ni rahisi sana, nayo ni
kushindana naye katika kufanya ibada na katika mambo mema, na kwa njia hii
ataipata sifa kama ya mwenzake na atakuwa ameshindana naye kwa njia
zilizoruhusiwa na sheria kama alivyosema MwenyeziMungu Subhaanahu wa Taala:
æóÝöí Ðóáößó
ÝóáúíóÊóäóÇÝóÓö ÇáúãõÊóäóÇÝöÓõæäó
"Na katika
haya washindane wenye kushindana".
Al
Mutafifiyn aya ya 26:
Wengine
wanapotuhumiwa juu ya makosa au ila fulani, utawasikia
wakijibu kwa haraka:
“Hata fulani pia anafanya hivyo”
Mtu huyu ilimpasa ajitetee nafsi yake bila kuwafedhehesha wengine.
Mwengine
utamsikia akizungumza juu ya masaibu yaliyomfikia mwenzake kwa kusema kwa mfano:
“Maskini fulani mambo yamezidi kuwa magumu kwake, namuonea
huruma”, kisha utamsikia akilitaja jina la mtu huyo
aliyefikiwa na masaibu.
Huenda
akawa mkweli katika kumuonea huruma mwenzake, lakini nia yake nzuri haimpi
uhuru wa kuzungumza juu ya mtihani wa mwenzake mbele ya
watu, hasa ikiwa hapana udhuru wowote wa kuyazungumza.
Siku
zo4"/>
Kujipendekeza Kujikurubisha Kujiona Baadhi
ya hadithi Yayoruhusiwa Yanayofaa kuchungwa Yasiyodhaniwa Shukrani
zote ni zake Allah. tunamshukuru,
tunamtegemea, tunafuata uongofu Wake na tunajilinda kwake kutokana na shari za
nafsi zetu na amali zetu zilizo ovu. Atakayeongozwa na
MwenyeziMungu hapana wa kumpotosha (kumpoteza), na atakayeachwa kupotea kwa
sababu ya kukataa kwake kufuata uongofu, hatopata wa kumuongoza. Ninashuhudia
ya kwamba Hapana Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah na
kwamba Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni mja wake na Mtume wake na
kipenzi chake mbora wa viumbe vyote. Ameutimiza Ujumbe, ameifikisha Amana,
amewanasihi Umma na amepigana Jihadi kwa ajili ya dini
ya MwenyeziMungu kama inavyopaswa. Mola
wetu zifikishe swala na salaam zetu kwa kipenzi chako
huyu Al Habiyb Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) uliyemsifia katika
kitabu chako kitukufu Ulipomwambia: æóÅöäøóßó áóÚóáì
ÎõáõÞò ÚóÙöíãò "Na bila
shaka una tabia njema kabisa." Al
Qalam-4 Kusudi
la kuandika makala haya lilikuwa ni kuandika maudhui
ya Ghiyba (kusengenya), kwani hayo ni maradhi yaliyoukumba umma, na wengi
hawafahamu hatari yake na namna yanavyoweza kumpotezea mtu thawabu zake zote
alizochuma kwa tabu ya kukesha huku akiswali na kufunga na kutoa sadaka na
kusoma Qurani nk. ÇÍÝÙ
áÓÇäß ÇíåÇ ÇáÇäÓÇä – áÇ íáÏÛäß Çäå ËÚÈÇä Chunga
mwanangu chunga Lisije
kukuponyoka Usije
ukakudunga Kwani
ulimi ni nyoka Kusudi
langu ni kubainisha hatari inayotokana na ulimi pamoja na shari zake na kufahamisha
namna ya kuyatibu maradhi haya pamoja na kusherehesha yale ambayo kwa ajili ya
ulimi yatampeleka mtu ima katika faida kubwa na radhi za Mwenyezi Mungu hapa
duniani na huko akhera, au katika hasara kubwa na ghadhabu za Mwenyezi Mungu
katika nyumba mbili hizo za Dunia na Akhera. Kusengenya
ni maradhi yanayoondoa mapenzi na kuleta chuki baina
ya ndugu, rafiki, jamaa, na hatimaye yanakula thawabu za mtu na kuzimaliza kama
moto unavyokula kuni. Mtume(Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Yamekufikieni maradhi ya waliokuja kabla yenu, Husda na chuki. Maradhi hayo ndiyo yanayonyoa,
yananyoa dini hayanyowi nywele. Naapa kwa yule
ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hamuingii Peponi mpaka muamini, na
hamuamini mpaka mpendane. Nikuambieni ni jambo gani
mkilifanya mtapendana? Enezeni (salam) amani baina
yenu". Ahmed
- Attirmidhy na Al Bazzar Kama
nilivyosema kuwa nilitaka kuandika juu ya maudhui ya Ghiyba peke yake, lakini kwa vile aya ya Ghiyba ndani ya Qurani inashamili mambo
matatu mengine, na yote ni muhimu sana katika jamii ya Kiislam, nikaona itakuwa
vyema kama nitazungumzia juu ya kila jambo angalau kwa uhaba, kisha nikamilishe
kwa kuyasherehesha vizuri maudhui haya ya Ghiyba - (kusengenya). Mwisho,
namuomba Mwenyezi Mungu aninufaishe mimi na
atunufaishe sote katika somo hili na aijaalie iwe hoja kwa ajili yangu siku ya
Kiama na isiwe hoja dhidi yangu, kwani Yeye ni Muweza wa kila kitu. Maana
ya neno 'Dhana' ni mtu kufasiri vibaya matendo au
maneno ya mwenzake kama anavyodhania yeye, kisha akaiendekeza nafsi yake na
kuyakubali yale aliyoyadhania akaamini kuwa ndio ukweli wenyewe na kuyasadiki. Wanaopenda
kuwadhania wenzao vibaya mara nyingi huwa ni dalili
kuwa wao ni watu wenye tabia mbaya, na kwa kawaida mwenye mwenendo mbaya siku
zote hudhania kuwa wenzake wote ni sawa naye. Mwenyezi
Mungu Anasema: íóÇ ÃóíøõåóÇ
ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ ÇÌúÊóäöÈõæÇ ßóËöíÑðÇ ãøöäó ÇáÙøóäøö Åöäøó ÈóÚúÖó ÇáÙøóäøö
ÅöËúãñ æáÇ ÊóÌóÓøóÓõæÇ æóáÇ íóÛúÊóÈ ÈøóÚúÖõßõã ÈóÚúÖðÇ ÃóíõÍöÈøõ ÃóÍóÏõßõãú Ãóä
íóÃúßõáó áóÍúãó ÃóÎöíåö ãóíúÊðÇ ÝóßóÑöåúÊõãõæåõ æóÇÊøóÞõæÇ Çááøóåó Åöäøó
Çááøóåó ÊóæøóÇÈñ ÑøóÍöíãñ "Enyi mlioamini!
Jiepusheni sana na (kuwadhania watu) dhana (mbaya)
kwani (kuwadhania watu) dhana (mbaya) ni dhambi. Wala
msipeleleze (habari za watu) Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine.
Je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?
La, Hampendi; (Basi na haya msiyapende). Na Mcheni MwenyeziMungu. Bila shaka MwenyeziMungu ni Mwenye kupokea toba (na) Mwingi wa kurehemu". Hujuraat
- 12 Katika
aya hizi MwenyeziMungu anatuamrisha tuepukane na
maradhi matatu yafuatayo:- 1.
Kudhania waislamu
wenzetu Dhana mbaya. 2.
Kupeleleza habari za
watu. 3.
Kusengenyana wenyewe kwa wenyewe. Kisha
MwenyeziMungu Subahanahu wa Taala akaikamilisha aya
kwa kutufahamisha kuchukizwa kwake na wafanyao maasi hayo yanayoondoa heshima
na mapenzi baina ya Waislamu kwa kumfananisha anayefanya maovu hayo na mtu
mbaya, mchafu, muovu, anayekula mzoga wa nyama ya ndugu yake aliyekwisha kufa. Anasema
Imam Al Zamakhshariy: "Kumdhania vibaya mtu wa kawaida au mtu anayejulikana kwa
wema wake ni haram, lakini si haramu kumdhania vibaya mtu anayejulikana kuwa ni
asi mwenye kufanya uasi wake dhahir shahir bila kumuogopa Mwenyezi Mungu wala
kuwastahi wanadamu wenzake, tena bila kujificha wala kuona haya, na hii ni kwa
sababu mtu wa aina hii yeye mwenyewe anakuwa keshajidhihirisha ubaya wake. Ama yule anayejisitiri, haijuzu kumdhania vibaya". Anasema
Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu): "Usilidhanie neno lililotoka kinywani mwa ndugu yako
Muislam kuwa amelikusudia vibaya, bali ulidhanie kuwa alikusudia kheri tu huku
ukilitafutia (neno hilo) udhuru wowote wa kheri unaoweza kulibeba ". Kutoka
kwa Abu Huraira (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Jiepusheni na dhana mbaya, kwani
hakuna uongo mkubwa kuliko dhana mbaya, na wala msipelelezane wala msibishane
wala msihusudiane wala msichukiane wala msiendeane kinyume, na kuweni enyi waja
wa Mwenyezi Mungu mfano wa ndugu". Bukhari
na Imam Malik Na
katika riwaya nyingine iliyopokelewa na Muslim na
Attirmidhy imekuja hadithi hii hii ikiwa na ziada ifuatayo: "Na wala si halali kwa Muislam kumpiga pande
(asimsemeshe) ndugu yake (Muislam) kwa muda wa siku tatu". Na
katika riwaya nyingine kutoka kwa Bukhari inasema: "Jiepusheni na dhana mbaya, kwani
hakuna uongo mkubwa kuliko dhana mbaya, na wala msipelelezane wala msibishane
wala msihusudiane wala msichukiane wala msiendeane kinyume, na kuweni enyi waja
wa Mwenyezi Mungu mfano wa ndugu kama alivyokuamrisheni (Mola wenu). Muislam ni ndugu wa Muislam, asimdhulumu, asimuache bila kumsaidia,
asimdharau, taqwa ipo hapa taqwa ipo hapa (akawa anaashiria kifuani pake).
Inatosha peke yake kuwa shari kubwa mtu kumdharau
Muislam mwenzake. Kila kitu baina ya Muislam na
Muislam ni haramu, damu yake, heshima yake na mali yake. Hakika Mwenyezi Mungu
haiangalii miili yenu wala sura zenu, bali anaangalia
ndani ya nyoyo zenu na matendo yenu". Bukhari Kutoka
kwa Haritha bin Noaman (Radhiya Llahu anhu) amesema
kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Mambo matatu si rahisi kuepukana nayo Umati wangu, Kuamini
nukhsi, (kuwa na) husda na (kudhania) dhana
mbaya". Mtu mmoja akamuuliza: "Tufanye nini ili tuepukane nayo
ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema: "Ukihusudu, sema; 'Astaghfirullah', ukimdhania mtu
dhana mbaya, usitake kumchunguza, na ukiamini kuwa jambo lina nukhsi, basi
lifanye tu (na umtegemee Mwenyezi Mungu)". Attabarani Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika hadithi hii
anatutahadharisha na mambo matatu pamoja na kutufundisha namna ya kuepukana nayo. Mambo
yenyewe ni; 1.
Kuamini Nukhsi 2.
Husda 3.
Dhanna mbaya Kuamini
'Nukhsi' ni tatizo kubwa lililoenea sehemu zote
ulimwenguni. Wapo wanaoamini kuwa baadhi ya nambari kama
vile nambari 13 zina nukhsi na hawakubali kuitumia nambari hiyo katika shughuli
zao zote. Hawakubali hata kuiandika nambari hiyo juu ya milango ya nyumba zao
au katika viti vya ndege, bali wengine hawakubali
kuvaa jezi za mpira zinazobeba nambari hiyo, nk. Wapo
wasiokubali kufunga safari yoyote ile siku ya terehe 13, na
ikisadifu tarehe hiyo kuwa siku ya Ijumaa, basi wanaitakidi kuwa nukhsi yake
itakuwa kubwa zaidi, na kwa ajili hiyo hawatoki hata majumbani mwao. Wengine
wanaamini kuwa baadhi ya siku kama vile Jumaane nk. zina nukhsi kusafiri ndani yake, na wengine wakikumbana na
paka mweusi njiani, huivunja safari na kurudi makwao. Hofu
za namna hii zilizoingia ndani ya nyoyo katika kuviogopa viumbe alivyoviumba
Mwenyezi Mungu au kuziogopa siku alizoziumba Mwenyezi Mungu, ni
dalili ya udhaifu wa imani na upungufu wa Itikadi sahihi, nayo ni kuamini kuwa
hapana anayeweza kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa
Taala. Þõá áøóä íõÕöíÈóäóÇ
ÅöáÇøó ãóÇ ßóÊóÈó Çááøåõ áóäóÇ åõæó ãóæúáÇóäóÇ æóÚóáóì Çááøåö ÝóáúíóÊóæóßøóáö
ÇáúãõÄúãöäõæäó "Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia
Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu!" At Tawbah - 51 'Husda',
maana yake ni kutamani neema aliyoipata mwenzio
imuondoke. Mfano
mzuri ni pale mtu anapopandishwa cheo kazini kisha
mwenzake anayefanya kazi naye akaona kuwa cheo kile alistahiki kukipata yeye. Kibinadamu
hili ni jambo la kawaida. Lakini mtu huyo anapoanza
kutamani mwenzake anyanganywe cheo alichokipata au afukuzwe kazi au apatwe na masaibu yoyote, muhimu cheo kile kimuondokee na akipate
yeye. Hiyo ndiyo 'Husda'. Huo ni mfano mmoja tu, na mara nyingine mtu humhusudu mwenzake
bila sababu yoyote. Kutokana
na 'Husda' yake, hasidi anaweza kudhurika yeye mwenyewe kwa kupata maradhi
mbali mbali kama vile maradhi ya moyo na shinikizo la damu, 'blood pressure'
au maradhi ya kisukari na mengineyo yanayosababishwa na kuathirika kwa moyo na
nafsi kutokana na kusugulika mtu roho yake huku akijiunguza kwa uchungu wa
husda. Ndiyo
maana Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akatufundisha kuomba Maghfira kwa Mwenyezi Mungu mara inapompitikia mtu husda
moyoni mwake ili asiiendekeze nafsi yake na kuendelea na husda yake
itakayomdhuru mwenyewe na kumpatia madhambi pamoja na maradhi mabaya kama hayo. Katika
hadithi iliyotangulia, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) aliposema: "Ukihusudu, sema;
'Astaghfirullah', alikusudia kuwa zinapoanza kumpitikia mtu fikra kama
hizo za kutaka neema aliyoipata mwenzake imuondokee, basi haraka aombe maghfira
kutoka kwa Mola wake, kwani Mwenyezi Mungu anayajuwa yote yanayotupitikia
nyoyoni mwetu. Mwenyezi
Mungu anasema: æóÑóÈøõßó íóÚúáóãõ
ãóÇ Êõßöäøõ ÕõÏõæÑõåõãú æóãóÇ íõÚúáöäõæäó "Na Mola wako anayajua yanayoficha vifua vyao na
wanayoyadhihirisha". Al
Qasas - 69 Mtu
anapoomba maghfira kwa Mola wake maana yake ni kuwa
amelitambua kosa lake na kwamba hatorejea tena kulifanya kosa hilo. Na kutokana
na hayo, mtu huyo ataacha kumuonea husda mwenzake,
atarudi kwa Mola wake Mwenye kusababisha yote hayo, na kumuomba Yeye tu Subhanahu
wa Taala ampatie cheo kama kile au daraja kama ile ikiwa vitu hivyo vina kheri
naye, au akinai na kile alichokuwa nacho. Maana
yake ni kufuatilia habari za watu kwa nia ya kutaka
kujua habari zao, au aibu zao au makosa yao. Tabia hii ni
kinyume kabisa na mafundisho ya Kiislam yanayotutaka tujishughulishe na
kufuatilia na kuyachunguza makosa yetu wenyewe na kujirekebisha ili
tusiyarudie tena, kwani hapana mtu asiyefanya makosa au asiyekuwa na aibu. Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Enyi mlioamini kwa ndimi zenu na
ambao imani haijaingia ndani ya nyoyo zenu! Msiwasengenye Waislam wala
msifuatilie kutaka kujua makosa yao, kwa hakika yule
anayefuatilia makosa ya Waislam, na Mwenyezi Mungu atafuatilia makosa yake, na
yule ambaye Mwenyezi Mungu atafuatilia makosa yake, basi atamfedhehesha hata
ndani ya nyumba yake". Abu
Daud - Attirmidhy na Abu Yaala - imesahihishwa na Sh.
Al Albani Kupeleleza
habari za watu ni katika dhambi kubwa sana
iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu Aliposema: æáÇ ÊóÌóÓøóÓõæÇ "Wala msipeleleze (habari
za watu)". Imepokelewa
kuwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Mtu anayesikiliza maneno ya watu huku wenyewe wakichukizwa
(bila idhini yao), atamiminiwa sikioni mwake shaba
(imoto iliyoyeyushwa) Siku ya Kiama". Bukhari Imepokelewa
pia kuwa usiku mmoja Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alipokuwa katika
zamu akilinda mji yeye na Abdulrahman bin Auf (Radhiya
Llahu anhu) alipita nje ya nyumba inayowaka taa na kusikia watu wakizungumza
kwa sauti za juu. Umar
akamuuliza Abdulrahman: "Unaijua nyumba ya nani hii? Abdulrahman (Radhiya Llahu anhu) akajibu: "Sijuwi". Umar (Radhiya Llahu anhu) akamwambia: "Hii ni nyumba ya Rabia bin Umayya na
waliomo ndani hivi sasa wanakunywa pombe. Unasemaje?" Abdulrahaman (Radhiya Llahu anhu) akasema: "Mimi naona kuwa sasa tumefikia pale alipokataza
Mwenyezi Mungu áÇ ÊóÌóÓøóÓõæÇ(Wala msipelelezane). Wakaondoka
wote wawili na kuelekea kwengine Kutoka
kwa Muawiya bin Abu Sufyan (Radhiya Llahu anhu)
amesema: "Nilimsikia
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema: "Ukianza kufuatafuata kupeleleza juu ya mambo ya Waislam
basi utawafisidi". Abu
Daud Kutoka
kwa Yaziyd amesema: "Mtu mmoja alikamatwa na kupelekwa
mbele ya Abdillahi bin Masaud (Radhiya Llahu anhu) akishtakiwa kuwa ndevu zake
mtu huyo zilikuwa zimerowa na kuchururika ulevi na kwamba zinanuka harufu ya ulevi.
Abdillahi bin Masaud (Radhiya Llahu anhu) akasema: "Hakika sisi tumekatazwa kupeleleza, lakini jambo
lolote likitudhihirikia lazima tulichukulie hatua". Abu
Daud Kusengenya
ni tatizo kubwa lililowakumba Waislamu wakiwemo hata
baadhi ya wanavyuoni. Kutokana
na chuki inayosababishwa na kusengenyana baina ya waislamu pamoja na mfarakano
mkubwa unaopatikana baina yao, ukijumlisha na hasara inayopatikana kutokana na
mfarakano huo, nimeona bora niyachambue zaidi maudhui haya ya Ghiyba huku
tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie katika kupunguza ukali wa Moto huu, na atujaalie
tuifahamu vizuri darsi hii na atupe uwezo wa kuyatekeleza maamrisho yake - Amin. Moto, ni jina linalofaa kuliita tatizo hili, kwa sababu kusengenya,
kunaziunguza thawabu za mtu aliyehangaika kuzichuma kwa Kuswali na Kufunga na kutoa
Zaka na kusoma Qurani na mengineyo kama moto unavyokula kuni. Ulimi
ulionolewa kwa ajili ya kusengenya watu ni sababu kubwa ya mtu kupoteza thawabu
zake alohangaika kuzichuma kwa tabu na pia ni sababu kubwa ya watu kutumbukizwa
kwa wingi katika Moto wa Jahannam kama alivyotufahamisha Mtume wa MwenyeziMungu
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika hadithi ya Muadh bin Jabal (Radhiya
Llahu anhu) iliyoshamili mambo yote muhimu katika dini na namna gani mtu
anavyoweza kuzipoteza thawabu zake zote hizo baada ya kuhangaika kufanya yote
anayotakiwa kuyafanya. Hebu
tumsikilize Muadh mwenyewe (Radhiya Llahu anhu) akituhadithia juu ya mazungumzo
yaliyopita baina yake na sahibu yake Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Muadh
bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) amesema: "Nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu; nitajie amali itakayoniingiza Peponi na itakayoniweka mbali na moto.
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema: ((Hakika umeuliza juu ya jambo kubwa mno, nalo ni jepesi kwa mwenye kuwepesishiwa kwalo na MwenyeziMungu
aliyetukuka. Umuabudu MwenyeziMungu na usimshirikishe
na chochote na usimamishe Swala na utoe Zaka na ufunge Ramadhani na uikusudie
kwa Hijja nyumba (ya MwenyeziMungu) ukiweza kuifikia)). Kisha akasema: ((Je nikujulishe pia na milango ya
kheri? Saumu humkinga mtu na moto, na Sadaka huzima
madhambi kama maji yanavyozima moto, na Swala ya mtu katikati ya usiku)). Kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akaisoma aya za 16 na 17 Suratul Sajdah; (("Huinua mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku ili kumuabudu Mola wao kwa kuogopa Moto na kutaraji
Pepo; na hutoa (Zaka na sadaka) katika yale Tuliyowapa. Nafsi yoyote haijui
waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho (huko Peponi)); Kisha akasema: ((Je nikujulishe nini kichwa cha jambo na
nguzo yake na kilele chake?)) Nikasema: "Ndiyo ewe Mtume wa
MwenyeziMungu". Akasema: ((Kichwa cha jambo ni Uislamu na nguzo
yake ni Swala na kilele chake ni Jihadi)). Kisha akasema: ((Je nikujulishe kisimamio cha yote hayo?)) Nikasema: "Ndiyo ewe Mtume wa
MwenyeziMungu". Akaushika ulimi wake, kisha akaniambia: ((Ufunge huu juu yako)). Nikasema: "Ewe Mtume wa MwenyeziMungu kwani sisi ni wenye
kuhesabiwa kwa tunayoyasema?" Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema: ((Amekukosa mama yako ewe Muadh, unadhani kwa sababu gani
watu watatupwa kwa nyuso zao katika Moto (Jahanam) isipokuwa kwa yale
yaliyochuma ndimi zao?))." Imesimuliwa
na Attirmidhy na akasema ni hadithi njema na sahihi Katika
hadithi hii Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anamfahamisha sahibu yake na
kipenzi chake Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) juu ya mambo yaliyo muhimu
katika Uislam moja baada ya jingine kufuatana na daraja zake. Ameanzia
juu ya ubaya wa shirki, kisha juu ya nguzo za dini, kama vile Swala na Zaka,
Kufunga na Kuhiji, kisha akamjulisha juu ya kheri inayotakiwa kupigiwa hodi
mara kwa mara, nayo ni funga za Sunnah zinazomkinga mtu na moto, pamoja na
kutoa sadaka kuwasaidia masikini, na kwamba sadaka hizo hufuta madhambi kama
maji yanavyozima moto, na kwamba Swala nyakati za usiku zinamnyanyua mtu daraja
za juu. Baada
ya kumjulisha juu ya yote hayo, akamfahamisha kuwa 'Kichwa cha jambo ni Uislamu', akimaanisha kwamba Muislamu anatakiwa kuuweka
Uislamu mbele kuliko jambo lake lolote lile na kwamba asikubali kutenda jambo
au kutii amri yoyote ile inayokwenda kinyume au kupingana na dini ya Kiislamu. Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimwambia Muadh (Radhiya Llahu anhu) kuwa haya
yote ni mfano wa nyumba na kama ilivyokuwa nyumba haisimami bila ya nguzo, basi
Muislamu bila ya kutimiza nguzo za Uislam kwa kuswali na kutoka zaka na kufunga
na kuhiji kwa mwenye uwezo, basi hawi Muislamu wa kweli. Kisha
akaendelea kumfahamisha Sahaba wake huyo (Radhiya Llahu anhu) kwamba kilele cha
Uislamu ni Jihadi. Na maana yake ni kuwa heshima ya
mpiganaji Jihadi iko juu, 'Kileleni', na hii ni kwa sababu Umma wa Kiislamu ni
Umma wa Jihadi ambayo kwayo tu ndiyo umma utaheshimiwa, na kwamba umma
utakapoiacha Jihadi na kuyakimbilia maisha ya dunia, basi utadhalilika. Mwisho
akamtahadharisha kuwa baada ya kutenda yote hayo na
kuzikusanya thawabu zake, itambidi aufunge ulimi wake, ama sivyo utakuja
kumpotezea thawabu zake zote na kusababisha kutumbukizwa ndani ya Moto wa Jahannam
juu mema yake aliyotenda katika Kufunga na Kuswali na kutoa Zaka na Kuhiji na
kupigana Jihadi. Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwauliza Masahaba (Radhiya
Llahu anhum): "Mnajua nini maana ya kusengenya (Ghiyba)?
" Wakasema: "MwenyeziMungu na Mtume wake wanajua zaidi." Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema: "Kusengenya, ni kuzungumza juu ya
nduguyo (Muislam) yale asiyoyapenda". Akaulizwa: "Unaonaje ikiwa ninayoyasema anayo kweli?" Akasema: "Ikiwa anayo kweli basi huko ndiko kusengenya, na
ikiwa hanayo basi hayo ni madhambi makubwa zaidi (kwa kumsingizia uongo)". Muslim Maulamaa
wote wamekubaliana kuwa Kusengenya ni Haramu na ni
katika madhambi makubwa (Kabair). Amesema
Ibni Kathiyr katika tafsiri yake: "Ghiyba (Kusengenya), ni haramu
pasipo na hitilafu baina ya maulamaa na hasameheki yeyote anayesengenya
isipokuwa ikiwa nia ya kusengenya huko iwe kwa ajili ya kupinga ushahidi wa
dhulma au kusahihisha makosa au katika kutoa nasaha". Anasema
Imam Al Qurtubiy: "Hapana hitilafu yoyote baina ya maulamaa kwamba kusengenya
ni katika madhambi makubwa, na atakayefanya kosa hilo
lazima atubu kwa Mola wake". Na hii ndiyo maana Mwenyezi Mungu Subhanahau wa
Taala akasema: "Je! Mmoja wenu
anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La, Hampendi; (Basi na haya
msiyapende)". Kama
ilivyokuwa hapana kitendo kibaya kuliko mtu kula nyama ya ndugu yake aliyekufa
asiyeweza kujitetea, basi hivyo hivyo hapana kitendo kibaya kuliko mtu
kumsengenya ndugu yake asiyekuwepo na kwa ajili hiyo hana
uwezo wa kujitetea". Na
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema: "Lililo baya zaidi kuliko mtu kula riba ni
kule kuendelea kwa mtu kuzungumza juu ya makosa ya nduguye". Attabarani MwenyeziMungu
ameitukuza heshima ya mwanadamu pale alipowaamrisha Malaika wake watukufu
wasiomuasi wamsujudie baba yao Adam (alayhi ssalaam),
kisha akamtukuza kwa kumruzuku vitu vizuri vizuri na kumwezesha kupanda
vipandio vya barani na baharini. Mwenyezi
Mungu anasema: æóáóÞóÏú ßóÑøóãúäóÇ
Èóäöí ÂÏóãó æóÍóãóáúäóÇåõãú Ýöí ÇáúÈóÑøö æóÇáúÈóÍúÑö æóÑóÒóÞúäóÇåõã ãøöäó
ÇáØøóíøöÈóÇÊö æóÝóÖøóáúäóÇåõãú Úóáóì ßóËöíÑò ãøöãøóäú ÎóáóÞúäóÇ ÊóÝúÖöíáÇð "Na hakika tumewatukuza
wanaadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini na tumewaruzuku vitu
vizuri vizuri na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba kwa utukufu
ulio mkubwa (kabisa)". Bani
Israil - 70 Kutoka
kwa Abdillahi bin Umar bin Khattab (Radhiya Llahu
anhu) alisema kwamba siku moja alimuona Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akitufu
huku akisema kuiambia Al Kaaba: "Uzuri ulioje ulio nao, uzuri ulioje wa harufu yako. Utukufu ulioje wako na wa Heshima
yako. Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad imo
mikononi mwake kwamba Heshima ya Muislamu ni tukufu zaidi mbele ya
MwenyeziMungu kuliko heshima yako". Ibni
Majah Huu
ndio utukufu wa heshima ya Muislamu mbele ya
MwenyeziMungu, na hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akaharamisha kuvunjiwa
heshima hiyo kwa kudhulumiwa, kudhaniwa vibaya, kupelelezwa na kusengenywa. Kabla
mtu hajaufungua mdomo wake kuanza kuzungumza juu ya makosa ya ndugu yake,
inampasa akumbuke kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: ãóÇ íóáúÝöÙõ ãöä
Þóæúáò ÅáÇ áóÏóíúåö ÑóÞöíÈñ ÚóÊöíÏñ "Hatoi
kauli yoyote isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari (kuandika)". Qaf
- 18 Na
kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema: Åöäøó ÇáÓøóãúÚó
æóÇáúÈóÕóÑó æóÇáúÝõÄóÇÏó ßõáøõ ÃõæáÜÆößó ßóÇäó Úóäúåõ ãóÓúÄõæáÇð "Hakika
masikio na macho na moyo hivyo vyote vitaulizwa". Al
Israa - 36 Na
hii ni kwa sababu Muislam anaamini kuwa macho
aliyopewa na Mola wake pamoja na ulimi na masikio, vyote hivyo ni amana na
kwamba siku moja ataulizwa juu yake. Bali Muislam anatakiwa avitumie viungo
hivyo katika mambo yanayomridhisha Mola wake, na kwa ajili hiyo pale anapoona
mazungumzo yanageuka kuwa kusengenya watu (kuzungumza habari za watu), akataze
na ikiwa hawamsikii basi ajitenge nao, kwa sababu dhambi anapata msemaji na
msikilizaji pia kama tutakavyoona kila tukiendelea mbele. Mwenyezi
Mungu anasema: æóÅöÐóÇ ÓóãöÚõæÇ
ÇááøóÛúæó ÃóÚúÑóÖõæÇ Úóäúåõ æóÞóÇáõæÇ áóäóÇ ÃóÚúãóÇáõäóÇ æóáóßõãú ÃóÚúãóÇáõßõãú
ÓóáÇãñ Úóáóíúßõãú áÇ äóÈúÊóÛöí ÇáúÌóÇåöáöíäó "Na wanaposikia upuzi hujitenga
nao na husema (kuwaambia wapuuzi hao),; 'Sisi tuna
vitendo vyetu (amali zetu) na nyinyi mna vitendo vyenu, amani juu yenu
(inayotokana na sisi - hamtasikia kwetu baya). Sisi hatutaki (kujibizana na) watu wajinga". Al
Qasas 55 Na
Akasema: ó æóÅöÐóÇ ãóÑøõæÇ
ÈöÇááøóÛúæö ãóÑøõæÇ ßöÑóÇãðÇ "Na
wanapopita penye upuzi hupita kwa hishima (yao)". Al
Furqan - 72 Anasema Bi bi Aisha (Radhiya
Llahu anha): "Siku moja nilimwambia Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam): "Muangalie Swafia yuko hivi". (Akaashiria kwa mkono wake kuonyesha
kuwa ni mfupi). Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamwambia: "Umetamka neno, lingechanganywa na
maji ya bahari basi maji yangebadilika". Huyu
ni Mke wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), mama wa Waislam (Radhiya Llahu
anha), alipoashiria tu kwa mkono bila ya kutamka kwa ulimi wake, akikusudia
kuwa mke mwenzake Bibi Swafiya binti Huyay (Radhiya Llahu anhu) ni mfupi, - juu
ya kuwa bibi Swafiya (Radhiya Llahu anha) alikuwa ni mfupi kweli, lakini Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alimkataza Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) na kumfahamisha
kuwa kufanya hivyo ni katika kusengenya na kwamba uzito wa dhambi ya kuashiria ni
sawa na kutamka kwa ulimi, na kama ishara yake ile ingechanganywa na maji ya
bahari basi maji yangebadilika. Imesimuliwa
na Anas bin Malik (Radhiya Llahu anhu) kuwa Waarabu
walikuwa wakitumikiana katika safari na kwamba katika mojawapo ya safari zao
pamoja na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), Abubakar na Umar (Radhiya
Llahu anhum) walikuwa na mtumishi wao akiwatumikia. Wakiwa
safarini, asubuhi moja waliamka na kumuona mtumishi
bado amelala. Mmoja wao akasema: “Muamshe, huyu analala kama yuko
nyumbani“. Wakamwamsha na kumwambia: “Nenda kwa Mtume wa MwenyeziMungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) na umwambie kuwa Abubakar na Umar wanakusalimia na wanataka chakula
(chao)“ Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamwambia: “Waambie mumekwishakula“. Walipoambiwa hivyo wakashangaa na
kumuuliza Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam): “Kitu gani tulichokula?” Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema: “Nyama ya ndugu yenu - Ninaapa kwa yule
ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, naiona nyama yake baina ya meno yenu“. Wakasema; "Tuombee maghfira". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema; "Muombeni yeye akusameheni". Hawa
ni Masahaba watukufu (Radhiya Llahu anhum) wakiwa
safarini kwa ajili ya jukumu tukufu nalo ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi
Mungu, lakini kwa vile wamemsema mwenzao kuwa; "Analala
kama yuko nyumbani“, bila mwenyewe kuwasikia, Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) akawaambia kwamba wamekwisha kula nyama ya ndugu yao huyo. Tutahadhari
ndugu zangu Waislam kwani mara ngapi tunasema maneno huku tukiyaona mepesi
ulimini mwetu bila kujuwa uzito wake mbele ya Mwenyezi Mungu; Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Hakika mja anaweza kutamka neno litakalomridhisha Mwenyezi
Mungu bila yeye mwenyewe kuhisi na (kwa neno hilo)
Mwenyezi Mungu atamnyanyua daraja nyingi. Na hakika mja anaweza kutamka neno
litakalomghadhibisha Mwenyezi Mungu bila yeye mwenyewe kuhisi, akaporomoka nalo
neno hilo ndani ya moto wa Jahannam." Bukhari
Utawasikia
watu wakisema kwa mfano: “Fulani anakula sana ” “Fulani bakhili”. Bali
wengine wanavuka mipaka zaidi na utawasikia wakisema: "Ah!
Nasikia utajiri ule kaupata kwa sababu ya
maunga". Au
wanasema; "Fulani mnafiki" Na
ukiwakataza watakujibu: “Kwani sisi hatumsemi vibaya eti, yote hayo anayo kweli.” Wengine
utawasikia wakisema: "Sisi hatuzungumzi kwa nia mbaya, bali nia yetu ni
kujaribu kuwasaidia, kwani katika kuzungumza huku huenda tukapata ufumbuzi wa
tatizo ". Wanaosema
hivi inawapasa wajuwe yafuatayo: Kwanza
kabisa lazima wakumbuke maana ya neno 'Kusengenya' kama
lilivyofasiriwa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pale alipowauliza
Masahaba wake (Radhiya Llahu anhu) iwapo wanajuwa maana ya neno 'Ghyba', Masahaba
(Radhiya Llahu anhu) wakamjibu: "MwenyeziMungu na Mtume wake wanajua zaidi" Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema: "Kusengenya, ni kuzungumza juu ya
nduguyo (Muislam) yale asiyoyapenda". Akaulizwa: "Unaonaje ikiwa ninayoyasema anayo kweli?" Akasema: "Ikiwa anayo kweli basi huko ndiko kusengenya, na
ikiwa hanayo basi hayo ni madhambi makubwa zaidi (kwa kumsingizia uongo)". Wakumbuke
kuwa kitendo chochote lazima kikubaliane na sheria. Nia
nzuri peke yake haitoshi kumsalimisha mtu na adhabu ya
MwenyeziMungu. Na kumsema mtu vibaya kwa nia mbaya au
nzuri akiwa hayupo huko ni Kusengenya. Tatu,
mwenye kutaka maslahi ya mwenzake anaweza kumnasihi aache mabaya na afanye mema, hata kama itambidi azungumze naye tena na
tena au kumtumia mtu mwenye hekima zaidi ikiwa atashindwa. Na kama baada ya kufanya yote hayo na kujaribu njia mbali mbali
za kisheria bado mtu huyo haachi maovu yake, basi amuache kama alivyo bila ya
kumfedhehesha wala kumsengenya. Katika
hadithi iliyotangulia ya mtumishi wa Abubakar na Umar (Radhiya
Llahu anhum) aliyeambiwa kuwa analala usingizi wa nyumbani, tumeona kuwa Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) aliwaambia wote wawili kuwa wamemsengenya mwenzao
ingawaje aliyetamka maneno yale ni mmoja wao na mwingine alisikiliza tu. Hii ni dalili kuwa msemaji na msikilizaji wote wana makosa na
wote wanapata dhambi. Hadithi
ifuatayo iliyosimuliwa na Abu Huraira (Radhiya Llahu
anhu) inatupa fundisho hilo hilo kuwa msemaji na msikilizaji wote ni sawa:- Anasema
Abu Huraiarah (Radhiya Llahu anhu): "Alikuja Al Aslamiy (Radhiya Llahu anhu) kwa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akatoa ushahidi dhidi ya nafsi yake mara
nne kuwa alizini, na alikuwa kila anapojishtaki, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akimkatalia (huku akimtafutia udhuru). Lakini ilipofika mara ya nne, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia: "Ulimwingila?" Akasema: "Ndiyo". Akamuuliza: "Mpaka ikapotea yako ndani ya yake?" Akasema: "Ndiyo". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamuuliza: "Kama inavyopotea 'mili' (kifuniko cha chupa ya wanja)
ndani ya chupa ya wanja na kamba ndani ya
kisima?" Akasema: "Ndiyo" Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamuuliza: "Unajuwa nini maana ya zina wewe?" Akasema: "Ndiyo, najuwa, nimefanya kitendo cha haramu kile
ambacho mtu anatenda na mkewe kwa halali". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akamuuliza: "Unakusudia nini kwa kauli yako hii?" Akasema: "Nataka unitahirishe ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akaamrisha apigwe mawe mpaka afe. Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
aliwasikia watu wawili katika Masahaba (Radhiya Llahu anhum) wakisema: "Mtizameni huyu ambaye Mwenyezi Mungu amemsitiri na hakuridhika mpaka alipopigwa mawe kama mbwa". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akanyamaza kimya bila kuwaambia kitu, na baada ya kwenda masafa marefu kidogo
akaona mzoga wa punda, akasema: "Wako wapi fulani na fulani?" Wakasema: "Sisi hapa ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akasema: "Shukeni mule mzoga huu wa punda". Wakasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, vipi mtu anaweza kula mzoga?". Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akawaambia: "Basi kile mlichokula katika heshima ya ndugu yenu muda
mchache uliopita (pale mlipomsengenya) ni kibaya zaidi
kuliko kuula mzoga huu. Naapa kwa yule ambaye nafsi
yangu imo mikononi mwake, yeye hivi sasa yumo ndani ya mito ya Peponi
anajichovya ndani yake". Bukhari
- Imam Ahmed - Al Bayhaqiy na wengineo Katika
hadithi hii, tunapata fundisho jingine kuwa msemaji na
msikilizaji wa ghiyba wote ni sawa, kwani juu ya kuwa aliyetamka maneno yale ni
mtu mmoja, na mwenzake alikuwa akimsikiliza tu, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) aliwaambia wote wawili: "Shukeni mule mzoga huu wa punda". Kisha
akawaambia: "Kile mlichokula katika heshima ya ndugu yenu muda mchache
uliopita ni kibaya zaidi kuliko kuula mzoga huu". Kutoka
kwa Kaab bin Malik (Radhiya Llahu anhu) akisimulia kile kisa cha 'Wale
watatu waliongojeshwa' - ambapo yeye ni mmojawapo - kwa sababu ya
kutokwenda vitani pamoja na wenzake siku ya vita vya Tabuk, alisema: "Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) alisema akiwa amekaa baina ya watu wake alipowasili mji wa Tabuk: "Amefanya nini Kaab bin Malik?' Mtu mmoja kutoka katika kabila la Bani Salamah akasema: "Kilichomzuwia ni shuka yake na kuipenda nafsi
yake". Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) akasema: "Maneno gani mabaya haya uliyosema? Wallahi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu
hatujapata kuona kutoka kwake (Kaab) isipokuwa kheri tupu". Hivi ndivyo Muislam anavyotakiwa. Afanye kama alivyofanya Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu), mara
anapomsikia mtu akimsengenya mwenzake amtetee, kwani katika kumtetea nduguyo
Muislam utapata radhi za Mola wako na kuepushwa na Moto siku ya Kiama. Kwa
hivyo unapomsikia mtu anamsengenya mwenzake wewe usijiingize katika bahari hiyo
na kupiga mbizi naye, bali umkataze na kujaribu
kumtetea kama uwezavyo yule anayesengenywa, kwa sababu ukinyamaza na
kusikiliza, ujuwe kuwa wewe na msengenyaji mko katika daraja moja ya maasi. Mwenyezi
Mungu anasema: Åöäøó ÇáÓøóãúÚó
æóÇáúÈóÕóÑó æóÇáúÝõÄóÇÏó ßõáøõ ÃõæáÜÆößó ßóÇäó Úóäúåõ ãóÓúÄõæáÇð "Hakika
masikio na macho na moyo hivyo vyote vitaulizwa". Al
Israa - 36 Na
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake, Mwenyezi Mungu
atamuondolea moto mbele ya uso wake Siku ya
Kiama". Ahmed
na Attirmidhy na wengine Na
akasema: "Atakayemnusuru mwenzake asiyekuwepo, Mwenyezi Mungu
atamnusuru duniani na akhera". Al
Baihaqiy Yote
haya ni mafundisho mema na makatazo makali kutoka kwa Mtume wetu mtukufu
Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa ajili ya kuujenga umma huu uwe
umma unaopendana, umma unaosikilizana, umma unaositiriana ili upate kuwa umma
wenye nguvu na kujishughulisha na mambo yatakayoweza kuupa nguvu na kuunyanyua
badala ya kujishughulisha na yale yatakayoudhoofisha na kuuangusha. Katika
kusengenyana yanapatikana maovu mengi sana yakiwemo
yafuatayo:- a)
Kwenda kinyume na sheria inayomuamrisha kila Muislamu
kumsitiri Muislamu mwenzake. b) Kueneza
na kuitia mizizi shaka katika mwili wa Waislamu na
kusababisha Waislamu wasiwe na Imani hata juu ya watu wema miongoni mwao. c)
Waislamu kushughulika na kusengenyana wao kwa wao na
kueneza chuki baina yao na kuacha kushughulika na yaliyo muhimu
yatakayowaondolea shida zao na shida za Umma. d)
Kumpa nguvu mwenye kitendo hiki na dhambi hii (ya kusengenya) na
kumfanya asitake kuiacha na aendelee nayo bila kujali. e)
Kila mwenye akili timamu anatambua kwamba jamii ya kiislamu haiwezi kunufaika na lolote kwa njia hii ya kumsengenya mtu aliyejisitiri na
aibu yake. Na ni faida gani inayoweza kupatikana
katika kumsengenya mtu aliyefanya madhambi yake kwa kujificha au aliyeificha
siri au aibu yake, au yule aliyesitiriwa na Mola wake? Yafuatayo
ni baadhi tu ya mambo yanayosababisha au kumpatia mtu
kisingizio cha kumsengenya mwenzake; Mara
nyingi ghadhabu hupowa pale mtu anapomuona yule anayemchukia akipatwa na masaibu, na huburudika roho yake kwa kumsengenya kila
anapopata fursa. Mtu wa aina hii dawa yake ni kuikumbuka kauli ya MwenyeziMungu
isemayo: óæÓóÇÑöÚõæÇú Åöáóì
ãóÛúÝöÑóÉò ãøöä ÑøóÈøößõãú æóÌóäøóÉò ÚóÑúÖõåóÇ ÇáÓøóãóÇæóÇÊõ æóÇáÃóÑúÖõ
ÃõÚöÏøóÊú áöáúãõÊøóÞöíäó. ÇáøóÐöíäó íõäÝöÞõæäó Ýöí ÇáÓøóÑøóÇÁ æóÇáÖøóÑøóÇÁ
æóÇáúßóÇÙöãöíäó ÇáúÛóíúÙó æóÇáúÚóÇÝöíäó Úóäö ÇáäøóÇÓö æóÇááøåõ íõÍöÈøõ
ÇáúãõÍúÓöäöíäó "Na yaendeeni upesi maghufira ya
Mola wenu na Pepo (Yake) ambayo upana wake (tu) ni (sawa na )
mbingu na ardhi (Pepo) iliyowekewa wamchao Mungu. Ambao hutoa katika wasaa na
katika (hali ya) dhiki, na wazuiyao ghadhabu na wanaosamehe watu (na wafanyao
ihsani); na MwenyeziMungu hupenda wafanyao ihsani". Aali
Imran 133-134 Na pia
akumbuke maneno ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) aliposema: "Atakeyeizuwia ghadhabu na hali ya
kuwa anaweza kuitowa, MwenyeziMungu atamuita (Siku ya Kiama) akiwa katikati ya
watu na kumtaka achague miongoni mwa Huurul ayni ili amuozeshe
anayemtaka". Imepokelewa
kuwa Imam Aliy Zeinul Abideen (Radhiya Llahu anhu) alikuwa mwingi wa kusamehe. Siku moja kijakazi wake alipokuwa akimmiminia
maji kwa ajili ya kutawadha kikamponyoka chombo cha
maji na kumuangukia Imam usoni pake na kumchana juu ya kipaji cha uso wake. Imam
akainua uso wake juu na kumtizama mtazamo wa kumlaumu.
Kijakazi akasema: “Mwenyezi
Mungu anasema; ‘æóÇáúßóÇÙöãöíäó
ÇáúÛóíúÙó’ “Na wazuiyao
ghadhabu” Akamjibu:
“Na mimi nimeizuwiya ghadhabu yangu.” Akasema;
“Na amesema; ‘æóÇáúÚóÇÝöíäó Úóäö
ÇáäøóÇÓö’ “Na wanaosamehe watu” Akamjibu; “Na mimi nimekusamehe.” Akasema:
æóÇááøåõ íõÍöÈøõ ÇáúãõÍúÓöäöíäó “Na Mwenyezi Mungu anawapenda
wafanyao ihsani”. Akamwambia:
“Nimekuachia huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. Na kutoka
kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
alinambia: "Ukiweza kuwa mtu asiyekuwa na chuki wala kuwaghadhibikia
wenzake wakati wote asubuhi na jioni, basi kuwa hivyo". Tulikuwa tumekaa siku moja pamoja na
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), akasema: "Sasa hivi ataingia ndani humu mtu katika watu wa Peponi". Akaingia mtu katika watu wa Madina. Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
akayarudia tena maneno yale siku ya pili na ya tatu yake na ya nne na zote hizo
alikuwa akiingia mtu yule yule katika watu wa Madian. Abdillahi bin Umar (Radhiya Llahu anhu) akamfuata yule mtu hadi nyumbani
kwake kutaka kujuwa jambo gani analolifanya hata akastahiki kuwa mtu katika
watu wa Peponi. Na katika riwaya nyingine aliyemfuata
alikuwa ni Abdillahi bin Amru bin al Aas (Radhiya
Llahu anhu), akakaa naye nyumbani kwake muda wa siku tatu. Anasema Abdillahi bin Umar (Radhiya Llahu anhu): "Siku zote hizo nilizokaa naye sikumuona akifanya
ibada zozote zile za zaidi isipokuwa anapokuwa usingizini alikuwa kila
anapogeuka akimtaja Mwenyezi Mungu". Siku ya mwisho akamuelezea juu ya yale
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliyosema juu yake. Yule mtu akasema: "Mimi kama ulivyoniona sifanyi
ibada zozote za zaidi isipokuwa kabla sijajitupa juu ya godoro langu
ninamsamehe kila Muislam aliyenikosea na silali mpaka nihakikishe kuwa moyoni
mwangu hamna husda yoyote ile juu ya mwenzangu kwa kheri aliyopewa na Mwenyezi
Mungu". Abdillahi (Radhiya Llahu anhu) akamwambia: "Hili ndilo lililokufikisha (Peponi)". Attirmidhiy
na Annasaiy Imepokelewa
na Ibni Majah na Al Baihaqiy pia kwa isnadi zilizo
sahihi kuwa Abdillahi bin Umar (Radhiya Llahu anhu) amesema: "Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliulizwa
'Watu gani walio bora?" Akajibu: "Wenye nyoyo safi, wanaopenda kusema kweli". Na
kutoka kwa Ibni Abi Dunya amesema kuwa Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Wengi kati ya umati wangu wataingia Peponi si kwa ajili ya
wingi wa kuswali wala wingi wa kufunga wala wingi wa kutoa zaka, bali wataingia
kwa rehma ya Mwenyezi Mungu na kwa usafi wa nyoyo zao na usalama wa vifua
vyao". Na
kutoka kwa Imam Ahmed na Al Baihaqih wamesema kuwa
Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Wamefuzu wale wenye kuzishughulisha nyoyo zao kwa ajili ya imani tu pamoja na kuzisalimisha nyoyo
hizo". Miongoni
mwa yanayomuingiza mtu katika ghiyba ni pale mtu
anaponyamaza kwa ajili kuwaridhisha marafiki ili wasiudhike naye kwa kuwavunjia
raha zao katika mazungumzo pale anapowasikia wakizungumza juu ya watu na ili
wasichukizwe naye wakamuona kuwa ni mzigo kwao ikiwa atawakataza kila mara kwa
kuwaambia: “Haramu, msifanye hivi, haijuzu, msisengenye watu”. Anayefanya
hivyo atajikuta anaishia kusaidia katika kuwasengenya waislamu wenzake na kudhani kuwa huko ndiko kuishi na watu vizuri. Hii,
dawa yake ni kuikumbuka Hadithi ya Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) aliposema: "Anayetafuta kumridhisha Mwenyezi Mungu bila kujali kama atawaghadhibisha watu, basi Mwenyezi Mungu
atamtosheleza, na kuwafanya watu wampende. Na anayetafuta kuwaridhisha watu bila
kujali kama atamghadhibisha Mwenyezi Mungu, basi
Mwenyezi Mungu atamsukumiza huko huko kwa watu." Mwengine hupenda kujinyanyua daraja
yake aonekane kuwa ni bora kuliko mwenzake kwa njia ya
kumtia kasoro mwenzake kwa kusema kwa mfano: “Fahamu yake Fulani huyu ni ndogo masikini” nk. Maneno
ya aina hii anayasema akiwa na nia ya kutaka
kujipendekeza na kujionyesha kuwa yeye ni bora kuliko mwenzake. Dawa
ya maradhi haya ni kuamini kwamba yaliyoko kwa MwenyeziMungu ni bora zaidi na
ndiyo yatakayobaki na kwamba dunia hii kwa MwenyeziMungu thamani yake ni ndogo
kuliko hata ubawa wa mbu, na kwamba huenda mtu huyo anayemdharau akawa ni bora
kuliko yeye mbele ya MwenyeziMungu kama alivyosema Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam): "Huenda mwenye nywele zilizotimka (masikini)
anayefukuzwa milangoni, akimuomba MwenyeziMungu akamkubalia dua yake". Nako
ni kuwapaka matope wenzao kwa kuzungumza juu ya makosa
yao kwa ajili ya kuwachekesha watu katika mabaraza. Watu wa
aina hiyo kila siku utawasikia wakileta habari mpya:- “Umesikia mpya sheikh! Nasikia fulani hivi, au fulani vile", na
watu wanacheka na kuyafurahia. Wengine
kazi zao za kujipatia rizki katika radio na television
na juu ya majukwaa ni kuchekesha watu kwa kuwafedhehesha wengine. Hawa
waikumbuke kauli ya Mtume wa MwenyeziMungu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) aliposema: "Adhabu kali itamthubutukia mwenye kuzungumza maneno ya
uongo ili achekeshe watu, adhabu kali itamthubutukia
adhabu kali itamthubutukia." Huenda
mtu anayependwa na watu alisifiwa katika kikao, na hasidi
akayasikia hayo akaungulika moyoni mwake, akataka kumpaka matope mwenzake ili
sifa ile pamoja na heshima aloipata imuondokee. Hasidi
huyo ajuwe ya kuwa anapotumia njia hiyo anamfanya mtu huyo awe juu yake kwa daraja duniani na akhera pia. Ikiwa
na yeye anaitaka sifa aloipata mwenzake, basi njia yakeMuhammad Faraj Al Saiy
Utangulizi
Dhana mbaya
Dawa ya Dhana
Nukhsi
Kupeleleza
Yaliyodhihirika
Ghiyba (Kusengenya)
Maana ya Ghiyba
Hukmu yake
Heshima ya Muislamu
Mifano ya Ghiyba
1- Kuashiria Kwa Mkono
2-
Waambie Mumekwishakula
3- Mwenye Kusengenya Na Msikilizaji Wote Sawa
Heshima ya ndugu yako
Sababu zake
1- Ghadhabu
2) Kuridhishana
3) Kujipendekeza
4) Kuchekesha watu
5) Husda