Itikadi ya Ahlus Sunnah
Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Aqida ya Ahlus Sunnah ni sahili na nyepesi, haina tabu kufahamika wala haina
mikanganyo. Haina tabu kuisherehesha. Bali inafahamika na
mtu wa kawaida kama inavyofahamika na mtaalamu. Mtu yeyote anaweza kuifahamu kwa wepesi kabisa.
Vitabu vyao vya Hadithi kama
vile Bukhari na Muslim na vingine, pamoja na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) yaliyonukuliwa ndani ya vitabu hivyo na
kuenezwa kila mahali ulimwenguni kwa njia ya isnadi yenye kufuata mfumo na
elimu ya hali ya juu, vitabu hivyo vinakubaliwa na sehemu kubwa sana ya umma
huu na vinatumiwa katika kuitimiza na kuisherehesha sheria ya Mwenyezi Mungu.
Maulamaa wake kama vile Imam
Abu Hanifa na Imam Malik na Imam Shafi na Imam Ahmad bin Hanbal na Ibnil
Mubaraka na Ibni Taymiyah na wenzao wengi wengine wanapendwa na kufuatwa na
asilimia zaidi ya 95 ya Waislamu ulimwenguni, kutokana na elimu yao kubwa na
masharti yao mepesi. Walikuwa daima wakisema: “Ukikuta
katika mafundisho yetu yanayokubaliana na Qur’ani au
Sunnah sahihi, basi yafuateni. Na kama hayakubaliani na hayo
basi yapigeni na ukuta.”
Watu wamedurusu sira zao na
mwenendo wao na elimu yao heshima yao, wakawakubali kama ni Maimamu wao
walioisherehesha Qurani tukufu na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa sallam) kwa njia ya kitaalamu na kwa uhodari mkubwa.
Viongozi wao walipambana na maadui wa Waislamu, wakaweza kuzifungua nchi nyingi sana
na nyoyo nyingi. Walitayarisha majeshi na wapiganaji
walioweza kuziteka nchi kubwa kubwa kuanzia Uturuki, sehemu kubwa ya Uchina na
Urusi. Afghanistan na Africa na Asia na sehemu kubwa
ya Ulaya, na kwa njia hiyo mamilioni kwa mamilioni ya watu waliingia katika
dini hii tukufu.
Walifanikiwa kote huko kuwatoa
watu katika giza la kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuwaingiza katika nuru ya
Uislamu, kuwatoa katika jeuri ya watawala wao, na kuwaingiza katika uadilifu wa
Uislamu, kuwatoa katika kuipenda dunia, na kuwaingiza katika kuipenda akhera
yao, na juu ya kuwa wao ndio walioziteka nchi hizo, lakini wananchi wake
wanandelea mpaka leo kuwapa watoto wao majina ya wafunguzi wale wa Kiislamu.
Utamkuta mtoto wa Kirusi au wa Kituruki au wa Ki Africa au Asia au Ulaya au
hata Marekani akipewa jina la Abubakar au Umar au Aly au Uthman au Muawiyah au
Khalid (Khalid bin Waliyd) au Harun au Salahuddin, nk.
Kutokana na
mafundisho ya maulamaa wao yaliyo mepesi yanayokubalika na akili ya mwanadamu
yeyote wa kawaida, madhehebu haya yalipendwa na kufuatwa na asilimia kubwa sana
ya Waislamu duniani.
Kuthibitisha
Kwa mfano katika kuzithibitisha
sifa za Mwenyezi Mungu, Ahlus Sunnah wanakubali na
kukithibitisha kila Alichokubali na Kukithibitisha Mwenyezi Mungu bila ya
kuchelewesha wala kubadilisha.
Mwenyezi Mungu Anaposema kuwa
Anao Uwezo, na sisi tunaamini kuwa Anao Uwezo.
Anaposema kuwa Anaona, na sisi tunaamini kuwa Anaona
Subhanahu wa Taala.
Anaposema kuwa Anasikia, na sisi tunaamini kuwa Anasikia. Na anaposema kuwa Anayo
macho, na sisi tunaamini kuwa Anayo Macho, Subhanahu
wa Taala, na Anaposema kuwa Anayo Mikono na sisi tunaamini kuwa Anayo Mikono,
na Anaposema kuwa Anao Wajihi, na sisi tunaamini kuwa Anao Wajihi Subhanahu wa
Taala. Lakini macho Yake na mikono Yake na Wajihi wake
na Kuona Kwake na kusikia Kwake hauna mfano wowote na kitu chochote.
áóíúÓó ßóãöËúáöåö
ÔóíúÁñ æóåõæó ÇáÓøóãöíÚõ ÇáÈóÕöíÑõ
Hapana kitu kama
mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona
Ashuuraa-10
Maulamaa wetu wametufundisha
kuzikubali sifa zote za Mwenyezi Mungu bila ya kukisia kwa
akili zetu namna yake au mfano wake. Kwa sababu kuzikataa sifa ambazo Mwenyewe
Amejipa Subhanahu wa Taala, ni makosa, na kuzifananisha sifa hizo pia ni
makosa.
Hapana kitu
kama mfano Wake. Naye ni
Mwenye kusikia Mwenye kuona
Mwenyezi Mungu anaposema:
íóÏõ Çááøóåö ÝóæúÞó ÃóíúÏöíåöãú
Mkono wa Mwenyezi Mungu Uko juu ya mikono yao
Al Fat’h-10
Sisi
tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu Anao Mkono. Kwa sababu Yeye Mwenyewe Subhanahu wa Taala
Amesema hivyo. Lakini hatuufananishi Mkono Wake na
vijikono vyetu.
Anasema mwanachuoni wa Kishia Al Sayed Muhammad Al Huseyniy Al Shiraziy katika
tafisri yake inayoitwa; Taqriyb al Qur’an fil Adh’haan katika kuifasiri aya
hii: “Mkono wa Mwenyezi Mungu Uko juu ya mikono yao.” “Aya
hii inazungumza juu ya Mashaba (Radhiya Llahu anhum) waliofungamana na Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) (chini ya mti), na katika
kufungamana, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
akiutandaza mkono wake huku matumbo ya vidole yakielekea juu, na wanapokuja
wenye kufungamana naye walikuwa wakiweka mikono yao juu ya mkono wa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam.)”
Aya hii ilitemshwa baada ya
Masahaba kufungamana na Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa sallam) walipokuja chini ya ule mti na kuiweka mikono
yao juu ya mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam),
ndipo Mwenyezi Mungu Aliposema;
Mkono wa Mwenyezi Mungu Uko juu ya mikono yao
Al Fat’h-10
Maulamaa wanasema: ‘Mguu wa meza hauwezi kufanana na mguu wa Seremala aliyeichonga
meza hiyo na kutengeneza miguu yake, kama vile mkono wa fundi aliyetengeneza
simu hauwezi kuwa sawa na mkono wa simu. Siku zote sifa za mtengenezaji
haziwezi kufanana na sifa za bidhaa yake.
Na Mwenyezi
Mungu Ndiye Mwenye mifano mikubwa.
Kwa hivyo Anaposema Subhanahu wa Taala kuwa anao
Mkono, na sisi tunakubali kuwa Anao Mkono lakini hatuufananishi na mikono wetu,
kwa sababu sifa za Muumba haziwezi kufanana na sifa za viumbe
Na katika aya nyingine Mwenyezi
Mungu anamuuliza Ibilisi:
ÞóÇáó
íóÇ ÅöÈúáöíÓõ ãóÇ ãóäóÚóßó Ãóä ÊóÓúÌõÏó áöãóÇ ÎóáóÞúÊõ ÈöíóÏóíøó ÃóÓúÊóßúÈóÑúÊó
Ãóãú ßõäÊó ãöäó ÇáúÚóÇáöíäó
Ewe
Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa
mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
Saad- 75
Sisi
tunaamini kuwa; kwa vile Mwenyezi Mungu amesema kuwa
Amemuumba Adam kwa mikono yake basi haiwezekani kuwa amekusudia kuwa amemuumba
kwa njia nyingine.
Ndani
ya Qur’ani tukufu Mwenyezi Mungu Anazungumza na watu
wa kila aina, wenye elimu na wasiokuwa na elimu. Na kusudi Lake Subhanahu wa Taala ni kuwafundisha watu hao waijuwe dini yao, juu ya
hitilafu ya ufahamu wao. Kwa hivyo haiwezekani Azungumze nao kwa
njia ya mafumbo au majazi akawa anasema neno huku akikusudia jambo au neno
lingiine.
Mwenyezi
Mungu angelitaka kusema kuwa amemuumba mwanadamu kwa
Kudra Yake, kwa mfano; basi Angelisema tu, pasingekuwa na haja ya kuutaja
mkono.
Na
katika aya nyingine pia Mwenyezi Mungu Anasema:
Ãóæóáóãú
íóÑóæúÇ ÃóäøóÇ ÎóáóÞúäóÇ áóåõãú ãöãøóÇ ÚóãöáóÊú ÃóíúÏöíäóÇ ÃóäúÚóÇãðÇ Ýóåõãú
áóåóÇ ãóÇáößõæäó
Je!
Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono
yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.
Yasin - 71
Na
hivi ndivyo ilivyo katika sifa Zake zote Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, kila Anapozitaja, ni juu yetu kusema: ‘Sam’an wa
ta’an’, tuzikubali bila kubabaisha maana yake wala kubadilisha wala
kufananaisha sifa hizo na sifa za viumbe.
Kwa
mfano Mwenyezi Mungu Anaposema:
ÅöäøóãóÇ
ÃóãúÑõåõ ÅöÐóÇ ÃóÑóÇÏó ÔóíúÆðÇ Ãóäú íóÞõæáó áóåõ ßõäú Ýóíóßõæäõ
Hakika
amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na
kikawa
Yasin -71
Tunapoisikia
kauli hiyo ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala,
hatuna budi kuikubali na kuiamini. Kwa nini? Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mwenyewe Amesema hivyo. Ikiwa
Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Hasemi, kwa nini
basi alisema kuwa; hukiambia tu: Kuwa! Na kikawa?
Na
katika aya nyingine Mwenyezi Mungu Anasema:
æóßóáøóãó
Çááøåõ ãõæÓóì ÊóßúáöíãðÇ
Na Mwenyezi Mungu alinena
na Musa kwa maneno.
Annisaa - 164
Bali
hata Qurani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu
Subhanahu wa Taala. Mwenyezi Mungu Anasema:
æóÅöäú ÃóÍóÏñ ãøöäó ÇáúãõÔúÑößöíäó
ÇÓúÊóÌóÇÑóßó ÝóÃóÌöÑúåõ ÍóÊøóì íóÓúãóÚó ßóáÇóãó Çááøåö Ëõãøó ÃóÈúáöÛúåõ ãóÃúãóäóåõ Ðóáößó
ÈöÃóäøóåõãú Þóæúãñ áÇøó íóÚúáóãõæäó
Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi
mpe ulinzi apate kusikia maneno ya
Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala
pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu
wasiojua kitu.
At Tawba - 6
Wengine wanasema kuwa Mwenyezi Mungu hakusudii hivyo, bali hayo ni majazi tu. Na maana yake ni kuwa Anaposema kuwa
Anasikia, hakusudii kuwa Anasikia kweli bali hayo ni majazi tu, na Anaposema
kuwa Anaona hakusudii kuwa Anaona kweli bali hayo ni majazi tu, na Anaposema
kuwa Anayo macho, hakusudii kuwa Anayo macho, bali hayo ni majazi tu, na Anaposema
kuwa Anayo mikono hakusudii kuwa Anayo mikono bali hayo ni majazi tu, na
anaposema kuwa Anao wajihi hakusudii kuwa Anao wajihi kikweli bali hayo ni
majazi tu…… SubhanaLlah!!!
Sisi tunasema; Majazi yapo, lakini majazi ni
kwa mfano mtu shujaa akaitwa Simba, au mtu muovu akaitwa nyoka nk. Haya ni majazi. Lakini maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyotuletea waja
wake kwa ajili ya kutufundisha dini yetu na kutujulisha sifa Zake Subhanahu wa Taala , hayawezi kuingia katika mfumo huu. Ni maneno ya kiarabu yasiyokwenda upande. Lugha ya kiarabu safi kabisa.
Mwenyezi Mungu Anasema:
ÞõÑÂäðÇ
ÚóÑóÈöíøðÇ ÛóíúÑó Ðöí ÚöæóÌò áøóÚóáøóåõãú íóÊøóÞõæäó
Qur'ani
ya Kiarabu isiyo na upogo (isiyokwenda upande), ili
wamche Mungu
Azzumar-28