ya
kuwasaidia wanaodhulumiwa na kwa ajli ya kuishi maisha ya kuheshimika isipokuwa
dini ya kiislamu.
Kwa atakayefuatilia aya mbali mbali za Qurani tukufu pamoja
na maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na ya
makhalifa wake (Radhiya Llahu anhu) atayaona yote hayo kwa uwazi kabisa, kwani
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anautaka umma huu kutumia nguvu zake zote
katika kuyatimiza hayo.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÌóÇåöÏõæÇ
Ýöí Çááøóåö ÍóÞøó ÌöåóÇÏöåö
“Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama
inavyostahiki (kupiganiwa).”
Al Hajj – 78
Kisha Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala öAkabainisha
kuwa jihadi ni Imani ya matendo, ambayo bila ya hiyo dini haikamiliki, Akasema:
ÃóÍóÓöÈó
ÇáäøóÇÓõ Ãóä íõÊúÑóßõæÇ Ãóä íóÞõæáõæÇ ÂãóäøóÇ æóåõãú áÇ íõÝúÊóäõæäó. æóáóÞóÏú
ÝóÊóäøóÇ ÇáøóÐöíäó ãöä ÞóÈúáöåöãú ÝóáóíóÚúáóãóäøó Çááøóåõ ÇáøóÐöíäó ÕóÏóÞõæÇ
æóáóíóÚúáóãóäøó ÇáúßóÇÐöÈöíäó
“Je! Wanadhani watu
wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?
Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na
kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha
walio waongo.”
Al An’kabut – 2 – 3
Kisha Akabainisha kuwa hii ndiyo njia aliyowaekea waumini,
na kwamba hapana njia nyingine itakayowaletea ushindi na kuwaingiza Peponi, Akasema:
Ãóãú
ÍóÓöÈúÊõãú Ãóä ÊóÏúÎõáõæÇú ÇáúÌóäøóÉó æóáóãøóÇ íóÃúÊößõã ãøóËóáõ ÇáøóÐöíäó
ÎóáóæúÇú ãöä ÞóÈúáößõã ãøóÓøóÊúåõãõ ÇáúÈóÃúÓóÇÁ æóÇáÖøóÑøóÇÁ æóÒõáúÒöáõæÇú
ÍóÊøóì íóÞõæáó ÇáÑøóÓõæáõ æóÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ãóÚóåõ ãóÊóì äóÕúÑõ Çááøåö ÃóáÇ
Åöäøó äóÕúÑó Çááøåö ÞóÑöíÈñ
“Mnadhani kuwa mtaingia
Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu?
Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye
wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi
Mungu ipo karibu.
Al Baqarah – 214
Akawataka Waislamu kujitayarisha vizuri na akawataka pia
wawe wenye kutisha mbele ya makafiri, Akasema:
æóÃóÚöÏøõæÇú
áóåõã ãøóÇ ÇÓúÊóØóÚúÊõã ãøöä ÞõæøóÉò æóãöä ÑøöÈóÇØö ÇáúÎóíúáö ÊõÑúåöÈõæäó Èöåö
ÚóÏúæøó Çááøåö æóÚóÏõæøóßõãú æóÂÎóÑöíäó ãöä Ïõæäöåöãú áÇó ÊóÚúáóãõæäóåõãõ
Çááøåõ íóÚúáóãõåõãú æóãóÇ ÊõäÝöÞõæÇú ãöä ÔóíúÁò Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö íõæóÝøó
Åöáóíúßõãú æóÃóäÊõãú áÇó ÊõÙúáóãõæäó
“Basi waandalieni nguvu
kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui
wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi
Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa,
na wala nyinyi hamtadhulumiwa”.
Al Anfal – 60
Na namna ya kujitayarisha inategemea wakati na hali ya
mambo, na neno ‘nguvu’, maana yake ni kutumia kila njia inayowezekana kutumika
kwa ajili ya kumuondoa adui.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
‘Hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika
nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha.”
Muslim
Na katika kujitayarisha ni kuchukua hadhari na kumuandaa
kila mwenye uwezo.
Mwenyezi Mungu Anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÎõÐõæÇú ÍöÐúÑóßõãú ÝóÇäÝöÑõæÇú ËõÈóÇÊò Ãóæö
ÇäÝöÑõæÇú ÌóãöíÚðÇ
“Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na
mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!
An Nisaa – 71
Na kuchukuwa hadhari hakukamiliki ila kwa kujitayarisha na
majeshi yanayoweza kupigana ardhini na baharini na angani.
Mwenyezi Mungu akatuamrisha
kupambana na adui tukiwa katika hali yoyote ile, iwe ya dhiki au katika neema,
nzuri au mbaya, Akasema:
ÇäúÝöÑõæÇú
ÎöÝóÇÝðÇ æóËöÞóÇáÇð æóÌóÇåöÏõæÇú ÈöÃóãúæóÇáößõãú æóÃóäÝõÓößõãú Ýöí ÓóÈöíáö
Çááøåö Ðóáößõãú ÎóíúÑñ áøóßõãú Åöä ßõäÊõãú ÊóÚúáóãõæäó
“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na
piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya
ni kheri kwenu mkiwa mnajua.”
At Tawba – 41
Uislamu unategemea zaidi nguvu ya imani kuliko nguvu ya
silaha na kwa ajili hiyo unatilia nguvu zaidi mambo ya kiroho na kuiamsha hima na azma ya mpiganaji.
Mwenyezi Mungu Anasema:
ÝóáúíõÞóÇÊöáú
Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÇáøóÐöíäó íóÔúÑõæäó ÇáúÍóíóÇÉó ÇáÏøõäúíóÇ ÈöÇáÂÎöÑóÉö æóãóä
íõÞóÇÊöáú Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóíõÞúÊóáú Ãóæ íóÛúáöÈú ÝóÓóæúÝó äõÄúÊöíåö ÃóÌúÑðÇ
ÚóÙöíãðÇ. æóãóÇ áóßõãú áÇó ÊõÞóÇÊöáõæäó Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóÇáúãõÓúÊóÖúÚóÝöíäó
ãöäó ÇáÑøöÌóÇáö æóÇáäøöÓóÇÁ æóÇáúæöáúÏóÇäö ÇáøóÐöíäó íóÞõæáõæäó ÑóÈøóäóÇ
ÃóÎúÑöÌúäóÇ ãöäú åóÜÐöåö ÇáúÞóÑúíóÉö ÇáÙøóÇáöãö ÃóåúáõåóÇ æóÇÌúÚóá áøóäóÇ ãöä
áøóÏõäßó æóáöíøðÇ æóÇÌúÚóá áøóäóÇ ãöä áøóÏõäßó äóÕöíÑðÇ
“Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu
wale ambao wanaouza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya
Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi
Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola
Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie
tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka
kwako?”
An Nisaa – 75-76
Na Muislamu anatakiwa awe na subira, kwani kama yeye
avyoumia basi adui naye pia anaumia, tena yeye anaumia zaidi kupita wao, na hii
ni kwa sababu ya hitilafu kubwa ya malengo yao.
Mwenyezi Mungu önasema:
æóáÇó
ÊóåöäõæÇú Ýöí ÇÈúÊöÛóÇÁ ÇáúÞóæúãö Åöä ÊóßõæäõæÇú ÊóÃúáóãõæäó ÝóÅöäøóåõãú
íóÃúáóãõæäó ßóãóÇ ÊóÃúáóãæäó æóÊóÑúÌõæäó ãöäó Çááøåö ãóÇ áÇó íóÑúÌõæäó
“Wala msifanye uvivu
kuwafuatia watu (walio maadui). Kama mmepata maumivu basi wao pia wanapata
maumivu kama mnavyoumia. Na nyinyi mnatumai kwa Mwenyezi Mungu wasiyoyatumai.”
An Nisaa – 105
Na Akasema:
ÇáøóÐöíäó
ÂãóäõæÇú íõÞóÇÊöáõæäó Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö æóÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú íõÞóÇÊöáõæäó Ýöí
ÓóÈöíáö ÇáØøóÇÛõæÊö ÝóÞóÇÊöáõæÇú ÃóæúáöíóÇÁ ÇáÔøóíúØóÇäö Åöäøó ßóíúÏó
ÇáÔøóíúØóÇäö ßóÇäó ÖóÚöíÝðÇ
“Walio amini wanapigana katika Njia ya
Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapigana katika njia ya upotofu. Basi
piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu.”
An Nisaa - 76
Na maana yake ni kuwa; lengo la Waislamu ni tukufu, na
ujumbe wao wanaotaka kuufikisha kwa watu ambao kwa ajili yake wanapigana jihadi,
ambayo ni risala ya haki na ya kheri, nayo ni kulinyanyua juu neno la Mwenyezi
Mungu ni tukufu pia.
Na Muislamu anatakiwa awe mwenye nyoyo thabiti kwenye
mapambano.
Mwenyezi Mungu Aanasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÅöÐóÇ áóÞöíÊõãõ ÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú ÒóÍúÝÇð ÝóáÇó
Êõæóáøõæåõãõ ÇáÃóÏúÈóÇÑó 15 æóãóä íõæóáøöåöãú íóæúãóÆöÐò ÏõÈõÑóåõ ÅöáÇøó
ãõÊóÍóÑøöÝÇð áøöÞöÊóÇáò Ãóæú ãõÊóÍóíøöÒÇð Åöáóì ÝöÆóÉò ÝóÞóÏú ÈóÇÁ ÈöÛóÖóÈò
ãøöäó Çááøåö æóãóÃúæóÇåõ Ìóåóäøóãõ æóÈöÆúÓó ÇáúãóÕöíÑõ
“Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru
vitani msiwageuzie mgongo.
Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo -
isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi atakuwa amestahiki
ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho
muovu.”
Al Anfal – 15 – 16
Kisha Akawajulisha juu ya mahali ilipo nguvu zao za imani Aliposema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÅöÐóÇ áóÞöíÊõãú ÝöÆóÉð ÝóÇËúÈõÊõæÇú æóÇÐúßõÑõæÇú
Çááøåó ßóËöíÑðÇ áøóÚóáøóßõãú ÊõÝúáóÍõæäó. æóÃóØöíÚõæÇú Çááøåó æóÑóÓõæáóåõ æóáÇó
ÊóäóÇÒóÚõæÇú ÝóÊóÝúÔóáõæÇú æóÊóÐúåóÈó ÑöíÍõßõãú æóÇÕúÈöÑõæÇú Åöäøó Çááøåó ãóÚó
ÇáÕøóÇÈöÑöíäó
“Enyi mlio amini!
Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili
mpate kufanikiwa.
Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala
msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi
Mungu yu pamoja na wanao subiri”
Al Anfal – 45-46
Kisha Akatujulisha juu ya nafsi ya Muislamu, na kwamba
lazima waipigane kwa juhudi zao zote, kwa sababu hawana isipokuwa hiari mbili
tu, ama wauwe au wauliwe, Akasema:
Åöäøó
Çááøåó ÇÔúÊóÑóì ãöäó ÇáúãõÄúãöäöíäó ÃóäÝõÓóåõãú æóÃóãúæóÇáóåõã ÈöÃóäøó áóåõãõ
ÇáÌóäøóÉó íõÞóÇÊöáõæäó Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÝóíóÞúÊõáõæäó æóíõÞúÊóáõæäó æóÚúÏðÇ
Úóáóíúåö ÍóÞøðÇ Ýöí ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóÇáÅöäÌöíáö æóÇáúÞõÑúÂäö æóãóäú ÃóæúÝóì
ÈöÚóåúÏöåö ãöäó Çááøåö ÝóÇÓúÊóÈúÔöÑõæÇú ÈöÈóíúÚößõãõ ÇáøóÐöí ÈóÇíóÚúÊõã Èöåö
æóÐóáößó åõæó ÇáúÝóæúÒõ ÇáúÚóÙöíãõ
“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali
zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu -
wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na
Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini
kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
At Tawba – 111
Akiuwa atapata ushindi, na akiuliwa atakuwa amekufa shahidi
na ataingia Peponi.
Mwenyezi Mungu Anasema:
Þõáú
åóáú ÊóÑóÈøóÕõæäó ÈöäóÇ ÅöáÇøó ÅöÍúÏóì ÇáúÍõÓúäóíóíúäö
“Sema; ‘Nyini hamtutazamii sisi ila (kupata) moja katika mema
mawili (ima kushinda au kuuawa mkapata Pepo).”
At Tawba - 52
Anayeuliwa katika jihadi kwa ajili ya kulinyanyua neno la
Mwenyezi Mungu hafi akatoweka kama wanavyokufa watu wa kawaida, bali wao
wananyanyuliwa na kupelekwa mahali pema zaidi na bora zaidi. Kwa hivyo kufa
katika njia ya Mwenyezi Mungu maana yake hasa ni kubaki.
Mwenyezi Mungu Anasema:
æóáÇó
ÊóÍúÓóÈóäøó ÇáøóÐöíäó ÞõÊöáõæÇú Ýöí ÓóÈöíáö Çááøåö ÃóãúæóÇÊðÇ Èóáú ÃóÍúíóÇÁ
ÚöäÏó ÑóÈøöåöãú íõÑúÒóÞõæäó. ÝóÑöÍöíäó ÈöãóÇ ÂÊóÇåõãõ Çááøåõ ãöä ÝóÖúáöåö
æóíóÓúÊóÈúÔöÑõæäó ÈöÇáøóÐöíäó áóãú íóáúÍóÞõæÇú Èöåöã ãøöäú ÎóáúÝöåöãú ÃóáÇøó
ÎóæúÝñ Úóáóíúåöãú æóáÇó åõãú íóÍúÒóäõæäó. íóÓúÊóÈúÔöÑõæäó ÈöäöÚúãóÉò ãøöäó
Çááøåö æóÝóÖúáò æóÃóäøó Çááøåó áÇó íõÖöíÚõ ÃóÌúÑó ÇáúãõÄúãöäöí
“Wala kabisa usiwadhanie
walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai,
wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.
Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa
fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma
yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.
Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi
Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini."
Al Imran – 169 – 171
Mwenyezi Mungu siku zote huwa pamoja na wanaopigana jihadi
na wala hawaachi mkono.
Mwenyezi Mungu Anasema:
ÅöÐú
íõæÍöí ÑóÈøõßó Åöáóì ÇáúãóáÂÆößóÉö Ãóäøöí ãóÚóßõãú ÝóËóÈøöÊõæÇú ÇáøóÐöíäó
ÂãóäõæÇú ÓóÃõáúÞöí Ýöí ÞõáõæÈö ÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú ÇáÑøóÚúÈó ÝóÇÖúÑöÈõæÇú
ÝóæúÞó ÇáÃóÚúäóÇÞö æóÇÖúÑöÈõæÇú ãöäúåõãú ßõáøó ÈóäóÇäò
“Mola wako Mlezi alipo
wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini.
Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na
wapigeni kwenye kila ncha za vidole.”
Al Anfal - 12
Kisha Mwenyezi Mungu anawatayarishia malipo mema hapa
duniani na pia malipo mema huko akhera.
Mwenyezi Mungu Anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂóãóäõæÇ åóáú ÃóÏõáøõßõãú Úóáóì ÊöÌóÇÑóÉò ÊõäÌöíßõã ãøöäú
ÚóÐóÇÈò Ãóáöíãò. ÊõÄúãöäõæäó ÈöÇááøóåö æóÑóÓõæáöåö æóÊõÌóÇåöÏõæäó Ýöí ÓóÈöíáö
Çááøóåö ÈöÃóãúæóÇáößõãú æóÃóäÝõÓößõãú Ðóáößõãú ÎóíúÑñ áøóßõãú Åöä ßõäÊõãú
ÊóÚúáóãõæäó. íóÛúÝöÑú
áóßõãú ÐõäõæÈóßõãú æóíõÏúÎöáúßõãú ÌóäøóÇÊò ÊóÌúÑöí ãöä ÊóÍúÊöåóÇ ÇáúÃóäúåóÇÑõ
æóãóÓóÇßöäó ØóíøöÈóÉð Ýöí ÌóäøóÇÊö ÚóÏúäò Ðóáößó ÇáúÝóæúÒõ ÇáúÚóÙöíãõ.
æóÃõÎúÑóì ÊõÍöÈøõæäóåóÇ äóÕúÑñ ãøöäó Çááøóåö æóÝóÊúÍñ ÞóÑöíÈñ æóÈóÔøöÑö
ÇáúãõÄúãöäöíäó
“Enyi mlio amini!
Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu?
Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na
piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya
ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni
katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika
Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.
Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura
itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!”
Ass’saf – 10 – 13
Kwa njia hii dini ya kiislamu iliwalea waliotangulia na
ikaweza kuingiza ndani ya nafsi zao imani iliyowawezesha kupambanua baina ya haki na batili na kuwawezesha kupata
ushindi na kuziteka nchi na iliwawezesha kuwamakinisha vizuri juu ya ardhi.
Mwenyezi Mungu öööAnasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ Åöä ÊóäÕõÑõæÇ Çááøóåó íóäÕõÑúßõãú æóíõËóÈøöÊú
ÃóÞúÏóÇãóßõãú
“Enyi mlio amini!
Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.”
Muhammad – 7
Na öAnasema:
æóÚóÏó
Çááøóåõ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ãöäßõãú æóÚóãöáõæÇ ÇáÕøóÇáöÍóÇÊö áóíóÓúÊóÎúáöÝóäøóåõã
Ýöí ÇáúÃóÑúÖö ßóãóÇ ÇÓúÊóÎúáóÝó ÇáøóÐöíäó ãöä ÞóÈúáöåöãú æóáóíõãóßøöäóäøó
áóåõãú Ïöíäóåõãõ ÇáøóÐöí ÇÑúÊóÖóì áóåõãú æóáóíõÈóÏøöáóäøóåõã ãøöä ÈóÚúÏö
ÎóæúÝöåöãú ÃóãúäðÇ íóÚúÈõÏõæäóäöí áóÇ íõÔúÑößõæäó Èöí ÔóíúÆðÇ æóãóä ßóÝóÑó
ÈóÚúÏó Ðóáößó ÝóÃõæúáóÆößó åõãõ ÇáúÝóÇÓöÞõæäó
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini
miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi
kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini
yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe
wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya
hayo, basi hao ndio wapotovu.”
Nur – 55
Muislamu analazimika kuwa thabiti mbele ya adui na ni haramu
kwake kurudi nyumba katika mapambano.
Mwenyezi Mungu anasema:
íóÇ
ÃóíøõåóÇ ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú ÅöÐóÇ áóÞöíÊõãõ ÇáøóÐöíäó ßóÝóÑõæÇú ÒóÍúÝÇð ÝóáÇó
Êõæóáøõæåõãõ ÇáÃóÏúÈóÇÑó. æóãóä íõæóáøöåöãú íóæúãóÆöÐò ÏõÈõÑóåõ ÅöáÇøó
ãõÊóÍóÑøöÝÇð áøöÞöÊóÇáò Ãóæú ãõÊóÍóíøöÒÇð Åöáóì ÝöÆóÉò ÝóÞóÏú ÈóÇÁ ÈöÛóÖóÈò
ãøöäó Çááøåö æóãóÃúæóÇåõ Ìóåóäøóãõ æóÈöÆúÓó ÇáúãóÕöíÑõ
“Enyi Mlioamini!
Mkutanapo vitani na wale waliokufuru basi msiwageuzie migongo (mkakimbia).
Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo -
isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki
ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho
muovu.”
Al Anfal – 15-16
Aya hizi zinawajibisha kuwa thabiti katika mapambano na
zinaharamisha kurudi nyuma isipokuwa katika hali mbili zifuatazo;
Ya kwanza – Kwa ajili ya mbinu za kivita kama vile kuondoka
mahali penye hatari zaidi na kukimbilia mahali bora, au kuondoka mahali
anapoweza kudhurika kwa urahisi na kukimbilia mahali anapoweza kusitirika, au
mahali pa chini na kukimbilia penye muinuko atakapoweza kupambana na adui kwa
urahisi zaidi.
Ya pili – Kurudi kwa nia ya kuungana na wenzake kwa ajili ya
kupambana kwa pamoja dhidi ya adui, au kwa ajili ya kuwasaidia wenzake hao,
yote sawa ikiwa wenzake hao wako karibu au wako mbali.
Kinyume na hivyo, kurudi nyuma kwa ajili ya kukimbia tu ni
mojawapo ya madhambi makubwa sana yatakayompelekea mtu kupata adhabu iumizayo.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Jiepusheni na mambo saba yaangamizayo.”
Wakamuuliza:
“Ni yepi hayo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?”
Akasema:
“Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, Uchawi, kuiuwa
nafsi iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia
mnapokutana na adui, na kuwasingizia uongo wanawake waliotakasika wasiojua
(maovu)."
Hata hivyo inaruhusiwa kukimbia vitani ikiwa idadi ya adui
inazidi idadi ya Waislamu mara mbili. Ama ikiwa idadi yao ni mara mbili tu (si
zaidi) au chini ya hapo, basi ni haramu kukimbia.
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:
ÇáÂäó
ÎóÝøóÝó Çááøåõ Úóäßõãú æóÚóáöãó Ãóäøó Ýöíßõãú ÖóÚúÝðÇ ÝóÅöä íóßõä ãøöäßõã
ãøöÆóÉñ ÕóÇÈöÑóÉñ íóÛúáöÈõæÇú ãöÆóÊóíúäö æóÅöä íóßõä ãøöäßõãú ÃóáúÝñ
íóÛúáöÈõæÇú ÃóáúÝóíúäö ÈöÅöÐúäö Çááøåö æóÇááøåõ ãóÚó ÇáÕøóÇÈöÑöíäó
“Sasa Mwenyezi Mungu
amekukhafifishieni, maana anajua ya kwamba kuna udhaifu (sasa) kwenu (kwa kuwa
vita vimeendelea kwa muda mrefu). Kwa hivyo wakiwa watu mia moja kwenu wenye
subira nawawashinde watu mia mbili kwao; na kama wakiwa elfu moja miongoni
mwenu nawawashinde elfu mbili; kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Na Mwenyezi Mungu yu
pamoja na wanaosubiri (yaani sasa wanaambiwa kila Mwislamu mmoja akabiliane na
makafiri wawili)."
Al Anfal – 66
Imeandikwa katika kitabu cha Al Muhadhab kuwa:
‘Ikizidi idadi ya makafiri juu ya Waislamu kwa
mara mbili basi inajuzu kwao kurudi nyuma na kukimbia, lakini wakiona kuwa
hawatoangamizwa, basi ni bora kwao kukazana barabara mbele ya makafiri na
wasikimbie. Ama wakihisi kuwa watakuja angamizwa, basi hapo watakuwa na hiari
mbili.
1- Inajuzu kukimbia - kwa sababu Mwenyezi Mungu Amesema:
æóáÇó ÊõáúÞõæÇú
ÈöÃóíúÏöíßõãú Åöáóì ÇáÊøóåúáõßóÉö
“Wala
msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.”
Al Baqarah – 195
2- Haijuzu kukimbia – kwa sababu baadhi ya
maulamaa wanaona kuwa udhaifu uliokusudiwa katika aya ni udhaifu wa nguvu na si
wa idadi.
Inajuzu kufanya hadaa na kusema uongo vitani kwa ajili ya
kumbabaisha adui, sharti visitumike (uongo na hadaa) katika kuvunja mikataba na
ahadi.
Mfano wa hadaa ni pale kiongozi anapomhadaa adui akamfanya
adhani kuwa ana jeshi kubwa sana na nguvu nyingi.
Katika hadithi iliyotolewa na Bukhari kutoka kwa Jabir (Radhiya
Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
amesema:
“Vita ni hadaa.”
Na imetolewa na Muslim katika hadithi ya Ummu Kulthum binti
Uqbah (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:
“Sijapata kumsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) akitoa ruhusa ya kusema uongo juu ya jambo lolote lile
katika mazungumzo ya watu isipokuwa katika vita au katika kuleta sulhu baina ya
watu na (pia) mtu anapozungumza na mkewe na mwanamke anapozungumza na mumewe.”
Uislamu umeruhusu vita kama ni jambo la dharura na ukaweka
vipimo maalumu juu yake, kwa mfano;
Asiuliwe isipokuwa anayeshiriki katika vita, ama
aliyejitenga asipigane vita, huyo haijuzu kuuliwa au hata kudhuriwa kwa jambo
lolote.
Imeharamishwa pia kuua wanawake, watoto, wagonjwa, wazee,
maulamaa wa dini, wacha Mungu na waloingia katika sulhu.
Imeharamishwa pia kuuharibu mwili wa aliyeuliwa kwa
kukatwakatwa, kuuwa wanyama, kufisidi mazao, maji, kuvichafua visima na kubomoa
nyumba.
Ni haramu pia kuua majeruhi, na kuendeleza chuki, na hii ni
kwa sababu vita ni mfano wa opreshen ‘operation’, ambapo anachotakiwa tabibu ni
kuyaondoa maradhi tu, na asivuke zaidi ya hapo.
Imehadithiwa na Sulayman bin Buraidah kutoka kwa kuwa Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anapomchagua kiongozi wa
jeshi au wa kikosi, alikuwa akimwita pembeni na kumuusia kumcha Mwenyezi Mungu
yeye pamoja na maaskari wake, kisha akimwambia:
“Piganeni vita kwa jina la Mwenyezi Mungu
katika njia ya Mwenyezi Mungu, piganeni na wanaomkufuru Mwenyezi Mungu,
piganeni lakini msichupe mipaka, wala msifanye khiyana, wala msiwaharibu maiti
kwa kuwakatakata, wala msiuwe watoto.”
Amehadithia Nafia kutoka kwa Abdullah bin Omar
(Radhiya Llahu anhu) kuwa katika baadhi ya vita, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alimkuta mwanamke ameuliwa, akakataza kuuliwa kwa
wanawake na watoto.
Muslim
Amehadithia pia Rawah bin Rabia (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimuona mwanamke ameuliwa
katika mojawapo ya vita alivyoshiriki na huenda akawa ni huyo aliyetajwa katika
hadithi iliyotangulia, akasimama mbele ya maiti hiyo kisha akasema:
“Hapakuwa na haja ya kumuua mwanamke huyu.”
Kisha akawa anaziangilia nyuso za Masahaba wake kisha akamwambia mmoja wao:
“Kamwahi Khalid bin Walid (umwambie); asiuwe
watoto wala mateka wala mwanamke.”
Na katika usia wa Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alompa Usama
(Radhiya Llahu anhu) alipompeleka katika nchi ya Sham alimwambia:
"Msifanye khiyana wala msishambulie bila
taarifa (ghadran), wala msikate kate maiti za adui, wala msiuwe mtoto wala mzee
wala mwanamke, wala msiunguze mtende wala msikate mti unaotoa mazao wala
msichinje mbuzi au n'gome au ngamia ila kwa ajili ya kula. Na mtakutana na watu
waliojitenga ndani ya mahekalu yao kwa ajili ya ibada, basi waacheni hivyo
hivyo walivyo."
Kisha akasema: "Nendeni kwa
jina la Mwenyezi Mungu."
Na usia namna huu alikuwa akitoa Omar bin Khattab (Radhiya
Llahu anhu) na wengine miongoni mwa Makhalifa wa Kiislamu.