‘Ayaat Madhluumah’ (Aya zilizodhulumiwa).

 

Utangulizi 1

 Malaika waliuliza?. 2

Ibilisi alikuwa Malaika?. 5

Ulikuwaje wasiwasi wa Ibilisi?. 7

Maneno aliyofundishwa Aadam

Kutufu Swafaa na Marwah. 10

Hekima ya kuoa zaidi ya mmoja?. 12

Mtume alificha jambo?. 25

Utangulizi

 

Shukrani zote ni zake Mola wa uliwengu wote, na mwisho mwema ni wa wamchao Mwenyezi Mungu, na hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu.

Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke yake Asiye na mshirika mwenye Ufalme na haki iliyo wazi, na nashuhudia kuwa Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni mjumbe wake na Mtume wake na mwisho wa wajumbe wake, na ni kiongozi wa wacha Mungu. Mola wetu mswalie na msalimie Mtume wako huyu pamoja na Masahaba wake na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Qiyaama.

 

Amma baad,

 

Hakika Mwenyezi Mungu Amemtuma Mtume Wake Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) awe dalili iliyo wazi juu ya waja Wake wote, na awabainishie yale aliyoteremshiwa katika Kitabu, na awe mfano mwema wa kuigwa na walimwengu wote, na ili watu wapate kuwa na muongozo mwema katika dini yao na dunia yao.

 

Ametumwa kutufundisha itikadi sahihi pamoja na hekima kwa ajili ya kutengenea hali za umma wake na kuwaweka juu ya njia safi na sahihi, ili watu wawe juu ya kitanga cheupe, mchana wake sawa na usiku wake, na asende kinyume na njia hiyo isipokuwa mpotofu.

Wakaifuata njia hiyo Masahaba wake (Radhiya Llaahu ‘anhum) na wale waliokuja baada yao na waliowafuatilia kwa wema. Wakaisimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kuyakamata mafundisho hayo kwa magego yao kwa kuifuata itikadi hii sahihi, na ibada na mwenendo na tabia. Na sisi Alhamdulillah tunaendelea kuufuata mwenendo wao huo kwa kufuata dalili zilizomo ndani ya Qur-aan na zilizomo ndani ya mafundisho yake (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuthibitishe juu ya njia hiyo sisi na ndugu zetu wote wa Kiislamu kwa kauli iliyo thabit katika maisha ya duniani na ya akhera na Atumiminie rehma Zake kwani yeye ni Mwenye kutoa kwa wingi.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala kwa kuniwezesha kutafsiri baadhi ya maudhui ndani ya kitabu hiki adhimu chenye faida nyingi sana, ‘Ayaat Madhluumah’ (Aya zilizodhulumiwa). Kimepewa jina hilo kwa sababu ndani ya Qurani tukufu zimo aya nyingi ambazo Waislamu wengi hawakuzifahamu maana yake vizuri na kwa sababu wasiokuwa Waislamu wale wenye kuudurusu Uislamu kwa ajili ya kuupiga vita, wanatumilia kutofahamika vizuri kwa aya hizi katika kuwagawa na kuingiza shaka ndani ya nafsi dhaifu.

 

Kitabu hiki kimeandikwa na Dr. ‘Umar bin ‘Abdil-‘Aziyz Qurayshi na kimepitiwa na Sheikh Dr. ‘Aidh Al-Qarniy mwanachuoni maarufu kutoka Saudia na ni mwandishi wa kitabu maarufu ‘Don’t be sad’ (Usihuzunike) na vitabu vinginevyo

 

Nimeamua kutafsiri baadhi ya maudhui muhimu yaliyomo ndani ya kitabu hiki (juu ya kuwa yote yaliyomo ni muhimu) kwa sababu ya kukithiri kufahamika vibaya maana ya nyingi kati ya aya za Qur-aan tukufu kutokana na ujinga uliokithiri kati ya Waislamu hasa katika wakati wetu huu, na muhimu zaidi ni kuwa nyingi kati ya aya zilizofahamika vibaya ni zile za misingi katika dini, na kwa ajili hiyo wale wanaopenda kufuata matamanio ya nafsi zao wakaichukua fursa hii na kuanza kujipoteza na kutaka kuwapoteza wenzao.

Kama tunavyoelewa kuwa maadui wa Uislamu wana msemo wao ‘Wagawe uweze kuwatawala’, kwa njia hiyo Waislamu wakagawanyika makundi mbali mbali, na maadui wa Uislamu wakaichukuwa fursa hii kuzidi kuwatenganisha.

 

Namuomba Mwenyezi Mungu Aniwezeshe kuyafikisha maana ya aya hizi kwa usahihi na Aijaalie kazi hii iwe halisi kwa ajili Yake na iwe katika mezani ya amali zangu njema na za kila msomaji siku ya Qiyaama – Aamin.

 

 

Kwa hekima gani Malaika waliuliza?

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

æóÅöÐú ÞóÇáó ÑóÈøõßó áöáúãóáÇÆößóÉö Åöäøöí ÌóÇÚöáñ Ýöí ÇáÃóÑúÖö ÎóáöíÝóÉð ÞóÇáõæÇ ÃóÊóÌúÚóáõ ÝöíåóÇ ãóäú íõÝúÓöÏõ ÝöíåóÇ æóíóÓúÝößõ ÇáÏøöãóÇÁó æóäóÍúäõ äõÓóÈøöÍõ ÈöÍóãúÏößó æóäõÞóÏøöÓõ áóßó ÞóÇáó Åöäøöí ÃóÚúáóãõ ãóÇ áÇ ÊóÚúáóãõæäó

“Na pale Mola wako Mlezi Alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa Zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyoyajua” Al Baqarah : 30

 

Maadui wa Kiislamu wakasema kuwa eti hapa Malaika wanambishia Mwenyezi Mungu, wakasahau kuwa kumbishia Mwenyezi Mungu si kitendo cha kuasi tu, bali ni kitendo cha kufru kubwa mfano wa kitendo cha Iblisi aliyelaaniwa.

Sisi tunasema kuwa msijaribu kuwakanganya watu, kwa sababu Malaika hawawezi kufanya kitendo cha kumbishia Mwenyezi Mungu, kwani wao wameumbwa kwa ajili ya kutii tu, na wamekingwa na kufanya uasi wa aina yoyote ile.

Mwenyezi Mungu Amesema juu yao:

 

áÇ íóÚúÕõæäó Çááøóåó ãóÇ ÃóãóÑóåõãú æóíóÝúÚóáõæäó ãóÇ íõÄúãóÑõæäó

“Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa Anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa”. At-Tahriym. 6

 

Na Akasema:

 

æóãóäú ÚöäÏóåõ áóÇ íóÓúÊóßúÈöÑõæäó Úóäú ÚöÈóÇÏóÊöåö æóáóÇ íóÓúÊóÍúÓöÑõæäó íõÓóÈøöÍõæäó Çááøóíúáó æóÇáäøóåóÇÑóáóÇ íóÝúÊõÑõæäó

“Na walioko Kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki. Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei” Al-Anbiyaa: 19 -20

 

Na Akasema:

 

Èóáú ÚöÈóÇÏñ ãøõßúÑóãõæäó áóÇ íóÓúÈöÞõæäóåõ ÈöÇáúÞóæúáö æóåõã ÈöÃóãúÑöåö íóÚúãóáõæäó íóÚúáóãõ ãóÇ Èóíúäó ÃóíúÏöíåöãú æóãóÇ ÎóáúÝóåõãú æóáóÇ íóÔúÝóÚõæäó ÅöáøóÇ áöãóäö ÇÑúÊóÖóì æóåõã ãøöäú ÎóÔúíóÊöåö ãõÔúÝöÞõæäó

 

 

“Bali hao (wanaowaita wana) ni watumwa waliotukuzwa. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri Zake.Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule Anayemridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.” Al-Anbiyaa: 26-28

 

Na Akasema juu yao:

 

íóÎóÇÝõæäó ÑóÈøóåõã ãøöä ÝóæúÞöåöãú æóíóÝúÚóáõæäó ãóÇ íõÄúãóÑõæäó

 

“Vinamkhofu Mola wao Mlezi Aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa.” An-Nahl: 50

 

Ikiwa hii ndiyo hali yao, na zile ndiyo sifa zao, na kwamba hawamuasi Mola wao, itakuwaje basi waibishie amri ya Mola wao aliyewaumba na kuikanusha hekima ya Mola wao? Kisha wajifanye wanajua zaidi kupita Mola wao? Haiwezekani kabisa kwao kutenda hayo.

 

Huenda ikawa hekima ya Malaika wale kumuuliza Mola wao juu ya kiumbe kile na vizazi vyake ni kutaka kujua uhusiano utakaokuwa baina yao na viumbe vile, hasa kwa vile mara baada ya kuumbwa kiumbe kile, Malaika waliamrishwa kumsujudia.

 

Na Mwenyezi Mungu Alijaalia pia wakati ule kuwepo Malaika wote wakubwa kama vile Wenye kuhifadhi na Wenye kuandika na Malaika wa wahyi na wa mvua na wa adhabu na wa mauti…. Wote hawa watakuwa na uhusiano wa daima na kiumbe huyu mpya katika maisha yake yote kwa ujumla.

 

Suali lao halikuwa na maana ya kupinga au kubisha au kukataa, hasa tukitambua kuwa kumbishia Mwenyezi Mungu ni kufru aliyoifanya Ibilisi aliyelaaniwa.

Waliuliza kwa sababu hawakuilewa hekima ya kuumbwa kiumbe hiki kipya, kwa hivyo wakataka kujuwa; kwa nini Allaah Anaumba kiumbe kingine? Je wao walipunguza haki yoyote katika amri za Mwenyezi Mungu ndiyo sababu iliyomfanya Mwenyezi Mungu Akataka kuumba kiumbe kingine?

Hapo ndipo walipouliza kwa kutaka kujua.

 

Kwa vile hata kabla ya kuumbwa binaadamu huyo, Malaika waliitaja sifa yake kuwa atafanya uharibifu, huenda ikawa ni kwa sababu Mola wao keshawajulisha hayo.

Pengine walielewa kuwa; kwa vile kiumbe huyu ameumbwa kwa udongo na ataishi juu ya ardhi, bila shaka watakuwa na tabia ya kheri na shari, na kwa ajili hiyo bila shaka yatatokea mapambano baina yao, na uharibifu na ufisadi.

 

Lakini pale Malaika walipojulishwa sababu ya kuumbwa kiumbe huyo na walipotambua namna Mwenyezi Mungu Alivyompa uwezo wa kupata maarifa na elimu, walimsujudia sajdah ya heshima na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).

 

 

 

Je, Ibilisi alikuwa Malaika?

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

æóÅöÐú ÞõáúäóÇ áöáúãóáÇóÆößóÉö ÇÓúÌõÏõæÇú áÂÏóãó ÝóÓóÌóÏõæÇú ÅöáÇøó ÅöÈúáöíÓó ÃóÈóì æóÇÓúÊóßúÈóÑó æóßóÇäó ãöäó ÇáúßóÇÝöÑöíäó

 

“Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri." Al Baqarah: 34

 

Hata aya hii wakaifanya kama ni dalili nyingine ya kuwababaisha watu kuwa eti Malaika wanafanya maasi.

 

Wakasema kuwa eti Ibilisi ambaye ni Malaika! Hakufuata amri ya Mwenyezi Mungu. Ibilisi aliyepinga alipokisia baina yake na baina ya Adam kwa akili yake iliyofisidika akasema:

 

ÃóäóÇú ÎóíúÑñ ãøöäúåõ ÎóáóÞúÊóäöí ãöä äøóÇÑò æóÎóáóÞúÊóåõ ãöä Øöíäò

 

“Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo” Al-’Aaraaf : 12

 

Kwa ajili hiyo akastahiki kutolewa katika rehma ya Mwenyezi Mungu na Pepo Yake. Kama ilivyokuja katika aya nyingi ndani ya Qur-aan Tukufu.

 

Kwa hivyo tunasema;  na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuleta tawfiyq kuwa; Mwenye kudai kuwa Ibilisi alikuwa Malaika, huyo amepotea, na hakuifahamu Qur-aan vizuri, na hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) keshatoa uamuzi Wake katika kadhia hii, na haijuzu kutanguliza kauli ya mwanadamu mbele ya kauli ya Mwenyezi Mungu au Mtume Wake (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Na haya yanapatikana katika Suratul-Kahf aliposema:

 

æóÅöÐú ÞõáúäóÇ áöáúãóáóÇÆößóÉö ÇÓúÌõÏõæÇ áöÂÏóãó ÝóÓóÌóÏõæÇ ÅöáøóÇ ÅöÈúáöíÓó ßóÇäó ãöäó ÇáúÌöäøö ÝóÝóÓóÞó Úóäú ÃóãúÑö ÑóÈøöåö ÃóÝóÊóÊøóÎöÐõæäóåõ æóÐõÑøöíøóÊóåõ ÃóæúáöíóÇÁ ãöä Ïõæäöí æóåõãú áóßõãú ÚóÏõæøñ ÈöÆúÓó áöáÙøóÇáöãöíäó ÈóÏóáÇð

 

“Na Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam! Walimsjudia isipokuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.” Al Kahf:  50.

 

Baada ya ukweli huu ulio wazi usiopingika, mtu anaweza tena kusema kuwa eti Ibilisi ni katika Malaika? Au anaweza kuzirudia zile kauli za Israiliyaat kuwa Ibilisi alikuwa Tausi wa Malaika na mwenye elimu kupita Malaika wote na mcha Mungu kupita Malaika wote na maneno mengine ya mfano huo?

 

Itakuwaje, wakati Ibilisi amekhitilafiana na Malaika kwa maumbile na tabia na mwanzo na mwisho na katika uhai na katika mwelekeo!

 

Kuna kushabihiana gani baina ya Ibilisi na Malaika? Wakati wao wameumbwa kwa nuru na yeye ameumbwa kwa moto? Wao hawamuasi Mola wao na wanafanya wanavyoamrishwa, wakati yeye amepinga amri ya Mola Wake na kuibishia hukumu ya Mola Wake. Wao hawaoi wala hawazai, wakati yeye anaoa na anao watoto, wakiwa upande wa maadui wa Mwenyezi Mungu.

 

Wao ni viumbe wasiofanya kiburi wakaacha kumuabudu Mola wao na wala hawachoki, wakati yeye alikataa na akajivuna na akawa miongoni mwa makafiri. Wao ni wenye kumtakasa Mola wao usiku na mchana, wala hawanyong'onyei, wakati yeye hima yake yote ni kwapoteza waja wa Mwenyezi Mungu, baada ya kuapa kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu kuwa atawapoteza watu wote isipokuwa wale asioweza kuwafikia katika watu wema. Na yeye ni yule asiyeiacha njia yoyote wala mlango wowote wa kuwapoteza viumbe isipokuwa ataufuata na kuingia kwa ajili ya kuwafikia.

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

ÞóÇáó ÝóÈöãóÇ ÃóÛúæóíúÊóäöí áÃóÞúÚõÏóäøó áóåõãú ÕöÑóÇØóßó ÇáúãõÓúÊóÞöíãó  Ëõãøó áÂÊöíóäøóåõã ãøöä Èóíúäö ÃóíúÏöíåöãú æóãöäú ÎóáúÝöåöãú

æóÚóäú ÃóíúãóÇäöåöãú æóÚóä ÔóãóÂÆöáöåöãú æóáÇó ÊóÌöÏõ ÃóßúËóÑóåõãú ÔóÇßöÑöíäó

“Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyonyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani” Al-A’araf:  16-17.

 

Tofauti zote hizi zilizotajwa baina ya Malaika na Ibilisi zinamfanya Ibilisi asiweze kuwa Malaika hata kidogo, tukiongezea ile hukmu Aliyoitoa Mwenyezi Mungu juu yake Aliposema:

 

 ÞóÇáó ÇÎúÑõÌú ãöäúåóÇ ãóÐúÄõæãÇð ãøóÏúÍõæÑÇð áøóãóä ÊóÈöÚóßó ãöäúåõãú áÃóãúáÃäøó Ìóåóäøóãó ãöäßõãú ÃóÌúãóÚöíäó

 

“Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.”

 Al-A’araf:  18.

 

linabakia suala moja, nalo ni kuwa; Ikiwa Ibilisi si Malaika pana hekima gani iliyojificha hata Mwenyezi Mungu Akasema ,wakamsujudia wote isipokuwa Ibilisi?”

 

Tunasema; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuleta tawfiyq; hii katika Lugha ya Kiarabu inaitwa ‘istithnaa munqati’a’, (kielezi kilichokatika), na mfano wake kama wanavyosema wataalamu wa Lugha kuwa mfano mtu anaposema: ‘Walikuja wote isipokuwa punda,’ au; ‘Akayala matufaha yote isipokuwa chungwa.’ Na pakasemwa; ‘wakamsujudia wote isipo kuwa Ibilisi’.

 

Kwa hivyo tunasema; Malaika walipewa amri ya kumsujudia Aadam, na Ibilisi alikuwa pamoja nao (lakini hakuwa mmoja wao – hakuwa mwenzi wao – hakuwa Malaika kama wao), kama tulivyoona katika dalili mbali mbali, na kwa vile wakati ule alikuwa pamoja na Malaika, na alikuwa peke yake miongoni mwa Malaika wengi, ikambidi na yeye asujudu pia, lakini alikataa kwa sababu asili yake kwa kuwa yeye ameumbwa kwa moto na hakuumbwa kwa nuru kama walivyoumbwa Malaika, asili yake ikamzidi nguvu, akaanza kukisia na kupima akajifadhilisha, na matokeo yake akaangamia. Ndiyo maana akapata laana ya Mwenyezi Mungu na ya watu wote.

 

 

Ulikuwaje wasiwasi wa Ibilisi?

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÞõáúäóÇ íóÇ ÂÏóãõ ÇÓúßõäú ÃóäÊó æóÒóæúÌõßó ÇáúÌóäøóÉó æóßõáÇó ãöäúåóÇ ÑóÛóÏÇð ÍóíúËõ ÔöÆúÊõãóÇ æóáÇó ÊóÞúÑóÈóÇ åóÜÐöåö ÇáÔøóÌóÑóÉó ÝóÊóßõæäóÇ ãöäó ÇáúÙøóÇáöãöíä ÝóÃóÒóáøóåõãóÇ ÇáÔøóíúØóÇäõ ÚóäúåóÇ ÝóÃóÎúÑóÌóåõãóÇ ãöãøóÇ ßóÇäóÇ Ýöíåö æóÞõáúäóÇ ÇåúÈöØõæÇú ÈóÚúÖõßõãú áöÈóÚúÖò ÚóÏõæøñ æóáóßõãú Ýöí ÇáÃóÑúÖö ãõÓúÊóÞóÑøñ æóãóÊóÇÚñ Åöáóì Íöíäò

“Na tulisema: Ewe Aadam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale waliodhulumu. Lakini Shaytwaan aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyokuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.” Al-Baqarah: 35-36.

 

Aya hii ilifahamika vibaya kutokana na hadithi za Israiliyaat (zilizosimuliwa na watu wa bani Israil kama walivyonukuu ndani ya Taurat). Imepokelewa katika riwaya za Israiliyaat maelezo ya mti aliokula tunda lake Aadam (‘Alayhis Salaam) kuwa ni mti wa ngano au mzabibu au tini nk.

 

Na imepokelewa pia katika Israiliyaat juu ya maelezo ya wasiwasi wa Ibilisi kwa Aadam kuwa hakuweza kumtia wasiwasi mpaka alipofanikiwa kuingia ndani ya mdomo wa nyoka, na nyoka wakati huo alikuwa na miguu mine mfano wa ngamia.

Imepokelewa katika Israiliyaat pia kuwa;

Na Ibilisi alipoingia Peponi pamoja na nyoka huyo alifanikiwa kumbabaisha Hawwaa na Hawwaa akaweza kumbabaisha Aadam!! Wote wawili wakala tunda, wakajikuta wako uchi, Aadam akajificha ndani ya mti, na Mwenyezi Mungu Akawa Anaita:”Uko wapi ewe Aadam.!!!”

Aadam akasema: “Nakuonea haya ewe Mola wangu kwani mimi niko uchi.” Akamuambia: “Isije kuwa umekula lile tunda nilokukataza?”

 

Mwenyezi Mungu Akamkasirkia nyoka yule aliyeingia Ibilisi ndani ya mdomo wake akamuambia: “Umelaaniwa wewe. Kuanzia leo miguu yako ni tumbo lako. Utasota juu ya ardhi na chakula chako kitakuwa ndani ya udongo, na uadui baina yako na wanadamu utakuwa wa milele.”

Kisha akamuangalia Hawwaa akamuambia: “Umelaaniwa wewe, umembabaisha mja wangu Aadam akala tunda la mti nilomkataza asile, kuanzia leo utabeba mimba kwa dhiki, na hutozaa mpaka utakapoyaona mauti mbele yako.”

 

Ukweli ni kuwa kilichotangulia ni mojawapo ya visa vya Israiliyaat vilivyonukuliwa katika Taurat iliyobadilishwa na kugeuzwa.. Hapana ndani ya Qur-aan dalili yoyote kuwa Hawwaa ndiye aliyembabaisha Aadam, na wala hapana mahali popote alipotuhumiwa Hawwaa, bali Mwenyezi Mungu Amesema:

 

ÝóÃóßóáóÇ ãöäúåóÇ

 

“Basi wakaula wote wawili.” Twahaa: 120.

 

Wote wawili kwa pamoja walikula.

 

Na ili Ibilisi aweze kuwababaisha Aadam na Hawwaa haikuwa lazima kwake aingie Peponi kupitia ndani ya mdomo wa nyoka au wa mnyama yeyote, kwa sababu ili kuingiza wasiwasi hapana lazima ya kukaribiana wala kugusana, bali wasiwasi unaweza kufanyika kwa mbali na kwa karibu pia.

 

Na nyoka huyu yuko vile vile tokea Alipoumbwa na Mwenyezi Mungu, hakuwa na miguu wala kitu cha kusimamia, bali yupo kama Alivyosema Mwenyezi Mungu:

 

æóÇááøóåõ ÎóáóÞó ßõáøó ÏóÇÈøóÉò ãöä ãøóÇÁ Ýóãöäúåõã ãøóä íóãúÔöí Úóáóì ÈóØúäöåö æóãöäúåõã ãøóä íóãúÔöí Úóáóì ÑöÌúáóíúäö æóãöäúåõã ãøóä íóãúÔöí Úóáóì ÃóÑúÈóÚò íóÎúáõÞõ Çááøóåõ ãóÇ íóÔóÇÁ Åöäøó Çááøóåó Úóáóì ßõáøö ÔóíúÁò ÞóÏöíÑñ

“Na Mwenyezi Mungu Ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu Huumba Ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” An-Nuur:  45.

 

Kwa hivyo haya yote yanatokana na hadithi za Israiliyaat zilizojaa ndani ya vitabu vya tafsiri ambazo Waislamu lazima watahadharishwe nazo.

 

 

 

Maneno aliyofundishwa Aadam na Mola Wake

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

ÝóÊóáóÞøóì ÂÏóãõ ãöä ÑøóÈøöåö ßóáöãóÇÊò ÝóÊóÇÈó Úóáóíúåö Åöäøóåõ åõæó ÇáÊøóæøóÇÈõ ÇáÑøóÍöíãõ

 

“Kisha Aadam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi Alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.” Al-Baqarah: 37.

 

Sababu ya kufahamika vibaya aya hii ni baadhi ya hadithi za Israiliyaat na hadithi ‘maudhu’u’ hadithi za uongo zilizopachikwa tu, katika tafsiri ya aya hii, zilizosababisha kufahamika vibaya, na kwa ajili hiyo zikapatikana hukmu mbaya zinazowaingiza watu katika mambo ya shirk na katika aina za shirk.

Miongoni mwa visa hivyo vya uongo ni kile kisa kinachosema kuwa; Aadam alipoasi na kula katika mti ule, akatizama katika nguzo za ‘Arshi akaliona jina la Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) liko karibu na jina la Mwenyezi Mungu, au akaona imeandkwa:

áÇ Åáå ÅáÇ Çááå ãÍãÏ ÑÓæá Çááå

 

Laa ilaaha illa Llaah Muhammadan RasuluLlaah

 

Aadam akasema: “Ewe Mola wangu kwa haki ya Muhammad nisamehe.”

Allaah Akamuambia: Umemjuaje Muhammad wakati bado sijamuumba?”

öAadam akasema: “Ewe Mola wangu uliponiumba kwa mikono yako kisha ukanipulizia roho inayotokana na wewe, nilipoinua kichwa changu nikaona katika nguzo za ‘Arshi imeandikwa ‘Laa ilaaha illa Llaah Muhammadan RasuluLlaah’ nikaelewa kuwa huongezi pamoja na jina lako isipokuwa jina la kiumbe unayempenda kupita viumbe vyote.”

Mwenyezi Mungu Akasema: “Umesema kweli ewe Aadam. Huyu ni kiumbe ninayempenda kupita viumbe vyote. Niombe kwa haki yake na nishakusamehe, na lau kama si Muhammad basi nisingekuumba.”

 

Zimepokelewa zaidi ya riwaya moja juu ya kisa hiki, Maulamaa wote ‘Ij’mai’ wanasema kuwa hadithi hii ni ‘maaudhu’u’ hadithi ya uongo iliyopachikwa tu, na wala hapana ibra yoyote kwa anayejaribu kuisahihisha, kwa sababu Qur-aan inaikanusha hadithi.

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

ÝóÊóáóÞøóì ÂÏóãõ ãöä ÑøóÈøöåö ßóáöãóÇÊò ÝóÊóÇÈó Úóáóíúåö

“Kisha Aadam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi Alimkubalia toba yake.”

Al Baqarah – 37

 

Kwa hivyo, Aadam alipokea maneno kutoka kwa Mola wake na Mola wake ndiye aliyemfundisha kutamka maneno hayo. Aadam hakujitahidi mwenyewe kuyatafuta maneno hayo wala hakuyavumbua yeye. Na maneno haya hayakuwa: “kwa haki ya Muhammad nisamehe.” Wala si kwa haki ya yeyote kati ya wanaozuwa, bali ni maneno aliyosema Mwenyezi Mungu Aliposema:

 

ÞóÇáÇó ÑóÈøóäóÇ ÙóáóãúäóÇ ÃóäÝõÓóäóÇ æóÅöä áøóãú ÊóÛúÝöÑú áóäóÇ æóÊóÑúÍóãúäóÇ áóäóßõæäóäøó ãöäó ÇáúÎóÇÓöÑöíäó

 

“Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.” Al-A’araaf: 23.

 

Na haya ndiyo walioyasema Maulamaa waliofanya tahakiki miongoni mwa wanaotafsiri Qur-aan na wakakubaliana. Na kama inavyosemwa; ‘njia bora ya kufasiri Qur-aan ni kwa Qur-aan.

 

Kwa hivyo Aadam alipokea maneno kutoka kwa Mola wake kama yalivyowekwa wazi na Mola wetu. Hapana haja ya kufanya ijtihadi wala kujidai katika jambo hili.

 

Na ubaya mkubwa zaidi katika jambo hili ni kuwa njia yao hii inaweza kuwapeleka katika shirk.

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

áóÞóÏú ÌöÆúÊõãú ÔóíúÆÇð ÅöÏøÇð  ÊóßóÇÏõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊõ íóÊóÝóØøóÑúäó ãöäúåõ æóÊóäÔóÞøõ ÇáúÃóÑúÖõ æóÊóÎöÑøõ ÇáúÌöÈóÇáõ åóÏøÇð

 

“Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.” Maryam: 89-90.

 

Kutokana na hadithi kama hizo watu wakaanza kuomba kwa Haki ya Muhammad na kwa jina la Muhammad na kwa Jaha ya Muhammad na hata kwa majina ya Mitume wengine na Mawalii, wakaisahau Haki ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) na Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Tawhiyd Yake.

 

 

Nini hukmu ya kutufu baina ya Swafaa na Marwah

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

Åöäøó ÇáÕøóÝóÇ æóÇáúãóÑúæóÉó ãöä ÔóÚóÂÆöÑö Çááøåö Ýóãóäú ÍóÌøó ÇáúÈóíúÊó Ãóæö ÇÚúÊóãóÑó ÝóáÇó ÌõäóÇÍó Úóáóíúåö Ãóä íóØøóæøóÝó ÈöåöãóÇ æóãóä ÊóØóæøóÚó ÎóíúÑÇð ÝóÅöäøó Çááøåó ÔóÇßöÑñ Úóáöíãñ

 

“Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya ‘Umrah, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mjuzi.” Al-Baqarah: 158.

 

Aya hii ni miongoni mwa Aya zinazoweza kufahamika vibaya, kwa sababu dhahiri yake inaonyesha kama kwamba ‘Sa’ayi’ (kutufu baina ya Swafaa na Marwa) si kitendo cha lazima katika Hija wala katika ‘Umrah, na kwamba si kosa kutufu baina yake, lakini ni kitendo kinachopendeza tu, kama aya ilivyosema: “si kosa kwake kuvizunguka.”

 

Ukweli ni kuwa tasfiri hiyo ya kuwa ‘Saa’yi’ baina ya Swafaa na Marwa si kitendo kilichowajibika siyo sahihi na aya haijakusudiwa hivyo.

Inaifasiri vizuri aya hiyo Hadithi iliyosimuliwa na Imaam Ahmad kutoka kwa ‘Urwah (Radhiya Llaahu ‘anhu) kutoka kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Llaahu ‘anha) kuwa amesema:

“Umeisikia kauli ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka isemayo: “Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya ‘Umrah, si kosa kwake kuvizunguka.”  Nikasema; WaLlaahi hapana ubaya kwa mtu yeyote ikiwa hajatufu baina yake (vilima hivyo).

 

Akasema mama wa Waumini ‘Aaishah: “Umesema vibaya kabisa ewe mwana wa dada yangu. Ikiwa maana yake kama ulivyoidhania, basi pangesemwa: ‘si kosa kwake ku(to)vizunguka vilima hivyo,’ lakini imeteremshwa kwa sababu watu wa Madiynah mahali pale walikuwa kabla ya kusilimu wakimuabudu Manata, na (baada ya kusilimu) ikawa wanapofika pale wanaona uzito kutufu (Sa’ayi) baina ya Swafaa na Marwa, ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipoteremsha aya: “Hakika vilima vya Swafaa na Marwa….”

Akasema mama wa Waumini ‘Aaishah: “Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akasunisha (akafundisha) kutufu mahali hapo. Na haijuzu kwa mtu kuacha kutufu mahali hapo.” Al-Bukhaariy na Muslim katika kitabu cha A- Hajj.

 

Na amesimulia Al-Bukhaariy kutoka kwa ‘Aaswim bin Sulaymaan, kasema: “Nilimuuliza Anas juu ya Swafaa na Marwa” akasema; “Tulikuwa tukiona kuwa ni matendo ya wakati wa ujahilia (kabla ya kuja kwa Uislamu), na ulipokuja Uislamu tukajizuia kutufu mahali hapo, ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipoteremsha: “Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu.” Al-Bukhaariy katika mlango wa Al-Hajj.

 

Na katika Sahih Muslim hadithi ndefu iliyosimuliwa na Jaabir (Radhiya Llaahu ‘anhu) alipokuwa akihadithia juu ya Hija ya mwisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alisema: “… Na baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kumaliza kutufu katika nyumba, alirudi katika nguzo akaigusa kisha akatoka kupitia mlango wa Swafaa huku akisema:

 

Åöäøó ÇáÕøóÝóÇ æóÇáúãóÑúæóÉó ãöä ÔóÚóÂÆöÑö Çááøåö

 

“Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu.”

 

Kisha akasema: “Naanzia pale alipoanzia Mwenyezi Mungu.” (Na maana yake ni kuwa kwa vile katika aya, Mwenyezi Mungu Ameanza kuitaja Swafaa kabla ya Marwa kwa hivyo na yeye Saaiy yake ataianzia Swafaa kabla ya Marwa.).

 

Na katika riwaya iliyosimuliwa na Imaam Ahmad, imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) huku akifanya ‘Saa’ayi’ alikuwa akisema: “Fanyeni ‘Sa’ayi’ kwa sababu Mwenyezi Mungu Amekufaridhishieni ‘Sa’ayi’.” Ahmad na Ad-Daaraqutniy

 

Kutokana na hadithi hii, baadhi ya Maulamaa wakasema kuwa kitendo cha ‘Sa’ayi’ baina ya Swafaa na Marwa ni nguzo katika nguzo za Hija. Na haya ni katika Madhehebu ya Imaam Ash-Shafi’y na waliokubaliana naye.

 

Na imesemwa pia kuwa ni wajibu na si nguzo. Kwa hivyo mtu akiiacha kusudi au akiisahau anatakiwa achinje.

 

Na wengine wakasema kuwa ni vizuri mtu kutufu lakini si nguzo wala si wajibu, lakini kauli ya mwanzo (ya Imaam Ash-Shafi’y) ndiyo inayokubalika zaidi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.

 

 

 

Hekima ya kuoa wake zaidi ya mmoja?

 

Mwenyezi Mungu anasema:

æóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊõÞúÓöØõæÇú Ýöí ÇáúíóÊóÇãóì ÝóÇäßöÍõæÇ ãóÇ ØóÇÈó áóßõã ãøöäó ÇáäøöÓóÇÁ ãóËúäóì æóËõáÇóËó æóÑõÈóÇÚó ÝóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊóÚúÏöáõæÇú ÝóæóÇÍöÏóÉð

“Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu.”

Annisaa -3

 

Mambo mawili yanawatatanisha watu katika aya hii, nayo ni:-

1.      Uko wapo uhusiano baina ya kutowafanyia uadilifu mayatima na kuoa mke zaidi ya mmoja?

2.      Si dhulma hii katika Uislamu kwa mwanamume aruhusiwe kuoa mke zaidi ya mmoja na mwanamke asiruhusiwe kuolewa na mume zaidi ya mmoja?

3.      Kisha kuoa huku mke zaidi ya mmoja kumewekewa sharti la uadilifu. Mwenyezi Mungu Amesema: “Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu.”

Na hili ni jambo lisilowezekana, kama ilivyoelezwa ndani ya Qurani katika sura hiyo hiyo.

Mwenyezi Mungu Amesema:

æóáóä ÊóÓúÊóØöíÚõæÇú Ãóä ÊóÚúÏöáõæÇú Èóíúäó ÇáäøöÓóÇÁ æóáóæú ÍóÑóÕúÊõãú ÝóáÇó ÊóãöíáõæÇú ßõáøó Çáúãóíúáö ÝóÊóÐóÑõæåóÇ ßóÇáúãõÚóáøóÞóÉö æóÅöä ÊõÕúáöÍõæÇú æóÊóÊøóÞõæÇú ÝóÅöäøó Çááøåó ßóÇäó ÛóÝõæÑÇð ÑøóÍöíãÇð

Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu

Annisaa – 129

4.      Na ikiwa kuoa huko zaidi ya mke mmoja kama ilivyoruhusiwa katika aya, kwa nini basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alioa zaidi ya hao? Alioa wake tisa wakati mmoja.

 

Mambo haya yaliyowababaisha watu yaliyomo ndani ya aya hii ni dalili ya kufahamika vibaya kwa aya, na kutokana na haya kukatendeka aina nyingi za ufisadi na kufru. Na jambo hili wamelifanya Waislamu na wasiokuwa Waislamu, na pia makundi mbali mbali ya mafisadi, na kila anayetaka kuitia ila dini hii akatoka katika njia ya Mwenyezi Mungu.

 

Tunaanza kusahihisha kufahamika vibaya kwa aya hii kwa kujibu hoja moja baada ya nyingine, kwa haraka na kwa muhtasari.

Tunasema; huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusahilishie na atupe tawfiyq;

Kuhusu uhusiano baina ya kutowafanyia uadilifu mayatima na kuoa wake zaidi ya mmoja, kwa mwenye kuzizingatia vizuri aya kumi za mwanzo za Surat Annisaa, ataona kuwa karibu aya zote zinaelezea juu ya mayatima, na baada ya aya ya mwanzo ambayo ndani yake imejumuisha baina ya usia wa kumcha Mungu, aya ya pili ikaanza moja kwa moja kuzungumza juu ya mayatima, iliposema:

æóÂÊõæÇú ÇáúíóÊóÇãóì ÃóãúæóÇáóåõãú

“Na wapeni mayatima mali yao.”

Annisaa – 2

Na hizi ni aya zenye kuamrisha kuhifadhiwa kwa mali ya mayatima na kuzichunga vizuri zisipotee, na zinakataza kuikaribia isipokuwa kwa njia bora kwa ajili ya kuhifadhi mali hiyo au kuifanyia biashara tena kwa uadilifu. Uadilifu huo unatakiwa ufikie kiwango cha hali ya juu kilichowekewa na Uislamu katika utukufu wa sheria zake na namna ya kulea mayatima na madhaifu.

Na katika hadithi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Åöäøöí ÃõÍóÑøöÌõ ÍóÞøó ÇáÖøóÚöíÝóíúäö: ÇáúíóÊöíãö æóÇáúãóÑúÃóÉö.

Mimi ninaharimisha (kupotea kwa) haki ya madhaifu wawili; Yatima na Mwanamke.

Ibni Majah na Ibni Hibban na Ahmad na Al Hakim na imesahihishwa na Adhahaby

 

Na mwanamke anapokuwa yatima, hapo anakuwa amejumuisha udhaifu mara mbili. Kwa ajili hiyo Uislamu ukaupa umuhimu mkubwa sana ‘haki za mayatima’ na ukasisitiza juu ya uadilifu mkubwa unaotakiwa katika kuhifadhi mali zao katika mandhari bora kupita zote zinazonasibiana na umuhimu wa sheria hii.

Ndipo Mwenyezi Mungu Aliposema:

æóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊõÞúÓöØõæÇú Ýöí ÇáúíóÊóÇãóì ÝóÇäßöÍõæÇ ãóÇ ØóÇÈó áóßõã ãøöäó ÇáäøöÓóÇÁ ãóËúäóì æóËõáÇóËó æóÑõÈóÇÚó ÝóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊóÚúÏöáõæÇú ÝóæóÇÍöÏóÉð

“Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu.”

Na hii ni kwa sababu wakati wa ujahilia, mwanamume alikuwa akilea mwanamke yatima nyumbani kwake, kisha binti huyo akishakuwa akapendezwa na uzuri wake na mali yake, mlezi wake hutaka kumuoa kwa sababu ya kujiepusha na gharama za kumlisha na kumvisha, na kwa vile yeye ndiye mlezi na msimamizi wa mambo yake, alikuwa akiruhusiwa kufanya hivyo. Kwa hivyo anamuoa kwa ajili ya mali yake na uzuri wake bila ya kulipa mahari wala kulipa haki yoyote katika haki zake. Ndipo Mwenyezi Mungu Alipokataza kitendo hicho Akaamrisha kuwafanyia uadilifu na kuwalipa mahari kwa ukamilifu kama wanavyolipwa wanawake wengine. Na kama hawataki basi wakaoe wanawake wengine wasiokuwa wao.

ÝóÇäßöÍõæÇ ãóÇ ØóÇÈó áóßõã ãøöäó ÇáäøöÓóÇÁ ãóËúäóì æóËõáÇóËó æóÑõÈóÇÚó

‘basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane’

 

Kama vile Uislamu ulivyokataza mwenendo huu usiokuwa na uadilifu ndani yake kwa mayatima wanawake, mkabala wake ulikataza pia njia nyingine ambayo mtu alikuwa akilea yatima ambaye hana uzuri wa hivyo wala hana mali, au anakuwa mzuri kidogo na ana mali kidogo, kisha mlezi huyo akataka kumuowa.  Mwenyezi Mungu Akateremsha aya isemayo:

æóíóÓúÊóÝúÊõæäóßó Ýöí ÇáäøöÓóÇÁ Þõáö Çááøåõ íõÝúÊöíßõãú Ýöíåöäøó æóãóÇ íõÊúáóì Úóáóíúßõãú Ýöí ÇáúßöÊóÇÈö Ýöí íóÊóÇãóì ÇáäøöÓóÇÁ ÇáøóáÇÊöí áÇó ÊõÄúÊõæäóåõäøó ãóÇ ßõÊöÈó áóåõäøó æóÊóÑúÛóÈõæäó Ãóä ÊóäßöÍõæåõäøó æóÇáúãõÓúÊóÖúÚóÝöíäó ãöäó ÇáúæöáúÏóÇäö æóÃóä ÊóÞõæãõæÇú áöáúíóÊóÇãóì ÈöÇáúÞöÓúØö æóãóÇ ÊóÝúÚóáõæÇú ãöäú ÎóíúÑò ÝóÅöäøó Çááøåó ßóÇäó Èöåö ÚóáöíãÇð

Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua

Annisaa -127

 

Na katika tafsiri nyingne, wafasiri wa Qurani tukufu wamesema pia kuwa pale Mwenyezi Mungu Alipokataza dhulma na kutowafanyia uadilifu mayatima, Alikataza pia dhulma na  kutowafanyia uadilifu wanawake kwa wenye kuoa zaidi ya mke mmoja.

 

Kwa hivyo kama ilivyoamrishwa kuwafanyia uadilifu mayatima, ikaamrishwa pia kuwafanyia uadilifu wanawake kwa wenye kuoa zaidi ya mke mmoja. Uadilifu unalazimika katika yote mawili, na huu ndio uhusiano uliopo katika aya baina ya kutowafanyia uadilifu mayatima na kuoa mke zaidi ya mmoja.

 

Imesimuliwa na Imam Bukhari kutoka kwa Urwa bin Al Zubeir kuwa alimuuliza Bibi Aisha juu ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

 æóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊõÞúÓöØõæÇú Ýöí ÇáúíóÊóÇãóì Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu                                              .

Akasema (Bibi Aisha): “Ewe mwana wa dada yangu, yatima huyu anakuwa ndani ya nyumba ya mlezi wake akishirikiana naye katika mali yake, akapendezwa na mali yake na uzuri wake, na mlezi wake akataka kumuoa bila ya kufanya uadilifu katika kumpa mahari yake akampa kama anavyowapa wengine. Wakakatazwa kuwaoa isipokuwa kama watawafanyia uadilifu, na kuwapa kile wanachostahiki katika mahari, na wakaamrishwa kuwaoa wanaowapenda katika wanawake wasiokuwa wao.”  Amesema Urwa: kuwa Bibi Aisha alisema: “Hakika watu walimuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kutaka fatwa juu ya aya hii, ndipo Mwenyezi Mungu Alipoteremsha: íóÓúÊóÝúÊõæäóßó Ýöí ÇáäøöÓóÇÁ Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Akasema Bibi Aisha: “Kauli ya Mwenyezi Mungu katika aya hii pale Aliposemana mnapenda kuwaoa,” kwa ajili ya uyatima wao ikiwa ni mpungufu wa mali au uzuri. (Lakini) Walikatazwa kuwaoa wale waliopendezwa na mali yao au uzuri wao katika wanawake isipokuwa kama watawafayia uadilifu kwa ajili ya kupenda kwao kuwaoa ikiwa wana upungufu wa mali au uzuri.”

Bukhari na Muslim

 

2- Wakasema: ‘Uislamu umemdhulumu mwanamke pale uliporuhusu kuoa mke zaidi ya mmoja na kuziumiza nyoyo zao, kisha haukufanya uadilifu wa kuwaruhusu na wao kuolewa na mume zaidi ya mmoja!!!’

 

Tunasema kwanza: Nani aliyemdhulumu mwanamke? Watasema: Uislamu.

Tunasema:    Na huu Uislamu ni dini ya nani? Watajibu: Dini ya Mwenyezi Mungu.

Tunasema:    Kwa hivo aliyemdhulumu mwanamke ni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala :

ßóÈõÑóÊú ßóáöãóÉð ÊóÎúÑõÌõ ãöäú ÃóÝúæóÇåöåöãú Åöä íóÞõæáõæäó ÅöáÇ ßóÐöÈðÇ [ÇáßåÝ: 5

öNi neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu

Al Kah’f -5

Tunasema pia: Je Mwenyezi Mungu Anaweza kudhulumu? Mwenyezi Mungu anasema:

æóáÇ íóÙúáöãõ ÑóÈøõßó ÃóÍóÏðÇ

Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote

Al Kah’f-49

Na Akasema katika aya nyingine:

æóãóÇ ÑóÈøõßó ÈöÙóáøóÇãò áøöáúÚóÈöíÏö

Wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja

Fussilat – 46

Na katika hadith Al Qud’sy  Amesema:

(íÇ ÚÈÇÏí Åäí ÍÑãÊ ÇáÙáã Úáì äÝÓí æÌÚáÊå Èíäßã ãÍÑãÇ ÝáÇ ÊÙÇáãæÇ(

Enyi waja wangu, Hakika Mimi nimejiharamishia dhulma na Nikaijaalia iwe haramu baina yenu, kwa hivyo msidhulumiane.

Muslim

Kisha tunasema: Na kwa nini Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amdhulumu mwanamke? Kisha kwa maslahi ya nani? Amdhulumu kwa maslahi ya mwanamume? Au kwa ajili ya uzuri wake mwanamume huyu kama wanavyosema, au kwa sababu gani?

Kwani mwanamke si kiumbe cha Mwenyezi Mungu, na mwanamume pia ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu? Kwa nini basi Mwenyezi Mungu amdhulume kiumbe kwa ajili ya kumpendelea kiumbe mwingine? Na kwani Uislamu umehalalisha kuoa mke zaidi ya mmoja kwa ajili ya maslahi ya mwanamume, au kwa ajili ya maslahi ya mwanamke katika daraja ya mwanzo?

Tuelimisheni enyi watu. Munayatizama vipi mambo haya, au ni wapungufu wa akili?!!

 

Ifuatayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Aliposema: “Basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane.”

Hapa Mwenyezi Mungu alifaridhisha au aliwajibisha? Hii ni rukhsa. Kwa hivyo kuoa mke zaidi ya mmoja si wajibu wala si fardhi, bali ni rukhsa iliyotolewa na Mwenyezi Mungu.

Kisha tunauliza: Kwani ni dini ya Kiislamu peke yake iliyoamrisha kuoa mke zaidi ya mmoja au ndiyo iliyoanzisha mwenendo huu?

Waislamu na watu wote kwa ujumla, wale wenye kufuata dini mbali mbali na wasiokuwa na dini wanaoa wake zaidi ya mmoja, tena wao wanaoa bila ya kiwango wala hesabu, bila kutimiza wajibu na bila ya kufanya uadilifu. Wanaoa bila kufuata kanuni wala kulinda uhusiano wa mke na mume, na bila ya kuulinda ubinadamu.

Kwa nini basi ulipokuja Uislamu ukataka kuyaweka sawa mambo haya ya kuoa mke zaidi ya mmoja katika nyanja zake zote, kwa kuweka idadi maalum ya kutoruhusu kuoa zaidi ya wane, na kupanga namna kwa kuweka sharti la uadilifu na sharti la uwezo wa kuongeza.

Sasa kwa kufanya hivyo ndiyo Uislamu unakosolewa badala ya kusifiwa? Na kwa nini unakosolewa Uislamu peke yake wakati amri hii imekuja ndani ya vitabu vyote vilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, na kufuatwa na umma zote?

 

Wakati wa ujahilia kabla ya kuja Uislamu, watu walikuwa wakioa zaidi ya mke mmoja. Warumi walikuwa wakioa wake zaidi ya mmoja. Wayunani walikuwa wakioa wake zaidi ya mmoja, Waajemi walikuwa hiyvo hivyo, hata mfalme wao alikuwa akioa zaidi ya wake mia moja.

Katika dini ya Mayahudi wanaruhusiwa kuoa wake zaidi ya mmoja. Ndani ya Taurati imeandikwa kuwa Mitume wanaotokana na Bani Israil walikuwa wakioa wake kwa makumi na mamia. Imeandikwa kwa mfano kuwa ‘Nabi Daud Alayhi ssalaam alikuwa na wake mia tatu, na Nabi Sulayman alikuwa na wake mia saba na vijakazi mia tatu.’

 

Katika Injili ya Manasara hapana panapokatazwa kuoa wake zaidi ya mmoja, na wakuu wa makanisa wanaoharamisha kuoa zaidi ya mke mmoja hawana egemeo lolote la kisheri. Wameitoa wapi hukmu hiyo? Kwanini kanisa linakifumbia macho kitendo cha kuoa zaidi ya mke mmoja kwa Wakristo wa bara la Afrika, wakati kitendo hicho kinafanywa hata na makasisi wa baadhi ya makanisa ya Afrika, kisha kanisa hilo hilo linaharamisha kufanya hivyo kwa Wakristo wa Ulaya?

 

Na sisi tunauliza; Kwani Dini ya Kiislamu ndio iliyovumbua kuoa wake zaidi ya mmoja kinyume na mafundisho ya dini nyingine zilizotangulia? Sasa ikiwa dini zote – zenye kufuata maamrisho kutoka mbinguni na wasiokuwa na dini - wameruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja, kwa nini basi Uislamu peke yake ulaumiwe?

Kisha tunasema pia; Je, Wakristo hivi sasa na watu wa Ulaya na watu wa nchi za Magharibi wametoshelezwa na mmoja na hawajatafuta wengine?

 

Hawajatafuta urafiki wa muda mfupi au mrefu na wanawake wengine? Kwanini basi wanaharamisha kuoa zaidi ya mke mmoja wakati wanahalalisha kuzini na mwanamke zaidi ya mmoja? Kwa nini wanaharimisha halali na wanahalalisha haramu? Kwa nini mtoto mchanga anatupwa au analelewa akiwa ni mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa? Na kwa nini hanasibishwi na baba yake wa kweli?

 

Zinaa imekithiri (imezidi) kwa upande wa Wakristo huko Ulaya na Marekani na katika jamii zote zilizoharamisha kuoa mke zaidi ya mmoja. Na watoto waliozaliwa nje ya ndoa wamekithiri huko Marekani. Idadi yao imeongezeka kwa asilimia sitini ‘60%’, na Ulaya idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia zaidi ya sabini na tano ‘75%’ . Na katika baadhi ya nchi zilizoharamisha kuoa wake zaidi ya mmoja, idadi yake inatisha sana, kwani watoto waliozaliwa nje ya ndoa inakaribia kuwa watoto watatu katika kila wane.

Wakati huo huo idadi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa katika nchi zinazohalalisha kuoa mke zaidi ya mmoja ni moja tu katika kila mia 1% .

 

Wanasema wataalamu wenye kuudurusu Uislamu katika watu wa Magharibi, wale wenye insafu kuwa; ‘Hii inatokana na sheria ya kuruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja iliyothibitishwa katika dini ya Kiislamu pamoja na uadilifu wake na usafi wake na sitara iliyo ndani yake.’

 

Nilitangulia kusema kuwa; Uislamu sio ulioanzisha ada ya kuoa zaidi ya mke mmoja, bali Uislamu umekuja kuweka idadi ya wake wane pamoja na masharti na hukmu, kwa sababu wakati wa Ujahilia (kabla ya kuja Uislamu) watu walikuwa wakioa wake kwa makumi na mamia.

Imepokelewa kuwa aliposilimu Aslam Gheylan Athaqafiy alikuwa na wake kumi, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuambia:

(ÇÎÊÑ ãäåä ÃÑÈÚÇ æÝÇÑÞ ÓÇÆÑåä(

“Chauga wane kati yao na uwa ache waliobaki.”

Ibni Majah na Ahmad na Imesahihishwa na Shekh Al Albani katika Sahiyh Ibni Majah (1589)

 

Na wapo pia waliosilimu wakiwa na wake wanane na wengine kumi, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwataka wabaki na wane tu.

 

Kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuoa wake tisa, hiki ni kitendo kinachomhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) peke yake, kama tutakavyoelezea kila tukiendelea mbele.Inshaallah.

 

Hekima ya mtu wa kawaida kuwekewa idadi ya wake wane inajulikana kuwa huu ndio upeo wa uwezo wake katika kuwasimamia na kutimiza wajibu wake juu yao katika kila Nyanja ya maisha. Na hii ni pamoja na uwezo wa kufanya uadilifu baina yao.

 

Mtu akiuliza; kwa nini Uislamu umekuja kukikubali kitendo cha kuoa mke zaidi ya mmoja na usikataze na kuuondoa kama ulivyoondoa baadhi ya sheria za zamani?.

Tunasema: Uislamu umefanya hivyo kwa sababu zinazohusiana na adabu na mwenendo mwema, na pia kwa sababu za kijamii na kwa sababu za kibinafsi.

 

Uislamu ni Neno la Mwenyezi Mungu la mwisho Alilohitimisha kwalo Risala Zake, kwa ajili hiyo Neno hilo likaja na ujumbe uliokusanya kila kitu. Ujumbe unaokubalika kila pembe ya dunia na kila zama na kila mtu. Uislamu haujaweka sheria kwa ajili ya watu wanaoishi mjini ukawasahau wanoishi majangwani na mashambani. Haujaweka sheria kwa ajili ya wanoishi katika sehemu za baridi ukawasahau wa sehemu ya joto. Uislamu unachunga haki ya kila mtu pamoja na mambo yote ya dharura kwa waja, kila mmoja kutokana na maslahi yake.

Wapo miongoni mwa watu wenye hamu kubwa ya kupata watoto, lakini wamejaaliwa kupata mke asiyezaa kutokana na umbile lake au kutokana na maradhi. Si litakuwa jambo la ukarimu kutoka kwake mwanamke huyo akimruhusu mumewe aoe ili apate kile anachokitamani, na wakati huo huo yeye anabaki mahali pake na haki zake zinadhaminiwa?

 

Wapo wanaume wenye uwezo mkubwa na nguvu za kufanya kitendo cha jinsia, hamu yake daima inakuwa kubwa, lakini amejaaliwa kupata mke mwenye uwezo mdogo na nguvu ndogo, au mgonjwa, au siku zake za hedhi ni nyingi, au mfano wa aina hiyo, na mwanamume anakuwa hana uwezo wa kusubiri. Kwa nini basi asiruhusiwe kuoa mwengine wa halali badala ya kwenda kutafuta mwengine wa nje?

 

Wapo wanawake waliokuwa vizuka wangali bado vijana wadogo, na wapo waliotalikiwa wakiwa bado wadogo, huenda pia idadi ya wanawake ikawa ni kubwa kupita ya wanaume – hasa kutokana na vita vinavyowamaliza wanaume na vijana – kwa ajili hii ni kwa maslahi ya jamii na maslahi ya wanawake pia kuolewa badala ya kuishi umri wao wote wakiwa vizuka au wajane wakinyimwa maisha ya ndoa, na utulivu na mapenzi yaliyomo ndani yake na pia wakinyimwa neema na tumaini la kuweza kwa mara nyingine kuwa mama.

Kwa kina mama wa aina hii wenye uwezo wa kuolewa ambao ni wengi kupita idadi ya wanaume, itawabidi waangukie mojawapo ya matatu yafuatayo:-

1.      Waishi maisha yao yote wakiungulika kwa kukosa kuolewa.

2.      Ama waharibike na kugeuka kuwa chambo rahisi kwa wanaume wanaopenda kuishi nao kwa haramu.

3.      Au waruhusiwe kuolewa na wanaume waliokwishaoa wenye uwezo wa kuishi nao kwa ihsani na wenye uwezo wa kuwasimamia kifedha.

 

Uwekezano wa mwanzo: ni dhulma kubwa kwa mwanamke ambaye hajafanya kosa lolote hata akastahiki kufanyiwa hivyo.

Ama uwezekano wa pili: Uhalifu mkubwa dhidi ya haki ya mwanamke na dhidi ya jamii na dhidi ya khulqa njema, na hili nasema kwa masikitiko kuwa ndiyo njia walioichagua watu wa Magharibi. Wao wameharamisha kuoa zaidi ya mke mmoja wakahalalisha kuwa na wanawake na wapenzi zaidi ya mmoja, eti kwa sababu imewabidi wawe na wanawake zaidi ya mmoja, lakini kinyume na mwenendo na tabia njema na kinyume na ubinadamu, kwa sababu mwanamume anamaliza hamu yake na matamanio yake bila ya kulichukua jukumu lolote juu ya natija ya kitendo chake hicho.

Ama uwezekano wa tatu: ndio pekee wenye uadilifu ndani yake na uliotahirika na wa kibinaadamu na unakubaliana na mwenendo na tabia njema, na ndio tiba ya maradhi haya,.na haya ndiyo yaliyokuja nao Uislamu na ukatoa hukmu juu yake.

Mwenyezi Mungu Anasema:

ÃóÝóÍõßúãó ÇáúÌóÇåöáöíøóÉö íóÈúÛõæäó æóãóäú ÃóÍúÓóäõ ãöäó Çááøåö ÍõßúãÇð áøöÞóæúãò íõæÞöäõæäó

Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?

Al Maidah-50

                                                                     

Huku ndiko kuoa zaidi ya mke mmoja kunakopigwa vita na nchi za Magharibi na Wakristo. Wakachukizwa nako wakati wamependezwa kuwa na wapenzi na kufanya kitendo cha jinsia na wanawake wengi bila ya kuwa na uhusiano wa ndoa na bila ya mipaka wala idadi. Wamefanya hayo kinyume na sheria na kinyume na adabu na bila ya kumheshimu mwanamke wala kizazi kitakachopatikana kutokana na kitendo kile cha kinyama. Sasa ni kundi lipi lenye msimamo bora, na ni kundi lipi lipo katika njia iliyoongoka?

 

Katika Uislamu imeruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja kwa sharti la uwezo wa mali na hali, na ikiwa sharti hizi mbili haziwezi kupatikana basi hairuhusiwi kuongeza. Kwa hivyo Muislamu lazima awe na uhakika kuwa anao uwezo wa kufanya uadilifu baina ya wake zake katika chakula na vinywaji na makazi na kharji. Ikiwa hana uhakika kuwa ataweza kusimamia yote haya kwa usawa na uadilifu basi ni haramu kwake kuongeza mke zaidi ya mmoja.

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

ÝóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊóÚúÏöáõæÇú ÝóæóÇÍöÏóÉð

“na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu”

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema:

 

ãä ßÇäÊ áå ÇãÑÃÊÇä íãíá áÅÍÏÇåãÇ Úáì ÇáÃÎÑì ÌÇÁ íæã ÇáÞíÇãÉ íÌÑ ÃÍÏ ÔÞíå ÓÇÞØÇð Ãæ ãÇÆáÇð

“Mwenye kuwa na wake wawili akampendelea mmoja wao dhidi ya mwengine atakuja siku ya Kiama akiuburura ubavu wake mmoja umeanguka au umepinda”

Abu Daud, Ibni Majah, Attirmidhiy na Imam Ahmad, na imesahihishwa na Sheikh Al Albaniy.

 

Na kupendelea kulikokusudiwa katika hadithi hii ni upendeleo katika haki zake mwanamke, jambo lisilohusiana na moyo, kwa sababu uadilifu uliotajwa katika aya ni uadilifu katika kuisimamia nyumba kwa hali na mali. Na hili ni jambo linalowezekana. Lakini haukusudiwi upendeleo katika moyo. Kwa sababu mwanamume anaweza kuwa na nishati usiku mmoja na usiku mwingine asiwe na nishati, kwa hivyo kinachokusudiwa ni uadilifu katika hali na mali na mwanamume anatakiwa amche Mungu katika jambo hili.

 

Kuhusu kauli yao kuwa; kwa nini Uislamu umemruhusu mwanamume kuoa mke zaidi ya mmoja lakini haukumruhusu mwanamke kuolewa na mume zaidi ya mmoja? Hakika hili ni jambo la kustaajabisha sana!!!

Itakuwaje mwanamke awe na mume zaidi ya mmoja, atawezaje kuwaridhisha wote, atawezaje kuwakusanya? Mtoto atanasibishwa na yupi kati ya waume hao, na mimba itakuwa ya nani?

Nani atakayekuwa msimamizi wa aila? Yeye ndiye atakayewasimamia waume zake au atamsimamia mmoja wao au atawasimamia wote? Sheria gani hii na dini gani hii na tabia gani hizi?

Wanataka kumgeuza mwanamume awe kitu gani? Na wanataka kumgeuza mwanamke awe kitu gani? Na wanataka kuigeuza jamii yetu iwe kitu gani?

 

3-        Wakasema pia : Uislamu umeruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwa sharti la uadilifu:

Mwenyezi Mungu Amesema:ÝÅä ÎÝÊã ÃáÇ ÊÚÏáæÇ ÝæÇÍÏÉ Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu. Kisha Qurani ikabainisha kuwa uadilifu huu hautawezekana  æáä ÊÓÊØíÚæÇ Ãä ÊÚÏáæÇ Èíä ÇáäÓÇÁ æáæ ÍÑÕÊã Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo kuoa zaidi ya mke mmoja ni haramu.kwa nassi ya Qurani!! Na kama inaruhusu basi Qurani inagongana yenyewe kwa yenyewe.

 

Tunasema : Maneno haya ni katika vichekesho vinavyoliza na yanatukumbusha maneno ya walevi na wahuni.wenye kutumia dalili kama hizi zenye kuchekesha mfano wa yule aliyelewa, na alipowaona watu wakitoka msikitini akawaambia: “Mwenyezi Mungu hajasema; ‘Ole wao wenye kulewa’ bali Alisema:  Ýæíá ááãÕáíä  ‘Ole wao wanao Sali,’

Bila kuikamilisha aya inayosema:Ambao wanapuuza Sala zao.’

Katika mfumo huu, tunakuta watu wanazungumza juu ya Uislamu na kuifasiri Qurani kwa njia zao.

Hakika Qurani imesema:

æóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊõÞúÓöØõæÇú Ýöí ÇáúíóÊóÇãóì ÝóÇäßöÍõæÇ ãóÇ ØóÇÈó áóßõã ãøöäó ÇáäøöÓóÇÁ ãóËúäóì æóËõáÇóËó æóÑõÈóÇÚó ÝóÅöäú ÎöÝúÊõãú ÃóáÇøó ÊóÚúÏöáõæÇú ÝóæóÇÍöÏóÉð

“Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu.”

Hili ni kweli, lakini uwezo uliokusudiwa hapa ni uwezo wa kufanya uadilifu katika makazi na malipo na maisha na mengine ya mfano huo kwa kiasi cha uwezo wako wote.

Na aya nyingine inasema:

æáä ÊÓÊØíÚæÇ Ãä ÊÚÏáæÇ

Wala hamtaweza kufanya uadilifu

Aya hii inatubainishia kuwa uadilifu usio na mipaka hauwezekani kupatikana, kwa hivyo kilichokusudiwa hapa ni uwezo wa kufanya uadilifu wa moyo, katika kupenda na kumili kunakohusiana na hisia za kibinadamu, ‘Mapenzi’.

Haya ni mambo yanayohusiana na moyo, na mwanadamu hana uwezo wa kuyamiliki baraabara, na nyoyo ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, Anazigeuza Apendavyo. Kwa hivyo ikiwa mume atampenda mmojawapo wa wake zake zaidi ya mwengine, kwa sababu yoyote ile, hii haina maana kuwa amdhulumu mwengine, au asifanyie uadilifu baina yao. Bali anatakiwa kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: “Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa.” Akageuka kuwa si mke wala si mjane. Na uadilifu unaotakiwa ni kutoyadhihirisha mapenzi hayo kwa wengine.

 

Huyu hapa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyekuwa akimpenda Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kupita wake zake wengine, lakini hakuwa akiyadhihirisha kwa wenzake, na alikuwa akifanya uadilifu baina yao kwa kila anachomiliki, kisha akisema:

(Çááåã Åä åÐå ÞÓãÊí ÝíãÇ Ããáß ÝáÇ Êáãäí ÝíãÇ Êãáß æáÇ Ããáß)

“Mola wangu, hakika hii ni seheumu yangu katika ninachomiliki, kwa hivyo usinilaumu katika Unachomiliki na wala similiki.”

Abu Daud na Attirmidhiy na Ibni Majah

 

Na hapa anakusudia kuumiliki moyo ambao unaweza ukamili zaidi kwa mke mwengine kupita wenzake.

Na alikuwa anapokwenda safari akipiga kura kwa ajili ya kumchagua mmoja wao, na yeyote itakayomuangukia ndiye atakayemchukua katika safari hiyo.

Bukhari

Alifanya hivyo kwa ajili ya kuwaridhisha, na kwa njia hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alihiji na wake zake wote.

 

Mwenyezi Mungu Amesema:

æóÅöä ÊõÕúáöÍõæÇú æóÊóÊøóÞõæÇú ÝóÅöäøó Çááøåó ßóÇäó ÛóÝõæÑÇð ÑøóÍöíãÇð

“Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.”

Annisaa – 129

 

Na maana yake ni kuwa; Kama mtasikilizana katika mambo yenu, mkayafanya yawe mema, kisha mkafanya uadilifu baina yenu katika yale mnayomiliki, na mkamcha Mungu, katika mambo yenu yote, hapo Mwenyezi Mungu atakusameheni katika yale mliyomili kidogo bila ya uwezo wenu wa kuumiliki moyo.

Tafsiri ya Ibni Kathiyr

 

4-        Kwa kumaliza tunasema: Wakasema kuwa ikiwa sheria hairuhusu kuoa zaidi ya wake wane, kwa nini basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akaoa zaidi ya hao, ikafika idadi yao wake tisa?

Wakasema pia kuwa eti hii ni dalili ya kupenda kwake wanawake (Swallah Lllahu alayhi wa sallam).

Tunasema: Inajulikana kuwa mke wa mwanzo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni Bibi Khadija binti Khuwaylid (Radhiya Llahu anha). Alimuoa akiwa kijana mwenye umri wa miaka ishirini na tano, na wakati huo Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) alikuwa na umri wa miaka arubaini na tano aliyewahi kuolewa kabla ya hapo na wanaume wawili, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hakuongeza mke mwingine wakati wote alipokuwa naye Bibi Khadija, mpaka alipofariki Bibi Khadija, na wakati huo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa na umri wa miaka hamsini au hamsini na moja.

Tunauliza; Je, mtu wa aina hii ni mwenye kupenda wanawake? Na Bibi Khadija ni mke wa pekee aliyemuoa kwa kutaka mwenyewe, na hii ni kwa sababu alimuoa kabla ya kuanza kuteremshiwa wahyi kutoka mbinguni. Lakini wake zake wote waliobaki, aliwaoa kwa amri itokayo kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, kwa sababa baada ya kuanza kuteremshiwa wahyi alikuwa hafanyi lolote bila ya kuletewa wahyi.

Mwneyezi Mungu Anasema:

æóãóÇ íóäØöÞõ Úóäö Çáúåóæóì Åöäú åõæó ÅöáÇ æóÍúíñ íõæÍóì

Wala hatamki kwa matamanio Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa

Annajm3-4

 

Baada ya kupewa utume akawa na kanuni inayokhitalifiana na watu wengine. Kwa hivyo kuoa kwake idadi hii ya wanawake lilikuwa ni jambo lenye kuhusiana na utume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Na inajulikana kuwa Mitume wote (Alayhimu ssalaam) walikuwa na mambo yanayowahusu wao tu, tofauti na watu wengine katika umma wao. Na kuhusika huku si katika mambo ya kuoa tu, bali ni katika mambo mengi mengine, ambayo hapa si mahali pake kuyataja, kwa sababu wasaa hautoshi kuyaelezea yote.

Bila shaka tukiweka upande kuhusishwa huku, tutaona kuwa ndani yake pana hekima kubwa, bali hekima nyingi tulizozifahamu na tusizozifahamu.

Pana hekima za kisheria na za kijamii na za kielimu nk. Kwa Hekima Yake Mwenyezi Mungu Alitaka wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) wabaki kuwa chini yake asiwataliki, kwa sababu akiwataliki haitokuwa halali kwa mwengine yeyote kuwaoa.

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóãóÇ ßóÇäó áóßõãú Ãóä ÊõÄúÐõæÇ ÑóÓõæáó Çááøóåö æóáÇ Ãóä ÊóäßöÍõæÇ ÃóÒúæóÇÌóåõ ãöä ÈóÚúÏöåö ÃóÈóÏÇð Åöäøó Ðóáößõãú ßóÇäó ÚöäÏó Çááøóåö ÚóÙöíãÇð

Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu

Al Ahzab -53

 

Na Mwenyezi Mungu alipowahiarisha wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam); iwapo wanamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, na wote walipochaguwa kumtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya akhera, Mwenyezi Mungu akawatunukia zawadi ya kumpa amri Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) asioe tena baada ya hao.

Mwenyezi Mungu Subhanahuwa Taala Akasema:

áÇ íóÍöáøõ áóßó ÇáäøöÓóÇÁ ãöä ÈóÚúÏõ æóáÇ Ãóä ÊóÈóÏøóáó Èöåöäøó ãöäú ÃóÒúæóÇÌò æóáóæú ÃóÚúÌóÈóßó ÍõÓúäõåõäøó ÅöáøóÇ ãóÇ ãóáóßóÊú íóãöíäõßó æóßóÇäó Çááøóåõ Úóáóì ßõáøö ÔóíúÁò ÑøóÞöíÈÇð

Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine ingawa uzuri wao ukikupendeza; isipo kuwa yule uliye mmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu

Al Ahzab-52

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyempa amri ya kuoa, na Yeye Ndiye aliyemkataza kuoa wengine baada ya hao na hakumruhusu kuwataliki.

Sasa kutokana na haya ndiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) analaumiwa? Subhana Llah!!

 

Kisha kuko wapi huko kupenda wanawake wanakomtuhumu, wakati alifanya hivyo kwa amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) peke yake ndiye aliyeolewa kabla ya kuanza kuteremshiwa wahyi, na kitendo hicho hakiwezi kuitwa kuwa ni cha kupenda wanawake.

 

Isitoshe, wake zake wote waliobaki hawakuwa bikira isipokuwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) peke yake, na wakati alipomuoa alikuwa binti mdogo mwenye umri wa miaka tisa, na kutokana na umri wake na mwili wake, uliokuwa mwembamba sana hakuwa na umbo lenye kuvutia, lakini Mwenyezi Mungu alitaka amuoe, Akamteremsha Jibril akimuonyesha mfano wa sura ya Bibi Aisha, na Mwenyezi Mungu akamuonyesha sura hiyo mara nyingi usingizini mpaka alipomuoa. Na kutokana na ndoa hii, usuhuba wake na Abubakar Al Siddiq (Radhiya Llahu anhu) ulizidi kupata nguvu, kama vile ulivyozidisha nguvu usuhuba wake na Umar bin Khataab (Radhiya Llahu anhu) baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kumuoa Hafsa binti Umar. Na katika wakati huo huo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimuozesha Uthman binti zake wawili Ruqayah na Ummu Kulthum, mmoja baada ya mwingine. Na pia alimuozesha binti yake Fatimah kwa Aly bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhum ajma’iyn).

 

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuoa Zaynab binti Jahash kwa hekima ya kisheria inayojulikana, kisha akamuoa Juwayriyah bintil Haarith, na huyu alikuwa binti wa kiongozi wa kabila lao. Alifanya hivyo kwa ajili ya kuzikaribisha na kuizunganisha nyoyo za watu wa kabila lake, na matunda yake ni kuwa watu wa kabila lake wote walisilimu mara baada ya kuolewa Bibi Juwayriyah. Wakati huo huo katika Waislamu kila aliyekuwa na mateka anayetokana na kabila la Bani Mustaliq alimuacha huru huku akisema: ‘Shemeji zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hawa.”

 

Na Bibi Safya binti Huyay Al Akhtwab alikuwa binti wa kiongozi wa kabila Mayahudi, na pia Abu Sufiyan alifurahi aliposikia habari za kuolewa binti yake Ramla ‘Ummu Habiybah’ na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), akasema: “Atapata wapi mfano wa Muhammad, huyu ni kijana asiyekuwa na kiburi hata chembe.”

Alikuwa siku zote akiona fahari kuwa binti yake aliolewa na Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mpaka Mwenyezi Mungu alipomjaalia kusilimu.

 

Ummu Salamah, baada ya kuuliwa mumewe katika vita vya Uhud, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimuomba amuoe kwa ajili ya kumsaidia kuwalea wanawe mayatima, na kwa njia hiyo hiyo alimuoa Sawudah binti Zam’ah na Zeinab bintil Haarith.

 

Na hivi ndivyo ilivyo, kila mke aliyeolewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kulikuwa na kisa chake na sababu zake na hekima yake.

Na kubaki kwao chini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni kwa ajili ya hekima kubwa, kwa sababu wao ndio waliokuwa mfano wa waalimu kwa Waislamu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuondoka duniani, na hii ni kwa sababu wao walikuwa na elimu juu ya yote aliyokuwa akifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ndani ya nyumba yake. Wakawafunza Waislamu wanawake kwa wanaume.

 

Juu ya yote haya, sisi binadamu tunaweza kuzijuwa baadhi ya hekima, wakati hekima nyengine zinaweza kujificha tusiweze kuzijuwa, lakini sisi tunaijuwa dini yetu, na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ametakasika na udhaifu huo, na kwamba hekima Yake haina nuksani wala makosa, na tunajua kuwa ikiwa mwanadamu haielewi hekima yoyote ile kwa ukamilifu, hii ni kwa sababu yeye ni mja dhaifu anayeweza kufanya makosa, lakini inambidi atambue kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu ni kubwa na haina makosa wala udhaifu.

Lakini hawa wenye kuitoa makosa hekima ya Mwenyezi Mungu au dini ya Mwenyezi Mungu au kumtowa makosa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), kama kwamba hawaelewi kuwa kwa kufanya hivyo wanamtoa makosa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Anayatoa makosa Mafundisho na Hekima ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, wakati yeye ni kipofu asiyeweza kuona uhakika wote, mjinga asiyejuwa maana.

Mwenye kuutafuta ukweli akauliza, ataujuwa, na utambainikia, lakini mwenye maradhi moyoni mwake, huwezi kumsaidia kwa chochote.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Åöäøóßó áÇ ÊóåúÏöí ãóäú ÃóÍúÈóÈúÊó æóáóßöäøó  ááøóåó íóåúÏöí ãóä íóÔóÇÁõ æóåõæó ÃóÚúáóãõ ÈöÇáúãõåúÊóÏöíäó

Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.

Al Qasas 56

 

Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alificha jambo?

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

æóÅöÐú ÊóÞõæáõ áöáøóÐöí ÃóäúÚóãó Çááøóåõ Úóáóíúåö æóÃóäúÚóãúÊó Úóáóíúåö ÃóãúÓößú Úóáóíúßó ÒóæúÌóßó æóÇÊøóÞö Çááøóåó æóÊõÎúÝöí Ýöí äóÝúÓößó ãóÇ Çááøóåõ ãõÈúÏöíåö æóÊóÎúÔóì ÇáäøóÇÓó æóÇááøóåõ ÃóÍóÞøõ Ãóä ÊóÎúÔóÇåõ ÝóáóãøóÇ ÞóÖóì ÒóíúÏñ ãøöäúåóÇ æóØóÑðÇ ÒóæøóÌúäóÇßóåóÇ áößóíú áÇ íóßõæäó Úóáóì ÇáúãõÄúãöäöíäó ÍóÑóÌñ Ýöí ÃóÒúæóÇÌö ÃóÏúÚöíóÇÆöåöãú ÅöÐóÇ ÞóÖóæúÇ ãöäúåõäøó æóØóÑðÇ æóßóÇäó ÃóãúÑõ Çááøóåö ãóÝúÚõæáÇ 37 ãøóÇ ßóÇäó Úóáóì ÇáäøóÈöíøö ãöäú ÍóÑóÌò ÝöíãóÇ ÝóÑóÖó Çááøóåõ áóåõ ÓõäøóÉó Çááøóåö Ýöí ÇáøóÐöíäó ÎóáóæúÇ ãöä ÞóÈúáõ æóßóÇäó ÃóãúÑõ Çááøóåö ÞóÏóÑðÇ ãøóÞúÏõæÑðÇ

Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliye mneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea. Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.

Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyo mhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa walio pita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa.

Al Ahzab – 56

 

Aya hizi zimefahamika vibaya kutokana na hadithi za Isariliyat zisizokuwa sahihi zilizopokelewa zenye kuzifasiri aya hizi. Na yamechangia zaidi katika kufahamika vibaya yale yaliyoelezwa katika visa hivyo juu ya cha ndoa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na Bibi Zeinab binti Jahash (Radhiya Llahu anha) baada ya kuwa keshaolewa kisha akatalikiwa na Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu).

Visa vya uongo vimeenea Mashariki na Magharibi, na wale wazungu wenye kuudurusu Uislamu kwa ajili ya kuupiga vita, wameitumia fursa hii kwa njia mbaya sana, wakatunga na kupamba hadithi na visa mfano wa visa vya sinema za kisasa.

Wakadai kuwa eti Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alitaka kumtembelea Zeyd bin Harithah aliyekuwa mtumwa wake aliyemuacha huru na kumfanya awe mwanawe wa kupanga, ‘adopted child’, na alipowasili nyumbani kwa Zayd asimkute, wakati huo huo upepo ulinyanyua pazia ya nyumba ya Zeyd, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akamuona Zainab akiwa amevaa nguo za kulalia au akiwa na mapambo yake, akafurahishwa na aliyoona na mapenzi yakaingia moyoni mwake, akarudi nyumbani kwake huku akisema: “Subhana Llah al Adhiym, Subhana Muqallib al Quluub”!!! Na Zeinab akamhadithia Zeyd yaliyotokea na yale aliyotamka Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na Zeyd akaenda nymbani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), akamuambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ulikuja kunizuru na huenda ulimuona Zeynab akakupendeza. Utamuoa wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akamuambia: ÃóãúÓößú Úóáóíúßó ÒóæúÌóßó æóÇÊøóÞö Çááøóåó ò Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu.”.

Wakadai kuwa eti mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) juu yake yalikuwa wazi kabisa, lakini yeye alitaka kuyaficha kwa kumuambia Zeyd (Radhiya Llahu anhu): “Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu.”, wakati ukweli ni kuwa alimpenda Zeynab na alitamani apewe talaka ili amuoe yeye.

Subhaana Llah!!! Hivi ndivyo zinavyosema hadithi za Israiliyaat, na hivi ndivyo wanavyozifasiri wale wazungu wenye kuudurusu Uislamu kwa ajili ya kuupiga vita. Bali wametamka mabaya kupita haya, mambo ambayo hayawezi kunasibishwa na Nabii wala Msemakweli wala hata na MchaMungu wa kawaida, sembuse kunasibishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Suali tunauliza; Kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kumzuru mtu yeyote bila ya kufuatana na mmojawapo wa sahibu zake? Au bila ya kuhakikisha kuwepo kwa anayetaka kumzuru? Na alikuwa akipeleleza kutaka kuona yaliyojificha ndani ya majumba? Au alikuwa akikaa nyuma ya milango akisubiri upepo upeperushe pazia apate kuona ndani ya nyumba?

 

Si yeye (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyetufundisha namna ya kuomba ruhusa ya kuingia ndani ya nyumba? Na kwamba tukishagonga mlango tusubiri mbali na milango upande wa kushoto au kulia tusiukabili mlango?

Atufundishe yote haya kisha ende kinyume na mafundisho yake?

Kweni Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hajawahi kumuona Zeynab kabla ya hapo hata mapenzi yaingie moyoni mwake siku ile?

Zeynab ni binti ami yake na alikuwa akimuona kabla ya kuteremshwa aya ya hijabu. Kweni si yeye ndiye aliyemuozesha Zeyd Bin Harithah? Na Bibi Zeynab alipokataa, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimshikilia kumuomba akubali mpaka ilipoteremshwa aya isemayo:

æóãóÇ ßóÇäó áöãõÄúãöäò æáÇ ãõÄúãöäóÉò ÅöÐóÇ ÞóÖóì Çááøóåõ æóÑóÓõæáõåõ ÃóãúÑðÇ Ãóä íóßõæäó áóåõãõ ÇáúÎöíóÑóÉõ ãöäú ÃóãúÑöåöãú æóãóä íóÚúÕö Çááøóåó æóÑóÓõæáóåõ ÝóÞóÏú Öóáøó ÖóáóÇáðÇ ãøõÈöíäðÇ

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi

Al Ahzab – 36

 

Na angelikuwa kweli anamtaka, kipi kilichomzuwia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) asimuoe Zeynab badala ya kumuozesha Zeyd kwanza kisha asubiri mpaka amuachishe ili amuoe yeye?!!!

 

Istoshe, hapana hata hadithi moja sahihi inayosema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kumuona Zeynab akiwa katika hali ile baada ya kumuozesha Zeyd.

Kisha tunauliza tena; Ni nani aliyeamrisha Zeinab aolewe na Zeyd bin Harithah ili iondoke ile ada ya kijahilia ya waungwana kukataa kuolewa na watumwa wao waliowaacha huru? Na wanawake wa kabila la kubwa la Kikureshi hawakuwa wakikubali wakati ule kuolewa na watumwa wao walioachwa huru, kwa sababu wakati ule ubaguzi baina ya watumwa na waungwana ulikuwa mkubwa sana, na lilikuwa ni jambo lisilokubalika kabisa wakati ule kwa bibi wa kungwana wa kabila la Kikureshi kukubali kuolewa na mmojawapo wa watumwa wao. na hivi ndivyo alivyofanya Bibi Zeynab, alikataa kuolewa na Zeyd (alipotakiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kufanya hivyo) mpaka ilipoteremka aya tuliyotangulia kuitaja.

 

Kisha nani aliyemuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kumuoa Zeynab baada ya kutalikiwa na Zeyd na kumaliza muda wake wa eda? Ni kwa ajili ya kuondoa ada nyingine iliyokuwepo wakati ule, ambayo ni ada ya kumgeuza mtoto wa kulea kuwa mtoto wa kupanga ‘adopted child’ na kugeuka mtoto huyo kuwa sawa na mtoto wa kumzaa akibeba jina na kabila la baba yake mpya, akiwa na haki ya kumrithi baada ya kufariki pamoja na hukumu zote za mtoto na baba yake.

 

Na hivi ndivyo iliyokuwa kwa Zeyd, ambaye baada kumuoa Bibi Zeynab hayakuwepo masikilizano mazuri baina yao, kwa sababu ya hitilafu ya tabaka iliyokuwepo baina yao, na Zeyd alikuwa kila mara akienda kushitaki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa kila mara akimuambia:  “Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu na uwe na subira,” mpaka pale Mwenyezi Mungu alipomjulisha kuwa Zeyd amtaliki Zeynab na kwamba wewe ndiye utakayemuoa kwa ajili ya kuondoa ile ada ya mtoto wa kupanga iliyoenea wakati ule baina ya watu, na kwamba wewe (Muhammad) na si mwingine utakayeibatilisha ada hii kwa vitendo kwa kutimiza amri ya Mwenyezi Mungu katika hilo.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akawa anaona haya kumpa habari hizo Zeyd, akahofia yale yatakayofuatilia baada ya makafiri kupata habari hizo, maneno watakayosema, na pia maneno yatakayosemwa na watu kuwa Muhammad kamuoa mke aliyeachwa na mwanawe.

Hapo ndipo Mola wake alipomkataza na kumjulisha kuwa hapana ubaya wowote katika yale Aliyoamrisha Mola wake.

Anasema Ibni Kathiyr (Mwenyezi Mungu amrehemu): Mwenyezi Mungu Amesema:

æóãóÇ ÌóÚóáó ÃóÏúÚöíóÇÁßõãú ÃóÈúäóÇÁßõãú Ðóáößõãú Þóæúáõßõã ÈöÃóÝúæóÇåößõãú æóÇááøóåõ íóÞõæáõ ÇáúÍóÞøó æóåõæó íóåúÏöí ÇáÓøóÈöíáó

Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Anaye sema kweli, Naye ndiye Anaye ongoa Njia

 Al Ahzab -4

Hili ndilo kusudi la kisa chote, na iliteremshwa aya kwa ajili ya Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu) aliyekuwa Mtumwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyemuacha huru kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimfanya kuwa mtoto wake wa kupanga, na hii ilikuwa kabla ya kupewa utume, na alikuwa akiitwa kwa jina la Zeyd bin Muhammad. Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Alitaka kuuondoa mwenendo huu na uhusiano  ule Aliposema:

Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa.

Na öAlisema pia ndani ya sura hiyo hiyo ya Al Ahzab:

ãøóÇ ßóÇäó ãõÍóãøóÏñ ÃóÈóÇ ÃóÍóÏò ãøöä ÑøöÌóÇáößõãú æóáóßöä ÑøóÓõæáó Çááøóåö æóÎóÇÊóãó ÇáäøóÈöíøöíäó æóßóÇäó Çááøóåõ Èößõáøö ÔóíúÁò ÚóáöíãðÇ

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu

Al Ahzab -40

Na hapa Akasema:

Ðóáößõãú Þóæúáõßõã ÈöÃóÝúæóÇåößõãú

Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu

Al Ahzab -4

Na maana yake ni kuwa; kule kuwafanya watoto wa kupanga wawe watoto wenu halisi hakuwezi kuwageuza wakawa watoto wenu kikweli, kwa sababu wameumbwa kutoka katika mgongo wa mtu mwengine, kwa hivyo hawezi kuwa na baba wawili, kama vile iliyvokuwa mtu mmoja hawezi kuwa na nyoyo mbili, "Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu."

Ndipo Mwenyezi Mungu Aliposema:

ÇÏúÚõæåõãú áöÂÈóÇÆöåöãú åõæó ÃóÞúÓóØõ ÚöäÏó Çááøóåö

 

Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu

Al Ahzab – 5

Ikaja kufuta ile hukmu iliyokuwepo mwanzo wa Uislamu ya kuruhusu mtoto kuitwa kwa ubini wa asiyekuwa baba yake, na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala akaamrisha kuitwa kwa ubini wa baba zao wa kweli, na kwamba kufanya hivyo ni kufanya uadilfu wa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

 

Imetolewa na Bukhari kutoka kwa Abdillah bin Umar kuwa amesema:

"Hakika Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu) alikuwa mtumwa aliyeachwa huru na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na tulikuwa tukimuita kwa jina la Zeyd bin Muhammad, mpaka ilipoteremshwa aya hii:" Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu."

Bukhari na Muslim na Attirmidhy na Annasaiy

 

Na walikuwa wakiwatendea sawa na watoto wao katika kila kitu, kama vile kubaki na wanawake wa nyumbani na mambo mengine, na baada ya kuondolewa hukmu hiyo, Mwenyezi Mungu Akaruhusu kuowa mke wa mtoto wa kupanga, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alipomuoa Zeynab binti Jahash, baada ya kuachwa na Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu), na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Akasema:

áößóíú áÇ íóßõæäó Úóáóì ÇáúãõÄúãöäöíäó ÍóÑóÌñ Ýöí ÃóÒúæóÇÌö ÃóÏúÚöíóÇÆöåöãú ÅöÐóÇ ÞóÖóæúÇ ãöäúåõäøó æóØóÑðÇ æóßóÇäó ÃóãúÑõ Çááøóåö ãóÝúÚõæáÇ

"Ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa."

 Al Ahzab – 37

Na katika aya nyingine katika Surat Annisaa Mwenyezi Mungu Amesema:

æóÍóáÇóÆöáõ ÃóÈúäóÇÆößõãõ ÇáøóÐöíäó ãöäú ÃóÕúáÇóÈößõãú

(Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu.

Annisai – 23

Tofauti na mke wa mtoto wa kupanga ambaye hatokani na mgongo wake.

 

Kuhusu mtoto wa kunyoyesha, kisheria anakuwa sawa na mtoto wa kuzaa kama ilivyoandikiwa katika Bukhari na Muslim kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alisema:

"Imeharamishwa kwa mtoto wa kunyonyesha kila kilichoharamishwa kwa mtoto wa kuzaa mwenyewe."

Bukhari na Muslim

 

Haikatazwi kumuita mtoto wa mtu mwingine 'Mwanangu' ikiwa umemuita kwa nia ya kumkirimu tu au kwa kumpenda.

 

Anasema Ibni Kathiyr katika kuifasiri aya isemayo:

æóãóÇ ßóÇäó áöãõÄúãöäò æáÇ ãõÄúãöäóÉò ÅöÐóÇ ÞóÖóì Çááøóåõ æóÑóÓõæáõåõ ÃóãúÑðÇ Ãóä íóßõæäó áóåõãõ ÇáúÎöíóÑóÉõ ãöäú ÃóãúÑöåöãú

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao.

Al Ahzab – 36

Amesema Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhuma): "Na hii ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikwenda nyumbani kwa Zeinab binti Jahash (Radhiya Llahu anha) kwa ajili ya kumposea Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu), na Zeinab akasema: "Sitaki kuolewa naye." Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema: "Sivyo hivyo, kubali kuolewa naye." Zeinab akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nijilazimishe?" Walipokuwa wakiendelea kuzungumza, Mwenyezi Mungu Akaiteremsha aya hii, na Zeinba alipoisikia akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu umeridhika awe mume wangu." Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema: "Ndiyo", akasema: "Kwa hivyo sitomuasi Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimemkubali."

 

Na riwaya nyingine inasema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alimposa Zeinab kwa ajili Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu), na Zeinab hakupendezewa, akasema: "Mimi nasaba yangu ni bora kuliko yake," na alikuwa mwanamke mkali. Mwenyezi Mungu akateremsha " æóãóÇ ßóÇäó áöãõÄúãöäò æáÇ ãõÄúãöäóÉò" mpaka mwisho wa aya.

Bukhari na Ibni Kathiyr katika tafsiri yake akinukuu kutoka kwa Imam Ahmad

 

Kisha akasema katika kuifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu Isemayo:

æóÅöÐú ÊóÞõæáõ áöáøóÐöí ÃóäúÚóãó Çááøóåõ Úóáóíúåö æóÃóäúÚóãúÊó Úóáóíúåö

Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu Aliye mneemesha, nawe ukamneemesha..

Mwenyezi Mungu anatujulisha juu ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyemuambia Zeyd bin Harithah (Radhiya Llahu anhu) ambaye Mwenyezi Mungu Amemneemesha kwa Uislamu na kwa kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amemneemesha Zeyd kwa kumuacha huru alipokuwa mtumwa wake na kumfanya awe mtu mwenye shani kubwa kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyekuwa akiitwa Kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na mwanawe Usama alikuwa akiitwa kipenzi mtoto wa kipenzi.

Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) alisema:

"Hajapata Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kumepeleka vitani isipokuwa lazima amuweke yeye kuwa kiongozi wao, na lau kama angeliishi baada yake basi angelimfanya awe Khalifa.