Bid’ah
Inayopambana
Na Sunnah
Muhammad Faraj Salem Al
Saiy
Shukrani
zote ni Zake Allaah Subhanahu wa Taala, tunamshukuru, tunategemea kwake msaada,
na tunajikinga kwake kutokana na shari za nafsi zetu na ‘amali zetu ovu. Yule
ambaye Mwenyezi Mungu Atamuongoza basi hapana wa kumpoteza, na yule
Atakayemhukumu kumpotosha (kwa kukataa kwake uongofu), basi hapana wa
kumuongoza.
Nashuhudia
kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah, Pekee Asiye mshirika, na
kwamba Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni Mtume wake na mjumbe wake
na kipenzi chake na mbora wa viumbe vyake.
Amma
baad,
Hakika
ya maneno ya kweli kupita yote ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muongozo ulio
bora ni wa Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na shari ya mambo ni
kuzuwa mepya katika dini, na kila uzushi ni Bid’ah na kila Bid’ah ni upotovu na
kila upotovu mahali pake ni Motoni.
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa mwanzo wa hutuba
zake akitamka maneno haya: "Na shari ya mambo
ni kuzuwa mepya (katika dini), na kila uzushi ni Bid’ah na kila Bid’ah ni
upotovu na kila upotovu mahali pake ni Motoni."
Na
hii ni dalili ya hadhari aliyokuwa akiichukuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) kwa kuwakataza umati
wake kuzuwa mambo mepya katika dini.
Waislamu
wote wanakubaliana kuwa tumekatazwa kufanya kitendo cha Bida'h, nayo ni kuzuwa mambo
katika dini ambayo Mwenyezi Mungu hajayatolea amri Yake. Hitilafu iliyokuwepo
ni kuwa wengine wanasema ipo Bida'h njema na Bida'h potovu, wakati wengine
wanasema kuwa Bida'h zote ni potovu kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah
Llahu alayhi wa sallam) amesema: "Kila
uzushi ni Bid’ah."
Kutoka
kwa Al-‘Irbaadh bin Saariyah (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa amesema:
"Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)
alitutolea mawaidha yaliyotutoa machozi na kuzilainisha nyoyo. Tukamuuliza:
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, haya ni (mfano wa) mawaidha ya kutuaga, kwa
hivyo nini unatuusia?" Akasema: "Nimekuacheni juu ya weupe, (juu ya
kitu kisafi) usiku wake sawa na mchana wake, hapotoki akatoka humo isipokuwa
mwenye kuangamia. Na atakayeishi miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi, basi fuateni
mliyokwishayajuwa katika Sunnah yangu (mafundisho yangu), na mafundisho ya
Makhalifa wema waongofu watakaokuja baada yangu. Yakamateni kwa magego."
(At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, Imam Ahmad na wengine.)
Na
akasema:
"Atakayezusha katika amri yetu hii (dini yetu) lisilokuwemo
anarudishiwa. (halikubaliwi).
(Al-Bukhaariy
na Muslim)
Wenye
kupendelea kufanya sherehe za Maulidi wanatafsiri kitendo cha wenzao wenye
kuyapinga kwa kukataa kuisherehekea siku hii kuwa ni watu wasiompenda Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).
Bila
shaka kadhia hii si nyepesi
Ukweli
ni kuwa mwenye kukataa kuisherehekea siku hii anakataa kwa ajili ya kuogopa
kufanya kitendo cha uzushi ambacho yeye mwenyewe (Swalla Llaahu ‘alayhi wa
sallam) hajapata kukifanya.
Ni
kitendo kinacholeta khitilafu nyingi baina
ya Waislamu, na si katika Sunnah yake (mafundisho yake)
Mwenye
kuacha kufanya kitendo kilichozushwa kwa sababu ya kuhofia kuingia makosani,
bila shaka huyo hawezi kutuhumiwa wala kulaumiwa, bali kinyume chake ni kuwa
mtu huyo yupo katika usalama kuliko mwenye kufanya kitendo ambacho asili yake
hata
Katika
hadithi niliyotangulia kuitaja, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi
wa sallam) alisema:
"Nimekuacheni juu ya weupe, (juu ya amri kisafi) usiku wake
sawa na mchana wake, hapotoki akatoka humo isipokuwa mwenye kuangamia."
Kwa
hivyo mwenye kuiacha sherehe hiyo au kitendo chochote kingine kilichozushwa
katika dini kwa ajili ya kuogopa asije akaingia katika Bid’ah, huyo anajiepusha
na "khitilafu nyingi" alizozitaja
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na anasalimika, kwa
sababu anajiweka juu ya weupe aliotuwachia juu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llaahu ‘alayhi wa sallam).
Mwenyezi
Mungu Anasema:
((Çáúíóæúãó
ÃóßúãóáúÊõ áóßõãú Ïöíäóßõãú æóÃóÊúãóãúÊõ Úóáóíúßõãú äöÚúãóÊöí æóÑóÖöíÊõ áóßõãõ
ÇáúÃöÓúáÇãó ÏöíäÇð)) [ÇáãÇÆÏÉ: 3].
Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na
nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.
(Al-Maaidah: 3)
Maulamaa
wanasema: "Kile ambacho siku ile ilipoteremshwa
aya hii hakikuwemo katika dini, basi leo hakiwezi kuwemo pia. Mwenyezi Mungu
keshaikamilisha dini yake na hakiwezi kukubalika tena kipya isipokuwa kile tu
aliochotuletea Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)."
Amesema Imam Ash-Shawkaaniy:
"Ikiwa Mwenyezi Mungu
Keshaikamilisha dini Yake kabla hajaichukuwa roho ya Mtume Wake, sasa ni kipi
tena hiki wanachokizuwa baada ya kukamilika kwake?
Na ikiwa wanaamini kuwa ni katika dini,
basi huko ni kutuhumu kuwa dini haijakamilika.
Na ikiwa wanaamini kuwa si katika dini,
basi pana faida gani kujishughulisha na (kuliendeleza) jambo lisilokuwemo
katika dini?"
(Qawl al Mufiyd uk. 38)
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Kila uzushi ni Bid’ah na kila Bid’ah ni
upotovu."
Na
akasema:
"Atakayeanzisha mwenenedo mwema " ÓõäøóÉð ÍóÓóäóÉð
katika Uislamu atapata ujira wake na ujira wa atakayetenda wema huo hadi siku
ya Qiyaamah bila ya kupungua kitu katika ujira wa waliotenda, na atakayeanzisha
mwenendo mbaya ÓõäøóÉð ÓóíøöÆóÉð atapata madhambi yake na madhambi ya
atakayetenda madhambi hayo hadi siku ya Qiyaamah bila ya kupungua kitu katika
madhambi yao ".
(Muslim
na At-Tirmidhy na An-Nasaiy na wengine)
Wengine
wakaifahamu vibaya hadithi hii, wakadhani kuwa; kwa vile pana kitu kinachoitwa:
" ÓõäøóÉð ÍóÓóäóÉð Sunnatun
Hasanah (Sunnah njema), kwa hivyo bila shaka mkabala wake ipo pia ÍóÓóäóÉ ÈÏÚÉ Bid’atun Hasanah' (Bid’ah njema), wakati ukweli ni kuwa hapana
kitu
Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Kila
uzushi ni Bid’ah." Kisha akarudia tena, akasema: "Na kila Bid’ah ni upotovu."
Amelitamka
neno 'KILA' mara mbili katika sentensi moja, kwa ajili ya kusisitiza juu
ya umuhimu wake, kwani angeliweza kusema: 'Kila Bid’ah ni uzushi na upotovu.'
Bila ya kulirudia neno 'KILA' mara ya pili.
Inaeleweka
wazi kuwa katika hadithi hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa
sallam) anazungumza juu ya Sunnah njema na siyo Bid’ah
njema, kwa hivyo hapana haja ya kuiunganisha hadithi hii na mambo mawili haya
yenye kutofautiana.
Huenda
ikawa wanajaribu kuiunganisha hadithi hii na ile kauli ya ‘Umar bin Al-Khattwaab
(Radhiya Llaahu ‘anhu) aliposema: äÚãÊ ÇáÈÏÚÉ åÐå "Ni’imat al Bid’ah
haadhihi", (kauli ambayo tutaisherehesha kila tukiendelea mbele
InshaAllaah).
Baadhi
ya Maulamaa wakasema: "Mtu atakayeisimulia
hadithi hii ya "Atakayeanzisha mwenendo
mwema ...ÓõäøóÉð ÍóÓóäóÉð kwa nia ya
kuipitisha Bid’ah yake, kisha asikielezee kisa kilichomfanya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ayatamke maneno haya, basi huyo anakuwa
sawa na mtu aliyeisoma kauli ya Mwenyezi Mungu:
óÝæóíúáñ áøöáúãõÕóáøöíäó öBasi ole wao wanaoswali
Kisha akanyamaza,
asiikamilishe kauli hiyo kwa kusoma:
ÇáøóÐöíäó åõãú Úóä ÕóáÇÊöåöãú ÓóÇåõæäó Ambao wanapuuza Swala zao
Kutoka kwa Jurayr bin AbdiLlaah (Radhiya Llaahu ‘anhu)
amesema:
"Lilikuja kundi la watu wa kabila
la kibedui (kabila la Madhr) wakiwa wamevaa nguo zilizoraruka, hawana
viatu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akaiona
hali
"Atakayeanzisha mwenendo mwema " ÓõäøóÉð ÍóÓóäóÉð katika Uislamu atapata ujira wake na ujira wa atakayetenda wema
huo hadi siku ya Qiyaamah bila ya kupungua kitu katika ujira wa waliotenda, na
atakayeanzisha mwenenedo mbaya ÓõäøóÉð ÓóíøöÆóÉð atapata madhambi
yake na madhambi ya atakayetenda madhambi hayo mpaka siku ya Qiyaamah bila ya
kupungua kitu katika madhambi yao ".
(Muslim
na At-Tirmidhy na An-Nasaaiy na wengine)
Anasema Imam Ash-Shaatwibiy:
"Katika hadithi hii, neno kuanzisha
hakujakusudiwa kwa maana ya kuvumbuwa au kuzusha, bali kumekusudiwa kuhuisha
matendo yaliyothibiti kuwa yamewahi kutendwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla
Llaahu ‘alayhi wa sallam), na dalili ni kuwa kilichomfurahisha Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni kitendo cha kutoa sadaka
kwa wingi, na la pili ni aina ya sadaka; marundu ya nguo na marundu ya vyakula.
Kwa hivyo sadaka haiwezi kuwa katika
uzushi (Bid’ah), kwa sababu
uzushi ni katika matendo yasiyokubaliana na sheria, kinyume na sadaka."
(Imam Ash-Shaatwibiy – Al-I’tiswaam juz. 1, uk. 233)
Haiwezekani
pasemwe kuwa pana Bid’ah njema katika dini, kwa sababu vitu hivi viwili
haviwezi kwenda sambamba hata siku moja – haviwezi kukubaliana, hasa kwa vile
Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) keshatamka kuwa:
"Kila uzushi ni Bid’ah na kila Bid’ah ni
upotovu."
Kauli
hiyo imetamkwa na kiumbe mwenye ulimi fasaha kupita ndimi zote zilizoumbwa na Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala), na ni kiumbe mwenye kuelewa vizuri kile
anachokitamka. Kwa hivyo haikubaliki tena aje mtu atuambie kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) hajakusudia kuwa Kila uzushi ni Bid’ah,
bali ipo Bid’ah njema na nyengine potovu.
Huenda
mtu akaliona jambo
Mwengine atasema: "Kujenga
shule pia ni Bid’ah hasanah, kwa sababu wakati wa Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) hapakuwa na shule."
Tunamuambia kuwa kweli
Kujenga
shule ni katika wasila, ni njia ya kuifikisha elimu na siyo elimu
yenyewe ambayo ni ibada, kama vile microphone 'kipaza sauti' ni wasila,
njia ya kuifikisha sauti ya Qur-aan na hotuba kwa watu, na Qur-aan na hotuba
ndiyo ibada, na watu wanapopanda gari kwenda Makkah, hilo gari ni wasila,
njia ya kuwafikisha watu, lakini siyo ibada, ibada ni kule kuhiji na kufanya ‘Umrah.
Kwa
hivyo mtu anapojenga shule hakusudii kuwa lile jengo ni ibada, bali jengo ni
njia ya kuifikisha elimu kwa wanafunzi, na anapoingiza vipaza sauti Msikitini hakusudii kuwa chombo kile ni ibada bali ni
njia tu ya kuwafikishia watu sauti, kama vile mtu anapopanda gari kwenda
kuhiji, anajua kuwa gari lile si ibada bali ni njia ya kumfikisha kwenye ibada
anayoitaka. Na hii ndiyo njia wanayotumia Maulamaa katika kutoa hukmu.
Wakati
mwenye kuleta Bid’ah yake, huyo anakusudia kuwa ni ibada, kwa kuiwekea njia
yake ya kufanya na makatazo yake na kuvumbua ndani yake mambo mengi
yasiyoteremshiwa amri ya Mwenyezi Mungu juu yake.
Kutokana
na ile kauli ya ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu ‘anhu) aliposema: "Ni’imat al-Bid’ah haadhihi" Mtu anaweza
kusema kuwa ipo Bid’ah njema.
Ukweli
ni kuwa ‘Umar hapa alilikusudia neno Bid’ah kwa maana ya kilugha na si
kwa maana ya Fiq'hi. Inajulikana kuwa katika kamusi ya Fiq'hi, neno Bid’ah lina
maana nyingine tofauti na maana ya neno
Neno
'Bid’ah' katika lugha ni neno zuri
Inajulikana
pia kuwa katika lugha ya Kiarabu neno moja linaweza kubeba maana moja katika
kamusi ya lugha, na neno
Neno
Swalah, katika lugha ya Kiarabu maana yake ni du’aa, na neno hilo hilo katika
kamusi ya Fiq'hi maana yake ni; ibada inayoanza kwa takbira na ina maneno na
vitendo maalum ndani yake na inamalizika kwa kutoa salaam.
Neno
Zakaah, katika kamusi ya lugha ya Kiarabu maana yake ni kujitakasa, na
neno
Zipo
sababu mbali mbali zinayoifanya ile kauli ya ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa
aliikusudia kilugha, na siyo kidini:
Sababu
ya kwanza ni kuwa kitendo cha ‘Umar kuirudisha tena Swalah ya Taarawiyh katika
mwezi wa Ramadhaan si kitendo cha Bid’ah kisheria kwa sababu kitendo hicho
kilifanywa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alipowaswalisha
Maswahaba muda wa siku tatu, kisha akaacha kwa sababu alihofia isije
ikafaridhishwa na kuwa nzito kwao. Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam) kufariki dunia, ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) akairudisha
tena Swalah ile kwa sababu hapakuwepo tena na ile hofu ya kufaridhishiwa, ndipo
‘Umar alipofurahi alipowaona watu wote wamesimama nyuma ya Ubay bin Ka’ab
wakiswali jama’ah, akasema: "Ni’imat al-Bid’ah
haadhihi." Hii haikuwa Bid’ah kisheria, bali ilikuwa ni kuihuisha Sunnah
iliyoanzishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliyewahi
kuwaswalisha mara tatu kisha akaacha kwa sababu iliyotoweka baada ya kufariki
kwake (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na yeye ‘Umar akaweza kuirudisha tena.
Na
sababu ya pili ni kuwa kitendo cha ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) hakiwezi kuwa
cha Bid’ah hata
"Fuateni mliyokwishayajuwa katika Sunnah yangu (mafundisho
yangu), na mafundisho ya Makhalifa wema waongofu watakaokuja baada
yangu. Yakamateni kwa magego."
‘Umar
bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu ‘anhu) ni katika Makhalifa wema waliokuja
baada yake, kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)
ameturuhusu kufuata mafundisho
Tunamaliza
kwa kusema kuwa Bid’ah ya kisheria, Bid’ah katika dini, kwa maana ya kuzusha
jambo jipya ambalo Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) hakuwahi kulitenda
haiwezi kuwa njema hata siku moja.
Anasema
Mwanachuoni Faqiyh, Muhammad bin Swaalih bin ‘Uthaymiyn (Mwenyezi Mungu Amrehemu):
"Mtu aingie msikitini kwa mfano, awakute watu wanaswali
Sunnah zao kila mmoja peke yake
Watu bila shaka watamuambia: "Unataka kutuletea uzushi
gani tena?" Yule mtu atawaambia: "Hapana, si uzushi kwani
tunamswalia nani? Si tunamswalia Mwenyezi Mungu? Isitoshe, Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) keshawahi kuswali Swalah za Sunnah jama’ah,
kama vile Swalah za Tahajjud na aliwahi pia kuswali Taarawiyh na akaswali Swalah
za kupatwa kwa jua na pia mwezi na aliswali Swalah za ‘Iyd jama’ah, na zote
hizo ni Sunnah."
Watu bila shaka watamjibu: "Lakini jambo hili unalotuita
ndani yake halijawahi kufanywa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi
wa sallam)."
Na hapa ndipo penye hekima yote," anaendelea kusema Mwnachuoni huyo Ibn ‘Uthaymiyn (Mwenyezi Mungu Amrehemu), "nayo ni kuwa kitendo chochote katika dini
asichowahi kukifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) au
kutuamrisha kukifanya basi hiyo ni baatwil, hata